KAKA MICHUZI! NIMEPOKEA E-MAIL HII TOKA KWA RAFIKI ZANGU WA U.K, HEBU MSAIDIE HUYU JAMAA KUPATA MWENZA KUPITIA BLOG YAKO JAMANI. AMEKUWA WAZI MNO HADI INAFURAHISHA.
"TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA"
Habari za masiku,
Samahani kwa kutokupa jina langu halisi,kwani nnachotaka kukueleza sitakupa jina langu kamili lakini naomba msaada wako nikifanikiwa siku moja ntajitambulisha kwa jina kamili live wakati tunakunywa chai au bia sehemu, naomba uifoward hii email kwa Watanzania unaowafahamu ili the right person awasiliane na mimi, ifoward bila editing tafadhari na asante.
Mimi ni Mtanzania mwenye miaka kati ya 35 na 43,sina tatizo la kulipa bill zangu wala maisha ya kawaida. Nilitambua kuwa nipo positive mwaka 2002 (nna virusi vya Ukimwi) nnatumia dawa na nnapata matibabu kama inavyositahili, nafanya kazi kama kawaida na hakuna dalili yoyote itakayomwezesha mtu asiyetumia vipimo au hasiye na hali kama yangu kutambua kuwa nnaishi kwa matumaini.
Tatizo nililonalo ni upweke na pia sipendi wala si vizuri kuwa na uhusiano na mtu asiye positive kama mimi nnachoomba ni itume hii email kwa watanzania unaowajua nao wataiforward mpaka mwenye hali kama yangu atakaponijibu kwa hii address: jameskisalu@yahoo.com
Ningependa mtu atakaenijibu asiwe na itikadi kali ya aina yoyote. Naomba aliye na upweke na aliye serious tu ndio anijibu na si kujaribu hili kujua undani wangu wakati wala hana shida kama yangu kwani atapoteza muda wake na wangu na hata akinijua haitasaidia chochote.
Tuvumiliane kwani wote bado tunapenda kuishi kwa raha na amani, hata kama wengine tupo positive.
Nimetumia njia hii kwani nahitaji Mtanzania Mwenzangu.
“SAMAHANI NI KWA WANAOISHI UNITED STATES OF AMERICA TU”.
Ahsante Sana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Michuzi....please....una maji ya kunywa karibu unisaidie..........

    ReplyDelete
  2. KAKA JAMES MUNGU ATAKUPA MWENZIO NA PIA UPWEKE UTAONDOKA. HONGERA KWA MOYO WA UJASIRI!!

    ReplyDelete
  3. jamani haya mwenzetu ndo huyo anatafuta mtu wa kumuuguza!

    ReplyDelete
  4. Kaka mtafuta mchumba,la kukusaidia kutafuta mchumba hilo sina uwezo nalo,lakini nataka nikwambie kwamba kwa uzoefu wangu wa kuuguza ndugu zangu wa karibu wenye HIV,i can confidently say kwamba HIV is no longer as life threatening as it used to be.we kaza buti,kula vitamins,mazoezi kwa wingi,lala mapema,msosi kama kawa,punguza alcohol intake(kama mnywaji usiache kabisa utapata depression,ila kunywa kiasi) na mwisho punguza rate ya ngono maana mbegu ni pure protein. believe me utadunda weeeeeeee mpaka hao wanaokunyooshea vidole(kama wapo) watapigwa chepe wakati we bado unajilia mikuku.i really wish u a very very long and happy life.

    ReplyDelete
  5. Jamaa ameanza kwa unyenyekevu na amemalizia kwa kiburi!
    Namkosoa kidogo, yeye angetoa wito wa kutafuta mwenzi ... hayo masharti ya ziada wangeambiana kwenye intavyuu.
    Naomba atoe closing date ya application!

    ReplyDelete
  6. Mungu ana makusudi kwa kila jambo, ni heri kaka unajua hali yako... all the best kaka utapata mwenza.

    ReplyDelete
  7. Anon 2.21 acha ujinga. Hivi watu wengine mkoje? We badala ya kumuombea mwenzako afya njema, unamuombea udhaifu. Nyie ndio mnaorudisha maendeleo nyuma. Kaka James, mi nakutakia nguvu na afya njema. I hope utapata mwenzako soon maana hapa kwa michuzi ujumbe unawafikia wengi.

    ReplyDelete
  8. Kaka Michuzi mshauri huyo bwana awaone "chama cha wanaoishi na Virusi vya Ukimwi" ni rahisi tu. Kuishi USA ni swala dogo tu.

    ReplyDelete
  9. Pole sana kijana, ukae ukijua kila watano wetu(wabongo) kuna chance ya 95% ya kuwa na positive mmoja kama wewe, kwa hiyo usijisikie uko mwenyewe.

    Pili, umeanza vizuri hadithi yako lakini mwisho umechemsha.....anyway, muulize google dating ya watu wa HIV positive, am sure atakusaidia, otherwise hapa utachezewa na kuchorwa tu.
    Goodluck.

    ReplyDelete
  10. We anon hapo juu osha kinywa chako upendavyo. The man is very clear, simple and sounds honest. Watanzania lazima tujue kwamba kuambukizwa haina maana mtu ni m*l*y* it can happen to anybody any time via any means.
    Destiantion ya mtu iko mikononi mwa Mungu (kwa wale wanao amini dini) na maisha ni mstari kila mtu ana wake.

    Eti anatafuta mtu wa kumuuguza, hata wewe leo unaweza jikuta kumebaki na mguu mmoja na utahitaji mtu wa kukushikia fimbo...

    Hujafa hujaumbika.

    Big up James live long and you will make it! siku hizi watu wenye virus wanaishi hata miaka 20 na bado science inafanya kazi who knows kuna siku dawa itapatikana!

    Nachukia watu wanao furahia maafa ya wenzao.!

    ReplyDelete
  11. Angekuwa anatafuta mtuwa kumuuguza asingesema ana maambukizi au asingelikuwa anatafuta mtu mwenye maambukizi.

    Lkaini huo ujumbe kwa vile aliyeutuma anasema ametumia jina sio halisi nashindwa kuelewa kama yeyeni mwanaume au mwanamke, je anatafuta mwenza wa kiume au wa kike, je yeye ni lezibiani au gei.

    ReplyDelete
  12. Kusema kweli James amekuwa mkweli sana, wengi wetu tunaficha usema ukweli kuwa ni waathirika.
    Tunakuombea upate mwenza na muishi kwa amani na upendo.

    ReplyDelete
  13. Jamani. Badala tu ya kutulia na kula vizuri ili arudishe afya yake anataka mpenzi!
    Kwaa niniii! Wwwhhhyyyy!
    Atazidi kukumaliza afya yako huyo. Tulia.

    ReplyDelete
  14. Kuna mawazo potofu kuwa mtu mwenye virusi vya UKIMWI akipata mwenza mwenye virusi vya UKIMWI wanaweza kuendeleza mapenzi bila ya tahadhari.
    Napenda kusema kuwa kuna jamii mbali mbali za virusi vya UKIMWI. Ikiwa mtu aliye na virusi vya UKIMWI akashirikiana katika tendo la ndoa na mtu mwenye virusi vya jamii tofauti na vile alivyo navyo, mtu huyu anaweza KUAMBUKIZA UPYA(HIV RE-INFECTION) na kufanya ugonjwa wake na fast progression.
    Anonymous
    http://drfaustine.blogspot.com/

    ReplyDelete
  15. Kama alivyosema anony hapo juu kama anahitaji company ya kuwa na mtu wa virus kama yeye ili muongee ambaye ni mbongo ni vizuri lakini kama anahitaji mtu wa kimapenzi sio vizuri kabisa kuwa na mtu mwenye virusi kwa vile vinatofautiana. Nadhani una council au social network groups na unaelewa haya.

    Watu wengi USA wanaishi na wake au waume zao salama baada ya kujulikana kuwa wana virus. Wanatumia vizuizi tu. Hivyo ninakushauri kama ulivyo mkweli ni heri utafute mtu na umweleze ukweli kuwa una virus na hapo mtaelewana. It is hard to get one lakini in the US anything is possible watu wanadate wafungwa sembuse wewe mwenye ugonjwa na umeshajua na upo under control. Googling utapata watu wengi tu kuliko huku kwa wabongo watakuchora tu kwa vile bado tuna fikira za ugonjwa huu kama kitu cha ajabu sana. Au hakiwezi kunipata au ni aibu wakati watu wengi sana wamezikwa nchini kwetu kwa ugonjwa huu. Hata mwenye nao hapa hawezi kukujibu kwa vile hajui wewe ni nani au kama unao kweli au unataka tu kuona ni wangapi wanao....Ni heri social network za US watu wenye nao wanakutana na kuongea so try those.

    ReplyDelete
  16. ACHA USANIII WEWE TUSHAKUJUA ZAMAN
    TUMESHAKUZOEA NA USANII WAKO.INGAWA
    UNA AKILI YA KUISHI MJINI.REGARDS

    ReplyDelete
  17. waelimishaji naona wamechoka; Madaktari mlipashwa kutuelimisha juu ya ukimwi kwenye huu mtundiko.
    Kidogo nijuavya kuhusu HIV/AIDS ni kwamba hivyo vidubwana viko vya aina tofauti, hivyo hata dawa za kuongeza nguvu ziko tofauti kutokana na aina ya vijidudu.
    Kwa mantiki hiyo si lazima waathirika wote kuwa wameathirika na vidubwana vya aina moja, kama vivyo ndivyo, basi anoni anayekwenda kwa jina la James anAwezapata maambukizi mapya ambayo yatamuwahisha KABURINI JAPOKUWA ANATUMIA DAWA ZA KUREFUSHA MAISHA

    ReplyDelete
  18. Pole sana Kaka James kwa upweke, na hongera sana kwa kuwa shujaa, kukubaliana na hali hiyo na kuipokea. Ni vigumu kwa wanadamu walio wengi kuikubali hiyo na kuishi kwa matumaini, lakini i hope one day Mwenyezi Mungu atakupa yule mwenye mapenzi ya kweli wa kuishi naye na kusaidiana kwa shida na raha. Ikumbukwe kuwa possitive sio kwamba ndo unakufa, la hasha, wengi wanadhani hivyo. Kama utakubaliana na hali yako, na kuipokea basi ninaamini ukifata masharti utaishi miaka mingi zaidi. Punguza pombe, Ngono (tumia condom), fanya mazoezi, jichanganye na watu wakati wote, usiwaze sana, kula vizuri (hasa matunda, mboga za majani). Naamini utakuwa mwenye furaha sana na haswa ukumpata mwenye mapenzi ya kweli kama unavyotaka wewe mkifarijiana. Kila la heri kaka James.
    Chiki

    ReplyDelete
  19. ACHENI LONGOLONGO ZENU ZA KIBONGO. JAMES ANATAKA MWENZIE MWENYE VIRUSI AISHI NAE WAWE WAKIONGEA LUGHA MOJA NA SI USHAURI NASAHA WALA POLE.MWENZENU YUKO MAJUU AMBAPO KUNA MATAASISI KIBAO YANAYODEAL NA UKIMWI,SASA UNAFIKIRI KUNA LIPI HAJALISKIA KUHUSU GONJWA HILO.NILITEGEMEA KUONA HIV POSITES TU HAPA WAKIRESPOND BUT THIS IS KIND OF PUTTING THEM OFF SASA COZ KILA MTU ANAJITIA MZIMA HAPA-LAKINI JIULIZE-JE UMEPIMA? LETS GET SERIOUS JAMANI.

    ReplyDelete
  20. JAMAA MWISHO MBONA BADO ANAMAHASIRA CANCELLING AONGEZE NDIO ATAFUTE MCHUMBA KWA UPOLE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...