Barua YA Wazi Kwa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Mheshimiwa Rais, hii ni barua ya kuelezea malalamiko yetu watanzania juu ya utendaji wa kazi wa TBS (Tanzania Bureau Standard), kufuatia hatua iliyochukuliwa na TBS kuwazawadia WTM utility-http://www.wtmutilityservices.com/ zabuni ya ukaguzi wa magari yanayosafirishwa toka United Kingdom kupelekwa Tanzania.

Muheshimiwa rais mengi ya malalamiko na maswali muhimu yameulizwa na wananchi, juu ya zoezi hili zima la ugawaji wa hii zabuni ambao umeenda kinyume na taratibu nzima za ugawaji wa zabuni hiyo. Baadhi ya sehemu ya hayo malalamiko yameelezwa wazi katika blog za wananchi, ambazo inaonyesha wazi malalamiko na kutoridhishwa kwao.

Kama utapata fursa pitia.
http://wemsas.blogspot.com/ Jumuiya ya Waswahili UK
http://www.tzcommunity.co.uk/ Jumuiya ya Watanzania UK
http://saidiyakubu.blogspot.com/2007/06/katika-taarifa-kwa-vyombo-vya-habari.html
http://tbswtmuncovered.blogspot.com/2007/06/tamko-rasmi-la-wtmtbs-uncovered.html

Muheshimiwa Rais, lazima ifahamike sisi wananchi hatuendani kinyume na taratibu za kudhibiti ubora wa magari au bidhaa nyengine zozote zinazoingizwa nchini toka nchi za nje, tunalopingana nalo ni ubora wa maamuzi ya TBS na ile kampuni iliyozawadiwa zabuni ya kufanya zoezi hilo, WTM utility

Muheshimiwa rais, kwa ufupi huku Uingereza, kipo kitengo maalum ambacho kinaangalia na kuongoza zoezi zima la ukaguzi wa magari madogo na makubwa(malori), kitengo hiki cha serikali kimeweka taratibu, njia na misingi kabambe ambayo kampuni ya WTM utility pekee haina au haiwezi kutimiza au kufikia viwango hivyo muhimu vilivyotolewa na VOSA-Vehicle and Operator Services Agency. Kitengo hiki maalum cha serikali ya Uingereza kinasimamia sehemu moja ya ubora wa magari yaliyo barabarani Uingereza kwa ujumla http://www.vosa.gov.uk/, au kwa jina maarufu inaitwa MOT.

Muheshimiwa rais, kitengo hiki cha serikali kinatoa vibali maalum kukagua magari kwa maelefu ya garage huko UK, ambayo idadi yake hadi kufikia mwaka jana ni 18300, ambavyo vinaendana na kanuni, ziliwekwa wazi kabisa kuhusiana na uangalizi wa magari yote Uingereza chini ya uangalizi wa kitengo hiki cha serikali- VOSA.

Swala la kujiuliza muheshimiwa Rais hawa WTM utility, wana garage moja au mbili katika nchi nzima ya Uingereza, na vile vile wanadai wanahimili mobile Units ambazo pia zitatumika katika zoezi hili la ukaguzi wa magari, hii peke yake inaenda kinyume na sheria na kanuni za sehemu ya ukaguzi wa magari, zaidi pitia hii tovotu inayoelezea wazi ya hizo kanuni za ubora wa sehemu ya ukaguzi.
Muheshimiwa rais, haya ni maswali muhimu ambayo tunakuomba sisi watanzania tunaoishi huku Uingereza, kuwauliza hawa TBS.

Je waliweza kuwasiliana na VOSA au ministry of Transport UK na jumuiya ya wafanyabiashara Uingereza na Tanzania, kuhusiana na zoezi hili zima la ukaguzi wa magari, kwa sababu ya kuuliza swala hili muheshimiwa rais ni kwa ajili ya kufahamu kama haya maamuzi yamepitia moja ya vipengele vyao vya kisheria katika kufikia maamuzi ya swala lolote linalohusiana na utungaji wa sheria ya viwango.
QUOTE
Preparation of Standards
Tanzania Standards are the national documents prepared through consensus of all interested parties i.e. consumers, producers buyers, research institutions, etc standard specify inter alia quality requirements for final products, sampling procedures, test methods, labelling, and good manufacturing practices… UNQOTE
Soma zaidi kupitia huo mtandao hapo chini..
http://www.tptanzania.co.tz/tbs_body.html
Je ni vipi WTM wataweza kuitumikia nchi nzima Uingereza, katika zoezi hili, hali ya kuwa garage ya zaidi 18000, ambazo zimesambaa Uingereza nzima, ambazo pia ndio zenye kufanya zoezi hilo hilo ambalo litafanywa na WTM utility, peke yake wenye garage 2 na mobile unit moja tu ?

Muheshimiwa Rais, sisi kama watanzania http://wemsas.blogspot.com/ tunaoishi huku UK, wengi wetu tunamadhumuni makubwa kabisa ya kuiendeleza nchi yetu katika sekta za kibiashara (import/export) na uwekezaji wa vitega uchumi ndani ya nchi. Yote haya ni makusudio ya kuweza kujisaidia na kujikwamua kiuchumi sisi wenyewe binafsi, ndugu, familia na watanzania walio chini kimapato, hii yote ni katika juhudi za kupigana vita na umaskini kama ilivyoolezewa katika ripoti ya mkukuta. http://www.povertymonitoring.go.tz/

Muheshimiwa Rais baadhi ya maelezo ambayo yameelezwa katika ripoti hiyo ya mkukuta moja wapo ni kipengele cha tatu Governance and Accountability. Mwenendo wa TBS unaenda kinyume kabisa na vipengele vyote vilivyoelezwa katika ripoti hiyo muhimu ya kuondoa umaskini. Muheshimiwa Rais, TBS inakiuaka na kuzorotesha juhudi za MKUKUTA, kwa hiyo basi inarudisha juhudi za wananchi walio wengi katika kujikwamua na umaskini.
Baadhi ya hivyo vipengele kutoka ripoti ya 2006 ni kama ifuatavyo.

Quote
MKUKUTA CLUSTER III: Governance and Accountability
Assessment of broad outcomes
Assessment of cluster goals:
GOAL 1 Structures and systems of governance as well as the rule of law to be democratic, participatory,
representative, accountable, and inclusive
GOAL 2 Equitable allocation of public resources with corruption effectively addressed
GOAL 3 Effective public service framework in place to provide foundation for service delivery improvements
and poverty reduction
GOAL 4 Rights of the poor and vulnerable groups to be protected and promoted in the justice system
GOAL 5 Reduction of political and social exclusion and intolerance
GOAL 6 Improve personal and material security, reduce crime, and eliminate sexual abuse and domestic
violence
GOAL 7 National cultural identities enhanced and promoted
Unquote

Muheshimiwa rais tunakwamishwa vibaya na vyombo vya serikali, kama hiki cha TBS, mstaafu mwenyekiti wa TBS hapo awali, Mwakyembe aliwahi kusema “TBS siyo jeshi la ulinzi la Polisi” ambapo baadhi ya hotuba yake ilitolewa na gazeti binafsi kwenye tovotu hii http://www.ippmedia.com/ipp/guardian/2007/03/26/87090.html

Maombi ya Wafanyabiashara na Wananchi kwa ujumla.

Muheshimiwa rais, tunachokiomba sisi wananchi tunaoishi huku UK, tunakuomba utumie fursa yako, kwa kuuunda tume maalum ya kujitegemea kuchunguza swala hili, kama hivyo itagua vigumu muheshimiwa rais tunakuomba kupitia taasisi ya kuzuia rushwa http://www.tanzania.go.tz/pcb/rushwa/majukumu.html, kuweza kulifikisha swala hili na kuchunguzwa ipasavyo.

Kwa kumalizia.

Muheshimiwa Rais Nitakupa hadithi moja NASA - National Aeronautics and Space Administration ya Marekani, walitumia karibuni milioni moja dola, kwa kufanya utafiti wa kalamu itakayotumika kwenye SPACE shuttle.. Russia waliamua kutumia PENCIL. Je hii habari inalingana na hii ?? Ni kitu cha kujiuliza.

Ni mahisio yetu serikali ingetamka rasmi kupitia TBS, kwamba gari yoyote inayotoka Uingereza, ambayo itatumika Tanzania lazima iwe MOT certified, hilo lingeeleweka wazi kabisa, wengi tungelikaribisha na kulihimiza.

Shukrani Sana kwa kuchukua ujumbe wetu, ni mategemeo yetu tutapata maamuzi ya haraka. Na vile vile tungependa kutoa pongezi zetu za wazi zikufikie wewe pamoja na utawala wako katika kuweka uwazi katika maamuzi ya kiserikali yanayohusu wananchi au nchi nzima kwa ujumla.

Daima tutatumia fursa hii kupitia tovotu yako maalum kuleta mapendekezo au hoja zetu pale inapotubidi tufanye hivyo.
http://www.jakayakikwete.com/tanzania/pages/Ask-the-President

Mungu Ibariki Tanzania.

Shukran!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2007

    Duh ebwanaa ndio,jamaa hawa wanadhani kila mtanzania anaishi London, mambo ya kupeana mtaji wenyewe kwa wenyewe yataisha lini na ndio maana rushwa na maendeleo ni ovyo tanzania,hawa jamaa wanataka kutu umiza tuu hawana lolote, wale kona..rahisi Handsome wtf is this..nae hana muda atatemwa tuu na wananchi kazi kuzurura tuu kama mwanamuziki anazindua album kha

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 16, 2007

    ljAmAnI mNaWeZa FuAtILiA gAmE lA sTaRs Na BuRkInA fAsO hApA. HaKuNa PiChA nI mAeLeZo tU LkN LIVE!!!!

    http://news.bbc.co.uk/sport2/hi/football/africa/6759819.stm

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 16, 2007

    jAmAnI mNaWeZa FuAtILiA gAmE lA sTaRs Na BuRkInA fAsO hApA. HaKuNa PiChA nI mAeLeZo tU LkN LIVE!!!!

    http://news.bbc.co.uk/sport2/hi/football/africa/6759819.stm

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 16, 2007

    asante kwa kunifahamisha kuhusu swala hii.

    Rais Jakaya Kikwete alipoulizwa kuhusa mambo ya rada, alijibu kuwa, kama rushwa ilikuwepo, angeomba chenji yetu kutoka kwa serikali ya UK. Hakusema chochote kuhusu kuandaa uchaguzi wa ununuzi wa rada hapa tanzania au kuomba 'chenji' kwa akaunti zile pale Uswisi.....

    Nauliza, je, barua hii itatusaidia vipi?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 16, 2007

    Mheshimiwa kifimbocheza, kinachotakiwa ni sisi kuhimiza majibu kutoka kwa mheshimiwa rais, yeye ameweka tovuti yake wazi ili sisi wananchi tuwasilishe kero sasa unapouliza itatusaidia nini hiyo barua hapo juu unakwamisha jitihada za kutaka kupata suluhisho la tatizo!! barua imejieleza vizuri tu tumia hekima tafadhali-Cass

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 17, 2007

    Cass, asante kwa jibu lako. Kwanza, mimi nimefurahi kusoma barua hii na kuona kuwa wananchi wanaomba uwajbikaji wazi. Nawapongeza waandishi kwa jitihada ya kupata suluhisho.

    Lakini wasiwasi nayo. Tumesoma kwenye vyombo vya habari kuhusu Benki Kuu ya Tanzania, Rada, IPTL, Richmond.... foleni ndefu. Lakini je, wananchi wamepata uwajibikaji? Sitaki kusema kuwa watu wasijitahidi. nasema kuwa itakuwa ngumu tu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 17, 2007

    NAITWA HAKI WA HAKI.
    SUALA LA TBS NA MAWAKALA WAO AMBAO NI WANAMTANDAO, NI WIZI WA WAZI NA UKIUKWAJI WA MISINGI YA UTAWALA WA SHERIA, HAKI NA USAWA.
    yAMESEMWA MENGI, NA JITIHADA ZA KILA NAMNA ZIMEFANYIKA HADI HII YA KUMTAKA RAIS AUNDE TUME AMBAYO NAYO ITATAFUNA PESA ZA WALALA HOI. HIYO SI SULUHISHO.
    KWA KUTUMIA MFANO WAKO WA NASA, JIBU NA DAWA MUJARABU NI SISI WATANZANIA NIKIMAANISHA SI TU WAISHIO UK BALI WATANZANIA WOTE KUUNGANA NA KULIPELEKA SUALA HILI MAHAKAMANI. USHAHIDI NA ITHIBATI ZIPO. MAHAKAMA IFANYE KAZI YAKE NA ITUPE HAKI YETU NA KUKOMESHA DHULUMA NA WIZI HUU.
    USIMWENDEE KIKWETE HANA LA KUKUSAIDIA. HUO NDIO UKWELI. ACHA SHERIA ITWAE MKONDO.
    NITAKUPA MFANO WA KAZI YA MAHAKAMA NA INAVYOTOA NA KUSIMAMIA HAKI ZA WATU. KUNA DIWANI MMOJA WA KATA MULEBA HUKO KAGERA, MH. HASSANI MILLANGA, ALINYANG'ANYWA UANACHAMA WAKE NA VIGOGO WA CCM KWA MIZENGWE NA KUKIUKA KATIBA YA CCM. REDIO TANZANIA ILITANGAZA WALIOSIKIA WATAKUMBUKA. KWA UJASIRI NA USHUJAA AKAFUNGUA KESI MAHAKAMA KUU KUPINGA DHULUMA NA UKIUKWAJI WA KATIBA YA CCM ULIOFANYWA NA VIONGOZI WAKE.
    HUKUMU ILIPOTOLEWA MH HASSANI ALIRUDISHIWA HAKI ZAKE IKIWA NI UANACHAMA NA UDIWANI.
    NAUUTUMIA MFANO HUU KUONYESHA KUWA HAKI HAIDAIWI KWA RAIS AU MWENYEKITI WA CCM, INADAIWA MAHAKAMANI. SWALI NI KWA NINI HATUTAKI KUIDAI HAKI HII MAHAKAMANI? AU HATUNA IMANI NA MAHAKAMA ZETU? AU NI KUPUMBAZWA NA KASI MPYA ISIYO NA MWELEKEO? NAOWAOMBA WATANZANIA WOTE KUSIMAMA KIDETE KUHUSU SUALA HILI HADI HAKI ITENDEKE NA IPATIKANE.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 17, 2007

    Ningeomba WTM watueleze magari yanayotakiwa Tz yanahitaji maongezeko gani ambayo hayapo kwenye standard yaliyonayo

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 17, 2007

    Kifimbocheza, hapa kinachotakiwa ni kuweka shinikizo kwa wanaohusika na waajiri wao. Suala la Benki Kuu ya Tanzania, Rada, IPTL, Richmond...foleni ndefu inaelekea wahusika hawakupata shinikizo la ktosha ndiyo maana they got away with it. Kama wangeikaliwa kooni hawa waheshimiwa, amini usiamini watu wangewajibika; we have seen this before.

    "Our lives begin to end the day we become silent about things that matter" - Martin Luther King Jr.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 18, 2007

    Ninaunga mkono hoja ya mweshimiwa hapo juu na nukuu yake ya Martin Luther King Jr. Kwa mtazamo wangu suala la WTM limetuleta pamoja Watanzania hasa tuishio nje, sasa wazee kwanini tusilifikishe suala hili mahakamani!? nina wasiwasi tutaishia kulalama tu na hapo ndipo itakuwa mwanzo wa mwisho wa maisha yetu kama Luther king Jr. alivyonukuliwa-Cass

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 20, 2007

    jamani naombeni kufahamishwa wastani wa magari yanayoingizwa tanzania kutoka uingereza ni kiasi gani(idadi) ili niweze kuchangia. kama idadi itakuwa ni negligible nitahisi kuna mgongano wa kimaslahi kati ya wamiliki wa WTM sijui na watu wanaoipigia kelele kampuni hii! naomba kuwasilisha!

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 20, 2007

    jamani naombeni kufahamishwa wastani wa magari yanayoingizwa tanzania kutoka uingereza ni kiasi gani(idadi) ili niweze kuchangia. kama idadi itakuwa ni negligible nitahisi kuna mgongano wa kimaslahi kati ya wamiliki wa WTM sijui na watu wanaoipigia kelele kampuni hii! naomba kuwasilisha!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...