HIVI MAJUZI NILIPOKUWA UKEREWE NILISIKIA KWAMBA NI ASILIMIA 13 TU YA WABONGO NDIO WAMEJIANDIKISHA KWENYE JUMUIYA YAO HUKO, NA KWAMBA ASILIMIA NDOGO ZAIDI WAMEJISAJILI UBALOZINI KATIKA KUTIMIZA ULE WAJIBU WA KAWAIDA WA KUTAMBULIKA KAMA UKO HUKO UGHAIBUNI. NIMEJIULIZA MWASWALI KADHAA NA KUKOSA MAJIBU.
WADAU NAOMBA MNISAIDIE KUJIBU BAADHI YA MASWALI HAYO.
MWENYE NIA YA KUCHAFUA HALI YA HEWA ASIJISUMBUE KWANI MAONI HAYO HAYATOONA MWANGA WA JUA. MASWALI NI KAMA IFUATAVYO:
1. KWA NINI WABONGO WENGI HAWAJIANDIKISHI KUWA WANACHAMA WA JUMUIYA ZAO UGHAIBUNI?
2. KWA NINI WABONGO WENGI UGHAIBUNI HAWAENDI KWENYE OFISI ZA UBALOZI WAO NA KUJISAJILI?
3. NINI UFUMBUZI WA SWALI NAMBA 1 NA NAMBA 2?
NAOMBA KUWASILISHA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 111 mpaka sasa

  1. wengi wao wazamiaji wanaogopa kupigwa miswali wakienda ubalozini kujiandikisha

    ReplyDelete
  2. ni swali gumu kujibu kwa niaba ya muhusika kaka michu, sababu ni wazi, kila mmoja aliyejitenga anakikwazo chake. hivi unapojiandikisha, kuna faida yoyote mbeleni!! unapojiandikisha naona hamna msaada wowote, zaidi ya usumbufu. nikitaka kuzamia nitashindwa sababu ninajulikana huko ubalozini. vile vile wabongo hawana mapenzi na mafanikio ya mbongo mwengine penginem, ndo maana wengine wanajitenge kujiandikisha kwenye uanachama.

    ReplyDelete
  3. I HOPE LEO UTAPOST COMMENT YANGU MAANA HUWA SICHAFUI HEWA ILA HUWEKI POST ZANGU.. AU KUNA MEMBERS????

    Tatizo ni kwamba wabongo wengi
    wamejilipua, huku tunajua kaka dada zetu wapo ughaibuni lakini kule wanajulikana kama wanyarwanda, wasomali n.k nawajua wengi na inanisikitisha sana. ok wawe huko wakumbuke bongo basi!! hawakumbuki hata kidogo inakera sanaaa dawa ni sisi tunaowafahamu kuwanyooshea vidole ingawa wengi pia wanajitenga na hawataki mazoea na wabongo wenzao

    ReplyDelete
  4. Sababu kubwa ni kukata tamaa. balozi zetu hazina msaada wa aina yoyote kwa Watanzania.Wengi wa maafisa ni majigambo na kutengeneza maisha tu.Hata mtu ukifikwa na tatizo haiwasumbui. Wangapi wanasota magerezani Italy, Ugiriki na kwengineko.Unapoingia katika balozi hawa jamaa huwa wanakuangalia kinamna kama vile hustahiki kuitwa binaadamu. Sasa ya nini ndugu yangu kujisumbua na kujiandikisha ?Waache wale nchi tu .

    ReplyDelete
  5. wabongo wengi ughaibuni wanafanya shughuli zisizorasni hivyo hawataki kujulikana wanafanya nini.Unapoongerea ubalozi unamaanisha hao ni wahamiaji halali na wabongo wengi tuko huku kama wahamiaji haramu,hivyo ni vigumu kujisajiri ubalozini.Utakuta wengi wa wanavikundi ni wanafunzi tu. kaka haya niyakawaida huku.

    ReplyDelete
  6. kwa sababu hawana makaratasi sasa hawajui nani wamuamini na nani wamkimbie. Better safe than sorry

    ReplyDelete
  7. ASANTE SANA BWANA MICHUZI,
    INAFURAHISHA SANA KUONA. BAADA YA BLOG HII KUWEKA PICHA ZA WATU NA MIJADALA KADHAA ILIYOWAKERA BAADHI YETU, NA KUTUELIMISHA WAKATI HUO HUO, SASA TUNABADILI KIDOGO MADA.

    NAJIBU SWALI:
    WATU WENGI, HATA MIMI SIJAJIANDIKISHA UBALOZINI, WALA UMOJA WA CHAMA CHA WATANZANIA KWASABABU:-

    1) NIKIWA HAPA USA, NILIWAHI KUPIGA SIMU UBALOZINI D.C. KUTAKA KUONGEA NA BALOZI -UJUMBE AMBAO NI BINAFSI. MAJIBU NILIYOPEWA NA DADA MMOJA, YALINIKATISHA TAMAA. NILISHAMWELEZA KWA JUUJUU KUWA SHIDA YANGU ILIKUWA YA BINAFSI KWA BALOZI, NA NAOMBA NIUNGANISHWE NIONGEE NAYE. NA KAMA HAITOSHI, NILIJITAJA JINA LANGU, ANAWANI YANGU, MJI, NA SIMU AMBAYO TAYARI NAO WANAIONA NI YA MJI NILIOPO KWA ILE CODE NUMBER. YULE DADA ALINIAMBIA KAMA SIWEZI KUMWELEZA SHIDA YEYE, BASI SINA SHIDA NA BALOZI. HAPO SIKUELEZWA KUWA TARATIBU ZAO BALOZI HUWA HAPOKEI SHIDA ZA BINAFSI, NA PILI HUYO DADA ALIKUWA MWENYE HASIRA KIDOGO, KAMA VILE HAIKUWA SIKU NJEMA KWAKE. KIBAYA ZAIDI, KUKAWA NA WAMAREKANI NA WAKONGO WAKIJADILI NAMNA WASIVYOPENDA HUDUMA ZA PALE UBALOZINI. IKAWA SASA NDIO WAMEONGEZEA MOTO ZAIDI KWANGU MAANA NILISHAONJA KITU KAMA HICHO.

    2) KUTOJIUNGA NA CHAMA FULANI INATOKANA NA KUWA VYAMA HIVI VINAENDANA NA MASLAHI BINAFSI ZAIDI KWA UONGOZI. UKIACHA KUSAIDIANA KWA WANACHAMA WAKATI WA SHIDA. VIONGOZI WANAKUWA NA TUHUMA ZA UBADHIRIFU WA FEDHA NK. PIA WANAWEKA MATANGAZO KWA WANACHAMA KUPITIA BLOG WAKATI SI WOTE WANAOSOMA BLOG.

    3) UKWELI BWANA MICHUZI, KUNA BAADHI WANAOKAA NJE YA NCHI KIMTINDO, NADHANI UNANIELEWA NATAKA KUSEMA NINI. WATU KAMA HAO, HAWATAKI HATA SIMU ZAO ZIJULIKANE, WALA MAJINA YAO MTAANI, NK. MAANA ZALI LIKIIBULIWA NA UHAMIAJI HUWA MOTO HAUZIMIKI, HADI UKAPOKELEWE NA VIJANA WA AFANDE MWEMA TZ.

    4) BALOZI HUKU NJE ZINA MSAADA MDOOOOOGO MNO BILA KUTETA. HAWAJAWAHI KUTOA WITO WOWOTE JUU YA WATANZAIA KUJIANDIKISHA KWAO. MIE NAHISI SIKU NIKISEMA NIWAPIHGIE SIMU KUJITAMBULISHA, WATASEMA, NANI KAKWAMBIA TUNAANDIKISHA RAIA WA TZ?

    5) NIKUULIZE SWALI NDUGU MICHUZI. ALIYESEMA ASILIMIA 13 TU, ANAJUAJE IDADI YA WATU WALIOINGIA NCHINI HUMO WAKATI UBALOZI WA TZ HAUHUSIKI NA IDADI YA WATU WALIONGIA UGENINI? MIE NAMWONA MTOA TAKWIMU KAMA ANAKADIRIA TU, HAINA TOFAUTI NA DADA YETU MWAJUMA.

    6) NATOA CHANGAMOTO MADA YAKO MICHUZI IWE CHANZO CHA KUWAUNGANISHA WATANZANIA NJE YA NCHI YETU.





    Mdau wa usa

    Asante sana Michuzi.

    ReplyDelete
  8. hakuna tofauti ya kujiandikisha au kutojiandikisha kwani hawasaidii chochote.

    ReplyDelete
  9. Kuna wabongo waliokuwepo ufghaibuni, halafu kuna wabongo waliokuwepo UAIBUNI, Wale waliokuwepo ughaibuni ni wale ambao wanatambulikana oficially kama ni wabongo, na wale waliokuwepo kule UAIBUNI (MOST OF THEM IN uk)ni wale ambao hawana utambulisho wowote kama wao ni wabongo,(Mujahidins)tunawaita, watu wa kujiripua, kwa hiyo utaona wengi wao katika UK wanashindwa kujiandikisha kama wao ni wabongo kwasababu hiyo ya kujiwasha. Ukizungumzia Ughaibuni, UK itoe. Huko Tunakuita UAIBUNI. Choo kitupu.

    ReplyDelete
  10. Sababu moja ni urahisi wa kujiandikisha. Niliwahi kujaribu kujiandikisha on-line lakini mfumo wa mtandao wa ubalozi ukawa haufanyi kazi vizuri na hivyo nikaacha. Hii ilikuwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Baada ya hapo nikazongwa na maboksi na hadi leo sijajaribu tena. Kwa hiyo neno ni "urahisi" wa kujiandikisha.

    ReplyDelete
  11. Vigumu kweli kuwa na jibu la moja kwa moja kwanini wenzetu walioko ukerewe na pengine nchi nyingine za ughaibuni wanashndwa kujitambulisha kwenye ofisi zetu za balozi katika maeneo waliyopo.

    Nianze na swali la pili maana naona ndio pahala penye uzito zaid, ukifuatiwa na swali la kwanza.

    JIBU LA SWALI LA PILI)Binafsi nikiri, sikuwahi kujiandikisha katika ubalozi wa ukerewe enzi nikiwa shuleni kule pale UCE, na hii ilitokana,kwa mtazamo wangu kuona kuwa hakuna msaada wa maana nitakaoupata pale ubalozini, ikiwa tu kubadilisha passport(wakati ule) ilikuwa ni mshikemshike. Huu ni mfano mmoja tu lkn tumeshaona malalamiko mengi sana kwa balozi zetu za nje kuwa na msaada mdogo wa watanzania walioko huko, Natumani kwa kuwa na bzlozi mpya mambo yatakuwa yamebadilika. Lakini pia nisilaumu serikali peke yake, hata sisi watanzania tulioko huko tunahusika kabisa kwa uzembe tu kama niliyokuwa nao mimi kwa kisingizio cha kutoona msaada wowote kutoka balozi husika, au kutokana na kuishi illegal nchini humo, maana takwimu zinaonyesha wengi wetu tumeenda kule kwa kisingizio cha kusoma lkn tusione darasa kwa muda wote wa visa. Obviously inakuwa ni ngumu kuongezewa muda wa visa, so njia peke iliyobaki ni kuishi kwa kujificha maisha yote na wengine wameshazidisha zaidi ya miaka kumi hawauoni uwapi mwanga zaidi ya kubaingaiza kwa kupiga box. sasa sidhani kama watakuwa na guts za kwenda ubalozini wakijua wanaishi bila ya vibali, na kwa wale wenzetu wa zanzibar walilekeea huko na kujivisha u asylum seekers enzi za machafuko ya zanzibar pia ni mwimbo ule ule...maana sababu zimeisha, hakuna machafuko tena. sasa factors hizo mbili kwa mtazamo wangu ni zinaleta ugumu katika zoezi hilo zima

    JIBU LA SWALI LA KWANZA)Pengine kwa ku sharubu jibu la swali la pili nipende kusema kuwa, pengine kwa kutoenda kujitambulisha ubalozini, imefanya kuwa ngumu kwa watu kwenda kujusajili kwenye jumuiya hii. Na pengine pia, abda jumuiya hii haijajikita katika kampeni za kujitangaza kisawasawa, sidhani websites pekee na aina nyingine ya matangazo yatatosha kutangaza jumuiya. Pengine sijui mfumo mzima wao, ila kwa maoni yangu kama bado, kungeanzishwa kampeni ya kuanzisha mashina madogomadogo kwenye vitongoji vyote ndani ya ukerewe ambavyo kazi ya kwanza ni kufanya sensa ya watanzania bila kujali kama wanaishi kihalali au la(hii ni kama changamoto) halafu kwa kushirikiana na ubalozi kuanza kuwa encourage watazania kwanza kujitambulisha kwenye ubalozi wetu na pia kujiunga na jumuia.

    JIBU LA SWALI LA TATU) kama nilivyokwisha kusema kwenye swali la pili, mi nadhani hizi jumuia za ughaibuni zinge play part kubwa sana kwa kuanzisha mashina vitongojini na kufanya sensa isiyo rasmi. kwa kushirikiana na ubalozi kwa kutumia majibu ya hiyo sensa then wwtumie ushawishi laini(soft approach) kuwavuta wenzao kujitambulisha ubalozi na kwenye jumuiya hizo. Baada ya hapo nadhani watu wote watakaoingia ukerewe watajiunga mara moja maana watakutana na shina katima sehemu wanazoishi..nafahamu kuwa kuna gharama kubwa kwa kufanya hivyo lakini naamini hakuna kitu cheap hasa tukizungumzia maendeleo ya mmoja mmoja na maendeleo ya nchi kwa ujumla.

    Mungu wabariki watanzania waishio huko, mungu ibariki Tanzania.



    mdau wako hapa, tuliekutana na ku share some ideas pale DOHA airport ukiwa unaelekea Frankfurt

    ReplyDelete
  12. Bwana michuzi hatufahamu jumuia hiyo inafanya nini, ina manufaa gani na itatusaidiaje. Isije ikawa tunajiandikisha halafu kumbe ikawa ni kujiunga na CCM, hiyo hatutaki. Maana huku imekuwa kila kukicha watu wanafungua matawi ya CCM.

    ReplyDelete
  13. tatizo sio sisi mzee ila wao wenyewe wamesahau kama kututafuta pia ni wajibu wao,, gharama za kusafiri kutoka sehem moja kwenda ingine hasa hapa Ukerewe ni kubwa hivyo tunawaomba watumie fungu wanalopewa na serikali yetu kuja kututambua na wasikae tu ofisini kutusubiri sisi wengi ni wanafunzi hatuna uwezo wa kusafiri kwenda kwenye mikutano ya umoja au inayoandaliwa na ubalozi....

    Solution kwa maswali yako kwa upande wa ukerewe,, Balozi na crew yake wafanye kazi na kushirikiana na waTZ wote na sio wa London peke yake maana kuna wengine wanauita ubalozi wa Tanzania London kwa kua balozi na crew yake wako karibu na watu wa london pekee..

    Asante Bro..!

    ReplyDelete
  14. Michuzi a.k.a misupu, ujanywa chai asubuhi???? jibu la swali no 2:Hawa watu wameozaaaaa! wataendaje ubolozini???? ufumbuzi ni ubolizi wa TZ kuwajibika wakishindwa wajiuzulu kama Lowassa, Karamagi, Chenge, Balali n.k

    ReplyDelete
  15. 1.
    Bwana Michuzi huku hakuna jumuiya za Watanzania bali kuna Jumuiya za CCM au Matawi ya CCM sasa si kila mtu anapenda siasa au ni mwana CCM.

    Mikutano mingi inayofanywa na balozi wetu ni ya CCM. Je tusiofanya siasa tuombe na sisi ubalozi wetu?

    2
    Hao watu wa ubalozi ukitaka kujua kama wanawatumikia watanzania piga simu ndipo utakapojua jinsi wanavyojibu kama utabahatika simu yako kupokelewa. HATA WEWE BWANA MICHUZI PIGA HATA HAPO ULIPO USIKIE.

    Hii niliona wakati wa kubadilisha passport utapiga simu siku nzima hazipokelewi hasa ukizingatia kulikuwa na option ya idara ya Passport so wanajua wewe ni mbongo.

    Na simu ikipokelewa basi utakavyojibiwa ni kama umemkosea huyo mtu. Infact hakuna customer service language.

    Pia nilienda kutengeneza document mwanangu alikuwa anasafiri infact ina - frustrate wale watu sijui hawako motivated na kazi zao? Ilifika wakati sijui nifanye nini ingawaje niliweka appointment baada ya kutumia hours kwenye simu najaribu. Sikupata mtu wakunisikiliza na ilionekana kila mtu alikuwa na mambo yake.

    Mwisho nikakutna na bwana mmoja ambaye nilikutana nae wakati wa kubadilisha passport alinitengenezea hizo document lakini guess what ILIKUWA NI FAVOUR. Sasa sijui kama hii ni isolated incident au ndio practice zao. Ila kila mtu niliyemuuliza jinsi wanavyofanya kazi pale alikuwa hajui MAY BE WANATAKA RUSHWA PIA.

    Kama Balozi hajui yote haya basi atakuwa hajui kama wafanyakazi wake wanafika kazini.

    Nafikiri hii inajibu swali lako la pili kama mtu ana-experience vitu kama hivi haoni haja ya kwenda kujiandikisha.

    MIchuzi usiyabanie maoni yangu ili watanzania wenzangu nao waseme kama ilikuwa ni INCIDENT MOJA BALI SI PRACTICE YA BALOZI YETU HAPA UK.
    Mzee wa shamba

    ReplyDelete
  16. JIBU NI RAHISI, HAKUNA HAJA YA KUANDIKA MENGIII, NI KWAMBA: MAISHA, AT THE END OF THE DAY IS A PERSONAL MISSION, SASA HIVI VYAMA VINAKUJA NA SERA KINYUME NA KILE KILICHOMTOA MTU KISHIMUNDU AU KAMACHUMU HUNA BUDI KUJIFANYIA SHUGHULI ZAKO KULIKO KUANZA KUJIUNGA NA VYAMA VYA KUCHOMA NYAMA NA MIDUARA. UBALOZI NI SEHEMU YA MWISHO KUKIMBILIA! HERI UKIMBILIE INS UTAPATA MSAADA. THE WHOLE THING ABOUT STATE ACTORS THROUGH DIPLOMACY NEED TO BE REVIEWED. MUUNDO WA EMBASSY NYINGI NI ULE ULIBUNIWA NA THEORIES ZA INTERNATIONAL RELATIONS KARNE YA 16! WHY BOTHER RINGING THE EMBASSY?

    ReplyDelete
  17. Hakuna mtu atakayeshindwa kujiandikisha eti karatasi hazijatulia kwani Ubalozi ni Immigration? Siyo sababu shida ya Ubalozi huku ni CCM mno kila wanachokifanya ni CCM sasa huku hatukuja kupigania uhuru.

    Ubalozi hauna msaada wowote waulize wameshasaidia watanzania hata hao waliojiandikisha.

    Pia hizo 13% sijui wamezipata wapi kama wanajua hizo asilimia ina maana basi wana jua kunawatanzania wangapi.
    Mkulima

    ReplyDelete
  18. Kujiunga na chama si lazima na kama wadau waliosema hapo juu kuwa hakuna faida yoyote unapokuwa na matatizo.
    Halafu vikao vingi vinafanyika London, watu wengine wapo mfano Manchester-ni gharama ambazo hazina faida!!

    ReplyDelete
  19. Mimi naishi glasgow Scotland, nakumbuka nilituma email tangu mwezi wa pili (Feb 2008) kujaribu kuulizia jinsi gani naweza kujiandikisha ubalozini mpaka leo hii sijapokea majibu.....sasa kama watu wanaoperate namna hayo sidhani hata kama inaleta hamu ya kuendelea na hatua zaidi.

    ReplyDelete
  20. TATIZO NI MAJUNGU KATIKA HIZO JUMUIYA NA VIONGOZI KUTUMIA JUMUIYA HIZO KWA MANUFAA YAO. NINEKWENDA KWENYE MISIBA; HARUSI NA SHUGHULI NYINGINE ZA KIJAMIII. BALOZINI WENYEWE WANATAKA UWASUJUDIE NA UJIKOMBE NDIO WAKUSIKILIZE, YA NINI YOTE HAYO!!!! SIJAONA NINACHOKIKOSA KWA KUTOJIUNGA NA HIZO JUMUIYA AU KUJIANDIKISHA UBALOZINI CHA ZAIDI NAJIEPUSHA NA MAJUNGU NA BIFU.

    ReplyDelete
  21. Bro Michuzi, nafikiri warekebishe maswali yao. Haingii akilini kwa mwananfunzi private sponsored kwa mfano, aliye hangaika mwenyewe kuanza kujaza fomu ya ubalozi wa Ujerumani. Haina tofauti na ile ya kuomba mkopo wa elimu ya juu nyumbani. Unataka kujua nini? Uliza maswali ya msingi watu tutajaza fomu online na kutuma, hamna hata haja ya kuonana na ubalozi.

    Mdau Deutschland

    ReplyDelete
  22. MICHUZI ASANTE KWA SWALA LINALONIKERA SIKU NYINGI JAPO KWA MLANGO TOFAUTI yaani balozi zetu.

    MAJIBU YA MASWALI YOTE MAWILI NI MFUMO USIOKIDHI WA BALOZI ZETU.

    KWANINI?

    1. WENGI WA WATANZANIA AMBAO HAWAJIANDIKISHI NI WALE AMBAO WAKO HUKO KUJITAFUTIA MAISHA AIDHA KWA MASOMO AU KUBEBA MABOX. HAWA NI WATU DUNI NA NI GHARAMA KUJISHUGHULISHA NA VITU KAMA HIVYO KWA KU-INITIATE WENYEWE TU NA BILA HAMASA NA SUPPORT YA MAKUSUDI YA BALOZI ZETU.

    2.MABALOZI KUFANYA KAZI ZA KIITIFAKI ZAIDI KULIKO ZINAZOGUSA MAISHA YA KAWAIDA YA WABONGO WA HUKO UGHAIBUNI. hii ni kwamba mabalozi wetu huko wanajiona 'mno' ni sehemu ya serikali hivyo nadhani wanapenda wafuatwe badala ya wao kuwafuata watanzania huko waliko. wako mkao wa kusubiri matatizo ndio wafanye kazi. sio proactive bali reactive.

    jiulize ni mabalozi wangapi wanaandaa hafla za kawaida za kukutana na watanzania katika miji mbalimbali kwa mizunguko hasa katika siku za kitaifa au hata za kawaida?

    pia ni wangapi katika majumuiko hayo wanaweza kupambanua itifaki za kichama na utanzania?

    kuna wakt huwa nashindwa kujua kazi za mabalozi huko ughaibuni zaidi ya kuwapokea viongozi wa kitaifa kwenye ziara tu.

    ofisi nyingine za kibalozi zina matatizo makubwa kiasi kwamba unapiga simu unapokelewa na mtu ambaye hata kiswahili hajui na bado anakuweka kwenye waiting list. hii imetokea mwaka juzi ubalozi wa tanzania Sweden (wenyewe wanajua). Kwa utendaji huo nani atavutiwa kujiandikisha?

    najua kuna wale wanaosema ni jukumu (labda hata sema ni sheria) kwa mgeni kujiandikisha na ni kwa manufaa yake. hiyo ni kweli lakini kwa utamaduni wa mtanzania hilo linakuja kunapokuwapo kwa matatizo.

    Lakini ni aibu kama taifa halifahamu watu wake wako wapi eti hadi wajitambulishe wenyewe. najua ni vigumu lakini wakitaka inawezekana.

    watanzania watajiandikisha kama balozi zetu zitabadilika na kufanya maswali yenye maslahi ya wazi kwa wageni na sio itifaki tu. mtu anajiuliza njiandikishe ili iweje? hivyo ni jukumu la hawa watu wanaolipwa vijisenti kuhudumia nchi nje huku kufanya kazi ya makusudi ya kuwaunganisha watanzania. wajue kazi wanazopaswa kufanya ni kuhudumia wananchi na si kuhudumia ofisi.

    UFUMBUZI
    1. UBALOZI UWE KAZI YA KIUCHUMI KULIKO SIASA KAMA ILIVYO HIVI SASA.

    2. MABALOZI na maofisa wao WAJISHUSHE NA KUTEMBELEA WATU WAO. MFANO BALOZI APANGE ZIARA ZA KUTEMBELEA MAJIMBO MBALI MABALI KWA MZUNGO AU VYUO VYENYE WANAFUNZI NA KUFANYA MAKONGAMANO YA KISOMI BILA ITIKADI ZA SIASA.

    3.MABALOZI WASHIRIKIANE NA WABEBA MABOX SI WAFANYABISHARA WAKUBWA TU WANAOKUJA UGENINI HUKU KUENDELEZA BIASHARA ZAO. WAWAKUZE HAWA WABEBA MABOX WAJIENDELEZA NAKUAPTA KIPATO KWANI WENGI HIZI WATAZILETA NYUMBANI KWA AJILI YA FAMILIA ZAO.

    4.MABALOZI WAWATAFUTIE AJIRA NA SHUEL WATANZANIA ILI NAO WAJE KUVUNA ULAYA WARUDISHE AFRIKA. MATANGAZO YA AJIRA/ELIMU YAFIKISHWE HUKO NYUMBANI NA WAJITAHIDI KUHAKIKISHA WATANZANIA WENGI SANA WANAPATA HIZO NAFASI SI NDUGU ZAO TU. HUKU AJIRA ZINATANGAZWA KILA SIKU LAKINI HUKO NYMABNI TAARIFA HAZIFIKI NA WALA MABALOZI HAWAWEZESHI ZIFIKE. they can do some thing

    5. MFUMO WA UBALOZI TUIORITHI UBADILIKE ILI UWE WA TIJA. UTAHSANGAA UNAPOKUWA HUKU NA KUONA MAENDELEO YA HUKU. MTU UNAJIULIZA HIVI HAKUNA WATU WENYE UWEZO WA KUAMSHA HISIA ZA MAENDELEO KWA KUIGA HUKU? HAO MABALOZI WANAFANYA NINI? MFANO MZURI ANGALI MISAADA INAYOTOLEWA KWANCHI YETU. MINGI KAMA SI YOTE NI SERVICE ORIENTED AMBAYO DAIMA DUMU HAILETI MAENDELEO ENDELEVU ZAIDI YA KULIWA TU. KINACHOHITAJIKA NI MISAADA YA KUWEZESHA UZALISHAJI HALISI MFANO MIUNDO MBINU.

    NITATOA MFANO; nasikia PM wa norway yuko huko na ametoa hela za msaada. jiulize alichosaidia. eti misitu sijui kupanda miti and the like. huyu alipaswa asaidie ujenzi wa barabara fulani tena si vibarabara bali hizi kubwa za kuunganisha mikoa. pamoja na priority zao kabla ya kuamua wasidie nini naamini mabalozi wetu wengeweza ku-coordinate vyema ikaja misaada ya maana na sio ile ya kuuwa mbu ya akina Mh. Bush. nadhani tunaweza kupanda miti na kuuwa mbu bila Bush na Mnorway. lakini ni vigumu kujenga miundo mbinu yetu. ahhhhh samahani labda nimetoka nje ya topic

    In short mabalozi hawafanyi kazi zao.

    ReplyDelete
  23. Kutojiunga au kujitambulisha kwa wa Tanzania inatokana na sababu mbali mbali.Kwanza vyama hivi zimekuwa viki tuhumiwa na Ubadhilifu wa pesa hasa kwa upande wa UK kutokana na ukali wa Maisha uliopindukia.Pia Balozi zetu kushindwa kuwa za msaada kwa Wabongo.Kama unashida ni bora uende balozi ya Kenya au Uganda kuliko ubalozi wa Tanzania.MUDA MWINGI BALOZI ANAPIGA KAMPENI NA KUENEZA ITIKADI ZA CCM.
    Sababu nyingine ni kama wengi wao ni warundi au wasomali kwa makaratisi,lakini hii haiwanyimi nafasi ya kutambulika kama watanzania.Ila wakifiwa basi jumuia za kisomali huwa zinawafuata ili kutoa misaada lakini JAMAA huingia mitini kwani kisomali hakipandi na huogopa kulipotiwa.
    MWISHO WA YOTE UWE NA MAKARATASI AU USIWE NAYO- BADO UNA HAKI YA KUJIANDIKAISHA UBALOZINI AU KWENYE VYAMA KWANI UBALOZI HAUSIKI NA STATUS YA MTU.

    ReplyDelete
  24. TATIZO MIMI NAONA JUMUIYA AMBAYO INAJITANGAZA SANA NI YA WANA CCM KWA HAPA UK. JE HAIWEZEKANI KUANZISHA JUMUIYA YA WATZ BILA KUJALI ITIKADI ZAO? SIO KILA MTU NI ANASHABIKIA CCM. BORA KUWA NA JUMUIYA ISIYOFUNGAMANA UPANDE WOWOTE..
    PILI, BALOZI ZETU NJE NI CHACHE NDIO WAJIBIKAJI. NYINGINE KWA KWELI HATA UKIWA NA SHIDA NI USUMBUFU MTINDO MMOJA, SASA MOYO WA KUJIANDIKISHA UBALOZINI UTATOKA WAPI, WAKATI UWAJIBIKAJI KWENYE HIZO BALOZI NI MBOVU. HALAFU HATA WATU WA MATAIFA MENGINE HULALAMIKIA SANA UTENDAJI KAZI WA BALOZI ZETU..

    ReplyDelete
  25. kwasababu wengi wao wamechenji asili yao na kusema kua wametokea somalia , burundi na ruanda .sasa wanaogopa hayo yasije yakamuharibia mtu maisha yake akarudishwa kwenye mgao wa umeme na kubeba maji kwa ndoo

    ReplyDelete
  26. The answer is simple Michuzi, thanks for raising the question at the first place, may be it is a start of a spirited dialogue for the benefit of us all.

    This is a simple answer to your question. NO NEED, residing countries, OFFER MORE than enlisting your name with GOVERNMENT BAZAAR- WHY REGISTERING??. Until there is a fundamental change, within those apparatus for the benefits of ALL TANZANIANS with clear outlook and benefits, then people will start scrambling to enlist themselves, but SO FAR IT IS A NO NO..

    I give you an example, IRISH IMMIGRANTS no matter how aliens, illegals you might call them in US and other part of the world, they consider them as their own, the government fight for their rights, by fighting for them in parliament sessions back home and lobbying the government officials, i.e SENATORS, current and presiding presidents to recognize them. Do you get the point.

    So far, this isnot happening with Tanzania government. They are left to rot, Yes they come in these countries to look for better future, for themselves and for the benefits of their offspings, but when it come to a simple issue like changing a passport it is a problematic. When it comes to dual citizenship it is again a problem, when it comes to help those in need, you are left to rot, when it comes to understand their need, your are left on your own to fight your own battle. There is no government official who came to UK, and even dare to ask those who are aliens/illegals to come foward and being recognised by the government. thats a NO, to an answer for that.
    No matter how illegals they may sound, they get more protection from residing countries than their own. That also would answer your question. They can achieve more getting education, healthcare, yes clean water, and many more benefits, than their mother countries, therefore a question will rise again WHY REGISTERING? probably somebody can sell that idea to many of us.

    BENEFITS - THE GOVERNMENT SHOULD RECOGNIZE AND TAP INTO IT.

    Aliens / illegals and legals citizen, count to 0.2 Billions US dollars of Tanzania Economy, the number keeps increasing. Therefore, people are sending more to Tanzania than ever before, but sluggish government fail to tap on that economy boost. INSTEAD you get people like CHENGE, taking them out of the country and shipping them oversea. Is that a way to win a trust. DIASPORA are investing more and more back home, than ever before, in construction and businesses, which provides tax and job for the jobless. All these comming from illegals and not subsidies from government, until the government realise that, then IT IS NO NO to enlist, CHINA, NIGERIA, GHANA, PHILIPINES, MEXICO, and the list goes on and on. THEY DO REALIZE THAT TREND, and they have at most appreciations of their legal and illegal citizens of their country.

    Until the government changed its attitude towards that, then there is a optimistic of change of mindset of many diaspora.


    God bless Tanzania.



    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  27. Michu unaweza kusema kuchafua hali ya hewa lkn siyo...check kama ukerewe huyo balozi dili zake ni kuongea na kina tatiana na kuhudhulia maasherehe na kuimarisha chama tawala huko nje...mambo ya maana hawashugulikii...kwa ufupi wapo kisiasa zaidi kuliko jukum zima la ubarozi.
    Kuhusu uwanachama wa jumuiya naona ni mambo ya maslahi binafsi japo sometime huwa inasave incase unakufa na unahitaji kurudi home....ni issue kwa kweli ila wabongo tunahitaji ushirikiano

    ReplyDelete
  28. MICHUZI HIZI BAROZO ZETU HAZINA MSAADA WOWOTE ZAIDI YA ROHOMBAYA ETI UNATAKA PSS AMBUKILE ANAKUULIZA UMEKUJA VIPI HAPA NAANAKUONA UNAYO PSS YA ZAMANI KUNA MWENZETU KAPIGWA NA WATOTO WAKIZUNGU LAKINI UBAROZI UMESHINDWA KUMSAIDIA WAKO WENGINE MAGEREZANI HAKUNA MSAADA WOWOTE ANGALIA WENZETU WAAZUNGU RAIA WAO HATA KAMA KAUWA BONGO WATAAKIKISHA HATA FUNGWA HUKO LAZIMA ALETWE KWAO KWAIO KWANGU HAKUNAUMUIMU WOWOTE WANDELEE NA FITIZAO TU

    ReplyDelete
  29. Kaka nashukuru kwa kuibua haya maswali. Mimi binafsi ni mwanafunzi na sijajiandikisha kwenye chama wala ubalozi.

    Swali #1 - Nafahamu kuwa kuna vyama, hapa nilipo mimi kuna vyama vingi sana kwa mtindo wa blogs, sielewi kipi ni kipi, vyote vinatoa taarifa kuhusu tanzania, sherehe za muungano, mwaka mpya, nk. Kwa kifupi sielewi shughuli za hivi vyama ni nini, kama taarifa, basi naingia kwenye blogs najisomea, naendelea na yangu. Hamna mahala panapoeleza shughuli zao, wala wanahitaji kutambua kama nipo, yaani nijiandikishe. Mi naviona kama magazeti tando tu.

    Swali #2 - Sababu kubwa ni utaratibu mzima wa kujiandikisha.

    Swali #3 - Ufumbuzi wa swali la #2 ninavyoona, balozi kwa kutumia mitandao yao wangeweka utaatibu rahisi kwa kujiandikisha(kwa mfano kujiandikisha online). Pili balozi ziweke maelezo bayana ya sababu na umuhimu wa watanzania kujiandikia maana wachangiaji wengi wameonesha wasiwasi wa kutoa taarifa zao. Kwa #1, Sisi wanafunzi tunaokuja huku, kitu tunachokifahamu ni balozi zetu, hivyo tungetambulishwa kwenye vyama rasmi vilivyo kwenye nchi/ states tunazoishi. Nina maana kwenye mtandao wa balozi kungekuwa na links za vyama rasmi, na hivyo vyama viwe na mitandao rasmi yenye taratibu rahisi za kujiandikisha na zinazosimamiwa na watu serious. Ni hayo tu.

    ReplyDelete
  30. Michuzi, I can only speak for myself. I have been in the UK of an on for over 40 years spent some in TZ during my schooling etc. Back in the 80s TZs in the UK tulikuwa united regardless of umekuja kufanya nini au background yako. As the numbers grew things started to change matabaka yakaanza. This whole thing was not helped having ubalozi ambao haukuwa na msaada wowote unless you knew somebody. Obviously this is changing but will take time to regain TZs in the UK's confidence.
    TZUK - I am noot familiar with perhaps wakiweka katiba, lengo na madhumuni yao wazi na watu wakafanya evaluation watapata wanachama.
    It always seems that walengwa katika jumuia kwenye maswala haya huwa ni watu wa aina fulani nasio the normal TZ mlalahoi ambae kwa njia moja au nyingine ameweza kufika UK .....
    Hao wanaudai kujilipua nk wanaongea pumba. Maana utamuondoa mbongo Bongo lakini Ubongo ni pale pale.....
    Thanks,
    Mzawa wa UK (Mkulia wa Bongo na UK)

    ReplyDelete
  31. Michuzi hii nzuri!
    We unafahamu hata nyumbani ukienda maofisi mengine ya serikali kwa huduma ilivyo hovyo. watu wanakuvutia midomo wakati ni wajibu wao. Hata police ukienda mpaka utoa pesa ndio wawe sreious hata kama unaripoti nyanya yako kauawa.
    balozi zetu huku ndio balaa. wfanyakazi wenyewe wa balozi wanahangaika tu hamna lolote. Ni ile tu kwamba wanaishi ulaya. Ubalozi wa tanzania Scandinavia unajua uko sweden. Unahudumia nchi kibao za huku. Sasa kama uko nchi nyingine ya scandinavia unajaribu kutuma hata email. Jamaa hawajibu wala hawana habari. Ukipiga simu unatifuliwa na majibu yanayoleta karaha vibaya. Nakumbuka wakati passport zilipobadiliswa watanzania wengi walifanya bidii kupatiwa mpya kutoka ubalozi. Basi jamaa wa ubalozi wakaona deal wakaanza kuweka gharama za uwongo. Walitudanganya gharama za malipo ya passport na baadae tulipogundua malipo halali, tulimfata balazi wetu stockholm, Sweden aturudishie pesa zatu. Ilikuwa balaa manaake walikuwa wameshakula cha juu (kama wanavyoita vijana).
    Nilidhani na ubalozi wetu scandinavia kumbe ni kila mahali. Hawa watendaji wa ubalozini wanakatisha tamaa watu kutafuta huduma hata kujiandikisha. Nilijisajili kwenye nett kwnai kunaform lakini hamna lolote.

    ReplyDelete
  32. Hivi Michuzi, huo ubalozi umejuaje kuhusiana na hizo takwimu za asilimia 13, au manono ya kuborongwa na watu, tupe link wapi umepapata hiyo. kama serikali inashindwa kujua nani waziri fisadi na asiye fisadi, itaweza kuweka twakimu.Jengine, kwa nini watu wajiandikishe ? Hao ambao wamekimbia hiyo nchi kwa manufaa ambayo wao wenyewe binafsi, sasa turudi kwenye shimo tena kwa misingi gani, hujafafanua ni vipi watu wajiandikishe kwa sababu gani ? Kwani kuna kujiandikisha na kuna faida ? faida ni ? na ?..

    MZAMIAJI- and proud.

    ReplyDelete
  33. Michuzi, wewe kwa kuwa unakuja na kuondoka nadhani hujakosea kuuliza, lakini balozi zetu hazina msaada wowote, bora kukosa ubalozi. Mimi nilisoma nchi fulani, tukaenda ubalozi kuomba watusaidie kupata ufumbuzi wa kusafirisha mizigo ya ziada ya vitabu, wakagoma matokeo yake tulivitupa uwanja wa ndege. Nipo hapa UK masomoni na vis ayngu halali na siendi ubalozini, wasumbufu tu hawana msaada. Kuhusu hizi jumuia, wewe Michuzi chimbuko lake hulijui. Ni kwamba, hapa mnapoanzisha jumuia kama hiyo, Serilkali ua UK inaipa fedha ya kuiendesha (Minority Support) sasa watu wanaokuwa mle kwenye jumuia wanagombana sana hata maana yake inakosekana. Naweza kukupa mifano ya jumuia zinazogombania hizo supports, sasa kwanini tuingie kwenye matatizo yasiokuwa ya msingi ya kufanya jumuia kubwa wakati watu wana interest zao. Mimi ubalozi siendi, jumuia sijiungi. Mwisho Michuzi acha vitisho vya watu wanapotaka kutoa dukuduku na kuwaita wanachafua hali ya hewa, kuna watu na akili zao unapo wadhalilisha hivyo, unawakosea sana.

    ReplyDelete
  34. Hakuna chochote tulichoona hata baada ya kujiandikisha. Hatuhusishwi kwa chochote. Wana physical address na za barua pepe. Kwa kifupi hakuna msaada wowote

    ReplyDelete
  35. Bro Michu mambo vipi? This is my opinion...
    Kila jamii hukua kimtazamo, kiupeo na kimaendeleo kwa kasi tofauti na jamii nyingine. Jamii za waTanzania nje ya Bongo zipo tofauti sana na Wakenya, Waganda, Wanigeria n.k. kwa wingi na how organised they are, nisingependa kujadili kwa undani hili, but...

    Swali la kwa nini diaspora yetu haipendi kuwa organised na kutambulika na mamlaka za nyumbani linaweza kuwa na majibu mengi,ya msingi na mengine ya labda ya kijinga tu. Kwa taarifa tu ni kwamba sasa Watanzania wanapevuka kiupeo na kimtazamo,ndio maana vitu kama dual citizenship na ushirikishwaji wa diaspora zetu yanazungumzwa sana kwenye jamii kupitia media na hata moja kwa moja kama hivi kwako Bro Misupu. Nadhani tuna muda mchache sana sasa Wabongo wataanza kupiga kura wakiwa huko ughaibuni waliko, kwa hiyo halitakuwa suala la kusubiri uwakilishwe na wale waliopo nyumbani. Why do you think kuna chama/vyama vinahangaika kila kukicha kufungua matawi huko ughaibuni kama tunavyoona kwenye blog hii? Inabidi tujiandae kuwa jamii iliyopevuka. Kujiandikisha na kutambulika ni muhimu kiusalama na kiutambulisho kama Watanzania. Bongo kila muda tunaona balozi zinafungwa ili wahakiki raia wa nchi zao, do you think they are stupid? Hapana! Hebu tuamke sasa jamani...

    Nuff luv wazeya!
    Mbongo King'ang'anizi.

    ReplyDelete
  36. Thanks kwa swali zuri sanaa.
    Kwanza jiulize ni vipi makada wa CCM wote ni Mafisadi?.Viongozi wote waliopo ndani ya CCM kwa njia moja au nyingine ni MAFISADI.
    Watanzania wengi walio nje wanalijua hili na ndo chanjo kikubwa cha kusababisha watanzania wengi kutokuwa na imani na nchi yaoo kwani viongozi wote hawafai.So ni vipi mimi au mtanzania mwingine ajishirikishe na viongozi ambao ni chanzo cha kukimbia bongo.Bongo ni kwetu so inabidi kuungana na kuangalia ni vipi tutajijenga ila watu wame loose hope since uongozi ni huo huo.hata mabalozi,jumuiya and so on.Bro misupu watanzania ni wapole ila si wajinga.

    najua huta weka ila ukisoma mwenyewe yatosha

    ReplyDelete
  37. MIMI BINAFSI ALIYEJIRIPUA SIMLAUMU NI MAISHA YAKE NA KIMPANGO WAKE, HATA MIE INGEKUWA VIDOLE HAKUNA NINGEJIRIPUWA KIRWANDA KISOMALI VYOVYOTE WACHA BINADAMU AISHI ANAVYOONA ATAFANIKIWA WACHENI MAJUNGU, TUKIJA KUHUSU KUJIANDIKISHA SASA, 1. KUNA JAMAAA KASEMA ETI WATU HAWAJIANDIKISHI SABABAU WANAJITENGA NA WABONGO SI KWELI. 2. BALOZI YA TANZANIA HATA UKIJIANDIKISHA HAIMJALI MTU YOYOTE. 3. TANZANIA BALOZI YAKE ENGLAND HAPO LONDON MPAKA AKITEMBELEWA NA SERIKALI YAKE NDIO WANAJIFANYA KUFANYA KAZI YAO. 4. SIJAWAHI KUSIKIA BALOZI YA TANZANIA INASAIDIA MCHANGO WOWOTE WA MAZISHI HAPA HAPA UK WALA KUSAFIRISHA ZAIDI WA JUMUIYA TU YA WATANZANIA HUMU HUMU UK. 5. UKIENDA UBALOZINI MAMBO YAO NI KAMA TUK KWETU TANZANIA UTAAMBIWA NJOO KESHO KUWA NJOO LINI SUBIRI SAA KAMA 1 NA NUSU MZUNGU AKIJA AKISHATOA DOLA ZAKE WANAMPA ANACHOTAKA SASA NDIO TABIA GANI HIYO? KAMATI ZA WATANZANIA MITAANI ENGLAND YANASAIDIANA KULIKO HATA HIYO BALOZI YA WATANZANIA UK. TENA WATANZANIA KAMATI ZAO UK WAMEANZA KUPIGA KELELE UGIRIKI WAWEKEWE KIBALOZI HUONI KAMA WANAJALI KULIKO SERIKALI YA TANZANIA NA BALOZI YAO CHAFU LONDON NAPOSEMA CHAFU SIO UCHAFU WA JENGO VUMBI NI UCHAFU WA TABIA.

    ReplyDelete
  38. WEWE ALIKULIPIA NANI TIKETI YA DAR - LONDON? MBONA UNAWAONEA HURUMA SANA WA UBALAOZI WATU HAWAWAGILII? WELL, KILA MTU ANACHOMA MUHOGO WAKE, KUANZIA CHENGE, MIMI KUJILIPUA NI BORA KULIKO EPA,SIWAINGILII NYIE MATAWI YA JUU HIVYO TUACHENI DILINI NA EPA KWANZA.

    ReplyDelete
  39. wewe dizzy umeshindwa kujiripuwa huna lolote wamekuwahi vidole tu. pole wewe sema tu hao wanyarwanda na wasomali wa uongo watakusaidia sio kuwaponda umejiandikisha ubalozi wa tanzania, dizzy sababu wapate kukugongea passport yako mapema wewe bongo unaitaja tu kwenda hujaenda unafikiri ndege bus lile unaenda tu mikoani?. wacha kuwaponda wenzako fanya yaliokupeleka mungu atakusaidia. wacha kila binadamu atafute maisha kwa urahisi anauuona dizzy wewe nenda kajiandikishe kama ukifa watakupeleka tanzania kwa pesa zao sijui ila hao hao warwanda na wasomali watakusaidia pesa za mazishi sababu mungu anasema wacha majungu anayekuzika hummjui ungesema tu watanzania tujiandikisheni sio kusema watanzania wanajiripuwa hawana mpango? hao hao ndio siku watakusaidiak uliko hiyo balozi. na ndio washanipa kibali uwengereza cha kuishi na tanzania mbona naenda tu namshukuru mungu.

    ReplyDelete
  40. kaka michu kwanza pole kwa kazi! tatizo kaka michu kwanza hakuna publicity ya huo utaratibu wa kujiandikisha au kujisajili sijui mimi niko huku ughaibuni karibu miaka 10 sasa sijawahi kusikia au kuona tangazo kuwa wabongo wanahitajika kwenda kujisajili ndio nasoma humu leo sasa wewe kaka michu umeshafika huku ughaibuni na unajuwa umbali wa sehemu moja kwenda nyingine sasa hizo imformation kama zinabaniwa au ndio wanapeana wenyewe kwa wenyewe watoto na vigogo wenyewe sisi kina kajamba nani tuliostrugle wenyewe kuja huku hizo habari zitatufikia kweli? not only that ukishajisajili ndio ukifariki ubalozi utakusafirisha? au unapata advantage gani au just kujulikana wabongo wangapi wako ughaibuni? kwa sababu nimeshaona wabongo kibao hawajajisajiri wakifikwa na umauti watu wanachanga na wanasafirishwa na nimeshaona wabongo kibao wamejisajiri na wakifikwa na umauti nao wanachangiwa wanasafirishwa lakini sio ubalozi unawasafirisha eti kwa sababu wamejisajili sasa whats the difference kaka michu? na mbaya kabisa kuna kijana mbongo alipata matatizo kuna kipindi fulani serikali ya hapa ughaibuni ikaonekana inapuuzia tatizo lile wabongo wakawasiliana na balozi wetu kutusaidia hili swala balozi akaahidi kulifuatilia lakini karibu mwaka wa pili huu sasa jiii hakuna jibu wala nini sasa whats proud being mbongo? i think its better for me to proud myself by showing my bongo passport than being registered for what benefit kaka michu, nadhani utakuwa umenipata point yangu kaka michu. ok kazi njema kaka

    ReplyDelete
  41. Mimi jamani sijawahi kuandika humu ila leo imenibidi,

    MICHUZI HUKU KUNA FITNA, MAJUNGUUUUUU SANA, YAANI HUO UMOJA WAO UKIINGIA NDIYO KAMA CHAMA, MI HATASIKU MOJA HAWATA NIONA KWAKWELI

    Oooh, UMEMUONA SIKU HIZI,KABADILIKA HUYO,hizo ndo story zenyewe huko, ukienda tu, umeshaanzisha topic mpya,

    MWEEE WABONGO WANA MAJUNGU SANA JAMANI

    ReplyDelete
  42. Bwana michuzi watu haendi ubalozi kujiandikisha kwa kuwa hakuna msaada wowote watapata huko, ukizingatia kuwa kuna baadhi hadi leo wanalilia passport zao (Angalia post zako zilizopita).
    Watu hawajiungi na vyama kwa kuwa navyo vimeundwa kuwaliza tu, kumbuka post zako zilizopita kuhusu watu walochangishwa pesa Washington, DC. Hatima yao ipo vipi sasa? Kuna majibu yeyote wamepewa au kurejeshewa fedha zao?
    Ina maana gani kwenda kujiunga na chama ukijua muda si mrefu tu utaumizwa kwa namna moja au nyingine, kama si kwenda kujiongezea maumivu ya kichwa? Ukichukulia wengine wanaishi kimtindo huku.

    Ukiritimba ubalozini ndo sababu watu hata hawajisumbui kutia timu huko. Na kibaya zaidi watu wanakuja huku na picha(experience) walizonazo juu ya huduma katika ofisi za serikali TZ. Hapo tu wanakoma, wanaamua kufanya shuguli zao za kila siku. Wakipatwa na shidwa wankusanyana, wanachangishana, wanasaidiana wenyewe kwa wenyewe siku zinakwenda. Nini kwenda kujitafutia usumbufu ubalozini?

    ReplyDelete
  43. Issa Michuzi vizuri imekuja mjadala kama huu, mie nakubaliana na jamaa wa kwanza ni kweli ukipiga simu mpokeaji anaona kama unamsumbuwa. ukienda wale wakubwa wote wamejichimbia ndani. waliojiripuwa wacha wajiripue kila mtu na life yake. Balozi ya Tanzania UK 1. Wanajali anayeenda kumpa dola watalii na wafanya biashara kwenda Tanzania kuliko matatizo ya mtanzania.

    2. Balozi Ukisema Asilimia 13 na uwakika hata 7 asilimia haifiki ila ni sensa ya uongo hakuna kitu hicho.

    3 Balozi ya Tanzania hawana hata Website Update za news ya kuhusiana itakuwaje sheria mpya za balozi za tanzania au nakosea jamani bora ISSA MICHUZI ana BLog hata Blog hawana.

    4 Tanzania hizo asilimia labda wamezipata baada ya watanzania kutaka passport zao mpya na wengine hata hawajui kama zimefika mie mpaka nimeona jina langu kwenye Blog Ya mtu. hapo ushawalipa pesa chungu mbovu wanapenda pesa sana ila likitokea tatizo hawakusaidie haina haja kujiandikisha nao kabisaa.

    Balozi ya Tanzania UK plz anzisheni website yenu tujue kinachoendelea huko.

    ReplyDelete
  44. Issa michuzi Next topic plz delete hii topic. Maana ushapa Asilimia kubwa wameona kwamba Balozi za tanzania nje hazina mpango bora somalia hawana balozi ndio tunaitumia hahaha. bye.

    ReplyDelete
  45. HATUJINDIKISHI MAANA TUNAOGOPA KUKOPWA NA SERIKALI YETU MAANA UKISHAJIANDIKISHA TU WAKISHAONA WATANZANIA NI WENGI HUKO WATAANZA MAMBO YA MICHANGO KWAHIYO KIUFUPI TU TUNAOGOPA KUKOPWA NA RICHMOND

    ReplyDelete
  46. MIMI MWENYEWE NIKO HAPA DC NIMEOZA SASA NINGEENDA UBALOZI SASA HIVI INGEKUWA NOMA ILE MBAYA HAPA DUNIANI TUMEKUJA KUTAFUTA MAISHA NDUGU ZANGU KWA HIYO KILA MTU ANA SIRI YAKE YA MAISHA.its better to be safe

    ReplyDelete
  47. Mimi nasoma uholanzi, ubalozi wa nchi za schengen ni Brussels Belgium. Shida ipo sana, tena kipindi hicho hicho cha kubadili passport, mtu unatoka nchi nyengine, licha ya msaa tofauti na umbali, humjui mtu, unawahi kwenda ubalozini kwkao, kupiga simu kupokea kazi, wakipokea hakunamajibu yeyote ya maana, haya umefika ulalozini yaani yule mama secretary kama hakuoni, tulikalishwa kama masaa mawili hakuna anachosema yupo kweney simu tu na rafiki yake. Mpk balozi kashuka chini katukuta tumekaa, anauliza mmefika sangapi kutajia anshanga mbona sijambiw akama kuna watu chini wapo, yule dada wacha aanze kudanganya eti tumefika dka 10 tu zilizopita. Ukweli wanauzii tena kwa watanzania wenye waume au wake waupe basi ndo wanaongezewa dozii hata kusikilizwa hawasikilizwi wanaambia si mchukue pasi zao mnataka nini za watanzania

    ReplyDelete
  48. mnanichanganya mnajua..kujilipua ndo nini?sisi tuliopo bongo hatuelewi

    ReplyDelete
  49. Shukran sana Bro Michu kwa kuanzisha gumzo hili. Mengi yamesemwa na Watanzania wenzangu na yote ni kweli kabisa si kwamba labda watu wana majungu la hasha hiyo ni hali halisi ya balozi zetu za kitanzania. Inasikitisha sana na inaumiza ndo maana Watanzania hatufiki kwa vitu kama hivyo. Kuja kwetu nchi za wenzetu tumejifunza mengi kutokana na service wanazozitoa na tofauti ni kubwa sana japokuwa nao wanamapungufu yao ya kibinaadamu. Wenzetu wanapokuwa na wito wa jambo fulani basi hawasiti kuitika.

    Kakaangu Michuzi juu ya watu kutoa madukuduku kama hivi na wanasoma lakini usitegemee any changes it's like mazungumzo baada ya habari. Mshipa wala hauwagongi sababu yao yanawaendea. Lakini wakumbuke huo sio ubinaAdamu wala uungwana wanatakiwa watimize na wawajibike kwa yale yaliyowaleta ubalozini hapo na si kwa maslahi yao binafsi. Ubalozi umegeuka kijiwe cha Juma Pinto na Suzan Mzee kufanyia dili zao. Aibu Aibu Aibu. Msitufanye vipofu kiasi hicho tuna macho na tuna akili zetu timamu. MNYONGE MNYONGENI LAKINI HAKI YAKE MPENI.

    Ni mimi Moyouchungu

    ReplyDelete
  50. YOTE TISA BABAKE WE MICHUZI HUJUI KINACHOENDELEA HAPA UK.
    WAAFRIKA NA WABONGO WENYE VITABU VYA UK AMBAO WAMEJILIPUA WANAPOENDA UBALOZINI KUOMBA VISA YA KWENDA BONGO PALE UBALOZINI NDIPO UTAPOTAMBUA JINSI GANI HAWA JAMAA WALIVYO NA ROHO MBAYA.
    AKIENDA MZUNGU NA GAMBA LAKE AMBALO NI SAWA NA LAKO (BRIT PASS) ATAAMBIWA ARUDI SAA TISA KUPEWA VISA YAKE; LAKINI KWA MWEUSI ATAPIGWA KALENDA NA ATAAMBIWA VIZA YAKE INATOKA BONGO!
    UKIWAKUTA WANAFUNZI WANAOFATILIA PASI ZAO UTAZIMIA. WAPO WALIOSOTA HADI MWAKA HUKU AKISOMA NA KUISHI KWA MASHAKA.
    HAO WANAOFANIKIWA KUPATA VIBALI VYA KUISHI HAWANA VIBALI VYA KUFANYA KAZI NA KUPATA PAUNDI NA NDIPO WANAPOANZISHA ILI WAINGIZE RUZUKU.
    KWA HIYO MLALALHOI AMBAYE HANA "NDUGU" UBALOZINI, HUONA BORA AJIWASHE NA KUPATA KIBALI AMBACHO SIO KITAMWEZESHA KUISHI BALI HATA KUFANYA KAZI NA KUPATA FEDHA.
    USISHANGAE WATU KUJIFANYA KUTUMIA MAMILIONI NA FEDHA ETI KWA KUITANGAZA BONGO KWA NJIA YA UTALII KUPITIA KWENYE MABASI TENA YA LONDON!
    HIVI HUKO LONDON KUNA WATU WA MAKABILA MANGAPI WENYE KUTAKA KWENDA BONGO! UTAMTANGAZIA MTURUKI, MSOMALI, WAKOSOVO, WAJAMICA AU WAGIRIKI ETI MT. KILIMANJARO IPO BONGO KWA HIYO NJOONI.
    KWA TARAIFA YAKO WEWE MICHUZI NA WENGINE, WASAFIRI WAKO MIKOANI. WENGI WAISHIO NJE YA LONDON NDIYO WANAOFANYA KAZI NA HUTAFUTA MUDA KWENDA KUJIPUMZISHA KENYA, DUBAI, AFRIKA KUSINI NA KWINGINEKO. LONDON NI ASILIMI NDOGO MNO.
    KAMA BALOZI ANAONA HAKUPATA WATU, SHUGHULI NDIVYO ILIVYO. ASILETE MAMBO YA KIZARAMO HAPA. WATU WANAANGALIA KAZI ZAO NA SIYO KUMFURAHISHA FULANI.
    MIMI NILISHANGAA SANA KUSIKIA SHEIN ANAKUJA UK ETI KUFUNGUA TZ DIASPORA. NA UKUMBUKE HIYO ILIKUWA NI SAFARI JK! AJABU KUBWA.
    YAANI WATU WANAKUFA NJAA, HAKUNA MAJI, HAKUNA UMEME, KIONGOZI WA JUU ANAFUNGA SAFARI KWENDA NCHI ZA ULAYA KUFUNGUA DIASPORA? KUNA TOFAUTI GANI KATI YAKE NA AKINA BALALI, CHENGE, LOWASSA KUTFUJA MALI NA FEDHA ZA UMMA!
    KWA NINI USIWEKE MJADALA WA KWA NINI CHENGE ANADAI MAMILIONI YA FEDHA NI VIJISENTI WAKATI HOSIPITALI HAZINA DAWA, WAALIMU HAWALIPWI MISHAHARA, BARABARA AMBAZO ZIPO CHINI HAZIPITIKI, MIFEREJI YOTE IMEZIBA NA KUSABABISHA MAFURIKO.
    RUSHWA SIYO LAZIMA APOKEE CHENGE PEKE YAKE. HATA WEWE MICHUZI UNAWEZA KUWA MLA RUSHWA NA KUFUNIKA HOJA ZA MAANA KUTUPA MAWAZO YA WALALAHOI KWENYE HOJA ZISIZO NA MSINGI! ETI DIASPORA?
    PIGA, GALAGAZA, UA, MTU ANAPOTAFUTA MAISHA POPOTE PALE INAJULIKANA. HATA WAINGEREZA WENYEWE WANAFAHAMU HILO NA NDIYO MAANA TONY BLAIR ALIWAHI KUMUOMBA BM KUFUNGUA KAMBI YA WASOMALI BONGO.
    KWA NINI? HUJUI KITU MZEE WEWE PANDA NDEGE, VAA SUTI NA FULANA YAKO RUDI BONGO ULE MAISHA MAZURI. BOX SI SAWA NA KUDANDA PALE SALAMANDER KUUZA BWIMBWI AU KUKWAPUA WAZUNGU MALI ZAO. NIMEPITIA HUKO NA NINAJUA UGUMU WAKE. HAPA NI RAHISI MNO KULIKO HUKO.

    ReplyDelete
  51. PROMOTING CCM GHETTOs ABROAD.

    I wouldn't like to see my ambassador affiliate himself/herself with political party, imagine any other political party opening a branch abroad, and the ambassador is asked to officiate the events, he would have his/her head chopped by his/her peers back home, probably loosing his/her job. Summoned back home on the express FLIGHT to bongo, given a library post as his/her demotion. I know they know this. SO WHAT'S THE POINT. I think it is wrong to officiate this event, they should stop doing that, despite being a member of that political party, it is morally incorrect and create a wave of suspicious and animosity on our young democracy within DIASPORA community, Embassy should be for each and everyone and not for one group over the other. May be someone can define Embassy and Ambassador so to speak, and their responsibilities, for the benefit of each of us. My general understanding and interpretation could be different to what is REALLY MEAN by the terminology.

    I can understand Michuzi, you probably only have one side of the story, from those who welcome you while in UK, but if you dare you could have gone to other part of the country get other side of the story, you will probably have fair and balance view.

    Majority of citizen who were denied a chance to better themselves either back home or abroad, they decided to take drastic action by declaring/seeking refuge to the government which seems to care. Until we start caring for our citizens then you will see a mindset CHANGE, but right now people are sticking with the right mind, stereotype, attitude and rightly so, who to blame them.

    People are fighting from the sidelines until they see the real change from within, and they think this is the right thing to do. THEY ARE ONLY DEMANDING A FAIR REPRESENTATION FROM OUR EMBASSY FOR ILLEGALS AND LEGALS-(and thats the job of embassy, don't they know that),and that is the problem. In due respect to Mrs. Maajar promoting this idea, The embassy workers DON'T understand their responsibilities, but themselves. Enough have been said about them. Are they reaching out to these local communities and organization, they are definitely not, i.e. recently we saw A coventry-UK resident who died of intoxication from banned substances(according to police report). yes enough have been said about the story, majority believed, he was involved with drug trafficking into the country. YES IT IS ILLEGAL and shameful act to engage on, but the UK government never at anytime thought of dumping the body, burn him, but instead they pay respect and hand over the body for respectful burials, whatever the circumstance. The Question is DID EMBASSY RICH OUT TO THIS PEOPLE, TO HIS FAMILY, DESPITE BEING ILLEGAL/LEGAL STATUS HE MAY POSSES. the same will be said about TZ-UK, they are only for self indulgence and promotion. WE NEED TO REACH OUT TO PEOPLE LIKE SAID OTHMAN, and others, and thats the bottom line, then we will be able to build a coalition and a sense of belonging to our EMBASSIES across the globe.

    and Finally, I think the ambassador should recruit locals diaspora with credentials(who understand the need of diaspora) and not bring people who are not QUALIFY, and most importantly CAN'T do their job. The staff who are promoted because of their dubious connection, their political affiliation, and not BY MERIT.

    We have a lot of qualified students who fit to do the job, who studied international relations in TOp universities around the world, who worked on international NGOs abroad/home and real qualifiers, but are left and not given that important positions. They are the one who can bring a just change and not mtoto wa fulani, I know fulani, he/she is fulani wa fulani, sorry guys for my french, but that's reality, and people are always suspicious of that system, because of its INEFFECTIVES, AFFILIATION PROBLEM, and THE ATTITUDE WITHIN, are not professional.

    People understand it is a long shot, but we will reach there sometime. It is a hope that worthy fighting and waiting for.

    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  52. mbona huiulizi serikali waloiba Buzwagwi wameishia wapi? au ule umeme feki wa RICHMOND umefikia wapi?
    haya ndiyo MAJUNGU.ukisikia majungu na fitina ndiyo hizo.
    nyie watu mnaokuja kuja na kujifanya tz uk, tz diaspora si mfanye mambo yenu na wala hakuna atakayewaingilia.
    kama kuna mtu kaja na kuzamia au hataki kujiandisha na CCM yenu iliyojaa fitina na ufisadi, ni juu yenu babake.
    kuna hoja ilitolewa kwenye picha za diasproa na muunguja aliyesema mbona watu wengine hawakuwa na taarifa ya mkutano huo?
    jibu alilopata toka kwa mmoja wa mwana DIASPORA-we mshamba hapo juu usilete mambao ua cuf na uzanzibar, siyo kila kitu lazima mfuatwe makwenu?
    hilo ndiyo jibu!
    SWALI LINGINE NI KWAKO MICHUZI;
    SAFARI YAKO YA KWEDA UK, BERLIN ZOTE UMEONEKANA UKIWA UMESHAFIKA HUKO. MBONA HAKUNA HATA MOJA ULIYOSEMA UNAENDA HUKO NA UTAONGOZA NA MAKAMU WA RAIS?
    MBONA HAKUNA MTU ALIYETIA SHAKA JUU YA FITINA HIYO. INA MAANA OFISI NZIMA YA DAILY NEWS UPO WEWE PEKA?
    MPIGA MADONGO

    ReplyDelete
  53. KAkA MICHUZI HUKU MAREKANI TULIKIONA CHA MOTO ENZI ZA BELINDA PALE RECEPTIONIST UBALOZINI/KAMA HUMJUI MTU PALE UTATAABIKA SANA BADALA YA KUSAIDIWA uLIKUWA UNANYANYASWA UTASEMa WEWE SIO MTANZANIA.NILISHUKURU NILIVYOMALIZA SHIDA YANGU YA PASSPORT KWANI ILINIUMA SANA KUONA WATU WA NCHI ZINGINE WANANYENYEKEWA SISI WATANZANIA TUNASUMBULIA HAWANA MSAADA WOWOTe.
    KUHUSU KUJIANDIKISHA WAKATI WA PASIPOTI MPYA ZINATOLEWA WATU WALIANDIKISHWA WOTE NA BALOZI WANAZI INFORMATION ZAO SASA HIO ASILIMIA 13 LABBDA NDIO WATANZANIA WENGINE WAJILIPUA UK MANAKE UBALOZI WANATAKIWA WAWE NA INFO ZA WATZ WOTE WALIO APPLY PASIPOTI MPYA.
    SWALA LA VYAMA VYA WATANZANIA MAJUU NIONESHE KITU GANI WALICHO ACCOMPLISH KINAWEZA KINIFANYA NIJIUNGE NAO ZAIDI YA MIPARTY YAO YA KULEWA NA KUTUKANANA.HIVI VYAMA KAMA VINGEKUWA NA NIA YA KUSAIDIA NYUMBANI BASI HATA VILE VISIMA ALIVYOZINDUA JAY Z TUNGEFANYA WENYEWE.TUNGEKUWA TUNAFA HARAMBEE HELA ZINUNUE MADAWATI wALE WATOTO WA SHULE KIGOGO WASINGEKUWA WANAKAA CHINI.SASA JUZI UMESIKIA CHAMA CHA D/C WATU WAMELIWA HELA ZAO ZA FEE YA NYUMBA ALAFU BADO MTU UNATAKA KUJIUNGA NAO.
    Mdau mhenga

    ReplyDelete
  54. Mimi ni mmoja wa watu ambao wamejiandikisha Ubalozini lakini kunapotekea swala lolote mfano mikutano hakuna anayekujulisha, pia unapokuwa na shida hakuna anayekusaidia sasa kwa muono wangu inawezekana wengi wa watu kama mimi mfano nikilalamika kwa marafiki wenzangu kuhusu mambo hayo na wao ndio wanaona hakuna sababu ya kujiandikisha.

    Kunakipindi kulikuwa na mpango wa kubadilisha passport,nadhani hapo ndio kila raia wa Tanzania walichoka kwani appointment ya kuchukuliwa vidole ilikuwa inachukua miezi 6 japo wengi wa watanzania waliutaarifu ubalozi kwamba viza zao zilikuwa karibu zinakwisha na walikuwa wanaitaji passport zaoharaka iwezekanavyo lakini ubalozi na mpango wao mzima mbovu walishindwa kusaidia watanzania na matkeo yake wengi walipata matatizo na Home Office ya Uk na wengine hata kukataliwa Viza kwa sababu walichelewa kupeleka maombi yao.

    Sasa leo hii ukiniambia nijiandikishe kwenye Jumuiya ya Tanzania ni nini hasa nitapata au msaada gani nitaupata.Wao wanajumuiya wanajali maslai yao lakini sio watanzania wanaoishi ughaibuni.

    Mfano ambao ni wa Kweli kabisa,sasa hivi ninapoongea kuna Mtanzania ambaye alikuwa ni mwanachama wa jumuiya ya watanzania Uk na sasa ni mgonjwa yupo Hospitali University college Hospital Euston, Ubalozi unafahamu na jumuiya pia inafahamu lakini mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja kutoka kwenye hiyo jumuiya au Ubalozini ambao unajua maendeleo yake. Sasa hayo ndio mambo wengi wanaona kwamba hakuna sababu ya kujiunga na jumuiya au kujisajili na ubalozi..........................japo wengine wanasababu zao za msingi nje na hizo nilizozitoa.
    Kimsingi watu wa Jumuiya ni wanafiki na hawanalolote la kuwasaidia watanzania na Ubalozi upo pale kupokea wageni tu na kushughulikia viza za watalii ambao wanakwenda nyumbani kwa maslai yao na Taifa lakini kuhusu watanzania waishio huku kila mtu anajua lake na hataki kusikia swala la jumuiya au ubalozi.

    Popo

    ReplyDelete
  55. KWA KWELI TUNAPENDA KUWA KARIBU NA BALOZI ZETU,LKN KUNA MICHOSHO MINGI AMBAYO INAKATISHA TAMAA NA MTU UNAAMUA KUWAKALIA MBALI.KUNA DADA MKENYA HAPO UBALOZINI STOCKHOLM.HUYU DADA KWA KWELI HUWA SIELEWI NINI HASA KWAKE NI KIZURI.KIMOMBO NDIO LUGHA YA DUNIA,NAKUBALI HILO.SASA HUYU DADA YEYE ATAKUONGELESHA TU HICHO KIMOMBO CHAKE,HATA KM UTAMJIBU KWA KISWAHILI.SASA KUNA SIKU NIKAPIGA,AKALETA HIZO YES,YES ZAKE MZUNGU KALA FENESI,NA MIMI NIKAAMUA SIKU ILE NIKUMBUKIE ENZI ZILE ZA SHULE"SPEAK ENGLISH" SASA ETI NAMSIKIA ANANIJIBU "SUBIRI" NIKAMSHANGAA SANA HUYU DADA WA KIBAKI KULIKONI TENA NA WEWE MTU NGELI NDIO NYUMBANI KWAKE!! SASA KAKA MISUPU KITU KM HICHO TU MTU TAYARI AMESHAKUKERA.HALAFU WANA MAJIBU YA AJABU MPK MTU UNASHANGAA UFANISI WAKE WA KAZI.MIAKA YA NYUMA PASS ZILIKUWA ZINABADILISHWA.MTU UNAPIGA SIMU UBALOZINI KUULIZIA UTARATIBU,ETI UNAJIBIWA"MAMA PASS HAZIBADILISHWI KM VITANDA" HIVI KWELI MTU KAISHIWA NA MSAMIATI KABISA NA HAJUI KABISA MATUMIZI YA LUGHA NDIO AJIBU NAMNA HIYO!! MICHOSHO KAKA YANGU MICHUZI UBALOZINI.

    ReplyDelete
  56. TUENDE UBALOZINI KUJIANDIKISHA ILI IWAJE?KILA MTU NA LAKE KAKA MICHUZI.

    EVERY MAN FOR HIMSELF AND GOD FOR US ALL..MAISHA KOMBOLELA,BUTUA UOKOE WENZIO.

    ReplyDelete
  57. Asante Sana Kaka michuzi Kwa hii ya leo bila kupoteza wakati ni hivi hao watu wanaofanya kazi ubalozini kama vile ubalozi wa uk ,spain,marekani,ugiriki,sweden yaani ubalozi wote wa bongo uliokuwapo nje ujerumani wanazotabia za ushamba kama tunavyosema wanaringa wanataka kupewa hongo kubembelezwa na unapiga simu time za kufungua ofisi saa mbili unaomba kuongea na balozi unaambiwa hajafika kazini mambo haya yalileta kasheshe kubwa sana sweden kwa kweli kila ofisi ya balozi za bongo hazina misaada yoyote watu wamechoka kunyanyaswa na hata ukienda na matatizo ya pasi wanakuzungusha vilevile ndio sababu wabongo wengi wana pasi za europer na pia naomba kaka michu peleka ukweli wetu huu mbele wanalipwa mshahara na kufungua ofisi eti tanzania embassy hamna lolote wabongo wanasema ukweli .

    ReplyDelete
  58. Kutokujiunga na jumuiya nadhani ni kwa sababu watu hawajaelezwa na kuelewa umuhimu wa kufanya hivyo...

    kuhusu kujisajili,experience yangu ni inefficiecy ya ubalozi wetu uliopo Ujerumani.Kuna form iko online lakini haijaziki online.
    Mimi nikaamua kuiprint na kuituma kwa posta.
    Sikupata response yoyote.
    Nikapiga simu kuulizia kama wamepata hiyo form...attitude niliyopewa ni kama vile ombaomba amegonga mlango!kwanza nikaulizwa: "sasa unataka nini kama umeshatuma form???kama uliituma basi itakuwa kwenye file"
    sasa kwa design hii kama kungekuwa kuna mwingine pembeni yangu anataka kujisajili sidhani kama angejiingiza katika hekaheka hilo.
    Na mimi pia mpaka sasa sijui kama niko miongoni mwa waliosajiliwa au lah kwa sababu sikupata confirmation.
    nawakilisha...

    ReplyDelete
  59. We endelea kuminya comments zetu, najua hutaki kutoa habari za Pinto kwasababu amekukirimu ulipokuwa huku, TAKRIMA mbaya kaka ila kifupi hao ndiyo wanaohodhi ubalozi waingia wakitoka kwa mapana na marefu. KWANINI WAO WAWEZE WANA NINI NA SISI TUSHINDWE TUNA NINI???????

    ReplyDelete
  60. Nitatolea maoni la ubalozini. Hii ni karne ya ishirini na moja lakini tembelea tovuti za balozi zetu uone kama utaona fomu ya Mtanzania kujiandikisha. Utaratibu wake umekuwa mgumu.
    Utaratibu rahisi ungekuwa hivi. Mtanzania unafika ughaibuni. Unatembelea tovuti ya ubalozi wako katika nchi hiyo na kuipata ile fomu unayoiprinti na kujaza maelezo wanayotaka uyaandikishe ikiwa ni pamoja na namba ya hati ya kusafiria hata picha kama wanazitaka. Unalamba stempu na kuituma barua ile kwa njia ya posta, biashara imeisha.
    Utaratibu rahisi zaidi ungekuwa wa kuzituma hizo fomu online, lakini kwa kujua mambo yetu yanavyoenda kunaweza kuwa na matatizo ya usalama mtandaoni.

    ReplyDelete
  61. KAKA MICHU WATU TUMEKIMBIA NCHI KUWAKIMBIA MAFISADI LAKINI BADO WANATUSARANDIA HUKUHUKU UGHAIBUNI KWA KUTUMIA UFISADI MPYA WA KUANZISHA JUMUIYA ZA KUTUFISADI HUKUHUKU NA WEWE KAKA MICHU WAMEKURAGHAI UNAWAAMINI KUWA NI WATU WEMA HIZO JUMUIYA NI ZA KUTUFISADI TU NA HUKO KUTUREJISTA NI KUTAKA TU KUJUA WANA IDADI YA WATU WANGAPI WA KUWAFISADI HAWAMPATI MTU HUKU! NA KAMA KUJIUZULU NDIO DAWA SIKU HIZI HATA VIBAKA WA MIFUKONI WANGEKUWA WAKISHTUKIWA WANAJIUZULU HADHARANI TU WANAACHIWA HURU KAMA MAFISADI MBONA WOTE TUNGERUDI BONGO KAKA MISUPU

    ReplyDelete
  62. Bwana michuzi kuna nchi nyingine zenye watanzania ambazo wala sio za kuzamia ila hahuna mtu yeyote mwenye nia ya kujiandikisha au kutambulika ubalozini. Hii inatokana na balozi zetu za nje ya nchi kutokuwa na msaa, Hizi ofisi zipo tu kama majina tuuu,hazina msaada wowote sasa mtu huwa anaona ni kupotezea muda.
    Kuhusu hivi vyama ni majina tu bwana michuzi. Huku nje hakuna vyama. Hawa jamaa wanajua wanachokipata,hakuna msaada wowote uwe umejiandikisha au hujajiandikisha.
    Na hata ukiwa umejiandikisha kwenye hivi vyama,utakereka tu majungu,fitina n.k!!!Bora tu kuishi kama mkimbizi!!

    ReplyDelete
  63. michuzi mi naona ungeanza na hili swali "NI ASILIMIA NGAPI WALIOOMBA PASSPORT KUPITIA BALOZI ZAO WAKAZIPATA"
    nadhani jibu lake lingekupa majibu ya maswali unayotafuta na hata usingeyauliza
    Ni kweli bora ukajiandikishe INS/homeland security kuliko ubalozi hata kama unaishi kikwale wanaweza kukusaidia

    ReplyDelete
  64. Kwanza Michuz nikupongeze kwa Uzalendo wako TO HAVE EVER THOUGHT OF EVEN ASKING YOURSELF ABOUT THIS WHOLE THING!Bila shaka baada ya kutopendezwa na jinsi watanzania walivyotawanyika hapo kwa Mama kila mmoja akijali mambo yake tu tofauti kabisa pengine hata wenzetu wakongo wanavyo thamini umoja na ushirikiano miongoni mwao huko ugenini.Kwa kweli tunatia aibu.Lakini chanzo chake ni nini basi?Ni huku huku nyumbani.Hili Michuz ni tatizo la muda mrefu sana.Sababu kubwa ni ULIMBUKENI NA UJINGA miongoni mwa viongozi wetu.Watanzania tumeshindwa kabisa kutambua kwamba dunia hii ni ya ushindani.Tumeshindwa kabisa kujenga sera na utaratibu utakao wawezesha vijana wetu wawe na ujasiri wa kutoka nje ya mipaka yetu wakahangaike na kujitumikisha huko ughaibuni na wakisha chuma mali wawe na malengo ya kutuma utajiri wao huku nyumbani bila ya mizengwe yoyote ili kuijenga nchi yao.Watakao diriki kuleta mali walioichuma huko ughaibuni wawe huru kurejea na kurudi wakati wowote ule hali itakapo ruhusu kufanya vile.Lakini mazingira yaliyo jengeka katika Balozi zetu kwa kipindi kirefu mno ni kikwazo hayo kutendeka na kwa kweli ni kichekesho.Ukianzia na suala la kupata tu ile Passport kwanza ni zengwe.Kupata Passport linachukuliwa kama ni bahati!Ni upendeleo ambao ni mahsusi kwa watu wachache tu wateule.Wengine wasipate fursa ya kutoka nje wakatoa tongotongo na kuuona ulimwengu mwingine unakwendaje.Ilikuwa ni mbinu za makusudi kabisa kuwafanya watanzania wabakie hapahapa nchini na ujinga wao wasije wakajanjaruka na kuanza kuhoji mambo.Tushukuru Mungu ujio wa Televisheni na Internet sasa watanzania wataweza kufuatilia kwa karibu kinacho endelea katika nchi zingine bila ya kulazimika hata kusafiri nchi za nje labda ukitaka mwenyewe.Kutokana na sera hiyo ndiyo maana hata wale walioajiriwa kwenda kushika ofisi zetu za Kibalozi sehemu mbalimbali duniani mara nyingi waliteuliwa kisirisiri tena kwa kujuana au kwa upendeleo mkubwa LAKINI SIYO KWA MASLAHI YA TAIFA.Hil lazima niliseme wazi kabisa atakaye chukia akanywe sumu ya panya!Wengi miongoni mwa maofisa walioteuliwa kwenda katika Balozi zetu za nje hawana sifa wala taaluma za kazi hiyo,dhahiri kutokana na aina yao ya utendaji kazi.Wengi hawajui kuwa Balozi wa Nchi katika nchi ya ugenini maana yake nini na wajibu wake ni nini.Wengi walipelekwa kishemeji tu au kulinda maslahi binafsi ya kujiimarisha zaidi kisiasa hapa nyumbani kwa kuwahamisha wale walio onekana wakorofi.Utashangaa katika Balozi zetu nyingi nchi yetu haitambuliki kwa wengi katika nchi hizo tofauti na wenzetu walivyofanya katika kukuza mahusiano ya kibiashara na utalii.Sisi msisitizo wetu mkubwa ulikuwa katika kuomba misaada zaidi kuliko kuitangaza nchi yetu ili kukuza utalii na biashara hapa nchini kwetu.Balozi akiteuliwa kwenda nchi fulani akifika kule kwanza ataingia kisirisiri hataki asumbuliwe na yeyote.Haoni umuhimu wowote wa kujaribu kuulizia kuna watanzania wangapi wanaoishi huko na wana maisha gani ili ajue atawasaidiaje.Lakini atapenda zaidi kutafuta ni nani aliyekwenda kule 'kihalali'kwa mujibu wa tafsiri zao maofisa wetu wa Balozi za Kitanzania ili aone ni hatua zipi za kuchukua.Badala ya yeye kugeuka BABA MLEZI akawakusanya vijana wake wote ili watambuane na kujenga mashirikiano ya karibu na hatimaye kuweka malengo ya pamoja na kubainisha mikakati ya kuchuma mali na kuituma huku nyumbani ili kuiendeleza nchi yetu,atajikweza na kujitenga aonekane kama yeye ndiye MTANZANIA HALALI NA MWENYE HESHIMA KULIKO WOTE katika nchi ile ya ugenini.Matokeo yake Balozi zetu nyingi zimeshindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo kwa maslahi ya taifa letu.Hadi hii leo Watanzania wanaoishi nchi za nje hawana haki ya kupiga kura kuchagua viongozi wao huku nyumbani,tukiwa tunatimiza miaka isiyopungua 47 toka tupate uhuru.KWANINI HALI HIYO IRUHUSIWE KUWA HIVYO?Hadi hii leo watanzania waliokwenda nchi za nje kwa malengo ya kuchuma mali hawaruhusiwi kuwa na Uraia wa nchi mbili ili waweze kuajiriwa kule kiurahisi au kufanya biashara na kisha iwe rahisi vilevile kwao kuweza kurejea huku nyumbani bila ya vikwazo vyovyote na kisha warudi huko ughaibuni wakaendelee na harakati za kujitafutia maisha.Wakizaa watoto huko nje wawe huru kuwaleta watoto wao huku nyumbani waje wawaone Bibi zao na Babu zao.Hakuna utaratibu wowote utakao watia motisha ya kutuma pesa na mali huku nyumbani ili kufungua miradi ambayo ingetoa ajira kwa vijana wengi hapa nchini.Kwa mfano kwa kutowatoza kodi kwa bidhaa na pesa watakazo tuma huku nyumbani.Balozi zetu nyingi kutokuwa na mtazamo wa kibiashara na ujasiriamali.Zimegeuzwa kama ofisi za Posta zikisubiri mtu aje atumbukize barua kuja Tanzania lakini sio wao watoke na kujitumikisha kwa kuwashirikisha watanzania wote waliopo huko ugenini bila ya kujali nani kaja kufanya nini na kaja kwa usafiri gani.Binadamu tumezaliwa tuhangaike ulimwenguni kote.Siyo kufugana kama Tumbili kwa manufaa ya kibinafsi.Kuwepo kwa hali kama hiyo ndiko kulikowafanya vijana wetu wengi huko ughaibuni wapoteze imani na wawakilishi wao katika Balozi mbalimbali.Akionekana mtu Ubalozini ataonekana kero badala ya kusherehekea mtoto mpotevu amepatikana anahitaji msaada gani,au ushauri gani na kadhalika.Utaulizwa kabila gani,hiyo inakuhusu nini mradi yeye ni mtanzania tosha!Kwa ujumla kwa mtazamo wangu BALOZI ZETU ni DISASTER!zitahitaji kusukwa upya na kuwepo kwa sera mpya kabisa itakayo tuvusha kutoka hapa tulipo ili na sisi tufikie hatua iliyofikiwa na wenzetu nchi zingine.Ulimbukeni,Ujinga,Ubinafsi,Maslahi binafsi ya kujijenga kisiasa,Kuwageuza watanzania mazumbukuku iwe rahisi kuwatawala,ni baadhi tu ya sababu muhimu zilizo zifanya Balozi zetu zishindwe kuliwakilisha Taifa la Tanzania ipasavyo kwa maslahi ya Watanzania wote katika ulimwengu huu wa ushindani mkali!Michuz sababu ni nyingi sana.Hizi chache kwa leo zitatosha ili wengine nao wapanue zaidi mjadala huu.NINI KIFANYIKE ILI KUONDOKANA NA TATIZO HILO?Majibu yake nitayatoa katika extended version muda mfupi ujao baada ya KUVUTA PUMZI kwanza.Asalaaam Aleikoooom!

    ReplyDelete
  65. 1. Watanzania wengi hawana imani na serikali na organs zake.

    2.Watu wako busy kuanzia kubeba box mpaka kufundisha vyuo vikuu.

    3.Ubalozi hauna mpango mzuri wa kujisajili online, kama upo hautangazwi.Pia hamna consulates za kutosha, kujisajili kwa wengi inabidi ufunge safari ndefu au kutuma vitu kwa snail mail.

    4.Watu wengine hawako nchi za watu kihalali na wanahofia balozi zetu, badala ya kututetea kama ilivyo kawaida zitaweza hata kutuchongea.

    5.Ujisajili ili iweje? Waliojisajili hawapati taarifa wala huduma yoyote.

    6.Privacy concerns among some civil libertarians.Mfano UK wanamuogopa Mama Maajar ataanzisha dossier la Watanzania wote wa CUF walioko huko.

    7.Wengine hawataki uwezekano wa usumbufu.

    8.Protest against the Kikwete/CCM administration.

    9.Serikali haiwezi kuwajali Watanzania walioko nje mpaka iwajali walio nyumbani.

    10.Kujisajili ubalozini? Watu washatupa passport katika choo cha ndege wakirudishwa kutoka shamba kubwa kuwa deported "back home" to Jamaica, only to flip some moves out of JFK.Halafu unataka wajisajili ubalozini, unacheza!

    ReplyDelete
  66. Swali zuri.

    Mimi siwezi hata siku moja kwenda kujiandikisha ubalozini. Why nikajiandikishe? Hakuna manufaa yoyote nitakayoyapata kwa kujiandikisha ubalozini.

    Balozi ziko pale ili kulinda maslahi ya serikali tawala. Pesa nyingi sana zinazotumiwa na balozi pale "wenye serikali yao" wanapotembelea ughaibuni. WaTZ wanapopata matatizo unaambiwa balozi hazina pesa.

    Ukisikia MTZ kapata matatizo ughaibuni, kama vile kufiwa, balozi wala hazitoi kitu cha maana, zaidi ya kutuma salamu za mazishi.

    Ukipata ugua (mfano kansa) usipoteze mda wako kwenda ubalozi maana watakuona kama ni "uchafu" tu.

    Ughaibuni (nazungumzia USA) kuna so many opportunities za kuweza kujikinga na emmergencies. Dola 20 za kimarekani (kila mwezi) zinaweza kukupatia life insurance ya at least 250,000. Ni bora kujinunulia ama kuinunulia familia yako nzima life insurance ili zikusaidie in case unapata matatizo, mfano ukitokea kupata kifo. Don't expect watu wa ubalozini kuja kukusaidia ukipata matatizo

    ReplyDelete
  67. Binafsi naona tatizo kubwa ni mfumo wa utendaji wa balozi zetu. Watu wengi wana nia ya kujiandikisha lakini kama ujuavyo huku tatizo ni muda na pesa pia kwani inategemea unafanya nini huku. Sasa kwa kuwa kujiandikisha kunahitaji mpaka ufike ubalozini na pia kwa kuwa watendaji wengi ufanyaji wao wa kazi siyo mzuri, watu wengi wanaona siyo muhimu kwenda ubalozini. Bolozi zetu inabidi zibadilike ili kuleta ufanisi vinginevyo watakuwa wanadanganya idadi ya wabongo waliopo nje na pia watashindwa kuwahamasisha wabongo kuchangia maendeleo ya nyumbani. Nadhani michuzi unaweza kutumia maoni yetu kuwashauri wahusika ili wafahamu sababu.

    ReplyDelete
  68. Michuzi acha kutuambia tunachafua hali ya hewa kwani hata Jongwe la kike ime-prove kwamba halikuchafua hali ya hewa kama ulivyoliandika.

    Sasa hii mada kwamnza naomba utujulishe kama RAIS WA TANZANIA anaweza kuyapata haya maoni maana hii ndio nafasi ya yeye mheshimiwa kujua nini kinawasumbua watanzania. Huwa hapati ukweli kwani akija huku huwa anakutana na hao wenye matawi ya CCM tu.
    HILO NDIO JIBU LA SWALI LAKO LA TATU - NINI KIFANYIKE.
    Mdau

    ReplyDelete
  69. swali zuri sana bwana michu,nami nilikuwepo wakati swala hilo linatamkwa na mheshiwa Balozi wetu lakini swali hilo lilitakiwa lianzie kwake yeye angetueleza toka ubalozi wa Tanzania uwepo UK umefanya nini kwa Watanzania waishio UK,Kama sio kupokea viongozi wanaokuja kuchekiwa afya zao.Mabadiliko ya mtizamo yaanzie pale ubalozini ndipo yatasambaa kwa Watz walioko hapa na kwa kuanzia hawa wachache wanaowafahamu.mimi wananifahamu lakini hakuna mtu aliyeniuliza hata nafanya nini hapa UK.Na niki rudi kule nyumbani watu wanapata taabu sana kupata visa pale ubalozi wa UK hata kama una sababu ya maana na ukiomba msaada serikali iingilie kati hakuna.sasa huku nitaamini vipi chombo cha serikali.Lakini bottom line nawaomba Watanzania tujiunge na hizo jumuiya kwa manufaa yetu na uchumi wa nji yetu ni lazima tukubali sote (serikali na watz)tumepotoka(misguided)

    ReplyDelete
  70. michuzi bwana!!wewe ulikwenda ubalozini na jibu ukapata,sema ulikuwa unataka waosha vinywa waongee..mafisadi hawapo tuu kwenye CCM hata ubalozini wapo..naona balozi alikupa maana halisi ya watu kuto kwenda pale..

    ReplyDelete
  71. Watanzania walio huku hawawezi kuogopa kujiandikisha eti kwa sababu wamejilipua, hawafanyi kazi rasmi au kwa sababu yoyote kwani hapo ubalozi HAWAANGALII STATUS kama ilivyochangiwa na mdau hapo juu. BALI WENGI HAWAONI UMUHIMU mimi binafisi ninanyundo 8 nimeenda ubalozi wakati wa kubadilisha pass na kama ingekuwepo njia ingine ya kupata pass bila kwenda ningeitumia.

    Kama humjui AMBUKILE hakuna utakachopata. Na 5 days a week wako kwenye mikutano kama kweli. Kuna siku nilipiga simu saa 4nikaambiwa yuko mkutanoni mtu wa idara ya passport nikapiga tena baada ya lunch nikapata jibu hilohilo.

    Naomba haya maelezo ya uya-forward kwa boss wa hizi balozi labda anaweza kufanya utafiti zaidi kuondoa hizi kero.
    Mdau

    ReplyDelete
  72. michuzi bwana!!wewe ulikwenda ubalozini na jibu ukapata,sema ulikuwa unataka waosha vinywa waongee..mafisadi hawapo tuu kwenye CCM hata ubalozini wapo..naona balozi alikupa maana halisi ya watu kuto kwenda pale..

    ReplyDelete
  73. Comments nyingi hapo juu zinaonyesha jinsi Watanzania tulivyo wajinga na dharau kibao zisizo na maana.

    Kwanza kuwa na kazi duni au kubeba box sio kitu cha kuona aibu. Kuna wenyeji wengi wanaofanya hizo kazi na wala hawaoni aibu. Ni bora kufanya hizo kazi kuliko kuwa mwezi wa mali za wananchi au kukaa Ulaya ukikinga mkono mwisho wa mwezi huku una uwezo wa kuchapa kazi.

    Pili watu wengi hawajui mihangaiko ya maisha huku Ulaya, haijalishi kama unafanya kazi kama ofisa au mbeba box, huku kila mtu anahangaika kweli kweli. Muda wa kwenda ubalozini bila ya kuwa na jambo la maana la kukupeleka haupo.

    Tatu, balozi zetu nyingi zinaongozwa na wababaishaji, makada wa chama, ambao wanawaona Watanzania wanaoishi nje kama wasaliti, hivyo kuwafanya Watanzania walio wengi kutokuona umuhimu wa kwenda kwenye hizo balozi.

    Nne, balozi zetu zimeshindwa kutumia technology ili kuwasaidia kuwakutanisha na Watanzania wengi zaidi. Watu bado wanaona mtu mpaka afunge safari kwenda sehemu na kuunguza pesa wakati kuna emails, kuna simu, kuna conferences na nk. Mfano ni ubalozi wa UK. Zaidi ya mara tatu wakati wa mikutano tumejaza forms na kuacha emails na contacts zetu zingine, lakini hata siku moja hawajawahi kutumia email kutujulisha. hata forum ya juzi, waliweka kwenye mitandao lakini hawakuwasiliana na Watanzania wengine kwa kutumia emails ambazo zimekaa tu kwenye mafile yao.

    Ni rahisi kwa Balozi kutembelea mikoani na kukutana na Watanzania kuliko Mtanzania mmoja mmoja kwenda ubalozini. Tatizo ni lile lile, kama la huko nyumbani, kufikiri Tanzania ni Dar es Salaam na Dar Es salaam ndio Tanzania. Balozi zetu zinaona kama zinawakilisha miji mikuu na hivyo kutokuona haja ya kwenda mikoani kukutana na Watanzania.

    Mwisho, ndugu zangu elemikeni, acheni ujinga wa kudharau kazi. Dharau kama hizo ndio zinatufanya tuwe wajinga, Wakenya wanakuja na kuchukua kazi hapo TZ, vijana wetu ni ubitozi tu na kujifanya wajuaji. Ni bora kufanya kazi yoyote halali kuliko kushinda kwenye magenge na mikono mifukoni.
    Waacheni Watanzania wakiwa nje, wafanye kazi yoyote ile wanayoamua kuifanya, kazi halali, kazi inayowapa ridhiki na uwezo wa kujilisha na kusaidia wengine. Hakuna haja ya kuona aibu hata siku moja. Wanaotakiwa kuona aibu ni akina Chenge na majambazi wenzake, ni mabitozi wa mjini na mikono mifukoni bila kufanya juhudi ya kutafuta kazi. Kazi zao kucheka wengine. Elemikeni ndugu zangu, vinginevyo ujinga ni mauti.

    ReplyDelete
  74. TO BE SHORT AND CLEAR,"Balozi za Tanzania hazina mpango na nijivunie Utanzania kwa kipi???UFISADI?Mimi msomali/mnyarwanda au Mrundi its better.Sina mpango wa kurudi huko "YA KAZI GANI KUJIANDIKISHA?Sio nikipata tatizo serikali au hio TZUK itanikingia kifua,Ya kazi gani sasa nijiandikishe?Kuzikwa huku au huko haimsaidii yoyote mfwa,Ya kazi gani sasa kujiandikisha?
    NGURUBANGE - Coventry

    ReplyDelete
  75. Ahsanteni sana kwa kutoa fursa kama hii. Kwanza kabisa tatizo ni kwamba wengi wa wafanyakazi hata baadhi ya mabalozi sio professionals. Amepelekwa pale kwa ajili yeye ni wa fulani ama fulani amempeleka. Tanzania kama nchi inatakiwa ichukue hatua.
    Jingine ni kuwa hata awe wa namna gani mtanzania popote pale alipo ubalozi ndio mama na baba yake. Wapi ushasikia mzazi kamilifu akamchagua mtoto wake. Hata kama ni mjizi ni mtoto wake tu.Hivyo ndugu zangu wabongo hata kama wewe ni mzamiaji bado wewe ni mtanzania tu. Na serikali ya tanzania lazima ifahamu kwamba yafaidika sana nawe kuwa ughaibuni kwani unachangia sana uchumi wa nchi kwa mapesa unayowatumia ndugu zako mara kwa mara.Hebu watoe statistic za pesa zinazoingia nchini toka kwa waTZ walioko nje.
    Hivyo nawasihi waheshimiwa viongozi wanaohusika wasiwalaumu waTZ ughaibuni ila wawatimue wote ubalozini wawaajiri professionals watakao wajibika inavyotakiwa.waige balozi za marekani, uingereza jinsi wavyoshughulikia watu wao ughaibuni

    ReplyDelete
  76. Tumejiandikisha online lakini hata kujibiwa kwamba umejiandikisha hakuna. Tunaitwa kupitia Blog yako kupiga kura za kuchagua Mwenyekiti wa CCM London. Basi watu wajiandikishe kwa Michuzi

    ReplyDelete
  77. Hivi kuna tofauti kani kati ya kujilipua na kuoa/kuolewa na raia wa nchi nyingine halafu ukabadilika uraia??? Na kuna ubaya gani? Watu wanafanya hivyo kwa ajili ya kutafuta maisha sio kwa kupenda tu. Nasoma haya maoni naona eti kuna mtu anasema tuwanyooshee vidole waliojilipua...mani wabongo tuache wivu ...huko....UK....mbona mna kazi!!!!! Muwanyooshee vidole ili iweje?

    Maisha popote haijali wee ni raia gani na unaishi vipi huko uliko. Hamna mtu anayependa kuwa mkimbizi nevertheless mkimbizi wa kujibambikizia wakati nchi yake anayoikana haina hata tatizo lolote ni amani tupu lakini mtu yuko radhi kuikimbia..

    Wengi huku macelebrity viongozi wa ngazi tofauti wala si wazaliwa wa hapa na sasa hivi wameshakua citizen na hamna anayewanyooshea vidole au kuwasimanga kuwa wamekimbia nchi zao.

    Back to your question. Mimi sipo UK lakini kama wangeleta hilo jambo huku USA sijui kama lingepokelewa kwa mikono miwili pia.

    1)Ubalozi huo hapo lakini umejitenga sana na raia wake. Hamna upendo wowote wa kuonyesha kuwa nchi yetu inatupenda kwa hiyo kama wakitaka kutuandikisha why will I care?

    2)Ni matatizo mangapi yametupata na hamna hata wa kuemail na kusema jamani how can we help? Yaani unaniambia mambo mengi tu yanayotokea hapa USA hayawafikii wao kabisa au wameziba masikio? Ubalozi jina tu watu wameshajizoelea kuwa wenyewe kama watoto yatima

    3)Kabla ya kuwaandikisha hao raia wao walikua wanawasaidia au wako karibu na raia hapo vipi? Na wakijiandikisha itawasaidia nini?

    4)Kujiandikisha italeta bias sana huko UK. Waliojiandikisha ndio watakua na first preference zaidi ya wengine kama raia halisi.

    5)I hope wangesema wanataka tu contact information za wabongo walioko huko. Ujiandikishe halafu iweje?

    6)Kuna privacy gani katika kujiandikisha huko? Hizo data zisije zikawa zinatumika kwa mambo mengin...Wanaguarantee vipi watu watakaojiandikisha information zao zitakua private?

    Kama walishindwa kukusanya data za watanzania wote walio nje wakati wanabadilisha passiport zao kwanini sasa hivi? Kipindi kile ndio ingekua rahisi sana kujua kila raia wa nchi yao kwa wale walioenda kuchange passiport walikua raia wa tanzania.

    Hao wahindi wanaohold passiport za TZ nao watajiunga kwenye hizi jumuia, au ni watanzania weusi tu. Nakumbuka nilivyokwenda NY city kuchange passiport watanzania weusi tlikua sawa na watanzania wenye asili ya kihindi?

    ReplyDelete
  78. Ndugu Michuzi huna kosa kwa kuuliza swali kama hili. na tumefurahi sana kwani swali limegusa mahala pake, na tunaomba uwapelekee haya maoni na majibu yetu kwa hao waliokutuma ubalozini. kwa kuchangia tu kwa nini watanzania hawajiandikishi kwenye balozi zao?
    (1) asilimia 90 ya wafanyakazi wote wa balozi zetu wanajiona miungu watu, kuanzia balozi mpaka karani.wanapenda kunyenyekewa.
    (2)Hawana msaada wowote na wabongo wana kheri wasaidie mgeni wakakuacha wewe mzawa. watakusaidia kama wewe ni mtoto wa somebody fulani au fisadi fulani au mnatoka kijiji kimoja (tena sio kabila).
    (3)Hawaudhurii mazishini wala kwenda kumuona mgonjwa hospital, kama wewe si mtoto wa fulani.
    huwa wanajifanya kufanya viparty vyao ikifikia siku za sherehe kama uhuru na kuwaita wabongo wajichanganye nao kinafiki sababu huwa wameshavuta pesa wizarani (mambo ya nje ) wanavuta mfano £30,000 wanafanya kijipati cha £1000 nyengine wanachikichia . nina mifano hai michuzi wa wawakilishi wetu huku.katika mabalozi ambao walikuwa wanasaidia watu wao ni katika miaka ya 80 kuna balozi nimemsahau jina ni mzee wa kisambaa alikuwa balozi wetu Khartoum sudan huyo hakuna mtu atakaye msahau kwa misaada aliyokuwa akiwasaidia watu kwa watu waliopita sudan miaka hiyo,mwengine balozi sykes alipokuwa Italy alikuwa mtu wa msaada sana alikuwa akiwatembelea wabongo waliokuwa cyprus na ugiriki mara kwa mara. lakini waulize wabongo waliokuwa China miaka ya 88,ujerumani miaka ya 86 na Misri 80. jinsi mabalozi wetu walivyokuwa washenzi wasio na msaada (majina yao nayahifadhi).nina miaka kama 20 sasa hapa UK sijasikia hata siku moja ubalozi wetu unasafirisha maiti kwa kwa pesa yake kama si michango ya watanzania wenyewe walio hapa.kwa hiyo Michuzi huko kujiandikisha hakuna msaada wowote hapa UK kama kufa utazikwa tu kama si wabongo wenzio basi council au kuumwa utatibiwa tu waingereza hawawezi kukuacha ukafa. so kwa nini nijiandikishe. TELL THEM GO 2 HELL or THEY CAN KISS MY A--.
    Zee la Kitaulo -UK

    ReplyDelete
  79. MICHU NAONA USHAPATA JIBU, KATIKA COMMENTS ZOTE HAPO JUU INAONYESHA BALOZI HAZINA MSAADA WOWOTE KWA WATANZANIA, MAANA HAWA WOTE WALIOCOMMENT NDIYO WATANZANIA WENYEWE UGHAIBUNI. SASA MICHU FUNGA MJADALA SEND ALL THESE COMMENTS TO JK.

    ReplyDelete
  80. Kuhusu ubalozi si wote ambao tupo bila makaratasi . Nazungumzia ubalozi wa Tanzania wash dc. Hawajui kabisa maana ya ubalozi . nakubaliana na kaka huko juu anayesma kuna dada anayepokea simu kwa hasira halafu ukiuliza maswali majibu unayopata ni short and attitude kibao . Hamna msaada wowote unatolewa na ubalozi huo . Ukiwana shida ni heri utafute watu mtaani . Halafu lazima umjue mtu kitu kifanyike . Siendi , walasijiandikishi maana hamna la maana linalofanyika kutusaidia or kutuinform wabongo

    ReplyDelete
  81. Mimi mdau ninaeishi London-UK, asante sana kwa nafasi hii chache. ni hivi, mimi sitaki kujiregister na ubalozi wetu hapa UK kwa sababu nyingi lakini naweka hapa chache tu kusave muda na nafasi:
    - Sipati faida yoyote nikijiregister
    -Kuna kujuana kwingi sana ubalozini hasa wakati unafuatilia barua muhimu muhimu.hakuna anayekujali, nakumbuka passport yangu ilitengenezwa na sura ya mtu mwingine, tena mtoto wa miaka kama 15 hivi, na sikupata hata msamaha toka kwao.
    -sisi watanzania tunapenda kujifanya tuna umoja lakini ukweli ni kuwa hatuna hata kidogo.

    Labda wanigeria wanao kushinda sisi.

    Asanteni.

    ReplyDelete
  82. Watu tumechoshwa na longolongo. Sio siri tatizo kubwa linalochangia ni kwamba kilia mtu anafikiria akijiunga na jumuiya au akiwa karibu na balozi atafaidika vipi(hasa kifedha) Kila mtu anataka ulaji. watu wanaendekeza njaa.

    ReplyDelete
  83. KARAHA,UHASIDI,MAJUNGU NA DHARAU NDIYO SABABU KUBWA

    ReplyDelete
  84. Jumuiya za huku zimekaa ki-CCM sana hazina utaifa ni U CCM tu, hivyo mi binafsi sion sababu ya kwenda kujiunga, Tunahitaji Jumuiya zisizo na itkadi yoyote huku ughaibuni.

    ReplyDelete
  85. Cha kushangaza Michuzi watu wanatoa comments za ukweli bila matusi lakini unazi block. Inaonyesha jinsi gani hauko tayari kama muanzishaji wa mjadala kuweka maoni ya watu wazi. Hii haitajenga blog yako badala yake itakufanya uonekane usalama wa taifa na umetumwa kutafuta maoni ya watu kuhusiana na ustawi wa CCM nje ya nchi.
    Handle ur bussiness man and dont be coward or a punk bado utakuwa na kazi dairly News bro.

    ReplyDelete
  86. Michuzi,

    I suggest one thing, take all these comments and send them to editorial board of Habari Leo and Daily News, and ask them to do justice print for the whole public to see. The REAL issues with our EMBASSIES OVERSEA.

    In business note sell them to other media outlet, they will be willing to take them, and put them on public domain.

    YOU WILL DO JUSTICE FOR EVERYONE.

    By the real DIASPORA.

    ReplyDelete
  87. namsikitikia kikwete mnaonaje hapa sweden watanzania tuandamane, kumtoa huyu mtu, maana amekiuka kabisa, sheria za ubalozi, anatakiwa kushtakiwa kabisa. wataznania mnaonaje hili.

    ReplyDelete
  88. michu vyama vyetu ni kama vijiwe, asilimia kubwa ya viongozi ni watu wenye personala ambitions, kunjnga cv, biashara etc, wewe mwenyewe ummeona, pili majungu jamani watz tunamajungu si mtaani mpaka mitandaoni wakikujua mbongo wataanza ooh uonekani umejitenga, arosto na mengineyo
    tatu hakuna agenda za maana zaidi ya starehe mimi mwe sijiungi na sitaki kabisa kugeuzwa dili
    kuusu ubalozi ni ufisadi, ukabila umejaa si wafagiaji mpaka wahusika wakuu ukikutana nao ooooooh wewe mtoto wa nani wanataka kujua sir name ili wadili nawe au la siwezi kujiunga nao.

    ReplyDelete
  89. Naungana na mdau wa April 22, 2008 7:16 PM. Mimi niko hapa US kihalali. Nilienda Ubalozini DC wakati mmoja kufuatilia passport. Kwa namna nilivyokuwa-treated inakatisha tamaa. Hizi balozi (may be siyo zote) inaonekna si za msaada sana.

    ReplyDelete
  90. Haya kiko wapi yale yale aliyoyasema Bibi Maendeleo leo yamejirudia. Nilivyvosoma ule mgazeti wake nikaona huyu dada ana wivu na watanzania wanaoishi nje. Sasa leo swali limekuja kwa njia nyingine lakini majibu yamerudi pale pale, MAJUNGU, UBINAFSI, KUTOPENDANA NA MENGI MENGINEYO.

    Haya kazi kwenu bora maisha yanaenda na siku zinaendelea ukiwa uko shule, unabeba box au unafanya kazi ofisini usiku ukiingia siku imetoka unasubiri kesho kama utaiona.

    Kuhusu mambo ya vyama mhu huo ni utashi wa mtu, wakati mtu mabills yamemzonga bado atakuwa na wazo la kujiunga na chama? Labda hicho chama kiwe na mchango wa kiuchumi kwa mlengwa, mwanachama akijua nikiwa mwanachama ninaweza kusaidiwa kujiendeleza masomo, kupata kazi au hata tu mkopo tusio na masharti yoyote na twenye riba nafuu akiwa na shida, hapo utaona watu wanajiunga. Lakini hivi hivi tu sio rahisi.

    Kuhusu Ubalozi kwanini wao ndio wafuatwe tu na wao wasifuate watu waliko ni utendaji gani huo wa kazi kukaa ofisini kusubiri watu wakufuate? Mbona hata JK hutoka kwenda mikoani kuangalia wananchi wake, kwanini wasiige hilo? Kwani wao hapo mwaka mzima january mpaka disemba wanafanya nini? Wanashindwa kutenga japo siku 5 kila mwezi za kuzunguka nchi, mpaka mwaka ukiisha atakuwa ameshamaliza nchi nzima. Na atajuaje sasa hali ya halisi ikiwa atakaa kusubiri watu wamfuate huko aliko ofisini?

    Ni hayo tu!

    ReplyDelete
  91. Muhidini, watru wmaesema ukweli mtupu kuhusu balozi zetu na jumuiya za kibongo, huku ughaibuni. Haishangazi kwa kuwa wnegi wa walio huku ni vizazi vya watu fulani hivi huko bongo na wengine tuliokuja kimpango wetu.
    Sasa tambua tu kuwa hivyo vizazi vya mafisadi ndo vipo msitari wa mbele kuhakikisha vinaliza wabongo kwenye jumuiya na vile vilivyopo ubalozini vinaendeleza tabia za wazazi wao huko serikalini bongo.

    Tatizo linakuja kuwa maisha huku hasa opportunities ni nyingi mno za kumfanya mtu asiwe tegemezi. kwa mfano kama ni masuala ya misiba tu, unachohitaji kufanya ni kuwa na bima tu ya maisha kwa familia yako, hii wala si ghali kwa mwezi unaweza ukawa unalipia $13.56 kama una umri wa miaka 30 hivi na ukiwa na Bank of America. Baadi ya waajiri hutnunulia wafanyakazi wao bima za afya, hivyo unapoumwa au unapokwenda kufanya uchunguzi wa afya, hausumbuki, bima inalipa. Na mambo mengi tu ambayo huko bongo huwa ni disaster yanapotokea huku unaweza kujikinga kabla hayajakupata. Tatizo watu wagumu kuchukua hatu wanapokuwa wazima bila matatizo, hivyo wanapokutwa na majanga kama vifo au magonjwa ndipo huanza kuhangaika, jumuiya zinakaa mbali na balozi hazifikiki, matatizo yanakuwa lukuki.

    Ushauri wangu kwa wabongo wote, achaneni kujiumiza kichwa kwa kukimbilia ubalozini mnapokutwa na majanga kwa kuwa HAMUWEZI KUSAIDIWA huko, lakufanya ni kuhakikisha wote
    mnanunua bima za maisha, afya (kama mwajiri unapofanya kazi hakulipii bima ya afya, acha kazi hapo tafuta sehemu nyingine) na bima nyingine nyingi tu ambazo zitaweza kukusaidia ukikumbwa na majanga. Ni bora ushindwe kuwaalika watu kuchoma nyama nyumbani kwako lakini uwe umejikinga.

    Tukubali kuwa hatuwezi kubadilisha attitude za mabalozi na wafanyakazi wao wala za viongozi wetu wa serikali mafisadi, iwapo wamekuwapo tangu uhuru na wanazidi kushamiri kwa kuwa wote ndo walewale, hakuna wa kumfunga paka kengele ndo maana wengine wanajeuri hadi kuita mabilioni vijisenti, kwa kuwa wanajuwa kuwa hamna wa kuwashughulikia kwa kuwa wanakula nao. Hata JK hawezi kuwashughulikia wengi wao kama si even wote kwani mpaka kufika hapo alipo ameshafanyiwa hisnai nyingi sana, ama na wao ama na jamaa zao ama na ndugu zao ama na baba zao. hivyo tusijidanganye.

    Tuchukue tahadhari, waachani na balozi zao wapigie majungu na kuunganishana dili za kifisadi. Swali kwako Muhidini, hivi unataka kuniambia kuwa Balozi hapa Wash., DC hakujua kuwa Richmond ni feki? Asitudanganye.

    ReplyDelete
  92. MIMI NI LECTURER WA UNIVERSITY OF DSM, NAONGEZA DEGREE HAPA CANADA -SUDBURY ONTARIO, NILIPOFIKA, NILIWATUMIA E-MAILS KADHAA UBALOZI WA TANZANIA HAPA CANADA, AMBAO MIMI SIWEZI KUSAFIRI KWENDA HUKO, UBALOZI HUKO MBALI TOKA HAPA NILIPO, NILIANDIKA E-MAILS KWA RAHA ZOTE NIKAJUA NITAJIBIWA NA WATANZANIA WENZANGU WALIOKO UBALOZINI, TENA MAY BE WAKANIKARIBISHA NA KUNIPA SOME PROCEDURES ZA JINSI GANI YA KUISHI N.K,

    SINA MPANGO WA KUISHI HUKU NIKIMALIZA NARUDI KWETU TZA KWA BABA, MAMA NA WADOGO ZANGU KIBAO ACHILIA MBALI MARAFIKI.

    SIJAJUA NA SITATAKA KUFUATILIA KWA NINI MPAKA LEO SIJAJIBIWA!!!!!! SIJAFURAHIA HILO HIVYO NAHISI PENGINE BALOZI ZETU HAZIWASAIDII WATU HAWAWAENCOURAGE WATU KUJIANDIKISHA MAANA MTU HATASAIDIKA KWA LOLOTE.

    NA NILIKUJA KIPINDI KIBAYA SANA CHA BARAFU,WAKANADA WEUPE RANGI TOFASUTI NA MIMI NDIO WALIONIELEKEZA KLA KITU, HUKU WATANZANIA WENZANGU WANADUNDA.

    SIJAJUA BALOZI NI NANI?? HIVYO SITAKI KUSIKIA LOLOTE KUHUSU UBALOZI WA TANZANIA NCHINI CANADA.

    PENGINE WANAFIKIRI WATANZANIA WENGI WANA MPANGO WA KUZAMIA HUKU,

    FOR ME I AM PROUD OF MY COUNTRY,SITAKI KUWA ''SECOND HAND CITIZEN''

    ReplyDelete
  93. MIE NITAFANYA UTAFITI NIKAJIANDIKISHE HALAFU MATOKEO NITAYALETA KWENYE BLOGU NA KILA KINACHOENDELEA NITAWAAMBIA. ILA KITU KIMOJA KINACHOONEKANA MARECEPTIONIST WA OFISI ZA UBALOZI WANAFANANA TABIA? KWANINII WHYYYYY?

    JIBU SIO PROFESSIONAL WAMEPACHIKWA NA JAMAA ZAO ILI WAPATE MKATE WAO. ILA HAWAJUI KUWA WANAWAVUNJIA HESHIMA NA KUWATUKANA WALE WALIOWAWEKA PALE ILI WAGANGE MAISHA YAO KWA KUTOTIMIZA WAJIBU WAO KWA WATEJA WAO. UKIWA RECEPTIONIST HATA KAMA HUKUSOMEA HIYO KAZI JIFUNZE, KUWA MNYENYEKEVU, UKISHIKWA SHIKAMANA, SOMA MASOMO YA JIONI! ELIMU IKUFUTE MATONGOTONGO YA KUONA ULAYA AU NJE YA NCHI AU KUWA RECEPTIONIST BALOZINI NDIO MWISHO WA KILA KITU. (najua wenyewe mareceptionist watasoma)

    KUHUSU VIKUNDI, NGOJA NISEME KUHUSU HUO MKUTANO ULIOFANYIKA HAPO LONDON WA DIASPORA. JE ULIHUSISHA WATANZANIA WANAOISHI NJE YA LONDON? MAANA NILIONA KAMA ULIKUWA MAALUM KWA LONDONERS. MIE MWANZO TU NILIPOLIONA LILE TANGAZO NIKAINGIA KWENYE WEBSITE YA WAANDAAJI KUJIREJISTA KWA SABABU SIISHI LONDON NINAISHI MBALI NA HUKO LAKINI NILIKUWA TAYARI KUSAFIRI NA KULIPA NAULI YANGU NA HATA KULIPA MAHALI PA KULALA ILI ANGALAU NIHUDHURIE NIKUTANE NA WATANZANIA WENZANGU. LAKINI CHA KUSHANGAZA, NILIVYOINGIA SEHEMU YA KUREJISTA, NIKAKUTA SURVEY FORM (NAHISI NDIO HIYO ILIYOONYESHA TAKWIMU YA KUWA 13% TU NDIO WAMEJIANDIKISHA KUTOKANA NA MAJIBU YA SURVEY). THAT WAS REALLY UNETHICAL UNAMWAMBIA MTU AJIREGISTE KUMBE UNAFANYA RESEARCH YAKO BILA CONSENT? NA TENA BAADA YA KUJAZA HIYO SURVEY NIKITEGEMEA MWISHO WA SURVEY NIMESHAWAPA DETAILS ZANGU, BASI WATANIAMBIA KUWA SASA UMEKUWA REGISTERED KUSHIRIKI KWENYE MKUTANO. (SIE WENGINE HATUENDI KWENYE MKUTANO AU KONGAMANO BILA KUJIREJISTA MAANA HUKU SIO KAMA UNAENDA KWENYE MKUTANO WA HADHARA MWEMBE YANGA!) LAKINI SIKUPATA MAJIBU YOYOTE KUWA NIMEKUWA REGISTERED KUSHIRIKI HILO KONGAMANO OR WHAT. INAELEKEA KULIKUWA NA KUJUANA KATIKA KUALIKANA AU KAMA ILIKUWA WATU WAENDE TU KAMA WANAENDA MWEMBE YANGA HAKUKUWA NA HAJA YA KUWEKA SEHEMU YA KUREGISTA HAPO KATIKA WEB YAO. NA PIA MGESEMA HUU MKUTANO NI KWA AJILI YA WAKAZI NA MAALWATAN WA LONDON TU WENGINE WALA MSIJISUMBUE. HEBU IFIKE WAKATI TUACHE YALE MAMBO YETU YA NYUMBANI YA KUFANYA VITU KWA KUJUANA NA KUONEKANA KUWA NA MIMI NILIONEKANA NA FULANI. KAMA KUNA NIA YA KUFANYA KONGAMANO KWA AJILI YA FAIDA YA WATANZANIA WOTE BASI VITU VIWEKWE WAZI. BY THE WAY NILIJARIBU KUREGISTA TENA HIYO REGISTRATION LINK IKAKATAA.

    NAJUA WENYEWE WATAJITETEA SANA LAKINI HAYA NDIO MAPUNGUFU YA WATU WALIOANDAA HILO KONGAMANO. NIMESHAWAHI KUSAFIRI NCHI MBALI MBALI AFRIKA KUSHIRIKI KWENYE MAKONGAMANO YA MAENDELEO YA AFRICA, NA HUKO NIMEJIFUNZA MENGI, NILICHOTAKA NI KUJIFUNZA KUTOKA KWA JAMAA WA KWETU PIA NA PENGINE KUCOMPARE. BY THE WAY HAPA NIMEKUJA KUSOMA TU AFTER 4 YEARS NARUDI ZANGU NYUMBANI KUENDELEA NA MAISHA YANGU!

    MTANZANIA EAST ANGLIA

    ReplyDelete
  94. HAYA BRO MICHU NADHANI MAJIBU YA SWALI LAKO UMESHAPATA NIKITAZAMA ASILIMIA 99 YA WABONGO UGHAIBUNI(SIO KAMA ASILIMIA ZAKO 13 HAHAHAHA) WANAPINGA KUJIANDIKISHA NA KUPONDA BALOZI ZETU KUWA HAZINA MSAADA WA AINA YOYOTE,WANAJIONA WAO NI MIUNGU WATU,WABAGUZI NA MAFISADI NAMBARI WAHED.SASA BASI KWA TAADHIMA TUNAKUOMBA UFIKISHE MAJIBU YETU KWA WAHUSIKA (KWA HAO WALIOKUTUMA) NA KAMA HUKUYAFIKISHA BASI UTAKUWA FISADI,USALAMA WA TAIFA,MBEA,MPEKUPEKU,FALA HUKUKULIA AGGREY, HUKUPIGIA BENDI YA DAR INTERNATIONAL NA UTAKUWA UNAJIPENDEKEZA KWA MAFISADI WENZAKO. LONG LIVE FREEDOM OF SPEECH --- ZEE LA KITAULO UK.

    ReplyDelete
  95. Hi
    sir michuzi tunakushuru sana kwa message zako tumezipokea,jambo moja muhimu sana sisi tumepokea ujumbe wako tunaomba na wewe ufikishe ujumbe wetu huu kwa wausika siotuumize vidole vyetu tu humu kwenye blog yako. Pili ni hivi ndugu zangu watanzania twaweza kuprint hizi comments na kuzichuja zisizo za maana na kuziwakilisha kunakohusika na maanisha foreign affairs kwani wao pia ni wahusika wa hizi barozi sizani kama michuzi ana nguvu yakuwakilsha ujumbe huu,hiyo maana naona itakuwa ndio mwisho wake wa ukuu wa wilaya ya tegeta asante sir michuzi kama ujumbe utafika mdau uk.

    ReplyDelete
  96. Jamani kuna mtu anafahamu jinsi ya kupata makaratasi - ninataka kuukana utanzania maana HATA RAIS MSTAAFU NAYE FISADI analipwa M146+ kwa siku.
    Mtafuta Karatasi

    ReplyDelete
  97. kaka michuzi mimi nina mfano hai nilifiwa na mama yangu aliyekuwa akiishi ughaibuni nikaenda kuchukua maiti nikiwa sijui mbele wala nyuma tulijitambulisha ubalozi kama ilivyo ada kwanza najuta kwenda huko maana hawakuwa msaada hata kidogo ni jumuiya ya watanzania walionipokea kunihifadhi na kuchanga fedha za kumsafirisha mama yangu sikuona cha afisa ubalozi wala kivuri chake

    je ungekuwa wewe umeenda ughaibuni
    kwa mara ya pili ungeenda kujitabulisha kwenye ubalozi au kwenye jumuiya? hata kama kwa kuzamia

    ReplyDelete
  98. Kwanza Ubalozi wenyewe sidhani kama wana job description hiyo ya uandikishaji kama wanayo basi ni wapuuzi, kwani hata ukienda pale utafikiri umeenda kuomba chakula...afisa wa ubalozi atakupita tu bila hata salaam.

    Pili, sidhani kuwa tunahitaji kwenda kupiga foleni kama vile tunapiga kura Tandale..watuwekee kwenye mtandao..ili tujiandikishe on-line, sisi hatukuja huku kushinda tunataime mida ya huo ubalozi(ubalozi wa Uingereza) kwani tunamambo mengi yaliyotuleta UK ambayo niya msingi kuliko hilo la kujiandikisha.

    Balozi mwenyewe celebrity, kesho utasikia hata kitchen part zinafanyikia ubalozini...anapenda sana kujionyesha mpaka hadhi yake iko mashakani....aangalie mabalozi wengine wanafanyaje na ajaribu kudelegate majukumu kwa maafisa wa Ubalozi, maana shughuri nyingine ni ndogo sana ambazo hazimfai yeye kuwepo kwenye shughuri hizo.
    Anatakiwa awe kwenye mijadara ya maana na siyo petty issues.

    Wengine tumeanza kumkumbuka Abdul Kadil Shariff...alikuwa balozi, hata ambao hawakuwa huku wanakumbuka mijadara yake ya maana...
    Kumbuka hata alivyokuwa anadiscuss issues na alivyoweza kusimamia msiba wa baba wa Taifa hapa London.
    Tunahitaji watu wa namna ile.
    Tatu,

    ReplyDelete
  99. kwa watanzania mtu ambaye ameondoka nchini kutafuta maisha wanamwona kama muasi, gaidi haipendi nchi yake. Ndio maana kwetu tuna msemo "Njooni nyumbani tulijenge taifa" Kana kwamba huwezi kujenga taifa long distance.

    Wakati kwa wenzetu hata maubalozi yao wanawasaidia kutafuta njia ya kuishi huku tuliko kama wamekuja kienyeji.

    Huko UK wasio na papers wakienda kujiregister...hao hapo wa ubalozi watawareport kwa Govt waondolewe......wakati huku tuliko waspanish million 12 wako illegal lakini kila siku ubalozini kwao wanaenda kuwapa ID manake wao wanaingia bila hata ya passiport na huko walikotoka ni vijijini hamna hata ID....Lakini wanawatengenezea ID bila matatizo.

    Halafu tatizo la maubalozi yetu ni kwa wale watu wanaobadilishwa kila miaka sijui mitatu au minne....Yaani wanakuja na zile nyodo za kwetu...zile nyodo za wafanyakazi wa posta na baadhi ya wafanyakazi wa bank. Mtu ukienda hapo badala ya kukuhudumia wanaanza kuongea kwenye simu. Basi hizo nyodo wakija nazo mpaka wakishajua life na kazi ni nini mara muda umeisha wanaondolewa wanakuja wengine.

    Halafu lingine hao watu wa hapo ubalozini wakishajua kuwa wewe unaishi huku wanaanza kuwa sijui na hasira au wanafikiri unawadharau au unajifanya unajua sana...Kumbe wala...siye huku maisha ni maisha na TZ ni always home sweet home.....Mtu akisema mwanafuzi they are so happy wth you lakini ukisema mimi nilishamalizaga shule zamani naishi huku...swali la kwanza lini ulienda TZ ...wakishajua ni lini ...wanaanza kuwa na different attitude....wangejua tu huku ......how we feel about our country wala wasingekua na mengi rohoni mwao...

    Tusipobadilika mentality zetu wengi watakua hawana time na mambo ya nchi yetu kabisa na wengi hawataishia kuwa na green card tu wataenda all the way kubadili uraia.....

    ReplyDelete
  100. Habari yako Mr. Michuzi, nadhani swali lako ni zuri sana. Kwanza naomba ni jibu straight to the point no bs around.

    Mimi binafsi nipo US kwa more than 1o years, ubalozi wa Tanzania nilishawai kuomba kwa wakubwa ufungwe kwani hauna kazi bali ni kuspend tax payer money unwise. Balozi zetu zinaendeshwa kwa kutumia 16th century strategy, ni center point za matatizo na sio kutatua matatizo.

    Mfano hapa US nimeshawai kupiga simu more than 10 times naulizia service ndogo kama kurenew passport lakini kuna huyo dada ambae anaenjoy tax payer money, huyu dada anakiburi kisicho mfano.

    Hakuna umuhimu wa kubaby sit something which doesn't benefit us. Kuhusu nchi nyingine sifahamu, lakini kwa US that is the case. Mfumo dume wa balozi zetu.

    Mfano mwingine, pale anapokuja kiongozi kama JK, nimeshawai kuwandikia balozi more than 5 times kwamba sisi watanzania wa jimbo fulani tunaomba kuonana na mkubwa kwa mazungumzo yetu binafsi. Majibu ya hao wawikilishi wa CCM hapo DC unaweza kutapika.

    So inconclusion, nikasema who cares, they don't pay my bills so to hell with the office.
    Ni hayo tuu
    Mdau wa Texas

    ReplyDelete
  101. mimi nipo UK ila siwezi kwenda kujiandikisha kutokana na kwamba ubalozi wetu una kero karaha. nilienda kubadilisha passport na kuna mwanamke alikuwa kwenye ofisi iliyo kwa ndani, ilimchukua dk 20 kutoka kuja kunisikiliza despite being alerted kwamba kuna mtu anahitaji huduma kwenye dirisha la passport.na huwezi kuamini niliomba kusaidiwa pen ili nijaze fomu, nikaambiwa hakuna pen, nenda ukanunue ya kwako.?? can u imagine? hivi mtu ukishajibiwa hivyo unadhani utakuwa na hamu ya kujiandisha. what for?? mie nadhani balozi zingeangaliwa upya ili uozo wote usafishwe then tutafikiria kwenda kujiandikisha.

    ReplyDelete
  102. lets cut the story short i live in the UK and our embassy has always been pathetic,the embassy is there to represent the government not the people from tz who live here,tanzanians have died in this country the embassy cant even contribute £100,we have our small assocciations which unite us and help each otha the embassy doesnt do jack to anyone except those few who licks the ambassadors #ss,excuse my language!

    ReplyDelete
  103. UBALOZI SIYO CCM AU CUF AU CHADEMA. UBALOZI NI AMANA YA SERIKALI
    LAKINI BALOZI ZOTE ZA BONGO DUNIANI ZIMEJAA U CCM. WASIOKUWA CCM WATAENDA VIPI KULE? AMKA WEWE NDUBWI

    ReplyDelete
  104. Mdau wa Tarehe April 22, 2008 11:47 PM, ambaye ni mwanafunzi-mwalimu huko Canada anasema hataki kuwa second class citizen.. Umeenda off point kidogo, na i hope kaka angu mpendwa Michuzi ataruhusu hii off-point yangu nayo uione ili upate jibu kwa maelezo yako.

    Haya nenda TZ kalipe kodi zako bongo halafu akina Chenge na Mkapa wazitie mfukoni. Afadhali mimi ninayeishi na kufanya kazi ughaibuni.. Silipi kodi yangu kuneemesha mifuko ya Chenge et al... Kodi ninayolipa inasaidia watoto wangu wasome kwenye shule zilizo kwenye the highest standards; mwanangu hahitaji kugombana na konda ili awahi shule kwani kodi yangu inamwezesha kupitiwa na school-bus nyumbani ambalo silipii extra cash ili nipate hiyo service; barabara zinajengwa kila siku bila kusubiri kwanza zijengwe za Moshi mjini.. At least I see the benefits of paying taxes.

    Nilifikiri kwa kuwa wewe ni mwalimu UDSM ungeweza kugundua hilo kwa haraka haraka. Inabidi urudie form six. ha ha ha!!!

    ReplyDelete
  105. Michuzi,

    Watu wametoa maoni yao kiufasaha. Hakuna mtu aliyejibu pumba humu.

    Mimi nakushauri ukimalizana na hii kitu um-printie Rais na waziri wake wa mambo ya nje (nina uhakika una access na hao watu), ili wapate picha halisi kuhusiana na the realities on the ground.

    Mimi ningemshauri Rais azifunge balozi zote na awe anatuma maofisa wa wizara ya mambo ya nje kwenye nchi husika kama kukitokea jambo ambalo linahitaji utekelezaji. Hii itakuwa ni cost effective kwa nchi na tax-payers funds zitaokolewa kwa kiasi kikubwa.

    Sikatai, kuwa na balozi nje ya nchi ni kitu kizuri kwa nchi husika, lakini kulingana na maelezo ya wachangiaji mimi naona hawa waliopewa majukumu ya kufanya huko nje wanatekeleza mambo kienyeji. Ingekua ni bora Rais akawa ana mabalozi pale ofisi ya mambo ya nje ambao wamepewa majukumu let's say Ulaya mashariki, Asia, Australia, ama amerika. Rais akiwa anataka kutembelea America kwa mfano, then huyo afisa anayeshughulikia mambo ya America ndio atasafiri let's say 3 days before rais hajaondoka ili kwenda kumwandalia mambo. Kwa kufanya hivi mambo yataendeshwa efficiently kulikoni kuwa na lijumba pale Washington DC ambalo linalipiwa mamilioni kila mwaka na hapohapo likawa limekaliwa na very arrogant people ambao ni useless kabisa na wasio na sifa na maadili ya kuwemo mle ndani.

    Nawasilisha

    ReplyDelete
  106. sioni sababu ya kujiandikisha ili niwanufanishe mafisadi/ kama hujui bwana michuzi government ya uk inatoa fungu kwa society yeyote hapa Uk, the more members you have the more money you will be allocated. hiyo bongo uk ni biashara tupu, ubalozi umeoza. nimeomba kubadirisha kitabu changu kuna jamaa anaitwa julius. sijui alitaka nimlambe? nimeamua kuwa msonji...raha tupu, nikjoa bongo naomba visa nawaona wazazi, nawachungulia mafisadi kwa mbali halafu nachukua pipa. waache watoto wa mafisadi wale nchi, tutaingia mwituni tuu,

    ReplyDelete
  107. Many have been said and it’d be insane to repeat what have been said by my fellow countrymen and women.

    But my question will go to you MICHUZI! “Did you ever ask in your blog or article in Daily News about Mr Balali’s where about or why our leaders (Chenge etc) don’t register their overseas accounts in our embassies or ‘Tume ya Maadili?” You are very good in asking things that don’t matter so much to the national interest. Yes, we know your blog is more ‘marketing driven tool’ than a ‘really media tool’, so your focus will always be to get as much audience as possible even if by publicising controversial headings, but should show a tiny of journalism ethics!

    Here you’ve tried to con people by introducing the issue of “Kujiandikisha Ubalozini” to attract many readers but not to help these hard working Diasporas as many people might have thought. You always cover your ‘back’ in things that matter most!

    If Ministry of Foreign Affairs can’t tell Balali’s where about, why should I go to our embassies to do what you called “Kujiandikisha”?

    Am I really bothered? I don’t think so.

    ReplyDelete
  108. Tatizo ni kwamba UBALOZI wetu si hapo UK tu bali kote duniani huwa hazina faida yoyote kwa watu wake, ukionekana balozini unaonekana kana kwamba unaenda kuombaomba, pia siku za nyuma kulikuwa na element za rushwa ufanyiwi kitu hadi utozwe kitu kidogo sijuwi siku hizi, pi ni usumbufu tupu ukienda kujiandikisha utaambiwa muhusika hayupo mara hivi mara vile, huwa maofisa hawawathamini watanzania, wakienda ubalozini wanaonekana kama wasumbufu tu. Pia kuna sehemu kwenye website ya kujiandikisha lakini haifanyi kazi ukujiandikisha ukitaka kutuma haiendi ni fake tupu, pia maofisa wanajiona kama miungu mitu hivi. Mpaka watendaji wajibadilike wataona watu wanaenda kujiandikisha, watu kuzamia it is none of anybody business watu wanatafuta maisha, bongo yenye jobs hakuna mpaka uwe mtoto wa kigogo ndipo upatiwe kazi, sasa kama mtu anaweza kuzamia wacha hazamia no harm on it, pia watanzania ni watu wasiopendana, wabinafsi, wachoyo, watu wa majungu, huwa hawapendi kupata kwa mtu mwingine, huku nje watu wa nchi zingine wanaumoja wanashirikiana katika kutafuta maisha si watanzania, ni umimi tu kila kitu mtu anataka kiwe chake si cha mtu mwingine hii hali ipo hata huko nyumbani, pia kwenye hizo jumuiya za DIASPORA watu wachache wanataka kufaidika wao ndo maana watu hawazijali ni upuuzi tupu. WATANZANIA TUNATAKIWA KUBADILIKA NA TUSAIDIANE KUONDOA UMASIKINI KWA PAMOJA.

    ReplyDelete
  109. Kaka michu , naomba kuuliza hivi haya mambo ya maana tunayo ongea huku saa ingine yanafikishwa kwa watu wanaohusika wayashughulikie au kunasafisha vinywa tu ?

    ReplyDelete
  110. POTELEA MBALI HATA YAKIFIKISHWA KWA HAO WAHUSIKA KWANI WEWE UNAOGOPA NINI ,KWANI WEWE MRUNDI,MSOMALI AU MZAIRE HEHHEEEE SHAURIYENU MLOFANYA MAMBO HAYO MIMI SIMO MCHANGA WA PWANI HUOOOOOOOOOOO

    ReplyDelete
  111. sasa huku watu wanaishi wakiwa si wabongo shauri yao hao walofanya vitu hivyo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...