Kijana Ramadhani Mussa (12) ambaye jana alikamatwa na kichwa cha mtoto mwenzie na kuanza kukinyoya damu hadharani pale kwenye lango la Hosptali ya Taifa Muhimbili, alishawahi kukutwa kwenye makanisa kadhaa ya jijini Dar es salaam akidai kudondoka na ungo na kisha kuombewa na wachungaji wa makanisa hayo, lakini mara ya mwisho alionekana ni kijana tapeli tu au wachungaji waliokuwa wakimuombea walikuwa wanafanya usanii kuvutia 'wauimini'!

Awali mtoto huyu inadaiwa alikutwa usiku wa manane kwenye Kanisa la Kilutheran pale Manzese na kuombewa na Mchungaji Jonathan wa Kanisa hilo baada ya kudai kuwa amedondoshwa na wachawi wakiwa kwenye ungo, ingawa waumini wengine walimuona kijana huyo kama mchawi na kutaka kumpiga.


Baadae inadaiwa alipelekwa Hospitali ya Mwananyamala ambako nako alitoweka kimiujiza, kabla ya kukutwa kwenye kanisa lingine Tabata na hatimaye Mikocheni kwa Mchungaji Rwakatare ambako ndiko alipoombewa akiwa na mwenzake kwa muda kabla ya kuambiwa kuwa ni 'matapeli' kwani hizo ndizo zao kujifanya wamedondoka kwenye ungo na kuibukia Makanisani ili kujipatia pesa!


Akiongea na kituo cha ITV jana, Mchungaji Rwakatare, ambaye pia ni Mbunge wa CCM wa kuteuliwa, alisema "Mungu amejitetea mwenyewe" kwa kuonesha kuwa walichokuwa wanakisema kuwa watoto hao walikuwa na mapepo hawakuwa wanaongopa.


"Laiti kama wangewaachia wawaombee, yule mtoto asingekufa wala yasingetokea yaliyotokea, lakini kwa sababu kuna watu wanajaribu kuwa kama Mungu, ndiyo maana haya yote yanatokea!
"Wamuache Mungu awe Mungu", alisema Mchungaji Rwakatare na katika hili inaoenekana mtumishi huyu wa Bwana amejipatia 'tano' zingine!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. dogo kala mkong'oto mpaka katoka udenda, astahili yake shetani wee.

    ReplyDelete
  2. "Laiti kama wangewaachia wawaombee, yule mtoto asingekufa wala yasingetokea yaliyotokea, lakini kwa sababu kuna watu wanajaribu kuwa kama Mungu, ndiyo maana haya yote yanatokea!
    "Wamuache Mungu awe Mungu", alisema Mchungaji Rwakatare Mchungaji/Member of Parliament.


    What ????

    I think Mr. Rwakatare you should resign your post as priest from your own congregation, you are not good enough, you could not get rid of the child' demons from the first place, you had your chances you failed it numerous times, including your fellow priests of other churches.

    I think your comments are insult to your own faithfull congregation, the church and most importantly the victim of this crime.

    I think you should concentrate praying for MAFISADI in parliament in Dodoma, they have more devious DEVILS and bad intentions in their head, than the psychiatric problems of this kid.

    I think you should leave it to the investigation of police and doctors to assess the psychiatric problems of this child, than your ill comment CCM radical.

    You groomed him, by acting demons inflicted kid, for the name of religion and he acted for REAL, and now you are accuse everyone.

    By Mchangiaji.

    ReplyDelete
  3. Wadau mimi huwa nasikia hawa waruka na ungo usiku huwa wako UCHI WA MNYAMA yaani kama walivyozaliwa sasa huyu Mtoto mboni kavalia shati zuri tuu na Tracks kazitoa wapi? ama Wachawi wa siku hizi wameendelea na wanakwenda na wakati na hii globolaizesheni? na swali langu lingine ni kwamba je huyu mtoto tunaweza kumkodisha na usafiri wake ? kwa maana mimi niko huku Ukerewe nabeba maboksi kama kawa na ningependa sana kuja kutembea kidogo nyumbani sema Nauli kwenye BA noma sasa anaweza akija huku na ungo wake akapata biashara sana kutuvusha watu overnight kuja bongo bila ya kusumbuliwa na eapoti officer wala nini , jamani wadau wenza dili hilo mtafute huyu mtoto na mama yake na kampuni yao kwa ujumla tuwauzie at least wataacha uchawi wafanye biashara ya maana badala ya kukaa nyama za binadamu !! Duu lakini hiyo noma ... Anyway hayo ni mawazo yangu tuu

    ReplyDelete
  4. Amen Mama Lwakatare mwacheni mungu aitwe Mungu!!jamani kumsema vibaya mtumishi wa mungu ni dhambi kubwaa,mamalwakatare alisema ukweli na magazeti yakamsema vibaya,ohh tapeli,ohh anataka ujiko..Sasa kiko wapi!!mtoto si huyo kweli mchawi..Mama Lwakatare Mungu akubariki mama...L.kyekue

    ReplyDelete
  5. Sasa kama kashaombewa na makanisa yote hayo kwanini haponi au haachi hou uchawi (kama ni mchawi)

    Huyu mtoto yawezekana na matatizo ya akili tuu na anatakiwa atibiwe.

    ReplyDelete
  6. ACHENI MUNGU AITWE MUNGU!WATU WASIWADHIHAKI WATUMISHI WA MUNGU!Maana MUNGU anaongea na watu wake kupitia watumishi wa MUNGU!Hata wakati wa MUSSA!MUNGU aliongea na MUSSA na hakuongea na wana wa israel wote!kwa hiyo basi TUWASIKILIZE WATUMISHI WA MUNGU!Maana MUNGU anaongea nasi kupitia wao!

    ReplyDelete
  7. Mimi nadhani huyo mtoto ana matatizo yakili. Wachawi wanakwepa sana makanisa.Kwanini kila wakati anaenda makanisani labda anamtafuta mungu kweli kweli.

    ReplyDelete
  8. ok, tuambie basi lini ananyong'wa

    ReplyDelete
  9. HAPO ZAMANI MJENGWA ALIANZISHA TOPIC YA KUKANDIA MAKANISA KUHUSIANA NA HUYU MTOTO . SASA HAWEZI HATA KUPOST HABARI HII.

    MJENGWA ANA WEAK PERSONALITY. HAKUBALI KUKOSEA .

    ASANTE MICHUZI KWA UPDATE .

    ReplyDelete
  10. Kwa kweli inasikitisha sana.Kijana anahitaji psychiatric help. Huyu kijana kwa umri wake hana capacity ya kufikiria matokeo ya vitendo vyake. Na ni watu wazima ambao huharibu mafikira ya watoto wadogo au vijana,kwa kwalisha information za kijinga.
    Dunia ya leo imeharibika, na wazazi lazima mue waanglifu na watoto wenu wadogo, mjue wanacheza wapi na wanaongea na nani wakati wote.
    Usiache mtoto wako acheze mtaa wa nyuma na hayuko mbele ya macho yako.Jirani yako mwema anaweza kuwa mbaya wako, daima mtoto mdogo lazima uwe unamuona wakati wote anapocheza, na kufundisha watoto wetu kuto ongea na watu ambao wewe mzazi huwajui.
    Its all about the saftey and well-being of our children. Tusisubiri mpaka mtoto anapoteza maisha yake ili tujifunze. Take care of your children, ndiyo maana tunaitwa wazazi.

    Social Worker

    ReplyDelete
  11. hi michu,mi hii habari ilinisikitisha sana....lakini sitaki kuamini kama huyu mtoto ni mchawi,kwanza kwa nini akiwa anawanga apite maeneo ya kanisani makusudi ili adondoke na wakati wachawi wenzake hawapitagi huko?pili na alivodondoka kwa rwakatare alikua na nguo sasa how alipanda ungo na nguo na wakati sio sheria yao?tatu amekamatwa na kichwa aha mtoto muhimbili then akakitoa hapo hapo na kuanza kukitafuna jamani hata kama ni mchawi kweli huwezi kufanya hivo mbele za watu...sikatai wachawi wapo ila huyu mtoto sio mchawi..wala nyama za watu wapo ila hawawezi kula hadharani ki hivyo
    nne huyu mtoto alisema anaenda kumpelekea shangazi yake hicho kichwa je waliomba awapeleke awaonyeshe huyo shangazi ake humo ndani? ah mi siamini bado!
    tano na la mwisho katika maelezo ya huyu kijana alisema yeye kachukua kichwa tu ila vipande vya mwili vingine amewaachia wenzake kila mmoja kagawana kivyake huko...sasa ishu inakuja mbona kiwili wili cha mtoto kilikutwa huko tabata tena chooni na hakikuwa kimekatwakatwa kama alivodai huyo mtoto kwamba wenzake wamegawana.
    huo ni mtazamo wangu,najua uchawi upo ila huyu ramadhan sio mchawi bali ni mtukutu na ana roho ya ukatili ndani yake na huenda ana pepo mchafu.
    sasa mtaona kitakachoendelea,kwa keli hii mbaya sana,mdau ritha.

    ReplyDelete
  12. huyu anonymous namba mbili ana chuki binafsi na lwakatare,anafikiri swala la maombezi ni la sku moja,hata ukiombewa leo halafu kesho ukarudia matendo yako ya zamani hakusaidii utabaki vilevile,huyo mtoto angeachwa kanisani watu wamtunze kiroho,THIS IS WARNING KWA WOTE WENYE TABIA YA KUWATUKANA WATUMISHI WA MUNGU, MUCH IS COMING

    ReplyDelete
  13. humu ndani wachawi kibao lazima wateteane

    ReplyDelete
  14. Jamani naona wengine tunabwabwaja hapa pasipo kujua kazi iliyopo ya kumfungua mtu aliyekwisha jikabidhi/kabidhiwa na kutumika kwa shetani. Si kazi ndogo na inajumuisha mambo mengi. Ni mapambano ya nguvu hasa maana shetani kamwe hayupo tayari kuachia mateka wake kirahisi. Hyu kijana mara zote alizodondokea makanisani muda waliopata watumishi kukaa naye ulikuwa mdogo sana, sana umeweza kumrudishia akili yake ya kibinadamu lakini bado hajakombolewa toka kuzimu kwa hiyo bado anatumika na shetani. Na naamini ni kwa maombi haya ya mwanzo ndyo maana mara kwa mara anakamatwa/umbuka anapokuwa katika shughuli zake za kichawi. Huyu si kichaa wala hana tatizo la akili, ni mtumishi wa kuzimu na kazi kubwa ya maombi inatakiwa. Kinachotakiwa ni ushirikiano wa wote, wazazi, waamini, watumishi wa Mungu pamoja na vyombo vyetu vya dola na serikali. Uchawi upo na watu wengi kwa kujua au kutojua wanatumika kuzimu jamani. Tufungukea jamani mambo haya ni ya ulimwengu wa kiroho na pasipo watu kukubali msaada/mwongozo wa roho mtakatifu itakuwa ngumu sana kumsaidia hyu kijana na ataendelea kufanya uharibifu zaidi na zaidi. Tuache kubisha vile ni Mama Lwakatare kasema.

    ReplyDelete
  15. Jamani ee, uchawi upo hata kwenye vitabu vya dini kumeandikwa. Inawezekana kabisa mtoto huyu kuwa mchawi. Kuanguka maeneo ya makanisa si jambo la ajabu kwa kuwa popote kulipo na nguvu za Mungu, hapafai kwa wenzetu hao(wachawi). Inawezekana wenzake kwa kuwa ni wazoefu wanajua jinsi ya kujikinga ndo maana hawaanguki. Suala la kwamba Ramadhan hana akili sawa sidhani kama lina ukweli kwa kuwa madaktari waliomchunguza walikiri kuwa ana akili timamu. Pia, kutoa kichwa na kukitafuna hadharani inawezekana ni kule kuweweseka, pengine alikiuka masharti yao akajikuta anafanya vitu ambavyo hakutarajia, au ni MUNGU kaamua tu itokee hivyo ili uwe mwanzo wake kuokolewa katika kifungo hicho. Aidha kuhusu kuombewa na kutoacha uchawi si jambo la dakika moja, hilo ni tatizo kubwa hivyo yahitaji muda na maombi kikwelikweli. Watumishi wa Mungu waachwe wafanye kazi yao bila kubughudhiwa na nina hakika watafanikiwa kumwokoa kijana huyo. Mungu si wa kuchezewa hata kidogo na hakuna linaloshindikana kwake. Tumeona wengi tu wakiokolewa kutoka katika vifungo mbalimbali.

    ReplyDelete
  16. anony wa 6
    ;42pm kwa sisi wakirsto tunaamini mtu anapoamua kuacha madhambi yake na kutubu inatakiwa amaanishe kabisa,mfano mchawi au mtu mwenye mapepo kama ataombewa hata kama mara milioni kama hajaamua kuteketeza zile zana alizokuwa anafanyia kazi mfano hirizi n.k huyo ni sawa na hakuna lazma mapepo yataendelea kumwandana siku zote,ataombewa lkn kutakuwa hamna badiliko lolote.huyo ni mchawi wala hana tatizo la akili.
    Ms Bennett

    ReplyDelete
  17. alikuwa anambip Mungu,sasa Mungu kampigia

    ReplyDelete
  18. MBONA KWENYE GAZETÄ° WAMEANDÄ°KA ANA UMRÄ° MÄ°AKA 18 ? UKÄ°LÄ°ACHÄ°LÄ°A MBALÄ° HÄ°LÄ° SWALA SÄ° DOGO Ä°NABÄ°DÄ° JAMÄ°Ä° NZÄ°MA YA KÄ°TANZANÄ°A TUTAFUTE UFUMBUZÄ° WA TATÄ°ZO HÄ°LÄ° KWANÄ° KTK MAHOJÄ°ANO YANAYOFANYWA NA POLÄ°SÄ° NA WAHUSÄ°KA ,MTUHUMÄ°WA HUKU AKÄ°ONGEA KWA UJASÄ°RÄ° ANADAÄ° ANAMÄ°LÄ°KÄ° VÄ°CHWA VÄ°NGÄ°NE 50 NA KAMWE HATOACHA HÄ°Ä° TABÄ°A,NA NDO MANA KTK NCHÄ° NYÄ°NGÄ°NE HUKU UGHAÄ°BUNÄ° WANAAMÄ°NÄ° WAAFRÄ°KA WANAKULA NYAMA ZA WATU NA SÄ°E TUNAKANUSHA TUKÄ°JÄ°TETEA KUWA NÄ° STORY ZA KWENYE MOVÄ°E LKN KUTOKANA NA MATUKÄ°O KAMA HAYA UKWELÄ° UNAJÄ°DHÄ°HÄ°SHA TARATÄ°BU

    ReplyDelete
  19. WAJIDAI KUSEMA KUWA YULE MTOTO ANAUPUNGUFU WA AKILI NI WANAFIKI. TUNAPISHANA NA VICHAA WANGAPI BARABARANI MBONA HAWACHINJI WATU ANGALIA YULE ANAYEKAA LANGONI MWA KUINGILIA OCEAN ROAD HOSPITAL KAJIPAKA UDONGO MWEKUNDU USONI MVUA JUA YUPO PALE YULE NDIYO KICHAA AU ANAUPUNGUFU WA AKILI LAKINI HUYU MTOTO/LEO WAMESEMA ANAMIAKA 18 HEBU ANGALIA ANAWEZA KUWA KIBABU MAANA HAWA WATU NI HATARI ANAWEZA TEMBEA UCHI WE UKAONA AMEVAA NGUO, ANGALIA NYUMBA WANAYOISHI NI FULL SUTI MABATI LAKINI HAWATUMII UCHAWI WAO KUJIKOMBOA KIUMASKINI. WATANZANIA TUAMKE SASA UCHAWI UPO UPO NA NDUGU ZETU WENGI WANAMALIZIKA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA. ANGALIA IDADI YA WATOTO NA WATU WAZIMA WANAOPOTEA DAR SIKU HIZI IMEONGEZEKA TUNASIKIA TU WAMEPOTEA LAKINI WAKIPATIKANA HATUPATI TAARIFA KWA HIYO TUNAAMINI HAWAJAONEKANA. POLISI CHUKUENI HATUA ZILIZOTHABITI JUU YA KIJANA NA FAMILIA YAKE KWA UJUMLA ANAWEZA KUYEYUKA KAMA ALIVYOPOTEA SEHEMU ZINGINE

    ReplyDelete
  20. Mwacheni MUNGU aitwe MUNGU

    "For the power of the wicked will be broken,
    but the LORD upholds the righteous". Psalm 37:17 au Zaburi 37:17

    ReplyDelete
  21. Ebwamna huyo mtoto wajaribu kumdadisi vzr aseme ukweli

    ReplyDelete
  22. Hakuna cha tatizo la akili. Huyo ni mchawi mnoooooooooo tena wakifanya mchezo atawapote hata huko polisi. Tena huyo ni Agent wa kuzimu kabisa inaelekea anavyopita juu ya makanisa anataka kushindana na nguvu za Mungu matokeo yake anakutana na nguvu iliyokuu kushinda yote ambayo ni ya Bwana Yesu Kristo ndo maana anatunguliwa. Usifanya mchezo na Mungu bwana. Hao wanaosema anatatizo la akili sio kweli. Rev. Rwakatare Mungu akutia nguvu na akushidie uzidi kuwatoa wachawi na kuwafungua misukule. Hizi ni nyakati za ishara na miujiza kwa kizazi hiki cha wasioamini nguvu za mungu. Tunakuombea Mungu Mchungaji Rwakatare Ukapambane na mifisadi huko Bungeni.

    ReplyDelete
  23. Hakuna mgonjwa wa akili anayekula vichwa vya watu,huyu na uhudini wake,yuko chini ya ulinzi na auwawe.Kill this kid please,i don't belive his story,first lesson to all who think this is a good idea to get fame.Kill this monster,one bullet will do the magic,please aim for the heart.Trust me bible won't cure this monster in human face.sorry the Bible was not designed to cure this kind may be try the other book or may be if you use real catholic rituals (extocists)

    ReplyDelete
  24. Mnajimu Maarufu Afriuka ya Mashariki na Kati, Sheikh Yahya Hussein anasemaje hapo kuhusu hili?
    Mishuzi hebu mtafute atumwagie nondo zake humu?
    Namwaminia sana yule

    ReplyDelete
  25. Anon wa 4.57 you must learn to think and not be among those who can't think and they are normally driven by opinon.
    Inawezekana kabisa fikra zako hizo ni "convetional wisdom" from your roots...mama rwakatare anayoyasema ni kweli...inapofika mambo ya imani watu wenye mlengo tofauti hujifanya kuwabeza wanaotaka kutoa msaada kama wa maombi vile eti kwa sababu wao hawaamini katika hilo..lakini kwa mtu mwenye busara na asiye fuata imani za kucopy na kupaste kutoka kwa waliomtangulia, atatumia hekima yake kuangalia ukweli uko wapi na kuufuata.
    You don't need alot of intelligency and gess work in this...watu wameombewa na wakapona na hilo limeandikwa kwenye vitabu vitakatifu...mama Rwakatare anavisoma na anajua hekima iliyomo..wewe unabisha tu kwa sababu hujihangaishi na kuvisoma na hivyo unabeba yale mambo ya kizamani uliyoambiwa na ..."convetional wisdom" ya kwenu huko.
    Books are for reading my dear...tafuta ukweli kwenye biblia au Msaahafu na utayakuta yote haya..yanafanyika na Mungu ni mkuu...na Rwakatare anaposema mwacheni Mungu aitwe Mungu hajakosea...hatuhitaji kuendelea kupoteza innocent kids like Salome just because ya uzembe wa kuyasoma na kufuata maandiko.
    Unabisha kwa sababu hutaki kuelewa na utakapokuja kufuatilia utakuta kuna milllions of souls tunazozipoteza kwa sababu ya kutojua neno/ kwa kukosa ufahamu.
    Mungu isaidie Tanzania, na mungu msaidie Rwakatare huko aliko kwani wapinzani wake ni wengi.

    ReplyDelete
  26. Please Mr mchuzi tunaomba tuwekee habari zote za huyu mbwa mwitu aliye mchinja maraika wa mungu,tunata haki itendeke,kama huo uchawi wao tuone basi.haukumiwe kunyongwa na yeye pia.

    ReplyDelete
  27. basi hapa kila mtu atajifanya anajua

    ReplyDelete
  28. jamani huyu Mungu mwacheni aitwe Mungu kwani huyu kijana kasha ombewa wapiii!!! pelekwa hosp wapi!!! jamani ile sheria ya kunyongwa ipo kama ipo basi naomba itumike.
    Sweet.
    Arusha

    ReplyDelete
  29. Samahani najua wengi mtashangaa nikiwaambia kwamba huyu mtoto si mchawi. Sijui kumuita kwa kiswahili ila kingereze ni excessive compulsive behaviour. Watu wengi wanaofanya vituko huanza na dalili za kawaida na watu hawashituki (kama kujificha kanisani). Moja huyu mtoto anapenda atention na anatamani asifiwe mtaani ndo maana kafanya vituko vingi. LKosa ubwa jamii haikutilia maanani nd maana kapaaribu na kila mtu anadhani mchawi.
    moja ya swali la kujiuliza anadai yeye na mama yake wachawi alafu yeye ni kiongozi. Mnajua mila za kiafrika thats impossible. Technicaly he is a serial kiler on the making and should neverbe late loose. Killing someone make him feel in control he will do it again whenever he has a chance..

    ReplyDelete
  30. Ukifikiri sana inatisha. Je kama huyu mtoto labda naye ni victim aliyeibiwa kwao na sasa anatumika bila kujijua na wazazi wake wa kweli wanajua alishafariki akiwa mdogo? Usishangae yule binti labda naye hakufa siku moja akaibuka huko na yake. Itabidi kufukua kaburi every year. Inahitajika hisoria kamili hapa hasa kuwabana huyo bibi yake, wazazi na jamaa zake. Na kama wako responsible na ushirikina na kusababisha kifo cha yule binti basi nao waishie jela. Wazungu wanaita Guilty by Association

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...