Dkt Shein kushuhudia mbio za Fisi Bagamoyo


MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Ali Mohamed Shein kesho Jumanne atashuhudia sanaa ya kucheza na kukimbia na Fisi kutoka kwa wasanii kikundi cha Sanaa cha Geita wakati akifungua Tamasha la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na waandaji wa Tamasha hilo, kikundi hicho ni miongoni mwa vikundi vitatu vilivyopangwa kufanya maonyesho wakati wa sherehe za ufunguzi wa tamasha hilo, zitakazofanyika kwenye jukwaa la kihistoria la Miembeleni katika Chuo cha Sanaa bagamoyo.

Msemaji wa Chuo cha Sanaa, Elangwa Mtahiko amesema mbali na Dkt. Sehin kushuhudia sanaa ya kucheza na wanyama hao jukwaani, pia atapata nafasi ya kuona ngoma za asili kutoka chuo cha Sanaa na kikundi cha Ruvu JKT ambacho kitacheza ngoma maalum ya Kizanzibar.

“Ngoma ya Kizanzibar ni kumfanya aone upande mwingine wa Tanzania, hasa ikizingatiwa kuwa yeye ametokea huko Tanzania visiwani, lakini pia kutakuwa na wimbo maalum ambao utaimbwa na chuo cha sanaa, na pia ngoma nyingine ya asili kutoka katika moja ya makabila ya huku Tanzania bara,” alisema Mtahiko.

Alisema pia pamoja na hayo pia Makamu wa rais atapata nafasi ya kuangalia maonyesho ya Sarakasi kutoka kwa wasanii wa chuoni na kikundi cha watoto cha Shada.Pamoja na shughuli za ufunzi pia Dkt Shein atakagua maonesho ya sanaa za ufundi na pia kukagua maendeleo ya ujenzi wa ukumbi mpya wa kisasa wa maonyesho (pichani) unaojengwa Chuoni hapo. mwisho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kwenye mbio za fisi mnampeleka Dr. Shein safari za ughaibuni wanakwenda manyang'au...

    ReplyDelete
  2. mbio za fisi! mh maendeleo! hivi mbio hizi zinasaidiaje kuondoa haya:maradhi,ujinga na umaskini? Je huu sio ukatili kwa wanyama? Waacheni fisi wakaishi huko kwao(porini),na nyie mkapande punda, farasi na ngamia. Na wewe Shein huna la kufanya?

    ReplyDelete
  3. hala hala FISI hao jamani!
    Hivi aking'atwa na hao fisi ndo ikatangazwa kwenye vyombo vya habari dunia nzima kuwa "Makamu wa Rais wa Tanzania Ang'atwa na Fisi" si itakuwa ni kichekesho hiki jamani!?!
    Mweeh!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...