Ndugu michuzi, mimi ni miongoni mwa wapenzi wa blog hii. Tunaipenda kwasababu ni moja ya chombo kinachosaidia wanyonge, kwa kupata habari , na kutoa habari zao pia. Nami nimeona nitumie uwanja huu kutoa dukuduku letu sisi wananchi wa Gongolamboto na vitongoji vyake kuhusiana na swala zima la Usafiri.

Kipindi cha nyuma tulikuwa tukiwacheka `Mbagala’ kwa jinsi walivyokuwa wakisota kwa usafiri. Lakini kwao sasa hivi mabasi yapo mengi ila tu foleni ndio kikwazo kwao. Adha hii sasa hivi imeelekea kwetu wakazi wa Gongolamboto na vitongoji vyake.
Adha hizi zimezidi kwasababu eneo hili la Gongolamboto na vitongoji vyake limekuwa haraka sana. Wakazi wengi wamejenga huko, hivyo idadi ya wananchi ambao wengi wao ni wafanyabiashara, wafanyakazi na wanafunzi imekuwa kubwa kuliko huduma kama za usafiri.

Tatizo letu kubwa ni usafiri. Tunaamuka saa kumi ili tuweze kufika makazini kwetu, lakini cha ajabu unaweza ukasota ukajikuta unafika ofisini saa tatu, na unarejea nyumbani saa tatu za usiku (unaacha watoto wamelala unawakuta wamelala).

Magari mengi yaliyopangiwa huko hayakamilishi `ruti’ zao, mengi yanakatisha njia. Mfano, wengi wetu ambao tunaishi Kipunguni, au vijiji vya karibu inabidi tupande magari matatu au manne hadi makazini kwa wale wanaofanyia kazi maeneo kama Msasani, Mikocheni, na nauli zake ni shilingi 350, kwa kichwa. Baya zaidi ili upate gari inabidi upande kwa mtindo uitwao `geuza nalo’ yaani ulipe nauli mara mbili, kwa kwenda nalo, angalao mwendo kiasi halafu ugeuze nalo, hapo unalipa mara mbili ya nauli hiyo.

Jaribu kufikiria mwenyewe mishahara ilivyo, halafu kwa siku kwa wale tunaofanyia kazi Mikocheni tunatumia shilingi zaidi ya shilingi elifu mbili kwa usafiri tu, je watoto watakula nini, utalipia nini ada zao, je utapata wapi hela yao ya matibabu ! Mwajiri hajui wala hajali kuhusu matatizo haya.

Tunaomba vyombo vinavyohusika waangaze eneo hili, watusaidie na sisi.
Barabara ziendazo vitongojini ni mbovu ajabu (Pitia Mombasa kwenda Kipunguni utaona mwenyewe, na kwingineko). Wale waliojisajili kusafirisha abiria maeneo haya kama hawawezi waseme, wapewe watu wengine. Yawepo magari ya moja kwa moja kutoka vitongojini hadi mijini, Kariakoo, Posta, Mwenge na kwingineko, kuliko kupanda magari mengi tofauti. Asubuhi na jioni matrafiki waangalie sana hawa madereva wanaokatisha njia.

Tunategemea mabadiliko ya haraka ili na sisi tufike ofisini tukiwa hatujachoka kwa sababu ya usafiri, kwani ni heri ya kwenda Morogoro unaweza ukafika mapema ukiwa na nguvu zako kuliko usafiri wa Gongolamboto.

Mimi Mdau wa Kipinguni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2008

    Acha kulalamika wewe... Magari yanakatisha safari, kwanini wewe unakubali kushuka?

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 22, 2008

    kwa nini mnachagua CCM? unasema Michuzi apeleke maoni kwa muhusika, muhusika si mmemchagua wenyewe?kwa nini masikio yenu mmeweka pamba? hamuwasikii akina Mbowe, Lipumba , Mrema, Mtikila wanasema kila siku wachagueni kero zenu ziishe? Kwa kifupi sana [na kwa uchungu sana} wali na kofia, na tshirt za CCM ndiyo zinakufanya uamke saa 10 usiku !!!!FIKIRIA SANA.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 22, 2008

    Hameni huko, kwani maisha yako Dar tu? Mnangangania nini huko Dar kama maisha ni magumu hivyo? Hapo jirani tu Kibaha maisha ni matamu, nenda Morogoro, Tanga, Iringa na Mbeya ndio usiseme, raha tupu. Mnangangania nini Dar kama si ulevi tu?

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2008

    MAJITU MENGINE HUMU NDANI SIJUI YANAVUTA BANGI!!UNAMSHAMBULIA NINI HUYO?YEYE KAOMBA MSAADA OHH MARA HAMENI,MARA KWA NINI UNACHAGUA CCM..SASA MNATAKA WOTE TUKAE MBEZI?AU TUKAE MIKOCHENI?ACHENI HIZO BWANA..KAMA NYIE MAISHA MMEYAWEZA NYAMAZENI..SASA KAMA WALIZALIWA NA DAR NA KUKULIA DAR UNATAKA WAENDE WAPI?NYIE MMEZAMIA ULAYA SHIDA TUPU NA MAKARATASI HAMMNA KILA SIKU MNAJIFICHA KUKWEPA POLISI...MICHUZI MIJITU MIJINGA HII...

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2008

    Swala si kuhama wala swala si CCM, hapa kikubwa ni utendaji wa viongozi wa TANROADS. Nasema hivuo kwa sababu kuu hizi zifuatazo (1) TANROADS sasa hivi wanaweka lami juu ya lami Nyerere Road lakini huku Pugu Road ambayo inaanzia lango la Jeshi Mpaka Chanika na Kisarawe ni mashimo matupu (2) TANROADS toka wavunje nyumba za walala hoi ni mwaka wa saba hata bara ya wenda kwa miguu hawajaigusa, hii inasababisha watembea kwa miguu has wanafunzi na waendesha baiskeli kugongwa mara kwa mara (3) Wahusika wameweka kituo cha kwenda G'mboto an kurudi mjini hapo banana ambacho kinashabihiana na hii inasababisha daladala zinazoshusha na kupakia kusimama mshazari ambo pia wanasababisha foleni kubwa
    (4) Magari yanayokwenda na kurudi KITUNDA yanageuza hapo banana pia ni chanzo kikubwa
    Mwisho enyi viongozi wa CCM (hasa madiwani na wabunge) hamchoki kusemwa kusemwa? Makongoro tuletee peas zetu za kujenga barabara ya Mombasa - Moshi Bar, na huyo Engineer wa TANROADS hapo Mombasa mna muogopa kaziba mabati mpaka maji yanakosa njia ya kupita na wenda kwa miguu wanapata shida hasa wakati wa mvua, JK au Mzee Pinda pateni hamu japo mupitie hiyo barabara ambayo imepewa jina la Mwalimu Nyerere lakini hata hakuna aneijali

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 23, 2008

    huko hatuhami na CCM hatutaacha kuichagua. Ila hao mafisadi na wangoje muda wao utawafikia wasije wakamlaumu mtu. Nyumba wamevunja na barabara wala hawaigusi. na nyie CCM mjisafishe kwani hata hujo upinzani hakuna malaika ndio maana tunaona heri ya nusu shari kuliko shari kamili,jiangalieni

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 23, 2008

    hamieni dodoma makao makuu.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 23, 2008

    Sitarudia yaliyoandikwa hapo juu kwani mengi yana mantiki. Nitakachoongeza tu ni wito kwa watoa maamuzi (decision makers) aidha wawe wanasiasa au watendaji, wawe wabunifu kidogo. Suala la kurekebisha barabara sambamba na hii ya Pugu inayoambaa ambaa karibu na reli ingesaidia sana kupunguza msongamano. La pili je haiwezekani kuitumia hii reli ikaweka mabehewa angalau manne kila siku asubuhi na jioni trip hata mbili mbili tu kutoka Gongo la Mboto mpaka stesheni? Kwa sababu treni haina foleni nafikiri hiyo safari ingechukua takribani dakika kumi tu, na ingepunguza sana msongamano. Tuwe wabunifu tusiwe tunafanya mambo kwa mazoeae tu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...