wengi tulialikwa kwenye sherehe za kutimiza miaka minne ya gazeti la uwazi miaka kama minne ilopita. gazeti hilo, ambalo linamilikiwa na eric shigongo (mwenye suti na tai) limeshazaa magazeti mengine kibao ikiwa ni pamoja na ijumaa, champion, amani na risasi yanayotoka mara moja moja kwa wiki katika siku tofauti.
magazeti kama uwazi, ambayo wengi hupenda kuyaita ya udaku, nayafagilia sana kwani ni changamoto ya uandishi na waandishi wengi bongo kwa kuandika na sio kuripoti habari zinazogusa jamii - ingawa saa ingine baadhi huwa yanapitiliza na kuishia kufungiwa kama si kuonywa ama kushtakiwa. hutumiwa pia kama mitambo ya kurekebisha tabia...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Michuzi, wenye suti wako watatu hapo, jamaa wawili na dada mmoja. Shigongo ni yupi?

    ReplyDelete
  2. Michuzi naomba uitafutie hii article inayohusu corruption katiba usafirishaji vitu kupitia bandarini. Mimi pia binafsi nimesikia hili ongezeko la gharama kuwa mtu unalipa mali mara mbili yake. wakiweza kuto majibu kuwa hii ni legit itakuwa vizuri. Lakini mpaka sasa inashindikana kueleweka kwa wengi kwa nini kuna kuwa na gharama ambazo hazina msingi. Article imetoka kwenye hii link.
    http://www.esrftz.org/anticorruption/CORU_out2_inc_archive.asp?49

    ReplyDelete
  3. Sasa wewe hapo juu,kwa akili yako huyo mama anaweza kuitwa eric shigingo au makusudi tu jamani.Na huyo jamaa mwingine unaedai kavaa suti,hiyo nayo suti...unajua suti wewe??kavaa koti na tai,na suruali ofcourse.Sasa aliyebakia ndo eric shigongo.Tuwe tunafikiria jamani...akili matope!

    ReplyDelete
  4. Unayemponda mwenziyo kwa kuuliza Shigongo ni yupi, umeanza vema lakini mwishoni umeharibu kabisa. Kama jamaa unadai kavaa koti na tai mbona hata huyo Shigongo kaavaa hivyo hivyo? Suruali yake ni tofauti na koti, kwa mantiki yako hata huyo hana suti au sivyo?

    ReplyDelete
  5. Hey hata mimi namsupport huyo hapo juu. Ingawaje mwanamke hawezi kuitwa Eric lakini mwanaume aliyevaa suit simuoni. Naona watu wawili wamevaa sport coarts na wengine wamedress up for occasion. It is not a big deal lakini penye utata lazima paulizwe. Kwa hiyo usimdharau anayeuliza na ukijibu validate your info first before hujawa wewe ndio mjinga. .

    ReplyDelete
  6. hakuna suti hapo!

    ReplyDelete
  7. kumbe hao ndi wambea wa nchi

    ReplyDelete
  8. Ja hapa kwenye blogu kumejaa vichwa vyenye hoja, namsapoti anoni wa kwanza kwa kuuliza, wenye suti wako watatu hapo. Kama Eric ni jina la mwanaume, then wako wawili. (by the way kuna Eric, Erick au Erica pia, so anoni 1 you had a genuine question that Michuzi MAY respond)

    ReplyDelete
  9. Naomba ufafanuzi...Mahausgel wanazipenda sana hadithi za Shigongo zile anaandika kwa kiswahili lakini title ya kiingereza, kwenye magazeti yake na pia huwa anatengeneza mifano ya novo..

    Naskia hizi hadithi anatoa kwenye novels za international novelists halafu anafanya direct translation from English to Kiswahili..Ni kweli?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...