mkuu wa chuo kikuu huria mh. john samwel malecela akimtunuku shahada ya kwanza ya sheria mfungwa anayetumikia kifungo cha miaka 50 katika gereza la ukonga haruna gombellar (54) katika hafla ya kutunukiwa shahada ya kwanza ya sheria katika hitimisho la mahafali ya 19 ya chuo hicho yaliyofanyika maalumu kwa mfungwa huyo kwenye bwalo la maafisa wa magereza ukonga, dar, leo.
gombellar ambaye alianza kutumikia kifungo hicho mwaka 1998, alipata nafasi ya kusoma mwaka 1999 ila masomo alianza rasmi miaka mitatu ilopita baada ya patashika za kisheria kufikia muafaka kati ya chuo na wizara ya mambo ya ndani.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Nimeguswa na juhudi za Bw huyu. Amefaninikiwa kupata digrii ya sheria ukizingatia ugumu uliopo jela. Sijui kosa lake ni lipi lililomfanya aende jela, lakini nadhani mtu kama huyu ameshajirudi na anaweza kutoa mchango mkubwa katika jamii.
    Napendekeza mtu huyu aachiwe huru. Parole Board huwa inakaa mara mara. Napendekeza wadau wa Blog hii waka-petition kuachiwa kwake kwa mamlaka husika.
    Naomba kuwasilisha hoja.

    ReplyDelete
  2. Mungu ibariki Tanzania. Hii ni hatua kubwa sana. Wakitoka huko ukonga angalau wana degree zao

    Hivi TZ hamna kufunguliwa kwa good behaviour? Miaka 50 kwa wenzetu angeikata 25 tu. Sasa 50 na umri wake ....???? Lakini degree hiyo itawasaidia walala hoi walifungwa na hawajui sheria na hawakua na lawyer wala a day in court.

    ReplyDelete
  3. wait a sec, ana miaka 54 na amepewa kifungo cha miaka 50, je akitoka atakua hai huyu? na sijui nikigezo gani kilichotumiwa kwani najua mtu akitaka kuwa mwanasheria lazima awe clean kwa maana hio hana makosa kwenye jamii. utailindaje sheria wakati wewe mwenyewe uliivunja? confuse

    Pili kwanini serikali haimpunguzii kifungo chake ili akaja uraiani akaliendeleza gurudumu letu la walala hoi.

    Tatu

    Hongera sana bwana Haruna

    ReplyDelete
  4. huyu jamaa kweli parole board inabidi imfikirie inaonekana kishajirudi..kweli hii ni history na ni mfano wa kuigwa katika jamaa,no matter how hard it is kila kitu kinawezekana,ni nia tuu na juhudi,hongera tena Haruna Gombella,hope watakuachia soon na uwe mfano mwema

    ReplyDelete
  5. HUYU BWANA KAENDA SHULE ILI AJE AANZISHE UPYA KESI YAKE. LAZIMA KUNA NAMNA. ANYWAY HONGERA SANA BWANA HARUNA KWELI ELIMU HAINA MWISHO

    ReplyDelete
  6. kaka michuzi hebu naomba fatilia kama huyu jamaa atauza hiyo digirii kwasababu yeye haitamfaa tena maana hata akitolewa jela atakuwa ana nyundo 80-90.

    ReplyDelete
  7. Free him,free him.It looks like he is about to show us the truth about some people who took him down.

    ReplyDelete
  8. Looo..!Huyu Malecela bado yupo tu!Anatoka wadhifa mmoja anaingia mwingine.Ni yeye tu anayewezakushikilia nafasi hiyo wengine aaaa..!Miaka nenda rudi viongozi wale wale!AIBU!!!

    ReplyDelete
  9. Ananikumbusha movie ya law abiding citizen "jamaa majambazi walibaka na kuuwa mwanaye" sheria haikuchukuwa mkondo ilibidi jamaa abukue sheria!! haha.. inatia moyo!

    watanzania tumejifunza kitu kimoja tu toka kwa bwana haruna "SHULE MUHIMU".. bongo flava hatufikishi popote

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...