The horrifying sight which traumatized shoppers and office workers in the centre of Luxembourg City last week has now been labeled as a protest against racism. The Belgian woman of Congolese origin who set herself alight in the middle of Place d'Armes told witnesses that she was! doing it to protest against racism, moments before she carried out the desperate act which has left her in hospital fighting for her life.
Maggy Delvaux-Mufu, a mother of three in her forties, alerted several national newspapers late on Tuesday morning last week that she would be burning herself alive on place des Martyrs at 12.45 am, before setting out accompanied by her husband to walk through the centre of town to her macabre rendezvous. The police were alerted and officers were deployed to the Rousegärtchen.
But the woman changed her plan when she came across a group of journalists gathered to cover an event organized by the 'Movement écologique' on Place d'Armes, opposite the Cercle municipal. She soaked herself in petrol before confronting the members of the press, announcing that she was about to sacrifice her life to protest against racism. Moments later, she struck a match, turning herself into a human torch in front of hundreds of people.
Delvaux-Mufu' s husband and passers-by jumped on the burning body, attempting to stifle the flames with coats and jackets. The sce! ne made several people feel unwell and many witnesses who filled the square at lunchtime were traumatized by the woman's shrieking screams of unimaginable pain. The flames were already extinguished when police, rescue services and the fire brigade arrived at the scene. One person is reported to have vomited after seeing the woman being transported into an ambulance. The events in Place d'Armes have also started a controversy regarding the authorities' lack of psychological support for witnesses.
Delvaux-Mufu was taken to the Bon Secours hospital in Metz , where she is being treated in a specialized ward for burns and is fighting for her life. Grand Duchess Maria Teresa visited the woman and her family at the hospital last week.
RTL television was the first to run a news flash about the incident on its website on Tuesday afternoon last week. 352 reported the bulletin in its news in brief section, shortly before going to print. Events preceding the incident only came to light later on in the week.
The 42-year-old Belgian citizen and her husband had been facing financial difficulties. They had recently indebted themselves by buying a Citroën garage in Oberwampach, before realizing they were missing the documents that would allow them to set up a business. Delvaux-Mufu wrote a letter to Le Jeudi recounting her story of bureaucratic difficulties and economic despair. "I'm against all forms of violence, but day after day, my family and I have to endure moral violence, discrimination, insults and much more from Mr Juncker's administration" , she said in the letter published last week.
Money problems had driven the woman to desperately plead her case at the Prime minister's office early on the same day of the incident. Her threat to burn herself alive on Place des Martyrs after being turned away by the authorities caused government officials to contact the police. A city-wide search was organized, but nobody could foresee the woman would change her plans."

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Hii imefikia hatua mbaya sana... nanpia inaonyesha ni jinsi gani maisha ya n'gambo yalivyo, si marahisi kuna vipingamizi vingi sana. Tubaki nyumbani tujenge taifa.

    ReplyDelete
  2. HUYO MAMA VIPI? AJE AONE WATU WEUSI NA MACHIKANO WANAVOBAGULIWA HAPA MAREKANI...NDO ATAJUA MAANA YA RACISM NI NINI..AU AKUONA ILE ISHU YA "JENNA 6"
    UBAGUZI WA WATU WEUSI HAUTAISHA SI ULAYA, SI MAREKANI WALA SISI AFRICA MAANA BADO TUNABAGUANA WENYEWE KWA WENYEWE..
    lakini pole zake at least she is trying to make a point. and i guess point well taken

    ReplyDelete
  3. Michuzi,
    Hapo nimeshindwa la kusema...!!Kama ubaguzi umetufikisha huko...Lol...tumekwisha....!!

    ReplyDelete
  4. Racism? If u r racial discrimminated kwani wanakutoa ngozi..
    Hapa UK tuna pata matatizo kama Hayo na wala hakuna hata Mtu mmoja aliyejichoma moto.. Huyo mama hajui thamani ya Maisha yake na wala hajui umuhimu wa mama kwa watoto wake,AU hajui kama Mungu kakataza kujiua. Halaf akishaprotest ndio Iweje,Wazungu wabaguzi wabaguzi tu.. kwani alitumwa AENDE Huko.. Mbona Africa kubwa na ina opportunities everywhere!!!
    We r here to make what we came for and not changing who we found. I'm against racist in anyway but not burning ya self.. thats too much jamani...halaf mtu kama huyo anayejichoma ananunua Nguo za Hilfiger na gucci nk,anasikiliza miziki ya wazungu,Piga shule ukomae nao humo humo,wakibana tumbukia kungine. Dunia Sio Europe na AMerica tu.. Anamjua L.Mittal?? Muhindi lakini Tajiri wa 5 Duniani,Mzee wa kimexico tajiri wa tatu duniani?
    We haya we...

    ReplyDelete
  5. NJOONI UTURUKI MUONE.TENA BLACKS
    WOTE HAPA TUNAONEKANA KAMA WAUZA UNGA.HAKUNA THAMAN JUZI WAMEMUUA
    MNIGERIA MKIMBIZI BAADA YA KUMCHUKUA KUTOKA MAKAZI ALIYOISHI
    ILA WAKASEMA WALIMKUTA NA DRUGS
    CHA KUSHANGAZA NI KUWA DRUGS
    HAWAKUONYESHA HATA CHEMBE

    MIEZI
    MICHACHE ILIYOPITA KIJANA MMOJA
    WA KIGHANA ALIPIGWA NUSURA AUAWE
    NA POLISI WA ISTANBUL,KISA ALIKUWA
    WANAONGOZANA NA MKEWE AMBAYE NI
    BINTI WA KITURUKI,ILA WAKAANZA
    KUMPIGA HADI MKEWE ALIPOSEMA ''BU
    EŞIM,DÖVMEYIN LÜTFEN'' YANI
    ''THIS IS MY HUSBAND DONT BEAT HIM
    PLEASE'' IKAWA SALAMA YAKE
    TUNAISHI KAMA DIGIDIGI HAPA.

    ASIKUDANGANYE MTU ETI HAWA
    NI WAISLAM WENZANGU SIJUI WAKRISTO
    WENZANGU.WAPI WEWEEEEEEEEEEEE.MTU
    MWEUPE NA DINI HAATHIRIKI HATA
    KIDOGO DINI INABAKI KATIKA DOCUMENT
    TU ILA IKIFIKA MAISHA ANARUKA FUTI
    MIA.HILO MLIO BONGO MLIJUE

    ReplyDelete
  6. its sad! hasa kwa sisi waafrika wenzake, inauma. yes, she is trying to drive a point home, na ni ujumbe vile vile kwa waliopo home, wasidhani maisha europe ni rahisi, ubaguzi ni laivu, tunaishi kichwa ngumu. pole zake huyu mama.

    ReplyDelete
  7. MADAI MENGINE YA UFISADI NCHINI

    2007-10-29 10:29:37
    Na Dunstan Bahai


    Ushirika wa vyama vya upinzani nchini, umeendelea kutoa madai ya kuwepo kwa viongozi mafisadi ambao waliunda kampuni hewa siku chache kabla ya uchaguzi mkuu ili kuchota mabilioni ya kufanikisha kampeni na uchaguzi kwa
    upande wa CaCM.

    Kwa mujibu wa taarifa zilizosomwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dk. Wilbrod Slaa na Mwanasheria wa chama hicho, Bw. Tundu Lisu, kampuni hizo zilitumika kuchota mabilioni ya fedha Benki Kuu (BoT) ili kuendesha kampeni na uchaguzi mkuu kwa upande wa Chama Cha Mapinduzi.

    Ushirika wa vyama hivyo unaundwa na vyama vya CHADEMA, NCCER- Mageuzi, CUF na TLP ambapo taarifa iliyosomwa ilitiwa saini na wenyeviti wa vyama hivyo lakini aliyekuwepo kwenye mkutano huo ulioshirikisha wananchi mkoani Dar es Salaam ni Mwenyekiti wa TLP, Bw. Augustino Mrema na wengine waliwakilishwa.

    Akisoma taarifa hiyo, Mwanasheria huyo alisema kampuni ya Deep Green Finance Co. Ltd iliyoanzishwa Machi 18, 2004, pamoja na madhumuni mengine, lengo lake ni kufanya biashara kama `mabepari` na wakopeshaji fedha na kwamba wakurugenzi wake (majina tunayo), mmoja ni kutoka New Zealand na wawili ni kutoka Afrika Kusini.

    Taarifa hiyo ilizidi kusema hata hivyo kwamba wakurugenzi hao wote ni wakazi wa Afrika Kusini na ni maofisa au wafanyakazi wa Nedbank Ltd ya Afrika Kusini.

    Kwa mujibu wa Dk. Slaa, kufuatia taarifa ya Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), wanahisa wa awali wa kampuni hiyo walikuwa ni mawakili wawili Watanzania ambao pia ni mawakili wa kampuni ya Tangold ambayo nayo imo kwenye orodha ya `mafisadi` wanaotajwa na ushirika wa vyama hivyo vya siasa.

    `Tarifa za kibenki zinaonyesha kwamba tarehe 1 Mei, 2004, Deep Green Finance ilifungua akaunti Na. 011103024840 katika tawi la Corporate la Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Dar es Salaam,` alisema Dk. Slaa.

    Alisema cha kushangaza siku ya ufunguzi wa akaunti hiyo ilikuwa Siku Kuu ya Wafanyakazi (Mei Mosi) na ilikuwa ya mapumziko na kwamba kampuni hiyo iliruhusiwa kufungua akaunti bila kuingiza wala kutoa fedha kwa zaidi ya mwaka mmoja, kuanzia Mei Mosi, 2004 hadi Julai 31, 2005.

    Kwa mujibu wa Dk. Slaa, kampuni hiyo haikuwepo kwenye orodha ya taasisi za kifedha iliyotolewa na Benki Kuu Agosti 21 mwaka huu ili kuonyesha kwamba imesajiliwa.

    `Hata hivyo, kwa kipindi kifupi cha miezi mine, kati ya Agosti 1 na Desemba 1, 2005 kampuni hii ilipokea jumla ya shilingi 10,484,005,815.39 kutoka Wizara ya Fedha na/ au BoT,` alisema.

    Alisema kipindi hicho kilikuwa cha mchakato au kampeni za uchaguzi mkuu uliofanyika Desemba 14, 2005 na kwamba kuanzia Desemba 11 mwaka huo hakuna fedha iliyoingizwa katika akaunti ya kampuni hiyo hadi Februari 27, 2007 ilipovunjwa kwa hiari ya wanahisa wake.

    Dk. Slaa alidai kwamba taarifa za sasa zinaonyesha kuwa faili la kampuni hiyo lililotakiwa kuwa BRELA limetoweka, hali iliyowaridhisha kuwa kampuni hiyo ilikuwa hewa.

    Naye Bw. Lisu ambaye ni mwanasheria wa CHADEMA alisema, kampuni nyingine ya Tangold, kama ilivyo kuwa kwa kampuni ya Deep Green Finance ilifunguliwa siku ya siku kuu ambayo ilikuwa mapumziko, Januari Mosi, 2003 kwa akaunti Na. 011103024852 NBC tawi la Corporate.

    Alisema nayo iliendesha akaunti hiyo bila kuweka au kutoa fedha kati ya Januari Mosi, 2003 hadi Agosti mosi, 2005 ilipoanza kuchota mabilioni ya fedha, nje ya dola 13,340,168.37 zilizohojiwa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.

    `Baada ya hapo Tangold Ltd haikupokea wala kuingiza fedha zozote kwenye akaunti yake hadi Juni 6, 2006 ilipohamisha shilingi 220,980,370 kwenda TISS,` alisema na kufafanua kuwa TISS ni kifupi cha Tanzania Intelligence and Security Service (Usalama wa Taifa).

    Alisema tangu kipindi hicho hadi sasa, kampuni hiyo haijaweka wala kutoa fedha katika akaunti hiyo.

    `Kwa maana hiyo katika kipindi cha miezi mine, Tangold Ltd iliingiziwa na BOT jumla ya shilingi 4,742,982,627.06 na ilifanya malipo kwa Deep Green Finance na Meremeta Ltd ya jumla ya shilingi 3,363,531,259.67,` alidai.

    Ushirika huo umezidi kudai kwamba kutokana na masuala hayo mazito, wanautaarifu umma kwamba iwapo serikali itashindwa au kukataa kuridhia kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi, hadi kufikia Novemba 25 mwaka huu, utatoa maelekezo kwa wanachama na wananchi kwa ujumla juu ya hatua za kuchukuliwa.

    Hata hivyo, walisema hawawezi kwenda mahakamani kwani haki inaweza kucheleweshwa au isipatikane kabisa na kwamba mahakama kuu yao ni wananchi ambao wamekwisha anza kutoa hukumu kwa kuwazomea viongozi wa serikali kwenye mikutano ya hadhara huko mikoani.

    ReplyDelete
  8. Nutter! atakua anapinga deportation huyo, anatumia racism tu kama sababu, ulaya kutamu jamani-mtu yuko radhi ajimalize kuliko kurudi kwao!!

    ReplyDelete
  9. KUDADADEKI..HII INATISHA

    Jamani Ulaya mnakimbilia wenyewe halaf mnabaguliwa mnaanza kulalamika na kujitia moto

    Why..... kwa ninii??? mnakimbilia huko?
    Africa is for Africans n Europe for Europeans.
    rudini makwenu mkajenge nchi zenu nyinyi, wenzenu wamejenga nchi zao nyie mwataka kwenda kuishi tu halaf mnakandia kwenu

    ..inasikitisha lakini ndio ukweli, nyumbani ni nyumbani na kusiko kwako sio kwako hata ujipendekeze vp

    ReplyDelete
  10. Mimi nikiongea kuhusu ubaguzi wa rangi watu wananiambia nimezidi! Eti niongelee mambo mengine. Ukweli watu weusi wanapambana na ubaguzi kila siku Ulaya na Marekani. Hapa USA siku hizi si wazi kama zamani lakini ipo ile ya chinichini (Subtle).

    Watu wakitoka Afrika wanakuwa na ndoto za ajabu kuhusu maisha Ulay/Marekani/Australia asante video na sinema. Wanashangaa kukuta watu wanahangaika na kufanya kazi duni kama kuosha wazee na mataira na kuzoa mavi.

    Haya huyo mama ame-make a point. Lakini kwa Marekani hapa nakuambia wazungu wanasema, "The world is less one ni-gg-er!"

    Ubaguzi unaendelea! Na Obama hawezai kushinda urais. Watu wanasema bora asishinde maana atauliwa kama Rais Kennedy.

    ReplyDelete
  11. WOW!!HAKUNA UBAGUZI WA RANGI DUNIANI NI MIZENGWE TU.WATU WOTE DUNIANI WEUPE,WEKUNDU,WEUSI,MANJANO
    KAMA WEWE SASA UNAJIHISI UNABAGULIWA KUTOKANA NA LANGI YAKO,FIKIRIA MARA MBILIMBILI KWA NINI? MICHUZI BADO ANAPOZI NA WEUPE WAKATI YEYE NI MWEUSI?
    SASA NAKUPATIA JIBU NA DAWA YA HUO UGONJWA.ELIMU ELIMU ELIMU,NENDA SHULE KASOME ELIMIKA ACHA KUPIGA SHORT KATI.ELIMU NDIO YENYEWE ITAKAYO KUKOMBOA,WATU WEUSI WALIOSOMA HUWEZI KUWASIKIA WAKILALAMIKA NA HIYO (RACIAL STEREOTYPE)SIJUI INAITWAJE KWA KISWAHILI MMOJA ASAIDIE HAPA.

    NDUGU YANGU POPOTE ULIPO DUNIANI NILAZIMA UELIMIKE.KWA INCHI KAMA MAREKANI HUWEZI KUFANYA BIASHARA KIHOLELA WATAKUFUNGIA.MIMI NIMEELIMIKA NA PIA NINA UPEO KIDOGO.SASA NAFANYA BIASHARA YANGU KWA MIAKA MINNE BIRA WASIWASI HAPA MAREKANI KWANI NINAKILA MAKARATASI YANAYOHITAJIKA,WATU WENGI HUWA WANAKUJA KWENYE BIASHARA YANGU WANABAKI KUSHANGAA KWAMBA MTU MWEUSI NDIO MWENYE MALI??MIMI WALA HAINISUMBUI HIO MAKE NAJUA HAWEZI KUFANYA CHOCHOTE.

    KWA HIYO RUDI SHULE,SOMA SOMA KISHA UTAONA MAMBO YALIVYO LAHISI.
    HAPA MAREKANI KUNA JAMAA MMOJA WENGI MNAMFAHAMU SANA BILLY COSBY
    HUYU MZEE HATETEI WALA KUSHABIKIA UBAGUZI WA RANGI ANAWAAMBIA WATU WAPIGE BOOK TU.WATAONA SIRI NA DAWA YA RACIAL STEREOTYPE .

    MAFANIKIO MEMA KATIKA ELIMU YAKO.

    ReplyDelete
  12. Nimefurahi kumsikia ndugu yangu akipigia debe shule, ni kweli yaweza kulipa! Lakini tusisahau kiini....je tunasoma au tunakariri waliyoandika weupe? Nadhani tunajitahidi kujishebedua tu na sisi tufanane na wao...Nitakupa mfano halisi..ili mbongo uonekane unazungumza jambo la maana lazima utie nakshi ya lugha ya kiingereza kidogo...usivyofanya hivyo unaonekaa fala tu! mfano..."WATU WEUSI WALIOSOMA HUWEZI KUWASIKIA WAKILALAMIKA NA HIYO (RACIAL STEREOTYPE)SIJUI INAITWAJE KWA KISWAHILI MMOJA ASAIDIE HAPA" hakika nakuambia mtu mweusi ni mtumwa tu na kwa mawazo haya tunahitaji wakina Mkwawa na Mwanamalundi wengi zaidi ili tupate akili ya kufahamu utu wetu! Kuna mwanafalsafa mmoja alisema tutafakari na kujipa nguvu wenyewe ili tujikwamue na mawazo ya kitumwa, hakuna mtu atakayetusaidia zaidi ya sisi watumwa wenyewe...!Nakumbuka watumwa wa kwanza kupelekwa marekani walikuwa weupe! Wakaona kama umeshindwa na huna jinsi zaidi ya kuwa mtumwa bora ufe tu ili kulinda utu wako, wakagoma kula, wakakosa nguvu na wakafa kwa wingi, hasara kwa bwana watumwa na biashara pia, lakini faida kwa waliobaki! Kwa hidhini ya Papa wakapelekwa weusi sita kutoka Australia, wakapewa matunda na misosi finyu na utumwa usiozungumzika, wa maumivu makali mpaka kuingiliwa.....na bado wakafakamia misosi na kuendelea kuwa wakakamavu, na ukawa mwanzo ya weusi kupelekwa kwa weupe na wale weupe waliopoteza maisha kwa kukataa udhalimu wakawa chachu ya mafanikio ya leo kwa weupe wengi! Ndugu zangu tutafakari....tunasoma au tunakariri...na kuhalalisha utumwa wetu kwa kukimbilia kwa mabwana zetu WEUPE kwa kila kitu...miili, vyakula, elimu na hata lugha jamani!????

    ReplyDelete
  13. Pole zake lakini tatizo ni kuwa watu wengine wakishakua naturalized citizens wanajisahau sana na kufikiria kuwa wameshakua weupe na barabara ndio imefunguliwa. Ukweli upo palepale wazungu na nchi zao hizi kama hutaki maubaguzi yao rudi home or just find a way to cope with that.

    Kama ni kujichoma si watu wote wangejichoma tu. Na kusingebakia hata mtu mmoja tena. Ubaguzi upo kila mahali na upo wa aina nyingi tu. Ubaguzi wa rangi, ubaguzi wa kijinsia, ubaguzi wa dini na hata mali. Kuna aina nyingi za ubaguzi sana tu lakini ni kujifunza jinsi ya kuishi. Ila wengine psychologia zao ziko fyatu ndio maana wako easy to react.

    Nilikua naangalia news nikaona team ya Giant football na nyingine kutoka florida zinaenda kucheza UK kwa mara ya kwanza sijui ili kutangaza huo mchezo wao nje ya USA.
    Katika mahojiano yao na wachezaji wakaonyesha kuwa kuna mchezaji wao mmoja anafurahia kwa vile anaenda nyumbani kuona familia yake huko UK. Kijana wanaye mwongelea ni mnigeria ambaye kumbe ni mbritish. Hapo hapo nikaona mchezaji mwenzake ambaye ni mweusi(Black American) anasema oh he is nigerian. He is not British. Akajibu kuwa wazazi wake walitokea nigeria lakini yeye pamoja na wazazi wake wote kwa sasa hivi ni wa british na wanaishi UK for ages. Yaani nilimwona sura yake ilivyonyong'onyea alivyokua anajieleza. You see hata weusi wa first generation wanadharau au hawataki kuona eti mweusi uliyekuja huku kwenye karne hii unajiita mbritish au mmarekan kama wewe babu na babu zako hawakuletwa huku watumwa kujenga madaraja na majumba yao. Hawataki kabisa kusikia hayo. Second generation immigrants’ hatuheshimiki kabisa na wazungu au weusi wenzetu waliofika hapa miaka hiyo. Lakini je ina worth kujichoma? ....Mh... I don't think so.

    ReplyDelete
  14. Uliyedai umeelimika,inaonekana kweli umeelimika ila umekosa akili.Rudia kukisoma ulichokiandika, utajua umekosa akili.Umekurupuka kudai ukisoma hubaguliwi.Siyo PhD tu hata ukiwa na PHF kama ipo, ubaguzi upo palepale.Labda mtaani kwako hakuna, lakini usi-generalize.

    ReplyDelete
  15. ebwana ndio kuna kujitetea mwenyewe kwa kusoma, ukiwa na vyeti vyako si rahisi kubaguliwa, lakini ipo bado kiushkaji. Ubaguzi pia tunachochea hadi africa, nikija mimi na mzungu wote tunavyeti sawa watampa kazi mzungu kwa sabu tu mzungu!!
    we unasema tukae africa, mbona wao walikuja enzi hizo, na sisi lazima tupatate tuanachotaka.

    ReplyDelete
  16. Hamna cha elimu wala nini...ubaguzi upo pale pale..wangapi tumesoma na huku makazini mwetu unaona mtu anapandishwa cheo kwa vile ni mweupe na wala hajakuzidi wewe kwa lolote lile? Na kuchapa kazi unachapa tena saa nyingine ni zaidi ya hawa weupe.

    Lile jengo lilivyoungua uliona weusi wangapi pale? Pale ilikua kupata kazi kwenye hizo office hapo labda umetoka harvard na weusi wako.

    Hata US justice lawyer juzi tu amesema haya Justice Says Law Degree 'Worth 15 Cents ...

    well sikatai elimu muhimu popote lakini still kuna obstacles nyingi sana tu ukiwa mweusi. Bill Cosby anasema hivyo tu lakini 75% ya mablack kuwa hivi sio elimu. Kijana wa watu walikua wanamfunga miaka 10 watu wamesema juzi ndio katolewa jela baada ya kupoteza miaka miwili bure jela....Wanasema alikua na akili na alikua ana future nzuri tu. Kosa lake ni kudate mtoto wa kizungu basi wakamsulubu.

    Yapo mengi tu tunayaona kila siku. Mtu akiiba kwenye news "a black man...this and that" lakini akiiba mweupe unasikia "a man expected to be 19 yrs old" unaona moja kwa moja kuna racial bias....

    Ila tukijidai kujichoma basi tutaisha.Bora nirudi kwetu nikiona maji yamefika shingoni.

    Ukweli ni kuwa wanuchungu na nchi yao kama sisi wengine tulivyo na uchungu na nchi yetu ila tofauti ni kuwa sisi tunawalamba na kuwasujudu wazungu walioko nchini.

    ReplyDelete
  17. Huyo anayesema ubaguzi Africa hakuna ni nani? Angalia Tanzania, wahindi wana wabagua weusi na kuwa treat kama wanyama kwenye viwanda vyo utakuta watu wanafanya kazi katika mzingira mabaya sana we nenda viwanda vya sabuni na rangi utasikitika.Vilevile unakumbuka kuna wabunge walilalamika kubaguliwa katika hoteli kadhaa akiwemo Mh.John Cheyo kwa hiyo sielewi ni wapi mtu mweusi hawezi kukutana na ubaguzi.
    Dallasfinesty

    ReplyDelete
  18. Sasa nyie ndugu zangu mnafanya nini mnaishi kwa kubaguliwa huku mnajua kabisa kuwa hamna raha na maisha ya huko!! Someni malizeni mrudi nyumbani!! Ni aibu sana kung'ang'ania mtadhani ni watumwa!!! African's kwetu ni Africa na Europe ni kwa wenzetu weupe jamani!! hebu tujifikirie nani ataendeleza bara letu kama sio sisi wenyewe!! Mmmm kazi ipo kwa mtindo huo!!

    ReplyDelete
  19. mhh! mi nashangaa watu wanazungumzia ubaguzi huko ulaya, hapahapa bongo wapo watu weusi wanawabagua watu weupe, waasia, waarabu, mashombe nk.tena hili linafanyika in broad daylight. ubaguzi upo pande zote. kubwa hapa ni hulka ya binadamu kujiona bora kuliko mwenzake - period. tubadilike anza na wewe.

    ReplyDelete
  20. Kawaida huwa tuna sahau kwamba ubaguzi unatendeka kila mahali hata kwetu Tanzania. ukichukulia issue ya ma housegirl watu wengi huwa wanawatreat wafanyakazi wa ndani kama wanyama, mfanyakazi atafanyishwa kazi wiki nzima, mwezi mzima hata mwaka mzima kama hana mahali pengine pa kwenda wakati mwingine bila malipo au malipo finyu. Ataamka saa kumi na mbili afanye kazi mpaka saa sita za usiku wakati wengine kwenye family wamelala je huo si ubaguzi?

    Mfano mwingine ni wahaya ambao huwa wanawatumikisha wakimbizi kutoka Rwanda na Burundi, yaani huwa wanawadharau kiasi kwamba awali nao na wana jina maalumu wanalo waita "washuti" ukiangalia hawa watu ni kama sisi tatizo ni kwamba wamekabiliwa na matatizo ya umasikini lakini wangependa nao waheshimiwe kama binadamu. Point ni kwamba kabla hatujalalamikia ubaguzi wa mzungu na mweusi tujiangalie sisi wenyewe tunaheshimiana kiasi gani.

    Sisi watanzania tuna tendens ya kudharauliana na kukashifiana inaonyesha hata hapa wengine wanakashifu watu ambao hawana elimu, kuna wengi ambao wangependa kuendelea na elimu lakini wazazi hawakuwa na uwezo wa kuwaendeleza. Kama kwali mmesoma mna capacity ya kuelewa system yetu ya elimu Tz ni % ngapi ya wanafunzi wanaofanikiwa kupass kuendelea na elimu ya secondary hapo sijaongelea high school na university. Only those parents with money can afford to provide higher education to their children, and don't forget that more than 85% of tanzanian population are living under US$1 pr day any one of you people could you tell me how these people can afford to pay education for their children? Isn't it another way of bulling our people?

    ReplyDelete
  21. huyo mama ni shujaa alitakiwa awekwe kwenye Guiness book,maana ndio mweusi wa kwanza kujiwasha moto kutetea wengine.
    wanasifiwa wanaojilipua kuua wengine,lakini huyo ni shujaa kuliko wao.mungu amsaidie apone haraka.
    GOD BLESS HER.

    ReplyDelete
  22. Habari za huyu Bi Delvaux-Mufu kujichoma moto ni za kusikitisha sana.Natumaini atapona na kuungana tena na familia yake.Inasikitisha kuona mtu anafikia hatua kali kama hii ili haki zitendeke.
    Mungu amsaidie apone haraka,pole nyingi kwake na familia yake.

    ReplyDelete
  23. Wewe anonymous wa Tues Oct 30,hr 8:49.Unasema wazalendo Tanzania wanabagua wazungu,mashombe,wamanga na wadosi?!Wewe ni mmoja wa hawa nini?Maana haya si kweli wadosi na wengineo wote uliosema wanabaguliwa na wazalendo ndio wanaojitenga na kubagua.Hii inafahamika waziwazi.Wanajisikia ni muhimu na bora zaidi ya wazalendo,hata ndoa baina yao na wazalendo zinapigwa vita na familia za kidosi,wamanga etc.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...