09/09/1984: waandishi waandamizi wakiwa katika mji wa mpakani wa rukunyu, kizila, bukoba, kikazi. toka kushoto ni isaack nantanga (maelezo), moshy kiyungi (maelezo), alfred hilary (redio tanzania), nathan rwehabura (rtd, mwanza), ignace karege (rtd, mwanza) na salca rweyemamu (uhuru na mzalendo)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Sibabaiki na matokeo—Richa
    KUSHINDWA MISS WORLD

    na michael maurus, sanya, china

    PAMOJA na kushindwa vibaya katika shindano la Miss World mjini hapa mwishoni mwa juma, mrembo wa Tanzania, Richa Adhia, amesema hajachanganyikiwa na matokeo hayo.

    Richa, binti mwenye asili ya Kiasia, hakufurukuta kabisa katika shindano hilo kubwa la urembo duniani, lililomalizika kwa Zi lin Zhang, mrembo wa China kuibuka kidedea.

    “Katika shindano lolote lile kuna kushinda na kushindwa, si kwamba sikuwa na nafasi ya kushinda,” alisema Richa, ambaye ushindi wake wa taji la Miss Tanzania ulizua maswali mengi kutokana na kupingwa na wadau.

    “Nilikuwa na nafasi, lakini bahati haikuwa yangu tu. Mambo yalikwenda kinyume na nilivyotarajia.

    “Najua sasa nasubiriwa kwa hamu nyumbani Tanzania, najua hiyo inatokana na kushindwa kwangu, sitatetereka kamwe katika kujieleza mbele ya Watanzania, hasa vyombo vya habari.

    “Mimi si wa kwanza kushindwa, timu ya mpira (Taifa Stars), ilifungwa katika uwanja wetu, sasa iweje mimi nipatwe na hofu tena nikiwa nimeshindwa nje ya nchi yangu?” alijitetea Richa. Akionyesha kukiri jambo hilo kumchanganya, alisema kwamba kwa siku tatu atakazokuwa safarini kurejea nyumbani, atahakikisha anatuliza akili yake ili akifika aweze kuwaeleza Watanzania kila kitu kwa kina kuhusiana na shindano la Miss World.

    “Lakini kikubwa itakuwa ni jinsi ya kujipanga kuelekea shindano lijalo,” alisema Richa, anayetarajia kutua Dar es Salaam keshokutwa, akitokea Dubai, alikopitia kufanya manunuzi ya vitu akiambatana na mama yake.

    ReplyDelete
  2. Next time peleka mwanamke mwenye shepu ya kiafrika. Mmemwona Miss Ghana lakini? Pole Richa!

    ReplyDelete
  3. kwa wale wanaolalama kuwa MCHONGA katurudisha nyuma,MCHONGA katuzuia kutokuwa na TV's,MCHONGA katu blah blah blah,napenda kuuliza hizi staili za mavazi waliovaa hawa wapendwa hapo kwenye picha ndiyo zile zile tunazoziona kwenye filamu na video za zamani huku unyamwezini.Swali langu ni hili ndiyo Tv's hazikuwepo enzi zile lakini inaonyesha hatukuwa mbali kistaili au siyo?
    Kuna watu walikuwa wanaendana na staili za majuu kama hawa.Sasa Tv's tulizonazo sasa zimebadilisha au kuongeza nini ambacho hakikuwepo au kupatikana kipindi kile?
    Najuwa kuna wale mtakao sema soka,kombe la dunia,blah blah vitu ambavyo tulikuwa tunafuatilia kwenye news(Redio,magazeti,majarida) na bado mpaka sasa kuna watu wengi duniani bado wanafuatilia kwa vyombo hivyo kwenye mabano.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...