Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kinondoni Kanali Mstaafu Godfrey Kajana Makaya amefariki dunia.
Taarifa kutoka kwa mtoto wa Marehemu, Bi. Doreen Makaya imearifu kuwa Kanali Makaya alifariki Ijumaa saa nne na dakika ishirini katika hospitali ya Aga Khan Jijini Dare-es salaam.
Kanali Mstaafu Godfrey Makaya alifanyiwa upasuaji mdogo wa Henia mapema tarehe 19 mwezi Novemba mwaka huu na kuruhusiwa kutoka hospitali tarehe 25 mwezi Novemba Mwaka huu. Hali yake ya afya ilibadilika ghafla hapo jana, akiwa katika hospitali ya Aga khan alipokwenda kwa ajili ya kwa ajili ya check up ya maendeleo ya operesheni aliyofanyiwa.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa alitakiwa arudi baadaye ili kumuona daktari majira ya saa nane mchana lakini akiwa anatembea kurudi kwenye gari, hali yake ilibadilika ghafla na kufariki muda mfupi baadaye majira ya saa nne na dakika ishirini asubuhi katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar-es-salaam.
Kanali Mstaafu Godfrey Makaya aliiongoza Wilaya ya Kinondoni kwa Kipindi cha zaidi ya miaka kumi na saba mfululizo kwa kuchaguliwa na wananchi na hadi mauti yalipomkuta alikuwa mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Kinondoni na Mjumbe wa Tawi la Sinza D.
Kanali Mstaafu Godfrey Makaya alizaliwa tarehe 01/09/1944. Alijiunga na jeshi la Wananchi tarehe 01/11/1966 na kustaafu mnamo tarehe 09/12/1997 akiwa Mkuu wa Chuo cha Mgambo Mbeya.
Mazishi yatafanyika jumatano tarehe 05/12/2007 kwenye makaburi ya Kinondoni jijini Dar-es-salaam kwa heshima zote za kijeshi baada ya kutolewa heshima za mwisho nyumbani kwake Sinza Madukani Mjini Dar-es-salaam. Martehemu ameacha watoto kumi na sita na wajukuu 29.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Poleni ndugu na jamaa wa marehemu. Kifo hakizoeleki. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema pepeoni.

    ReplyDelete
  2. Upumzike kwa amani kwa kazi kubwa uliyosaidia katika ujenzi wa Tanzania!

    Kwangu ni masikitiko makubwa kuachwa na mwanafunzi mwenzangu tuliyeanza naye darasa la kwanza hapo Majita Bwasi (Kurwenge), Musoma!

    Kanali Makaya hakuwa tu mwanafunzi mwenzangu katika shule ya msingi, bali pia tunaungana ki-ukoo!

    Kajana, uliitwa "kajana" kwa makusudi! Ni kweli ulikazana sana maishani, kama jina lako linavyojieleza wazi!

    Ingawa niko mbali ughaibuni, najumuika na familia ya ndugu Kanali Kajana Makaya katika wakati huu mgumu wa majonzi na maombolezo!

    Yegho wa Makaya, Nyamuanga Karugabha abhe n'omwoyo gwao kajanende na kajanende!

    ReplyDelete
  3. Poleni sana ndugu wa marehemu hayo ndiyo maisha na ni lazima tuyataraijie "Mungu huumba na kutwaa"

    RIP Mzee Makaya.

    Mzee wa TBS

    ReplyDelete
  4. Familia ya Makaya poleni na msiba huu mzito,

    Adolf,Lulu,Verediana,Max,Sweet,Dora ndugu jamaa na marafiki wote.

    Poleni kwa msiba

    ReplyDelete
  5. Upumzike kwa amani na upendo Marehemu Makaya.

    Nilipokea kwa masikitiko makubwa msiba huu baada ya kupigiwa simu na Doreen,Aneth na baadae ujumbe wa maneno kutoka kwa Elias Makaya.Yote haya ni mapenzi ya Mungu.
    Marehemu Makaya alikuwa mtu mwema sana.Nasema hivyo kwani nilimjua siku nyingi sana na ni shemeji yangu aliyekuwa amemwoa marehemu dada yangu (mama Nyagabona)mimi binafsi nina majonzi makubwa kwa kumpoteza shemeji yangu.

    Niko huku ughaibuni sitoweza kuhudhulia mazishi ila watakao kuwepo Mungu awajalie sana.
    Ni milimu ja Nyamuaga na Inyamuanga ibhasakile bhona muchipindi cha jisigitanye jinu ejechalo.
    Kaka Born Again Pagan tuzidi kuwasiliana.
    Majita.

    ReplyDelete
  6. Born again kumbe umekula chumvi? Comments zako sometimes nilikuwa nafikiri wewe ni teenager. Poleni kwa Msiba

    ReplyDelete
  7. POLENI SANA ....
    Dorothy Makaya , ndugu ,jamaa na marafiki wa marehemu Mzee Makaya kwa kuondokewa na mzee wenu.Hayo yote ni mapenzi ya mwenyezi mungu. kilicho baki ni kumwombea Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema pepeoni.(Amina)
    Mtani wako Dr. Balilemwa .B

    ReplyDelete
  8. VICTOR,pole sana,god giveth,god taketh. may he rest in peace. its been a long time buddy,remember the mlimani days

    ReplyDelete
  9. Ndani ya Misiba hakuna furaha lakini mwisho wa siku huwa tunakuwa na furaha ya kwamba Mpendwa wetu ametutoka na yupo in a Better Place...

    Nimemfahamu Mzee Makaya tangu nikiwa Shule ya Msingi pale alipohamshiwa Mbeya katika Shughuli za Ujenzi wa Taifa na alikuwa ni mzazi wetu. Na sikuishia hapo nikaja kuwa jirani yake Sinza Madukani.

    Tutakumbuka kwa Ucheshi wako, Moyo wa Kusaidia na kwa Msimamo wako Thabiti kwa yale ambayo unaamini ni kweli.

    Lenin, Dickson, Nickson, Aneth, Elias, Victor, Jesse, Sweet fahamuni kwamba huu si mwisho wa safari bali ndio mwanzo wa kuyaenzi yote yale ambayo Mzee wetu alisimama akiyaamini.

    Mungu Amlaze Mahale Pema Peponi.

    * RIP *

    ReplyDelete
  10. Kwako Mama Makaya, SuperVisor wangu
    pale International Telephone Exchange miaka ileee, Pole nyingi kwa msiba huu mkubwa kwako na familia. Mungu awape AMANI na FARAJA KUU....

    ReplyDelete
  11. Kwa niaba ya familia ya marehemu Kanali Makaya. Napenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa sala na faraja ulizotupatia katika msiba huu mkubwa kwenye familia yetu. Mwenyezi Mungu awe nanyi na mengine mengi.
    Mtoto wa marehemu MAKAYA ELIAS G. WASHINGTON D.C

    ReplyDelete
  12. Kwa niaba ya familia ya marehemu kanali GK makaya. Tunapenda kuwashukuru ndugu zetu, Jamaa na marafiki wote mliotusaidia wakati wa msiba na baada ya msiba. Nikaribu miaka miwili sasa toka ututoke. Upendo wako,uongozi wako na mufundisho yako yanaleta maana zaidi katika familia yetu. Ubarikiwe. Adolph Makaya Sweden.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...