MWANDISHI wa habari mwandamizi Godfrey Mhando (63) amefariki dunia leo asubuhi jijini Dar es Salaam kwa matatizo ya moyo.
Mhando ambaye hadi kifo chake alikuwa mhariri msanifu (sub-editor) wa gazeti la KULIKONI, linalochapishwa na Kampuni ya Media Solutions Limited alifariki leo asubuhi muda mfupi baada ya kufikishwa katika hospitali ya Burhani.
Familia ya marehemu ikielezea kuhusu kutokea kwa kifo chake, ilieleza kuwa Mhando leo asubuhi alikuwa amejiandaa kuelekea kazini, lakini kabla hajaondoka nyumbani, alijisikia vibaya, hasa kubanwa na kifua na mapigo ya moyo kuongezeka, ndipo alipopelekwa hospitali ya Madonna, iliyopo Tabata.
Hata hivyo, madaktari walishauri apelekwe hospitali ya Amana, ingawa familia iliamua kumpeleka hospitali ya Burhani ambako alifariki dunia hata kabla ya kuanza kupatiwa huduma.
Mhando aliwahi kuajiriwa na Kampuni ya magazeti ya Chama Cha Mapinduzi ya Uhuru na Mzalendo ambako alifanya kazi kwa muda wa miaka 30 kabla ya kustaafu mwaka juzi kujiunga na Media Solutions Limited kama mwajiriwa wa muda (part-time staff).
Alizaliwa mwaka 1944 jijini Dar es Salaam na kupata elimu yake ya msingi katika shule ya Mchikichini kuanzia mwaka 1952 hadi 1955 na kuendelea na shule ya kati ya wavulana ya Uhuru hadi mwaka 1959 alikohitimu.
Kuanzia mwaka 1960 hadi mwaka 1964 alijiunga na Shule ya Sekondari Kiungani, Zanzibar na baadaye kwenda Chuo cha Kimataifa cha Mawasiliano ya Umma cha Szechoslovakia ambako alisoma uandishi wa habari na kutunukiwa stashahada.
Alirejea nchini na kuanza kazi Uhuru na Mzalendo akiwa mwandishi wa habari na mwaka 1990 hadi 1991, alikwenda Ujerumani kwa masomo ya Sayansi ya Jamii katika chuo cha Magdeburg ambako alitunukiwa stashahada.
Mhando ameacha mke na watoto kadhaa. Taratibu za mazishi zinapangwa na familia ya marehemu Mhando nyumbani kwake Tabata Segerea, eneo la Mangumi.

UTAWALA
Media Solutions Limited
30 Oktoba, 2007

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. RIP. ..

    Kulikua na mwandishi sijui mtangazaji naye alikua anaitwa something like Tido Mhando sijui ndio yeye.

    Hizi heart attack hazina jinsi wanasema asprin a day can save your life lakini siku ikifika imefika.

    Poleni wafiwa

    ReplyDelete
  2. Salamu zangu za rambi rambi ziifikie familia nzima ya Marehemu Muhando. Alikuwa jirani yangu pale Victoria kwa kingunge. Pole sana Mama Maumba,maumba, toni, zawadi, na watoto wengine wote wa Marehemu.
    We are sailing together in this tough time to endure the lost of beloved dad and neighbour.

    Katty.
    Wilmington, DE.

    ReplyDelete
  3. Poleni wafiwa. Dunia ya uandishi wa habari Tanzania umepoteza mwingine katika kipindi kifupi.

    Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni. AMEN.

    ReplyDelete
  4. HAYA NI MAMBO YA MA KUKU BIA NA KITI MOTO

    ReplyDelete
  5. Poleni sana wafiwa!!! Mdau hapo juu amenikumbusha sana familia ya Marehemu Mhando kwani mi pia nilikuwa jirani pale Victoria, alikuwa mzee mmoja mcheshi na mkarimu, Mungu amlaze mahali pema peponi, Amen!

    ReplyDelete
  6. Anony wa 10/31 10:00 unawika, u don't know shit about the late Muhando, mzee alikuwa dingi poa sana,very mshkaji na anaheshima kubwa sana katika fani ya uandishi bongo. U could better shutup since you seems not to know shit. Word.

    ReplyDelete
  7. Kaka Michuzi vipi bwana mbona maoni yetu wengine unatubania, na hakuna kibaya tulichoandika? haki sawa kwa wote, siku njema

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...