Hellow Mr. Michuzi,


nadhani u mzima. Ingawa siyo mdau wa Blog yako ila ni mfuatiliaji , msomaji na mpenzi mzuri sana wa blog hii. Sielewi sifa za kuwa mdau lakini tuyaache hayo ila nakutumia picha alipozikwa Rais wa Malawi Kamuzu Banda. Sijui ni kiasi gani cha fedha kilitumika kujenga kaburi hilo ila kweli wamalawi wameamua kumuenzi kiongozi wao huyo. Pamoja na yote sehemu hiyo ya kaburi imekuwa ni kivutio kikubwa kwa watalii wengi wafikapo huko malawi. Nami nilibahatika kufika huko kama mtalii wa kibongo. Sijui Baba yetu wa taifa alizikwa vipi ila naomba kama itawezekana tuwekee picha ya sehemu alipozikwa na kama ilishawahi kuwekwa tafadhali nijuze ni tarehe gani uliweka. Maana wengine hatujawahi fika butihama.

Kazi njema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 21, 2008

    Ndugu yangu, wabongo nafikiri kila kitu mpaka tufundishwe, tatizo siasa nyingi mno, tuna vivutio vingi sana vya watalii ambavyo havijaendelezwa hasa mijini na maeneo ya mambo ya kale. Kuna majengo ya zamani na makaburi ya watu mashurhuri ambayo jamii haijui na kama yangetangazwa yangekuwa vivutio vikubwa vya utalii. Mfano kaburi la Sokoine lingejengewa vizuri na vitabu vingi na maandiko yanayomhusu yangewekwa pale, watu wangekwenda kuzuru pale kama watalii. Makaburi ya machifu na viongozi wa makabila yangewekwa kwenye kumbukumbu na kutangazwa tungekuwa mbali. Tutaendelea kushangaa vya wenzetu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 21, 2008

    dada asante kwa picha ya Kaburi la Kamuzu Banda..Baba wa Taifa yeye hakupenda makuu,aliona haina haja yeye kuzikwa kwa umaarufu wakati wananchi wake ni masikini..hata mie niliona ni haki kabisa,Malawi ni nchi ya tatu duniani kwa umasikini lakini rahisi wao walimzika kama king..mimi sioni haja ya kuwas na kaburi kubwa kama shamba,,,na isitoshe hata kama kuna watalii wanakuja kuangalia kaburi hawalipi kiingilio chochote,na watalii sio wengi kama unavyosema..nimewahi kufika hapo na ninapajua sana..asante kwa picha mdau Norway

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 21, 2008

    Samahani kwa kwenda nje ya mada!
    +++++++++++++++++++++++++++++++++
    fainali za leo mbona hujaweka picha tuanze kutabiri nani zaidi mashetani wekundu na the blues.

    all in all,,....Liverpool a.k.a Bwana la Maini ndio Babu Kubwa angalia nani wababe UK!
    Man Utd (1968, 1999), Liverpool (1977, 1978, 1981, 1984, 2005), Nottingham Forest (1979, 1980), Aston Villa (1982). Aston Villa in 1982 Chelsea (patupu) Arsenal(next year)

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 21, 2008

    hakika binadamu hakuna kama kufanya mazuri dunian MASIKINI MAREHEMU MAPESA YOTE HAYAKUMSAIDIA KITU ALLAH YAALAMU KAMA NI KWELI ALIHUSIKA NA UFISADI AU LA ILA FUNDISHO KWETU NI KUWA BINADAMU NI KUGOMBANIA KUWA MWADILIFU MBELE YA MUNGU.
    MUNGU AMUONDOLEE MADHAMBI YAKE NA AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI AMEN.

    RAISI KIKWETE HAKIKA UNAYO NAFASI NZURI YA KUISHI MILELE KATIKA PEPO PINDI UTAKAPO TAWALA KWA UADILIFU TUNAKUOMBEA UWEZE KUFANYA HIVYO AMEN

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 21, 2008

    Mdau hapo juu, kwanza nakubaliana na wewe katika suala zima la kumuenzi baba wa Taifa letu, Mzee Kambarage. Lakini kwa ninavyomfahamu mimi mwalimu nyerere ukimjengea mkaburi mkubwa na magharama kama huo wa banda, anaweza kufufuka na kutuamuru kuwa tubobomoe na tumjengee kaburi simpo.
    Baba wa taifa ndo rais pekee wa Afrika ambaye siyo tajiri.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 21, 2008

    wewe unasema ni mfutiliaji wa Globu yetu hii tukufu kisha unasema hujawahi kuona picha za alikozikwa Nyerere? Sijui wabongo tutaacha lini ulongo!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 21, 2008

    dah linapendeza,ila na umasikini wao Malawi,si hiyo hela wangejenga barabara zao!?!?!?!?

    miss keys

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 21, 2008

    I am not a preacher and I hate being judgmental,I am simply making an observation and sticking my neck out (to be chopped?)
    I was appalled when I saw this. How can this be justfied in a country full of ravenous pot-bellied kids and in the face of a ravaging depopulating aids epidemic of almost biblical dimension. Coming to think of it the edifice reminds one of firaunis of misri A man should be humble in life and left humble after death.Look at King Fahds (1921-2005) grave, google for the picture

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 21, 2008

    Asante sana!mchochea mambo wa Malawi! ni hivi marehemu Easting Angwazi Kamuzu Banda wa Malawi alipofariki Malikia wa Uingereza na familia yake huko U.K walitoa ufadhili mkubwa wa mashishi yake likiwemo jeneza au sanduku lililopambwa kwa Zahabu na alizikwa nalo kwa maana hiyo basi kwa usalama wa kukwepa vibaka wasije kulichimbua ndio maana kumejengwa hivyo!
    Siyo heti wamalawi walimpenda sana
    Rais wao Easting Angwazi Kamuzu Banda! hata kidogo
    Hila si jambo baya kwa sisi watanzania kuhiga mfano huo kwa kuwaezi viongozi wetu kama vile marehemu Sokoine,Bibi Titi Mohamed,Mwalimu Nyerere,Abeid Karume,Abdurahaman Babu na wengine,
    Lakini mtu huenziwa kwa kumbukumbu njema sio tu kwa kuwa alikuwa kiongozi!mtu kama marehemu Tip Tip utamkumbuka kwa mema yepi?wakati watumwa wengi waliokwenda Uhajemi yeye ndiye aliwauza!au wale walikuwa MASLUTANI wa ZANZIBAR utawakumbuka kwa yepi?

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 21, 2008

    SASA MBONA HIZI HABARI HAZIELEWEKI, KAFARIKI DC BOSTON AU? SOMETHING DOES NOT ADD UP.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 22, 2008

    KAKA TRIO-5:46, naomba utueleze hizo picha tunaweza tukazipataje, usiposema, utakuwa umejishushia sana afadhali ungejiita anonyo,

    wengi hawajaona picha ya kaburi la mwalimu nyerere, sasa tatizo liko wapi au uongo unatoka wapi??

    mdau
    canada

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 22, 2008

    wewe 9:32 pm hujui husabu nini! hapa unaadd kisha unasabutrakti then unajumlisha halafu unatoa uanagawa kwa EPA chini juu ya BENKI KUU kisha unatoa TWIN TOWERS halafu unakanseli balali plus serikali=UFISADI hilo ndilo jibu, SASA SIJUI UNATAKA ADD UP IPI TENA! THIS IS SIMPLE MATHS.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 22, 2008

    KAKA TRIO POSTI PICHA HAPA,USIKIMBIEE SWALIIIII POSTI PICHA ZA MWALIMU NYERERE,AU KUBALI KUDHALILIKA!!


    HALAFU ANONYMOUS WA 9:32 HAPA TUNAMUONGELEA RAIS WA ZAMANI WA MALAWI,WEWE UNALETA ISHU ZA BALALI,NYIE NDIO MNAOINGIAGA VICHWA VICHWA EMBU SOMA KICHWA CHA HABARI NA HABARI YENYEWE...PLIZ ACHA BLA-BLA NA PUMBA ZILIZOKITHIRI!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 22, 2008

    SAMAHANI WADAU KWA KWENDA NJE YA MADA KIDOGO!
    mimi kunajambo linanishangaza sana,ingekuwa ni ktk MATAMSHI tu nisinge kuwa na cha kusema sana,maana najuwa kunawatu movement za ulimi zinakuwa ngumu,pia ingekuwa ni ktk typing errors ningeona mtu kakosea maramoja nikajuwa kapitiwa tu!lakini mtu anatype kisha anarudia mara nne,tano,n.k kweli hapa ni tatizo la KABILA au ni UVIVU WA KUJIFUNZA LUGHA SAHIHI?
    mhaya akitamka MAHISHA BORA sitamlaumu,lakini akiandika MAHISHA BORA??? lazima ana shida ktk ubongo ya kutambua kipi sio sahihi na kipi ni sahihi!!!
    maneno kama hebu-EMBU,furaha-FULAHA,FURAA,FULAA??ng'ombe-NGOMBE,hifadhi-IFADHI,dhani-thani,mradi-MLADI,MULADI.taarifa-TAALIFA,habari-ABALI,HABALI n.k
    sasa kama kiswahili inakuwa taabu,je lugha tofauti na kiswahili inakuwaje?maana kwa kiingereza ukikosea herufi UMEBADILI MAANA.
    mfano:- hail-ail.
    tupende kushirikisha bongozetu jamani ili tusipotoshe maana,potelea mbali midomo ulimi huteleza ,lakini kuandika hapo sikubali haka kaugonjwa ka makabila!!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 22, 2008

    ubadilishaji wa herufi unachanganya kuelewa maana!:-
    jibu-jipu
    bibi-pipi
    sasa kiingereza ndio usiseme kabisa:-
    1.are you to visit your[haunt]aunt.
    2.we are living on the [hearth]earth.
    3.can you [eat]heat the wire.
    4.do you [ave]have 1000$
    5.i need to inhale fresh[hair]air
    na mwisho kwa leo
    6.i[eat]hate you!!!
    sasa mnao tetea kabila zenu kuwa ndio chanzo cha kusababisha muandike vituko kwa kuchanganya herufi jioneeni wenyewe hapo juu inakuwa imekaavipi kwa kimombo!!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 23, 2008

    sijawahi kuona pumba kama za humu ndani!
    watu wako nje ya mada, wengeni wanaleta mambo yao ya lugha. Swala kubwa ni kaburi la Banda.
    Ila mimi sijaona sababu ya m singi eti kaburi la nyerere lijengwe kifahari wakati jeshi walimjengea jumba na akalitolea nje.
    Lazima mjue kuwa yale ni mambo ya kupita na tuache upuuzi wa kijinga. Mjengee kaburi mipesa mingi wakati raia wanakufa njaa???
    NB: Watanzania wengi tuna imani zakidini basi tusiyaseme mabaya ya waliotutangulia katika haki (marehemu) ilihali wako katika hukumu, mdau anayeleta habari za Balali..yamepita wakubwa yuko mbele ya haki, anapata chake kwa maulaana tumuombeeni amani ya kudumu.
    ^^^---0---^^^
    Mdau-Mkuu

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 23, 2008

    wewe anonymous wa 5:35 na 6:00 UNAONGEA NINI NA ILI IWEJE???PELEKA DARASA LAKO HUKO HUKO,JIBU SWALI SIO UNALETA MADA ZINGINE ZISIZOTAMBULIKA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...