President Jakaya Mrisho Kikwete grants a charter to the Chancellor of the the New Dodoma University former President Benjamin Mkapa during a colourful ceremony held at the State House in Dar es Salaam this afternoon.


Seven Public universities were granted the charter during the ceremony. They include Mzumbe University, Sokoine University, The Open Univesity of Tanzania, Muhimbili University college of Health sciences, Ardhi University, and University of Dar es Salaam


HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, KWENYE SHEREHE YA KUTOA HATI KWA VYUO VIKUU,VIWANJA WA IKULU, DAR ES SALAAM TAREHE 5 MACHI, 2008


Mhe. Waziri;
Waheshimiwa Naibu Mawaziri;
Wakuu wa Vyuo, Makamu Wakuu wa Vyuo Vikuu,

Profesa Nkunya ametukaribisha kwenye shughuli hii.
Niruhusuni niwakaribishe nyote hapa Ikulu. Ni furaha na heshima kubwa, kupewa fursa ya kufanya kazi hii adhimu ya kutoa Hati za Vyuo Vikuu saba vya umma. Hati zinazotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Vyuo Vikuu ya mwaka 2005.
Pengine watu wengi wanajiuliza kwa nini leo wakati vyuo vikuu hivi vimekuwepo kwa miaka mingi ukiacha labda Chuo Kikuu cha Dodoma. Profesa Mbwete ameeleza vizuri. Sababu ni kuwepo mahitaji ya kufanya hivyo kwa mujibu wa sheria mpya ya 2005. Lakini pia ni ule ukweli kwamba, baadhi ya vyuo kama cha Muhimbili na cha Ardhi, vilikuwa sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na sasa vinakuwa vyuo vinavyo jitegemea.

Pongezi:

Napenda kuitumia nafasi hii kuwapongeza Wakuu wa Vyuo Vikuu, Wenyeviti na Wajumbe wa Mabaraza ya Vyuo Vikuu pamoja na Makamu Wakuu wa Vyuo Vikuu, Manaibu wao na Wahadhiri wote kwa kazi nzuri waifanyayo ya kuliwezesha taifa letu kupata nguvu kazi yenye elimu na taaluma. Nawapongeza pia kwa kukamilisha masharti yaliyowawezesha kupata hati zao leo. Naamini itawahamamisha wale ambao hawajamaliza wafanye hivyo. Mmetoa na mnaendelea kutoa mchango muhimu sana kwa maendeleo ya nchi yetu na watu wake. Nawasihi tafadhalini endeleeni na moyo na juhudi hizo hizo au hata kuzidi.
Natambua kuwa wakati mwingine mnafanya kazi zenu katika mazingira ambayo yangestahili kuwa bora zaidi. Napenda kuwahakikishia kuwa kuyafanya mazingira yetu ya kufanyia kazi na kufanya mazingira ya wanafunzi wenu kuwa bora zaidi kwa kuishi na kusomea, ni dhamira yetu ya kudumu. Ni dhamira endelevu. Tutaendelea kutimiza hayo kila tupatapo uwezo na hasa katika kila bajeti. Tumekuwa tunafanya hivyo huko nyuma, tunafanya hivyo sasa na tutafanya hivyo siku za usoni.
Ili tujihakikishie maendeleo endelevu sasa na siku za usoni, hatuna budi kupata watu wengi waliopata elimu ya juu hususani elimu ya Chuo Kikuu katika fani mbalimbali za kusaidia kusukuma kwa kasi zaidi gurudumu la maendeleo.
Ni kutokana na kuutambua ukweli huo ndiyo maana kuwekeza katika elimu ya juu limekuwa jambo la kipaumbele cha juu kwa Chama na Serikali. Bila ya shaka mnakumbuka kuwa Chama cha TANU kilitoa jengo lake pale Lumumba kwa ajili ya kuanzisha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Kadhalika miongoni mwa mambo ya mwanzo mwanzo kabisa kufanywa na Serikali ya Tanganyika huru wakati ule ni ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pale Mlimani kilipo sasa. Kuendeleza elimu ya juu, kumeendelea kupewa kipaumbele cha juu mpaka sasa.
Ndiyo maana tangu Lumumba mwaka 1963 na sasa tunavyo Vyuo Vikuu vya Umma 7 na Vyuo Vikuu vishiriki 3.
Kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma chenye upeo wa kuwa na wanafunzi wengi kuliko vyote nchini, na kuendelea kupanua vyuo vikuu vilivyopo sasa kwa majengo, kazi na wanafunzi ni ushahidi tosha wa ukweli huo. Hata hivyo bado tuko nyuma.

Wakati nikiendelea kuwathibitishia kuwa tutaendelea kupanua na kuchukua hatua za kuimarisha elimu ya juu nchini, naomba nisisitize au kuomba mambo machache muhimu.

Jambo la kwanza, lazima tutafute njia ya kuongeza wahitimu wa fani za sayansi na teknolojia. Ni ukweli ulioje kuwa ni wahitimu hawa pengine wengine ndiyo chachu kubwa ya kuleta mageuzi na maendeleo nchini. Sifurahishwi na idadi ndogo ya wahitimu kwenye fani hizi hivi sasa nchini.
Hatuna budi kuirekebisha hali hiyo vinginevyo maendeleo yatachelewa sana na hata pale tulipofanikiwa kuna hatari ya kurudi nyuma. Natambua haja ya kulitazama tatizo hili kwa mapana hata kwa maana ya kuuangalia mfumo mzima wa elimu nchini. Lakini, hata haja hiyo hakuna mahali pengine pa kusema jambo hilo likapata sikio sikivu kushinda hapa leo. Wahusika wote wapo. Naomba mkalifanyie kazi.

Jambo la pili, ambalo ni ombi ni kuwataka muitazame mitaala yenu ili iweze kutoa jibu kwa kuwa na wahitimu wanaohitajika katika soko la ajira. Aidha, mitaala yenu pia iwawezeshe vijana wanaohitimu kuweza kujiajiri wenyewe iwapo hawatapata kazi ya ajira au wataamua kujiajiri wenyewe.
Kwa ajili ya hili la pili pengine mafunzo ya ujasiriamali yangetolewa kwa wanafunzi wetu ili wapate a,b, c za kuanzisha na kuendesha shughuli zao za kuwapatia kipato. Jambo hili litawapa moyo wa kujiamini na kujua la kufanya wanapoamua au wanapolazimika kujiajiri.

Jambo la tatu ambalo ni ombi kwenu, ni kuwataka muendelee kuhakikisha kuwa viwango na sifa za kitaaluma vya wahitimu wetu vinaendelea kuwa vya juu. Vyuo Vikuu vyetu vya Umma vinayo sifa hiyo nchini na popote duniani, ni muhimu kuidumisha sifa hiyo. Shahada katika fani fulani itolewayo hapa lazima itambuliwe kuwa shahada popote duniani. Isiwe kwamba mhitimu wetu anapovuka mipaka ya nchi yetu hadhi ya shahada yake ni sawa na diploma kwingineko.

Kama nilivyosema, sifa yetu ni nzuri duniani. Tuidumishe. Nalisisitiza hili kwa kuwataka msijisahau. Hatari hiyo inaweza kutokea hasa wakati huu kunapokuwa na wahitimu wengi wa Form VI na mahitaji ni makubwa na nafasi na upanuzi unakuwa wa kasi kubwa.

Ombi langu la nne kwenu ni kuangalia uwezekano wa kuongeza matumizi ya teknolojia ya kisasa ya mawasiliano na habari katika kufundishia (ICT). Naamini tukiongeza matumizi yake tutawafikia watu wengi zaidi na tutapunguza hata gharama za kujenga majengo kwa ajili ya kuwaweka wanafunzi darasani. Pamoja na hayo niwaombe pia tuhimize mafunzo ya ICT kama chombo mtambuka katika kuleta maendeleo.

Jambo la tano ambalo nalo ni ombi kwenu ni kutaka vyuo vikuu vyetu viwekeze katika shughuli za utafiti na ushauri. Pamoja na kazi ya kufundisha, vyuo vikuu ni chemchem ya mawazo mapya na bora zaidi ya kufanya mambo na kukabili changamoto katika jamii. Hii ina maana ya kuwa vituo vya utafiti ili vipate mawazo mapya na bora ya kushauri jamii. Natambua kazi hiyo inafanyika lakini nawaomba mfanye zaidi.
Kwa upande wangu nitataka wenzangu serikalini na katika jamii kujenga tabia ya kutumia kazi za utafiti zinazofanywa na vyuo vyetu vikuu na taasisi nyinginezo nchini.

Kabla ya kumaliza nieleze matumaini yangu kuwa vyuo vikuu vingine navyo vitapatiwa hati zao mapema iwezekanavyo. Natambua kuwa vilivyobaki ni vyuo vikuu binafsi. Wasije wakaona wamebaguliwa. Sekta binafsi inatoa mchango muhimu katika kutoa elimu ya juu nchini.
Mwaka huu asilimia 45 ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa vyuo vikuu wamejiunga na vyuo binafsi. Ni wabia muhimu. Napenda kuwahakikishia ushirikiano na msaada wa serikali pale unapohitajika, katika uwekezaji wao katika elimu kwa ujumla wake.

Mwisho, nimalize kama nilivyoanza kwa kuwapongeza kwa haya tuliyofanya leo na kuwatakia kila la heri. Nawahakikishia kuwa Serikali itakuwa pamoja nanyi.


Ahsanteni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. charter ni nini?

    ReplyDelete
  2. Apewae ndie aongezwae ilikuwa kama jana Rais mpendwa Ben alipomkabidhi ufunguo wa ikulu Rais Jk na leo hii ni yeye Rais Jk anamkabidhi vibwanga Ben .Halafu kuna wale wanaosema eti Rais ben kachukuwa hiki nakile akiwa madarakani nyinyi mlitarajia afanye nini kama ni kweli hayo mnayoyasema mimi siamai hivyo kwani Mkapa ni mtu wa mungu pia alikuwa hatoki Kanisani hawezi kufanya wizi kama kachukuwa ni ule ujira wake kidogo tu isitoshe alishasema amewacha uchumi katika hali nzuri sana na hilo naamini na ndio maana walikuja baada yake na kuona uchumi mzuri ndio yalitokea hayo yaliyotokea wajinga ndio waliwao na ndio pale mzee wetu makamba huwambia watu kuwa mavi ya wazungu ndio yanayotumika kufanyiwa sahani na watu hufurahia sana na kupiga makofi

    ReplyDelete
  3. WABEBA BOX TUONGEZE BIDII..KAZA BUTI MWANANGU..

    Tanzanian Diaspora now significantly contributes to GDP

    2008-03-03 08:45:25
    By Guardian Reporter, IPPMedia

    A latest report by the UN`s International Fund for Agricultural Development (IFAD) says Tanzanian Diasporas sent a total of USD313 million in remittance money into the country in 2006.

    This amount constituted 2.4 percent of the country�s Gross Domestic Product (GDP). Kenyan Diasporas transferred to their motherland USD796 million, which was 3.8 per cent of that country�s GDP.

    Ugandans living abroad managed to send to their homes USD642 million, representing 6.9 per cent of the country�s GDP.

    IFAD says remittance flows to and within Africa approach USD40 billion.

    Countries in Northern Africa (for example, Morocco, Algeria and Egypt) are the major receivers in the continent.

    Eastern African countries depend heavily on these flows, with Somalia standing out as particularly remittance dependent.

    For the entire region, annual average remittances per migrant reach almost USD1, 200 and on a country-by-country average represent 5 per cent of GDP and 27 per cent of exports.

    Ethiopians in Diaspora sent a total of USD591 million in remittance money to Ethiopia in 2006, and this amount is nearly 4.4 per cent of Ethiopia`s GDP.

    Sub-Saharan Africa has over 30 million people in the Diaspora.

    Of all the world�s regions, however, Africa`s predominant migration is intraregional, the report said. Remittance flows to and within Africa approach USD40 billion.

    North African countries such as Morocco and Egypt are the continent`s major recipients, the report stated. The annual average remittance per migrant is USD1, 358. The top five recipients of remittance money are Morocco, Nigeria, Algeria, Egypt and Tunisia.
    SOURCE: Guardian

    ReplyDelete
  4. Tujiulize kwa nini Tanzania bado ya mwisho miongoni mwa nchi za Afrika ya Mashariki na Kati na hata Afrika Kaskazini na Kusini katika hilo?Kwa nini vijana wetu walioko nje ya nchi bado wanaishi kwa kujificha ficha na kuogopa kama vile kwenda kuishi nje ni uhalifu?Kupata Pasi ya Kusafiria nje(PassPort)bado hapa nchini inachukuliwa kama ni bahati au upendeleo(Favour or Luck)kwa nini?Wakati mwingine inachukuliwa kama ni tahadhari ya kiusalama(Security Concern)hata bila sababu za kimsingi kutokana na sababu za kibinafsi(out of selfish motives) kwa nini?Wakati kupata PassPort ni haki ya kikatiba ya kila mtanzania.Watanzania wangapi wanalijua hilo?Je,kwa wale waliobahatisha kwenda nje na sasa wanaishi huko,Balozi zetu za nje zimechukua jitihada gani ya kuwakaribia watanzania hao na kuwafanya wajisikie wako huru na wawe na uzalendo wa kukumbuka kutuma sehemu ya mapato yao nyumbani kwa faida yao hapo baadaye lakini pia kwa faida ya familia zao na Taifa kwa ujumla?Je,mazingira yaliyopo hapa nyumbani yanavutia kwa kiasi gani kuwashawishi hao vijana wetu walioko nje watamani kutuma mapato yao huku nyumbani?Kama yupo aliyetuma pesa hapa nyumbani na akakabiliwa na vikwazo mbalimbali ningemuomba kupitia Blogu hii atujulishe watanzania wengine ili kusudi hatua zifaazo ziweze kuchukuliwa.Kwa mfano pesa hiyo itakayo tumwa hapa Tanzania itakatwa KODI kiasi gani?Mtanzania aliye lazimika kuchukua Uraia wa nje ili kumrahisishia mambo yake ya Utafutaji huko ugenini lakini bado yeye ni Mtanzania kwa kuzaliwa na angependa kutuma pesa na kuwekeza hapa nyumbani kwa faida ya watoto wake ambao pengine amedhamiria lazima hapo baadaye warejee kwa Babu zao na Bibi zao hapa nyumbani Tanzania,je, bado atakabiliwa na pingamizi zipi za kisheria(sheria ambazo kwa maoni yangu hazitufai na hazitatusaidia katika kujenga nchi yetu katika ulimwengu huu wa ushindani na utandawazi)?Katika mwaka mmoja tu wa 2006,Watanzania waishio nchi za nje walituma hapa nyumbani Tanzania Dola za Kimarekani milioni 313,wenzao wa Kenya waishio nje walituma kwao Kenya Dola za Kimarekani milioni 796,wenzao wa Uganda walioko nje walituma Uganda Dola za Kimarekani milioni 642,ilhali wenzao wa Ethiopia walioko nje walituma kwao Ethiopia Dola za Kimarekani milioni 591.Katika Bara zima la Afrika Pesa ambazo zimekuwa zikihamishwa kutoka nje kuja Afrika au kutoka nchi moja ya Afrika kwenda nchi nyingine ya Afrika katika utaratibu huu zilifikia Dola za Kimarekani Bilioni 40 katika mwaka mmoja tu wa 2006.Siyo pesa ndogo hata kidogo.Kukiwa na utaratibu mzuri utakao wahamasisha vijana wetu walioko nje watamani kutuma mapato au sehemu ya mapato yao hapa nyumbani na vizingiti vyote visivyo na maana vikaondolewa hakika tutapiga hatua moja kubwa sana mbele kimaendeleo.Nimejaribu kutoa ufafanuzi kidogo kwa faida ya wana Blogu wetu popote pale walipo ili waweze kuwa huru zaidi katika kuchangia mawazo kwa faida ya Taifa letu na kupiga fita Ukiritimba uliosukwa makusudi kabisa ili kulinda maslahi binafsi na himaya za watu walafi na mafisadi wakubwa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...