mdau alieko chuo kikuu cha korea university na mwenzie tairo priscus kwa kufuata maelekezo ya jk na kampeni zake za kutangaza nchi walishiriki maonyesho ya vyakula yaliyoandaliwa hapa mjini suwon nje kidogo ya seoul.
walifarijika sana kuona wakorea walivyomiminika kwenye banda lao kuonja vyakula vya kitanzania na kusema kuwa wamevipenda( pilau, ugali, kuku, maharage, chai na kahawa za kibongo). wanasema soko la kahawa na chai huko ni kubwa sana inabidi jitihada zifanyike ili tuweze kuuza kahawa na chai yetu.
vile vile walifarijika kuwa kwa kuongea na wakorea wengi sasa wanafahamu mlima kilimanjaro, serengeti na ngorongoro vipo bongo na wanasisitiza jitihada zaidi zinatakiwa kufanyika kwani baadhi yao huwa hawazijui nchi zetu, kama wanazijua basi kwa mabaya kama vita, malaria, njaa na ukimwi.

pichani toka shoto ni mdau mwega na wa katikati ni mdau tairo anayesoma chuo kikuuu cha ajou university ambaye ndiye muandaaji mkuu. maonyesho hayo yaliandaliwa na ajou university, mjini suwon, Korea ya Kusini. wadau wameleta picha hizi kujaribu kuwaonyesha wabongo wenzao kwani licha ya kusaka nondozz pia wana jukumu la kuitangaza nchi kama jk alivyofanya pale alivyozindua rasmi pale new york kampeni maalum ya kuitangaza bongo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hivyo ndiyo tanzania inaandikwa kwa kikorea?kweli wametokesea adabu

    ReplyDelete
  2. let me take this opportunity to congratulate these two guyz(tairo&mwega) for being good ambassodors to our contry,there in south korea,bravo!

    i know you're alwayz been hardworker eversince.

    mchau,j.

    ReplyDelete
  3. Nimegundua Michuzi unapenda kuchokonia watu.Hii sentensi chini
    "Chuo Kikuu cha Korea University"
    Hipo sawa kweli au macho yangu yanamakengeza?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...