Mdau mkuu wa Libeneke na nanihii
THIS BLOG IS PROUDLY SPONSORED BY VODACOM, TANZANIA'S LEADING CELLULAR NETWORK. | NDOVU SPECIAL MALT "THE SMART CHOICE" Karibu katika hii Globu ya jamii. Una karibishwa kutoa maoni yako yoyote yatakayo jenga taifa letu. Ila nawaomba tuweze kujieshimu kila mmoja wetu kwa kutumia lugha zisizochafua hali ya hewa. Yaliyomo humu hayahusiani kwa vyovyote vile na hariri za magazeti ya Daily News, HabariLeo na Sunday News. Maoni yanayotolewa na wasomaji si ya globu ya jamii, ni ya mtoa maoni isipokuwa pale itavyoeleza vinginevyo. Akhsanteni sana na tuendeleze Libeneke.



 

Tuesday, March 14, 2006
warsha ya muziki

bob rudala wa inafrika band akichangia katika warsha ya muziki bagamoyo leo
 
© Michuzi | Tuesday, March 14, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 17
Sunday, March 12, 2006
posta ya zamani

mojawapo ya majengo ya zamani ya dar ni posta ya zamani
 
© Michuzi | Sunday, March 12, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 7
jk na miss utalii wa bongo

jk akiwa na witness manwingi ambaye ni miss utalii bongo na pia miss utalii africa 2005. jana alishika nafasi ya miss personality. hapa ni ikulu ambapo jk alikaribisha wahiriki wote mia na ushee hiyo jumamosi mchana na jioni mkewe mama salma alikuwa mgeni rasmi ambapo miss south africa Henri Van Schalkwk ndie aliyetangazwa miss tourism model of the world 2006 kwenye ukumbi wa ubungo plaza jana usiku
 
© Michuzi | Sunday, March 12, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 24
bongodalisalaaaaam!

vijana wakijimwaya na chakacha bongo
 
© Michuzi | Sunday, March 12, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 40
madentidit
 
© Michuzi | Sunday, March 12, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 20
mh. amina chifupa wa mpakanjia

huyu ndiye mheshimiwa mbunge amina chifupa wa mpankanjia a.k.a mama shughuli, mmoja wa wabunge mashuhuri vijana
 
© Michuzi | Sunday, March 12, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 18
sumo ndani ya bongo

wacheza sumo wa kijapani wakionesha namna ya kucheza mchezo huo katika ukumbi wa don bosco jana
 
© Michuzi | Sunday, March 12, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 1
Friday, March 10, 2006
Afrikali

hawa ndo vijana machachari wa afrikali group, kundi linaloundwa na vijana wengi toka sisi tambala. juzi tu walikuwa los angeles na mwezi wa nne wanaelekea sweden pengine na finland. anaewahitaji anistue...
 
© Michuzi | Friday, March 10, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 2
makene kazini

basi kaka makene hivi ndo mambo yanavyokua-ga kwenye nguna
 
© Michuzi | Friday, March 10, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 6
Daladalaz

we damija, nimekuambia hama vinguguti uje kariakoo, umegoma. ona sasa washindwa panda basi
 
© Michuzi | Friday, March 10, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 4
Thursday, March 9, 2006
wabongo stareheni

baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi wa tanzania music awards jana dar
 
© Michuzi | Thursday, March 09, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 17
Wednesday, March 8, 2006
waraka toka kwa simba

Kwa kupitia vyombo vya habari inawezekana ukawa umeona kuna kundi dogo la wabunge wa kipindi kilichopita waliokutana Dodoma tarehe 27 Desemba 2005 na kuamua kuunda Taasisi walioipa jina la “TANZANIA ECONOMIC FORUM”.Kwa heshima, napenda kukuarifu rasmi kwamba jambo hilo lilitokea, na kwamba Taasisi hiyo inakusudiwa iwe ya kuwaunganisha wananchi wa kila aina wataohamasika kujiunga nayo.Madhumuni ya barua hii ni kujaribu kukushwawishi, kwa namna ya peke kwako, uwe mmoja ya waasisi wa chombo hiki, ambacho kitashugulikia zaidi masuala ya kiuchumi kwa jinsi yanavyogusa maisha ya Mtanzania wa kawaida.Katika kipindi cha miaka kumi ya awamu wa tatu ya utawala wa Mheshimiwa Rais Benjamin Mkapa, nchi yetu ilishuhudia mambo makubwa matatu yaliyoathiri hali ya maisha ya Mtanzania.Mabadiliko ya mfumo wa kisiasa na kiuchumi ambayo yalileta demokrasia ya vyama vingi pamoja na utekelezaji wa sera za uchumi.
Ndani na muongo huu nchi ilikabiliwa na misukosuko ya kisiasa baina ya vyama tofauti na ndani ya vyama vyenyewe. Kadhalika kipindi hiki kilionyesha dhamira ya serikali kujitoa katika umilikaji wa rasilimali za Taifa na udendeshaji wa uchumi. Sekta binafsi ilipewa fursa ya kushika hatamu na kununua mashirika yaliyokuwa ya ummaJuhudi za kufufua Ushirikiano wa Africa ya Mashariki pamoja na kubadilisha mfumo wa ushirikiano na nchi za kanda ya kusini mwa Afrika.
Ni Katika kipindi hiki hatua za kisheria zilifikiwa na kuielekeza nchi yetu kwenye soko la pamoja na nchi za kanda ya Africa Mashariki (EAC) na nchi za kusini (SADC) Utandawazi ulipamba moto kwa kasi kubwa zaidi katika kipidi hiki cha utawala wa awamu ya tatu. Athari za mtindo wa biashara huria ya kimataifa zilijitokeza kwa nguvu sana wakati huu. Kushiriki kwa Rais Mkapa katika tume ya kongamano mbalimbali za kimataifa sio tu kuliipatia heshima nchi yetu, lakini pia kuliwafungua macho baadhi ya Watanzania juu ya ushindani mkali wa kibiashara na kiuchumi unaotukabili na nchi zingine.
Haya Mambo matatu hayakuwa mapya kabisa. Yote yalikuwapo siku zilizopita kwa kiwango Fulani, lakini yalipata nguvu sana kuitekelezaji katika muongo huo.Athari iliyojitokeza zaidi kwa maisha ya Tanzania, Juu ya mambo haya matatu, ilikuwa ni kiuchumi. Serikali za awamu zilizopita kwa vipindi mbalimbali zlijaribu kubuni na kutekeleza mbinu za kusaidia.Pamoja na juhudi za serikali zetu zilizopita, wabia wetu wa kimataifa nao walitoa fursa mbalimbali ambazo zilikusudia kutuwezesha kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi. Mifano michache itafaa kuiangalia :-
“Open General License” – OGL ( Tangu awamu ya Kwanza)
“Commodity Import Support” CIS
“Debt Conversion Programme”
“Microfinance Policy”
“Economic Empowerment Policy”
“MKUKUTA, MKURABITA, AGOA, EBA N.K”
Sambamba na hayo, awamu ya tatu ya Rais Mkapa ilijitahidi sana kujenga misingi imara ya uchumi wa Jumla (Macro-economy). Baada ya kuimarishwa utaratibu na tabia ya kulipia madeni, kuongeza ukusanyaji wa kodi, kudhibiti mfumuko wa bei na thamani ya sarafu ya Taifa, kuboresha miundo mbinu ya usafiri na mawasiliano, na baada ya kuonyesha dhamira ya kuipa nguvu sekta binafsi na kuitambua kama mtambo wa kuzalisha mali na kukuza pato la Taifa, wawekezaji walivutiwa na kuanza kuwekeza katika sekta mbali mbali za uchumi.Serikali ya awamu ya tatu ilifanya marekebisho makubwa katika sekta ya fedha na kuvutia mabenki ya nje kuingia nchini. Huduma za aina hii zilisisimua kwa kiasi kikubwa biashara ya kimataifa katika sekta hasa za madini, Utalii na uchuuzi wa bidhaa na nje na ndani.Haya yote ni mazuri na lazima yaendelezwe kama ambavyo Mheshimiwa Ras Kikwete ameahidi kuyaendeleza katika awamu ya nne. Lakini ni vema tutambue kwamba mafanikio haya kwa kiasi kikubwa sana yamewagusa Wananchi wachache waliomo katika sekta rasmi ya uchumi.Watanzania wengi bado wana hali duni ya kimaisha na hawajaguswa na faida zilizopatikana katika sekta ya uchumi wa kisasa. Rais Kikwete ameahidi juhudi za kuinua hali ya maisha ya Watanzania kwa kuwaingiza kwenye njia kuu za Uchumi wa kisasa.Tunaamini kwamba, kwa misingi iliyokwishawekwa katika awamu zilizopita, hasa awamu ya tatu kiuchumi na tukizingatia neema za maliasili ambazo tunazo nchini, awamu ya nne imekuja na ari ambayo inaweza kabisa kutimiza matarajio ya wananchi. Lakini uwezekano wa kutimiza matarajio hayo utategemea sana juhudi za tawala katika ngazi za serikali kuu, Tawala za Mikoa, Mamlaka mbalimbali za dola, Taasisi mbalimbali za kiraia (Civil society) na hasa juhudi za wananchi kwa jumla wao.Tukienda pamoja na kushirikiana na kwa kueleweshana juu ya vita vya kiuchumi inavyoikabili nchi yetu, ni dhahiri Serikali ya awamu ya nne itaweza kutimiza ahadi zilizotolewa kwa wananchi. Neema za maliasili tunazokusudia hapa ni pamoja na watu wenye fani mbalimbali, na wenye moyo wa uzalendo unaowahurumia Wananchi masikini wanaotafuta riziki zao katika sekta ya uchumi isiyotambulika.Ili tutambue uzito wa tatizo la maendeleo ya wananchi wa Tanzania, ni vema tuchambue jinsi tulivyo!Katika Wananchi takriban milioni 35, nusu yetu ni wazee wenye umri wa miaka 65 na zaidi, pamoja na watoto na Vijana mpaka umri wa miaka 18. Waliobaki ni wananchi milioni 17.5 wa umri kati ya miaka 18 na 65 ambao ndio nguvu kazi wanaobeba mzigo wa kuwatunza watoto, Vijana na wazee.Takwimu na taarifa rasmi zilizofikishwa katika kamati ya Fedha na Uchumi ya bunge mwaka jana zilionyesha kwamba wananchi wanaotambulika katika sekta rasmi ya uchumi ni milioni mbili tuu.. Hawa ndio wanaofanya kazi za Kuajiriwa na ujiajiri. Ndio wanaolipa kodi kwa utambulisho rasmi, pamoja na kutumia huduma za kibenki na fursa mbalimbali zilizoandaliwa na dola kwa ajili ya maendeleo ya sekta binafsiWananchi milioni 15.5 wanafanya kazi za kila aina, katika sekta zote za uchumi bila kujulikana na vyombo vya dola. Hii ndiyo sekta kuu ya pili ya uchumi usiojulikana kwanjia sahihi na rasmi. Wananchi hawa wana rasilimali zao ambazo hazitambuliki na kwa hiyo haziwasaidi katika maendelo ya kisasa. Hawakopesheki, hawalipi kodi na hawawezi kutumia fursa nyingi zilizoandaliwa na serikali kwa ajili ya maendeleo yao. Hata hivyo wanaona jinsi nchi ilivyobadilika sura kwa maana ya majengo mapya, mabarabara, magari, umeme, usafiri na mawasiliano.Wananchi hawa milioni 15.5 wanatambua faida zinazopatikana katika sekta rasmi. Wachache wanaojaonja anasa za utandawazi kwa matumizi ya simu za mkono, TV, na radio. Lakini wengi wao bado wako mbali sana na faida za uchumiwa kisasa ambazo kama tunavyoona zinawagusa wananchi milioni mbili tuu. Na hata hao milioni mbili, ni wachache miongoni mwao ambao ni wachezaji wa kweli katika shuguli za uchumi wa sekta rasmi. Katika Kipindi cha mwaka uliopita wa fedha 2004/2004, idadi ya akaunti katika mabenki yote nchini ilikadiriwa kama laki tatu tuu (300,000). Sehemu kubwa sana ya hata wao wananchi milioni mbili waliomo katika sekta rasmi ya uchumi hawapati faida ya huduma za benki. Nao pia hawakopesheki katika mazingira yaliyopo hivi sasa.Suala la mzingi, ambalo ni lazima tulipatie jawabu haraka, ni jinsi tutavyoweza kuvuta nguvu zetu za kitaifa ili nchi yetu ikabiliane na ushindani wa kibiashara na kiuchumi katika mazingira haya ya utandawazi.Tanzania imo vitani. Ni vita ya kiuchumi inayolazimisha tufungue mipaka yetu, siyo tu kwa jili ya bidhaa za kutoka nje lakini pia kwa ajili ya wafanyakazi na wawekezaji ambao wanavutiwa na fursa nyingi za kujitajirisha zilizomo nchini mwetu.Hii ni hali ambayo haiepukiki na wala si busara kujaribu kujiepusha nayo. Tunachotakiwa kufanya haraka sana ni kuwashitua wananchi wetu, kuwasisimua na kuwaanda kwa vita kali ya kiuchumi. Mahindano yetu na nchi zingine yanatutaka tuzalishe mali katika sekta zetu zote za uchumi zitazoongeza pato la Taifa kwa kasi kubwa zaidi.Tanzania ina nafasi na fursa ya kufikisha katika masoko ya Dunia bidhaa zinazotakiwa duniani. Tusipozalisha bidhaa hizo sisi wenywe pamoja na kushirikiana na tuwatakao kwa mtindo utaolinda maslahi ya taifa letu hivi sasa, baadaye (na baadaye hii ni miaka kama kumi na tano hivyi) Dunia itatulazimisha tufanye kama Dunia inavyotaka.Kazi ya kuwatayarisha wananchi kwa mapambano haya ya kiuchumi, na kazi ya kuvuta nguvu zote za Taifa kwa ajili ya vita hii, haiwezi kufanywa na Serikali peke yake, Bunge peke yake, Vyombo vya wafanyabiashara au kundi lolote peke yao.Tunadhani ni bora tuunde chombo kitachowajumuisha watu wa fani mbali mbali, makundi ya kila aina, viongozi wa Taasisi za kisiasa, Kibiashara, kiroho na taaluma, Chombo ambacho kitachambua kwa undani mipango yote na fursa zilizoandaliwa na serikali kwa ajili ya kuwawezesha wananchi kujiendeleza. Kwa mfano, ni watu wachache mno wanaojuwa habari za MKUKUTA, MKURABITA na mifuko mbali mbali yenye malengo ya kuwasaidia wananchi. Chombo hiki kitatafiti taratibu zote na fursa zote zilizowekwa na serikali yetu, na hata Taasisi za kimataifa, ambazo zinakusudia kutuwezesha kukuza uchumi na kuboresha maisha ya wananchi. Taarifa sahihi juu ya yote haya itakuwa inatolewa kwa namna ya kuwaelimisha watu ili waweze kuchacharika katika sekta zote za Uchumi.Tunakusudia kuwashwawishi wananchi wanaharakati wa maendeleo, wajiunge na chombo hichi ambacho madhumuni ya msingi ni kuhimiza maendeleo ya wananci kwa kujenga taratibu sahihi za ushirikiano endelevu baina ya serikali na watu.Tarehe 18 Machi 2006, Jumamosi saa nne asubuhi tutakutana katika ukumbi wa hoteli ya Royal Palm Movenpick, Dar es salaamNi maombi na matumaini yangu kwamba utakubali kujiunga na chombo hiki cha kiraia ambacho azma kuu ni kujenga ushirikiano wa dhati na vyombo vya dola ili kwapamoja tupigane vita vya kuondoa umasikini na kujenga uwezo wa nchi yetu kwa mashindano ya kiuchumi na mataifa mengine. Kujiunga kwako nacho kutakipatia chombo hiki heshima na kutuwezesha tuaminike na tuwe msaada mkubwa kwa serikali katika juhudi za kuwaletea wananchi maendeleo.Tunamini kwamba, pamoja na wewe, idadi kubwa ya wananchi wasiopungua mia moja watakuwa amejiunga na kulipia ada za uanzilishi wa Taasisi hii. Rasimu za katiba inandaliwa ili baada ya kukubaliwa na kikao, ambacho kitachagua uongozi, tutachukuwa hatua za usajili na kuanza shuguli zitazokusudiwa.


(Mwenyekiti wa Muda)

Iddi Simba

Kwa maelezo zaidi andika kwa http://uk.f537.mail.yahoo.com/ym/Compose?To=info@tanzaniaeconomicforum.org

PS: Picha haihusiani na waraka huu. ni kuonesha jinsi pilau linavyogawiwa kwenye shuhuli...
 
© Michuzi | Wednesday, March 08, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 4
Tuesday, March 7, 2006
manzese

hapa ni manzese. ajali zimepungua baada ya uzio huu kuwekwa kwani yatakiwa mtu kuvuka pahala pake.
 
© Michuzi | Tuesday, March 07, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 5
kamati ya harusi

ule mkao wa kula na ndoa ya mkeka vilizaa hii harusi ambapo wanakamati tulofanikisha twatambulishwa na mwenyekiti wetu
 
© Michuzi | Tuesday, March 07, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 4
ndesanjo hapa ni marangu

mambo ya marangu kyara
 
© Michuzi | Tuesday, March 07, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 3
mkao wa kula

tofauti na ndoa ya mkeka (iso rasmi) na ya kawaida ni kwamba ya mkeka hakuna shaba kama hii ya kawaida ambapo jamaa wamekaa mkao wa kula wakingoja sahani la pilau huku wakiwa wameshanawa (maji) kiasi cha nusu saa iliopita. makene nakuona udenda wakutoka hapo
 
© Michuzi | Tuesday, March 07, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 4
ndoa ya mkeka live!

hii ni ndoa ya mkeka ambayo ni ndoa ya kiislamu ambapo muoaji anapeana mkono na ba mkwe na kujibu maswali ya ndoa akiongozwa na shehe. mke mtarajiwa huwa chumba kingine, viapo vya ndoa vikikamilika ndipo mume anaenda kumshika mkono. neno 'ndoa' ya mkeka limekuja baada ya zoezi hili kufanyika wakati mtu anafumwa na mtoto wa mtu ambapo kinachihitajika hapo no mkeka na shehe tu. picha hii ni ndoa halali ilofanyika ijumaa ilopita kule kigamboni...
 
© Michuzi | Tuesday, March 07, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 3
manara

huyu ni haji manara, mwanae sunday manara 'kompyuta', ambaye bahati mbaya ama nzui kipaji chake ni cha kuongea na si kabumbu kama alivyokuwa baba yake. haji ni mtangazaji mashuhuri wa redio na pia mtoa mada moto kwenye mihadhara ya soka kama anavyoonekana hapa akichangia sababu za kuporomoka kwa soka bongo
 
© Michuzi | Tuesday, March 07, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 8
wanae daktari hukwe zawose

jina la dk. hukwe zawose laendelezwa na vijana na ala zake kama kawa
 
© Michuzi | Tuesday, March 07, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 2
deliniuzu

haka ndo kachumba ka habari ka deliniuzi nnakosotea waya mie. nimekaweka makusudi kwani naomba mnisaidie mawazo. hivi sasa kazi ya ajira bomba na mshiko si mbaya. tatizo biashara nayo imechanganya na ili iendelee kumea yahitaji muda wangu wote. niko njia panda. nijimwaye kwenye sekta binfasi ama niendelee na jobu la ajira? naomba msaada jamani. niko njia panda
 
© Michuzi | Tuesday, March 07, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 25
Monday, March 6, 2006
salaam kwa igp mwema...

walinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi wakiingia kwenye karandinga kufuatia salaam kwa igp mwema zilizotolewa leo na jamaa waliovamia standard chatered bank na kuingia kizani na 300m/- za kampuni ya shivacom kabla hawajakabidhi benki. walinzi 12 wamechukuliwa kuhojiwa na inasemekana jamaa watano, mmoja demu, walihusika na tukio hilo lililokuja masaa 48 tu tangia igp mwema aapishwe.
 
© Michuzi | Monday, March 06, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 9
mwaka 1990 haukuwa mbaya...

mwalimu akiwatambulisha madiba na winnie kwa wabongo waliofurika neshno kumpokea baada ya kusota gerezania miaka kibao...
 
© Michuzi | Monday, March 06, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 5
jeff, husikii tu???????

hivi we jeff una nini lakini... hata upande wa urusi ambako bei ni sh 500 we unadandia ukuta. ebwanaaa eeee tumekuchoka sasa. acha usulubiwe...
 
© Michuzi | Monday, March 06, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 0
Sunday, March 5, 2006
mwaipopo, ujumbe umefika!

sasa we john mwaipopo ndo nini kuturusha roho na kadaladala kako namna hii?
 
© Michuzi | Sunday, March 05, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 5
mapokezi ya madiba

wanafunzi wa jangwani wakisubiri kumlaki madiba siku alipozuru bongo mara baada ya kutoka gerezani mwaka 1990. hii pia ni mojawapo ya picha zangu za awali. aliesimama na bango nyuma ya neno amandla ni jamillah mwanjisi (alikuwa mwandishi sasa ni bosi ngo ya kimarekani ya pact) anayekenua nyuma ya neno jangwani ni fatma fereji nasikia yuko ughaibuni kwa sasa. wengine nimewasahau. nawakumbuka hawa wawili sababu waliulizia picha hii ilipotoka gazetini.
 
© Michuzi | Sunday, March 05, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 1
boeing 737 la atcl

huenda wengi hamjui kuwa ndoa ya atc and saa imekaribia ukingoni na sasa twataka kodi ndege na kufufua atc yetu wenyewe
 
© Michuzi | Sunday, March 05, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 3
twataka chetu

wastaafu wa iliyokuwa jumuiya ya afrika mashariki wakingoja chao hazina mwaka jana. wengi tayari wameshalipwa, waliobaki (wengi wao warithi) wako katika harakati za kuthibitisha uhalali wao. lakini kazi iliwapata kudai chao
 
© Michuzi | Sunday, March 05, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 1
kampala

nilikua kampala kwa mafunzo ya uhariri na nilipangwa gazeti la new vision kwa mazoezi. nyuma makao makuu ya ne vision na ukutani ni matoleo ya gazeti hilo la serikali ya uganda linalojiendesha kibiashara kama sisi hapa deliniuzi ambapo hatupati ruzuku kama wengi wanavyodhania
 
© Michuzi | Sunday, March 05, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 2
bomoabomoa

bomoabomoa imenoga bongo, na majengo mapya kuibuka. tatizo sikumbuki picha hii nilipiga wapi. naomba msaada, enyi mlio ughaibuni...
 
© Michuzi | Sunday, March 05, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 3
madiba na mai waifu wake zilipendwa

madiba akipokewa na dr omar ali juma unguja siku chache baada ya kutoka kifungoni. hii ni mojawapo ya picha zangu za awali za viongozi toka niingie deili niuzi. da mija nasubiri jibu, upooooo?
 
© Michuzi | Sunday, March 05, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 7
mtimkubwa akitia mbolea

ah, na ukame huu acha mtimkubwa asaidie kwa kutumia ukulima wa umwagiliaji
 
© Michuzi | Sunday, March 05, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 9
madiba na my waifu wake

da mija upoooo?
 
© Michuzi | Sunday, March 05, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 4
Friday, March 3, 2006
jk na na viongozi wake wapya wa jeshi la polisi

amiri jeshi mkuu jakaya kwikete akiwa na igp mpya saidi mwema (gwanda buluu), dci robert manumba (suti kulia) mkuu wa fedha na utawala clodwig mathew mtweve nyuma yao ni alfred tibaigana bosi wa dar na paulo amani moses chagonja anaekuwa mkuu wa operesheni na mafunzo. hii ni baada ya kuwaapisha leo ikulu. anaepiga chebo nyuma shoto ni igp zilipendwa omar mahita
 
© Michuzi | Friday, March 03, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 9
mwalimu na bongo

mchoro huu umo ndani ya makumbusho ya mwalimu nyerere, butiama. naomba tafsiri yake
 
© Michuzi | Friday, March 03, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 3
daladala za musoma

hizi ndizo daladala za musoma ziendazo visiwa vya jirani na mbali
 
© Michuzi | Friday, March 03, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 1
gari la kisasa la faya

gari la kisasa la faya lenye shingo ndefu kupita jengo lolote bongo lipo nchini tayari kupambana na moto wa aina yoyote.
 
© Michuzi | Friday, March 03, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 4
Thursday, March 2, 2006
saa necha mzigoni

nani kasema ni jk pekee mwenye uwezo wa kujaza watu sehemu kama kirumba stediumu? haya, huyu hapa saa juma necha akiwa na wanaume jijini mwanza hivi karibuni. maswaaaali...
 
© Michuzi | Thursday, March 02, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 8
wazee wetu

wazee wetu muhimu nchini hawa
 
© Michuzi | Thursday, March 02, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 9
ajali

maskini jamaa kagongwa na gari ambalo limeingia mitini. sijui atafanyaje sasa...
 
© Michuzi | Thursday, March 02, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 2
mionzi bado wamo

ian mwaisunga (shoto), pili malundila na aloyce makonde wa kundi la dansa la kiafrika la kisasa (african contemporary dance) wakionesha mchezo wao mpya uitwao 'triangle' katika ukumbi wa utamaduni wa urusi. angalia viti vilivyo tupu, kuashiria wabongo hawamaindi kabisa tamaduni. wao ni ndombolo na bongoflava tu...
 
© Michuzi | Thursday, March 02, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 1
simba wa vita asiyechoka

simba wa vita rashidi mfaume kawawa juzi katimiza miaka 80 ya kuzaliwa lakini bado tu anapenda kuitumikia tanzania kana kwamba ana umri wa miaka 18. hapa ni katika kikao kimojawapo cha nec, dodoma
 
© Michuzi | Thursday, March 02, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 5
rais wangu

nampenda rais tarja wa finland. niligongana nae mitaani hivi... ila nilimstukia jamaa aliyevaa jaketi jekundu ni jamaa-flani, au vipi mtimkubwa. huyu bibie anasahau yalomkuta palme wa sweden?
 
© Michuzi | Thursday, March 02, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 6
hali halisi

jamani hili ndilo bwawa la mtera na hivyo ndivyo jinsi maji yalivyokauka. mvua isiponyesha ndani ya mwezi mmoja ujao, tumeumia kwani uzalishaji umeme ndo utakuwa kaput kwa asilimia 70
 
© Michuzi | Thursday, March 02, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 4
Wednesday, March 1, 2006
picha yangu bora ya 2005

mama anna mkapa akiwa na laura bush dar katikati ya mwaka jana ndo picha yangu binafsi bora kwani ni mie pekee nilieipata kwa kukisia kabla wangetokea kwenye kamlango na iliwachukua hatua takriban nane kuketi, hiyo ikiwa ni ya tano hivi. kikubwa walishikana mikono kwa sekunde kama tatu tu. wengine wote, hata wa kutoka marekani, walikosa hii ya kushikana. ndo maana ilipotoka ubalozi wakaja kuniomba
 
© Michuzi | Wednesday, March 01, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 11
nyumba ya nancy

hii ndo nyumba ambayo miss tanzania na miss world africa nancy sumary aliahidiwa. cha ajabu hadi leo hajakabidhiwa na nimeongea na lundenga leo analeta hadithi ndeeeefu. nasikia wenye nyumba wana mgogoro wa kifamilia ndo maana hadi sasa hakijaeleweka. mdhamini ocean sandals ndiye aliyeitoa na akasema ina thamani ya milioni 70 za madafu. mwaka huu mdhamini ni vodacom
 
© Michuzi | Wednesday, March 01, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 2
jeff msangi akipata khabari yake..

jeff msangi utaacha lini kukwea ukuta neshno? si unaona sasa...
 
© Michuzi | Wednesday, March 01, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 6
Tuesday, February 28, 2006
warembo wa miss utalii ya dunia wakiwa neshno

warembo wa miss utalii ya dunia walikuwepo neshno siku yanga ilipombamiza mtibwa 3-0. tatizo walikaa upande wa simba halafu ati wakawa wanashangilia 'adui'
 
© Michuzi | Tuesday, February 28, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 1
zawadi kwa john mwaipopo wa yanga

hii ni siku yanga ilipofungua dimba la ligi kuu na kuichapa mtobwa 3-0 neshno... na kuanza kuongoza ligi ile pyeeee! tehe tehe tehe. nasikia wanaomba ligi isimamishwe watangaze ubingwa leo. mwaipopo upo?
 
© Michuzi | Tuesday, February 28, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 4
warembo wa miss utalii ya dunia

warembo wataoshiriki fainali za miss utalii wa dunia wakila pozi bongo tayari kwa mpambano lililohamishowa dar toka arusha hapo machi 11. nyooooooote mnakaribishwa.
 
© Michuzi | Tuesday, February 28, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 7
Monday, February 27, 2006
jumba la ajabu

hili ndilo jumba la ajabu zenj, ambapo ilisemekana nguzo zake hizi zilijengwa kwa kutumia watu. ukweli ni kwmba hadi wakati huo hakukuwa na jumba kubwa la ghorofa visiwani unguja na bara. pia liliitwa jumba la ajabu kwa kuwa lilikuwa la kwanza kuwa na umeme (wa jenereta) pamoja na lifti.
 
© Michuzi | Monday, February 27, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 5
Sunday, February 26, 2006
mwamkumbuka huyu?

je, kinababa na kinamama wa ughaibuni. mwamkumbuka huyu?
 
© Michuzi | Sunday, February 26, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 6
jeff msangi akipata khabari yake..

haya ndo madhara watu kama jeff msangi wanayokumbana nayo mara baada ya kuruka ukuta kuingia neshno...
 
© Michuzi | Sunday, February 26, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 7
Friday, February 24, 2006
veterani

maulid dilunga "mexico" aliyekuwa yanga na sasa ni mfanyabiashara na mshauri chama cha mpira, fred felix 'minziro' alikuaga yanga sasa kocha wa ruvu stars, lawrence mwalusako kachezeaga yanga na pan sasa anafanya kazi katika kampuni binafsi na mmoja ya wasomi wachache wachezaji, mtemi ramadhani alikuwa tra sasa mratibu moro united na pia, leogard chilla tenga alichezeaga pan na timu ya taifa na sasa raisi wa chama cha mpira na pia kibosile kampuni ya landlover, zamoyoni mogella 'golden boy' alichezea simba kisha yanga na taifa stars na sasa anafanya biashara, nimesahau, juma jenerali mkambi alichezea yanga na taifa sasa anafanya biashara na ni mshauri tff na juma mensah pondamali, alichezea pan sasa ni kocha wa makipa na ni mfanyabiashara. natumai alieomba ataridhika kiasi...
 
© Michuzi | Friday, February 24, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 3
bwawa la mtera

hapa ndipo kitovu cha umeme cha bongo ambapo sasa kinakauka kutokana na kukosekana mvua kiasi hata serikali imetangaza tenda ya kupata mtu atayeweka mitambo ya umeme ya chupa ya chai
 
© Michuzi | Friday, February 24, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 7
Wednesday, February 22, 2006
joini njema

hapa ni forodhani, unguja, mida ya saa kumi na mbili jioni...
 
© Michuzi | Wednesday, February 22, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 5
utamu wa sindimba

kila ijumaa kuna onesho la ngoma nyumba ya sanaa ambapo sisi tambala, simba theatre na kyandu music hupokezana kwa zamu. na sheria ni kwamba wimbo wa mwisho kabla ya pazia kushuka, lazima kundi likaribishe watazamaji kucheza kama mnavyoona wenyewe
 
© Michuzi | Wednesday, February 22, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 9
machinga matatani

machinga wakiwa chini ya ulinzi wa mgambo wa site kwa kosa la kuuza nyanya barabarani
 
© Michuzi | Wednesday, February 22, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 11
zawadi kwa damija

damija. hawa ndo sis tambala ya sasa...
 
© Michuzi | Wednesday, February 22, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 4
halima shariff

huyu ndiye halima shariff ambaye sasa ni kamishna
kwenye kamisheni ya ukimwi (TACAIDS) akitoa mada kwenye semina ya ukimwi dodoma juzi. yeye, rose kalemela ambaye ni mkurugenzi wa swissaid, khadija riyami anayetangaza voa, ichikaeli maro aliyeko benki ya dunia, dar, ni kinadada waandishi waandamizi wakali wa bongo ambao niliwakuta daily news nilipojiunga na gazeti hilo januari 1, 1990.
 
© Michuzi | Wednesday, February 22, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 6
uwanja wa vita

jamaa akipiga chebo mahali ambapo mlinzi wa duka la fedha la macsoms alipokula shaba na majambazi walioingia kwa gia ya muuza ndizi na kupora mamilioni kwa kutumia zaidi ya robo saa. polisi walifika robo saa baada ya jamaa kuanza
 
© Michuzi | Wednesday, February 22, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 6
simba wa vita

simba wa vita mzee rashidi mfaume kawawa na mkewe
 
© Michuzi | Wednesday, February 22, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 4
kilua

mcheza ngoma ya kilua toka ujiji, kigoma
 
© Michuzi | Wednesday, February 22, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 1
lipumba na tibasana

mwenyekiti wa cuf akipiga stori na kamishna laurent tibasana, mkuu wa operesheni na mafunzo jeshi la polisi, akiwa na cheo cha tatu toka juu. wa pili ni wilfred mwansasu, mkuu wa utawala na fedha
 
© Michuzi | Wednesday, February 22, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 5
watoto bongo

watoto wakicheza kwa furaha bongo
 
© Michuzi | Wednesday, February 22, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 5
tiba

huyu ndiye alfred tibaigana, mkuu wa polisi dar
 
© Michuzi | Wednesday, February 22, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 11
Tuesday, February 21, 2006
taifa stazi

hapa ni uwanja wa majimaji, songea. je waweza sema hii ni timu gani na hawa ni kina nani?
 
© Michuzi | Tuesday, February 21, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 13
Monday, February 20, 2006
ulinzi kibao

polisi akilinda benki. nji sasa imetulia na kuleta wasi wasi kuwa labda kweli hawa jamaa hushirikiana na jamaa. unaambiwa hata loba hamna siku hizi bongo!
 
© Michuzi | Monday, February 20, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 8
mtandao musoma

vijana wakicheza michezo ya kompyuta katika kefu mjini musoma
 
© Michuzi | Monday, February 20, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 3
kikwete na pcb (takuru)
HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWENYE UFUNGUZI WA MKUTANO WA TAASISI YA KUZUIA RUSHWA (TAKURU) MBEYA, 20 FEBRUARI, 2006


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Utawala Bora),
Mhe. Philip Marmo;
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais(Mazingira),
Mhe. Mark Mwandosya;
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,
Mhe. John Mwakipesile;
Mkurugenzi Mkuu wa TAKURU,
Meja Jenerali Anthony Kamazima;
Viongozi wa Serikali,
Viongozi na Watumishi wa TAKURU.

Kwanza kabisa nawashukuru kwa kunialika kuja kufungua mkutano wa mwaka huu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa.. Nimekuja hapa leo kujifunza. Meja Jenerali Kamazima anaelewa vizuri moja ya nguzo za uongozi Jeshini kuhusu wakati gani wa kutafuta habari. Moja ya wakati wa kufanya hivyo ni pale unapopewa eneo jipya la kuongoza. Huna budi ulijue vizuri eneo lako kwa kujifunza yote yahusuyo eneo hilo, ufahamu mipaka yake, ujue eneo lako ikoje, uwajue askari wako, ujue uwezo wao na uyajue matatizo yao. Hivyo, niko hapa mbele yenu leo kutimiza wajibu huo wa kiongozi katika vita dhidi ya rushwa.
Ndugu Mkurugenzi Mkuu,
Watanzania wamenipa ridhaa ya kuwaongoza na niliwaahidi kuendeleza kupambana na Rushwa. Nilisema vile kwa kujiamini kwani nilijua nyie mpo. TAKURU ndio askari wa mstari wa mbele katika vita hii. Mmekuwa mnaifanya vizuri. Naamini tukishirikiana tutapata mafanikio zaidi. Kwa hiyo nimekuja hapa kufanya mambo matatu muhimu. Kwanza kabisa kuwaambia kwamba Serikali ya Awamu ya Nne imeamua kuendeleza mapambano dhidi ya rushwa kwa ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya. Nimekuja kuwaambia kuwa nawategemea sana katika mapambano haya. Napenda kuwahakikishia kuwa niko pamoja nanyi bega kwa bega na nitawapa kila aina ya ushirikiano katika harakati zenu za kupambana na maovu haya katika jamii. Pili, nimekuja kujifunza zaidi kuhusu harakati zenu, mafanikio yenu, na matatizo yenu katika vita hivi. Shabaha yanguhapa ni kutaka tuelewane juu ya njia na mbinu bora zaidi za kuendeleza mapambano haya! Na, tatu nimekuja kuwaeleza matarajio yangu na ya Watanzania kwenu katika vita hivi.

Ndugu Mkurugenzi Mkuu,
Napenda mwanzoni kabisa mwa hotuba yangu niwashukuru kwa kazi kubwa, na nzuri mnayolifanyia taifa letu. Pia nawapongeza kwa mafanikio mliyoyapa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita. Nimefurahi kusikia kuwa mmefanikiwa kufungua ofisi karibu katika kila Mkoa na katika Wilaya nyingi hapa nchini. Vile vile, mmeajiri na kusomesha wachunguzi na watumishi wengine wengi na wazuri na hivyo kuimarisha uwezo wenu wa kiutendaji. Pia mmefanya kazi kubwa ya kuelimisha umma kuhusu athari za Rushwa na mbinu za kupambana nayo. Kwa ujumla nimefurahi kuona kiasi gani mmejenga uwezo wa kitaasisi kupambana na rushwa katika mazingira mapya ya sasa. Aidha, nafurahishwa na ushirikiano na mawasiliano mazuri yaliyopo baina yenu na Wizara na Idara mbalimbali za Serikali ambayo yamewezesha utekelezaji wa mapendekezo yenu juu ya mbinu na mikakati ya kupambana na rushwa nchini.

Ndugu Mkurugenzi Mkuu,
Nawapongeza pia kwa kuandaa Mpango Mkakati (Strategic Plan) wa TAKURU wa miaka mitano ijayo (2006-2011) ambao, pamoja na mambo mengine, unatoa maelekezo ya namna ya kupambana na rushwa kubwa ambazo zina athari kubwa kwa uchumi wetu. Ni matumaini yangu kwamba mtajipanga vizuri kuutekeleza mpango wenu huo kwa nguvu zenu zote. Mimi na wenzangu Serikalini tutakuwa nyuma yenu kuwatia moyo na kuwapa ushirikiano unaostahili.
Vilevile, nimetiwa sana moyo na habari katika taarifa ya Mkurugenzi Mkuu kwamba katika kipindi cha miaka kumi iliyopita, pamoja na changamoto zinazowakabili, kazi yenu ya uchunguzi na upelelezi katika Wizara mbalimbali imewezesha kuokoa zaidi ya Shilingi bilioni 50 ambazo zingefujwa kwa njia ya rushwa. Hili peke yake, licha ya kazi nyingine nyingi kubwa na muhimu mnazofanya, linatosha kuwanyamazisha wale wenzetu wanaohoji ufanisi wa jitihada zenu na haja ya kuendelea kuwepo kwenu.

Ndugu Mkurugenzi Mkuu na Ndugu Washiriki,
Serikali ya Awamu ya Tatu imefanya kazi kubwa katika juhudi za kupambana na rushwa katika miaka kumi iliyopita. Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Rushwa ulitengenezwa mwaka 1999. Sheria mpya za kuimarisha mapambano dhidi ya Rushwa, kama vile Sheria ya Fedha ya 2000 na Sheria ya Manunuzi ya Serikali ya 2000, zilitungwa. Kanuni na taratibu nyingi mpya zilitengenezwa na za zamani ziliimarishwa ili kuleta uwazi na uwajibikaji. Mwanya mkubwa wa rushwa na ufujaji wa mali ya umma ulipunguzwa kipenyo chake. Taasisi ziliimarishwa na nyingi mpya – kama vile TRA na Tanroads – zilianzishwa. Utumishi wa umma uliboreshwa kutoa motisha na kuongeza ufanisi.
Mafanikio ya hatua hizo yalionekana. Mapato ya Serikali yaliongeza na matumizi yalisimamiwa vizuri. Uwazi ukaongezeka na watu wakaanza kuogopa kuomba, kutoa na kupokea rushwa. Hata hivyo, pamoja na juhudi zote hizi, wote tunafahamu kwamba rushwa bado ipo ndani ya jamii yetu. Kiwango cha rushwa ndogo ndogo kinapanda kwa kasi hasa katika mahakama, polisi, ardhi, huduma za afya na sehemu nyingine. Huo ndio ukweli. Kwenye Serikali za Mitaa nako hali sio nzuri. Rushwa kubwa nayo inaongezeka hasa kwenye mikataba na manunuzi ya Serikali. Hali ni mbaya vilevile kwenye shughuli za kisiasa. Imefikia sasa hali ya watu kujenga imani kwamba bila kuhonga mtu hawezi kuchaguliwa kuwa kiongozi. Kwa hiyo changamoto bado ni kubwa, licha ya mafanikio ya miaka kumi iliyopita.
Nyie ndio kikosi cha dafrao katika mapambano haya na ndio wataalam wa kuendesha vita dhidi ya rushwa kisayansi. Nimeelezwa kwamba moja ya mada zenu katika mkutano huu ni mwelekeo wa TAKURU katika kupambana na rushwa kuanzia mwaka huu. Ni matumaini yangu kuwa mtaitumia vizuri fursa ya mkutano huu kuzungumzia na kuelewana kuhusu namna ya kuendeleza mapambano haya kwa ari zaidi, nguvu zaidi na kasi zaidi siku za usoni. Ningependa kuona kwa namna gani mmejipanga kwa mbinu na mkakati kuikabili rushwa kubwa na rushwa inayowakera wananchi vijijini, mitaani na maofisini.

Ndugu Mkurugenzi Mkuu,
Tatizo la rushwa lina historia ndefu kwenye kila jamii ulimwenguni kote. Rushwa imekuwepo tangu binadamu walipoanza kuwa na mamlaka na dhamana ya kiutawala na kiuongozi kwa binadamu wenzao. Sio tatizo la Tanzania pekee; wala sio tatizo la Afrika pekee. Rushwa ipo kwenye nchi zinazoendelea na zile zilizoendelea; ipo kwenye nchi za kidemokrasia na za kidikteta. Lakini, kuwepo kila mahali duniani haina maana kuwa ni jambo halali na linalokubalika. La hasha!! Rushwa ni kitu haramu na kisichokubalika.
Chimbuko la rushwa ni tamaa ya baadhi ya watu waliopewa dhamana ya utumishi na uongozi wa umma kutumia mamlaka yao kwa manufaa yao binafsi. Ni matokeo ya mmong’onyoko wa maadili binafsi (personal ethics) wa watu hao kiasi cha kuwafanya wasiogope na wala kujali kabisa kuvunja maadili ya kazi zao na imani ya umma kwao. Kuzidi kuenea kwa rushwa katika jamii ni ishara ya mapungufu katika uwezo wetu wa kitaasisi kuizuia. Pia ni ishara ya kushindwa kwa ushawishi wa kisiasa, kijamii na kidini kwa jamii ili ichukie, ikemee na iikatae rushwa. Mafanikio katika vita hivi yanategemea ushirikiano wa nguvu za kisheria na dola, ushawishi wa kijamii, dhamira ya kisiasa, na uimara wa maadili binafsi na ya jamii.

Ndugu Mkurugenzi Mkuu,
Rushwa ni kitu hatari sana kwa maendeleo ya taifa letu. Ni dhuluma kubwa kwa haki za jamii. Na kwa wakati huu tunapoelekeza nguvu zetu nyingi katika kuinua uchumi na kuondoa umaskini, rushwa ni kikwazo kikubwa sana. Kisiasa, hasa kwenye chaguzi za viongozi wenye mamlaka ya umma, rushwa inazorotesha ukuaji wa demokrasia. Inawanyima wananchi haki yao ya kikatiba ya kuchagua na kuchaguliwa kwa kuifanya haki hiyo iwe ya watu wachache wenye uwezo wa kifedha. Rushwa inafanya uongozi kuwa kitu kinachonunulika kama bidhaa. Hii inapunguza uhalali wa mamlaka za uongozi na utawala kwa wanaoingia kwa rushwa. Ikiachwa kushamiri rushwa inapunguza imani ya wananchi kwa mfumo mzima wa demokrasia. Kwenye vyombo vya haki rushwa inazorotesha utawala bora na utawala wa sheria. Inahatarisha amani na utangamano wa nchi kwa kuleta dhana kwamba haki inauzwa na haiwezi kupatikana kwa njia ya kawaida. Hatuna budi kuipiga vita rushwa kwa nguvu zetu zote.

Ndugu Mkurugenzi na Ndugu Washiriki,
Rushwa ikikithiri inaweza kuwa hatari kwa usalama wa nchi. Kwa kuwa rushwa ni jambo linalowakera wananchi linaweza kuwafanya wawachukie watumishi wa umma na Serikali yao hasa wanapokata tamaa kwa kushindwa kupata haki, huduma na usalama wao. Wananchi wanaweza kupoteza imani kwa viongozi wao na Serikali yao na hivyo kuvuruga mshikamano, utangamano na utulivu katika nchi. Ikifikia hatua hiyo rushwa inaweza kuwa tatizo la kisiasa na kiusalama. Wananchi wanaweza kubuni na kuanzisha njia na mifumo sanjari na mbadala ya kutafuta haki na kujilinda wao na mali zao. Ushahidi wa hili tunauona kwenye umaarufu wa vikundi vya ulinzi kama vile Sungusungu na kuongezeka kwa vitendo vya wananchi kujichukulia sheria mikononi (mob-justice). Kwa kutambua ukweli huo na hatari zinazoweza kutokea hatuna budi basi tupambane na rushwa kwa nguvu zetu zote na uwezo wetu wote.
Mapambano dhidi ya rushwa ni vita halali kabisa kwa jamii kupigana na kupata ushiriki. Athari za Rushwa kwa uchumi ni kubwa. Rushwa inapunguza kasi ya kuleta maendeleo kwa vile fedha zinakwenda mifukoni mwa watu badala ya kufanya shughuli iliyokusudiwa ya kuiletea jamii maendeleo. Serikali hupoteza mapato stahiki. Miradi hutekelezwa chini ya kiwango na huduma zitolewazo kuwa za kiwango cha chini au hata kuwa duni kabisa. Rushwa inaongeza gharama ya kufanya biashara. Matokeo yake ni kwamba bei ya bidhaa huwa kubwa isivyo stahili na mzigo hubebeshwa mwananchi. Gharama za kufanya biashara zikiongezeka, kutokana na rushwa, tunatengeneza uwanja wa ushindani wa kibiashara usio sawia/tambarare kwa washindani wote. Kampuni zilizo na washirika kwenye Serikali na vyombo vya mamlaka ya umma – hata kama hazina ufanisi ndizo zinazonufaika. Kampuni ambazo hazina washirika au hazina uwezo wa kugharamia rushwa, na mara nyingi hizi huwa ni zile ndogo, zinashindwa kushindana kwa ukamilifu.
Kutokana na rushwa utendaji wa Serikali na shughuli za umma huyumba . Hadhi ya Serikali mbele ya wananchi hushuka hasa pale sheria na taratibu haziheshimiwi. Unapokuta taratibu za mipango miji, hifadhi ya mazingira, usalama barabarani, na nyinginezo hazifuatwi, dhana hujengeka kuwa Serikali haiko makini katika usimamizi wa ubora wa huduma kwa wananchi.

Ndugu Mkurugenzi Mkuu,
Kuna dhana potofu kwamba rushwa inarahisisha mambo kwa kuondoa ucheleweshaji (cutting the bureaucratic red-tape). Dhana hii haina msingi kwa sababu wapokea rushwa hujibunia mikakati, sheria na taratibu ndefu za kuongeza ucheleweshaji ili kutengeneza mianya na mazingira zaidi ya kupata rushwa. Na mara nyingi wanaoathirika na mbinu hizi za wapokea rushwa ni wale wanyonge wasio na uwezo wa kutoa rushwa.

Ndugu Mkurugenzi Mkuu,
Nimefurahi kwamba mna mipango na mikakati mizuri ya kupambana na rushwa. Lakini, ukweli ni kwamba ili mfanikiwe, na sisi wengine Serikalini hatuna budi tuchukue hatua za makusudi za kisera na kiutendaji zitakazoongezea nguvu juhudi zenu. Ningependa kuona kuwa kila kiongozi katika eneo lake awe ndiye kamanda wa vita hiyo pale alipo. Waziri afanye hivyo na Katibu Mkuu pia. Hali kadhalika Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na wengineo wote wafanya hivyo. Naamini tutapata mafanikio ya kutia moyo.
Moja ya aina ya rushwa yenye kero kubwa kwa wananchi wa kawaida ni ile yakutakiwa kumlipa chochote “kitu kidogo” mtumishi wa umma ndipo apate huduma. Mtu kuambiwa “sijaamka leo” au “mkono mtupu haulambwi” ni dhuluma na inakera sana. Ni kweli kwamba kishawishi kikubwa cha rushwa hii inawezekana kuwa kipato kidogo kwa watumishi wa umma. Jawabu lake kwa kiasi kikubwa linawezekana kuwa ni kuongeza kipato cha watumishi wa umma. Niliahidi kulishughulikia suala hili. Ni makusudio yangu kuwa miezi michache ijayo niunde tume ya kuangalia maslahi ya watumishi wa umma. Lakini kama kwa watumishi wala rushwa imeshakuwa ni hulka ya kuomba na kupokea rushwa inawezekana kabisa kuwa hatua hizo hazitasaidia. Huenda ndiyo kwanza wakapandisha dau.
Ndiyo maana basi hatuna budi kulitazama suala hili kwa mapana zaidi. Tubane mianya ya rushwa na tuzidishe mapambano. Sisi, kwenye Serikali Kuu na Serikali za Mitaa lazima tuongeze uwezo na ubora wa utoaji huduma na kuhakikisha kuwa kuna haki na usawa kwenye upatikanaji wa huduma. Tusimuonee haya anayefanya kinyume cha hayo. Wakati mwingine rushwa inatokana na wananchi wenyewe kutokuzifahamu haki zao. Tukiongeza juhudi kwenye elimu ya uraia na kuwahamasisha wananchi kuchukia na kukataa kutoa rushwa tutapiga hatua. Naomba nyie wenzetu mtusaidie kwenye hili. Najua mmefanya kazi nzuri katika kutoa elimu kwa umma. Naomba muendelee. Elimu haina mwisho na elimu kuhusu mapambano haya haina ukomo.
Natambua pia kuwa mmefanya jitihada kubwa katika kupambana na rushwa ndogo ndogo. Tuwe wakali zaidi katika mapambano hayo. Pasiwepo na kulegeza uzi. Mtandao wa ofisi zenu mpaka kwenye ngazi ya wilaya pamoja na elimu kwa umma vimesaidia. Lakini, changamoto kubwa iliyoko mbele yenu ipo kwenye rushwa kubwa kubwa na rushwa nono nono. Kwa muda mrefu sasa TAKURU imekuwa ikilaumiwa kwa kushughulikia rushwa ndogondogo inayohusisha watumishi wa vyeo vya chini. Mara nyingi uongozi wa TAKURU umekuwa ukijibu na kuelezea ugumu na muda mrefu unaotakiwa kupata ushahidi wa rushwa kubwa kubwa. Maelezo kwamba rushwa ni rushwa tu, hata kama ni ndogo na yale ya ugumu wa kupata ushahidi wa rushwa kubwa kubwa hayajawaridhisha wananchi walio wengi. Watu wanataka kuona tatizo hili linashughulikiwa ipasavyo kwani rushwa kubwa kubwa ndizo zinazodumaza maendeleo.

Ndugu Mkurugenzi Mkuu,
Natambua kwamba, taasisi yetu imekuwa na kazi kubwa ya kujiunda upya na kujijenga upya kwa watu, ujuzi, stadi, dhamira na nyenzo kukabiliana na rushwa kubwa. Kwa miaka kumi iliyopita mlikuwa mkifungua ofisi mikoani na wilayani, mmekuwa mkiajiri na kusomesha watumishi wenu. Kwa ujumla mmekuwa mkijijenga kimiundombinu na kitaasisi. Naamini kazi hiyo imefanyika vizuri, nawapongeza. Naomba sasa muazimie kwamba miaka mitano ijayo itakuwa ni ya kuonesha matunda ya kazi yenu, ya kujipanga kwenu.
Tumieni mkutano huu kuangalia ni namna gani mtaboresha mbinu na maarifa yenu katika kupambana na rushwa hizi kubwa vilivyo. Hayo ndiyo matumaini yangu kwenu na ndiyo matumaini ya Watanzania wenzetu wote wenye nia njema na nchi yetu.
Mkurugenzi Mkuu,
Naomba nitaje maeneo kadhaa ambayo nadhani itakuwa busara kuyatilia mkazo katika mipango yenu.
Tayari nimetaja rushwa katika mikataba. Kadhalika nimeshaelezea, Bungeni, nia yangu ya kutaka kuangalia upya taratibu za kuingia mikataba zinazotumiwa na serikali, mashirika ya umma na idara zinazojitegemea kwa nia ya kubaini mianya ya rushwa na kuongeza uwazi na uwajibikaji ili kulinda maslahi ya umma. Naomba TAKURU isaidie katika zoezi hili na kuishauri Serikali juu ya mapungufu yaliyopo katika taratibu zilizopo sasa ili yarekebishwe.
Katika zoezi hili, msisahau kuangalia pia michakato ya majadiliano, viwango vya utekelezaji, muda wa utekelezaji, kuhusika au vinginevyo kwa mamlaka za udhibiti wa utekelezaji (regulatory agencies) na hatua sahihi za kuchukua endapo masharti ya mikataba yatavunjwa.
Ni jukumu lenu TAKURU kutumia ujuzi wenu kubaini mapema mikataba batili au ile isiyokuwa na manufaa kwa taifa na kuishauri serikali ili ichukue hatua zinazostahili kabla fedha na mali havijapotea. Kinga ni bora kuliko tiba.
Eneo la pili lenye tuhuma ya kuwa na mianya ya rushwa kubwa kubwa ni la manunuzi/ununuzi (procurement/purchases) Serikalini. Sina budi kukiri kuwa Sheria ya Manunuzi na taratibu nzuri na rahisi za ununuzi zilizowekwa zimesaidia sana kupunguza ukubwa wa kipenyo cha mwanya wa rushwa katika eneo hili. Hata hivyo bado kuna maneno yahusuyo upendeleo, mgawanyo usio sawa, kutokuwepo uwazi wa kutosha wala ushindani halisi kwa kuwa washindani wengine hupewa habari za viwango vya gharama mapema. Kadhalika kuna madai kuwa ununuzi hauzingatii gharama na ubora wa bidhaa. Kwa ajili hiyo yapo madai kuwa wakati mwingine bidhaa zinapewa gharama za juu zaidi na kama gharama ni za kawaida basi baadhi ya bidhaa hazifikishwi kwa mnunuzi kwa maelewano baina ya wanunuzi na wauzaji. Fedha nyingi za serikali hupotea kupitia mwanya huu wa rushwa. Fuatilieni taratibu za manunuzi na ununuzi serikalini kubaini na kuziba mianya ya rushwa katika eneo hili nalo. Nia yangu ni kutaka kuona pesa kidogo tulizo nazo zinatumika kwa manufaa ya umma na watu walio wengi na siyo kuendeleza maslahi binafsi ya watu wachache.
Eneo jingine ambalo ningependa mlizungumze katika mkutano huu ni matumizi ya udanganyifu katika miradi ya taifa, na hasa ile inayofadhiliwa na nchi za nje. Yapo malalamiko dhidi ya udanganyifu na matumizi mabaya ya fedha za miradi mikubwa inayofadhiliwa na wahisani ama pekee yao au kwa ubia na Serikali yetu.
Mimi naamini Serikali inaweza kudhibiti matumizi ya fedha ili wananchi ambao ndio walengwa, wanufaike. TAKURU ifuatilie madai ya kuwepo rushwa na udanganyifu katika taasisi husika na ichukue hatua zinazostahili zilizopo katika mamlaka yake kisheria. Kwa yale ambayo yako nje ya uwezo wenu toeni ushauri serikalini kwa hatua muafaka na kuziba mianya ya rushwa katika maeneo hayo.

Mkurugenzi Mkuu na Ndugu Washiriki,
Vile vile, niongelee rushwa kwenye shughuli za kisiasa, hasa kwenye uchaguzi. Nililiongelea jambo hili Bungeni Disemba mwaka jana, lakini nataka nilirudie tena. Yameanza kujitokeza mawazo na hisia kuwa kunaanza kujengeka utamaduni kuwa uongozi unaweza kununuliwa kwa fedha. Matendo mengi ya wagombea, mashabiki na wapambe yanaelekeza hivyo. Wasiwasi wangu ni kwamba, tusipokuwa waangalifu, nchi yetu inaweza kuwekwa rehani kwa watu wenye fedha za kununua uongozi au wanaoweza kupata fedha za kufanya hivyo. Jambo hili linanisumbua. Nakubali kwamba fedha ni nyenzo mojawapo muhimu katika kufanikisha uchaguzi, kwa kila chama na kwa kila mgombea. Lakini, fedha kutumika kununua ushindi si halali.
Kwa maoni yangu hatuna budi kupiga vita jambo hili ili tuzuie isije kuwa utaratibu wa kawaida na utamaduni. Tutakuwa tumekwisha. Ningependa sana kupata maoni yenu juu ya nini kifanyike tukomeshe jambo hili la hatari. Bado ninayo dhamira ya kutekeleza azma yangu ya kutaka jamii tulizungumze jambo hili na hatimaye tuelewane kuhusu utaratibu halali, ulio wazi, wa chama au mgombea kutafuta fedha za uchaguzi; na utaratibu halali, ulio wazi, wa chama au mgombea kutumia fedha hizo.

Ndugu Mkurugenzi Mkuu,
Nimesema mambo mengi ya kufanywa na Taasisi ya Kuzuia Rushwa. (Prevention of Corruption Bureau), kwa imani yangu kwamba TAKURU inao wajibu huo na inaweza. Kwangu mimi neno la msingi katika jina la taasisi yenu ni Kuzuia, (Prevention).
Nataka mzidi kujijenga kwa upande wa kuwa kweli ni taasisi ya kuzuia rushwa. Kuelimisha umma namna ya kupambana na rushwa ni mbinu muhimu ya kuzuia. Nimetiwa moyo sana na jitihada mlizokuwa mnazifanya kwa upande wa kuelimisha umma na kuwasisitizia wananchi wakatae kutoa hongo, hata kama matokeo ya kukataa ni bugudha, kunyanyaswa na pengine hata kunyimwa haki. Nawaomba muendelee kuwajenga imani wananchi ili wanapodaiwa rushwa wakatae kutoa.
Nawaomba mtengeneze mikakati ya kuwafanya wananchi waione hatari ya rushwa kuwa kubwa zaidi kuliko manufaa yake. Hatimaye, tunaweza kufika mahali ambapo rushwa itakuwa haivumiliki katika jamii ya Tanzania. Hili litafanikiwa kwa kuweka msisitizo kwenye kuelimisha, kuhamasisha na kuwachochea watu wachukie, wakatae na waianike rushwa.

Ndugu Mkurugenzi Mkuu,
Pamoja na majukumu hayo mnayo kazi ya msingi ya kutambua na kuwadhibiti wanaohusika na kutoa na kupokea rushwa; kuwakamata na kuwashitaki. Kwa maana hiyo basi, taaluma ya msingi ya TAKURU ni uchunguzi na upelelezi. Huwezi kukamata na kushitaki wanaotuhumiwa kula rushwa bila kuwa na utaalamu na miundombinu ya uchunguzi na upelelezi. Nimefurahi kuona katika taarifa yenu mnazidi kujiimarisha kwa watu na mafunzo stahiki. Bado mnahitaji kuongezewa watu na fursa zaidi za mafunzo. Niseme tu kwa leo kwamba nimeipokea taarifa yenu na maombi hayo. Acheni tukaifanyie kazi na Waziri muhusika na Utawala Bora.
Sambamba na hili, nawaomba nilisisitize suala la maadili ya watumishi wenu. Hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kuhusu mahakama kwamba rushwa inaweza kuwepo kila mahali lakini ikishaingia kwenye mahakama basi haki itakuwa imetoweka. Mtu unaweza kusema hivyo hivyo kwamba ikiwa ndani ya TAKURU uadilifu utapotea mapambano dhidi ya rushwa hayatawezekana. Ningependa sana kuona kwamba chambo chetu hiki kinakuwa na viongozi na watumishi wanaotukuka kwa sifa za uadilifu na kwamba hawatuhumiwi au kufikiriwa kuwa wala rushwa. Napata faraja kuona kuwa jambo hili mnalipa uzito unaostahili na kulisisitiza. Nawasihi muendeleze msimamo huo huo. Msilegeze uzi hata mara moja kwa heshima ya TAKURU na maslahi mapana ya Taifa letu.
Kwa hiyo nimefurahi kusikia kwenye maelezo ya Mkurugenzi Mkuu kwamba katika mkutano huu mtapata wasaa wa kupitia kwa kina Code of Conduct ya TAKURU ambayo
mmeshaiandaa. Nawatakia kila la heri katika majadiliano yenu.

Ndugu Mkurugenzi Mkuu,
Nimeyasikia maelezo yahusuyo ubutu wa Sheria ya Kuzuia Rushwa na ucheleweshaji wa marekebisho ya Sheria hiyo mambo ambayo mmesema ni vikwazo vikubwa katika kufanikisha vita dhidi ya Rushwa nchini. Nashauri Waziri wa Nchi anayehusika na Utawala Bora akae na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, waangalie tatizo liko wapi na kulipatia ufumbuzi.

Ndugu Mkurugenzi Mkuu,
Nawashukuru tena kwa kunialika. Nawatikia kila la heri kwenye kazi yenu hii ngumu na muhimu kwa taifa letu. Kama nilivyosema awali, mategemeo yetu ya kushinda vita dhidi ya rushwa yapo kwenu. Tutashirikiana kwa karibu na kwa hali na mali. Naomba msiwe taasisi ambayo iko mbali na wananchi, washirikisheni wananchi. Msipofanya hivyo ni sawa na samaki kuwa nje ya maji kwa vyovyote vile uhai wake utakuwa mashakani. Nguvu yenu ni wananchi. Watumieni, waelimisheni wajengeni imani na taasisi hii wawasaidie.
Yapo maeneo mengi ya kushughulikiwa, na mengine mengi mnayajua wenyewe. Lakini kwa leo niishie hapa. Mengine tutaelekezana mara kwa mara katika utaratibu wa utendaji kati yenu na ofisi yangu. Natambua sana kuwa kazi yenu ni kubwa, na nzito na nyeti. Muione hivyo, mpangilie mipango yenu kwa kutambua ukweli huo. Katika kufanya hayo, naomba wakati wote mkae mkijua kuwa niko pamoja nanyi daima. Naomba nimalize kwa kuwasihi kuheshimu na kuzingatia kanuni ya ukweli na kuepuka kuonea au kusingizia watu. Chunguzeni, chunguzeni kila mnaloambiwa na kusikia ili mpate ukweli. Lakini msionee wala kutisha watu.
Mkurugenzi Mkuu, Viongozi na Watumishi wa TAKURU, baada ya kusema hayo mengi nina furaha kutamka kwamba mkutano huu umefunguliwa rasmi.
Asanteni sana kwa kunisikiliza
 
© Michuzi | Monday, February 20, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 6
Sunday, February 19, 2006
mahita matatani na cuf

wanachama wa cuf wameandamana kushinikiza igp mahita apigwe chini baada ya kuwatuhumu ujambazi...
 
© Michuzi | Sunday, February 19, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 7
jeshi la...

hapana, hawa si intarahamwe ama banyamulenge bali ni askari mgambo wa jiji la dar wakiwa kwenye doria. ni hodari sana hawa kuvamia wauza nyanya na mchicha
 
© Michuzi | Sunday, February 19, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 3
kinama wamo nao

nadhani mmesikia kwamba yanga na simba mwaka huu itachezeshwa na mwamuzi mwanamke. basi ndiye huyo...
 
© Michuzi | Sunday, February 19, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 3
vivutio si wanyama tu

hapa ni arusha national park
 
© Michuzi | Sunday, February 19, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 0
no smoking

ndata wa bongo kwa no smoking ndo wenyewe, hasa kwa vibaka na si majambazi
 
© Michuzi | Sunday, February 19, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 4
ben na anna

mzee mzima akilisakata na mkewe kwenye hafla jana usiku, ikiwa ni mtoko wake wa kwanza tangia atundike daruga mwezi desemba
 
© Michuzi | Sunday, February 19, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 10
Saturday, February 18, 2006
mnazi mmoja

hivi hapa pana mnazi kweli?
 
© Michuzi | Saturday, February 18, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 3
mafundi wa ndege bongo

mafundi wa ndege za serikali mzigoni. bongo tunao wataalamu waliobobea kwenye anga hizi...
 
© Michuzi | Saturday, February 18, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 7
kashangae feri

soko jipya la samaki magogoni
 
© Michuzi | Saturday, February 18, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 2
Friday, February 17, 2006
ofisi za daily news

kwa mlioko nje kwa zaidi ya miaka minne na hata wengine mlio hapa bongo, hii ndo ofisi mpya za magazeti ya daily news na sunday news ambako ndiko nakula mzigo. ni mtaa wa samora, si mbali sana na picha ya bismini, juu ya benki ya middle east ltd.
 
© Michuzi | Friday, February 17, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 5
zawadi kwenda washington dc

tenga na ndolanga. da'adija upoooo? unakumbuka hawa jamaa walivyokuwa wakikusumbua kila ulipokuwa watafuta stori? pole sana. naona umepumzika sasa.
 
© Michuzi | Friday, February 17, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 2
zawadi kwenda washington dc


zawadi kwa kaka hamza akiwa dc
 
© Michuzi | Friday, February 17, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 3
mambo niaje?

jamaa wa kipemba akiziingiza kwa mtasha bustanini forodhani, unguja
 
© Michuzi | Friday, February 17, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 6
bunge laahirishwa

waziri mkuu EL akiahirisha bunge leo baada ya kukaa kwa mara ya kwanza toka uchaguzi mkuu.
 
© Michuzi | Friday, February 17, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 3
Thursday, February 16, 2006
chalinze

washkaji wakitoka basi lile na kukimbilia lingine kuuza bidhaa kama njugu, korosho, ndizi n.k. mjini chalinze
 
© Michuzi | Thursday, February 16, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 2
nguva

wataalamu wakimalizia kazi ya kumtegeneza nguva aliyevuliwa kisiwani mafia na kuamuliwa kuwekwa makumbusho ya taifa kumaliza ubishi kwamba hawa wanyama ni nusu mtu nusu samaki
 
© Michuzi | Thursday, February 16, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 2
dar

dar nayo haijachacha lakini... mlio ughaibuni nambieni nimeipiga nikiwa jengo gani?
 
© Michuzi | Thursday, February 16, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 4
zenj empire

sheria msumeno
 
© Michuzi | Thursday, February 16, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 2
kilometa ngapi hadi bongo?


ndesanjo anajua alama hii i wapi...
 
© Michuzi | Thursday, February 16, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 2
posta

jamaa akipokea barua posta mpya. je, wa ughaibuni, haya mambo bado yapo ama mambo ya kuletewa hadi mlangoni. sie tufanyeje tufikie huko?
 
© Michuzi | Thursday, February 16, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 6
hodi zenj

mojawapo ya boti za abiria ikikata maji kuelekea zenj. kwa kawaida boti za kasi huchukua dakika 90 kufika na nauli bei ni sh. 12,000/- kwa kicha , lakini kama hii ni tujisaa tutano tu na nauli ni kuanzia 2,500/- hadi maelewano...
 
© Michuzi | Thursday, February 16, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 3
manzese

barabara ya morogoro kama ionekanavyo leo toka juu ya daraja la manzese, dar
 
© Michuzi | Thursday, February 16, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 4
watwangaji na wapepetaji wakuu

asha baraka na kaka yake baraka msiilwa, wamiliki wa africa stars entertainment inayoendesha bendi za african stars 'twanga pepeta' na african chipolopolo (zamani african revolution) wakitete jambo.
 
© Michuzi | Thursday, February 16, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 6
wameshalamba tena...

makachero na askari magwanda wakihoji dereva na abiria wa gari hili walioporwa mkoba na majambazi kweupeeee karibu na taa za tazara. aluta kontinua...
 
© Michuzi | Thursday, February 16, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 3
Wednesday, February 15, 2006
no smoking

jamaa aliyetaka 'kuharibu' nje ya ubalozi wa uingereza akiwa anakula 'no smoking'.
 
© Michuzi | Wednesday, February 15, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 7
jangwani enzi hizo

mwalimu akihutubia jangwani mwaka 1957, bi titi akiwa naye benet. huyu mama jamani katoka mbali kweli, basi tu mambo ya bongo. lakini angalau ana kamtaa kalikoitwa jina lake kama kumbukumbu
 
© Michuzi | Wednesday, February 15, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 3
kina migiro

profesa cleophas migiro akiwa na mkewe dk. asha-rose migiro kwenye hafla. profesa ni mwanasayansi mheshimika duniani katika nyanja za mazingira na pia ni mwenyekiti wa bodi ya tbs, shirika la viwango la bongo. mkewe ni waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa.
 
© Michuzi | Wednesday, February 15, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 4
ulinzi mkali

siku hizi kila kona dar kuna njago wenye mtutu katika kuimarisha usalama wa raia
 
© Michuzi | Wednesday, February 15, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 2
mwenge stars

na hawa je? MtiMkubwa Mkavu upooooo?
 
© Michuzi | Wednesday, February 15, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 4
enzi hizo....

wenye kumbukumbu hebu tupeni majina ya walume hawa...
 
© Michuzi | Wednesday, February 15, 2006 | Permalink | Mtumie Rafiki Yako | Maoni 12


Idadi ya watu
eXTReMe Tracker