Nakupa Hi sana tena sana Mr.Michuzi!!!!!

Habari za huko kwetu Bongo, ninapenda kutoa shuikrani zangu nyingi kwako Michuzi kwa kutupatia habari na picha mbalimbali zinazo tukumbusha nyumbani. Mimi nipo hapa Italy mji wa Cesena, mtanzania ni mimi peke yangu hapa mji wa Cesena, ni mpweke sana. Lakini kwa blog yako Michuzi inanifariji sana tena sana, yaani ninafuraha sana kwa hii blog. Hongera sana tena sana, ninakutakia mafanikio mema mengi, nikija Bongo nitakuja kukutembelea. Salamu nyingi sanaaaaaaa......!!!!!!!!

- Mdau Baraka Franco Chibiliti

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. kaka rudi nyumbani, kwanini ukae mpweke huko wakati huku umetuacha watu milioni kadhaa... i hope unasoma, ukimaliza unarudi home uje tujenge taifa wote, I HOPE TO GOD KUWA HAUJAZAMIA NA UMEKUWA MBEBA MABOKSI.

    ReplyDelete
  2. OYAA WE SIO WALID KWELI AU MNA FANANA?

    ReplyDelete
  3. Italy sehemu kama hizo, unafanya nini? wasomea upadri? ni kawaida huwa wanawatenga sana ili wasipate vishawishi, so vumilia, ukimaliza shule, waumini kibao wanakungojea makanisani...
    kaa salama, and enjoy your time there,,utakuja kuwasimulia nduguzo na wajukuu(wakianza kuruhusu mapadri kuoa)

    ReplyDelete
  4. Tupo wengi best, ila ndio hivyo wengine tumeshajilipua tayari (Kama mimi). Nitakutafuta mzee, ila sio tena unitibulie kunitambulisha kwamba na mimi ni Mtanzania mwenzako, utakuwa umenimaliza, au unajua nini, wait nisawazishe mambo ya pepa na nini, ikitiki nakutafuta au siyo?
    Bila shaka hii picha na ujumbe umeutuma hivi karibuni, manake kama ni 2004 labda utakuwa ushatimua bongo labda, we wakaa kihalali, mpaka kujiweka kwa michuzi duh, hamna noma wala nini na mimi ngoja nisawazishe mambo ntajitoa hata kama ni summer natuma picha zangu za winter, nimepania kishenzi.
    Box time, kwaheri

    ReplyDelete
  5. wewe hapo juu 1:21 pm acha umbea au kujishaua kwani Michuzi ni Officer wa uhamiaji huko unakoishi? Kwani hata kama wewe umejilipua picha yako ikiwa hapa kuna noma gani? Watu wengine bwana!!!!!

    Wangapi kila siku huku tunawaona na wala hamna anayeshughulikia ni jinsi gani wanaishi nchi za nje?

    Wewe mapepe tu yamekuzidi.

    Mbona watu wengine wanakutana kwenye party hapa Uk na hamna anayejali kuwa kajilipua yupi au yupi hajajilipua? Wacha hizo ...ukiona dume linaongea ongea mambo hayo haliko nje ya nchi kama lipo nje basi sio dume...Mambo hayo yakusmea sema kujilipua au nini waachie watoto

    Kama unaakili jinsi unavyotafuta kuishi nje ya nchi ni juu yako na wala sio jimpya au la kushangaza sana.

    Grow up....

    ReplyDelete
  6. Michuzi nimepost comments yangu lakini umeikalia...Ila niseme tena kuwa he is rude whomever posted this up here..

    You can just write to people with no manner at all....hata kama ni hafula ya kupongeza boss wako but tell him to be nice to people... especially people who.....

    With this language your boss will find himself there alone with his entuorage.

    Tell him that we always gather for the loves of our country but who cares about free dinner. He put as if we just show somewhere with no mind of our own.

    Treat people with dignity and you will be respected.

    ReplyDelete
  7. Sasa si urudi nyumbani? Unalalamika upweke kivipi wakati siku hizi mawasilano nje nje. Simu TXT, internet, magazeti mitandao ya kudeti sasa hapo upweke unautaka mwenyewe. Tafuta demu ujivinjari naye

    ReplyDelete
  8. Duh mdau wa 30, 2007 1:21:00 AM EAT, umenichekesha sana sana kaka, yaani unaandika kama unaongea naye uso kwa uso...!!!
    Unamwambia Chibiliti achijani yuko peke yake njomba muko wengi, Chibiliti, Chikoloboi, na Chipoku lol
    Pole kwa upweke Mdau ndio maisha si unajua watanzania tuna Auto Serch miguuuni kila pahala utatukuta pambana kaka watakuja tuu.

    ReplyDelete
  9. Mdau Baraka come fai a dire che sei solo?ia mai girato in cesena?anche noi viviamo gli'..mgosi tembea kwani tuko mbona hauko peke yako tuko kama 68 hivi wabogo hapa cesena wale ninao wajua mimi.mjomba ukijitembeza kama popo hakuna mzalendo atakujuae Quindi gira gira gira poi troverai.ciao ciao.

    ReplyDelete
  10. Aaah hivi mjomba kumbe ni wewe mzalendo? mimi nilifikiria popo wa ki sene "ndanga ndef mangi fii"manake wako wengi hapa Cesena,mwaga razi ya contact tuta ku cerca.

    ReplyDelete
  11. Kak michu hebu kampeni ili pekecha pekecha waende huko cesena,wakawapekeche watu wasije wakapata prostate cancer.Mpweke kwani hakuna Dove au mbuni huko? usitusumbue

    ReplyDelete
  12. KILICHOKUTOA KWA NDUGU ZAKO KUJA HUKU NA LEO UPIGE KELELE YA UPWEKE,WATU TUNA MIAKA 25 HUKU MAHOLLAND NA POA TU,KWANZA GOZIGOZI LA WABONGU HATUNA MPANGO NALO,KWANI WABONGO NOMA,UNAMKARIBISHA KESHO ANATAKA MKEO,AMIA NAPOLI UKAROGWE.

    ReplyDelete
  13. Kaka hamia Modena,Roma au Vicenza kama unataka kuwa karibu na waBongo wenzio!!

    ReplyDelete
  14. HEBU ONA JAMANI KACHOKAA, EBU NANYIE WABEBA BOKSI WENGINE MUWE MNATOA PICHA ZENU TUWAONE MLIVYOCHOKA UKULI MCHEZO!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 15, 2010

    Michuzi hebu tupe elimu zaidi kuhusu hiyo saratani ya tezi la kibofu! Maana inavyoelekea wazee wengi gonjwa hilo ni kiboko linatesa! - Emmanuel (Makole Dodoma)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...