Mtanzania mwenzangu,
Ujumbe huu unakujia kwa sababu wewe umo kwenye familia ya kitanzania ya wanablogu.
Kwa muda mrefu imekuwepo nia ya kukutana ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu nchi yetu. Muhimu zaidi ni kuangalia jinsi gani blogu zinaweza kutumika kama taasisi mpya za umma kwa nchi changa kama yetu ya Tanzania.
Sasa la mgambo limelia...kuna jambo. Tafadhali tembelea www.harakati.blogspot.com ili uone mapendekezo muhimu ya mkutano wetu wa kwanza. Ukishatembelea usikose kuacha maoni yako kama unaafiki tarehe na muda uliopendekezwa.
Ahsante.
Jeff Msangi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Ahsante kwa taarifa hii.Ni kweli kabisa kwamba blogu hivi sasa zinatumika kuleta maendeleo na mapinduzi fulani duniani kote.Mfano mzuri ni kule Misri.Kwa muda nilikuwa najiuliza ni lini watanzania nasi tutaanza kutumia tekinolojia kama hii kufikisha ujumbe kwa serikali na wananchi wenzetu tukizingatia kwamba magazeti ya nchini kwetu mengi ni "pro government" na hivyo serikali haipati maoni ya wananchi wa kawaida.
    Jeff Msangi na wenzako,hongera sana kwa wazo hili.Historia itawakumbukeni,hata mkishindwa mtakumbukwa kwa kujaribu.Nitaungana nanyi siku hiyo nikiweza.

    ReplyDelete
  2. Duh! I never thought this was possible.Jeff Msangi,you are genius!

    ReplyDelete
  3. Pengine wazo zuri kuliko yote ambayo nimeyasikia mwaka huu.Hongera Jeff Msangi.
    Mkiweza kuanzisha mchakato wa namna hii,umoja wa namna hii, ni wazi kabisa kwamba mnaweza pia kuungana na kusaidia watoto yatima,walemavu,walioathirika na ugonjwa wa akili(mental health),kinamama na vijana wanaohangaika nk.Mnaweza fanya hivi kwa kuchangishana hata dola moja moja tu kwa siku.Kwanini sisi watanzania ndio tuwe kipimo cha umasikini duniani?Kwani sisi,pamoja na hali zetu duni,hatuwezi kusaidiana wenyewe na kuachana na tabia ya kuwa ombaomba wa nchi za magharibi?

    MAKWETA

    ReplyDelete
  4. michuzi naona unaogopa sana kugungiwa globu yako mpaka umetoa habari ya jana kuhusu mtoto wa pm,manake watu walibwabwaja sana.

    ReplyDelete
  5. Hii imetulia sana ndugu zangu, acha tushiriki ili kuleta mawazo mpya ya umoja... nadhani italeta kuheshimiana zaidi, coz tukakuwa wa karibu zaidi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...