SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA FAMILIA YA MAREHEMU DAUDI BALALI

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Ndugu Daudi Balali kilichotokea tarehe 16 Mei, 2008 huko Boston, Marekani.
Wakati huu mkijiandaa kwa mazishi yake baadaye leo, napenda kutumia nafasi hii kutoa mkono wa rambirambi kwenu na kwa ndugu zenu wote.

Naungana nanyi katika wakati wenu huu mgumu na wa majonzi makubwa kutokana na msiba mkubwa uliowakuta. Tunaelewa machungu mliyonayo kutokana na kuondokewa na mpendwa wenu na kiongozi wa familia. Ni kazi ya Mungu haina makosa.

Tunawatakia mazishi mema. Tuzidi kumuombea marehemu apate mapumziko mema.
Amin.

IMETOLEWA NA OFISI YA MAWASILIANO, IKULU
TAREHE 23 MEI, 2008

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...