mh. ali hassan mwinyi rais wa awamu ya pili

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Aliifanya nchi kuonekana NYEPESI SANA yaani kila mtu kujifanyia atakavyo na madhara yake yalionekana maboya RUKSA ndo yalisumbua sana

    ReplyDelete
  2. Sera nzuri za kutajirisha wananchi, ambaye hakutajirika wakati wa Mwinyi ni uzembe wake mwenyewe ila hakuwa serious dhidi ya rushwa.

    ReplyDelete
  3. Mzee Ruksa..uongozi ulimshinda.

    ReplyDelete
  4. Aliweza kufungua nafasi za kibiashara baada ya mfumo wa kijamaa ambao ulianzishwa na mtangulizi wake. Ila udhaifu wake alishindwa kuendesha miaka 5 ya mwisho ya uongozi kila mtu alikuwa anajifanyia analotaka bila kufuata na taratibu za nchi, rushwa ilishamiri sana kipindi cha mwinyi, na mwisho mfuko wa bei ulikuwa katika kiwango cha juu. kuna kashfa za ajabu ajabu kama issue ya chavda, na baadhi ya viongozi kusafirisha nyara za serikali kwenda nje ya nchi

    ReplyDelete
  5. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  6. yanni huyu ndo kaabisaaaaa! hamna kitu, bora hata mrema!

    ReplyDelete
  7. Haikuwa rahisi kutawala baada ya Raisi kama Nyerere aliye kaa muda mrefu na kupendwa na percentage kubwa ya watu, influence ya wazanzibar pia ilimpotosha hakuwa huru kutawala, confusion, ndoo maana haikuonekana kitu cha maana alichafanya.
    Aurely

    ReplyDelete
  8. Matatizo ya Mwinyi yalikuwa

    1.Uwezo wake wa kusimamia walio chini yake ulikuwa mdogo mno.Yeye aliwaamini mno watu aliowachagua.Akishawachagua aliwaacha waendelee bila usimamizi mkali wa karibu.Hakujali kuwasimamia kuhakikisha wanafanya kazi barabara.Matokeo yake walio chini yake waliamua kufanya mambo ya hovyo bila kujali kwa kujua kuwa Raisi si mfuatiliaji wala msimamiaji mzuri wa walio chini yake.

    2.Alikuwa mkimya na mpole kwa kila mtu mpaka kwa mashetani wala rushwa na vibaka serikalini na kwenye mashirika ya umma.

    3.Sera ya kung`ang`ania kuzungukwa na marafiki ilimfanya ashindwe kuwa mkali kwa rafiki zake walipokosea.

    Alipenda kuzungukwa na maswahiba marafiki zaidi badala ya kuchagua kuzungukwa na wachapa kazi wa uhakika.

    Matokeo yake alijikuta kazungukwa na watu wa karibu ambao wengine walikuwa wanafiki wakubwa waliojifanya marafiki mchana wakati usiku wana ajenda za siri.Mfano ni Kighoma Malima,Augustino Lyatonga Mrema,Profesa Ibrahim Lipumba ambao walikuwa rafiki zake na watu wa karibu lakini baadaye walitoroka na kuanza kuzomea kuwa CCM iliyokuwa chini yake kuwa haijafanya lolote.Ina maana wakati walipokuwa na nafasi kubwa walizopata kwa urafiki zaidi kuliko utendaji walizitumia kumwangusha badala ya kumsaidia.Na yeye alishindwa kuwakemea sababu ni maswahiba na marafiki.Mfano kuondolewa kwa Kighoma Malima Ilikuwa ni baada ya ujasiri wa hali ya juu wa Raisi Kikwete kumtaja hadharani bila kuogopa ndio ulisaidia.

    Alisahau kuwa katika utendaji huhitaji marafiki zaidi bali watendaji ambao wakifanya vibaya ukiwanunia wanaweza hata ingia chini ya mvungu wa kitanda kwa hofu.Tofauti na marafiki ambao ukichukia wata- take easy sababu wanakujua.

    ReplyDelete
  9. Ah!ye mwenyewe alishasema,alikuta hewa chafu,akafungua madirisha hewa safi iingie.Sasa ile hewa haikuingia yenyewe,ila vumbi,takataka n.k navyo viliingia.sasa tu comment nini?kamaliza mwenyewe kila kitu!

    ReplyDelete
  10. Uongozi wake ulikuwa safi kiasi, kidogo alikuwa anawaamini sana washauri wake ambao kwa kiasi kikubwa walimshauri vibaya.Nakumbuka issue ya madini airport! Mbaya zaidi mshauri wake mkuu alikuwa Kitwana Kondo!! Hebu fikiria hapo, ndimu ukichanganya na sukari unapata ladha gani?

    ReplyDelete
  11. Niliwahi kukutana na mwandishi mmoja wa habari wa nchi fulani kusini mwa Afrika, akaniuliza Wa TZ mmliwezaje kuendesha nchi kwa miaka KUMI bila rais? Nikamjibu kwa swali kama kawaida yetu, kwanini akaniambia miaka KUMI ya AHM nchi yenu haikuwa na rais, katika maana ya kiongozi. Hatari kubwa.....

    ReplyDelete
  12. RAIS BOMBA KULIKO WOTE,aliijaza mifuko ya watu mapesa,hakuwa na kinyongo na mtu,alianzisha kukutana na watu na kutatua matatizo yao.
    katika kipindi chake cha urais niliweza kununua Toyota mark II nne,mbili nikafanya taxi bubu na mbili nikawa najaza mapesa kwenye buti everytime.Ni rais bomba alietufanya wengi tupate utajiri na kuishia ughaibuni,Je Mungu akupe gunia la chawa?Mungu amjalie maisha marefu rais wetu mpendwa wa awamu ya pili,bila yeye nisingeweza kuwa na nyumba za nguvu nne na pia kuruka ughaibuni.Long live, ALI HASSAN MWINYI.
    UBAYA
    Kwa ukweli hana ubaya baba wa watu hakuwa na roho mbaya kwa mtu yoyote.
    Wambea wana habari ndo walikuwa wazushi tu.

    ReplyDelete
  13. One thing I can say about Mwinyi is the lack of education, he was uneducated person, but great man, friendly and very understanding.

    ReplyDelete
  14. Tatizo katika uongozi wake alikuwa na akina profesa malima kama alivyosema anony hapo juu tatizo lilikuwa ni uongozi mzima hata hao mnaowaita kuwa wezi akina Malima walikuwa wanapeleka maoni yao kwenye kamati kuu ya CCM sasa wenye kauli waniambie kulikuwa na wachumi wangapi na hili ndo tatizo la ujumla katika uongozi wa siasa za kijamaa na kikomonisti kila kitu kipite kwenye mikono ya chama wasipokiafiki wenzio basi ndo kimekwisha hata kama kina nafuu kwa wengi, Mimi sio muumini wa siasa za kipinzani lakini ukweli lazima tuseme wanojua wakawaulize akina Edwin Mtei nini kiliwatoa hazina je ni ujinga wao wakutojua kitu kama redio zilivyokuwa zinatulundika ujinga au ni kupinga kwao kwa baadhi ya mambo ambayo kimsingi walikuwa wanajaribu kumkanya mzee hambiliki (JKN) kuwa iko siku tutakuwa hoi, kwa taarifa yenu wako baadhi ya wasomi kwenye vyuo vikuu ambao wanajua kuwa hao unowaita wezi kama Profesa Malima waliandika vitabu vyenye kutoa mustakabali wa maswala ya kiuchumi kwenye nchi za kiafrika na Tanzania lakini kwa kuhofia kuwa watakuwa wasaliti basi wakaacha na yaende hivyo hivyo madhali kamati kuu CC imeamua basi iwe hivyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...