wazee wa busara wakimshamgilia kassim baada ya kufanya bonge la shoo

kassim hemed mganga akiimba kibao chake cha 'haiwezekani' usiku kuamkia leo ngome kongwe. kijana huyu wa tanga ni mmoja wa masupa staa waliokuja juu kwa kasi sana kwa sauti nzuri na uwezo wa kutawala jukwaa. akiwa mtoto wa mwanamuziki wa zamani wa urafiki jazz kassim ana kipaji nechuro na akama atafunga buti atafika mbali sana. yeye ni mmoja wa matunda ya kundi kali sana katika bongo fleva la tip top connection

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. mwanangu kassim nyimbo yako hii super ile mbaya mademu wakibongo hata wakikenya waliopo u.s wanaifagilia sana hasa hasa wa new york na D.C yani tukiwa na mawazo tunaifungulia nyimbo yako basi mawazo yote yanayayuka mwanangu hongera sana, hivi sasa niko offisini namuaza mpenzi wangu huku nakula nyimbo yako na kuburudika. hongera sana, njo u.s ku perform, njoo njoooo kassim weeee.

    ReplyDelete
  2. kaka michuzi hawa wasanii wa bongofleva badala ya kujenga wanajengua zaidi kuliko kujenga.angalia sasa ni wao ndiyo waliofanya neno nyimbo litumike katika umoja wakati lenyewe asili yake ni wingi,hivyo kuua neno wimbo ambalo hasa ktk umoja ndiyo linastahili na si nyimbo.kama mdau kutoka 'us' alivyoandika "nyimbo yako hii super----" badala ya kusema "wimbo wako huu super----"ni ulemavu ambao umekomaa tangu hapa tz hadi huko ughaibuni kwa kweli inasikitisha na kuuma sana.hebu wasaidie hao wasiojua makosa kama haya.na hasa hawa wasanii kwakweli wanaharibu kama si kubananga lugha yetu ni aibu huko duniani hasa ukutane na mkazi wa huko ambaye alikuja hapa tz kujifunza kiswahili halafu karudi kwao.umeongea hivi halafu yeye anakusahihisha utajisikiaje? kwakuwa wao ndiyo waliharibu,basi ni wao ndiyo watengeneze hasa kwakuwa watu wengi huwasikiliza kupitia vyombo vya habari ama kwenye matamasha yao mbalimbali.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...