mdau katutumia hii ya wanandoa mashombe wa kiingereza ambao wamejaaliwa kuzaa mapacha ambapo kurwa na dotto hao ambao wote ni wasichana mmoja mzungu mmoja ni mmatumbi pyua. wataalamu wanasema hii inatokea kwa nadra sana kwa kipimo cha mtukio milioni moja kwa tukio moja kama hili. wadau, hii imekaaje?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Huenda moja alibadilishwa hospitalini.

    Lakini ni kweli genetically inaweza kutokea kama wazazi wote wawili wana ancestors wa kizungu.

    Hapa USA ilitokea kuwa wazazi wa kizungu walizaa mtoto mweusi na nywele za kipilipili kabisa. Kumbe wote wawili walikuwa na ancestors weusi ila walificha hiyo habari kwa ajili ya ubaguzi mkali hapa Marekani enzi hizo miaka ya 50!

    ReplyDelete
  2. mama ya watoto anajua siri yake

    ReplyDelete
  3. hakuna uchawi hapo ni genetics na inheritance tu.Hao wana genes za wazazi wao wote,ambazo zitaendelea kurithishwa kwa mtiririko huohuo vizazi hadi vizazi.
    Mimi sioni cha kushangaa
    LaLu

    ReplyDelete
  4. Hii kitaalamu inawezekana. Kila mmja wetu anazaliwa na genes za rangi ya nyeusi na nyeupe. Inategemea ipi kati ya hizo ni dominant gene. Ikiwa dominant gene ni nyeusi basi rangi ya ngozi itakuwa nyeusi, vile vile ikiwa nyeupe basi ngozi itakuwa nyeupe.Ikiwa recessive genes za baba mweusi na mama mweusi zitaungana, basi mtoto atakuwa Albino.
    Ikiwa baba/mama ni mzungu na mama/baba mwafrika. Hapa genes zao za rangi ni dominant. Hivyo watoto hutoka chotara, lakini upo uwezekano mtoto akawa mzungu au mwafrika katika uzao huu. Hivyo hivyo, katika uzao wa machotara hawa, HAISHANGAZI kuona watoto hawa mmoja akiwa mweusi na mwingine mzungu.Natumai sijakuchanganya zaidi.

    Anonymous
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  5. That is stupid!

    ReplyDelete
  6. HIYO KALI BABU MICHU, LAKINI MBONA HATA MAMA ANAONEKANA KAMA SHOMBE ASILIA?

    ReplyDelete
  7. Hii ni kweli kabisa, matukioa haya ni machache. Sayansi ya namna hii ilishawahi kuelezewa kwa undani sana na gwiji wa biolojia, Bw Gregor Mendel (1822-1884). Soma zaidi hapa katika kiungo hiki (http://anthro.palomar.edu/mendel/mendel_1.htm).

    By: mheshimiwa_2000@yahoo.com

    ReplyDelete
  8. Huyu alipiga wawili kwenye muda sio mrefu. Wakati yai linarutubishwa ngoma zote zikaanguka, yaani mayai mawili yakarutubishwa moja toka goli la kwanza, na yai la pili toka goli la pili watu tofauti ngoma ndio inatoa hiyo kitu. Haya sio identitical twins bali na mapacha wasiofanana. Goli la kisigino, mama anajua siri yake

    ReplyDelete
  9. Huwezekano wa mmoja wa watoto hao kubadilishwa hospitalini pia ni mkubwa sana.Hii imewahi kutokea.Ingekuwa vyema zaidi kama tungejua vipimo vyao vya DNA vinasemaje.Kama kweli hao watoto ni wa baba na mama mmoja,basi kuanzia hapo tunaweza kujadili vinginevyo.

    ReplyDelete
  10. Hapa panahitaji uchunguzi zaidi wa ukweli kwani mwanaume anaonekana kuwa ni mhamiaji toka uarabuni au asia na mwanamke ni mhamiaji toka afrika, marekani zote mbili au nchi za karebiani. Lakini yote hayo si hoja ni lazima kujua hisitoria ya babu na bibi zao.

    ReplyDelete
  11. hivi haya maneno chotara na shombe ni tafsiri sahihi ya watu waliochanganya damu? shombe alikuwa ni mcongo aliyekuwa na damu ya kizungu. nachoelewa ni kuwa chotara ni mchanganyiko wa kihindi na kiafrika (chotri)sasa waafrika wengine wasio wakongo au asiye mhindi wanaitwa nani kwa kiswahili sahihi? nataka tu kujua labda wewe michuzi unaelewa

    ReplyDelete
  12. Mimi naona tumuulize BUSHOKE mwenzetu huyo anaweza kuwa MUME BWEGE!!!

    Namuonea huruma sana huyo mtoto wa kizungu akikuwa anaweza kufikiri hao sio wazazi wake masikini lao mambo mengine bwana!! Anatia huruma

    ReplyDelete
  13. Jamani msiwaonee uwivu wenzenu watoto wao ni wazuri sana hongera zetu, mimi kwa nafsi yangu nahisi huyu ni zeluzelu wa kishombe maana kwakweli wanafanana hakuna cha kuiba hospitali wala cha mama anajua mwenyewe alikotoa, hakuna cha goli lilipingwa muda si mrefu wala nini acha uwivu we 3:51 am mama anajua siri yake nini wewe angalia wakwako wanafanana acha hizo.

    ReplyDelete
  14. Mimi walasishangae kwani hapa kwetu wapo wengi wanazaliwa na weusi na mtoto hanakuwa mzungu kabisa. mimi ninamapacha na wote wazungu kabisa sasa mimi nilihiba kwa mwanamke mwenzangu.hakukuiba kwani wa kwenye yai moja ndio maana wote wakike walihigia kwa wakati mmoja.hongela sana.

    ReplyDelete
  15. michuzi baba anafanya night shift sasa wewe unazani nini hapo.Mwambie jamaa acheck kama miguu inafanana na jirani wao hapo.

    ReplyDelete
  16. Kumbe Bushoke alichemsha,jamani mlikuwa wapi kumpatia shule kama mambo haya jamni?Inatia raha angalia jamani walivyopendeza!

    ReplyDelete
  17. jirani kapiga tiktaka hapo!

    ReplyDelete
  18. HAPO HAKIELEWEKI KITU MPAKA JERRY SPRINGER AU MAURY ATUAMBIE DNA INASEMAJE NINA WASIWASI KUNA MTU ALIFANYA KUFURU....
    kasera

    ReplyDelete
  19. Hii kali.
    kitaalamu ni vigumu kutoa maelezo yasiyo na ukinzani juu ya ishu hii.
    hawa ni 'identical twins', watoto wa jinsi hii wametokea kwenye yai moja( la mama) lilikutana na mbegu ya baba moja. kisha lilivyokuwa linasafiri likapasuka mara2. watoto wanaotokea wanakuwa na jinsia moja na kufanana sana kwa kila kitu.
    kuna uwezekano mapacha wanaofanana kutofautiana baadae kama wakiishi mazingira tofauti( environmental factor).
    ugumu wa hawa ni hiyo environmental factor haipo sababu ni watoto.
    nafikiri itafungua ukurasa mpya wa kisayansi na tafiti nyingi zaidi.

    Dr A.A.M(BW)

    ReplyDelete
  20. hawa watoto inaonekana ni wa ivf, mama yao amepandikizwa kwa bahati mbaya mbegu za kwao na za watu wengine ambao ni wazungu

    ReplyDelete
  21. Hii inawezekana kwani nilikutana na mapacha hapa Marekani mmoja mweusi na mwingine mzungu. Nilibishana nao waliponiambia ni mapacha mpaka waliponiletea picha za utotoni. Wazazi wao mmoja mzungu mwingine mweusi.

    ReplyDelete
  22. Mhhh!! Jando linatisha!!! unaona vijimambo hivyo???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...