Maoni yangu ni tofauti na yako ingawa yanalenga haja ya kupunguza msongamano hapo Jijini. Hii inawezekana kabisa. Mapesa ya kufanya hivyo yapo kwani Tanzania yetu si masikini; ni tajiri. Tunafuja mapesa yetu bure.

Fikiria, hao mawaziri karibu sitini ni wa nini, kama sio ku-“exercebate the so-characterised” umasikini wetu? Hawa “mawaziri” na “wizara” zao wanamaliza mapesa kwa mishahara ya wafanyakazi, kuwapamba kwa magari ya fahari na majumba, marupurupu, ubadhirifu, ufisadi, na kurudufisha huduma.

Tulishindana na Benki Kuu ya Dunia, washauri wetu wa uchumi, kututaka tupunguze sekta ya serikali (umma) ambayo ilikuwa imeota kitambi. Tukashauriwa kuipeleka “gym” ikafanye mazoezi ya kukonda; ikakonda! Lakini sasa tumerudia yale yale ya kuota kitambi, tena kikubwa zaidi! Ikiwa kitambi kwa binadamu leo hii ni “skandali”, basi hata kitambi cha serikali nacho ni “skandali”!

Najua nchi kongwe (kama Uingereza, Ujerumani, Ufaransa) zilikuwa tayari na dola (the state) kabla vyama vya siasa kuanzishwa. Nchi changa (kama Tanzania) zilikuwa ni lazima ziunde vyama vya siasa ili zijenge “the state” ambayo ingejenga nchi. Matokeo ya kuota kitambi hicho yalikuwa ni mafanikio ya kujenga nchi.

Leo hii eti tunaambiwa mambo yamebadilika. Kuna kuoana baina ya sekta ya serikali na ile ya binafsi. Ndoa hiyo ndio kitovu cha maendeleo ya kujenga nchi….bado tunajenga nchi mpaka leo!

Kurudia ya Jiji la Dar, tunalipendelea sana jiji hili. Linazidi knawili. Wengine kati yetu wanalifananisha na New York au Shanghai kwa madhari yake. Tuliache Jiji hili lilivyo bila ya kulinyonga. Lakini Jiji la Dar limeshindwa kudhibiti wingi wa magari kwenye barabara zilizotengenezwa wakati wa Gavana akiwa ndiye mwenye gari, na wakati wa kutaka kutoka na gari hilo, barabara zilifungwa.

Mpaka sasa, serikali imekataa kuhamia Dodoma; inazidi kujenga nyumba za mawaziri na maafisa wa serikali Dar! Nchi imetumia mapesa mengi kwa ajili ya hayo “Makao Makuu Dodoma” toka enzi za “Sir” George Clement Kahama! Na “over cost” yake inazidi kila mwaka, licha ya ufisadi wa wafanyakazi wake kukopa mapesa na kujijengea majumba yao. Hii inajulikana hata kwa TAKUKURU! Tuache kuhamia Dodoma!

Itatubidi tuunde “our own format of decentralisation”, ambayo ni “home grown” ili kuendeleza baadhi ya miji yetu mingine na kupunguza msongamano wa magari jijini Dar na taabu nyinginezo.

Lakini tuendeleze miji mingineyo kwa kuhamisha wizara fulani kutoka Dar es Salaam. Kila mwaka tuhamishe kundi moja la wizara. Baada ya miaka kama kumi hivi, Tanzania itakuwa imebadilika sana!

Niruhusu nifupishe orodha ya wizara zetu ziwe wizara 15 tu. Orodha iwe fupi kama mini-sketi lakini ndefu kiasi cha kusetri huduma za lazima, kama ifuatavyo:

Dar es Salaam: Fedha na Menejimenti ya Utumishi wa Umma; Mipango (Mipango, Uchumi, Uwezeshaji na Kazi); Habari, Utamaduni na Michezo; Nje (Mambo ya Nje, Mashirika ya Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Mashariki); na Ulinzi na JKT.

Dodoma: Uhusiano wa Ndani (Muungano, Siasa na Uhusiano wa Bunge); Elimu (Elimu, Ufundi, Sayansi na Teknolojia; pamoja na kuwa Makao Makuu ya Vyama vya Siasa ili viwe karibu na Bunge “tukufu”.

Arusha: Maendeleo (Makazi, Jamii, Jinsia na Watoto); Sheria (Katiba na Utawala Bora); Mambo ya Ndani na Usalama wa Raia; ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa Nairobi na Kenya Kusini.

Mwanza: Afya na Ustawi wa Jamii, na Mazingira Nishati, Madini na Miundombinu, ikiwa ni pamoja na kuwa jiji la kuhudumia biashara ya Ziwa Victoria, Rwanda, Uganda, na sehemu za Kenya Magharibi. Mwanza iwe senta ya madini.

Kigoma: Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Maendeleo ya Vijana, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa biashara ya Ziwa Tanganyika, na DCR Mashariki, Burundi na hata Rwanda.

Mtwara: Uzalishaji (Viwanda, Biashara na Masoko). Mtwara hauna budi kupewa hadhi mpya kama senta ya huduma za mpango wa “Mtwara Corridor” – kwa ajili ya Malawi na Zambia na sehemu za Msumbiji Kasikazini. “Daraja la Umoja” kwenye Mto Ruvuma ili kuunganisha Tanzania na Msumbiji sasa linajengwa baada ya kulisubiri kwa miaka mingi tangu Awamu ya Kwanza – wakati Msumbiji inapata uhuru wake! Mtwara iwe senta ya gesi.

Mbeya: Ardhi, Maji, Mifugo, Kilimo, Chakula na Ushirika; ikiwa ni pamoja na kutoa huduma kwa nchi za Malawi na Zambia. Ni kitu cha kutia shime kuona kuwa uwanja wa ndege wa kimatiafa unaendelea kujengwa mjini Mbeya. Uwanja huu utasaidia pia kuinua maendeleo kwa mikoa ya kusini, ikiwa ni pamoja na kuinua hali ya utalii kwa mikoa hiyo ya kusini.

Miji hiyo iwe na wizara ambazo nimeziunganisha. Tuwe na Mawaziri Wadogo 15 tu wakisaidiwa na nyongeza ya Makatibu Wakuu, endapo italazimika. Wizara hizi zitagawanya katika mafungu matano.

Kila fungu la wizara zilizotawanyika lisimamiwe na afisa mwenye sifa za nidhamu na uchapaji kazi (mwenya madaraka makubwa zaidi ya makatibu wakuu) ili kuweza kufuatililia maazimio na miradi mbali mbali ya serikali kulingana na manifesto ya chama tawala (na kudhibitiwa na “chama tawala kivuli” kikisaidiana na vyama vingine vya siasa.

Naona kumekuwepo na kuteuliwa kwa maafisa wapya wa kumsaidia Waziri Mkuu katika kusimamia mipango ya sera za serikali.

Hii itasaidia sana kuangalia ni vipi tunavyotekelza yale ya Hotuba Rais aliyotoa alipokifungua Bunge la Awamu ya Nne. Na itawasaidia sana Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kuweza kufuatilia, kukagua na kudhibiti miradi na maazimio yaliyowekwa.
Born Again Pagan

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. KAKA NAUNGANA NA WEWE!!! JK NEEDS TO SEE THIS; HATA AKIANZA MWINGINE AKAMALIZA TUTAFIKA MBALI.TATIZO WATANZANIA (WAAFRIKA)TUNATAKA CHANGES OVER THE NIGHT....HII HAITATUPELEKA POPOTE.
    NAUNGANA NA WEWE ASILIMIA 101.

    MTANZANIA BORA.

    ReplyDelete
  2. HUU NI MJADALA MUHIMU SANA KWA NCHI YETU AMBAYO BAADA YA MIAKA ZAIDI YA 40 YA UHURU,NI KAMA TUNAANZA KURUDI NYUMA BADALA YA KUSONGA MBELE,HII NI NCHI YETU WADAU CHANGAMKENI MTOE MAONI MAKINI NA ENDELEVU NAJUA VIGOGO PIA WANASOMA HII BLOG NA YATAYAINGIA MASIKIONI.
    maoni ya mdau ni mazuri ingawa kuna mengi ya kufanyika zaidi ya hayo,licha ya kupunguza mawizara yaliyolundikana kama nyanya kariakoo ni budi tu-foresee how we should deal with dividing this country into not more than 6 states or provinces whatever you should call em,by doing so we gonna cut down the following;
    1.the No of reginal and district principals respectively
    2.cut down the No of legislative representatives since in each state there should b only a govenor and one legislative representative,this will also directly have impact on the No of ministries and ministers respectively.
    For those 2 outline above we can figureout that we would serve bilions that are wested as salaries and expenses for running reginal and district offices.

    Then this amount of money has to go into improving our
    EDUCATION,SALARIES OF CIVIL SERVANTS INDUSTRIAL SECTOR AND AGRICULTURE.

    ReplyDelete
  3. SIMPLE, VISIONARY, NATIONALIST.
    Mimi binafsi naishi Marekani na nimeamua kuanzisha familia huku huku! Siku zote ningali katika ukuaji wangu nilikuwa na ndoto ya kuwa siku moja nitashiriki katika kulijenga taifa letu la Tz na kuishi hapo na familia yangu!
    Kumbe ukweli ni tofauti kabisa! sisemi kuwa hauna wazalendo isipokuwa ni kuwa ukiwa mzalendo utakuwa dui wa watu wengi sana serikalini ambao kwao wao kushika nafasi za kisiasa walizonazo ndizo AJIRA ZAO NA CHANZO CHA KIPATO CHAO!Hivyo kwa mtu mwingine yeyote kufanya ama kutoa wazo ambalo kwao ni sawa na kutishia MLO wao ni kujitengenezea maadui!

    ReplyDelete
  4. Idea nzuri ya kupunguza baraza la mawaziri na liamuliwe moja kama kweli Dodoma ni makao makuu.

    Hilo la kuweka wizara katika mikoa tofauti halitafaa kwani wizara lazima ziwe answerable to where there is a sitting president, in our case, Dar. Ila basi labda TZ iwe kama federal state na kila mkoa liwe na bunge lake na mkuu wa mkoa awe wa kuchaguliwa na kila mkoa litoe mbunge mmoja au wawili kulingana na ukubwa/uwingi wa watu kwenda bungeni Dodoma kama vile wafanyavyo USA. Mikoa iwe na uwezo wa kukusanya kodi zake zenyewe na kuzitumia hizo kodi bila ya kwanza kuzipeleka wizarani Dar.

    Mawaziri/naibu mawaziri 60 sio mchezo ati!!

    ReplyDelete
  5. Maoni yako ni mazuri sana! Ukiondoa kile kipengele cha Wizara ya Mazingira, Madini, Nishati na Miundombinu kuwa pamoja. Hiyo itazorotesha utendaji kazi kwa zote hizo ni Wizara kubwa na nyeti sana kwa maendeleo ya taifa hili.

    Pia kuweza wizara katika mikoa mbalimbali ni kuongeza gharama za uendeshaji hasa ukizingatia ubovu wa miundombinu tuliyonayo nchi hii kwa sasa! Vikao vya baraza la mawawaziri, makatibu wakuu wa wizara, wakurugenzi na makamishisha wa wizara vitaleta matumizi mengine yasiyo ya lazima sana kwa serikali. Wizara zote ziwe katika mji mmoja. Ila ukubwa wa baraza la mawaziri ndio uangaliwe upya!

    LAKINI, kwa mambo yanavyoendeshwa na serikali ya safari hii iliyojaa uliapaji wa fadhila, ushkaji wa kupindukia, uzembe wa kutofuatilia mambo ya msingi wala kutekeleza ahadi wanazotoa majukwaani, maoni yako yataishia kapuni. Lakini, kwa sababu kila kitu kina wakati wake, ipo siku atakuja mtu/watu wenye masikio ya kusikia, watasikia, pia ambao bado ni wazalendo halisi wa nchi hii, watayafanyia kazi.

    ReplyDelete
  6. Naona mawazo yanazidi kutirirka! Hii safi sana!

    Niongeze: Sina hamu na Dododma kuwa Makao Makuu. Tumepoteza mapesa mengi na muda mwingi. Na wakubwa hawataki kwenda kuishi D'ma!

    Uamuzi ulifanywa kulingana na "erstwhile calculations" ya njia za usafiri na mawasiliano ya karne ya 19! Sababu kubwa eti D’ma ni katikati. Ilikuwa ni lazima kwa wa-Bunge wakutane katikati ya nchi wa kutoka mpakani.

    Usafiri kwa wa-Bunge wengi ulitegemea garimoshi na mabasi (na ndege kidogo) kufika Dar karibu juma moja kwa wengine. Mawasiliano kwa njia ya simu nayo yalikuwa ni shida. Leo hii kuna I’net!

    Uamuzi huo pia ulikuwa "purely ideological and policy calculations: Moja, D'ma ilionekana kuwa ni ya shida sana (ukame na okosefu wa maji kwa wakulima na wafugaji wa Kigogo). Ilisemekana kuwa baadhi ya wananchi walikuwa wakifa bila kujulikana huko kwenye makazi yao ya jadi.

    Mbili, D'ma ilikuwa ni "pilot project" ya ujamaa vijijini; kuanzisha Vijiji vya Ujamaa badala ya "Village Settlements" (Makazi Mapya) zilizokuwa zimeanzishwa kwa misaada na Israel - iwe mifano ya Kibbutz (Vijiji vya "Ujamaa" wa huko Israel).

    Tatu, hizi "village settlements" zilishindikana kwa sababu wananchi wengi hawakupenda kuishi namna hiyo, licha ya serikali kutumbukiza mamilioni ya fedha na vifaa: Upper Kitete (Mbulu), Ikwiririi (Pwani), Luganga (Iringa) na nyingine huko Handeni.

    Nne, ili kuunga mkono sera ya watu kuhamia vijijini huko mkoani D'ma, Nyerere aliamua pia kuhamia D'ma (Chamwino hiyo).

    Wenye kupendekeza kuwa "labda TZ iwe kama federal state", hili pia lina utata wake. Kwa mfano hapa Amerika, serikali za States zina nguvu sana hata kushinda serikali ya Federal. Nitatoa mifano minne:

    Moja, George Bush amshinde Al Gore huko Florida (state) na mbele ya Mahakama Kuu (federal). Mahakama Kuu ilitii amri ya State!

    Mbili, ukichukulia haki ya kupiga kura (the right to vote), utaona kuwa haki hii ni ya State. Rais inaidhinishwa upya (extension of voting rights) ingawa Weusi walipewa haki hiyo miaka ya 1960s! Lakini ni haki ya muda tu.

    Kama Rais asipofanya hivyo, Weusi watajikuta hawapigi kura! Kwahiyo, analazimika kufanya hivyo la sivyo Weusi watampa cha mchanja kuni.

    Tatu, kwa kuwa States zina haki ya kujitungia sheria zake, kuna wahujumu wa sheria hizo kukimbilia katika State ambazo hazina sheria ya namna hiyo, kama hujuma hiyo haiingilii sheria za Federal!

    Nne, State nyingine zinalia kuwa zinapunjwa. Kwa mfano, wafanyakazi wengi wa Jiji la New York (New York State) wanakaa katika miji ya New Jersey, Connecticut na Philadelphia States.

    Jiji huwa linalia kuwa linanyonywa kwa sababu wafanyakazi halo wanalipwa mishhahara na New York State bila kusaidia sana kodi katika jimbo hilo.

    Mfano wangu hapo juu ni kuwa na sheria moja kwa nchi nzima.

    Mgawanyo wa wizara, kama nilivyoshauri hapo juu, ni "tentative" tu. Itabidi wataalmu wa serikali na "public administration" wakae chini wachambue ni wapi wizara gani iende au iunganishwe na ipi.
    Najua ni vizuri Rais akae karibu karibu na wasaidizi wake (mawaziri na makatibu wakuu).

    Lakini katika njia za mawasiliano ya leo, hakuna haja ya Rais kukaa nao karibu karibu, kama kuku na vifaranga! Rais anaweza akafanya “tele-conferencing”! (CHEKA).

    Sana sana, itabidi Rais atembelee wizara zake, kama njia mojawapo ya ukaguzi na udhibiti wa malengo ya umma. Na hii itasaidia ajira huko mikoani kuliko kuwa wa-Tanzania wengi kuangalia Dar es Salaam tu!

    Wanakijiji wenzangu, zidini kutoa mawazo yenu ili tuondokane na urasimu wa karne ya 19 na ka-tabia ka u-kubwa kubwa uliojaa Dar!

    Ni lazima tuwafikie wananchi waliko wengi. Hebu fikirieni kuwa na Wizara ya Kilimo na Ufugaji mjini Dar es Salaam. Miji mingi ya Kiafrika ina paka na mbwa wengi kuliko mbuzi na kondoo! (CHEKENI)!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...