Distinguished Fellow Tanzania and All Africans in the Diaspora.

It is with great happiness, and enthusiasm that I send warm greetings to you and your family. I do wish many blessing to your family’s health, wealth, progression at work, and all aspects of your life as I am corresponding to you.


Please consider this letter as a special invitation to meet and talk with our Distinguish member of parliament (Mbunge Kigoma KasKazini Mr. Kabwe Zuberi Zitto) who will be in town on his tour organized by the STATE DEPARTMENT.


I would also like to express my deepest appreciation From the Honorable in accepting our short notice Invitation to come and seat down for a Dinner format meeting where most of us would like to know what’s going on back home with all the political commotion, as far as our domestic and foreign affiliation is concern.


In doing so, I pledge to all Tanzanian who would like to meet the Honorable leader to come on time, as he will be arriving by plan at 4.30pm and we will like to start our short meeting by 5.30pm so he can be back to his hotel by midnight.


He will be here for one day tour in Michigan. My prayer is that our continue success in building a unified Tanzania community.


Please feel free to contact myself or any board members with information or suggestions. My hope is for continued blessing for you and your family.



DAY ; SUNDAY 5/04/08

TIME :5.30PM SHARP

PLACE: MFINANGA
RESIDENCE

Sincerely,

Mr. Ayub Mfinanga
Chairman, TAMI.
586-354-5479

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 58 mpaka sasa

  1. CHONDE CHONDE WANA MICHIGANI NA WEZENU HUKO MLIKO.MSIKUBALI PEPO LA KUFUNGUA MATAWI YA CHAMA. TUDUMISHE UMOJA WA KITAIFA HAYO MATAWI TUWAACHIE TUU HAO WANATHIHIEM WA LONDON.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 01, 2008

    Jamaniee hebu tumieni kiswahili kuliko kuhangaika na lugha ya watu. Kwani hao wanaotaka kukutana na huyo Kabwe ni wazungu au waswahili? Na huo mkutano mtaongea kwa kiinglish au kiswahili. Huwa nasikiaga kichefu chefu pale watu wenye lugha yao tena nzuri wanaponga'nga'nia kuwasiliana kwa lugha ya wenzao, hebu tuwaige wachina na wengineo wanaothamini lugha zaa. Mwe!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 01, 2008

    Hebu mmoja na amuulize mheshimiwa suali hili, jee safri yake na alipofikia imegharimu serikali kiasi gani? jee kiasi hicho cha fedha kingelisaidia mangapi kama zingelitumika nyumbani kwa waliomchagua walala hoi? kuna jipya gani atakalotwabia ambalo hatujawahi kulisikia kiasi kwamba afunge safari kuja huko?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 01, 2008

    Safari yake imegharamiwa na serikali ya Marekani kwa kupitia sijui kitu kinaitwa Young leaders, blah, blah, blah! Kwa hiyo serikali haijatoa hata senti tano kapata udhamini kupitia ubalozi wa marekani kama sikosei atakuwa alijaza mwenyewe fomu kuomba huo udhamini. Mie kwenda kwake huko kwa kuwa ameenda kama ziara ya mafunzo wala sina shida naye kuhusu hili. Linalonikera ni hilo la sie weusi kutothamini chetu, sasa huo mbarua wewe matatizo ya grammer humo nani unamwandikia mzungu au mswahili? Hivi kwa nini bado tunapenda kutawaliwa kifikra. Ni lini nyie watanzania mlio nje (sio wote baadhi yenu) mtaacha kudharau lugha yenu na kuanza kuithamini. Wakenya wanafaidika na kufundisha kiswahili huko nje, nyie mmeng'angana yes yes mzungu wa wales kala mafenes!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 01, 2008

    Naungana na anony wa pili hapo juu kuhusu suala la kutumia lugha za watu halafu lugha zenyewe za kujifunzia ukubwani!Nchi nyingi tu wanatumia lugha zao kuwasiliana hivi huyo mwandishi alikuwa anamtangazia nani? Au alitaka wamarekani nao wajue kuwa kuna mgeni 'muhimu' huko! Inaboa sana na hasa lugha ikilazimishwa mana inapoteza ladha! na haileti hata appetite kuisoma! Tujikwamue kifikra jamani kuwa na akili au kuonekana umesoma si lazima kujua Kiingereza tu!tujivunie lugha yetu!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 01, 2008

    Nilipoanza kuisoma hiyo barua baada ya kuona picha ya mheshimiwa nikafikiri yeye ndiye aliyeandika nilianza kujiuliza!Mh badae nikaona kumbe si mheshimiwa mwenye picha ila mheshimiwa mwingine! Jamani lugha ya Kiswahili mbona nzuri tu! kusema la ukweli hilo tangazo halivutii!sijui kama mhusika ulilirudia kulisoma!Haya tunashukuru ujumbe umefika!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 01, 2008

    Jamani hata Kiswahili chenyewe wengine kinatushinda na hata humo tutatafuta makosa. La maana ni kuwa ujumbe umefika; mnakaribishwa wale mlio maeneo ya "The D".

    Tumaini, sijui ni wapi umepata wazo la kufungua chama, Zitto anakuja kutembea kama mbunge wa Tanzania na mkusanyiko huu siyo wa chama au itikadi. NI Watanzania kukutana na mbunge wao.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 01, 2008

    Lugha rasmi Tanzania ni Kizungu na Kiswahili kila mtu ana uhuru wa kuandika lugha anayoitaka. Nyie mnaojifanya wazalendo mbona hamkuja na na wazo lenu jipya badala yake mnatoa mifano ya China na nchi zingine sijui kenya wanafundisha ugoro gani!

    Kama kweli nyie ni wavumbuzi msingalitoa changamoto ya kuwaiga waChina au hao wamatiafa wangine, kujeni na wazo lenu ili na nyie muigwe.

    USIMWAMBIE MWENZIO ANA CHONGO WAKATI HUJATOA BORITI NDANI YA JICHO LAKO.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 01, 2008

    Kwani kutumia lugha aliyoitumia kuna kosa gani? Sijaelewa mnacholalamika ni nini haswa maana kama ujumbe umefika na mmelewa. Kila mtu ana uhuru wa ku-communicate kwa lugha ambayo mwenyewe anaona yuko comfortable. Pia ujumbe huo unaweza kuwa umelengwa kwa waAfrica wengine waliopo hapo. Ndio maana akasema, "and all Africans in the Diaspora." Sio kwamba kila mtu mwafrika anaongea kiswahili na pia kama alivyosema wanakaribishwa wote wanataka kwenda. Sasa kabla hamjaanza kulalamika inabidi muelewe content ya ujumbe wenyewe na pia kutumia lugha za wenzetu sio kosa la jinai. Na hii fikra kwamba mtu ukitumia lugha za watu basi unakuwa kama mtumwa ama brainwashed ni fikra zilizopitwa na wakati. Mtu ana uhuru wa kutumia lugha yeyote ile hata angeandika kipare as long as yuko comfortable.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 01, 2008

    Ni kweli kabisa walalamikaji kuhusu lugha wana hoja. Bwana Mfinanga umeboa kweli. Hicho kiingereza chako ungewaachia watoto wa shule ya Uhuru!

    Pendekezo kwa Michzi: Je, inawezekana kuifanya blog "yetu" kuwa ya kiswahili tu isipokuwa pale ambapo ni lazima kama vile nyaraka za muhimu zilizo kwenye lugha tofauti na nukuu ambazo lazima ziwe kama zilivyoandikwa. Maana kwa kweli hii lugha inatia kichefu-chefu sasa.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 01, 2008

    Nyie wote hapo juu... huyo mtu kaandika kuwajulisha kinachoendelea sasa mna kaa kumsema angeandika kwa kiswahili... nyie wote ndio mna onekana "wajinga"... English, " y'all looked uneducated people and embarrassing our NATION"

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 01, 2008

    Swala hapa sio lugha. Swala ni usahihi wake. Ninyi mnaotetea kwa kujifanya kwamba mko educated hiyo lugha iliyotumika hapo ni ya mtu educated hiyo? Nyie si ndio mnaokimbia hapa kwenda marekani kama mnaosma kumbe mnazunguka tu kuiga ujinga wa ma-black. Na dalili ya kwanza kabisa ya mtu yeyote mbaye hajafika shule ni kujifanya educated.
    Huyo mtu aliyeandika tangazo, ameandika kama kiongozi wa jumuiya ya watanzania, Michigan. Kama anatumia lugha ya kiingereza au kiswahili lazima aandike kwa ufasaha na usahihi kama kuna makosa ya kizembe watu wanayo sababu ya kulalamika kwa sababu anawakilisha jamii ya kitanzania ya walioelimika na wasioelimika kama nyie mnaotetea.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 01, 2008

    Kwani kuna uhusiano wowote kati ya kuwa educated na kuandika kiingereza?
    Hapana isipokuwa kuna malimbukeni wanaofikiri kwamba ukiandika au kuzungumza kiingereza maana yake umekwenda shule. Ndio kama huyo anon wa 7:30 ambaye ukisoma maandishi yake tu unajua hamna kitu mukichwa.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 01, 2008

    we anon unayesema watu wanaenda marekani hawasomi wanakalia kuiga ma black,una chuki binafsi...watu wengi wanaoenda marekani wanasoma na kufanya kazi ambazo zinawasaidia hata ndugu zao walioko bongo...wote mliokalia kumkosoa mwandishi wa hilo tangazo mnapoteza muda..mi sielewi,kwani hamjaelewa tangazo au?ujumbe mmeupata sasa mnalalamika nini?hata kiswahili chenyewe siku hizi kimearibika,maneno ya mtaani eti ndo mnaita kiswahili,mbona msiende kuwakosoa hao ka mnajifanya vifimbo cheza??ovyooooooo....

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 02, 2008

    Nadhani hawa kina anons watakuwa wameelewa. Ujumbe ni kuwa tunawakaribisha wale wanaotaka kuja kukutana na kusaliana na Shujaa wa Buzwagi, Mbunge kijana kupita wote wa kuchaguliwa toka Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

    Karibuni.

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 02, 2008

    Nyie kweli mna matatizo. Hicho kiingilishi kina tatizo gani? Ajitokeze basi bingwa wa lugha anioneshe makosa yako wapi maana mie naona mwandishi ametumia kiswa-nglish safi kabisa.Swahili Grammar inaweza kutumika kueleza kitu kwa maneno ya lugha nyingine. Sasa mlitaka aogope hadi lini? Yeye mwenyewe hadi akapata kibali cha kufanya kazi sijui kusoma huko kwa kaka Bushi alifanya language test sijui wanaiita Tophili kama jina la mjomba wangu na akafaulu kwa points zaidi ya 6.5? So ni bora tuongelee theme ya ujio wa huyu mheshimiwa badala ya kumjadili huyu mtendaji wa tawi sijui la CCM au la Chadema ya mheshimiwa Zitto.
    na 'Cheusidawa'

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 02, 2008

    Jamani napenda kiswahili kweli. Kaka naomba urudie tangazo hili kwa kiswahili please. Wengine english is not reachable you know. Basi wasikukosoe sana tusaidie sie waswahili ambao kwa kweli hatujaelewa chochote hapo. Mie nimeambulia neno Zitto Kabwe na Chicago tu.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 02, 2008

    jamani kunavitu vingine huwa vinachekesha sana, haswa pale watu wanapo vipa uzito vitu visivyo na umuhimu huku wakiacha vile vyenye umuhimu.
    jamani cha msingi hapa kwa mtizamo wangu ni kwamba ujumbe unafika au haufiki?maana kama ni swala la kukosoa lugha, utajikuta unakosoa hata kiswahili chenyewe unachodhani unakifahamu, mimi binafsi kiswahili sekondari kidato cha nne nilipata daraja c, wakati kiingereza nilipata A. sijisifu kwakuwa japo sikifahamu kiingereza sana maana sio lugha yangu ya kuzaliwa,lakini wengi wetu humu na kwingineko tunabofoa tu,kwa maana hiyo wala msiwape pessure watu kuhusu lugha anayotumia,nimesoma na watu wa nchi mbalimbali nako taabu ni ileile tu,wanabofoa wengi wao pia kama wabongo tu! zamani nilikuwa naongea na kuandika kiingereza kwa ufasaha lakini sikuhizi najikuta pia hata manenomengi yamenitoka,na spelling ninakosea sana tu! nahii nikutokana na ukweli kuwa nimekaamuda mrefu nikisoma na kuongea kwa lugha nyingine tofauti na kiingereza, lakini hii hainifanyi mimi kutokuwa nimekwenda shule. maana achilia utaalam nilio nao ktk fied yangu, pia nafahamu lugha nyingi tu, kiasi kwamba naweza kutafuta usahihi halisi wa neno fulani toka ktk original language lilikotokea na kulitumia kwa misingi yake.
    naomba tu niseme tusiwahukumu watu kwa grammer yao,cha msingi tuwe tuna angalia theme tunayozungumzia ni nini na ujumbe je umefika?maana kwa sasa hata mimi siwezi kujuwa ni lugha gani naifahamu kwa ufasaha,maana si kiswahili,si lugha ya baba wala si ya mama,si zinginezo takribani 10 za mataifa mbalimbali, naza ndani ya tanzania takribani 30.lakini kwakuwa mimi sio linguist iam not guilty for not being perfect in languages, wha i do care is that the intended message has reached the targeted audience!!!!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 02, 2008

    Proper English jamani. Ni distinguished, siyo distinguish. Na ni "to all Tanzanians" plural kwa sababu ya wingi wa noun Tanzanians. Kuongea kiingereza SIO KUJIFANYA MZUNGU. Ndio maana tukija huku lugha inakuwa shida...

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 02, 2008

    Yooh man relax! Men! niandike kiswahili no way, kiswahili no please kutakuwa na tofauti gani kati yangu mie niliye States na aliye Bongo, men kiswahili, siwezi kuongea sawasawa kinanishinda, I can't write it men!

    Niko States sio, nikiongea kiswahili nitachafua mdomo!

    Ujinga mtupu, hata hicho kiingereza chenyewe hamkijui, kiswahili ni lugha ya taifa, tena ni lugha ya kiofisi, kama unatuma ujumbe kwa ajili ya jamii ya kitanzania tumia kiswahili. Acheni kujidai na kiingereza cha kujulia uzeeni, ala, thamini chako japo kibaya. Tena hii tabia ngoja leo niseme, utakuta mtu anachangia mada humu kwenye blogu, tena mada yenyewe ya kiswahili, watu wote wanachangia kwa kiswahili, utakuta mtu kaandika mchango wake kwa kiingereza, sasa huwa nashindwa kuelewa hivi ukinadika huo mchango kwa kiswahili akili haifanyi kazi au? au umedesa hayo mawazo mahala sasa inakuwa ni kuja kubandika tu humu kwenye blogu. Tukija huo ujumbe hapo juu, ni bora uandika kwa lugha unayoijua kuliko kuandika kwa lugha usiyoijua kiingereza cha kuongea ni tofauti na cha kuandika. Mtakalia hivyo hivyo yeah men< I wanna this I wanna that. Na hapo watoto wenu wakiwa wakubwa hawajui hata hicho kiswahili cha kubabia. Na aliyewadanganya kuzungumza kiingereza ndio kuwa educated nani huyo? Kama ni hivyo kusingekuwa na shule na vyuo katika nchi za watu wanaozungumza kiingereza maana ndiyo lugha yao sasa elimu ya nini? Pumba!

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 02, 2008

    I dont know about you but mimi naota kwa kiingereza kwasababu wabongo wala so wengi nilipo na nishajiolea mnugu. Ashakum is not cursing lakini mimi sioni tatizo la hiyo taarifa to be in English.
    Wabongo tuachane na milawama na tujitokeze in hundreds tumsikilize young blood what he got to say about what it do back home.

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 02, 2008

    hao wanaopiga kelele ya kiingereza ni darasa la saba bongo. Curricullum hairuhusu masomo kwa umombo na ukimwaga umombo basi wewe ushaelimika.
    Huo ni ulimbukeni wa bongo mbona kuna wabongo waliosomea maeneo mengine ambayo hicho kiingereza hakitumiki je tuseme hao hawajaenda shule.
    Sarungi kasoma urusi.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 02, 2008

    Wabongo mbona tuna stress za ajabu? Tatizo liko wapi ujumbe unawahusu watu waliokuwa michigan wengine from no where wanaingilia kuanza kutafuta kukosoa.acheni waliopewa ujumbe watajua wenyewe watu kibao hapa wanatuma maoni yao kwa english au kiswahili, ujumbe kama hujakufikia ujue haukuhusu na sio lazima kila kitu mtoe comments jifunzeni kusave energy kama hio habari hapo kama hauko michagan una hiruka tu nenda kwenye habari nyingine ambayo unaona inakuhusu kwa karibu zaidi.
    Mdau katoto

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 02, 2008

    WATANZANIA WENZANGU MNANIANGUSHA JAMANI KABLA ATUJAKOSOA TUJARIBU KUANGALIA VIZURI.HUYU MTU HAJAKOSEA KUTUMIA ENGLISH KWANI LENGO LA UJUMBE WAKE KUWAFIKIA WAAFRIKA WOTE SIO WATANZANIA TU, " to all tanzanians and africans " .TATIZO TUNA PAPARA SANA YA KUKOSOA NA KUJIFANYA TUJUA~SANA NDIO MAANA TUNASAINI MIKATABA MIBOVU KILA SIKU.
    Zitto kabwe supporter tawi la manzese.

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 02, 2008

    this´s box hang-over! tabu kweli kweli.. na hawa ndio wabongo halisi, ubishi hadi kaburini! duh. pole mtoa tangazo ulie mwalika mh. kabwe nyumbani kwako! nadhani kama mna jumuia ingekuwa bora zaidi kama jumuia ingekodi ukumbi.. ni ushauri tu msinigombanie kama mpira wa kona, tena mechi ya jana!

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 02, 2008

    WOTE NAARIKWA NA KARIBUNI SANA JAMANI.
    By MANUMBU

    ReplyDelete
  27. MWANAKIJIJI HIVI NI KWELI HUNA TAARIFA KUNA MATAWI YA CHAMA CHA THITHIEMU YAMEFUNGULIWA HUKO LONDON NA INDIA? NI YA WARAKA WANGU NIKUONYA TABIA HIYO ISIIGWE. KIKAO KITAFANYIKA NA HUWEZI KUJUA MAWAZO YA WAUDHURIAJI. THIS IS JUST PREEMPTIVE STATMENT(YA KUTUEPUSHA NA HAYO)

    TUMAINI GEOFREY

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 02, 2008

    TANZANIA LUGHA YA KIINGEREZA HAIPANDI HATA KWA WALIOMALIZA CHUO KIKUU, LUGHA YA KISWAHILI NDIYO KABISA AIBU TUPU KWANI IMEKWAMA KWENYE BOMBA, KILA KITU BOMBA, R, L, na DHA, NI MFANO TU WA MANENO YENYE UTATA MTUPU KUANZIA CHEKECHEA MPAKA CHUO KIKUU. MAMBO YOTE POA.

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 02, 2008

    People are just haterz, what diference does it make? Tangazo ni kwa watanzania waishio USA, and not Keko au Kimara. So, plz chill out. Let USian do their thing's.

    Third worlders always worries about small things. Kingreza au kiswahili doesn't make any difference. WE ALL LEARNERS, and mistake is part of learning, so you quit pointing fingure on stupid staff.

    Thanks
    Mdau wa USA Shina #1

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 02, 2008

    Hii inasikitisha sana. Lugha za wenzetu sio zetu, ujumbe ungefika vizuri tu kwa kiswahili.Nilikuwa siamini nilichokuwa nasoma hapa.Mpaka naona aibu kumalizia ili tangazo/barua/ hata sijui ni nini. Mwenyekiti una represent hiyo jamii, tafadhali ukifanya mambo, uwe pia unafikilia wana jamii zako unao warepresent. This is Sad.Post kiswahili kama unajua kiingereza kimepitia pembeni, au elimu chini ya mti au elimu ya watu wazima.Peace out

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 02, 2008

    Sijui nianzie wapi, ngoja nianzie mwanzo we annon ulieanza na AI DONO ABAT YUU, makosa kawaida ktk lugha, we mwenyewe umesoma umeona zako mnugu sijui mnungu kila mtu ameelewa ulimaanisha mzungu, na hiyo ...it do back home karibu kila mtu hajaelewa, mi nmeelewa 'yanayojiri kule bongo'. Wanasema lugha inawasilisha maana na si herufi. Waht I waht to say is (iyo waht ya kwanza umeisoma 'what' iyo ya pili umeisoma 'want') kumbe ubongo huenda zaidi ya herufi. Waamerika husema it do, it dont, we was, u was, you kiddin men, yote ni makosa ktk kiingereza ila maana imekubalika na imepitishwa, kiswahili vivyo hivyo 'fainali uzeeni' 'unanrushia stimu' 'tusepe zetu' hivi tunaita slang au vya mtaani, neno mshkaji sasa ni neno rasmi. Lugha inakua. Utata hapa ni kwanini ametumia kiingereza. Jibu ni kwa vile anaalika Afrika nzima. Kuandika chenye makosa ni BORA KULIKO KUTOANDIKA, Nnamiliki tovuti na ni lugha mchanganyiko kiingereza na kiswahili ebu niambie settings na configuration unasemaje kwa kiswahili, ndo mana hata mwenye blog hii ameacha Permanent link, post a comment n.k yawe km yalivyo, ngumu kutohoa, kuna tovuti moja wemeweka 'habari mvunjiko' ati wanamaanisha 'breaking news' si kweli na haileta maana yoyote. Breaking hapa ni kuchomoza/tokeza na si kuvunjika. Tosha
    APAKATI. apakati_ya_chembe_au_kidevu@yahoo.com

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 02, 2008

    Inasikitisha kwa kweli inasikitisha sana...kwa nini sisi kazi yetu ni kukaa na kuongelea mada ambayo haimpeleki mtu kokote? Huyu kaka kachukuwa muda kutoa hii mada ya maana na baada ya kujadili mada au kuchangia kinini kiulizwe na wenzetu kwa muheshimiwa Kabwe tunakaa kuongelea nani kaongea proper English and not..mwisho wa siku ni kuwa lugha imeeleweka na hii si shule au ofisi kwa hiyo mtu uhitaji kukaa na kuproof read hapa.....let it go guys! Hao wachina mnaoongelea mmefika China nyie na kuona maendeleo? Hii globu ni ya jamii kwa hiyo freedom of speech... Ongeleeni mada na maendeleo acheni umaskini wa roho....ndiyo maana atuendelei sijaona maendeleo yanayoletwa kwa mtu kutoongea kiswahili lakni yanayoletwa na ufinyu wa mawazo na chuki na kutothaminiana na kutokuwa na moyo wa kusaidiana. Kwa sabau kuna choice ya kuweka anonymous basi watu wanachukua fursa ya kuleta mabeef yao hapa..kama wewe ni mwanaume au mwanamke halisi weka basi jina lako na masahihisho. Kuku wee.
    TANZANIA IDUMU..UMOJA UDUBU...KARIBU MUHESHIMIWA KABWE.....

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 02, 2008

    Anon May 2, 12:31 mawazo yako kidogo yako kama yangu. mi maimuna pia, sina tatizo ya kuwa english ni proper au la! sijui gramar au kanachoya jaje?(anasema vipi)kusikili? (umesikia)? hayo sebu(siwezi) kabisa. ila lilonchanganya kabisa ni hiyo tarehe hapo chini, nimebaki na mawazo kuwa mambo yalishakuwa au ndo yanipitiii(yamenipitaaa)?

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 02, 2008

    " my fellow tanzanians and to all africans "sasa hii (to all africans)"NDIO INAYOSABABISHA MDAU KUTUMIA LUGHA YA KIMOMBO ACHENI JAZBA JARIBUNI KUFIKIRIA KWA UNDANI ZAIDI.SIO SWALA LA KUWA EDUCATED OR NOT NI COMON SENSE TU MNASIKITISHA~JAMBO DOGO KAMA HILI LIMEWARUSHA ROHO MKITAKA MDAU ATUMIE KISWAHILI AKATI WALENGWA WAKO MICHIGAN.
    NDIO MAANA WAKINA KARAMAGI WANAJIONGEZEA MIKATABA KWA UDANGANYIFU KWA SABABU WATANZANIA HAWASOMI WAKAELEWA WANAJIFANYA WAJUAJI SANA/

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 02, 2008

    Jamaniee hapa kinachoendelea ni kuwa huu ujumbe au hii taarifa ingeongelewa kiswahili ili ieleweke kwa ufasaha na ingependeza zaidi, kwani wengine wetu kiinglish not richabo ndo ukaona hasira yote hiyo na lawama kedekede, na malalamiko yote hayo wanatutetea na sisi wengi, ambao tunaitwa hatukusoma hapa kwakuwa kiinglish chetu cha kuombea maji, ila inapokuja shida yoyote hata asosoma anahitajika m.f maziko majanga,kupiga kura, nguvu kazi ya asosoma pia inahitajika kwa sana tu.

    Sasa fikisheni ujumbe kwa lugha nyepesi ili kila msomaji humu apate ujumbe, aelewe kinaongelewa nini hapa,naamini hilo ni lengo kubwa la muandishi kwani tuko katika kueleweshana na kufundishana hapa walioko nje na walondani hapa bongo tujue yanayojiri kila mahali humu kijiweni. sio kuonyeshama makarama humu. michuzi anajitahidi kutupasha Khabari tusiifanye kazi yake ikawa ngumu au haina faida kwa jamii, kwa kukosesha wengine maelewano.

    ReplyDelete
  36. TAFADHALI KAKA JIKWAMUWE KUTOKA KWENYE UTUMWA WA KIAKILI,AU KISWAHILI KINAKUTIA AIBU KAMA WENGI WA TZ WANAVYOONA.

    AIBU.

    ReplyDelete
  37. Kijana anonymous Said.
    Naweza kusema hujuwi ukizungumzacho
    unasema "it doesn't matter if it is swahili or english".Ina-matter bab-kubwa kijana.Soma kiingereza na lugha zote zilizopo duniani hvyo ndivyo inavyotakiwa.lakini wasiliana na watu wako kwa lugha yako, huo ndio ujanja ambao wa tz wengi hatuna,angalia wenzetu wa asia na wengineo. AMKA

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 02, 2008

    Ujumbe umefika kwa watanzania wote.
    Huyo anayesema ulikuwa mahususi kwa wana wa Michigan tu nadhani umekosea sana, nini maana ya habari?
    Unataka kutuambia tusifatilie yanayojiri sehemu zingine tofauti duniani kwa sababu hakutuhusu huko,ni mara ngapi unaingia humu kwenye blog?pale tu unapoambiwa kuna habari inayokuhusu ama ulikuwa unajaribu kusema nini?tafadhali usitu discreminate.
    M-Makunduchi haujapitwa hiyo ndio style wanayotumia wamarekani kuandika tarehe wanaanza na mwezi-siku-mwaka tofauti na huku kwetu tunaanza na siku-mwezi-mwaka.Sasa naona bwana mwenyekiti ametumia style ya pale alipo.

    Tuonane.

    ReplyDelete
  39. Mwanakijiji na wengine mtakaokutana na Zitto naomba mmuulize kwa niaba ya wengine "je alipogombea ubunge wa Afrika Mashariki alikuwa na lengo gani?".

    Mimi nilitegemea mbunge anayepinga ufisadi awe mstari wa mbele kupinga kuwepo kwa jumuiya zinazoharibu rasilimali.Bajeti ya jumuiya ya Afrika Mashariki yote inaishia kwenye vikao na pesa hizo ni za watu wanaokosa maji na chumvi!!!

    Zitto mwaka 1999 tulikuwa naye katika majidiliano ya kuwahusisha wananchi kwenye uanzishwaji wa jumuiya ya Afrika Mashariki na mojawapo ya mambo tuliyojadili ni kwamba mapendekezo ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo yameandikwa kiingereza...

    hii imeambatana na malalamiko ya wengi katika mjadala huu,hivyo nadhani ingawa kulikuwa hakuna haja ya kufanya zaidi ya asilimia 60 ya mjadala huu kuwa juu ya lugha,lakini swala la lugha ya kiswahili kupewa kipaumbele lina umuhimu wake.Zitto anajua hilo labda kama kabadili mawazo!

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 02, 2008

    Nafikiri Bwana Mfinanga ana bahati sana na sidhani kama wakati mwingine atakapoandika ujumbe kwa lugha yoyote ile atautuma kama alivyoutuma huu bila kucheki grammatical error na hata spellings. Tena atawatumia watu wnegine walio karibu yake kama Katibu (Huyu ndiye mwandishi, pengine jina la Bwana Mfinanga limewekwa tu kwa kuwa taarifa lazima itoke kwa Mwenyekiti) na wangineo kabla ujumbe haujatoka mbele ya kadamnasi.

    Kujitetea kusema eti mradi ujumbe umefika na kuna walengwa wengine ambao si Watanzania na hawajui kiswahili nalo ni kosa kubwa sana kwa sababu kumbe ujumbe huu ulikuwa wa hadhira kubwa inawahusisha na wengine wasojua kiswahili basi ulitakiwa uandikwe na ukaguliwa kuwa hauna makosa yoyote kwani kwenye computer kuna spell check na mengineyo.

    Wakati mwingine kama lugha unayotumia ina matatizo kidogo jaribu kuandika kwa bullet points na kutumia sentensi fupi fupi, fupisha ujumbe wote na andika vile vitu vya muhimu tu.

    Kuna siku tulitukanwa na mzungu aliyekuja kuaudit kazi yao, sisemi mahala, lakini alituuliza hivi kwenye computer zenu hicho kitu kimeandikwa spell na grammar check vya kazi gani? Tatizo huwa tunafikiri kwa lugha zetu wenyewe za asili kisha tunaandika kwa lugha ya watu wengine na hapo huwezi kuepuka makosa katika lugha, cha msingi ni kuwa mjanja na kuandika sentensi fupi fupi na kuisoma kwa sauti wewe mwenyewe ili uone kama inaleta maana iliyokusudiwa, kisha mpe mtu mwengine aisome ili naye akwambie kama kuna makosa au la. Sasa hapo unaweza kuituma kwa hadhira iliyokusudiwa. Haya mambo ya kusema aah mradi ujumbe umefika ndio yaliyoifikisha nchi hii hapa tulipo, watu wakikosea na wakaambiwa wamekosea basi huja na visingizio kibao, ooh wananichukia, wananionea na hatuko tayari kukosolewa hata kidogo!

    Mimi nafikiri watu walioshauri kutumika kwa lugha ya kiswahili wameshauri baada ya kuona ujumbe una makosa ya kilugha na hao wakongo, wanaija na waafrika wengineo kama wanakuja kusoma blogu ya Michuzi basi ujue wana ufahamu wa kiswahili, kwa sababu Michuzi anatumia kiswahili kwa sehemu kubwa sana na anatusaidia na sie wengine ambao midomo inatamani kuongea kiswahili lakini hakuna mtu wa kuongea naye ila tunapata nafasi ya kujumuika na wenzetu kwa lugha yetu yenyewe. Nina muda mrefu sijazungumza kiswahili lakini humu napata nafasi ya nafsi yangu kuongea kiswahili japo mdomoni hakitoki lakini moyoni ninakisema kwa haya ninayoandika. Nakipenda na kukithamini kiswahili kwa sababu ni changu!

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 02, 2008

    we mwanakijiji inaonesha wewe ndo ulileta hilo tangazo mbona kila wakati kimbelembele ch akulitetea eh?unajua unakimbelembele sana wewe

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 02, 2008

    Mhu!!! Iam not realy joining these crackheads. Lakini sikujua kama wabongo tunatalent nyingine kama za ki nigeria!!!!!!!
    Mulox

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 02, 2008

    Sasa mtahudhuria kikao au? maana watu walioko hapa States hawasumbui, watu wako bize wanahangaika kutafuta pesa, wakati wengine wanasahihisha kingereza tu. Natumai, ni vyema kushikilia bango swala la msingi kuliko kuzungumzia lugha, kiswahili au kingereza hayo maamuzi ya mtu. halafu mtu kutumia lugha fulani si utumwa ila ni namna ya mawasiliano ili mradi mnaelewana mnazungumza nini.

    Mkutano mwema.

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 02, 2008

    HUU UJINGA SASA, YAANI MNAMSEMA TU HYO JAMAA, MPAKA BASI, HIVI TANZANIA TUNAONGEA KISWAHILI AU KIINGEREZA,MAOFISI TA SERIKALI WOTE WANAWASILIANA KWA KIINGEREZA, ACHENI UJUAJI JAMANI, JAMAA ALIKUWA ANAALIKA WATU WOTE WAAFRIKA,

    NANI HUWA ANAANDIKA KIINGEREZA BILA MAKOSA YA GRAMMAR, HAKUNA DUNIA HII, I MEAN HATA WAZUNGU WENYEWE WANAKOSEA, EVERY LANGUAGE HAS COMMON MISTAKES.

    HIVI MNAOTOA HOJA ZA KISWAHILI KITAWAFIKISHWA WAPI?? TUNADANGANYANA HUMU, WATU WASEME WAONGEE, WAAANDIKE KISWAHILI, NCHI IMEBINAFSISWHA HII, MTU ANIELEZE FAIDA YA KISWAHILI IN GLOBALISATION WORLD.

    HUKU WATOTO WENU WAKO INTERNATIONAL SCHOOL, KILA KONA NCHI HII UNAHITAJIKA HUJUE KIINGEREZA , PENGINE NADHANI KUANZIA LEO MAONI YANGU YATAKUWA YA KIINGEREZA POPOTE PALE, HILI NINAPOFANYA KOSA WATU WANANIKOSOA, AMBAO PIA WENGI WAO HAWAJUI.

    MICHU ATANIREKEBISHA, NO WAY OUT WE ARE NOT CHINESE, JAPANESE, TULISHAFANYA MAKOSA KISWAHILI HAKITAMSAIDIA YEYOTE, HATUNA KIBURI HICHO NCHI YA NNE KWA UMASKINI DUNIANI, MPAKA KIJIKO TU HATUWEZI KUTENGENEZA TUNASUBIRI TOKA NJE YA NCHI, ACHILIA MBALI VITU VINGINE.WATOTO WALIOSOMA ULAYA NA INTERNATIONAL SCHOOOL NDIO WANAPATA KAZI NA WENGI WAO NI WATOTO WA WAKUBWA, HUKU TUNAWALALAMIKIA MAFISADI HAO KUMBE WAAJIRI WA KIGENI HAWAJUI HILO WANAANGALIA UWEZO WA MTU.

    TUSIDANGANYANE

    KISWAHILI HAKINA FAIDA TUMESHINDWA TUKUBALI TU.

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 02, 2008

    HAHAHAHAHA,WABONGO HAOO UTAWAJUA TU!WALA HUITAJI KUULIZA HAWA WANAOBISHANA HAPA KINA NANI?YAANI KUMKOSOA HUYO MWANDISHI NDO MNAONA LA MAANA KULIKO KUFIKIRIA YALE MTAKAYOENDA KUMUULIZA MH.KABWE?HAFU MNATAKA MAENDELEO NCHINI,KWA MWENDO HUU TUTAFIKA KWELI?ETI MNALALAMIKA KWANINI KATUMIA KISWAHILI,MMESIKIA NCHI ZOTE ZA AFRICA ZINATUMIA KISWAHILI?MANAKE YEYE KAKUSUDIA KUALIKA WAAFRICA WOTE,AU MLIKUWA HAMTAKI WAAFRICA WENGINE NAO WAJUMUISHWE?..SWALA LA KWAMBA KAKOSEA HICHO KIINGEREZA NALO HALINA MPANGO,UJUMBE UMEFIKA NA UMEELEWEKA BASI!HAYA WALE MNAOPENDA KUPOTEZA MUDA NIKOSOENI,WALE MNAOPENDA MAENDELEO NA TUACHENI ISHU YA LUGHA TUFIKIRIE YA MUHIMU YA KUONGEA NA KABWE

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 02, 2008

    NYIE MASELA VIPI NYINYI? UMASKINI GANI MPAKA A KUFIKIRIA NYIE? JAMAA KAWAALIKA NA WAAFRIKA WENGINE PIA NDIO KATUMIA ENGLISH KWA SABABU WASINGEELEWA KISWAHILI MASELA ACHENI UBISHI WAKIJINGA CHANGIENI HOJA ZA MAANA.WEWE MDAU UNASEMA HII NI HABARI KWA WOTE/ HIO SIO HABARI NI TANGAZO LA MUALIKO KWA WATANZANIA NA WAAFRIKA WOTE WALIOKUWEPO MICHIGAN.KWANINI USIMSUBIRI KABWE AKIRUDI UMUALIKE KATIKA ENEO LAKO NA WEWE UTOE TANGAZO LA KISWAHILI LA MUALIKO.TUJITAHIDINI KUTUMIA AKILI ZETU KWA UNDANI ZAIDI NA KWENYE MAMBO YA MAANA ACHENI UPUUZI KILA WAKATI.

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 02, 2008

    Ndugu zangu, mimi ninaona mjadala huu ni halali. Ugomvi si kutumia Kiswahili au Kiinglish, ugomvi ni matumizi sahihi ya lugha pamoja na utambulishi. Huu ni mjadala ambao ni muhimu na umeshika kasi huko nyumbani. Tukichagua Kiswahili au Kiinglish hatuna budi tuzitumie lugha hizi kwa usahihi wake, hususan tunapokuwa tunatoa ujumbe kwa hadhira kubwa kama hiyo iliyokusudiwa na mtoa tangazo. Kwa hakika kuna makosa mengi ya kisarufi ambayo hayakuhitajika kujitokeza.
    kacha

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 02, 2008

    NYIE MNAOPENDA KUKOSOA WENZENU MTAFIKIRI NYIE MKO PERFECT MNABOAAA..NYIE NDO MNAOBISHAGA HADI VITU VYA KIJINGA, JITU UNAKUTA LINABISHA ETI UPINDE WA MVUA UMEKOSEWA KUPANGWA RANGI ZAKE..UJINGA MTUPU.KAMA WE MSTAARABU NA UMEPATA UJUMBE BASI FIKIRIA YA MAANA UTAKAYOCHUKUA KWENYE HUO UJUMBE..KUMBUKENI HILO NI TANGAZO TU JAMANI,MNA JAZBA KAMA NINI!!WALENGWA WA UJUMBE WAMEKAA KIMYA,WALE LISILOWAHUSU NDO WANABWABWAJA HAPA..MA MDOGO UK

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 02, 2008

    YAANI HAYO MAKOSA MADOGO TU AMBAYO WALA UJUMBE UJAPOTEA NDIO UMEWAFANYA MJE JUU KIASI HIKI? KWELI STRESS ZA MAISHA NOMA.KUNA JAMAA MMOJA ALIONESHWA CNN YEYE KAZI YAKE KUZUNGURUKA KILA MJI MAREKANI ANAREKEBISHA MANENO YALIOKOSEWA KWENYE MATANGAZO KAZI HIO INAWAFAA SANA.
    HIZO COMMENTS ZAIDI YA 50 YALITAKIWA YAWE MASWALI AMBAYO WATU WAKAMUULIZE MUHESHIMIWA ZITTO KUHUSIANA NA MAFISADI.KUMBE WATU HAWAJALI KABISA MAMBO YA UFISADI WANACHOJALI NI MWENYEKITI WA TAMI HAJUI ENGLISH KWA MAKOSA MADOGO HAYO.UJJINGA MTUPU.
    MWENYEKITI WA WASHINGTON D.C FANYA MPANGO WA KUMUARIKA ZITTO KWANI KUNA MAZITO MENGI KUHUSU NCHI YETU TUNATAKA KUYAJADILI.

    ReplyDelete
  50. AnonymousMay 02, 2008

    Message Delivered!!!!!
    Stop talkin BULLSHIT, instead post some intelligent questions to help our fellow Tanzanian in Michigan to ask Mr Kabwe.....Dammmm Wabongo utawajua tu.
    Mdau T-Dot

    ReplyDelete
  51. AnonymousMay 02, 2008

    Kaaazi kweli kweli!

    Nimeburudika sana na mpambano huu. Enhe endeleeni jamani. Eti "mwanakijiji ana kimbelembele sana" . teh teh!

    ReplyDelete
  52. AnonymousMay 02, 2008

    Huko kusingizia eti kuna watu wengine wa nje wanataka au wanaenda kumuangalia Zito Kabwe wanamjuaaaa? Acheni kumkweza mtu jamani anajulikana humo humo Bongo basi, hata huko kwao kwa Wabembe wenziwe jirani tu pua na mdomo na Kigoma sidhani kama wanamjua. Nendeni mkamsikilize mje tena mutuandikie kwa kiinglish alichowaambia. Lakini mkija mje na lugha sahihi yenye kueleweka. Sana sana ni kufungua tovuti yake na tovuti ya Chadema na kuwandikisha wanachama wapya. Jambo gani jipya atakolilosema huko ambalo hamlijui? Kama mafisadi kila siku mambo yanaanikwa magazetini, kama Muafaka kila kitu kiko wazi, haya labda asema anataka kugombea urais mwaka 2010 ndilo litakalokuwa jipya. Maana kama kungekuwa la kujadili sidhani kama watu wangepoteza muda humu kujadili lugha badala ya kujadili mada, kwa sababu hakuna kipya au mpya kwenye mada. Nyie wenyewe mmejionea kila aliyeingia humu anajadili lugha, hiyo ni dalili tosha kuwa hakuna jipya!

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 03, 2008

    Yaani siamini watu tunagombana kuhusu lugha tu,hata kama angetumia kisukuma,kinyamwezi zote lugha za tanzania ikiwamo kiswahili na kiingereza.Sasa watu wanakaa kulalamika tu..mimi nadhani kuna watu wanastress zao hapa ndio wamepata mahala pa kuzitolea...fikirieni vya kudiscuss pamoja na Mr Zitto mnakaa kubishana kuhusu lugha..let me start...hivi Mheshiwa ile report ya madini inawezaje kuisaidia nchi kupata kodi kuliko ilivyo hivi sasa?

    aika monoko.....mseme na hapo

    ReplyDelete
  54. AnonymousMay 03, 2008

    Kiswahili hakikatazwi, ila Kiingereza pia muhimu wadau. Chondechonde!!

    Na visa za kuja huku marekani muombe ziwe za Kiswahili basi. Ebo! Jifunzeni maneno magumu hapo kwenye "waraka wa mfinanga kwa watu wake." Kuna maneno lukuki hapo magumu, kama vile that, family, most, welcome, all, n.k

    Sev

    ReplyDelete
  55. AnonymousJune 16, 2008

    tutakalia maneno tu bila kufika popote kwani cha muhimu ni ujumbe umefika, umefika namna gani kwa lugha gani si muhimu. Ebu jamani tupunguze kulalamikia vitu ambavyo havitupeleki popote!

    ReplyDelete
  56. AnonymousJune 16, 2008

    Nawashukuru nyote kwa kuchangia mawazo yenu juu ya suala hili.
    Baada ya kusoma mawazo yenu nimegundua kitu kimoja ambacho watanzania tulio wengi bila ya kujijua tunalemaa nacho.UBISHI.
    Huyu ndugu aliyeandika barua ametumia uhuru wake wa kujieleza kwa kutumia lugha ambayo kwa hali aliyo nayo sasa ndiyo anayoitumia huko aliko bila shaka.hakuna ubaya.
    Hoja hapa ni kwamba huyo Bwana zito anakwenda huko marekani kama ambavyo watanzania wengine wanavyokwenda,ila yeye ni mmoja kati ya wenye kinafasi katika jukwaa la wanaotuwakilishia mawazo yetu (Sio wanaotuwasilishia)pale Dodoma.Sasa kwa mtazamo wangu aliyeandika ujumbe ule kwa njia moja au nyingine ameona anaweza akatumia kanafasi ka huyo bwana zito lau abebe machache kwa wale watakaofika kwenye mkutano huo baada ya kuupata ujumbe huo.
    Lugha hapa sio hoja ya msingi sana.
    Acha walioelewa ujumbe waelewe.wafike kikaoni waongee.wale na wanywe.wazungumze.Baadae wafanye majumuisho ya mazungumzo yao na watuandikie kwa yoyote nasi tujue,kama kuna ulazima,dhumuni na matokeo ya kikao hicho.
    Kuendelea kulumbana ili kuendeleza UBISHI hakuna maana yoyote zaidi ya kutoka nje ya mada na kujishaua.
    Wachangiaji wengi tu mmechanganya lugha.si kosa,ndio kujifunza.Kwa taarifa tu ni kwamba hata waingereza
    wenyewe au waswahili wenyewe wana walimu ambao taaluma yao ni kufundisha lugha hizo tu.Hamshangai?lugha haina uzawa ndio ujifanye waijua,kosa.jifunze.
    Watanzania tuko zaidi ya milioni 35.Ni wangapi mliopo ulaya? ni asilimia ngapi?.Sasa nawaomba sana,wengine ni baba,shangazi,mjomba,nk.ya wale waliopo huku.Wengine hatuna ndugu hata wa dawa zaidi ya nyinyi kama watanzania wenzetu tu.Jengeni umoja,tengenezeni jumuia ndani yake mkiunda kamati zenye kila aina ya taaluma mnayoiona bila kubagua,ziwe huru.tengenezeni utaratibu angalau kukutana kila mwezi mara moja katika sura ya kitaifa mkijadili mambo mbalimbali
    katika utamaduni wetu ule ule wa vikao vya harusi na misiba.kila kikao kionyeshe maendeleo kwenda mbele.Baada ya mwaka mtaachana na ubishi wa kitoto juu ya lugha,nani kagharimia safari,msifungue matawi,nk.Tunaambiwa Marekani na ulaya ni nchi zilizoendelea.Ninyi mko huko.katika vikao vyenu mtajadili hatua wanazofanya wenzetu kwa sababu mnaziona kwa macho ili nasi tufuate angalau kwa zile zilzizo ndani ya uwezo wetu.Mfano kujali muda,kujadili mambo badala ya watu.
    Sisi tunatakia tusikie tu kwamba ndugu zito amealikwa na jumuia ya watanzania waliopo nchi fulani na katika kikao hicho mambo yaliyojadiliwa yalikuwa ni.........na wanajumuia walimkabidhi mbunge huyo ujumbe ufuatao kwa serkali,Bunge,Waziri...blah blah...
    na majibu yanatarajiwa yapatikane katika kikao kijacho.mambo hivyo.
    Wachache miongoni mwenu mliopo ughaibuni punguzeni majidai kidogo.Wengi tulitaraji hasa mliopo Marekani ndio mngeongozana na wana Sullivan.Matokeo wamekuja,wakapokelewa na waliowapokea,wakaonyeshwa wajasiria mali ambao ni wake,wajomba nk.wao.sio wehu tukaishia kushangaa wanavyotushangaa.Ninyi ndio msaidie,tunaomba.Hatupendi na wala sio sifa mbunge kama zito leo inakuwa nongwa kwenda ulaya inakuwa jambo kuuuubwa la kujadiliwa hivi ambapo majadiliano haya yangekuwa ya kuelemishana na kujua huko kuna nini na huku kuna nini.sisi tuleteje vinyago nanyi mtaviuzaje.Nadhani watanzania tuamke,tuachane na hii dhana ya kila kukicha tunawaona wanasiasa ndio wataalamu.wanajua kila kitu.
    Tunataka wanasiasa wanyooshwe mambo
    wataalamu watimize wajibu wao na tuheshimu na si wanyonge tusonge.vinginevyo,basi tundeleze UBISHI.Je jua linazunguka au dunia ndio inaozunguka?Yai na kuku kipi kilianza.

    ReplyDelete
  57. The Utamu yafungiwa tena!!!
    Hizi ni habari za kuaminika kabisa ile blogspot iliyekuwa inawanyima watu usingizi yafutwa na Google Inc. Hivyo watanzania kaeni kwa amani ila sio mwanzo wa kufanya mambo ya kishetani.

    Mdau, Brum, UK

    ReplyDelete
  58. tungekuwa tunatumia hizi nafasi kujadili ni jinsi gani tutaiendeleza nchi yetu au tuchangishane mihela kwaajili ya kupeleka watanzania nje wakajifunze kutengeneza generator za umeme na mambo mengine mengi sio kuagiza maexpert, page nzima imejaa comments za kupondana tu.
    the utamu imefungwa lakini tutaikumbuka coz ilisaidia baadhi ya watu kutunza utamaduni wao, sasa itakua km bomba la maji limefunguliwa.japokuwa na the utamu mwenyewe alianza kuandika vitu ambavyo c vya kweli. by lizy London

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...