juma nature akigawa vitabu mashuleni wakati wa ziara zake za mikoani. masikini msanii huyu mahiri kakosa kwenda copenhagen kwenye tuzo za mtv.alaumiwe nani? nasaka mchawi nikimpata ntammwaga. stei tyund

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Michuzi, hakuna haja ya kusaka mchawi hapa. Hao MTV ni wabaguzi na hawana mpango wala maana yoyote!! Malengo yao ktk kutoa tuzo hilo ni kujitafutia soko, full stop.
    Kama walimtaarifu Nature kuwa ameteuliwa kugombea tuzo hilo na wanashughulikia safari yake ya kwenda huko kwa nini wasiwasiliane naye kuhusiana na mambo ya safari?
    Pili, kwenye award show hawakutaja hiyo nafasi ya African Act award hata kidogo!!!! Walionyesha awards zingine zote kasoro hiyo, maana yake nini??
    Heri Nature alipobaki nyumbani na hakujiahangaisha kwenda kwenye show.
    Muziki TZ inalipa siku hizi kwa hawa vijana, na Nature ni moja ya wanamuziki wenye jina na malipo mazuri kwa kazi zao, Hashindwi kununua tiketi hata siku moja na kama walimuahidi kumtumia tiketi hakuona sababu ya kununua kwa hela zake.
    Kama lilivyo kwa maendeleo ya bara letu kwa ujumla, Nchi zilizoendelea huwa hazipi nafasi kwa Afrika, iweje leo kwenye mambo ya Muziki waipe nafasi? Yaani hata ile kutangaza kuwa kuna wanamuziki wa Afrika, hawakutaja. Au ndiyo kama zile za Oscar na Grammy, wanapofanya pre-show awards ili kutoa awards kwa 'genre' ambazo si kubwa sana? Na mara nyingi wahudhuriaji ni wachache sana.

    ReplyDelete
  2. Very smart guy....way to go J. Nature, way to go.

    ReplyDelete
  3. Bw Michuzi sidhani kama kuna haja ya kutafuta mchawi!! Mchawi wa nini na asaidie nini? hapo cha kuangalia ni: Nature kapoteza muda kiasi gani, pesa kiasi gani na kaumia kiasi gani na hao MNet watamfidia vipi? swali: Je Nature alipata taarifa ya kimaandishi au ya kizushi au ilitangazwa kwenye vyombo vya habari? baada ya kupata majibu ya maswali haya, kinachofuata ni nature kutafuta mwanasheria aliyetulia amsaidie kuwaeleza hao MNet wampooze huyu Bwana Mdogo. ni muda mrefu amekaa bila kujishughulisha na its obvious kuwa amepoteza muda mwingi na pesa pia kwa ajili ya habari hii ya MNet. lazima Nature ameumia sana na anastahili kulipwa damages kwa uchafu huu walioufanya Mnet, yaani wamemdhalilisha na kusababisha baadhi ya watu kutomuamini nature na kuona kuwa alikuwa anajikomba kwao!! na kujifagilia!!
    hao ni kukomaa nao tu, wamlipe USd kadhaa apooze maumivu. i believe akiwasogeza mbele ya haki watampa fweza tu (General Damages), hakuna ubaguzi wa rangi na kupotezeana muda. ni wabongo wangapi wametoa mijicho kwenye Tv na nature hawakumuona! ni wangapi wamem-support kwa mail na kupoteza pesa na mafuta ya generator (si unajua bongo hakuna umeme) na bado nature hata kwenye mabaki ya washiriki hakuonekana!!
    atafute ushauri wa kisheria

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...