jkm, bwm na peter onu wakiwa kwenye mkutano wa 17 wa oau huko addis ababa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2006

    Dah Ben Nkapa alikuwa bado ana nywele za kutosha hapo kichwani utosini. Ni mwaka gani huo na alikuwa na cheo gani? manake naona amebeba mkoba kama mwandishi wa habari vile. Au ndio alikuwa mbeba brifu kesi ya mwalimu?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2006

    Wakati huo TANESCO, NBC, NUWA (DAWASCO), Bulyanhulu, Kahama, Buhemba n.k vilikuwa miononi mwa wananchi. Mikataba ya Kimangungo haikuwepo watu wasikonde mchezo?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2006

    Benjamin William Mkapa was born on November 12th, 1938 at Masasi, Mtwara Region. Between 1945 and 1951 he attended primary school at Lupaso and Ndanda Schools where he attained a Standard Eight School Certificate.

    He completed his 'O' Level education at Ndanda Secondary School in 1955 and proceeded to Saint Francis College (now Pugu Secondary School; where the late former President of Tanzania Mwalimu Julius K. Nyerere was a teacher) for his Advanced Level Secondary Education.

    In 1959, Mr. Mkapa joined Makerere University College in Uganda and obtained Preliminary Arts (1959) and Bachelor of Arts Degree (Hons) in English (1962).

    He worked as a district administrative officer in Dodoma and Dar es Salaam for one year before joining the Foreign Service in 1963.

    Having joined the ruling party, the Tanganyika African National Union (TANU), Mr. Mkapa was appointed managing editor of the party's newspaper in May 1966. In July 1974 he was promoted to press secretary for President Julius K. Nyerere and was subsequently appointed Director of SHIHATA, the first Tanzanian news agency, in 1976.

    President Mkapa's long diplomatic career included a number of high postings, such as High Commissioner to Nigeria (in 1976) and Minister for Foreign Affairs (from 1977 to 1980).

    He became Minister for Information and Culture in 1980-82; and again Minister for Information and Broadcasting in 1990-92.

    In 1982, he served as High Commissioner to Canada and between 1983 and 1984 as Ambassador to the United States of America. He returned home in 1984 where he was again appointed as Member of Parliament and Minister for Foreign Affairs. In 1992, he served as Minister for Science, Technology and Higher Education, prior to being nominated for President in 1995, and Chairman of his Party, Chama Cha Mapinduzi, in 1996.

    In October 1995 he garnered 62 percent of the vote in Tanzania's first multiparty elections and began his term as President in November 1995. President Mkapa was re-elected with overwhelming mandate in 2000 and is now serving his last term in office.

    Throughout his political career, President Mkapa has worked inexhaustibly to strengthen democracy, entrench civil rights and fight poverty, while increasing the country's exposure to international trade and investment. He is active in conflict prevention, management and resolution in the Great Lakes Region and is an active player in regional economic co-operation within the East African Community, and the Southern African Development Community (SADC). He is currently the Chairman of SADC.

    President Mkapa is also the Co-Chairperson of the World Commission on the Social Dimension of Globalisation. He is co-chairing with President Tarja Kaarina Halonen of Finland.

    President Mkapa holds two honorary doctorate degrees from Soka University in Japan (1998) and Morehouse College, Atlanta, USA (1999). His main hobby is reading. He is married to the former Anna Joseph Maro, and they have two sons

    JINA KAMILI: Jakaya Mrisho Kikwete
    UMRI: 55
    ELIMU: DEGREE
    WADHIFA WA SASA: Rais

    Ndugu Kikwete amekuwa katika utumishi wa chama kwa miaka 30 na katika utumishi wa serikali katika nafasi mbalimbali za Uwaziri kwa miaka 17.
    Baada ya kumaliza masomo yake ya Chuo Kikuu mwaka 1975 na kupata Shahada ya Uchumi, akiwa na umri wa miaka 25 tu, Ndugu Kikwete alijiunga katika utumishi wa chama cha TANU (Tanganyika African Natuional Union). TANU ndiyo iliyoongoza mapambano ya kudai uhuru nchini na Februari 5, mwaka 1977, iliungana na chama kilichoasisi Mapinduzi ya Zanzibar, ASP (Afro-Shirazi Party) na kuzaliwa CCM.
    Ndugu Kikwete alianza utumishi wa chama akiwa Katibu Msaidizi wa TANU wa Mkoa, mwaka 1975-1977. Baadaye akawa Katibu Msaidizi wa CCM, Zanzibar, mwaka 1977-1980; Ofisa Utumishi wa CCM Makao Makuu, mwaka 1980-1981; Katibu Mtendaji wa CCM, Mkoa wa Tabora, mwaka 1981-1983; Mkufunzi wa Siasa katika Chuo cha Uongozi wa Jeshi, Monduli, mwaka 1983-1986 na Katibu wa CCM Wilaya ya Nachingwea na baadaye ya Masasi Mwaka 1986-1988. Amekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM tangu mwaka 1982 na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM tangu mwaka 1997 hadi sasa.

    Katika utumishi wa Serikali, Ndugu Kikwete alianza kwa kuteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, mwaka 1988-1990. Baadaye akawa Waziri wa Nishati, Madini na Maendeleo ya Maji, mwaka 1990-1994; Waziri wa Fedha, mwaka 1994-1995 na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, mwaka 1995-2005. Amekuwa Mbunge tangu mwaka 1988 hadi sasa katika Jimbo la Chalinze.
    Maisha yake:
    Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete alizaliwa Oktoba 7, mwaka 1950 katika kijiji cha Msoga, Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani. Ni mtoto wa sita wa Mzee Khalfani Mrisho Kikwete.
    Baada ya Elimu ya Msingi mwaka 1958-1961, Ndugu Kikwete alijiunga na Shule ya Kati Lugoba mwaka 1962-1965. Mwaka 1966-1969 alisoma Shule ya Sekondari ya Kibaha na mwaka 1971-1972 alisoma kidato cha tano na cha sita katika shule ya Sekondari ya Tanga. Mwaka 1972-1975 alisoma Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alihitimu Shahada ya Kwanza ya Uchumi. Alijiunga katika mafunzo ya Maofisa wa Jeshi katika Chuo cha Uongozi wa Jeshi Monduli, mwaka 1976-1977 na baadaye Mafunzo ya Makamanda wa Jeshi katika chuo hicho hicho, mwaka 1983-1984. Kikwete ni Ofisa Mstaafu wa Jeshi katika cho cha Luteni Kanali.
    Ndugu Kiwete ni mtu mwenye haiba na mvuto mkubwa na ana maono ya mbali katika uongozi. Ana mke, Salma, na watoto wanane – wanaume sita, wanawake wawili.

    JINA KAMILI: Dr Ali Mohamed Shein
    UMRI: 57
    ELIMU: Masters Degree in Medical Biochemistry
    WADHIFA WA SASA: Vice President

    DATE OF BIRTH: 13 March 1948
    MARITAL STATUS: Married with children
    NATIONALITY: Tanzanian
    EDUCATION
    PRIMARY LEVEL: 1956 - 1964: Gulioni Primary School, Zanzibar. Award: Primary School Leaving Certificate
    SECONDARY EDUCATION: 1965 - 1968 Lumumba College, Zanzibar, Award: GCE (O' Level)
    1969 - 1970 Preparatory Faculty Vorenezh State University, USSR
    Award: A Level Certificate
    UNIVERSITY EDUCATION: 1970 - 1975 Odesa State University, USSR: Award: Masters Degree in Medical Biochemistry.
    1984 - 1988 Medical School University of Newcastle Upon Tyne, England - UK: Award:
    Doctor of Philosophy (PhD) in Clinical Biochemistry and Metabolic Medicine, specialising in "Inborn Errors of Metabolism"
    OTHER COURSES: Organization of Blood Transfusion Services and Operation of Blood Bank, Stockholm Sweden 1981
    Planning for HIV/AIDS in Developing Countries - University of East Anglian Norwich - UK 1995

    A course in Management and Situation Leadership - Dar es Salaam 1994
    PROFESSIONAL AND LEADERSHIP EXPERIENCE
    May 1969 September 1969 - Clerk and later on Deputy Principal Secretary (B), Ministry of Education, Zanzibar.
    1976-1984: In charge of Clinical Laboratory and Head of Pathology Pepartment, Ministry of Health, Zanzibar.
    1989 - 91: Specialist - Clinical Biochemist and Head of Pathology Department, Ministry of Health Zanzibar.
    Nov. 1991- July 1995: Program Manager, Zanzibar AIDS Controls Program, Ministry of Health, Zanzibar and Adviser to the Ministry on Laboratory Services and Clinical Pathology Services.
    From 29-10-1995: Appointed Member of The House of Representative.
    6th November 2000: Elected Member of The House of Representative, Mkanyageni Constituency
    12th November 1995: Appointed Deputy Minister of Health, Zanzibar
    22 Nov. 2000: Appointed Minister of State President's Office Good Governance and Constitutional Affairs, Zanzibar.
    13th July 2001: Appointed Vice President of The United Republic of Tanzania.
    POLITICAL EXPERIENCE
    1966: Joined Afro shirazi Party Youth League (ASPYL)
    From Jan. - Dec. 1968: Public Secretary ASPYL Lumumba College ASPYL Secretary, Zanzibar Secondary Schools.
    1969: Joined Afro Shirazi Party
    13 June 1977: Joined CHAMA CHA MAPINDUZI - CCM
    2 September 1977 - Member of CCM National Executive Committee

    PARTICIPATION IN DIFFERENT PROFESSIONAL COMMITTEES
    Member of WHO Expert Committee, African Region 1990 - 1994 (Listed from Ministry of Health Zanzibar)
    Member of Academic Council of Muhimbili University College of Health Sciences 1990 - 1995
    Member of Advisory Committees in the Ministry of Health and others, Zanzibar Revolutionary Government 1989 - 1995

    MEMBERSHIP IN PROFESSIONAL ASSOCIATIONS
    Member of Association of Clinical Biochemists of UK, 1985 - 1992
    Member of Association of "Clinical Pathologist for Eastern Southern and Central Africa (APESCA) 1992 to Date
    Member of Association of Clinical Pathologist of Tanzania 1992 to Date
    Member of International Association of Inborn Errors of Metabolism 1987 - 1991

    RESEARCH PAPERS AND PUBLICATIONS
    Short communications/posters - 29
    Full papers - 3
    Thesis - 2 (M.Sc & PhD)

    CONFERENCES AND SEMINARS
    I have attended various local and International conferences and seminars in different capacities inter alia as resource person and delegation leader.

    OTHERS
    Internationally well travelled

    HOBBIES
    Athletics, football, reading scientific books and magazines.


    JINA KAMILI: AMANI ABEID KARUME
    UMRI: 67
    ELIMU: Diploma
    WADHIFA WA SASA: RAIS



    Ndugu Amani Abeid Karume ni mzaliwa za Zanzibar, Amezaliwa Novemba 1, mwaka 1948. Amekuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi tangu mwaka 2000, baada ya kushinda katika Uchaguzi Mkuu.
    Amekuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM tangu mwaka 1992, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM tangu mwaka 2000 na Makamu wa Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, tangu mwaka 2002. Desemba mwaka 2002 ateuliwa pia kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar.
    Ndugu Karume alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar mwaka 1990, akiwakilisha jimbo la Rahaleo, Unguja. Kati ya mwaka 1990-1995 alikuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa kuteuliwa kutoka Baraza la Wawakilishi.
    Alikuwa Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar mwaka 1990-1995 na Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi mwaka 1995-2000.
    Katika utumishi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Ndugu Karume pia aliwahi kuwa Mhasibu, Wizara ya Fedha, mwaka 1969-1970; Mhasibu Mkuu mwaka 1970-1971; Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, mwaka 1971-1974; Katibu Mkuu, Wizara ya Mipango, mwaka 1974-1978 na Katibu Mkuu, Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, mwaka 1978-1980.
    Amemuoa Shadya na wana watoto sita. Ni mpenzi wa michezo, utunzaji wa bustani na kujisomea.


    JINA KAMILI: Augustine Lyatonga Mrema
    UMRI: 60
    ELIMU: DEGREE (Elimu)
    WADHIFA WA SASA: Mwenyekiti Taifa (TLP)

    Alizaliwa karibu miaka 60 iliyopita yaani mwaka wa 1945, katika mkoa wa Kilimanjaro, Kijiji cha Kilaracha kilichopo katika Wilaya ya Moshi vijijini, Mheshimiwa Mrema ambae kwa sasa ni Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) ni mzaliwa wa pili katika familia ya watoto watano ya Mzee Lyatonga Mrema.
    Mwaka wa 1955 -1963 alianza masomo yake ya darasani mpaka middle school katika Wilaya yake hiyo hiyo ya nyumbani ya Moshi vijijini, mnamo mwaka wa 1964 mpaka 1965 Mrema alijiunga na Chuo cha Ualimu cha Mtakatifu Patrick.
    Baada ya kumaliza mafunzo yake ya Ualimu na kupata kazi, Mheshimiwa Mrema alianza kuchukua mafunzo yake ya sekondari ambapo mwaka wa 1968 alifanya mtihani wake wa kidato cha nne, wakati huo mitihani ikitoka Chuo Kikuu cha Cambridge cha nchini Uingereza.
    Mwaka wa 1970-71 Mheshimiwa Mrema alijiunga kwenye mafunzo maalumu ya siasa na uongozi katika Chuo cha Kivukoni na mwaka wa 1980 na 81 alienda chini Bulgaria ambako alifanikiwa kutunukiwa Diploma ya sayansi ya Ustawi wa jamii na Utawala.
    Augustine Lyatonga Mrema baada ya hapo alifanya kazi mbalimbaliza kijamii na kichama kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Pacific mwaka 2003 ambako ametunukiwa Shahada ya Sanaa katika Sayansi ya Jamii.
    Bwana Mrema alianza kazi mwaka 1966-69 kama mwalimu akifundisha shule mbalimbali za mkoa wa Kilimajaro na mwaka 1972-1973 aliteuliwa kuwa mratibu wa elimu wa Kata. Mwaka wa 1974-80 Augustine Lyatonga Mrema alichaguliwa kuwa mwalimu wa siasa katika wilaya mbalimbali kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi.
    Mwaka wa 1980-1982 bwana Mrema alichaguliwa kuwa Mwalimu wa Chuo kikuu cha usalama wa Taifa na mwaka 1982 - 1984 bwana Mrema aliteuliwa kuwa Kaimu mkuu wa usalama wa Taifa mkoa wa Dodoma, mwaka 1983-1984 aliteuliwa kuwa Katibu wa timu ya ulinzi na usalama makao makuu Dodoma.
    Mwaka wa 1985 Mrema alirudi katika Jimbo lake na kugombea Ubunge ambako alishinda, lakini hata hivyo aliwekewa pingamizi Mahakama Kuu ya Kilimanjaro na wakati kesi ikiendelea Mrema alipelekwa katika mkoa wa Shinyanga, Wilaya ya Kahama kuwa Afisa Usalama wa Taifa katika wilaya hiyo na mwaka 1987 alishinda rufaa yake na kurejeshewa ubunge wake.
    Aligombea ubunge kwa mara nyingine mwaka 1990 na akafanikiwa kutetea jimbo lake tena safari hiyo kwa kishindo na akarudi bungeni kwa mara ya pili. Alichaguliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani mwaka 1990-1994, na wakati huohuo mwaka 1993-1994 aliteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu cheo ambacho hata hivyo hakikuwepo kwenye Katiba ya nchi.
    1994 alibadilishwa Wizara hiyo na kuhamishiwa katika Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana na Michezo. Alijiengua rasmi CCM mwaka 1995 na kujiunga na Chama cha NNCR - Mageuzi alikokuwa Mwenyekiti wa Taifa na mgombea Urais kupitia chama hicho.
    Mrema ambaye sasa ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour (TLP) aligombea urais mara ya pili mwaka 2000 kupitia (TLP), na sasa anagombea tena kwa mara ya tatu kupitia chama hicho


    JINA KAMILI: Ibrahim Lipumba
    UMRI: 56
    ELIMU: Profesa (Uchumi)
    WADHIFA WA SASA: Mwenyekiti Chama cha Wananchi (CUF)

    Profesa huyu wa Uchumi alizaliwa mwaka 1952, mkoani Tabora katika familia ya Baba Mzee Haruna na Mama Mwantumu, nyumbani kwao ni mkoani Tabora hivyo kabila lake ni Mnaywezi na ni mtoto wa pili kuzaliwa katika familia ya watoto watatu wa Mzee Haruna.
    Mwaka wa 1976 alimaliza shahada yake ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo alikuwa mwanafunzi bora, katika Idara ya Sayansi ya Jamii akiwa amejikita katika masuala ya Uchumi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilimbakisha chuoni hapo kama mkufunzi msaidizi.
    Kwa miaka 19 mfululizo Lipumba aliendelea kufanyakazi katika Chuo kikuu cha Dar es Salaam huku akipanda ngazi taratibu kutoka Ukufunzi msaidizi, mhadhiri mwandamizi hadi Profesa mshiriki.
    Mwaka wa 1993 mpaka 1995 Profesa huyu alipata heshima ya kwenda kufundisha katika Chuo cha Williams kilichopo nchini Marekani katika Jimbo la Massachussets akiwa Profesa mwalikwa. Mwaka wa 1996 hadi 1998 Profresa huyu alikuwa Jijini Helsinki nchini Finland kama Mtafiti mwandamizi katika World Institute of Economic Research.
    Wakati wa Utawala wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Profesa huyu aliteuliwa na Rais Alhaji Ali Hassan Mwinyi kuwa mshauri wa Rais wa mambo ya uchumi.
    Amefanya kazi mbalimbali za utafiti wa kiuchumi na kutoa ushauri kwa mashirika ya kimataifa kama vile Benki ya Dunia (WB), Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Sweden Agency (SIDA), Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Norway (NORAD) na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark.
    Pamoja na hayo Profesa huyu ametoa ushauri wa kitaalamu Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland, Benki Kuu ya Tanzania na katika Taasisi ya uchumi na Utawala wa Fedha wa Mashariki na Kusini mwa Afrika (MEFMI).
    Mwaka 1995 aligombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Wananchi (CUF) ambapo hata hivyo aliangushwa na Rais Benjamin William Mkapa, pia alikuwa nyuma ya mgombea wa NCCR - Mageuzi bwana Augustine Lyatonga Mrema, mwaka 2000 aliingia tena ulingoni safari hii akifanikiwa kushika nafasi ya pili lakini nyuma tena ya Rais Benjamini William Mkapa anaemaliza muda wake.
    Profesa huyu anasema katika kupambana na umasiki uchumi wa Tanzania ya leo unatakiwa kukua kwa kasi kama ilivyo kasi ya ukuaji wa kiuchumi wa mataifa ya Singapore, Thailand, Malaysia na nchi nyingine za Asia ambazo uchumi wao unakua kwa kasi, lakini hilo limewezekana tu kutokana na kuwawezesha Wazalendo wa nchi hizo kumiliki uchumi wao.
    Profesa Ibrahimu Haruna Lipumba amemuoa Bi. Georgina Mtenga ambae ni mfanyakazi wa UNICEF, na mwaka huu ni awamu yake ya tatu anajaribu kuusaka Urais wa Tanzania akiwa na wenzake tisa wanane wanaopigana na nguvu za mgombea wa Chama cha Mapinduzi Jakaya Mrisho Kikwete katika kuona kuwa wanakiondoa Chama hicho kongwe katika Utawala ambako kimedumu kwa miaka 44 sasa.
    Hamis Machano ndio mgombea mwenza wa Profesa Ibrahim Haruna Lipumba.


    Matokeo ya uraisi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar:

    Mgombea Chama Kura Asilimia
    AMAAN ABEID KARUME Chama Cha Mapinduzi 239,332 53.2
    SEIF SHARIF HAMAD Chama cha Wananchi 207,303 46.1
    HAJI MUSSA KITOLE Jahazi Asilia 2,110 0.5
    ABDULAH ALLY ABDULAH Democratic Party 509 0.1
    SIMAI ABDURAHMAN National Reconstruction Alliance 449 0.1
    MARIAM AHMED OMARI Sauti ya Umma 335 0.1

    Matokeo ya Uraisi Serikali ya Jamuhuri ya Muungano Tanzania:
    Mgombea Kura Asilimia
    JAKAYA KIKWETE (CCM) 9,102,952 80.2
    PROF. IBRAHIM LIPUMBA (CUF) 1,327,125 11.7
    FREEMAN MBOWE (CHADEMA) 668,736 5.9
    AUGUSTINO MREMA (TLP) 84,901 0.7
    DR. SENGONDO MVUNGI (NCCR Mageuzi) 55,819 0.5
    MCH. CHRISTOPHER MTIKILA (DP) 31,083 0.3
    EMMANUEL MAKAIDI (NLD) 21,574 0.2
    ANNA SENKORO (PPT-Maendeleo) 18,783 0.2
    PROF. LEONARD SHAYO (MAKINI) 17,070 0.2
    PAUL KYARA (SAU) 16,414 0.1

    *Tangu uhuru nafasi ya uwaziri mkuu nchini imekuwa ikishikiliwa na wanaume:
    1. Julius Kambarage Nyerere – Desemba, 1961 – Aprili, 1962
    2. Rashid Mfaume Kawawa - Aprili, 1962 - Aprili, 1964
    3. Rashid Mfaume Kawawa - 9/11/1975 – 15/2/1977
    4. Edward Moringe Sokoine - 15/2/1977 – 8/11/1980
    5. Cleopa David Msuya - 8/11/1980 – Februari, 1983
    6. Edward Moringe Sokoine - Februari, 1983 – 12/4/1984
    7. Salim Ahmed Salim - Mei, 1984 – Novemba, 1985
    8. Joseph Sinde Warioba - 6/11/1985 – 8/11/1990
    9. John Samuel Malecela - 8/11/1990 – 2/12/1994
    10. Cleopa David Msuya - 5/12/1994 – Novemba, 1995
    11. Frederick Tluway Sumaye - 28/11/1995 – 28/12/2005
    12. Edward Ngoyai Lowassa – 29/12/2005 – To date.

    Samuel Sitta (29 December 2005) becomes the fourth Speaker of the National Assembly after Chief Erasto Mang’enya, who held the position from 1961 to 1967, Chief Adam Sapi Mkwawa (1967-1994) and Msekwa (1994-2005).


    ** KIKWETE:

    Alizaliwa Oktoba 7, mwaka 1950 katika kijiji cha Msoga Wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.

    Elimu.
    1958-1961 - Shule ya Msingi Msoga
    1962-1965 - Shule ya Msingi ya Kati ya Lugoba
    1966-1969 - Shule Sekondari Kibaha
    1970-1971 - Shule ya Sekondari Tanga
    1972-1975 - Chuo Kiku cha Dar es Salaam, Shahada ya kwanza ya Uchumi
    1976-1977 - Mafunzo ya Afisa wa Jeshi
    - Mafunzo ya Uongozi wa Jeshi Monduli
    1983-1984 - Mafunzo ya Makamanda wa Jeshi

    Nafasi alizowahi kushika
    1975-1977 - Katibu msaidizi wa TANU wa Mkoa
    1977-1980 - Katibu Msaidizi wa CCM, Kisiwani Zanzibar
    1980-1981 - Afisa Utumishi wa CCM makao makuu
    1981-1983 - Katibu wa CCM Mkoa Tabora
    1983-1986 - Mkufunzi wa Siasa katika Chuo cha uongozi wa Jeshi Monduli
    1986-1988 - Katibu wa CCM Wilaya ya Nachingwea na baadaye Masasi
    1988-1990 - Naibu Waziri wa Nishati na Madini
    1990-1994 - Waziri wa Nishati, Madini na Maendeleo ya Maji
    1994-1995 - Waziri wa Fedha
    1995- Hadi sasa - Mbunge wa Chalinze
    1995-2000 - Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
    2000-2005 - Aliteuliwa tena kuuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2006

    Kisomo cha Karume mbona haujaonyesha? Watu ambao mnawapiga madongo kwamba hajasoma ndio hao wanaondesha INJI

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2006

    anony wa hapo juu umeonge point,huyo Karume hana kisomo chochote.Hiyo Diploma ni kizibio tuu.Huyo ni form 6 tuu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 25, 2006

    Sijui nani kasema au kamusi gani imenena kuwa ufasaha wa matusi ndio utatuzi au uchangunuaji wa maada maana kuna vijana wengine bila kutumia matusi basi hawana raha huyu mwizi ,huyu mshenzi kama wewe kweli mapafu yako yametanuka na unauchungu wa kweli na nchi yako kama akina Ken Sarawiwa basi njoo bongo fungu idhaa yako au kipindi tuwasilishie maoni yako ntafurahi sana kukijua kipaji chako

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 25, 2006

    Aise huyu Sir Ben anaonekana kuwa mwanafunzi wa Baba wa Taifa, nadhani hata Nyerere alikuwa akidhani hivyo. Kumbe huju jamaa alikuwa msanii tu akisema ndiyo kwa kile alichosema Mwalimu. Nyerere alipokufa kaanza kujilimbikizia mali na wenzake na wamefanya ulaji dili kubwaa kweli kweli. Kama wazungu wanamtuhumu Mugabe kwa nepotism na ufujaji wa fedha za umma kwa nini wanamwacha Ben?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 26, 2006

    UKIIBA NA UKATOKA MADARAKANI KWA AKILI INARUHUSIWA HIYO,LAKINI KAMA WEWE NI MWIZI NA KISHA UNAVUNJA KATIBA HAPO UNATAFUTA MATATIZO,HAPO AKILI NI KUIBA NA KISHA KUONDOKA KWA ETI KUHESHIMU KATIBA.MUGABE,(KAUNDA) ,MUSEVENI WANATAFUTA YANAYOMKUTA CHARLESI.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 26, 2006

    Huyu mtaalamu wa ubinafsishaji wa mashirika ya Umma, na anayekumbatia wawekezaji wa umma na mtaalamu wa kubinafsisha rasilimali za taifa letu, na ambaye hawasikilizi wananchi wake, anawaona hawafaii na amabaye anaona watanzania hawana akili ya kuongoza mashirika yao wenyewe badala yake anaona makaburu ndio wenye uwezo wakutuongozea mashirika yetu kumbe alianzaa kufaidi mafao tangia zamani, embu amngalia kitambi wakati mzee wetu kakonda. Ana mengi yakujibu maana Tanzania imeharibiwa na huyu mtu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...