Habari za leo kaka Michuzi,ninayo furaha kuwaletea habari kuwa hatimaye Umoja wa watanzania waishio nchini switzerland yaanzishwa rasmi leo siku ya jumapili tarehe 25 mwezi wa 5.


Mkutano huu uliohudhuriwa na watanzania wengi tu waishio Geneva pamoja na miji mengine ya karibu uliweza kujadili na kupitia katiba ambayo ilipitishwa na kukubalika kuwa muongozo wa jumuiya hiyo.


Umoja huo utajulikana kama Tanzanians Association in Switzerland kwa kifupi TAS.


Kwakweli mimi binafsi kaka michuzi nimefurahishwa sana kuanzishwa kwa umoja huu maana ni jambo lililokuwa wazi kuwa wengi wa watanzania waishio nchini humu walikuwa na hamu ya kuwa na jumuiya itakayoweza kuwakutanisha wakati wa raha na hata wakati wa shida.


Pamoja na mambo mengine mengi Umoja huu pia umelenga kuwawezesha watanzania waishio nchini humu kuweza kuunda mikakati itakayo wasaidia katika nyanja mbalimbali hasa ya elimu kwa vijana na watoto wao na hata maendeleo ya kiuchumi wakiwamo nchini hapa na kwingineko.


Mheshimiwa Balozi Marten Lumbanga ambaye ndiye Balozi wa Tanzania kwa Umoja wa Mataifa hapa Switzerland ameteuliwa kuwa Patron wa jumuiya hio.
Pamoja naye viongozi wa jumuiya hio ni kama ifuatavyo:

Mlezi-----------------------Balozi Mh. Marten Lumbanga
Mwenyekiti-----------Dr.B. Nyenzi
Makamu M/kiti---------------Mrs. Mpatwa,
Katibu----------------------Mr.S.M. Sillayo
Katibu Msaidizi------------Mr. B. Luvanda
Mhasibu-----------------Mr.I. Lupatu


Kwa niaba ya watanzania wote waishio hapa napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza sana na kuwatakia kila la heri katika nafasi zao ili waeze kuiongoza vema jumuiya hii.
mdau,

geneva.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 26, 2008

    Mbona wazee tu huko Swiss hakuna Vijana??

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 26, 2008

    Hallo Mkuu wa Wilaya Mpya ya Tegeta, Bw. Michuzi a.k.a Misupu, hao jamaa zetu wa Swiss hiyo picha waliipiga kabla ya kutoka nyumbani (TZ) nini ??? Mbona wote wanaonekana kama hawako Uswisi ??? Jamani msituangushe inatakiwa muonekane kama mkom majuu kweli na mnawakirisha ipasavyo !!!! Lakini hata hivyo nawapa HONGERA kwa kuweza kuwapata viongozi wenu wataowasaidia kwa jambo moja au jingine.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 26, 2008

    kaka michuzi asante kwa habari hii , mimi ni mdau wa swiss na nimefurahia kuanzishwa kwa umoja huu maana tulikuwa tukiona tu wenzetu wa kitanzania nchi nyingine ,

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 26, 2008

    Hongereni sana kwa kuanzisha umoja huo.Hope utawasaidia.
    Anony namba 1:Suala la uzee au ujana NOT so important nadhani ungekaa kimya.

    Anony 2:Wewe ndo baadoo mshamba wa zamani unayedhani kukaa majuu siku hizi ni dili!Ulitaka waonekane kama wako uswisi ili iweje.Hao nawapa Big up kumbe mtu anaweza kuwatambua kama watanzania kirahisi.Wanablog kila siku wanapiga kelele.IF YOU HAVE NOTHING TO DO,DON'T DO IT HERE.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 26, 2008

    Haya Kumekucha Watanzania!Haya ndiyo mambo ambayo tumekuwa tukiyasubiri yatendeke.Hayawi hayawi sasa yamekuwa.Nawapongezeni sana kwa uamuzi wenu wa busara.Nawatakia mafanikio tele bali kuleni lakini msisahau huku nyumbani.Nyie hatuwezi kuwaonea haya.Vijana wetu.Mjitumikishe,Hangaikeni lakini muwakumbuke wenzenu huku nyumbani.Mahitaji ya shule,huduma za afya,vyombo vya usafiri wa maji na nchi kavu,maji salama nk ni makubwa.Sisemi mvitoe bure bali kumbukeni KUWEKEZA HUKU NYUMBANI.Msitupane mshikamane katika raha na shida hiyo ndiyo jadi yetu lakini msilee uzembe.Nwatakia kila la kheri katika Umoja wenu na shughuli zote kwa ujumla.TZ.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 26, 2008

    Michuzi kwenye backbround mbona kama frame za madirisha na huo mlango vina rangi ya kijani.Siyo mambo ya CHAMA CHA MAZINGAOMBWE(C.C.M)

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 26, 2008

    Lupatu wakilisha wahasibu kama ulivyokuwa IFM late 90s.
    Mdau.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 26, 2008

    michuzi asante taarifa, huyu mzee anaonekana kuw ana busara, ila watoto wake, wengine nasikia wana tabia ngumu, malezi si yanaanza nyumbani halafu kwenye jamii, ni ushauri tu, asante kwa taarifa usibane hii.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 26, 2008

    watu wengine pumba tu humu ndani mxiiiiiiii ngoja nijitokee

    wewe anon wa 1,UMEONGEA NINI NA ILI IWEJE?daywaka kakosa kazi eee...hayaa na bado!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 27, 2008

    Jumuia ya watanzania ya watanganyika? mbona hakuna hata mzanzibari mmoja? au imesahaulika kuwa tanzania ni tan/ganyika zan/zibar (tan zan i na a ni iko kwenye majina yote). Na msitwambie kama huko hakuna watanzania wa asili ya zanzibar, wapo tunawajuwa na nimewaona wengi nilipofika huko mwaka juzi.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 27, 2008

    Mimi namuunga mkono huyo Bwana aitwaye Atifugwege Mwakanyamale, kwani alichongea ni sahihi kabisa kwa maana hao ni wawakilishi wetu huko hivyo hawana budi kuwa smart wakati wote hasa wapigapo picha za utambulisho.

    Nawe ANONY wa 4.53 PM, nadhani umeongea pumba kama si utumbo kwani huyo Bw. Atifugwege alikuwa anawakilisha mawazo yake na sio kama wewe ulivyomjibu na inaonyesha UELEWA wako ni mdogo hivyo NAKUSHAURI urudi tena shule kama wewe ulishindwa (school drop-out) ili uweze kuwa na upeo kama wenzio na sio kuropoka !!!!

    CIAO

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 27, 2008

    michuzi usibane, niliwahi sikia baadhi ya watoto wake wamemshinda tabia, na watu wanajua, sema wanawavumilia tu, hongera zake kuwa mlezi usibane hii tafadhali.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 28, 2008

    Hivi huyo Sillayo ni baba wa yule binti tuliyekuwa tunamwita road block pale faculty of law udsm? maana huyo mdada alikuwa tinginya si mchezo,yaani akipita kariakoo sijui inakuwaje, maana wamachinga kwa tabia za kusumbua wadada wenye maumbile makubwa !

    mdau boston

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 29, 2008

    Hongera Mrs Mpatwa kwa kuchaguliwa Makamu M/Kiti. Sisi jirani zako wa Regent Mikocheni tupo nyuma yako.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 29, 2008

    Nichukue nafasi yakipekee kabisa kumpongeza huyu mdau aliye piga picha nakuchukua hatua yakushare habari hii pamoja watanzania wenzake,pole kwa "comment" za baadhi ya watu, hao wapo katika kila jamii na wana "role" zao so wasikuvunje moyo, keep it up mdau. Then ningependa kuwaasa au kutoa maoni yangu kulingana na experience niliyo nayo. Nimatumaini yangu kuwa "team" iliyochaguliwa itakuwa inavigezo vyote vya uongozi ila napenda kuwakumbusha kumtanguliza mungu katika hiyo kazi, kazi yakuongoza watanzania sio lelemama. watanzania niwatu wakujibana sana. (wabinafsi na wasio na mtazamo wa mbali) fungua mabano utaiona context iliyo ndani ya usemi huo..kila la heri waswiss mnayo mifano yakuiga. Kidumu T.A.S

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 30, 2008

    Kaka michuzi napenda kukushukuru kwa blog yako ambayo inatuwezesha sisi watanzania mbalimbali tulio nje ya nchi na hata wale walio nyumbani kuweza kupata habari ya yanayojiri.
    Kuhusu kuanzishwa kwa jumuiya hii ya watanzania waishio uswiss ni jambo ambalo limenifurahisha sana na linaonyesha mshikamano wetu hata tukiwa mbali na nyumbani.napenda kumuunga mkono mdau hapo juu kuwa ni kweli kuongoza watanzania sio kazi ndogo yahitaji busara,
    kwani kwa mfano tu ukiangalia katika baadhi ya comment hapo juu utagundua kuwa kuna watu ambao kazi yao kila siku ni kuwavunja moyo wengine na hata kuharibu kwa mfano mtu anadiscuss watoto wa fulani walimshinda ili nini?ina uhusiano gani na umoja ulioanzishwa,au sijui mtu alikuwa road block chuo kikuu so what?hio inahusika vipi na umoja ulioanzshwa?kwakweli ni wakati umefika watanzania tubadilike,tunapopewa habari za maendeleo basi tuchangie kwa hoja za kujenga na sio kubomoa.
    mdau kuwait

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...