SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA FAMILIA YA MAREHEMU DAUDI BALALI

Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Ndugu Daudi Balali kilichotokea tarehe 16 Mei, 2008 huko Boston, Marekani.
Wakati huu mkijiandaa kwa mazishi yake baadaye leo, napenda kutumia nafasi hii kutoa mkono wa rambirambi kwenu na kwa ndugu zenu wote.

Naungana nanyi katika wakati wenu huu mgumu na wa majonzi makubwa kutokana na msiba mkubwa uliowakuta. Tunaelewa machungu mliyonayo kutokana na kuondokewa na mpendwa wenu na kiongozi wa familia.
Ni kazi ya Mungu haina makosa.

Tunawatakia mazishi mema.
Tuzidi kumuombea marehemu apate mapumziko mema.
Amin.

IMETOLEWA NA OFISI YA MAWASILIANO, IKULU
TAREHE 23 MEI, 2008

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 24, 2008

    ish, kumbe naye yumo!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 24, 2008

    yaaani Hapo ndo unajua CCM flip flop sana!!!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 24, 2008

    HAYA!!

    MMEUMBUKAAAAAA... HAOOOOOOO...IONE MISURA YENU! HAHA MARA PLASTIC SAJARI,MARA KAFICHWA,MARA NINI,MARA OOH SERIKALI ITANGAZE

    MSHATANGAZIWA SASA... BALALI IS DEAD

    ACHENI NDOMONDOMO

    LEILA SHAKUM - THE NIECE

    ReplyDelete
  4. Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Ndugu Daudi Balali kilichotokea tarehe 16 Mei, 2008 huko Boston, Marekani.

    Jamani huyu Rais wetu vipi?
    yaani mpaka sasa bado anasema Ballali alifariki Boston?
    Yaani ukisikia kuwa wa mbili havai moja ndiyo hapaa!

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 24, 2008

    tanzanian don't cry any more,
    you cry by the time nyerere pass away!
    its over now, ....
    we trust them...they betrays us.
    we trust them they dishonor us!
    they dishonor your country for very few dolars in their foreign acc'
    leave the country dragging feet in no movement for every thing!
    sorry ma' fellow tanzanian,
    changes in not coming yet.
    stop weeping....my country,

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 25, 2008

    Nyie watu vipi? Si mlisema mbona serikali iko kimya haijatoa rambi rambi, haya rambi rambi zimetolewa, sijui mnaleta vitu gani tena. If he is dead, and you believe he is not dead, you wont bring him back to earth. Subirini na nyie siku zenu zikifika mkatae mseme wakati bado!

    RIP Balali

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 25, 2008

    leila nimependa comments zako, yani kama nakuona vile unavofanya kwa vitendo! lakini nafikiri watu wana uhuru wa kutoa maoni kwa namna wanavoona jambo kutoka katika pembe tofauti.na ndio maana kuna sehemu ya maoni na ujue hii dunia imejaa artists huwezi kujua nani ana kipaji mpaka aingie kazini na hiyo itakuwa pale inapobidi.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 25, 2008

    Hivi wewe Leila unayedai kuwa ni Niece wa marehemu Balali mbona hueleweki uko upande gani wa serikali, wa Watanzania walipa kodi? kwanza hata huoneshi hata kama una uchungu maana tangu hizi taarifa za msiba zitokee wewe kutwa uko kwenye blog ya Michuzi, sasa si ujumuike na wenzio kwenye msiba huko nyumbani kwake? au umeewa kidogodogo na serikali ili uigize tu hapa? watu wana uchungu na hiki kifo kisischoeleweka na tumechoshwa na serikali kuwapoteza watu just like that!!!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 26, 2008

    NASIKIA KAFUFUKIA UARABUNI
    KWAHEEERI!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 26, 2008

    anon wa 10:35 umeongea POINT!..huyu LEILA anatuzingua tu hapa.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 27, 2008

    huyu laila ndo alivyo...hata kule bc anakurupukaga,naona ndo kanunua kakompyuta

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 28, 2008

    hakuna chakuumbuka wala nini, bado hakuna kitu cha kuprove kafa. hata picha ya mwili wake. inawezekana kuwa ni mchezo tu huu. mbona hata picha ya marehemu mtoto aliyechinjwa ilitolewa humu? leteni picha ya marehemu balali.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 28, 2008

    huyu niece wa balali mbona ana jina la kiarabu jamani?isije tukawa tunajipendekeza bure,ili tuambulie urithi..mna undugu nae au?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...