kuna wadau wameomba tulijadili hili gumzo hapo chini kwa kina
HILL’ SCHOLARS BLAST DUAL CITIZENSHIP IDEA
BY JIANG ALIPO
Daily News; Wednesday,April 11, 2007 @00:02
SCHOLARS have blasted the idea of dual citizenship saying it would benefit only a few Tanzanians living abroad.
The sentiments came out clearly at a symposium on: “Unbinding the Dual Citizenship Debate: Which Way Tanzania?” organised by the Institute of Development Studies (IDS) of the University of Dar es Salaam (UDSM) yesterday.
Presenting a paper entitled: ‘Why Dual Citizenship?’ Masters Degree student Martin Mandalu said proponents of the idea were people who wanted to move freely between two countries, something which cannot be done by most Tanzanians.
“Dual citizenship is interest of the minority, especially those living abroad but do not want to give up the benefits they get while still getting benefits of Tanzanian citizenship,” said Mr Mandalu.
“If they truly love this country they should come and stay here. Why allow them to come and go?” asked Dr Colman Msoka, directly challenging the advocates of dual citizenship.
Dual citizenship would lead to divided loyalty, he added. Presenting a paper on the economic implications of dual citizenship, another student, Fabian Mahundu, said the status would open doors for foreigners to own land as it would be their right as “citizens” of Tanzania.
Opening the symposium, the IDS Director, Prof Bertha Koda, said the issue needed serious discussion as citizenship was a sensitive matter and touched on the lives of all Tanzanians.
On the other hand, IDS co-ordinator Dr Peter Kopoka said that denying the right of dual citizenship to those desiring it, would be equal to depriving a basic human right to a group of people.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 48 mpaka sasa

  1. Soma blog yangu upate maoni yangu juu ya hili.

    ReplyDelete
  2. Mimi nadhani maoni ya wasomi wa mlimani ni sawa kabisa. Uraia wa nchi mbili kwa nchi maskini kama Tanzania haufai kwa sababu utanufaisha watu wachache sana. Tena ni hatari kwa usalama wa nchi yetu. Kuna baadhi ya watanzania wakitoka nje, mara moja huanza kusema maneno mabaya juu ya Tanzania. Utasikia bongo hakufai, bongo hakuna mpango, bongo ngoma tupu. Sasa fikiria mtu aliyemufilisi wa fikira kama huyu umpe uraia wa nchi mbili, matokea yake ni kuwa utaungana na maadui wa Tz, kutumaliza kabisa. Watu wa aina hii wacha wabakie manamba huko ughaibuni. Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  3. Hili mimi pia ninalikubali, maana mpaka sasa siyo siri kwamba kuna watanzania wachache sana ambao wanahitaji huo mfumo. Kwa watanzania wa kawaida hawatafaidika na mfumo huu, hivyo hauna maana yoyote.

    ReplyDelete
  4. I hope JK atafuatilia maoni ya walala hoi. Kwa vile kila siku ukizikiliza hotuba zake kwenye net unasikia unajua lazima tufanye kama wakubwa zetu wanavyofanya.
    Ni kweli dual citizenship ni kujichimbia shimo tufe peke yetu. Watu wachache ana ndio watakaofaidika. Na kama ni hiyo kuingia na kutoka kama unajambo la kufanya lipa visa ni only $100. Na wala hamna maswali kama tukiomba visa za kwenda nchi nyingine. Na kama unaipenda nchi hii kwanini uliiikana to begin with. Na kama unaipenda sana kuliko uraia wako ulionao basi hamia wetu.
    Mambo ya dualcitizenship uchumi wenyewe mdogo.

    Kwanza ni wangapi wanahitaji hii kweli ukizingatia majority walioko nje wabongo hawana hata uraia wa hizo nchi walizoko.

    ReplyDelete
  5. amakweli watanzania mmelala. mtazidi kutawaliwa maisha yenu yote. dual citizenship ndio waindi na maatajiri wengi wa tanzania wanazo. nyerere kawaziba macho nyie. ngono kweli iko bongo kwanini mfiche?mna chukua vitu too personal. amkeni jamani

    ReplyDelete
  6. Nyie hapo juu mawazo yenu ni mafupi. Inaelekea mnafahamu kinachoendelea Tanzania tu na si dunia nzima.

    Wake up! This is a global economy. Nyie inaelekea mmejaribu kuja ughaibuni lakini mkanyimwa visa. hahahahahahahahahaha!

    ReplyDelete
  7. Dual citizenship tutajadili hapa weee, kwa taarifa yenu mbona wengine tayari tunauraia wa nchi mbili. Shauri yenu fanyeni mambo yawe wazi sasa muone kama hatujajitokeza watu zaidi ya million hapo bongo wenye kushikilia passport mbili au hata tatu. Wanaopinga hili suala ni jelous tu hamna lolote, siku ukipata uwezo wa kuwa international traveller ndio utaona kuwa dunia sasa hivi ni kijiji kimoja na sio kama mnavyofikiria, Kubalini nyinyi acheni kuendeshwa na jelous.

    ReplyDelete
  8. Uraia wa nchi mbili kwa faida ya nani? Jibu Uraia wa nchi mbili kwa faida ya Tanzania na vizazi vyake vijavyo siku za mbele. Nasema watu tuko wenye uraia wa nchi za nje na vile vile tumepiga shule pale Mlimani. Mawazo na fikra zetu zilikuwa kama wale watoto pale Mlimani wanaopiga kelele tu. Hii si kwa faida ya wachache. Kwa sababu ukiwa na Uraia wa nchi kubwa bado unaweza kuingia na kutoka Tanzania na ukafanya jambo lolote wanavyofikiria kuatarisha usalama wa Tanzania. Dar Es Salaam kuna nini la maana pale? Wamachinga? au Vumbi tu na Vibaka. Sasa ni usalama gani? Uchumi umekufa. Nchi haiendelei na mawazo ya watu yameganda. Dola $50 mpaka $100 ni ndogo sana kulipia viza dilishani pale JK Nyerere Airport. Sisi watu wa Ughaibuni tunachotaka tu ni heshima kutoka kwenye nchi yetu ya asilia. Vinginevyo hakuna haja ya wabongo wanaoishi Ughaibuni kuingia kwenye ma debate ya Michuzi, Jambo na zinginezo. Kitu kimoja ninachokijua kwa uhakika, wale vijana pale Mlimani kila siku wanalala na kuwaza ni vipi wataweza kupanda ndege kwenda Ughaibuni. Hii inanikumbusha katika mada mojawapo za Michuzi kusagia Ughaibuini, lakini kila siku anawaza Manchester United/ Liverpool n.k Lakini nakuhakikishia Bw. Michuzi wabongo wa huku wameshazoea mambo ya michezo na vitu kama Soccer au NBA Basketball havichanganyi mtu akili kabisa!.

    ReplyDelete
  9. Je kuna hasara gani ya maana ambayo inaweza kusababishwa na "dual citizenship"? Wenzetu waliotuzidi kimawazo wanatumia "dual citizenship" kuzuia "brain drain" na kunyanyua hali ya kiuchumi ya wananchi wazawa kwani "dual citizenship" itawasaidia wazawa wenye mapesa kuja kuwekeza nyumbani pia. Hao wazungumzaji wa chuoni mlimani wanafanya mazoezi ya kiingereza tu; mfano wa "debate" zilizokuwa zikifanya pale Azania na Tambaza. Tuachane na hizo "debate" na tuzungumzie zaidi faida, maana tunao watu wetu wako mpaka NASA, soon to become NBA star, Harvard wanachukua mikwaju US wanaukacha U-Tz kutokana na sheria mbovu. Jamani tufikirie japo kidogo maana damu nzito kuliko maji!
    Babao

    ReplyDelete
  10. mimi nafikiria katika hii dunia ya utandawazi tutoe mawazo mgando kama hawa wasomi wa mlimani,angalau watoke nje ya nchi waone jinsi dunia inavyokwenda la sivyo tutaendelea kuwa manamba kwa kung'ang'ania eti utaifa, kila mtu ni mtanzania, katika hii dunia ya utandawazi kila mtu is looking for green pasture,some times hazipokuwa na uwezo wakuwa raia katika hiyo nchi anayotafuta maisha eg scandinavia countries,UK ,canada na usa,uhakika wa kupata kazi yenye kipato stahili kama raia wa nchi hizo unakuwa haupo,i hope kama anauwezo wa kupata dual citizen ship itamsaidia kupata kazi stahili yenye kipato cha kutosha bila ya kuukana urai wake wa kitanzania, Si wote wanaopenda kuukana uraia ila ugumu wa maisha, kukata tamaa ya kunyanyuka kiuchumi ndio kunamfanya mtu asiwe na alternative bali aukane uraia wake ingawa roho inamuuma.
    Hicho kipato cha uhakika anachokipata kitasaidia kuingiza foreign currency kwenye mzunguko wa fedha nyumbani tanzania
    through hela anazo watumia wazazi wake, dada ,kaka na ndugu zake wengine au hata miradi kama small and medium enterprenuar enterprises (SMES)ambayo itatoa ajira na kuinua hali za watanzania wengine nyumbani,kama tunavyo jua informal sector ndio ichangia sehemu kubwa ya ajira nyumbani, huo ndio ukweli.
    wenzetu india,china, philipines wametumia njia hii ya dual citizen ship kuinua uchumi wa nchi zao, sasa ni miongoni mwa nchi zinazokuja juu kiuchumi duniani, wewe angalia wahindi wana uraia wa kila sehemu, kuanzia canada hadi TZ kwenyewe, angalia hizo dola wanazopeleka kwao india.

    tutake tusitake huo ndio ukweli(facts), dual citizen ship ni muhimu, Watz tuamke sasa, tutumie usomi wetu kutambua dunia inavyo kwenda, tuache siasa iwe kwa wana siasa na mawazo yetu yasiwe na mgando. tutaishia kuwa manamba kwenye nchi yetu na wageni tunawapa uraia ili wachume vizuri waka wekeze kwako tubaki na mashimo huku sie wenyewe tunawanyima ndugu zetu wa damu uraia.tuache unafika sasa, tuamke,tusije vuta shuka wakati kumeshapambazuka!!!!

    NAJUA NITATUKANWA KWA KUSEMA UKWELI HUU ILA AMBAYE ANAUPINGA AWE WA KWANZA KUNIRUSHIA JIWE.

    ReplyDelete
  11. Mimi nafikiri kwamba hawa wanaotoa maoni kutoka ughaibuni wameshapoteza kabisa dira na hawana tena uchungu na nchi yao Tanzania. Wanafikiria zaidi maslahi yao binafsi na sio ya nchi. Wanataka wakishindwa kumoja waje kutest zali Bongo au vice versa. Mimi nimekaa nje ya Tanzania (Australia) sasa kwa miaka zaidi ya 10 na bado sijaukana uraia wa nchi yangu pendwa. Nimekuwa Permanent resident kwa miaka 6 sasa na bado sitaki kuwa raia wa nchi nyingine. Ninakwenda nyumbani kila baada ya miaka miwili na investment zangu Bongo hazina tabu yoyote. Sihitaji dual citizenship ili niweze kuishi Bongo na Australia. Nawaomba mfikirie zaidi madhara yanayoweza kuipata nchi yetu kuliko faida zenu. Katika eneo letu la Afrika Mashariki na kati, Tanzania ndio pekee iliyo na amani ya kutosha na uchumi ambao bado haujatumiwa to the maximum capacity. Ukuruhusu dual citizenship utafungua malango wa Wakongo, Watutsi na Wahutu, Waganda kwa Wakenya kufurika nchini (kwa nini wasije wakati wanastahilli kuwa raia?). Wakishajaa wataanza kujichukulia ardhi, biashara na nk na kuuchukua uchumi wetu mikononi mwao. Wana elimu kushinda sisi na wako aggressive kutushinda. Uchumi wetu ukishakuwa mikononi mwao wataamua jinsi ya kuiongoza nchi yetu. Sisi tutaishia kuwa watazamaji. Kama mna uelewa wa kutosha mtagundua kwamba nchi zilizoendelea ziliingia kwenye dual citizenship baada ya kuumiliki uchumi wao. Wewe unapopewa urahia kwao hubalishi chochote zaidi ya kuendeleza walichokwisha anzisha. Hivyo basi ningeomba tuliache hili suala kwa muda ili nchi yetu ifikie level inayokubalika. Tusaidie nchi yetu kwa kadiri tunavyoweza ili ndugu zetu waelimike, wawe more aggressive, uchumi ukue, tutumie zaidi rasilimali zetu ndio tufungue malango kwa wengine ili na sisi tupate faida y akutoka nje kuwekeza zaidi amabcho tumeshakianzisha kwetu.
    Naomba kuto hoja

    ReplyDelete
  12. Cha kustaajabisha ni kwamba matawi ya CCM yanafunguliwa nchi za nje ili kuwakumbatia Wabongo wanaoishi nchi mbali mbali ili wawe wanachama wa CCM.

    Pamoja na kwamba CCM inajua wengi wa Wabongo hao wameshachukua uraia wa huko wanakoishi ama wako mbioni kufanya hivyo hakuna tathmini yoyote inayofanywa ili kuwachuja wale ambao "Sio Watanzania". Kwa maana nyingine CCM inaruhusu kuwa na wanachama ambao "sio Watanzania" lakini hao hao CCM kwenye swala la uraia wa nchi mbili wamekaa kimya kama hawapo au hawajui kinachoongelewa. Kama kawaida ya undumila kuwili wao.

    Majirani zetu ama wamesharuhusu uraia wa nchi mbili ama wako mbioni kufanya hivyo. Watanzania wamefungua macho kwamba kuna nchi nyingine elimu yao ina thamani kubwa sana na wala hawatishiki na hili la "kupoteza Utanzania" pale watakapochukua uraia wa nchi nyingine. Na idadi ya wasomi wanaoenda nje itaongezeka kila kukicha.

    Faida za Tanzania kuruhusu uraia wa nchi mbili ni kubwa na nyingi mno ukilinganisha na hasara, lakini hata mkipigiwa wimbo bado itakuwa ni kama juhudi za kumpigia mbuzi gitaa. Eti watakaonufaika ni wachache, sasa swali langu kwenu hivi Tanzania kuna sera ngapi ambazo zinawanufaisha Watanzania wote milioni 38? Kuna zile ambazo zinawanufaisha wabunge tu, au mawaziri tu n.k? Je kuna ubaya gani wa sera ya uDC kunufaisha wachache!?
    Acheni ntimanyongo!!! Watu hawawezi kuendelea kusaga lami eti kwa kukumbatia uzalendo, wakati kuna nchi nyingi ambazo zinahitaji elimu na vipaji walivyonavyo. Dunia ya leo sio ile ya mwaka 47.

    Simama Dede.

    ReplyDelete
  13. Mimi nadhani maoni ya wasomi wa mlimani sio sawa kabisa maana walitakiwa kutoka faida na hasara za Uraia wa nchi mbili sio kutizama upande mmoja
    kama hapa chni wanayosema bila kutizama faoida yake
    1) Masters Degree student Martin Mandalu said proponents of the idea were people who wanted to move freely between two countries, something which cannot be done by most Tanzanians. Ni kweli kabisa lakini mbona kuungana kwetu na kenya na Uganda ni watu wachache ndio wanaouweza kusafiri na pia ni kama vile vile hapo bongo kuna vijana wengi wanaowezo wa kufanya vizuri UDSM lakini hawapati nafasi ya kusoma.
    2)Dual citizenship is interest of the minority, especially those living abroad but do not want to give up the benefits they get while still getting benefits of Tanzanian citizenship,” said Mr Mandalu. Hapa ndio jamaa Mandalu kaonesha sio msomi wa UDSM kwanza kila mtu duniani anayo haki yake na hii kukiuka Human rights ya wabongo waliokuwa nje na sio wabongo wote ndio wakimbizi,hii ndio fikira finyu.. wengi wa wabongo wapo nje ndio wamesoma kama wanao master kama mbili au tatu na Doctor sasa hawa watu wakipewa nafasi kama hii ni rahisi kurudi na kufanya vitu vya maana bongo. Wapo watu wanataka kufanya biashara nayo pia hii itasaidia uchumi wa bongo kama kodi, ushuru lakini kama wanatoa Uraia wa nchi mbili watizame sheria kama ni lazima mtu wawe mbongo wa kuzaliwa na kuishi kama miaka 10 ili isiwape faida watu wa nchi ingine kama walioa hapa bongho au walionunua uraia.
    3)“If they truly love this country they should come and stay here. Why allow them to come and go?” asked Dr Colman Msoka, directly challenging the advocates of dual citizenship wow wewe ni mbongo kweli " nyumbani ni nyumbani " ndio maana hata kama mtu hakifa nje uwa tunafanya juu chini kumrudia bongo. kwanza, wewe ndio nani mpaka umpangia mtu mahali pa kuishi, watu kwenda nje sio kuwa wanatafuta maisha kwa namna mmoja au ingine kama wengine tulikuwa tumefanya vizuri hapo bongo lakini nafasi za kazi zinakwenda kwa undugunazeee au wengi wao wanafamily hapo bongo wanatuma misaada..
    4)Dual citizenship would lead to divided loyalty, Fabian Mahundu, said the status would open doors for foreigners to own land as it would be their right as “citizens” of Tanzania..he he ndugu ya Mahundu sijue wewe unaogea divided loyalty gani ? na kama unafikiria foreigners watachkua land yetu sawa tuweke shria hapazo zitawapana ili wabongo tupate faida kama wetu wa nchi ya nje wao wanatunga shria kwa ajili ya watu wa nchi yao hata kama kuwapana foreigners kwa sheria fulani fulani mfano iwe kwa wabongo waliozaliwa bongo sio kwa watu walikuja... asante Bwana Michuzi kunipati nafasi hii ila naomba wasomi wa bongo wasio na wasiwasi maana watakiwa kufanya researching ili wajua mambo sio kumdangaya rais watu kwa point ndogo ndogo, na hii ndio ikamfanya Rais kwenda nje kuomba msaada kwa wasomi kuja kusaidi mambo ya sheria wakati tuna wasomi wengi ila kazi zao tu kumdanganya rais... next time Mr JK wafukuze watu wasiowajibika au wanakuombia detail za uongo...
    c uuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  14. Kwa maoni yangu, nakubaliana kabisa na wazo la kuzuia uraia wa nchi mbili "dual citizenship" tunazo sababu nyingi za msingi. hata zile za miaka ya nyuma enzi ya vita baridi bado zipo hai mpaka leo lakini kwa jina jipya la utandawazi na kuboresha biashara na vitega uchumi " trade facilitation and investments". ila kama hoja ni wakubwa wametubana tuikubali ili watumalize kabisa, basi tuikubali kwa masharti kwamba, hao "dual citizens" wasiruhusiwe kumiliki ardhi, na kushiriki uchaguzi wowote kwa maana ya kupiga au kupigiwa kura. Lakini pia tuzidi kulijadili. Tunao wenzetu wengi huko ughaibuni, pamoja na wahindi wanaoona mbele ya pua yao tuu! Lazima watalazimisha "dual citizenship". Naomba kuwakilisha.

    ReplyDelete
  15. Haya ni mawazo ya watu walio na akili ya shule tu lakni kama akili yako imekomaa ni wazi kabisa utaliangalia ili swala siyo tu kwa mafanikio ya mtu binafsi lakni kwa mafanikio ya Taifa pia. Offcourse, watu watarip benefits kutokana na hiyo lakni tuangalie nchi yetu ilipo. Kama tunawaingiza watu wa nchi nyingine nchini kwetu na kutukanyaga na kupeleka utajiri nchini kwao kwa nini tusiencourage haya maendeleo kwa watanzania wenyewe knowing somewhere there will be those whose interest are in Tanzania. Fikiria viongozi wanaochaguliwa kuiakilisha nchi wanachaguliwa kuwa ingawa hiyo nafasi inawanufaisha lakni nchi pia inanufaika nao in one way or another. Tuachake akili finyu ambazo hazina kina.

    ReplyDelete
  16. hahahaha, nyie kaeni tu na uraia wenu wa bongo kwanza mnakaa chini hamna viti vya kutosha hapo mlimani. ngoja tuache wahindi wawakongoloe wana uraia wa india wanakuja bongo wanachukua uraia wa bongo tena. mnaona mnatubania wazawa kumbe mnajizibia misaada yetu endeleeni kusoma kwa kukaa chini huku mnapigwa disko hahahaha
    visa ngumu bwana hahahaha
    hata hivyo hakuna wa kutulipa bongo tulishazoea cheki kubwa kubwa biashara zenyewe wizi tu wa wadosi

    ReplyDelete
  17. Sijui kama wasomi hao wamefanya utafiti wa kutosha.

    Nchi hii wanaofaidi ni wale wenye uraia wa nchi mbili.Waarabu na Wahindi.

    Ndiyo maana bidhaa nyingi toka India na Uarabuni ndizo zimejaa hapa.Raia wa nchi hizo waliopo hapa nchini wanazileta na wanatajirika kuliko wazawa.

    Wasomi wa Tanzania wajue kuwa nchi kama India hata wewe ukigoma uraia wa nchi mbili wao raia wao wa kihindi wanawapa uraia wahindi wenzao bila kujali wewe unataka nchini kwako au hutaki.Marekani,na nchi nyingi za uarabuni ni hivyo hivyo.Wanawapenda sana waarabu,wahindi na wazungu wenzao.

    Hivyo kama Tanzania haitaki hilo ni shauri yake.

    Kwa hiyo kama hatutaki uraia wa nchi mbili in maana tunayemwonea ni Mswahili Ngozi nyeusi siyo mwarabu au mhindi.Sasa kwa nini tuingize ubaguzi ndani ya nchi? Wageni wawe huru kuwa raia wa Tanzania na nchi nyingine na wenyeji wazawa weusi wasipewe hiyo facility.

    Halafu kitu kingine wamenichekesha wasomi wa Mlimani eti watu wachache watafaidi.Hivi watanzania roho ya korosho tutaacha lini?
    watanzania wenzio wakifaidi wawe wengi au wachache kwa nini tusifurahi? Ili mradi watanzania wenzetu wamefaidi.Watanzania kwa roho mbaya!!

    ReplyDelete
  18. Ndugu MICHUZI NA WATANZANIA WOTE,
    Kwanza niwashukuru sana walioleta hii mada hapa, na wote wanaochangia. Haijalishi wanakubaliana ama wanapinga wazo la uraia wa nchi 2. Anayepinga au kukubali, anasaidia kuuonesha umma, ni watu wangapi wana mtazamo upi, na kwanini, nk. Baadhi yao kama mie binafsi nimefurahi kujua wana mawazo mafinyu kiasi gani.
    Hao vijana wanaopinga kutolewa uraia wa nchi 2 nasikia wanasoma shahada ya uzamili (master's). Hebu angalia arguments zao. Hivi hao wanakuja kuandika nini dissertation au thesis zao kupata hiyo shahada? Msomi kama huyo anatakiwa kuchambua mambo katika mtazamo ambao ni mpana, unaoangalia jambo katika pande 2. Hawa vijana wametoa conclusion bila argument, supporting details and examples. Hizo ndio dalili zinazonionesha kuwa watu wanapata shahada ya kwanza kwa kukariri madesa, afu wanajikuta wametumbukia kwenye master's. Kwanza hawana exposure kimawazo. Wanachojua wao ni ile 'here say' na influence ya public opinion, ambayo si lazima iwe sahihi siku zote.
    Nyie vijana, mnapoongelea kuwa uraia wa nchi 2 utaufaisha wachache , mnataka wawabebe mwende nao huko waishiko? Maana kama sivyo, kwanini hamwoni kuwa hao wachache wana pesa kuliko mamilioni yenu mnaolilia demokrasia hapo, na hizo pesa ikifungguliwa mianya, wahamasishwe kuwekeza nchini TANZANIA. Ni swala tu la serikali kuwa serious, kuwavutia wenye pesa zao, na utaona wanafanya maendeleo nchini TZ.
    Mawazo yenu ni ya ubinafsi zaidi kuliko hao mnaowafikiria. Waafrika wengi tuna mawazo ya ubinafisi mno. Kiswahili kimetangazwa kuwa lugha ya Afrika mfano ktk AU, lakini baahi ya nchi zinapinga, kisa wanaona tu wivu sababu Kiswahili siyo lugha katika nchi zao, badala ya kuanzisha mikakati ya kukifundisha kwao kipanuke. Cha ajabu unakuta vyuo vingi ugenini kama hapa USA, zaidi ya 50, wanafundisha Kiswahili. Hakika, nawaambia wenye mawazo mafinyu kama hao vijana wa DS - Master's, acha wadumae hivohivo. Na kwa taarifa yenu, double citizenship haina role ya kumfanya mtu kuwa tishio la usalama kama mlivosema. Angalia nchi zenye utaratibu huo, kila unakoenda unakuwa raia na unababwa na sheria zake. Msiongee kama tu mmetoka kulala. Kuwa na uraia huo siyo kwamba ndio hakuna taratibu zinazombana mtu huyo, la hasa. Kila nchi yenye dual citizenship, raia wake wa namna hiyo huwa wachache kuliko wasiokuwa nazo, huo ndio ukweli. Vinginevyo Watanzania wote waanze shughuli zao nje. Pia kumbukeni, uraia wa nchi 2 una faida nyingi ambazo tukianza kuzitaja tulio nche mtasema tunajipendelea. Hizo faida zinanufaisha hata ndugu na jamaa walioko TZ. Tena mkiwabania walioko nje wasipate uraia wa nchi 2, mnajisumbua tu, maana haipunguzi kitu. Nyumbani wataendelea kurudi na nje watakaa, na nchi yenu wataichukia sasa. Maana wameshajua mlioko TZ mmejaa roho mbaya juu yao. Hamna mapenzi kwao.
    ACHA ROHO MBAYA. Wasomi wenye bongo kichwani hawawezi kuafiki mawazo 'simple' ya hao jamaa wanaopinga. Hata rais mwenyewe anazijua faida zake kuliko mnaopinga. Mwenzetu ametembea na utandawazi anauona katika namna mbili tofauti, sio upande 1 tu. Wekeni kizingiti mbaki hivo mlivo, na mtazidi tu kuwa na dhiki zenu hivohivo.

    ReplyDelete
  19. HIVI WADAU MKIAMBIWA KUNA WASOMI MNADHANI KULETA WA PALE MLIMANI? HAYO NI MAMBUMBUMBU YAKIJA KIWANJA KUSOMA HAYAJUI KITU KABISA HATA MTIHANI WA DRIVING LICENCE YANASHINDWA SASA MKIBISHANA NAYO MNAPOTEZA MUDA, HAMNA KITU KICHWANI YAMEKOSA VISA HASIRA ZINAISHIA KWENYE DUAL CITIZENSHIP. BILA KUJALI HAO HAO WACHACHE WATAINUFAISHA NCHI! MBONA NYERERE ALIRUHUSU VYAMA VINGI WAKATI NI WACHACHE TU NDIYO WALIVITAKA? ACHENI KUJADILI ISSUE NA MAMBUMBUMBU..NDIYO HAYO HAYO YAMESOMA YANAKULUPUKA KUFANYA VITU VYA KIJINGA KAMA KUUA MTU ALIYE KUGONGA GALI YAKO!

    ReplyDelete
  20. Let me explain Dual Citizenship/ Nationality in the case of USA since I have been here for a while...
    The concept of dual nationality means that a person is a citizen of two countries at the same time. Each country has its own citizenship laws based on its own policy.Persons may have dual nationality by automatic operation of different laws rather than by choice. For example, a child born in a foreign country to U.S. citizen parents may be both a U.S. citizen and a citizen of the country of birth.

    A U.S. citizen may acquire foreign citizenship by marriage, or a person naturalized as a U.S. citizen may not lose the citizenship of the country of birth.U.S. law does not mention dual nationality or require a person to choose one citizenship or another. Also, a person who is automatically granted another citizenship does not risk losing U.S. citizenship. However, a person who acquires a foreign citizenship by applying for it may lose U.S. citizenship. In order to lose U.S. citizenship, the law requires that the person must apply for the foreign citizenship voluntarily, by free choice, and with the intention to give up U.S. citizenship.

    Intent can be shown by the person's statements or conduct.The U.S. Government recognizes that dual nationality exists but does not encourage it as a matter of policy because of the problems it may cause. Claims of other countries on dual national U.S. citizens may conflict with U.S. law, and dual nationality may limit U.S. Government efforts to assist citizens abroad. The country where a dual national is located generally has a stronger claim to that person's allegiance.

    However, dual nationals owe allegiance to both the United States and the foreign country. They are required to obey the laws of both countries. Either country has the right to enforce its laws, particularly if the person later travels there.Most U.S. citizens, including dual nationals, must use a U.S. passport to enter and leave the United States. Dual nationals may also be required by the foreign country to use its passport to enter and leave that country. Use of the foreign passport does not endanger U.S. citizenship.Most countries permit a person to renounce or otherwise lose citizenship.

    Information on losing foreign citizenship can be obtained from the foreign country's embassy and consulates in the United States. Americans can renounce U.S. citizenship in the proper form at U.S. embassies and consulates abroad. I hope Wadau Mmenielewa vizuri!

    ReplyDelete
  21. DUAL CITIZENSHIP/NATIONALITY...
    I would like to post comments in this blog but will only base on the case of USA.
    The concept of dual nationality means that a person is a citizen of two countries at the same time. Each country has its own citizenship laws based on its own policy.Persons may have dual nationality by automatic operation of different laws rather than by choice. For example, a child born in a foreign country to U.S. citizen parents may be both a U.S. citizen and a citizen of the country of birth.

    A U.S. citizen may acquire foreign citizenship by marriage, or a person naturalized as a U.S. citizen may not lose the citizenship of the country of birth.U.S. law does not mention dual nationality or require a person to choose one citizenship or another. Also, a person who is automatically granted another citizenship does not risk losing U.S. citizenship. However, a person who acquires a foreign citizenship by applying for it may lose U.S. citizenship. In order to lose U.S. citizenship, the law requires that the person must apply for the foreign citizenship voluntarily, by free choice, and with the intention to give up U.S. citizenship.

    Intent can be shown by the person's statements or conduct.The U.S. Government recognizes that dual nationality exists but does not encourage it as a matter of policy because of the problems it may cause. Claims of other countries on dual national U.S. citizens may conflict with U.S. law, and dual nationality may limit U.S. Government efforts to assist citizens abroad. The country where a dual national is located generally has a stronger claim to that person's allegiance.

    However, dual nationals owe allegiance to both the United States and the foreign country. They are required to obey the laws of both countries. Either country has the right to enforce its laws, particularly if the person later travels there.Most U.S. citizens, including dual nationals, must use a U.S. passport to enter and leave the United States. Dual nationals may also be required by the foreign country to use its passport to enter and leave that country. Use of the foreign passport does not endanger U.S. citizenship.Most countries permit a person to renounce or otherwise lose citizenship.

    Information on losing foreign citizenship can be obtained from the foreign country's embassy and consulates in the United States. Americans can renounce U.S. citizenship in the proper form at U.S. embassies and consulates abroad. Thank you all!

    ReplyDelete
  22. Ni haki ya kidemokrasia iliyoko kwenye katiba ya Nchi ya Tanzania kwa mtu kwenda kokote na kuishi kokote iwe ndani au nje ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania.

    Kukataa ni kuwanyima uhuru ulioko katika katiba.Kukubali ni kuonyesha ukomavu wa Demokrasia nchini.

    Kama katiba inaruhusu kwa nini tuanze kubana watu kuwakatalia uraia wa nchi mbili hata 40?

    Mimi nawashangaa wasomi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam.
    Namshukuru Sana baba yangu aliuza ng`ombe zake zake zote 60 ili nije kusoma Marekani.Ningesoma Tanzania naona na mimi nigekuwa kituko wa mawazo finyu kama hao.

    Ni kichekesho wasomi wa Chuo cha Dar es salaam kupinga demokrasia ya mtu kuwa huru na kuwa raia iwe wa nchi moja au mbili au hata mia.Hivi kweli elimu ya Demokrasia wanasoma hicho chuo?

    ReplyDelete
  23. Mkitaka kujua faida ya ulaya wa nchi mbili kumbukeni Waziri wetu wa Fedha wa miaka mingi Amir Jamil, alijifanya mtanzania/ muhundi miaka kibao, siku aliyokufa Serikali ikataka kumzika kwa heshima zote, ikastukia jamaa alikuwa na mkoba wa kicanadia, matokea yake alizikwa na maponjoro wenzake hapo Toronto….

    ReplyDelete
  24. Hapa inaonekana kwamba nyie wenzetu ambao mlifanikiwa kuzamia ughaibuni hamuipendi nchi. Maana nyie kwenda kuishi huko ndiyo mnajiona mna akili na uelewa wa kila kitu, kiasi kwamba hadi mnafikia kuwaponda wasomi wa UDSM. Wengi wenu mlisoma hapa bongo, sijui ndugu zenu waliwaunganishia kwenda huko kwa kutumia hiyo hiyo serikali mnayoiponda leo, halafu mnajiona mme-win maisha. Hoja zenu zote ni za kijinga tu. Kama nyie ni Watanzania halisi naamini mngekuja huku ili tubanane humu humu. Lakini nyie mmepata hivyo Master's vyenu basi mnajiona ndiyo ma-geniuos kupindukia. Hivi mjiulize tangu mmezamia huko ni wangapi wamewekeza ndipo wajenge hoja ya kuwa raia wa nchi mbili, zaidi zaidi vidola mnavyotuma kwa wazazi wenu au wadogo ambavyo havina impact yoyote katika uchumi wa nchi. Nynyi huku ndiyo mmetawaliwa kifikra na hao wakoloni, maana mliikimbia nchi kwenda huko kuwa raia daraja la chini "second class citizen" halafu leo hii mnasema Tanzania tumelala, yaani nyie mnaona wanavyofanya wazungu ndiyo ujanja hivyo nasi tuige. What is globalisation kama siyo ukoloni mamboleo, na huo mfumo ndiyo mnaoutaka. Kwa kweli mnaboa, mimi naamini kama kweli nyie wazalendo njooni/rudini huku, siyo kuishi huko na kufanya vibarua mnajiona mmepata. Tanzania ni ya watanzania na itajengwa na watanzania, hivyo kama unaona Tanzania tupo nyuma, wewe kama Mtanzania njoo tuijenge nchi na siyo kuwa kuongelea maendeleo ya Watanzania wakati huchangii lolote. msiwe na mawazo ya kikimbizi, mnahifadhiwa huko kwa hisani halafu mnajifanya mmeukata. Ujanja ni kusoma huko na kurudi ujenge nchi siyo kuzamia huko. Wasomi wa UDSM wako sahihi, maana ndiyo hao wachache wanaouwakilisha umma wa Tanzania, kuliko wewe uliyezamia huko unamuwakilisha nani kama siyo kwa maslahi yako binafsi. Mheshimwa Michuzi hawa jamaa wa huko ughaibuni inabidi uwe makini nao sana kwenye blog yako maana wanajiona wasomi wakati hawana lolote wamejawa na ujinga tu wa kuamini kwamba Ughaibuni ndiyo kuna maisha bora. Njooni mjenge nchi yenu huku msipende vya dezo/bure (ready made)mtaolewa huko.

    ReplyDelete
  25. hao so called wasomi ni just another SAD CASE...tatizo sio kwa sababu wanapinga hiyo dual citizenship ila hizo sababu wanazotoa ni pumba ambazo sijawahi kuona na inaonekana wengi ni akili fupi tuu na roho ya kwanini? can you believe huyo mende eti anasema...if they truly love this country they should come and stay,why allow them come and go,na hawa ndio wasomi au wafagizi tuu?

    ReplyDelete
  26. Ubaya wa watanzania katika kila mjadala wanatia personal feelings. Kwa wivu pia hatujambo. Mungu ibariki Tanzania, viongozi na hasa watu wake. Uraia wa nchi mbili hauna ubaya wowote lkn mpende msimpende watu tunao tayari bila kibali official mimi nikienda tz natumia passport ya tz nikija huku natumia ya hapa na enjoy benefits za nchi zote mbili.

    Akhu nife maskini?! shauri zenu alalae usimwamshe
    Waridi

    ReplyDelete
  27. Watu wanatambiana maendeleo, wengine ndo kwaaaanza wanatambia kuishi Ughaibuni. Sasa mpaka usawa huu unajilinganisha na mtu alienyimwa viza, pole!

    ReplyDelete
  28. It is high time our countries start aknowledging our contributions to the society and give us more support.
    We demand this for ourselves and our offsprings born abroad.
    What a shame we did not get those schollarships like the brothers discussing this topic now had.
    It doesnot matter what passport I hold I will always be a Tanzanian at heart.
    All I am asking is my dear country to acknowledge that my son and daughters are Tanzanians as well.
    Otherwise I would have to cheer for them when the play for FRANCE national team !
    JK

    ReplyDelete
  29. Naona watu wengi hawapendi dual citizenship kwa sababu eti utanufaisha watu wachache sana. Kipi bora watu wachache kunufaika au watu zero kunufaika?

    ReplyDelete
  30. It is plain to see Our Schoolars have more often than not failed us !
    All these years of post colonial rule, Tanzania has not benefited much from our wasomi.
    It has been a catalogue of errors throughout the time. I can not see why we Tanzanians (born and breed !) can trust them on this .
    These wasomis have little or nor exposure at all of hence do not stand a chance to give their opinions.
    We are as much of Tanzanians as they are, but our similarities ends there !
    Let me point out this ! We are significant part of our country and want to be involved more !
    We want to vote !
    We want to be known as Tanzanians as well !
    and for George sake, These bigwigs thinks that is too much to ask !
    Kalagabaho ! Sisi ni watanzania kama mnataka ama laa ! tunataka muifanye official tupate vitabu vya kijani pia ! kama hataki tutapata na kama mnataka pia !
    Alamsiki !
    ABDUL

    ReplyDelete
  31. Michuzi naomba utusaidie kitu kimoja jaribu kwenda money gram au western union uulize watanzania walioko nje walicontribute kiasi gani mwaka jana , halafu baada ya hapo hizo data zipostiwe. Tusibishane tuu kama viraza ngoja tufuate facts hawa vijana wa UDSM pamoja na mwalimu hao wamekuwa misinformed.

    ReplyDelete
  32. INASIKITISHA KUONA MTU ALIYEISHI NJE YA NCHI KWA MIAKA 10 (MFANO HUYO JAMAA WA AUSTRALIA HAPO JUU), BADO HAJUI MAANA YA DUAL CITIZENSHIP-HAWA NDIO WATANZANIA AMBAO BADO WAKO ENZI ZA UJIMA, JE UTAWALAUMUJE WALE AMBAO WAKO NYUMBANI NA HAWAJAWAHI KUTOKA NJE YA NCHI??

    KWA KUANZIA, MAANA YA DUAL CITIZENSHIP HAIHUSIANI NA RAI WA NCHI NYINGINE ZA AFRICA, NI WATANZANIA AMBAO WANASTAHILI URAIA KWA MUJIBU WA SHERIA ZILIZOPO. KWA HIYO MTU YOYOTE ANAYEOGOPA WATUSI, WAHUTU ETI WATAKUJA KUCHUKUA URAIA, BASI NAOMBA AANZE KUJIELIMISHA MAANA YA DUAL CITIZENSHIP.
    AHSANTENI

    ReplyDelete
  33. Mengi yeshasemwa, nawasilisha niliyoyasoma leo kwenye ujumbe wa barua pepe toka kwa rafiki:

    Hawa wasomi wametoa pointi zifuatazo, that dual citizenship will:

    1. penalise Tanzanians because they dont have free movement (i.e. no free labor movement);
    2. itawanifaisha waTanzania walioko nchi za nje to the disadvantage of those at home; and
    3. it will allow foreigners to own land.

    Labor mobility and disadvantage for "wananchi"
    Navyoona mimi (warning: i have a vested interest here as a Tanzanian living abroad who wants the laws changed!!)point one and two hazina msingi kwani allowing the free movement of labour across borders is a policy issue that the Government will need to adress to comply with EAC requirements.
    The articles of federation, or whatever, commit the 3, now 5, governments to working towards this goal - kwahiyo point hii haina substance really. Kuwanufaisha watanzania abroad haina msingi pia because the opposite is true, that is waTZ hao wanataka kuishikilia TZ citizenship - this should actually maximise the chances of them bringing home wealth/mali created abroad.

    Wakiacha uraia mali hii itaishia nje - a very real issue kwani kuna madoctor,waliimu,engineers na maexperts wengi kutoka Africa ambao wanafanya hivyo - building the economies of the West because Governments in Africa do not allow them the opportunity to securely transfers their savings back home - kwasasa i think lazma uhonge kama unataka kufanya hivyo. Also kumbuka kwamba kuna watu wanchi za nje wengi tu (wasouth africa/wahindi etc) ambao wanarudisha divideds/profits za biashara zao makwao, as we speak, so the laws really don’t address or stop this fact - uraia utawapa incentive kuinvest hizo faida badala ya kuzituma "nyumbani".

    Dodgy foreigners owning our land
    So, having said this,it brings us to the last point which is the one that has substance au lenye msingi, the issue of foreigners owning our land. This is a real issue because foreigners (although they will not be foregners if they are citizens) owning land could raise security, economic and dual loyalty issues which, on the face of it, could be tricky to resolve. These are dealt with below.
    Economic issues could arise when rich foreigners outbid locals to purchase prime land, a move which can lead to social disintegration, in the local term, inequity and dislocation for some or a 2,3 tiered society ( off course this doomsday scenario overlooks the fact that the new owners might use the land more productively - through new technologies & know how - and create jobs in the process). Security issues arise where foreigners end up owning strategic pieces of land which might jeopardize the security of the nation in times of war etc. But again this overlooks the fact that in such circumstances the Government can legislate to change the law and compulsory acquire land - as Mwalimu Nyerere did enzi za ujamaa etc. On the question of loyalty, naona, at the end of the day, a piece of paper does not necessarily truly testify to someone’s loyalty, kuna watu wengi ambao, although they were/are not citizens of a specific country the loyalty they show through their actions goes beyond what most nationalists/patriotic people would ever dream of doing!

    Kwahiyo while this ownership issue seems big I don’t think it is enough on its own to stop reforms. Personally, I think the Government should change the law to allow dual citizenship and get around the land ownership problems by requiring that dual citizens who want to own land must go through a review board to ensure that the transaction will not adversely affect the country and will create welfare for Tanzanians. Most western countries do: the USA, Australia etc all allow dual citizenship and allow many “foreigners” to own land in their countries without any problems. Indeed a number of us wabongo in the west are beneficiaries of this.,from what I can tell Australia or the USA are not exactly suffering from such decisions. They get around the problem by setting up rigorous processes for vetting foreign ownership of strategic land and other “sensitive” assets, as a sovereign country we will reserve this right. Australia has its foreign investment review board (FIRB) which reviews all large foreign investment proposals to make sure that they are in the national interest.FIRB pays particular attention on reviewing the impacts of proposals to buy land in rural/regional areas to ensure these don’t adversely affect the communities and people there. We can also do this quite easily.

    On royalty, the US prevents anyone not born there from running for the presidency (i.e. candidate must be a natural born citizen) so na sisi tunaweza kutunga sheria zinazostahiliwa kuthibiti swala hili by extending such requirements to sensitive offices. So to end, mimi binafsi naona hawa wasomi wafanye more extensive analysis,preferably on countries that have dual citizenship, kwenye kuchangia kwenye debate instead of relying on short sighted and, at times, emotive logic.

    ReplyDelete
  34. Nimejaribu sana kusoma mawazo yaliyotolewa na wasomi wa chuo kikuu (UDSM) na vilevile kupitia mawazo ya wachangiaji katika blog hii, kwa ujumla ninayaheshimu sana.
    Lakini Mawazo ya Mandalu ni ya kinadharia zaidi and probably in the future anaweza kuwa a very good academician. Sijaona hiyo paper yake lakini kama kilichoripotiwa ni sahihi basi he lacks alot na inabidi afanye jitihada zaidi ili aweze kuwa msomi wa kuaminika na kuaminiwa. Sijambo lakudharau sana kwani matatizo mengi yanayotokea katika kufikia maamuzi yanayohusu maslahi ya taifa na wananchi wake huchangiwa na watendaji wasiokuwa na uwezo wa kujenga hoja sahihi.
    Dr. Coleman katika hoja yake juu ya mjadala huu sina hakika kama alikuwa katika upande wa kutoa changamoto hasi tu au kama ndio mtazamo wake chanya, basi ananipa mashaka makubwa juu ya kazi zake. Mimi binafsi simfahamu, na wala sijui ni mtu wa tabia gani. Lakini hata hivyo anaweza akatueleza kwa kinaga ubaga juu ya mawazo yake juu ya suala hili la uraia wa nchi mbili.
    Kama ambavyo ilivyodokezwa kuwa suala la uraia ni suala nyeti sana na vilevile kuwakatalia watu wachache kitu ambacho wanakihitaji ni kuwanyima haki zao za msingi.
    Kwa mfano, Katika maeneo ya kijamii kama hapo UDSM wanajamii wenye ulemavu ni wachache sana ukilinganisha na watu wote, lakini huwezi ukapinga miundo mbinu isibadilishwe ili kuwanufaisha wachache wenye ulemavu. Kwa vile wao wanahitaji miundo mbinu fulani usipowapatia ujue unawanyima haki yao ya kimsingi katika kushiriki sawa na wanajamii wengine.
    Si busara hata kidogo kupinga kitu tu eti kwa sababu wewe hutakitumia, la hasha, kumbuka wewe ni binadamu hujafa hujaumbika, unaweza siku ya siku ukawa pia ni mfaidika wa miundo mbinu hiyo labda uliyoipinga kwa kupewa wachache wahitaji.

    Jambo la msingi ambalo ninataka kulisema hapa ni kwamba mambo duniani yanakwenda kwa kasi kubwa sana, ambapo katika nchi zetu zinazoitwa 'nchi zinazoendelea' hatuendani na kasi hiyo. Zamani kulikuwa na msemo kwamba inabidi tukimbie ilituwakute hao waliondelea, sasa hivi nadhani tunatambaa, ukweli kabisa tumeachwa mbali kulikoni kipindi kile tuliposema tukimbie.
    Nichotaka kuchangia na wanablog wenzangu ni hivi, serikali ipo kwa ajili ya kuendesha nchi lakini maendeleo ya nchi huletwa na wananchi wenyewe na hususan wanapoweza kugundua fursa zilizopo na kuzitumia ipasavyo. Tuwe wabunifu sana na tutumie muda mwingi kwa kufanya kazi.
    Nawasihi wanazuoni wakae chini walete hoja zilizofanyiwa utafiti WAKUTOSHA na ambazo ni non-personal.
    Namalizia kwa kusema 'NAUNGA MKONO HOJA YA URAIA WA NCHI MBILI'

    ReplyDelete
  35. Michuzi nakushukuru saana kwa kutupa nafasi hii sisi Wazalendo kwa kuweza kubadilishana mawazo. Mimi ningeshauri wale wananchi wenzangu mlioko nyumbani na haswa wale ambao bado hamjafanikiwa kutoka mfanye utafiti(research)wa hasara na faida za hiyo "dual citizenship".
    "Exposure" ni kitu muhimu sana na ndio maana unaweza kuwatofautisha miongoni mwa viongozi wetu tulionao, jinsi wanavyo miliki madaraka yao.
    Basi wana blog tusitukanane, tujaribu tu kuwaelewesha wale wenzetu ambao hawafikirii mbali yaani huko tunakoenda.

    ReplyDelete
  36. acheni kuandika magazeti hatuna muda wa kusoma, kama huwezi kuandika mistari miwili acha kuchangia. mlimani hakuna wasomi akili zimeshazoea kukariri hawana upeo, na sisi hatuwezi kurisk tumetumia nguvu nyingi sana kuja ughaibuni na hii sio kazi bure kuna sababu

    ReplyDelete
  37. SIJUI KWANINI HAMTAKI DUAL CITIZENSHP. MNAOKATAA MUSWADA HII NI KWAMBA MPO BONGO NA HAMWEZI KUTOKA KWENDA HATA KENYA NDO MAANA MNAONA SERIKALI IKATAE. HEBU LIANGALIENI HILI SUALA KWA UNDANI ZAIDI SIO MNAROPOKA TU ETI KWAMBA WATU WACHACHE WATANUFAIKA. ACHENI HIZO. HAO WANAFUNZI WA MLIMANI NDO MAANA HATA KUPATA KAZI BAADA YA KUMALIZA SHULE WANASHINDWA KWA SABABU BADO WANA ZILI AKILI ZA NYERERE?

    ReplyDelete
  38. Kuna nchi kama UK haziwanyanganyi uraia wao na zinawapa wa kwao.
    Hapo nani mwenye faida?Hajakana kwao na ana dual citizenship

    ReplyDelete
  39. My 10 cents.
    Dual citizenship is an important matter and I belive there are valid arguments for both sides. However, I think it's important to base ones arguments from a neutral vantage without launching attacks on the basis of whether someone is in Tanzania, outside of Tanzania, rich, poor, educated, uneducated e.t.c

    Ad hominem arguments, [also known as argumentum ad hominem (Latin: "argument to the person", "argument against the man") consists of replying to an argument by attacking or appealing to the person making the argument, rather than by addressing the substance of the argument (wikipedia)] are thus irrelevant.

    Let us put our differences aside and figure out how to help this nation of ours.
    Have a blessed day,
    ~Dave.

    ReplyDelete
  40. Jamani tulishasema zamani kuwa graduates wa UDSM na wanafunzi wa pale wengi bado ni VILAZA au kama wanavyojulikana na wengi kwa jina la VIHIYO. Mtaala mzima wa kile chuo inabidi ufanyiwe marekebisho makubwa ili wanafunzi wanaosoma na kumaliza UDSM waweze kuwa na upeo wa kuchanganua mambo mbalimbali kiufasaha na kwa uelewa wa hali ya juu. Wengi wanaomalizaga pale halafu wakapata nafasi za kusoma abroad hushangazwa na jinsi ule mtaala wa UDSM ulivyowadumaza na kuwafanya wagumu wa kuchanganua mambo.

    Majibu ya hawa wanafunzi wa Masters na hata huyo Mkufunzi wao yanaonyesha mapungufu makubwa kwenye uelewa wa suala la uraia wa nchi mbili. Kila nchi inayoruhusu uraia wa nchi ina sheria zake ambazo mara nyingi zinawekwa ili kulinda na kuhakikisha raia wao wa kuzaliwa hasa wale wenye roots kwenye hiyo nchi husika wanachangia kikamilifu maendeleo ya hiyo nchi.

    Mtanzania wa kuzaliwa Tanzania na mwenye ndugu au hata wazazi ambao bado wapo Tanzania na akaenda kuchukua uraia mfano wa Marekani hata akae nje miaka 20 siku zote mapenzi yake yatabaki kuwa ni Tanzania. Jamani dunia inabadilika na zile siasa za zamani za kijamaa zimeshakufa kwa hiyo ndugu zangu wa UDSM hebu think globally na muondokane na fikra za kijima na kijamaa.

    Mungu Ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  41. aaah mimi namhurumia sana rais wangu jk, kama hao ndio wasomi wanaopaswa kumshauri kisera, kuplan mipsango ya maendeleo na mikakati ya kupunguza umaskini, wana lack exposure na kuwa na mawazo mgando kama hayo ya kupinga tu dual citizen bila hata facts za maana. hawajui hata dunia inaendaje now,curricculum ya elimu inafaa ibadilishwe sasa TZ ili kuinua ki exposure ya nini kinaendelea duniani, tutaishia kuwa manamba na wivu tu,
    dual citizen ship ni muhimu, am surein two years jk ataipitisha.

    ReplyDelete
  42. Michuzi:
    Hao wabongo walio ughaibuni ukiwauliza ni sababu zipi ziliwafanya waukane uraia wa Tanzania, nyingi zitakuwa sababu BINAFSI, siyo kwamba walikuwa na vision ya kuisaidia Tanzania kwa wakati huo! Na hata baada ya kupata uraia, walio wengi focus yao imekuwa'family' na ndugu wa karibu...siyo taifa. Hata ukienda kupata data za pesa zilizotumwa kupitia Western Union/Money Gram, nyingi ni kwa ajili ya ada tu na kusaidia ndugu, not serious money. Ni kwa sababu hizo hizo na UBINAFSI, ndiyo wanakuja na hii hoja. Swala siyo ubaya wa hoja, bali nia ya watu wanaileta hiyo hoja. Kwanza umeshaona mwenyewe baadhi ya comments za hapa kwenye blog, wengi wanaonesha kuwa egostists, wanadhani hawana cha kupoteza. Kama huna cha kupoteza kwa kukataliwa uraia, sasa kwa nini unahangaika? Mnapotetea kizazi kijacho, kwani mlipochukua uraia wa nchi nyingine hamkufikiri juu ya repurcusions zake? POOR PLANNING ON YOUR PART DOES NOT NECESSARILY CONSTITUTE AN AUTOMATIC EMERGENCY/RESPONSE TO ANOTHER PART.
    Halafu hao wanaojiita wasomi walio nje, kwa nini wanadhani wako more smart na analytical kuliko walio nyumbani? Kwa nini wanakandia ubora wa elimu ya UDSM? Wanajua ni watu wangapi wanajiunga na masomo nchi za nje (Higher level)kwa kutumia vyeti vya UDSM, na wakifika huko wanakuwa monsters (yaani wakali?, kuonesha kuwa background yao inatambulika na vyuo vya nje na wana justify kwa matokeo mazuri? Wengi wanaokandia UD ni wale waliokosa admission pale na wakazamia nje na kuanza shule 'community colleges' na`'intensive english programs' ambazo ndiyo wametumia kupatia viza!
    Hoja ni nzuri lakini nia ya walioipendekeza ndiyo inatakiwa kupimwa kwenye mizani. We need justification ni kwa vipi watanzania walio nje wanachangia uchumi (acha hizo dola chache za wazazi na ada). Swala siyo exposure/lack thereof, swala siyo WIVU wa wasomi wa UDSM, swala ni NIA nzima ya walio nyuma ya huo muswada, kwa perspective ya tabia za ki Tanzania!
    Asante

    ReplyDelete
  43. Wasomi wa chuo kikuu wote wana vikwapa. Na wengi wao ni washamba waliotoka vijijini. Asilimia kubwa ya wasomi wa Udsm wana Ukimwi.

    ReplyDelete
  44. Nchi nyingine ukipata uraia na una miaka ya chini ya 27 - kama sikukosea kwa mfano Amerika, inakubidi ujiunge na jeshi.

    Kama vita itatokea kati ya Amerika na Tanzania, utapigania upande gani?

    Kama u raia wa nchi mojawapo, kwa mfano Amerika au Uingereza au Ufaransa au Ujerumani, na vita itokee kati ya nchi yako hiyo na Nigeria au Libya au Angola au Sao Thome and Princippe au Sudani, utapigania nchi gani?

    Ukiwa raia wa Tanzania unajumuishwa katika ulinzi wa Bara letu.

    ReplyDelete
  45. Ningependa Dual Citizenship iwepo.
    Kwa yenu yote hapo juu ongezeni:
    1. Naamini elime (ya kitabu) UDSM iko juu na wote waliopita hapo vizuri hawapati taabu ktk masomo zaidi nje.Inabakia msemo kuwa kwenda shule sio kuelimika kimaisha...
    2. Ninavyoelewa mimi hoja ni MBONGO kupata uraia wa pili na sio mraia wa nje kupata uraia wetu na kubakiza passport ya kwao. Wote tunaelewa kuwa pass yetu inanunulika na watu hawajifunzi hata maneno kidogo ya kiswahili!!!
    3.Mtu kuwa nje hakumfanyi yeye awe less tanzanian.
    Blackmpingo

    ReplyDelete
  46. Siamini kuwa mtu anapata shahada ya pili kwa kuandika pumba kama hizo hapo juu. Mpaka leo watu hawajui faidi ya uraia wa nchi mbili. Hizo nchi zote ambazo kikwete ana omba omba zina uraia wa nchi mbili. Jaribuni kuwaiga basi.

    ReplyDelete
  47. UJUMBE KWA DADA MGOSI!
    MGOSI UNA HASIRA KICHIZI, SASA KWELI UNATAKA KUKOMPARE ELIMU YA BONGO NA UK,AUSTRALIA AMA MAREKANI? WAKATI WEWE UNAKAA CHINI PALE UD WENZAKO WANAFUNDISHWA HUKU WANA KULA BURGER DARASANI,WAKATI WEWE UNAANDIKA PAPER SIKU TANO KWA MKONO WENZAKO KILA CORNER KUNA COMPUTER, WAKATI UNASUMBULIWA NA SUP. WENZAKO WANA DUNDA TU, KUNA MILOLONGO MINGI SANA JARIBU KUJIULIZA MASWALI MADOGO TU, KWA NINI MAKENYA NA MAGANDA YANAPATA KAZI KILAHISI BONGO? JIBU SI LEFU WABONGO MLIOSEMEA NA KUKULIA BONGO WENGI WENU NI MAMBUMBUMBU! UNAONA KUNA WIMBI LA MABONGO YANA ENDA KENYA NA KUKOMBA KAZI? HAYA ONA JINSI WIMBI LA MABONGO YALIYO MALIZIA UGHAIBUNI YOTE YANAKOMBA KAZI NZURI NZURI TU MGOSI MIMI NAKUHESHIMU LAKINI KIWANJA NOMA NJOO UJIONEE USINGOJE YA KUSIMULIWA DADA YANGU, BY THE WAY KIKWETE WATOTO WAKE WAKO LONDON, SUMAYE ANASOMA HAVARD, MKAPA VIJANA WAKE WANASOMA CANADA NA WEWE UDSM DAMN! MBONA HASIRA INANIPANDA!

    ReplyDelete
  48. Michuzi blogu yako imetembelewa na watu wengi,fine, tatizo wenye vichwa vya aina gani! Katika koments 47, chini ya 10 zina point, zilizobaki ni maoni ya vijamaa vinavyobalehe! Mbaya zaidi vinavyobalehe wakati ishakuwa "jioni"!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...