miss tz 2007 ni richa adhia ambaye hivi tunavyoongea yamebaki masaa machache kabla hajapanda jukwaani kwenye kinyang'anyiro cha miss world 2007 huko sanya, china. tumuombee ushindi binti yetu huyu anayetuwakilisha.
MUNGU MBARIKI RICHA
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE
AMINA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Pole kaka Michu, Pole wapenzi wa Richa , pole sote watanzania, kwa ufupi, RICHA HASHINDI KESHO,,vichekesho vitupu huko China, watu wanatucheka sana sasahivi kuwa watanzania tulikosa mtu mwenye asili ya kwetu kabisa, tukapeleka mhindi, Richa kutwa anashinda na miss India wanaongea kihindi, RICHA HASHINDI..wala kwenye 10 bora HAYUMO...MARK MY WORDS......

    ReplyDelete
  2. dada mzuri, anafaa, ila hapati ushindi huyu, hata wa Miss world africa, thubutuuu, unadhani wao wajinga wampe miss world africa mhindi wanajua vita vitakavyotokea katika bara zima, so sorry guys, hampati kitu, not this time...

    ReplyDelete
  3. michuzi mbona umetubania picha ya miss tanzania 2004? bwana mdogo michuzijr katudokeza kwamba anaolewa leo...

    ReplyDelete
  4. Kushinda inawezekana, mbona marekani wanapeleka mamiss weusi?? Issue sio colour, ingekuwa hivo dunia hii isingekalika!

    ReplyDelete
  5. Kushinda inawezekana, mbona marekani wanapeleka mamiss weusi?? Issue sio colour, ingekuwa hivo dunia hii isingekalika!

    ReplyDelete
  6. michuzi anaweza asiiweke kabisa picha ya miss 2004 Faraja, sababu si kwamba anaolewa leo,,no, ni kuwa Michu anaogopa mascud,,maana hizo blog zingine walizoweka hii habari, yamerushwa mascud sijui niseme mabomu ya machozi ya ajabu, kuhusiana na bwana na bibi harusi........KASHESHE..michu eeh, weka tu kama comment mbaya sana si utaibania,,tupe uhuru wetu bwana, mie nina usongo ...

    ReplyDelete
  7. All the best Richa! fly the Tanzanian flag with pride.

    ReplyDelete
  8. Michuzi huyo ni miss Lundenga nani alikwambia ni miss Tanzania????
    bania comment kama kawaida yako

    ReplyDelete
  9. Hata Malasyia miss wao ni mhindi vile vile ingawa mchanganyiko na mzungu, sasa huyo miss India ni Mgoa unataka wasiongee pamoja? mbona nyie mkikutana wabongo hamuachi kuongea kiswahili?

    Kha huu ubaguzi umezidi sasa, pelekeni basi miss mwingine huko.

    Wazee wa kukuwadi mwaka huu hawapati kitu, wamezoea kukuwadia wana wa wenzao safari hii wameula wa chuya!!!Subirini mwakani.

    ReplyDelete
  10. Mimi Mmatumbi na huyu Miss Tanzania wetu akirudi lazima nijipendekeze, nataka kuoa. Mnaoleta za kuleta subirini sherehe, demu bomba huyu.

    ReplyDelete
  11. Tarehe Friday, November 30, 2007 9:11:00 PM EAT, Mtoa Maoni: Anonymous

    NAUNGANA NA WEWE MKONO MOJA.

    ReplyDelete
  12. Nyie mnaofananisha America kupeleka watu weusi na Bongo kupeleka muhindi siyo wazima kabisa. Go back and get both sides of the countries history.

    ReplyDelete
  13. Kila la kheri Richa, Mwenyezi Mungu akutangulie katika harakati za kutangaza nchi yetu ya watanzania. Niko pamoja nawe katika hili na daima tutawaonga mkono wale wote wanaojitolea kutangaza nchi zao. Hakika huu ni uzalendo usio kuwa na kifani.

    oxoxoxoxox

    ReplyDelete
  14. haya jamani mimi ndo anon wa 9:11 niliwaambiaje, RICHA HASHINDI,,,haya kiko wapi, MISS CHINA MWENYEWE KACHUKUA USHINDI,,,POLE ZETU, TUMETIA KICHEKESHO NCHI ZA WATU, POLE LUNDENGA,,,POLE MICHU,POLE WATANZANIA, CONGRATULATIONS TO ME,,,MTABIRI WA MAMBO.........

    ReplyDelete
  15. ACHENI UNAFIKI WATANZANIA.KATIKA WOTE MLIOWATUMA WANGAPI WALIFANIKIWA? HAYA MAMBO YASHAPITA VIONGOZI WENU WENYEWE HAWAWAKILISHI VIZURI NJE ITAKUWA HUYO RICHA. SASA MESSAGE KWA WATU WOTE WANAOANDAA MASHINDANO YA MISS KUANZIA WILAYA, MKIWAONA WAKINA DADA WOWOTE WANATAKA KUGOMBEA UMISS WENYE ASILI YA RICHA AU RANGI KAMA RICHA AU RANGI YOYOTE AMBAYO SI NYEUSI AU MAJI YA KUNDE WAWAKATILIE KUGOMBEA .MANAKE NAONA WATANZANIA SASA WANAJIFANYA NA WAO WANATAKA UZAWA WA RANGI SASA.RICHA SIO KOSA LAKE YEYE KAENDA KAMA MSHINDANI MWINGINE NA MSHINDI MMOJA TU KATI YA 109.NA SASA MUWATOE WABUNGE WANAOWAKIL;ISHA BUNGENI WAKINA MOHAMED ENTERPRISES.RUSHWA ZAO MNAKULA IKIJA SEHEMU AMBAYO HAMPATI KITU NDIO MNAONA RANGI ZAO.TAFUTENI MAISHA.WEWE RICHA AU WEMA SEPETU ANGESHINDA MISS WORLD INGEWASAIDIA NINI KUGOMBOA UMASKINI TULIOKUWA NAO .UMASKINI WA MAWAZO NA MAISHA NDIO UNATUFANYA TUWE NA ROHO ZA KOROSHO. 2007 NCHI MJINI MAJI HAYATOKI,UMEME HAMNA ,BARARA MBOVU .MIJITU

    MICACHE NDIO INAFAIDIKA NA NCHI YENYE UTAJIRI WAKUWEZA KUKIZI MAHITAJI MUHIMU YA WANANCHI WAKE.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...