magwiji wa muziki bongo. toka shoto ni kikumbi mwanza mpango a.k.a king kikii, shem ramadhani karenga na ramadhani mtoro ongara a.k.a dokta remmy. pamoja na kutumikia fani hiyo kwa umri wao wote lakini wengi kama wao wana hali duni na serikali inabidi iamke kwani ufisadi kwenye muziki upo mwingi kuliko inavyodhaniwa hasa ukizingatia kwamba sheria ya hakimiliki ipo toka enzi hizo lakini haina meno kwani hakuna alieng'atwa nayo hadi dakika hii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Hivi hili neno UFISADI lina maana gani? manake kila kitu siku hizi UFISADI..zamani lilikuwa linahusiana na mambo ya ngono sasa siku kila kitu ufisadi..naomba maelezo wadau

    ReplyDelete
  2. KWa kweli nakubaliana na hilo Bro.Michuzi. Kwa sababu walioko kwenye mamlaka ya kusimamia sheria za haki miliki kwa wasanii ni wale ambao kama wanavyojulikana siku hizo mafisadi. Tangu nimeanza kusikia kuwa lipo Baraza la Sanaa la Taifa-BASATA na viongozi ni wale wale akina SHOGHOLO CHALI. Wao wanakula na kuishi kwa migongo ya wasanii kwa kutumia mirija ya Wadosi a.k.a Wahindi. wamekuwa madarakani kwa muda na hakuna wanachofanya katika kutetea maslahi ya wasanii kwa ujumla. Wasanii nao kwa njaa zao huwa wanapeleka kitu kidogo kwa mzee mzima huyo.Naomba nikwambie wasanii wa kike wengi katika fani ya uigizaji majukwaani wanamjua mzee CHALI.Tusitarajie wasanii kutajirika kwa style unayoisema.

    ReplyDelete
  3. Huyo chali jina lake lenyewe kasheshe CHALI sasa unategemea nini kwa wasanii wa kike

    ReplyDelete
  4. Hali zao ni duni kwa sababu ya wanamuziki wengi kuwa laifisti. Kama ni serikali basi wengi tunamaisha duni na tunahitaji msaada waserikali, mkulima anahitaji msaada wa pembejeo na mfanyikazi wa serikali je?

    ReplyDelete
  5. Jamani naomba kuuliza. HIVI KING KIKI ANAPIGA WAPI SIKU ZA WEEK-END SIKU HIZI?

    Naomba kufahamishwa!

    ReplyDelete
  6. Maisha bila Yesu ni bure na ubatili mkubwa.. kamuulize Dr remmy na Thobias Chidumule maisha kwao ni tambarale!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...