jk akipiga ngoma kuashiria kufunguliwa kwa tamasha la 25 la sanaa jana usiku chuo cha sanaa bagamoyo. jumla ya vikundi na wasani 51 toka ndani ya nje ya nchi kushiriki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Picha safi sana! Motisha kwa wachezaji pia!

    ReplyDelete
  2. Hapa nimemkubali. Ukizingatia kuwa tokea enzi za mkololoni watu wamefunzika kudharau ngoma za kiasili , basi huu ni motisha sana.Katika kila nchi zilizoendelea muziki wenye kupewa heshima kubwa ni wa asili ya kwao. Kikwete ananifurahisha sana anavyotoa changa moto kwenye sanaa na hata michezo . Kwa maana ni miaka mingi imepita bila ya kuwa na kiongozi atambuaye umuhimu wa sanaa na michezo katika kujenga utaifa.

    ReplyDelete
  3. Yap! JK umerudi zama zileee! Hapa Mwananchi kuna pia ulichukuliwa ukipiga ngoma lakini ile ilikuwa baab kubwa kwani ulikuwa umevaa kitamaduni pia. Ulipoenda Uwanja wa Taifa kuishabikia Taifa Stars ulipiga track suit, sasa mbona kwenye ngoma umesahau kuvaa kibantu au Kiafrika? Nipe tano.

    Anyway hilo si jambo kubwa, la muhimu hapa ni kwamba umeweka mbele utamaduni wetu tangu haujawa Rais. Nakupa tano kwa hilo.

    ReplyDelete
  4. JK, kuna malaya mmoja ATL amedai atakukabidhi kalenda ya inayoonyesha utamaduni halisi wa mwafrika.

    ReplyDelete
  5. I can't agree more with you Chemi Che-Mponda.

    ReplyDelete
  6. eeeee mzeee hapo juu unaoonyesha umekasirika kweli!!lakini una kila haki ya kukasirika bwana ukweli tuukubali utamaduni wetu sio huu wa huyu dada anachokifanya kama ni kutafuta pesa basi machangudoa wa pale nyumbani wasisumbiliwe maana nao wanatafuta riziki au kutokana huyu anafanya kimataifa!!!!

    ReplyDelete
  7. Hii inamaana tukumbuke utamaduni wetu pia. Siyo wale wanaokwenda ulaya/marekani na kusomba mila na baada ya kuchezewa shele wanataka kuhalalisha mila hizo kwetu bongo. Tunaomba wakumbuke kuwa sisi watanzania tunatakiwa tubakie watanzania.

    Tunashukuru rais wetu anatukumbusha ngoma zetu. safi sana.

    ReplyDelete
  8. Mimi naona mwenye matatizo ni MICHUZI kwa sababu amekuwa akipiga kelele kila mara watu wasitumie lugha ya matusi katika blog yake lakini imeshindikana, sasa ningemshauri kama kuna utaalamu angefanya ili message za matusi zisiweze kuwa posted basi tungefurahi sana. Sijaona ubaya wa picha hata moja iliyo kuwa posted na bwana MICHUZI lakini naona aibu sana kwa kusoma matusi machafu na hakuna hatua anazo chokua kuifanya hii blog isiwe na hayo matusi. Bwana MICHUZI wengine tuna watoto wa umri mdogo ambao kila mara wanapenda kuingia katika blog yako kujionea maendeleo ya Tanzania ukizingatia wameondoka wakiwa bado wadogo na wanaipenda bado nchi yao sasa wanapokutana na matusi mazito katika blog yako na wewe kama mmiliki wa hii blog umeshindwa kabisa kuonya kwamba yeyote atakaye ingia katika hii blog na kupambana na matusi ni hiari yake! Nakushauri Mzee michuzi utafute mbinu kitaalamu kuzuia haya matusi kwa kweli yanawa affect sana watu ambao una post picha zao, na wengine sisi tunao ingia kwa nia njema kuangalia blog yako. Usipo angalia italeta chuki miongoni mwao na wewe mwenyewe. Kuna blog nyingi zinaweza kuchuja comments za watu kabla ya ku postiwa kwa hiyo hata wewe MICHUZI ungeweza kufanya vivyo hivyo. ASANTE SANA BROTHER MICHUZI NINATOA MAONI TU

    ReplyDelete
  9. Jamani haya mambo ya JK kupiga ngoma hayawezi kusaidia kitu , kama hataweza kutimiza ahadi alizozitoa ....

    ReplyDelete
  10. Inawezekana ni yeye mwenyewe michuzi akitaka kuandika mitusi anajiita anonymous. Shame on whoever...

    ReplyDelete
  11. You can take mzaramo out of Uzaramo, but you can never take uzaramo out of Mzaramo. Hongera mweshimiwa rais, mwongozo kwa mifano na vitendo.

    ReplyDelete
  12. nice...i love my president kwa kweli and i believe we have 5 years za kuwa suprised na kushangazwa na his ways...!way to go,JK!

    ReplyDelete
  13. Ni jambo la kusikitisha kuona watu wanampa JK credit simply kwa sababu anajichanganya na watu na kupiga ngoma , Binafsi sijali kama Rais anajichanganya au lah ! Ninachojali ni kiongozi ambaye atatuondolea matatizo yetu watanzania .

    Ni majuzi tuu JK amesema wanafunzi watakaosomeshwa na serikali katika elimu ya juu ni wale wenye division one tuu , hakuna hata mtanzania mmoja aliyelalamika kama kawaida yetu tunafurahia anavyopiga ngoma na anavyoenda masokoni kuulizia bei ya nafaka !

    Watnzania tumelishwa nini ? Nani katuloga ? Kwa nini hatuoni mbali ?

    ReplyDelete
  14. Way to go JK
    aliko

    ReplyDelete
  15. kwani jk akipewa kalenda k2 gani.itakua inamliwaza mama akiwa hayupo kama mnahisi ule ni umalaya washamba nyinyi.rasi mwenyewe kaisha tupigia debe kina dada tuvae vimini na m2 asituguse kasema kufanya kinyume na hapo ni ushamba uliopitwa na wakat.na m2 yoyote asithubutu kumsingizia yeye kapiga marafuku.mzee social huyu.wasenge nyinyi.picha za mwenzenu nyinyi maneno yanawatoka.kumamae zenu watumieni wazazi hela za mboga popote walipo.

    ReplyDelete
  16. mr jk wasaidie watoto wa babu sea!Please daddy.

    ReplyDelete
  17. Hivi serikali itaendelea kusomesha watoto wa shule bure mpaka lini? I don't see a reason for Government kusomesha mtoto yeyote either kapata Div I, II, or III. Baada ya uhuru, in the 1960's and 1970's it made sense for the Government kusomesha watoto wa shule wenye grade nzuri. We needed few people to take over some of the Govenment jobs and so forth. But, 40 something years later? tunataka watoto wetu wasomeshwe bure na serikali? Wake up people! Take care of your own kids education!they are not Government kids.

    ReplyDelete
  18. Anon ,

    Hapo juu stop being naive and stupid ! Please take time to read others comments before exposing kutoelewea kwako, kitu tulichokuwa tunazungumzia ni serikali kuwakopesha hela wanafunzi wa vyuo vya juu na sio kuwalipia . Na hili jambo linafanywa dunia nzima hata nchi zilizoendelea zinafanya hivyo .

    Kwa hiyo kwa uwezo wako mdogo wa kufikiri unadhani mzazi analipwa kima cha chini anao uwezo wa kumsomesha mtoto wake chuo kikuu mind you is only being paid shs 65,000 kwa mwezi !

    Tatizo watu wengi wanaangalia mambo katika mtazamo mdogo .

    ReplyDelete
  19. Waungwana, hii hali ya kutukana na kuwavunjia watu heshima imekithiri, na hivyo hatutaendelea kuivumilia isipokuwa kuifanyia kazi. Nimeunganisha kikundi cha watu watano wenye nia dhahiri ya kupambana na hili suala. As from now on, we will crack down and find out which computers were used to send those profanity massages. Hatuna uwezo wa kukuchukulia hatua yoyote kisheria, bali tutaweka majina ya wahusika humu ili pengine hao waliotukanwa ndio washughulike na wewe, hili si jambo la mchezo maana hali hii imetuchosha.

    ReplyDelete
  20. Kigerera na Trio Kaka,
    Na assume and hopefully ndio hivyo, mko nje ya nchi na uongo family zenu mnaweza kuziendesha japo kwa kubadilisha mboga. Ninachoweza kuwashauri nikuwa wakumbukeni watoto wa dada zenu kaka zenu na wengineo mlionao karibu ili wapate hiyo elimu. Ninahakika mnaweza kumudu dola 2000 hivi kwa mwaka. Watanzania ni wajinga wakutupwa. Mnawatetea lakini leo hii wanaweza kuandama kupinga hicho mnachosema. Rejeeni suala la mapanki, waliandamana wakati jioni wanaenda kukuta kitoweo ni mapanki.

    ReplyDelete
  21. Hongera Bwana Michuzi kwa picha nzuri ya Rais Kikwete akienzi utamaduni kwa kuzidunda ngoma kule Bagamoyo. Huenda ni inshara nzuri kuwa suala la utamaduni litapewa kipaumbele katika ajenda na sera zake.

    Hata hivyo, pamoja na hilo ningependa kuungana na wale wote waliosema kuwa serikali ya Bwana Kikwete haikufanya vizuri kuamua kuwa eti ni vijana wenye division I (wavulana) na I na II (wasichana) ndiyo watakaokopeshwa ili kuendelea na masomo ya chuo kikuu. Jambo hili sidhani kuwa limefanywa kwa kutafakari vyema matokeo.
    Kwanza, lazima tukubaliane kuwa Elimu ni Ufunguo wa maisha. Watu wengi leo hii Tanzani wana hali nzuri za kimaisha sababu ya elimu zao au za ndugu zao. Elimu ndiyo mtaji pekee wa kuaminika katika dunia ya leo ya utandawazi. Cha maana ni kuwa iwe elimu bora na inayouzika popote pale duniani.
    Kwa hiyo, kwa kitendo cha serikali kuamua kwamba mikopo ya elimu itolewe kwa makundi hayo tu ni kuangamiza wengi. Ni kujenga matabaka (ambayo tayari yamekwishajengeka) ya wenye kusoma (na kwa hiyo wenye nazo) na wasiosoma (na kwa hiyo wasio na chochote). Mgawanyo huu utaipeleka nchi kubaya. Wenye nacho wataendelea kuwatumikisha na kuwanyonya wasio nacho. Tutaingia katika mfumo unaofanana na utumwa.
    Kama serikali imeamua watu wajisomeshe na kwa kuwa wazazi wenyewe uwezo wetu ni mdogo (kiuchumi), na serikali imeamua kutoa mikopo, tafadhali iheshimu sheria iliyopitishwa na bunge iliyokuwa inasema kuwa kijana Mtanzania anayepata udahili (admission) katika chuo kikuu chochote hapa nchini basi huyo ndiye anayestahili kupata mkopo. Jamani, huu ni mkopo. Mtu huyu hapewi fedha hii moja kwa moja. Ni fedha ambayo atairejesha pindi amalizapo masomo yake. Naiasa serikali ya Bwana Kikwete irejee kule.
    Viongozi wetu wa dini ingefaa waishinikize serikali kuzingatia jambo hili, kwamba, sifa ya mtu kupata mkopo ni kupata udahili katika chuo kinachotambulika na serikali, basi.

    Jambo jengine ni suala la umeme. Ni wakati serikali ikiri waziwazi kuwa tatizo la umeme ni kubwa na hatuliwezi sisi peke yetu (kama nchi). Serikali itangaze kuwa hili ni janga, ni janga katika kipimo kile kile kama yalivyo majanga mengine ya njaa, ukimwi, malaria, tsunami (Asia), kimbunga (kama cha katrina kule USA) na njaa (miaka ya 80 kule Ethiopia). Hapa tunahitaji mataifa ya nje yaingilie kati kuweka mambo sawa. Kutusaidia kwa technical know-how na hata mtaji wa fedha wa kuanzisha vyanzo vingine vya umeme (makaa ya mawe kule kiwila; upepo; jua na kadhalika). Injini za kukodi za kuzalisha umeme ni mzigo mwingine kwa sisi walipa kodi, Mtera limejaa tope, hata ukileta mvua za WaThai (bahati mbaya wamepinduliwa) bado tatizo halitaisha. Kinachotakiwa ni ufumbuzi wa kudumu. Watu wengi wamejiajiri na kuajiriwa katika biashara zinazotegemea umeme. Umeme usipokuwa wa uhakika, unategemea watu hawa waishi vipi.

    Kwa hiyo, Mheshimiwa Rais piga ngoma lakini ukumbuke kuwa kuna masuala mengine yanayodai your immediate attention. Watu wanapima mwelekeo wa uongozi wako kwa namna unavyoshugulikia matatizo hayo niliyoyajadili hapo juu. Nadhani umeshasikia kuwa wengine wameshaanza kutafsiri usemi wako wa Ari mpya NGUvu mpya na KAsi mpya kuwa ni ANGUKA. Angalia bwana tusije anguka ndani ya mwaka mmoja tu ya uongozi wako. Kila la kheri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...