Pole na kazi Bw. Michuzi,
Naomba kushae na wadau, Picha za Wanyamapori wa Pori la Akiba la Selous. Sifa moja ya wanyama waliopo katika Pori hili ni kuwa wanaishi katika mazingira ambayo bado hayajaharibiwa na shughuli za binadamu, ni wapole kama utakavyoona, tupo nao kama ng`ombe.
-Mteleka, S.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Michuzi bwana na wewe mambo yako yankera sana sie tunataka picha za harusi mwanawani za kale kabinti ka eight five sasa unatuletea wanyama aaaa mambo gani lakini.tunaomba picha basi au walikupiga marufuku? sio njema kabisa mwanawan.

    ReplyDelete
  2. "Kama ng'ombe" siyo kweli. naona mupo mbali kidogo hapo...sogeeni kama mpaka hatua mbili hivi tuuone huo ugemu wenu

    Halafu kesho tupigieni picha mko karibu na NYATI

    ReplyDelete
  3. Washukaji tuache ushamba wa kuongea mineno kama tunaharisha ili kuchekesha watu washikaji wanawaonyesha sehem ya kujidai nyinyi minenoya kijinga au harusi itatusaidia nini uroda anakula mbunge!

    ReplyDelete
  4. Huku tu hatujawaamulia, ukienda india hawa wanawachezea, wanawapanda kama farasi na wamefundishwa mpaka kucheza muziki (nachi). wakiruhusu tuwafuge mtaani mi nitamfundisha kucheza mchiriku

    Ila kazi iko kwenye kulilisha dude hili mpaka lishibe, maana linakula pick up nzima ya majani kwa siku

    ReplyDelete
  5. Du si mchezo, ila ufahamu kwamba tembo wa Selous wamezoea kuwindwa na hivyo mara nyingi huwaga hawafagilii kuona binadamu wanawasogelea kwa miguu!!! ni hatari maana pia kumbuka kwamba wild animal behaviours are unpredictable. Kingine labda Matriach wa group hilo (yaani tembo jike mkubwa kiumri) ambaye ndiye kiongozi wa group hakuwaona maana kwa kawaida tembo wengine humsikiliza yeye, hapo angeamrisha kazi ifanyike...du pangekuwa patupu!!!!Otherwise bonge la kifagizi, hizo ni memories nzuri!!!! ze mdau

    ReplyDelete
  6. Hivi nyinyi kina ANONYMOUS vipi mbona siwaelewi, wa kwanza ni yupi na wapili ni yupi?
    hakika siwaelewi.
    Back to mada, wanyama ni rafiki wa binadam tangu siku nyingi ila tumewaharibu sisi binadamu kwa kushindwa kuwa nao karibu. Hatuwatembelei tulikowatengea kuishi na wakija kututembelea sisi vijijini kwetu tunawaua.

    Wenzetu wanawafuga wanaishi nao.
    Big up Mr Michuzi, anaetaka picha za harusi mwambie atume za harusi yake humu.

    ReplyDelete
  7. Tembo akianza kuwafukuza mtaweza kukimbia kweli?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...