promota mashuhuri nchini wa muziki wa injili alex msama akiongea leo na waandishi wa habari kukanusha habari kwamba mwimbaji wa nyimbo za injili alieko ziarana marekani rose mhando anatuhumiwa kutapeli milioni 9.

msama amesema kwamba si kweli rose alitapeli pesa hizo, na si uwongo kwamba mwimbaji huyo alikopa hizo pesa toka kwa mchungaji dk. dickson chilongani wa dodoma huku akiwa ameweka rehani gari aina ya RAV 4 kwa makubaliano kwamba pesa hizo zingerejeshwa baada ya miezi mitatu.

msama, alitekuwa shahidi wa rose kwenye makubaliano ya mkopo huo, alisema matarajio ya kurejesha hizo pesa ndani ya miezi mitatu yaliingia dosari baada ya shoo kadhaa zilizoandaliwa kuzaa matunda hafifu na kupelekea mtafarauku ambao anasema ulisuruhishwa na rose kuweza kwenda kufanya maonwesho marekani bila kama ilivyopangwa.

alikiri kwamba deni bado halijalipwa lote lakini azma ya kufanya hivyo iko pale pale hivyo kuita makubaliano hayo kuwa ya utapeli sio sahihi.

habari ambayo nusura imkoseshe rose mhando trip ya marekani kabla hajaruka kuelekea huko.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Huyo mchungaji yeye katoa wapi hiyo hela yote kama sio hela za waumini?

    Mishahara ya wachungaji wa TZ tunaijua yeye hela za kukopesha huku na kule anapata wapi?

    ReplyDelete
  2. Wacheni kufanya dini kuwa biashara wewe mchungaji na wewe Rose yaani umeenda kukopa hela ili utangaze dini waongo nyie au ndio alikuwa anataka apate hela anunue Audi Q7 kama ya huyo jamaa hapo juu

    ReplyDelete
  3. Wacheni kufanya dini kuwa biashara wewe mchungaji na wewe Rose yaani umeenda kukopa hela ili utangaze dini waongo nyie au ndio alikuwa anataka apate hela anunue Audi Q7 kama ya huyo jamaa hapo juu

    ReplyDelete
  4. Na kama walikopeshana kihalali lazima walisaini "mikataba"...heheheheh...na huo mkataba una siku ya kulipa na ukishindwa ni interest nyingi zaidi. Mambo ya kutangazia kwenye vyombo vya umma sio vizuri. Mlipokopeshana mlitangazia umma?

    ReplyDelete
  5. Mmhhh!
    Nasikia harufu ya ngono hapa!

    ReplyDelete
  6. HATA MIMI NAHISI KWA MBALI KUNA
    HARUFU YA URODA HAPA.TENA WA URODA
    WA PESA.KAZI KWELI KWELI
    WACHUNGAJI WENGINE KWA NGONO TU
    HAWAJAMBO.

    ReplyDelete
  7. ROSE UNAKIPAJI CHA NGUVU HUYO PEPO ALIYEMUINGIA MCHUNGAJI ASIKUHARIBIE KIPAJI CHAKO BIBIE..WACHUMBA WAPO KAMA HUJAOLEWA TENA DENDA LINAWATOKA BIBIE...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...