habari Mr. Michuzi.
Naifurahia sana blog yako. Najifunza mambo mengi sana, pia siku hizi sioni sababu ya kununua magazeti maana habari nyingi nazipata kupitia blog yako hii.

Mimi ni dada mwenye umri wa miaka 27. Ninaishi Dar es Salaam. Ni mkristo wa dhehebu la Lutherani (KKKT) Natafuta Mchumba
Mr. Mchuzi. Naomba unisaidie katika hilo. Kwa yeyote atakayepatikana tuwasiliane kwa email hii. mwananzali2004@yahoo.com.

Asante.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 29 mpaka sasa

  1. MHN, HEBU WACHA KUYEYUSHA WATU WE UNAEJIITA MWANANZALI KWANZA JINA LAKO KAMILI UMELIBANIA HALAFU HUJAJIELEZA KWA KIREFU KAMA MANKA ANGALAU..........HALAFU UNATAKA MCHUMBA HAHAHHAHAAAAAA HUYO UTAEMPATA LABDA NI MJINGAMJINGA KAMA WEWE LOH..........MDAU
    UK

    ReplyDelete
  2. Huko kanisani unakoenda hakuna watu? Majirani je? Kazini? Kote unakopita huoni watu unategemea wa mtandaoni usiowajua? Unatupa mashaka, kipo unachokificha ndio maana hao wa karibu unawaogopa! Kama kweli u mwaminifu na mtulivu, kwa umri huo mdogo hivyo wa miaka 27 sioni kwa nini ukose mchumba katika mazingira unayoishi na watu ambao una nafasi ya kuwaelewa vizuri! Na pengine una uhakika kuwa watu unaokutana nao (kazini, shule, kanisani, misibani, shereheni, jirani, nk) hawatakutafuta maana wanayajua makasoro yako ambayo unataka kuwabambikia wasiokujua! Kwa mwendo huu, muoaji makini haji kwako ng'o, watakuja wadanganyaji, watu wa kuja "kukuchora" kujua ukoje, na usishangae wote hao wakakuacha! Tulia binti, u mdogo sana bado, wenzio umri huo bado wako vyuo vikuu wewe unasaka wanaume mtandaoni?

    ReplyDelete
  3. lol !!mie nilikuambia unageuzwa dating agency hukusikia kazi kwako.

    ReplyDelete
  4. Nitumie picha kwenye e-mail yangu, mimi nafuata uzuri tu.

    ReplyDelete
  5. toa picha yako basi tukuone siku hizi tunapenda kuona kwanza.

    ReplyDelete
  6. Wala sio mjinga wewe ndio mshamba wala hauko UK, kuna ndoa nyingi sana za internet siku hizi ,japo watanzania tunajifanya kuzipinga ni ushamba hamna lolote, mliyakataa weeee magari ya automatic eti ya vilema sasa hivi ni fasheni.

    Mtu atakayemtka huyo dada atamwandikia e-mail, watakutana wakikutana sio ndio watakuwa tayari wachumba, ndio mwanzo wa mawasiliano.

    Huyu sio MANKA MSAIDIANE JAMANI.

    mdau canada

    ReplyDelete
  7. Toa picha basi tukuone, labda una makengeza tutaqkujuaje?, we hutafuti mchumba bali unajaribu kusanifu watu

    ReplyDelete
  8. Wachumba wako huko washington DC wengi tu.Sasa kazi kwako jichomeke tukuzike na wewe.Anyways call me 442083524460.Natafuta mchumba pia

    ReplyDelete
  9. dada wala haijatosha hiyo inatakiwa uelezee kidogo uko wapi,unafanya nini etc..pia angalau utaje sifa kiduchu za mchumba umtakae.

    ReplyDelete
  10. Mume mwema hutoka kwa Bwana Mungu Kwani huko KKKT unkosali huwezi kumwomba Mungu akupe mume hadi unaanza kuomba watu kwenye blog?

    Biblia inasema amelaaniwa amtegemeaye Mwanadamu sembuse anayetegemea hata kama anamtegemea mwanadamu amtafutie mume.Blog haziwezi kukupa mume mzuri.

    ReplyDelete
  11. TUNAKUTAKIA KILA LA KHERI, SASA NAKUREKEBISHA SIO MR MCHUZI NI MICHUZI, MCHUZI WA MAPENZI UTAUJUA UKIJAALIWA KUOLEWA,UTAUFUTA SANA!

    ReplyDelete
  12. This is bullshit man, if ya real serious cant u put your cell no.? Usitake kuanzisha league isiyo na maana kama ile ya manka!

    ReplyDelete
  13. Hivi watanzania tulilaaniwa na nani? Mtu kaweka ujumbe wake hapa, kwa nini muanze kumtukana na kumrushia maneno?

    Kama huna comment kwa nini usisome na kukaa kimya? YAANI HII INADHIHIRISHA UNANGA WA WAAFRIKA ESPECIALLY WENGI WETU WATANZANIA.

    If you got no comment..just read and move on, ya nini uanze kumwambia oohh mtegemee Mungu, jina lako si sahihi...kanisani hawakuoni, una kasoro na mengine kibao..we unafikiri yeye hana akili? This is too low jamani...kwa mtu mwenye uwezo na uelewa kama wengi wetu humu..hata wa kutumia computer!!!

    Watanzania wenzangu tujifunze kuishi na kasoro za wenzetu. lets cerebrate diversities and embrace differences. Heshimuni mawazo ya wenzenu hata kama hamyakubali. Heshimu haki ya mtu kuyatoa hadharani.

    Siyo kwamba kila mtu inabidi afikirie kama wewe! Please.

    Again nawaasa wenzangu kama huna cha kuchangia kaa kimya wacha wengine wachangie. Hatuwezi kuwa na mawazo yanayofanana. Tujifunze kuheshimu mawazo ya wenzetu hata kama hatukubaliani nayo. Mipango ni kuchagua na siyo kuchaguliwa!

    Anyway siwezi kuandika sana, maana comment kama hizi zinareflect jamii yetu ya Kitanzania iko vipi. Hawa ndo wapiga kura wa Kikwete...kazi tunayo kama taifa.

    Kibaya walioko nje sijui UK, US nk ndo ungetegemea wawe understanding kwa sababu ya exposure waliyonayo! But its to the contrary....inaboa sana. sijui tunajenga taifa la namna gani!

    DADA NAKUTAKIA KILA LAKHERI KATIKA SEARCH YAKO.

    God bless you!

    ReplyDelete
  14. Kwani UK ni wapi jamani nisaidieni. Si ndo Ukonga au...

    ReplyDelete
  15. mdau wa canada umesema kweli,ndoa zinazofungwa watu kuanza kujuana kwenye internet zipo kibao,mimi mwenyewe mmoja wapo.afta kuwa disappointed na x b/f nikaamua kutafuta kwenye internet nilipata interest nyingi but kati ya zote nilivutiwa na mmoja kukaamua kufahamiana kwa karibu though yeye alikuwa mbali sana lkn haikuwa tatizo tukakutana baada ya 8months kufahamiana kwenye internet tukaona tuendelee kuwa karibu zaidi ilichua kama mwaka 1 na nusu kufahamiana vizuri then tukaamua tuoane,tumeoana na tunapendana ajabu.nakupa moyo dada usisikilize maneno ya waosha vinywa hizi dating site zinasaidia ila unatakiwa uwe makini usije ingia mkenge maana kuna matapeli pia.weka email yako nikupe mbinu

    ReplyDelete
  16. umenipata, sharti langu moja tu, usiwe bikira maana mimi mwenyewe sio bikira.

    ReplyDelete
  17. Huyu dada inawezekana ni Manka Mushi sababu wachaga wengi ni KKKT.Kaona abadili namna ya kupata mume baada ya ile ya kwanza kushindikana.

    ReplyDelete
  18. Anony wa 10:31,march 27, umesema sahihi, mimi huwa nashangaa sana hili jambo, unajua watu wamesahau tumetofautiana, culture, mitazamo, mawazo, maamuzi,lifestyle, malezi, sijaona sehemu yoyote kwenye blog hii michuzi analazimisha lazima utoe maoni, na hii ni dalili ya matatizo na mtindio wa ubongo, ambao bado wengi wanao, this is free area for anybody to ask anything for his benefits, so long hakuathiri wewe kwa namna yoyote.Dada hajatukana , kaomba kwa heshima, JAMANI AMBAYE YUKO INTERESTED NA YEYE AWASILAINE NAYE NA WAKIKUTANA SIO KUWA WATAKUWA NDIO WACHUMBA,HALI KADHALIKA HUYO DADA HAWEZI KUMKUBALI MTU YEYOTE KISA ATI KWA SABABU ALIOMBA KUPITIA KWENYE BLOG.

    GLOBALIZATION MEANT TO CHANGE, people a different, kuna watu wanatamaduni na mawazo tofauti.

    aiiiiiiiii!!!!! acha nichekemie.....kama hata mnaoweza kutumia internet na kompyuta bado mawazo yenu yako dormant and miaka ya 47, what about those our sisters and brothers ambao hawajasoma!!!! kumbe elimu wakati mwingine haimsaidii mtu hata akiwa UK au USA au anywhere?? why dont u mind your bussiness ?? huu ushamba

    mbona kuna vitu vingi na blo nyingi kwenye internet???, ni lini utakapojua watu wametofautiana??

    This is shame to you all guys.


    Michuzi ebu tutafute mchawi nani ameturoga??

    watu mnakuwa mafisadi mpaka kwenye mawazo na nia za watu wengine??

    mdau-canada

    ReplyDelete
  19. Anon mar 27. 10:31 Pole kwa kuumizwa na baadhi ya comments za humu ndani ni hivi, si wtanzania wote wenye fikra potovu na kutokuwa wakarimu katika kutoa misaada hata ya ushauri. na usiwe ma mawazo kuwa labda hii ni jamii ya wa-tz wanavyokuwa hapana wapo wa-tz waadilifu wenye ukomavu wa kimawazo. Haya ndiyo yale matunda ya mbegu zipandwazo wakati wa utoto wa tabia aidha za utundu au upuuzi au utoto, Waache waoshe vinywa ni mali yao hawalipi vat. hivyo wanafikiri vile haonekani au anafurahia hutoa uozo wake au kutuonyesha vitabia vyake potuvu kwa kutokua na busara, wahenga husema kuwa tabia haina dawa, na mazoea yana tabu pia wanasema asiyefunzwa na mamae hufunzwa na ulimwengu. Ipo siku watakuwa na watakuwa na watoto, na watoto hao hao wao watawaendea kwa kuomba ushauri juu ya hilo, kwa vile hana uzoefu wa kutoa maneno ya uzima atakumbuka bora angejifunza kufariji wengine na kuongea na kufikiri busara ya kumjibu kijana wake endapo atatingwa na jambo na kukimbilia kwa mzazi wake ambae ni yeye.

    Dadangu sasa hao ndo wachumba wanojitokeza humu. Kuna andiko linasema limjazalo mtu ndilo limtokalo, nao wanaojibu humu utawajua tu kwa maneno ya upuuzi na ya chuki na uchoyo.
    ushauri wangu Tafuta marafiki unaokuwa nao na jaribu kuwa mwangalifu pamoja na kuwa nae atajaribu sana kuficha madhaifu yake ili akupate muombe mungu sana akupe uamuzi mzuri juu ya huyo ambae utakuja uishi nae usiku na mchana
    Mdogo wetu nakutakia maisha mema endapo utafanikiwa.

    ReplyDelete
  20. hongera sana dada.unampango mzuri na utapata mtu,tena si kama wengine wanavyosema eti utapata mjingamjinga.
    kwajinsi ulivyo present message yako ni sawa,pia siolazima kutumia jinalako halisi,katika public kuhifadhi confdentiality hadi pale unapo ridhika kuweka wazi jinalako nihaki yako yamsingi. ndiomaana hata wengi wa wachangiaji hapo juu wanatumia anonymous badala ya kutaja majinayao.je tuseme nao wote wanakasoro na walichochangia ni feki?may be! lakini kwa uelewa wangu nahisi wengi wa wanao kuponda wanaweza kuwa ni akinadada wenzio wasio na ujasiri wa ku-take risck to try at the best of their level.
    mimi nimwanaume pia natafuta mchumba,nikonje ya africa,pia nimesoma and i hope tutawasiliana.
    waache wanao ponda na kuzuga eti hivi siosawa, wakae then watakuja kustuka is already too late.
    kwa anayesema kuhusu kumtegemea mungu nisawa,lakini huenda hawaelewi nini maanayake. huwenzi kukaa usijishughulishe kutafuta unayo yahitaji ukisubiri mungu akuletee,mungu ata kutengenezea mazingira mazuri kama anavyo watengenezea ndege wa angani,lakini jukumu la kuruka na kwenda kutafuta ni lao wala sio la mungu. so you did the best you could,sasa mungu ndie anaweza kumfungua macho wakufaana nawewe ili mfikiane.
    nawa encourage pia na wengine ku-take the same initiative it may work out!don't be ashamed, no one is perfect! if God were to find the perfect one on earth, then i don't think that there is any one who could qualify! since all of us we are prone to err. cha msingi tu ni kusahau the past and move on! and that is life. otherwise you can spend the whole life reacting to the past history, but for me i choose to spend my entire life creating a new history,and each time bettering my weakness to a more positive way of life.
    HONGERA SANA, I WISH YOU THE BEST.

    ReplyDelete
  21. Anony wa thursday 10:31 Am nakubaliana na wewe 100% humu ndani utafikiri watu bado wanaishi zama za ujima. Tena hao walioko nje ndio usiwahesabu kabisa maana baadhi wao ni washamba wa ajabu wewe angalia comments zao. Sijui kwa sababu ya kukaa darasani na wakitoka darasani wanaishia kuosha vyombo, kufagia na kufanya kazi nyingine za fatiki sasa maisha watayajuaje? na hata wakipata nafasi ya kutoka ni usiku kwenye nightclubs na pubs, huko wanajifunza nini kwa wao kuwa nje ya nchi? Hawana muda wa kubadilishana mawazo hata wao kwa wao au kuona dunia inavyosonga, muda mdogo wakipata ni humu ndani ya blogu za watanzania na kusoma magazeti ya bongo basi. Hata muda wa kusoma vitabu nje ya vile wanavyolazimishwa kuvisoma shuleni hawana. Hapa sisemi ni wote nasema baadhi kulingana na comments tunazoziona humu ziko so narrow minded. Grow up. Wako walio nje lakini wanaonekana kabisa kuwa wamejifunza mengi kutoka huko nje na wanatoa mchango wa kuridhisha wanapochangia mawazo yao. Lakini wengine, mhu utashangaa hata huko shuleni wanasoma nini!

    ReplyDelete
  22. UK NI UKONGA NA US NI USAMBARA!.
    ACTUALLY UTAMADUNI WA KUTAFUTA MCHUMBA KUPITIA VYOMBO MBALI MBALI VYA KUPASHANA HABARI KAMA MAGAZETI ETC NI KITU CHA KAWAIDA KATIKA BARA LA ASIA ESPECIALLY INDIA. KWA HIYO SISHANGAI, USIFE MOYO DADA UTAMPATA TU, BUT YOU HAVE TO BE VERY WISE IN MAKING UR DECISIONS....!
    MDAU INDIA.

    ReplyDelete
  23. UK ni Ubungo Kibangu.

    Anonymous ndio nani jamani? Kila nikija yeye ndio wa kwanza kutoa comment..Kama haitoshi, anajijibu mwenyewe, anabishana mwenyewe. Habebi box nini?

    Anonymous Original.

    ReplyDelete
  24. haya ni mapepo wewe demu lazima utakuwa kimeo hapa bongo we uza wanunuzi wapo

    Cole

    ReplyDelete
  25. Mpaka tumepata muda wa kusoma comments na kuzijibu sijui kurumbana....ukosefu wa kazi za kufanya huo
    na huyu mtafuta mchumba nae hayuko serious hata kidogo si uende kwenye ma web date huko kwanza miaka 27 utakuwaje desperate hivyo ndugu yangu kuwa mtulivu na umuombe mungu wakati ukifika mungu atakupa mtu wako kuwa na imani dada... na maisha ni vyo vyote kuna watu hawajaolewa na wanaishi maisha mazuri sana just be positive na uamini maisha ni wewe mwenyewe unavyopanga na kumshirikusha mungu

    M-KKKT mwenzio

    ReplyDelete
  26. nenda kwenye dating site za waafrika wapo kibao hata wanaume wa kibongo pia wapo utasoma profile zao na wewe ucreate ya kwako watu wasome pia.itakuwa rahisi kwako.all the lucky

    ReplyDelete
  27. Utapata mume mwema humuhumu wala usijali. NAKUOMBEA MUNGU

    ReplyDelete
  28. Big up Dada upo so strong ingawa sio rahisi kumridhisha kila mtu anachofikiria kwa kuanzia hapo pazuri mwenye nia na wewe atatafuta njia ya kukupata.

    ReplyDelete
  29. Kazana kuomba dada utapata mchumba. Tena huko KKKT kuna walokole wanaoombea watu na kufanikiwa mambo yao, waone hao wakusaidie.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...