vijana wa kikundi ch utamaduni cha shada kinachoundwa na vijana wa mjini bagamoyo wanaofuliwa chuo cha sanaa bagamoyo wakila tizi tayari kwa ufunguzi wa tamasha la sanaa la 25 la bgamoyo ambalo linafunguliwa kesho na jk, ikiwa ni mara ya kwanza mkuu wa nchi kufanya hivyo katika historia ya tamasha hilo la kila mwaka.

Niko hapa kuhudhuria hili tamasha, kaeni mkao wa kula....

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Matunda ya MtiMkubwa Tungaraza. Nasikia ndiye aliyekianzisha wakati akisoma hapo miaka hiyoo.

    ReplyDelete
  2. Basi mti mkubwa sasa ataitwa "mti mkubwa sana sana."
    Michuzi, macho yako tayari kutazama picha za tamasha.

    ReplyDelete
  3. Binadamu katika uhai wake huwa ana kumbukumbu fulani ambazo ktu hazitoki akilini mwake. Moja ya kumbukumbu zangu ambazo katu hazitatoka akilini mwangu ni wanangu wa Kikundi cha Shada.

    Cheche huzaa moto. Siku moja ya Jumamosi mwaka 1988 Nikiwa Chuo Cha Sanaa Bagamoyo watoto walinikuta nafanya mazoezi ya kuigiza pekee yangu. Wakakaa kutazama igizo langu. Basi wale watoto nikaanza kuwachekesha. Wakacheka sana tena mno. Walipomaliza kucheka nikawaambia "..tuchezeni ngoma.." Wakasema "..sawa.." Tukaanza kucheza ngoma ya Malivata ambayo ni mkabala wa ngoma ya Sindimba. Tukacheza sana. Ngoma ilipofika saa kumi na mbili jioni nikawaambia tuonane Jumamosi ijayo saa kama ya leo. Jumamosi iliyofuata wakaja wale niliokuwa na Jumamosi iliyopita na wenzao. Tukafanya tena mazoezi ya ngoma na kuigiza. Siku hiyo kulikuwa na maonyesho ya kila mwezi ya wanachuo. Nikamuomba Mwalimu Muhusika na maonyesho Mwalimu Richard Kyando ruhusa ya kuwapandisha watoto jukwaani. Mwalimu Kyando akanijibu "..No problem, how many items do you have?.." Nikamwambia "..Nina ngoma moja tu.." Akanijibu "..Ok, nitakuweka item ya katikati.." Nikamwamnia "..Asante mwalimu.." Niakmuomba Mama muhusika wa idara ya maleba/costumes aniazime maleba, naye akakubali kuniazima.
    Wakati wa onyesho nikawapandisha watoto jukwaani. Wakacheza ngoma vizuri sana kwa kulinganisha mazoezi ya siku mbili, lakini walikuwa wamezoea kutuona tukicheza zile ngoma kwa hiyo wakawa wanacheza kwa kuigiza wasanii wa chuoni. Walipomaliza kucheza wakafurahi sana. Nikawasifia sana halafu nikawaambia mazoezi Jumamosi saa yetu ile ile tisa mpaka kumi na mbili jioni. Stafillullahi, Jumamosi ilipofika nikajikuta kuna kundi kubwa sana la watoto limekuja mazoezini. Nikawa sijui jinsi la kuliendesha. Nikaamua kwamba siku hiyo nitawasimulia hadithi. Nikawasimulia hadithi nilipomaliza nikawambia tucheze ngoma wote. Tukacheza ngoma. Walipoondoka nikafikiria nini cha kufanya nao kwa sababu nimeshaanzisha jambo kwa hiyo nilitafutie namna ya kulimalizia. Baada ya kufikiri kwa muda nikaona bora nimuombe Mkuu wa Chuo ruhusa ya kuendesha kikundi cha watoto. Usiku nikamuendea Mkuu wa Chuo, Mwalimu Rashid Masimbi nikamwambia azima yangu na kumuomba ruhusa ya kuendesha kikundi cha watoto. Mwalimu Masimbi akanijibu "..Hamna tatizo. Hili suala limekuwa katika mijadala yetu na tumejaribu kulifanya, sasa kama wewe unajitolea kulifanya fanya ukihitaji msaada tutakusaidia.." Nilipotoka ofisini kwa Mkuu wa Chuo nikamfuata rafiki yangu Marehemu Basil Jia nikamueleza azima yangu na kwamba nimepata ruhusa kwa Mkuu wa Chuo kuitekeleza azima hiyo. Marehemu Jia alitokea kikundi cha JWTZ cha Kapteni Komba. Marehemu alikuwa fundi wa kupiga ala mbali mbali za kiasili na uchezaji na ufundishaji ngoma chungu nzima za kiasili. Marehemu Jia akaniambia "..Tungaraza, tutakuwa pamoja..Hiyo nia yako ni safi sana.."

    Jumamosi ilifuata watoto wakaja kwa wingi zaidi. Nikawagawanya makundi mawili moja ala uchezaji jingine la upigaji. Marehemu Jia akiwafundisha wapigaji mimi nikiwafundisha wachezaji. Baada saa moja ya mazoezi Marehemu jia akaniambia "..Hebu tujaribu kuunganisha pande hizi mbili tuone.." Kilichotokea hapo sikuweza kuamini macho wala masikio yangu. Watoto walipiga ngoma, wakaimba na kucheza utafikiri wamefanya mazoezi miaka mingi pamoja. Marehemu Jia akaniambia "..Hawa wanajua kucheza na kuimba lakini bado hawajaijua sanaa kwa hiyo itabidi uwafundishe usanii.." Sikumuelewa anamaanisha nini hasa. Basi huo ndiyo ukawa mwanzo wa Kikundi cha Shahada ambacho jina lake lilinikuliwa vibaya likawa Shada kwa sababu walifikiri nilikuwa namaanisha Shada ya chipukizi la maua.

    Mawili makuu nitakayoikumbuka Shada ni onyesho lao walilofanya UDSM, Nkrumah Hall mwaka 1988 miezi michahche baada ya kikundi kuanzishwa. Nakumbuka jinsi walivyowainua watazamaji vitini muda wote wa onyesho lao. Lakini nakumbuka zaidi jinsi walivyosahihisha kosa kwenye mchezo wao wa kuigiza. ilikuwa ni katika onyesho la tatu ambapo mmoja wao alijisahau na kuanza kuzungumza mambo ya onyesho la nne. Kwa sababu tulikuwa hatuna prompter ilikuwa vigumu kumstua kama kakosea. Mtoto mmoja ambaye alikuwa njee ya jukwaa akakimbia jukwaani huku anapiga kelele kama ni sehemu ya onyesho la mchezo. Mimi na wenzangu tukiwa tumepigwa butwaa kwamba mchezo umeharibika. Alipofika jukwaani akabadilili mwendo wa mchezo na wenzake waliokuwa wameelewa kwamba mwenzao alikuwa kapoteza dira ya mchezo wakampokea na kurudisha tena mchezo onyesho la tatu. Ndipo yule aliyekuwa kapotea akagutukia na kurudisha nyumba mchezo. Hakuna aliyeelewa kilichotokea isipokuwa sisi na Shada pekee yetu. Sitasahau kitendo kile katika maisha yangu yote ya uigizaji. Lakini sitasahau jinsi onyesho lilivyokuwa kiboko kiasi cha watu mbali mbali wakiwemo Maprofesa wa UDSM walivyokuja kuniuliza maswali mengi sana na kutoa pongezi.

    Jingine ni siku nilipomaliza chuo. Siku ya kuondoka Chuoni nilikuwa naondoka asubuhi sana ili kuwahi nyumbani kwenye arusi ya dada zangu ambao waliolewa siku moja. Nikadamka saa kumi na moja asubuhi kujitayarisha kuondoka chuoni kwenda Dar es Salaam. Wakati ninatoka bafuni nilipotazama mbele ya bweni nikakutana na kundi la watoto takribani ishirini. Nilipomaliza kuvaa na kutoka nje ya bweni nikakuta kundi kubwa sana la watoto na wengine wakiwa na wazazi wao. Wale watoto walikuwa wamekuja kunishukuru, kuniaga na kunisindikiza. Wakati najikusanya kuagana nao lile kundi likaongezeka sana. Watoto wakanisindikiza mpaka kituoni. Kufika kituoni nikawakuta watoto wengine wananisubiri. Nikapanda pick up nikawapungia mpaka walipopotea toka kwenye upeo wa macho yangu.

    Nilikiacha kikundi kikiwa na wanachama zaidi ya mia tatu! 300! Nilipomaliza nilimkabidhi mwanafunzi mwenzangu mwingine. Ninafurahi kujua kwamba kikundi bado kipo miaka kumi na nane! Miaka 18! tangu kilipoanzishwa. Ijumaa na Jumamosi nitakutana nao na pengine nitapanda jukwaani na wanachama waanzilishi.

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  4. Bwana Tungaraza nimesoma kwa makini kile ulichoandika bila kuachia njiani yaani neno kwa neno kama wasemavyo waswahili. Kama kila mmoja akilirithisha ujuzi na taaluma yake kwa watoto kama ulivyofanya wewe, nina hakika Tanzania ya miaka ishirini ijayo itakuwa imeondokana na matatizo mengi sana. Wewe ni mfano bora na nawaomba wengine wafuate nyayo.

    ReplyDelete
  5. Mti Mkubwa, kumbe title yako si bure aisee. Yaani kama kabila la mti inabidi nikuite mbuyu, hii legacy uliocho sio ndogo. Mola azidi kukusaidia katika juhudi zako za kusapoti utamaduni wa taifa letu.

    ReplyDelete
  6. Well done Tungaraza,
    Historia itakukumbuka kwa jema kama hili.

    Michuzi,naandika hii post jumatatu asubuhi kwa saa za hapa nilipo.Kama MtiMkubwa alipanda jukwaani na watoto hao nina uhakika ulipata picha,tafadhali usiache kuzituma.

    ReplyDelete
  7. Fidel Fidel Fidel! That's the way Brother kitu ambacho nitaongeza. anza kunusia kwenye kuandika Script ambayo inaonesha maisha yako hicho ulichokifanya si kidogo. Nakutana na vikundi vingi sana vya wapiga Djembe hawa ni Wamerikani weusi ambao wanajali culture inaniwia ngumu hasa wanulizapo tunataka kujua sanaa ya Kitanzania. Story yako ni kubwa na inauzika sasa Fidel jaribu kumcontact Charles Mhuto ana contact zangu siwezi (kuweka simu yangu hapa) tuone nini tutasaidiana. Maaana hawa mabwana wanataka kusikia something different. maana Afrika si djembe toka Senegal tu bali kuna vikundi kama hicho ulichokianzisha.

    ReplyDelete
  8. Mti Mkubwa Tungaraza kama wengine tunavyomuita "Mkulu" kwa lugha ya Kiluguru au Kizaramo ambao ni wenyeji wa mikoa ya Moro au Dar jina hilo linamaanisha "Mkubwa". Jina hilo kwa kweli limebeba dhima nzima ya huyu ndugu yetu maisha yake na matendo yake kwa ujumla.
    Kwa wale tuliobahatika sio tu kuishi naye lakini kuonja kikombe kutoka kwenye hazina yake kubwa ya Utu,ucheshi,upendo na mapenzi yake makubwa kwa wanadamu wenzie, naamini kabisa kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu kuwa tumebahatika!
    Ni ngumu kumuelezea Mkulu kwa maneno haya machache kwenye blogu, lakini napenda kuungana na mtoa maoni wa hapo juu kuwa kuna umuhimu wa ndugu yetu kutoa Script ya maisha yake...lakini si hilo tu! Mkulu ana kipaji cha kuigiza lakini pia kuandika na kuelezea mambo mengi yanayofanyika nyumbani na duniani kwa kila hali.
    Binafsi nimekuwa nikimlilia hii hazina asije akatumbukia nayo kaburini siku itakapowadia bila ya kuiweka katika hali ya maandiko ili sio tu sisi tuliobahatika kuishi nayo tupate kuisoma bali hata wale wasiowahi kumuona na hata wale watakaozaliwa kesho wapate nafasi ya kuona mchango wa Watanzania kwa Taifa lao.
    Naamini Mkulu baada ya kukumbushia kilio changu cha kuweka hazina yako katika maandishi, utafikiria tena suala hilo na kulipa uzito unaostahili.
    Nduguyo

    ReplyDelete
  9. Mti Mkubwa Tungaraza kama wengine tunavyomuita "Mkulu" kwa lugha ya Kiluguru au Kizaramo ambao ni wenyeji wa mikoa ya Moro au Dar jina hilo linamaanisha "Mkubwa". Jina hilo kwa kweli limebeba dhima nzima ya huyu ndugu yetu maisha yake na matendo yake kwa ujumla.
    Kwa wale tuliobahatika sio tu kuishi naye lakini kuonja kikombe kutoka kwenye hazina yake kubwa ya Utu,ucheshi,upendo na mapenzi yake makubwa kwa wanadamu wenzie, naamini kabisa kutoka kwenye sakafu ya moyo wangu kuwa tumebahatika!
    Ni ngumu kumuelezea Mkulu kwa maneno haya machache kwenye blogu, lakini napenda kuungana na mtoa maoni wa hapo juu kuwa kuna umuhimu wa ndugu yetu kutoa Script ya maisha yake...lakini si hilo tu! Mkulu ana kipaji cha kuigiza lakini pia kuandika na kuelezea mambo mengi yanayofanyika nyumbani na duniani kwa kila hali.
    Binafsi nimekuwa nikimlilia hii hazina asije akatumbukia nayo kaburini siku itakapowadia bila ya kuiweka katika hali ya maandiko ili sio tu sisi tuliobahatika kuishi nayo tupate kuisoma bali hata wale wasiowahi kumuona na hata wale watakaozaliwa kesho wapate nafasi ya kuona mchango wa Watanzania kwa Taifa lao.
    Naamini Mkulu baada ya kukumbushia kilio changu cha kuweka hazina yako katika maandishi, utafikiria tena suala hilo na kulipa uzito unaostahili.
    Nduguyo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...