Ni ajabu na kweli. kuna kuku hapa tz wanaolea bata. ukiwa dar tembelea bamboo bar, kinondoni kwa John Fedha, utajionea. kwa mujibu wa uchunguzi wangu, jirani ya bar hiyo kuna jamaa anafuga kuku na bata. huwa anachukua mayai ya kuku na kuyaweka kwenye kiota cha bata ambaye anayaatamia hadi kutotoa. ujanja utumikao ni kwamba kwa vile uatamiaji wa kuku huchukua siku takriban 14, wakati bata ni siku kati ya 29 na 40, jamaa hukadiria muda wa mayai ya bata na kuyaweka chini ya kuku ambaye, baada ya kutotoa, hujua ni vifaranga vyake. na huvilea kama vitoto vyake, na ni mkali kama kawaida ukivisogelea. ni sayansi nyepesi lakini yenye kuhitaji ubongo na uvumilivu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Sasa michuzi hizi ndio picha zako...mzee una jicho. Sijui umelichanjia?????? Picha safi sana hii. Picha zako ni kama hadithi fulani tamu sana....heri umeingia kwenye blog...

    ReplyDelete
  2. Hawa kuku wanakatiza machinjoni au? Maana pembeni naona kama kuna damu vile!

    ReplyDelete
  3. Hahahaha
    Lakini mtoto wa bata ni bata tu, kama ilivyo kawaida ya watoto wa bata humtangulia mama yao, vivyo hivyo na hawa watoto bata wa kuku wanamtangulia mama yao mlezi kuku.

    ReplyDelete
  4. WHY???????
    YANI SIJAJUA NI KWANINI MTU AFANYE HIVO, TUELIMISHA PLEASE! JE KUNAFAIDA YEYOTE AU ALITAKA TU KUCHEKI KAMA KUKU ATAGUNDUA.

    OTHERWISE HAINA MAANA.

    ReplyDelete
  5. Mimi kinacho nikera saaana MR Michuzi ni kuwa na Viongozi Average Mind..wenye uwezo mdogo kufikiri na kuamua...Sasa kama wakati huu wa uchaguzi mto kwa sababu anaweza kushika mike na kuongea mbele za watu basi anafaa kuwa kiongozi....Je ndugu zangu tutafika kweli!!..Mimi nasikitika sana..wanwake wapo wanaoweza kuongoza na wengine do wana faa kwenye social activities na sio maendeleo ya nchi...Kama Taifa Tuwe Makini Tusijipendekeze kwa kiongozi yeyote ..Cheo ni dhamana...asiyeweza awapishe wengine Taifa Litaenda Shimoni.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...