Mwili wa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Dr. Daud Timoth Said Ballali (65) aliyefariki Ijumaa iliyopita umehifadhiwa katika Nyumba ya Maziko ya De Vol iliyoko mjini Washington DC, nchini Marekani ambako inasubiri mazishi siku ya Ijumaa.

Taratibu za ibada na mazishi ambazo KLHN imepata nafasi ya kuziona inaonesha kuwa Gavana Balali alifariki tarehe 16 hapo Washington DC na atazikwa hapo hapo siku ya Ijumaa. Misa ya kumwombea Marehemu itafanyika katika Kanisa Katoliki la Mt. Stephen Shahidi mjini Washington DC anuani yake ni ST. STEPHEN MARTYR CHURCH 2436 Pennsylvania Ave, NW Washington, DC 20037.

Ibada hiyo ya mazishi itaenda sambamba na kuuona mwili wa Marehemu kuanzia saa nne asubuhi. Hata hivyo shughuli hiyo nzima ni kwa ndugu, jamaa, na marafiki wa karibu na si kwa hadhara ya kila mtu atakaye kushiriki. Marehemu atalazwa katika makaburi ya Wakatoliki ya Gate of Heaven eneo la Silver Spring, MD.

Hata hivyo haijajulikana kwa uhakika kama mwili wa marehemu utazikwa ardhini kama ilivyo desturi ya kiafrika au utateketezwa kwa moto kwani makaburi hayo yanatoa huduma hiyo pia. Kama ulikuwa ni usia wake kuteketezwa basi kwa kanuni za Kanisa Katoliki basi itafanyika mara tu baada ya ibada.
Kwa kanuni za Kanisa Katoliki mwili uliolazwa kwa njia ya kuteketezwa kwa moto mabaki yake (majivu) hawapewi familia, kusambazwa au kugawanywa katika mafungu madogomadogo na badala yake ni lazima viwekwe ardhini au kwenye sehemu maalumu inayotumika kwa maziko ya namna hiyo.

Dr. Ballali ambaye amefariki akiwa amezungukwa na wingu kubwa la kashfa dhidi yake na dhidi ya taasisi aliyoingoza inasemakana aliacha usia uliotaka atakapofariki basi azikwe Marekani. Hata hivyo pamoja na kashfa nyingi zilizoandikwa na vyombo mbalimbali vya magazeti na kutangazwa majukwaani Bw. Ballali hakuwa mtuhumiwa yeyote na hakukuwa na kesi yoyote ile ya kihalifu dhidi yake na hivyo amekufa kama raia na mtu huru.

Hata hivyo Dr. Balali ilidaiwa kuwa aliandika barua ya kutaka kujiuzulu kutokana na hali mbaya ya kiafya uamuzi ambao haukujibiwa hadi pale taarifa ya uchunguzi wa EPA ilipotoka na Rais Kikwete kutengua uteuzi wake kama Gavana wa Benki Kuu.
Hata hivyo, taarifa ya Rais iliyosomwa na Katibu Mkuu kiongozi haikusema kama Gov. Ballali ni mhalifu, anatafutwa, au kwa namna yoyote ile amefanya makosa ya kisheria. Hilo lilithibitishwa siku chache zilizopita ambapo Ikulu walitangaza kuwa walikuwa hawamtafuti Ballali na ya kuwa kokote alikokuweko alikuwa ni “mtu huru”.

Ni kwa sababu hiyo basi ibada ya mazishi inatarajiwa kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiongozwa na Balozi wa Tanzani nchini Marekani Bw. Ombeni Sefue, watumishi wa idara mbalimbali alizowahi kuzitumikia ikiwemo IMF, ndugu zake ambao wamewasili siku chache zilizopita, na baadhi ya Watanzania kadhaa waishio maeneo ya Washington DC. Gavana Ballali ameacha mke na familia.

Raha ya milele umpe ee Bwana
Na mwanga wa milele umuangazie
Apumzike kwa amani.
Amina.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2008

    we tulishasikia ni kibaraka

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 22, 2008

    MIMI NAKUJA HAPO NAJIMIKSI KWENYE MSIBA NATAKA NIONE KAMA NITAFUKUZWA.UBINAFSI MPAKA KWENYE MISIBA DUUUh.ETI MSIBA SIO KWA WOTE.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 22, 2008

    Haki ya nani kufa kufaaana. Manake huyu mtu angekuja toa ushahidi, sisi mafisadi tungekua kwa hali mbaya sanaaaaa. Lakini sasa hivi mambo mswano na kesi ya EPA ndio imeishia hapo. Mafisadi 3 serikali 0 na mpira umekwisha.

    Fisadi Original

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 22, 2008

    Kanisa hili liko karibu kabisa na kituo cha tren cha Foggy Bottom kwenye orange/blue line na GW Uni versity, hapa Washington DC. Namba ya simu ya Kanisa ni 202-785-0982, na website yao ni.www.ststephenmartyrdc.org. Sasa hivi kanisa halipoe simu (labda wamechukua kitu kidogo) na website yao haisemi chochote kuhusu last respect ya mzee. Kwa kuwa mimi nadhani ni mtanzania pekee ninayekaa karibu kabisa na kanisa hili, basi nitakuwepo kesho kushuhudia mhasimiwa Balali akiagwa na nitawapa yaliyojir. Mzee P.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2008

    HUYU BALALI NI KIBOKO. KATUMIA HELA ZA UFISADI KUFAKE HIS OWN FUNERAL. JAMAA AKIWEZA KUWAJAZA WATANZANIA UJINGA ATAKUA KIBOKO.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 23, 2008

    hata KLH wamelipwa na balal ili kutangaza msiba kwa wabongo wenzio, KLH mbona nyie ndo mnasema ni wakombozi wa wadanganyika, sasa hapa hapa imekuwa vipi?? mbona ndiyo sivyo! Balal kawaachia EPA ngapi hapo hadi mnaanza kumpamba!!,
    Dhiki mbaya sana kumbe!
    Kumbe hata mwanakijiji ukipewa urais wa bongo kwa jinsi unavyojidai una uchungu na nchi yako utaanza Kutufisadi tu kawa!, nimeogopa sana!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 23, 2008

    who cares.?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 23, 2008

    RIP Balali...
    Shut up watanzania! Shut up! Get better things to do that ctiticise someone who is deceased... The only judge here should be GOD....If God forgave him who am I to judge? We all have our flows and if we confess no matter how big our flows with our sins are forgiven.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 23, 2008

    What really baffles me is the way most Tanzanians agree to be fooled and made to believe that the BoT scandal was entirely the work of late Dr Ballali. That so long as the main presumed culprit was silent, or his whereabouts not known, or now he's dead, the government is safe. And almost every Dick and Jane out there is caught up by this poorly manipulated fiasco.

    Moving to fire him was also meant to confirm this line of thinking, that the government also feels that all these things WERE JUST ONE PERSON'S actions!! With good friends he dished out Sh133bn for their business interests, in the ABSENCE OF GOVERNMENT AWARENESS AND APPROVAL!! This is a BIG LIE that the late Ballali had to endure and live with, until his death. Poor Tanzanian minds!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 23, 2008

    Mzee P.Tutakushukuru sana kama ukijimix nakutuletea habari za huo msiba.Hapa Bongo baadhi tunaamini kwamba ni changa la macho kabisa.Yaani huwezi kuamini leo kuna gazeti limeendika kwamba mke wa Balali(inaonekana ni mbabe sana) amesema kwamba hakuna picha itakayoruhusiwa kupigwa,Sasa hii mbona inatuletea utata?Halafu kumbe mama mzazi wa Balali kule Iringa naye amesikia msiba wa mtoto wake kwenye vyombo vya habari(hii inatupa picha gani?) na pia kwanini huyo mama mzazi hajaenda kuuzulia huo msiba?.Kuna gazeti limeandika kwamba mama mzazi anaiomba serikali isaidie kuirejesha maiti nchini.UTATA tu.Au hajafa nini?Ebu watu wa uko Washington DC mtusaidie kutupatia ukweli.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 23, 2008

    Yaani hapo hakuna cha ushahidi wala nini!!,mwili unachomwa bwana...yaani na rambirambi wanataka!!mahela yote hayo...watanzania watalipishwa kodi jamani kufidia maheala yote ya EPA..

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 23, 2008

    MI NINA MASHAKA KWAMBA HUYU FISADI NAMBA 1 HAJAFA. HAWA WANACHOTAKA KUFANYA NI KUTUZUGA TU WATANZANIA. KAMA KAFA KWANINI MSIBA UWE WA KIBAGUZI?. JAMANI TUWENI MAKINI HAPO KUNA UFISADI TENA HAPO.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 23, 2008

    NARUDIA TENA DAWA NI MOJA "TAKBIRI ALLAW......"

    KWANINI TUSIIGE MFANO WA WAIRAQ KAMA KWELI TUNA UCHUNGU? .

    HUU NI UPUMBAVU WANA KULA NA KUNYWA KWA JASHO LETU HALAFU WANAJIDAI ETI WAFU ..... HII KWELI NOMA .

    NA HAO WALIO MZOMEA MKAPA NASIKIA WAMEPELEKWA MAHAKAMANI JAMANI WANA KOSA GANI ? WANGEANZA KUSTAKIWA KWANZA WALIOTUAMBIA KUNA UFISADI HALAFU NDO SISI WAZOMEAJI MI NITAWAZOMEE TU KUm@'\/$8* ZAO SISI TUNA LALIA GONGO NA BAMIA WAKATI MTOTO WA EDO ANAKUNYWA KILA SIKU TENA KWA KUTANUA FLORIDA NA WAPAMBE KINA KINJE MWE HALAFU MNASEMA CHICHIEMU MBAY HAPANA
    MICHU USINIBANIE MI NINA MACHU......

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 23, 2008

    Mi naona bora achomwe tu,aanze kuufaidi moto toka hapa duniani.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 23, 2008

    Shemejiiiiiiii ah ! we wacha wale tu zamuyetu itafika

    tutakapo mwambia ramadhani mla vichwa na damu za watu afuatilie isu na mtandao waooo at list tuambulie hata lile fuvu

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 23, 2008

    haijalishi kafa au hajafa , tunachotaka kusikia na kutokifungia macho sisi tulio hai ni pesa za EPA zirudi na mafisadi wenzie either na wao wafe au wachukuliwe hatua tumechoka !

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 23, 2008

    Mtoa habari sijamwelewa, anaposema Gavana Balali ameacha mke na familia. Hii ina maana gani?

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 23, 2008

    kwani hatuwezi kukodi alkaida wawashughulikie mafisadi wa TZ? manake tunaweza sikia chenge naye kafia huko halafu akachomwa moto. manake BALAA Kisha chomwa kwani yee ndo kaanza yote haya nyambafu

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 23, 2008

    Samahani jamani, hivi Huyu hayati Balali alizaliwa wapi? na ni Mtanzania kutoka mkoa gani? Maana hakuna hata article moja inayomwelezea kuwa marehemu ametokea wapi, isije ikawa siyo Mtanzania!!!!

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 24, 2008

    Offcoarse nisema sio comment but nataka kusema serikali ya Tanzania na viongozi wake kuanzia Kikwete ni wanafiki na waongo kwani hapa majuzi tulisoma kuwa waziri wa mambo ya nje alisema Balali hajulikani alipo iweje leo tuambiwe Kafia Nchini Marekani tena Hospitalini na sio getho.Jamani nyie watu wa serikali ndio mnapumbaza Tanzania kwa mambo ya Ufisadi nasema MSHINDWE KWA JINA LA YESU WEWE UNAYETIITA RAIS WA TANZANIA NA SERIKALI YAKO MBOVU (CCM)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...