waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa mh. bernard membe akiongea wakati wa hafla ya kumpa baraka za serikali na kumkabidhi bendera ya taifa kwa miss tz 2007 richa adhia mchana wa leo kwenye makao makuu ya kituo cha uwekezaji, dar. kwenye hotuba yake hiyo amesema serikali itatumia mbinu mpya kuitangaza nchi, ikiwa ni pamoja na kutumia fani ya urembo na warembo katika kunadi vivutio vya kitalii kibao vilivyopo bongo. mrembo huyu anatarajiwa kuondoka kwenda sanya, china wiki hii tayari kuingia kambi ya miss world ya mwezi mzima kabla ya fainali zinazotarajiwa kufanyika huko desemba 1.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Naona ndio tulipoelekeza nguvu zetu, mashindano ya urembo, kucheza ngwasuma, kutukuza mafisadi nk.
    Wakati ka nchi kadogo kama Rwanda kanajiimarisha kuhakikisha kanakuwa hub ya ICT kwenye kanda afrika mashariki ya kati na kusini, sisi tuko bizi kuhakikisha mrembo wetu anakabidhiwa bendera ya taifa kwenda kutuwakilisha uchina.
    Jamani, f#@$ when are we going to get our priorities right?
    Hivi hii amani na utulivu ambayo tumekuwa nayo miaka yate mbona haiakisi maendeleo yoyote ya ki uchumi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...