wacheza sinema maarufu toka hollywood matt damon (kulia) na ben affleck (shati jeupe nyuma) wakipozi na wadau walipotembelea bongo wiki ilopita. hawa mabwana waliokuja na kuondoka kinyemela walikuwa hapa kungalia namna ya kutoa msaada kwa wenye shida kama vile yatima

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hawa wawili ukiambiwa kuna rafiki wa kweli basi ndio hawa they are very down to earth na ukiangalia historia yao kweli utajua kuwa kuna marafiki na marafiki ulimwengu huu.

    Hawataki makuu kabisa hawa ndio maana hata Ben alimshindwa J'lo na sasa hivi yupo so fine na mke na mtoto wake na huyo mwingine naye poa na mke wake na step daughter wake na mtoto wake ...I love them so much ....

    ReplyDelete
  2. Karibuni nyumbani lakini jitahidini muwe waangalifu ili misaada iwafikie walengwa. Kwani kuna kundi la mbwa koko wachache/mafisadi, ndiyo mbwa koko wanaweza kula pesa zote na walengwa wasipate kitu.

    ReplyDelete
  3. Kama kuna wanafiki hapa duniani basi wa kwanza ni wadhungu. Huku Marekani kuna watu wanalala mabarazani kibao,wanaitwa "homeless" hawana nyumba wala ardhi, hawana msaada wowote toka kwa mtu, eti wao wanakimbilia kusaidia Africa!!! Hapo kuna utata. Sipendi unafiki.

    ReplyDelete
  4. Hela zinaenda kwa wajanja wachache tu. Bora wangewekeza kwenye mambo ya kutengeneza kazi. e.g wafungue kiwanda ambacho kitaajiri watu. ila misaada ni buree kabisa. Miaka mingapi sasa toka misaada imeanza kumiminika ila hakuna kipya?

    ReplyDelete
  5. Mje kuwekeza sio kutoa misaada.Wawekezaji wa Ukweli sio matapeli wa kukwepa kodi. Misaada inazidi kutufanya tuwe masikini. Fungua kiwanda cha uzalishaji hapo mambo yatakuwa mazuri

    ReplyDelete
  6. Mimi nimekerwa na hawa watu wanaowalaumu Ben na Matt kuja kusaidia Tanzania wakidai kwamba Marekani kuna homeless kibao. Sasa homeless si wana misaada kibao hila ni walevi na wanatumia drugs. Kama ni chakula na homeless shelter zipo nyingi tuu, kwahiyo hawa ni ma homeless wanaojitakia.Na kuhusu huyu jamaa anayetaka wafungue viwanda. Kama mtu anataka kukusaidia wewe kaa chini na usaidiwe usianze kutaka makuu. Kusaidia Africa kwa wao ni tax saving purposes wakati wewe mwafrika unanufaika, na kuingiza hela kwenye Circulation. Kufungua kiwanda bongo ni kujitia headache tuu kwa mtu kama Ben na Matt.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...