Bwana Michuzi,
Nimesoma kwa makini habari yenye kichwa cha habari noma kwenye blog yako. Nikiwa kada mwenye uchungu wa nchi hii nimeonelea nami niweke mambo sawa kwa kujibu kila lililosemwa, na ushahidi nnao. Ni kwamba, Bwana Michuzi, yote yalosemwa ni uongo wa mchana usiokuwa na kichwa wala miguu. Hao bwana asikudanganye mtu, ni wenzetu ambao sasa wamegundua matumaini waliokuwa nayo yametoeka baada ya nyota ya CCM kurudia kung'ara. Wamepoteza muelekeo hawana pa kushika.Hivyo wameamua njia hii ya uongo na kupakana matope.Bahati mbaya nayo haitasaidia kwa sababu ni uongo wa kitoto. Na wewe Bw. Michuzi usipoibandika hii kitu hapo chini nitajua kuwa na wewe ni hao hao kwani ilitoka kwenye mtandao huo huo ila mahasidi wakaminya na kukuletea ya upande mmoja tu, nawe ukaingia geji. Washindwe!
Si Mwingine ila ni mimi,
Mdau Nambari wani wa Nambari wani

1.Hadithi ya Bw.Gogo: JK hana swahiba Bagamoyo anayeitwa Gogo ambaye kanunuliwa gari ya Nissan na kuzunguka misikitini nchini kuhamasisha Waislamu kumuunga mkono JK wakati wa mchakato wa kutafuta uteuzi ndani ya CCM.Ama kweli njia ya muongo ni fupi.Mchakato ulikuwa ndani ya CCM hapakuwepo na haja ya kuzunguka misikitini.Kutafuta nini?Hakuna kura kule? Mwandishi amethibitisha asivyokuwa mwana CCM ingawaje anajifanya ni mmoja wao. Pia amethihbitisha asivyomfahamu JK.Yeye(JK) si mdini na hakuna wakati wo wote ametumia Uislamu wake kutafuta kura kabla, wakati na hata baada ya mchakato.Yuko hivyo hata sasa na atabaki hivyo kesho na kesho kutwa.
2.Kutekwa Anna Kilango: Anadai "ana ushahidi wa kuhusu Ana Kilango kutekwa ENEO LA GAIRO nje kidogo ya mji wa Morogoro,kuibiwa shilingi milioni mbili na kufanyiwa mambo mabaya." Mtu mwenye kudai kuwa na ushahidi anashangaza pale anaposhindwa kujua kuwa Gairo si nje kidogo ya mji wa Morogoro bali ni kilomita 125 kutoka Morogoro.Pia kwamba Ana Kilango hakutekwa Gairo. Kesi iliendeshwa hadharani Mahakamani asibabaishe watu kuwa anazo habari za siri za kutoa.Kama kweli anao ushahidi zaidi ya ule wa Polisi mbona hakuwapa Polisi wakati kesi inaendeshwa mpaka ikaisha zaidi ya mwaka mmoja na nusu sasa. Hata kama alishindwa kuwapata Polisi angempa habari hiyo Ana Kilango au Mzee Malecela ambao wangemshukuru sana kwani wangenufaika nayo sana kwa maana ya kesi na siasa wakati ule. Kutunga na hata kutoa uongo huo sasa hauna tija na wala hautambabaisha mtu ye yote.JK
hakuhusika na wala hakuna rafiki yake aliyehusika na tukio hilo la ujambazi.
3.Ngono na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda mwaka 2004: Huyu mtu anastahili kupuuzwa na kudharauliwa kwa uongo wa kijinga. Mwaka 2004 Uganda haikuwa na Waziri wa Mambo ya Nje mwanamke.Waziri alikuwa marehemu Wapakabulo na baada ya kufariki yeye akateuliwa Bw.Sam Kutesa anayeendelea mpaka sasa. Hili la JK kufanya ngono kwa siku mbili mfululizo na kushindwa kwenda mkutanoni halina msingi wowote. Rais Museveni hajaandika barua ya aina hiyo kwa sababu haikuwepo sababu ya kufanya
hivyo.
4.Fedha Chafu: CCM wala JK hawajapokea hata senti moja kutoka kwa Rais Joseph Kabila. Hapakuwa na haja ya kufanya hivyo. JK na CCM haijachangia hata senti tano kwenye uchaguzi wa Joseph Kabila na Chama chake. Hawajahi kuombwa na hivyo hawakuwa na sababu ya kufanya hivyo.Serikali ya Tanzania ilitoa mchango kwenye mpango wa SADC kuisaida Tume ya Uchaguzi ya DRC uliobuniwa na kuchangiwa na nchi wanachama wa SADC. Michango
iliratibiwa na ilitolewa kupitia Sekretariet ya SADC Gaborone, Botswana. Kamwe mchango huo haukupelekwa kwa mgombea ye yote binafsi, bali kwenye Tume tena kwa kuwapatia vifaa vilivyohitajika kufanikisha uchaguzi.
5.Millennium Towers Hotel: Madai ya JK kuwa na swahiba yake Jack Gotham katika hoteli hiyo na kufanya vitendo vya ngono na msichana wa UDSM ni uongo mtupu.Kwanza JK hana uswahiba na Jack Gotham. Ni watu wanaofahamiana lakini si watu waliowahi kuwa pamoja wakati wo wote katika hotel hiyo kwa ajili hiyo inayodaiwa.Hawako karibu kiasi cha kufikia kufanya hayo yanayosemwa.Ni maneno ya hasidi mwenye nia mbaya tu kwa JK. Lakini hapa amechemsha.
6.Klabu karibu na Red Cross: JK hajawahi kutembelea klabu hiyo maisha yake yote.Hata yeye haijui jina kama vile ambavyo hata mwandishi haijui.Isitoshe hajawi kukaa pamoja na vijana hao katika klabu au bar au mahali pengine po pote.Hivyo basi kuhusishwa na mkutano na vijana aliowataja mwandishi katika klabu hiyo na hadithi zote zinazodaiwa kutokea kwa ajili hiyo ni mambo
yasiyokuwa na hata chembe ya ukweli.Ni mambo ya kugushi tu.Hakika mwandishi hamfahamu JK ndiyo maana amesema mambo ambayo hata mtoto anajua uongo.JK hakuwa na matembezi ya klabu wala bar yo yote hapa jijini.
7.Kuoa mke kutoka Uarabuni: JK ana mke mmoja tu Salma. Hana mke mwingine, si kutoka Uarabuni wala kwingineko. Hadithi ya kuoa mke mpya ni upuuzi mtupu. Hii ni Bongoland kama mwandishi kakutana na tapeli shauri yake.Siku nyingine akikutana nae amtake ushahidi wa ndoa. Morogoro kuna kijana kawaibia watu wengi kwa kujiita mdogo wa JK aitwaye Yusufu. Alikamatwa na sasa anatumikia kifungo.
8.Hoteli ya Serengeti: Kwa kuwa suala la kuoa mke mpya ni jambo la uongo hivyo hadithi ya JK kuchukua eneo Serengeti la kujenga hoteli kwa ubia na mke huyo si jambo la kweli.JK hajengi hoteli po pote pale.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. Hehehe Kaka Michuzi naomba chonde chonde chonde chonde natamani niseme zaidi ili tu hii comment isitupwe kapuni....

    Inawezekana nna upungufu katika kufahamu vitu ila hii habari aisee hunidanganyi imetoka front na front hasa maana hili beat sio kidogo....

    Heheheh naona Biti limekuja kwa njia ya MDAU NAMBARI WANI WA NAMBARI WANI....mi labda ni mdau wa milioni 37 kati ya milioni 37+ lkn bado nastahili kuona na kujua kuwa hili suala limeonekana na atleast nimefurahi....

    I hope hutanibania kaka michuzi maana kweli nimeomba sana na nazidi kuomba hii kitu uipost kama ya bwana mkubwa ilivyokuwa posted....

    ReplyDelete
  2. Inaonekana unamjua sana JK!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  3. O.K Its enough now, aliyeuliza kajibiwa, u guyz get a job or something to do. Word.

    Katty,
    Wilmington, DE.

    ReplyDelete
  4. Pole sana ndugu yangu kwa kupoteza muda wako na kuamua kumjibu huyo mpuuzi.

    ReplyDelete
  5. MZEE ES utamjua tuu

    nashangaa this time hujasema NONSENSE!

    watu wa jambo forums utawajua tu

    ReplyDelete
  6. Ok kaka Michuzi naona hapo ngoma draw. Nafikiri wote wawili wameridhika na watalala salama.

    Mzee wa TBS

    ReplyDelete
  7. Kumekuchaaa!!

    Hivi mie huwa nashangaa sana na siasa za Tanzania, hivi tulifanya uchaguzi kumchagua Rais mwaka gani vile?? Nafikiri 2005 kama sikosei maana nimeshasau siku nyingi.

    Watanzania kwa siasa, yaani tangu wakati wa kampeni, uchaguzi umeshapita mtu kashinda tena kwa kishindo, bado watu wanaendelea na kampeni za uchaguzi wa 2010 au?

    Hivi jamani lini tutaacha maneno na kufanya kazi kwa vitendo, uchaguzi ukipita aliyeshinda kashinda aliyekosa kakosa, tutakalia uchaguzii, Siasaaa, huku kazi haziendi gumzo gumzo gumzo.

    Hebu tufanye kazi sasa tuone hii nchi inakoelekea!! Khaa.

    Tusubiri 2010!!

    ReplyDelete
  8. Mheshimiwa Rais ni Mheshimiwa Rais tuu.wewe usiyetaka kuheshimu heshima ya Mheshimiwa tena wa hali yajuu kama Rais basi utakuwa na upungufu wa akili.Na labda akili zako hazina akili.Hivi wewe nani alikudanganya kuwa hiyo ndiyo "Freedom of speach"Kumchafulia mtu jina tena sio mtu wa kaida kama wewe na mimi ,tuu kwa kudhani wewe ni mjuaji zaidi basi utakuwa unajidanganya na nafsi yako.Watu kama wewe ndio mnaotuletea matabaka na chuki miongoni mwa viongozi na wananchi,hii ndiyo inapelekea nchi nyingine zenye wapumbafu kama wewe kuingia kwenye machafuko ya yenyewe kwa wenyewe.Kwa bahati mbaya wantanzania "we know better" Tena kuna mwingine kajaribu kukufananisha wewe na CHADEMA,mimi nakuona wewe ni IDDY AMINI.

    Mkererkwetwa wa nchi yetu.
    USA.

    ReplyDelete
  9. Hadithi zote mbili ni za uwongo! Naona jamaa anafanya mazoezi ya kuandika hadithi magazetini. Inavyoonekana Kaandika then akajijibu...kweli hapo bongo kuna watu hawana kazi ya kufanya. Unakaa cafee au kazini kutunga hadithi za Abunuwaz!! Michuzi usiendekeze story za uwongo personal kama hizi..blog itakosa Ladha! MDAU USA

    ReplyDelete
  10. HIVI NI RAIS WA NCHI GANI ANAWEZA KUTETEWA KWA HOJA ZINAZOONEKANA ZIMEJAA TU PROPAGANDA? HUYU ALIYEMTETEA JK. ANAONEKANA KWANZA HAJUI HATA KISWAHILI. HAPO NDIO UJUE RAIS ANA TIMU YA OVYO SANA. JUU KABISA AMESEMA "TA]arishi hauwawigi". HICHO KISWAHILI SIJUI NI CHA KAKABILA? HUYO RAIS ANAAIBISHWA SANA KWA KUTETEWA HOJA ZAKE NA WATU WASHAMBA KAMA ALIYETUNDIKA MTUNDIKO HAPO JUU. TANZANIA IMEKWISHA. NDIYO MAANA SASA TULIOZAMA NCHI ZA WATU HATUNA MPANGO WA KUISHI TENA HUKO. MAANA KILA MTU AMEKUWA MSANII, TOKA RAIA HADI WATU WA 'ZE COMEDY' NGOMA SULUHU.

    Potezeni muda kusoma mawazo ya wajinga, mtakosa kufanya kazi zenu.

    ReplyDelete
  11. Tangu hadith ya mwanzo nilikuwa nafuatilia kwa makini, inaelekea wana-Chukua Chako Mapema mmepata mkuki kumoyo.
    Yliyosemwa ni mengi mimi siyajui kama ni kweli au uongo na wala siko huko kwenye hizo articles, ila nauliza mtu unaposema tufanye kazi hii nchi inaokoleka, umefikiria unachokisema??? Nchi hii haitakaa ikaokoleka mpaka pale mtakapo kubali uovu unaofanywa na viongozi wenu.

    Hata ukifanya kazi kiasi gani viongozi hao hao watakukandamiza kwa namna ambayo hutaielewa coz you have much faith in 'em.
    Think twice about viongozi wetu na nchi yetu kuna ambao wamekiri wenyewe kwa midomo yao kuwa walikuwepo madarakani toka TANU, na mpaka leo wako madarakani. Na ninaamini zaidi ya 50% ya wafanyakazi na viongozi wa serikali walikuwepo madarakani tangu 70s. Je katika kipindi hicho walichokaa madarakani, hali ya maisha ya mbongo wa kawaida imeboreshwa au ndio imewekwa ICU? Na ukigeuza karata upande mwingine hali za hao viongozi zikoje? Mi ninavyofikiri ni wakati wa kuwawajibisha viongozi na kuacha ushabiki usio na mwelekeo na watu kujiita wanachama wakereketwa. Upinzani nawasifu sana na nitaendelea kuwasifu. walivyoiwajibisha serikali mpaka imeundwa kamati ya kufuatilia mambo ya madini. Pamoja na kuwa naamini haitatatua tatizo sababu wengi katika kamati hiyo ni wale wale waliokuwa wakiikubali mikataba hiyo kwa miaka zaidi ya 20.
    Hivyo mi nawaunga mkono wote wanaojaribu kuwawajibisha viongozi kwa namna yoyote ile. walichaguliwa wawajibike na sio kwenda kupiga makofi bungeni.

    Naomba kuwakilisha na mwenyekiti naomba usinibanie.

    ReplyDelete
  12. bro michuuuuuu!!!! mambo hayo naona wote ni wajinga!!tuanze na yamepata wasemaji??lakini mimi yule wa (1),aliye toa shutuma,yeye kama alikuwa anajua yote hayo mbona akusema wakati ule wa ushanguzi!!!sasa wadangayika wameisha danganywa ndio leo anaanza kuropoka maneno mengiii!!yeye sasa kama kweli ana asila atafute mambo ya kuazia 2005 mapaka 2010 wakati wa uchaguzi atuereze,sio eti ifike 2012 ndio anaanza kutupa mambo ya nyuma!!siasa za bongo ni sawa na mchuzi wa mbwa unywewa ukiwa wamoto,kwa sasa ameisha cherewa!!hayo mambo labda serekali za wenzetu ndio wanaweza kufuatilia!!!
    (2)wewe msemaji wa pili,nashangaa sana,kujifanya unamjua saaaana jk,kwani jk pia ni binaadamu kama wewe au mtu yeyote,ina wezekana alifanya au la!?kwani wewe unatakiwa uombe ushaiditu sio kila kitu hapo unakanusha tuuuuu!!??hata kama CCM iko kwenye damu,mtu kama alikikosea anatakiwa hambiwe au akemewe,sasa unathani JK yoyete anayo fanya ni sawa!!??kwa vile wewe unamuusudu au unapata kitu kutoka kwake,mimi ni hayo tu ila napenda kusisitiza kuwa huu wakati sio wa siasa kwani siasa zimeisha pita,sasa tunatakiwa kufanya kazi Jamani,tuache LONGO LONGOOOOO AZINA MAANA, TUSUBILI MWAKA 2010,MICHUZI WAABIE HAO WANAO KALIA MANENO BADALA YA KAZI!!!?///
    DIRTYCASH~SEOUL

    ReplyDelete
  13. acheni kufanya kampeni za 2010 kama alivyosema mmoja ya wadau hapa.. wewe mkereketwa, siku zote ulikuwa wapi?.. KAMA WEWE KWELI NI KIDUME na kama uko na EVIDENCE kuhusu mheshimiwa PREZIDAA, songa front basi ukamueleze mheshimiwa JK kuwa anayoyafanya siyo fresh.. ingeleta maana zaidi hasa kwa mtu msomi kama yeye..kuwa kidume kama blaza MISUPU hapa alivyoamua ku muvuzisha liujumbe lako humu ktk blog.. hivi usemi wa kuwa UKIMCHUNGUZA SANA BATA HUTOMLA HAUUJUI YAKHE?

    ReplyDelete
  14. WEWE MICHUZI USIPOANGALIA WATU WATAHAMISHIA FORUMS ZAO HUMU. HAYO NAONA YA WOTE WAWILI NI MAMBO YA JF. SASA KAMA MTU ANATAKA ATAENDA HUKO HUKO JF. HAPA SIE NAONA UNATUCHAFULIA BLOGU WENGINE TUMESHAACHA SIKU NYINGI KWENDA HUKO JF TUMEONA HAMNA JIPYA HIZI NDIO ZAO KUCHAFUANA KUTUKANANA. MIE SIJAIONA KAMA SIASA ZA NAMNA HIYO ZIKO EFFECTIVE.

    KAMA MTU ANATAKA KUWA POLITICIANS AKAFANYE KAZI KWENYE JAMII HUKO WATAMUONA NA ATAKUWA AMEJITANGAZA, TENA KAZI ZIKO NYING TU HUKO ZA KUKUPA UMAARUFU NYINGINE HAZIHIAJI HATA MTAJI KAMA KISOMO CHA WATU WAZIMA AU ELIMU YA URAIA, HUKOO KUNAKO WAPIGA KURA, HALAFU AINGIE MSAMBWENI UCHAGUZI UKIFIKA SIO KUFANYA KAMPENI ZA SIASA KWENYE BLOGU HAISAIDII KWA SABABU MAJORITY YA WATU HAWASOMI BLOGU.

    KAFANYE SOMETHING PRODUCTIVE AND CONSTRUCTIVE.

    ReplyDelete
  15. Jamani eeeh kumbukeni ule usemi usemao "LISEMWALO LIPO............ wewe unekataa hizi shutuma kama ulikuwepo na Jk saa zote ama .......!!!!!!! Mimi nasema JK ndio ni Mheshimiwa weu Rais BUT yeye ni BINADAMU and HE IS NOT PERFECT !Kwa nini wangu mnataka kusahau hilo na kumfanye yeye kama nani??! haya mambo hata kama yapo na hizi habari watu msijifanye kuziba masikio tunazisikia saaana mtaani na ni siku nyingi hata kabla ya uchaguzi wa mwaka 95, ikafikia kiasi hata baba wa Taifa akampa JK wakati ule wa ughaguzi 95ya kwamba "Kijana wee bado hujatulia amuachie Mkapa nchi kwanza halafu utafuata............ " alikuwa na maana yake wee unamuona nani mgombea Urais alitinga NEC wakati wa kupitisha jina la Urais kikao kile cha 1995 na suti "WHITER than WHITE " he he he , JK sio mchezo ni brother man wa nguvu hajambo,sema Urais tuu protocol inambana kidogo. Anyway bila ya kupoteza hoja mana nilikuwa memory lane kidogo....... Ni kwamba wee unaekataa hoja zote usituzingue vilevile hapa sisi sio watoto wa chekechea na nyie wengine woote mnaojitia hizi shutma ni uongo mtupu acheni zenu deep down mnajua kuna valid points ya kwamba Rais wetu ni mpenda Ngono and thats a fact hata kama hizo hadithi zimerembwa but at the end of the day wabongo woote tunajua JK ni mtu wa totoz , kila mtu ana udhaifu wake as long as haya affect taifa letu na aendelee tu, tena bora ya hayo kuliko angekuwa kama jamaa alieondoka kunenepeana kwa kula hela ya Taifa letu.Sisi haya hayatuhusu hako kama ni kastarehe kake yana mwisho wake siku ya siku woote hao watamkimbia atabaki na Bi Salma wa watu....Kama hizi habari zote anasingiziwa kwa nini asingiziwe yeye tuu, mbona hatukuyasikia haya ya wanawake kwa Mkapa , yeye hadithi si zilikuwa nyingine! Bora ya Mzee Ruksa alijiwekea bayana kwamba yeye ana waifu zake wawili na hakuna mtu alioifanya ishu ... Mtu kama ni public figure ujue ya kwamba huna privacy hivyo basi ukitaka watu wasikukalie kooni mambo kama yana kaukweli ndani yake wee Kubali tuu yaishe ama kaa kimya sio mnajitia kukataa kila kitu hapa ndio unafanya watu wanazidi kutaka kujua undani na kukuchimba so my advise is kama mnaona hizi shutuma ni uongo mtupu then still just Shut Up kwa sababu mimi binafsi na wengi tunajua kwamba kitu kama sio kweli then hakiku-touch sana sasa kwa wewe kumjibia JK hoja kwa hoja na point kwa point inafanya watu tufikirie mara mbili mbili ya kwamba mayb hizi shutuma zina kaukweli ndani yake mana inaonekana mkuki umechoma ku-moyo .................haloo, Swala lililoko hapa ni kwamba Mheshimiwa JK na serikali yake huu ni mwaka wa pili unaishia tangu tumekupa nchi na bado tunahangaika na UMEME...... yani hii ni karaha kubwa sana kwa sisi wananchi tena wana CCM wakereketwa tunashindwa jinsi ya kujieleza kwa wapinzani. Sasa nyie mlioko Serikalini tafadhali badala ya kupoteza muda kwenye mablogu kukanusha shutuma kama vile viongozi wetu ni Perfect wasio na madhaifu yao, muda huu mngetumia kututafutia ufumbuzi wa kero za wananchi kama hili swala la mgao wa umeme. Huu ndio ubadhirifu wa muda wa Nchi na JK sisi tulivyokupa kura zetu tulikuwa tunajua sana weakness zako lakini tuna imani na wewe sasa wee endesha nchi tafadhali hayo mengine utajijua wewe na familia yako na MWENYEZI MUNGU wako kesho siku ya siku ya-umul-hisabu. Bwana Michuzi tafadhali toa maoni yangu mana najua zako wewe saa nyingine unabania ....... Na mie ni KADA mwenzio vile vile ........ CCM OYEEE.

    ReplyDelete
  16. somo kubwa sana tinalotakiwa kujifunza hapa ni kwamba TANZANIA YETU IMEKUA, ni jambo la kujivunia kwamba mada hii INAZUNGUMZWA,kuna watu wawili hapa wanahitaji heshima na kuenziwa kwa kiasi cha juu sana, MICHUZI na MHESHIMIWA, kwa sababu Michuzi tuongee ukweli sasa hivi angekuwa rais aliyepita ungekuwa ndani kwa UCHOCHEZI na KASHFA,au ungeambiwa wewe ni raia wa Malawi [ najua wewe una asili ya Mbeya kidogo ] wakati wewe ni njia tu ya kupitisha mawazo ya jamii, hata ukikatazwa bado watu wanayafikiria haya kila kukicha. Na MHESHIMIWA naye anastahili pongezi kwa kuruhusu yeye kujadiliwa kwa namna hii, kwa sababu najua asilimia 100 anajua sasa hivi kuna mjadala huu na anafuatilia, hata kama hajui watoto wake lazima wanafuatilia, najua pia akikupigia simu Michuzi uondoe mjadala huu, utafanya hivyo mara moja, lakini hajafanya hivyo.Ameonyesha ukomavu wa hali ya juu sana, this is beyond Mwinyi alivyokuwa anachorwa, this is beyond Mkapa alivyokuwa anachorwa na kina Kipanya, this si bigger.
    Mpaka hapa JK amepata kura yangu 2010, na mimi siyo CCM, na sijawahi kupiga kura toka zile kura za kulazimishwa na headmaster.

    ReplyDelete
  17. JK tuhuma za ngono zitaisha lini? ukitamka ngono tanzania basi umemtaja JK. ni kama Nyerere na Ujamaa, au Papa na Ukatoliki.

    ReplyDelete
  18. eeh bwana eeh !! Anon wa 4:16 umenikumbusha mbali sana na zile kura za kulazimishwa na Headmaster noma !! kumbe watu wengi tumepitia hiyo ?? Yaani mimi nakumbuka tukatolewa class kwenda kupiga kura hapo ni baada ya mkwara mzito sana kutoka kwa headmaster ......... he he he. Anyway JK a.k.a Kikwete I salute you , you are the man , mpaka sasa kaka Mivhuzi bado yupo mtaani anatuletea habari , mana saa hizi kweli angukuwa mhujumu nchi katinga mahabusu kwa kumkashifu Rais!!.... mama kweli bongo tumekua kisiasa ....!!haya mambo ndio yanayotendeka huku tuliko Western world , simly called "Freedom of Speech" na hii inaonyesha ukomavu wa kisiasa. Kwa hiyo basi namuunga mkono anon mwenzangu , mimi ingawa najua JK hizi shutuma za wewe na totoz zina ukweli ndani yake but I have not lost my faith in you as a leader of my great NAtion and nor will I ever do that so help me the Almighty , na kura yangu ipo kapuni 2010 nitarudi kuja kukupigia don't worry.......Mungu Ibariki TZ, na mjaalie RAis wetu maisha marefu na uongozi bora inshallah na umpe uwezo wa kuovercome weakness yake hii.Bwana JZ alijisemea girls.girls girls girls ........ you can't blame a man for being a man eeh.

    ReplyDelete
  19. hehehehehehe huyu jamaa utadhani ni special aide to the president.....ambaye pia hata huwa kwenye muvu za usiku huwa haendi....mwambie usiku hakuna msururu ni kigari ka polisi kimya kimya na landrover tu........tunakuwaga wote viwanja...tehettetetehhehe

    ReplyDelete
  20. Kada uliyeandika huu upuuzi wako hapo you better get a life fool.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...