Shikamoo anko Michuzi!
Nimesikia hili neno 'Kubemenda mtoto' nikashindwa kujuha maana yake, naomba msaada tutani kwa wadau wanisaidie - ikiwezekana hata kwa kimombo naomba nifahamu ni nini...
Mdau wako mpenzi
Esta,
Lindi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 45 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 23, 2008

    kama kweli una nia ya kujua swali lako basi ungeanzia kwenu una shangazi au bibi zako wewe na ungeuliza na wange kupa jibu unataka kutukanwa wewe na ndio unakuja kuuliza hapa.Kama ujui ilo basi ata tigo ujui ni nini wewe na unaweza toa tigo?kaulize kwenu na uwe na busara za kuuliza

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 23, 2008

    Ester Lazima Ujuwe hilo neno!
    Kumbemenda maana yake kwakimakonde ni 'KUNTIMBANGILA' yaani kuendeleza ngono kipindi mtoto yupo mdogo sana hadi kumuathiri mtoto.
    nadhani ukikuwa utajua maana utaambiwa umlee mtoto wako na babake apunguze interuptions ili mtoto anyonye miaka miwili swaaaafi.

    Kitaalam wanasema sio issue sana ingawa kikubwa ni kuhakikisha hupati mimba na pia unakuwa msafi kwani jasho la ngono humuathili mtoto..

    Mimi mtoto sana so sijuwi zaidi ya hapo!

    G7
    UK

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 23, 2008

    Kubemenda maana yake ni pale mama anayenyonyesha kulala na mwanamme mwengine mbali na baba wa mtoto, hapo anakuwa amembemenda mtoto wake, maana watoto wengine huugua kwa sababu hiyo na hudumaa yaani hawakui vizuri.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2008

    sasa wewe huko ulikosikia hilo neno kubemenda nadhani ndiko jibu liliko,BWANA WEWE.CHAWA?HASWA HUO NKOA WA LINDI,

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2008

    maana yake ni "kulakatua"

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 23, 2008

    KUMBEMENDA MAANA YAKE NI KUMPIGA MTOTO KWA NGUVU ZOTE NI KM KILUGHA CHA WAMARABA WA HAPO LINDI WALE WANAOSEMA BAAAAA WEWEEE NDIO WAJUZI SANA WA MANENO HAYO MDAU MKAZI WA LINDI SABASABA

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 23, 2008

    we binti acha uzushi!mama gani asiyejua maana ya kubemenda tena aishie pwani?kwa ufupi kubemenda ni hali anayo pata mtoto kuchelewa kutembea hasa ikitokana maingiliano ya unyumba kwa mama anae nyonyesha upo hapo!

    ReplyDelete
  8. Dada Esta. Yaani Wahaya huwa mnanimaliza. Mbali na ujanja wenu wote na kujifanya mmesoma sana kwa nini lakini herufi h inawapa taabu namna hiyo? Sasa tazama hapo eti unasema "...nikashindwa kujuha..." Kujuha ni nini? Neno -juha kwa Kiswahili sanifu ni mtu mpumbavu, mjingamjinga n.k. Sasa unaposema nikashindwa kujuha unamaanisha nikashindwa kuwa mpumbavu? Kuwa makini na lugha tafadhali...kubemenda mtoto katika Sheng (Kisheng) kule Kenya ni kufanya mapenzi na msichana (mzuri). Naamini kuna maana zingine na wadau wengine watachangia.

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 23, 2008

    Baaaa,Somo Esta kwani wewe ukutolewa mwali(unyago)mimi siyo mtaalamu lakini nilikuwa nakushangaa tu wewe wa kutoka kusini nilifikiri ndiyo mnamjua zaidi haya mambo but guess what...usikonde umefika mwake utapata kila aina ya jibu hapa ndani ya nyumba,Good Luck Somo

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 23, 2008

    dada Siyo Kujuha ni kujua

    ReplyDelete
  11. NILIVYOJULISHWA MIMI NI KWAMBA KAMA MAMA ANANYONYESHA MTOTO HALAFU AKAJIHUSISHA KIMAPENZI NA MWANAUME ABAYE SIYO BABA WA MTOTO, MAZIWA YANACHAFUKA NA YANALTA ATHARI KWENYE MAKUZI YZ MTOTO. HASA UPANDE WA VIUNGO VYA MWILI

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 23, 2008

    Umeshindwa "kujuha" maana ya kubemenda kwa sababu wewe mwenyewe pia ni "juha"

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 23, 2008

    Kubemenda i Kubeba mimba wakati ukiwa na mtoto mdogo anayenyonya hali ambayo husababisha HORMONE za mama kuanza kutoa virutubisho vya mtoto aliyepo tumboni na kumwacha anayetaka kunyonya akiwa hana kitu na hivyo kuathiri ukuaji wake na pengine hata kushambuiwa na magonjwa.

    DR. MMIMBAJI

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 23, 2008

    ...Mdau wako mpenzi, Esta...

    Mimi nina wasiwasi hapo Michu. Natumaini mkeo hataiona hii.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 23, 2008

    We Esta muongo, mtoto wa Lindi hujui kubemenda? au unataka hoja tu?

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 23, 2008

    Acha usanii wewe....yaani mwanamke wa Lindi usijue maana ya Kubemenda...kama ungekuwa umetoka Shinyanga ningekupa jibu, naona unatu-twist hapa

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 23, 2008

    kubemenda mtoto maana yake ni kufanya mapenzi na mwanaume mwingine asiye baba wa mtoto wakati unanyonyesha, kubemenda ni kuwa mtoto hakui anagota hapo hapo, hivyo wenyeji wanasema mtoto umembemenda.... kwa kiingereza sijui kama wanatafasiri vipi hili, ila neno hili lilikuja juu baada ya gazeti la udaku kuandika msanii mmoja kuwa anambemenda mtoto ndipo nasie tukatoka tongotongo, kwenye kamusi halipo ila kwenye kamusi ya mtaani lipo !! nadhani ni neno la wenyeji wa mkoa wa dar es salaam.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 23, 2008

    kuna muda fulani ambao mwanamke akijifungua na haswa akiwa ananyonyesha atakiwi ale uroda kwani akila uroda na haswa bila mpira basi yale maziwa anayonyonya mtoto huwa yanakuwa na hitilafu ambayo yanaweza yakampatia mtoto hafya mbovu,upele na kadhalika. sasa mtoto akiwa kwenye hali yiho ndo huitwa kabemendwa.

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 23, 2008

    Unashindwa KUJUHA au Unashindwa KUJUA,rekebisha kiswahili chako nadhani wewe Mhaya wa Bukoba kwa akina Mpoki.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 23, 2008

    Mhh Ndugu Ester, Naomba kwanza kunyoosha lugha, neno " KUJUHA" Nafikiri usahihi ni "KUJUA". Kubemenda nafikiri ni neno linalotumika kumaanisha kupiga mtu/mtoto kwa mkono bila kutumia fimbo.Kwa mfano kumpiga ngumi, konzi/kwenzi, au kofi.

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 23, 2008

    Kubemenda ni kumtafuna mtoto kama Ramadhani Juma!!na mtoto kuvaa makandambili makubwaa na kuarisha kwa mbele..

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 23, 2008

    Mtu mwenyewe unaishi lindi,halafu unajifanya hujui Kubemenda si uongo huo!!usitufanye sisi Kideo bwana...

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 23, 2008

    kubemenda mtoto hutokea mama anapobeba mimba nyingine huku angali na mtoto mwingine mchanga aliyejifungua karibuni. Kutokana na misukosuko ya kawaida ya ujauzito, malezi ya mtoto aliyemchanga huwa siyo ya kuridhisha, hivyo mtoto anavyoofu kiafya, hali hii ikitokea ndio tunasema mtoto kabemendwa.

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 23, 2008

    Michu naona hii blog inaelimisha wengi, Mimi mwenyewe nina miaka 39 leo ndo mara ya kwanza nasikia hiyo " kubemenda"

    MICHU TUENDELEZE LIBENEKE HAPA

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 23, 2008

    Msimlaumu jamani mimi mwenyewe nilikuwa sijui maana yake

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 24, 2008

    Ama kwa hakika asiye funzwa na mamae hufunzwa na Ulimwengu !!! wewe Esta hivi una umri gani lakini ? Mimi naona kuna mengi huyajui na hii ni kutokana na kwamba inaonyesha wewe ni mpayukaji sana na mjuaji mno ndio matokeo yake haya shangazi zako na bibi zako na dada zako wanakuangalia na ujuaji wako sasa ndio haya unakuja kujiadhirisha hapa bloguni kwa jamii. Mimi nakushauri ndugu yangu kama umewakosea omba samahani na uache kupayuka ili uwekwe chini wakupe maana na maadili, vitu ambavyo ni muhimu sana katika maisha ya mtoto wa kike haswa wa KiTanzania la sivyo ndugu yangu umelosti mlosto wa nguvu,kwani hapa sio Unyagoni hii ni blogu so usiweke silaha mahala pasipohusu. Si unajua ule usemi wa " Asiyejua maana ...........??". Ndimi Mdau Nambari Wani wa UK

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 24, 2008

    Weka basi hiyo picha yako ili tukuone sio unataka kujua tuu au njoo nikuonyeshe jinsi inavyokuwa
    mimi nipo nangulukulu lindi

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 24, 2008

    Brother Michuzi nadhani hii Mada naomba uitafutie thread yake pekee kwani sio juu ya maana ya kubemenda bali juu ya suala lenyewe.

    1. kitaalam nasikia hatakama mama kapata mimba nyingine anaweza kuendelea kumnyonyesha mtoto mpaka miezi mitano hadi saba bila madhara. Tuachane na waropokaji kama kuna waliosomea. sio waliokariri humu ndani watuambie nini hasa nikweli. ningependa waongee kupitia tafiti zilizo sanikishwa.

    2. wengi humu wamecoment kwamba ni pale ngono ikifanyika kati ya mama na mume ambaye siye baba wa mtoto.. Is it true? and how does make sense kwani still they are same sperms!!

    All the best wazee!

    G7
    UK

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jaman msimlaumu hata mm cjui maana ya kubemenda,, naomna mnifahimshee

      Delete
  29. AnonymousMay 24, 2008

    TO YOU MCHANGIAJI MAHIRI!

    ACHA UKABILA!
    ACHA UKABILA!
    ACHA UKABILI!

    na uache kwa nguvu zoteeeeeeee - shindwa na ulegeeeee..na kisifanksheen

    kokutelela

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 24, 2008

    Hapa nimeamini kuna mambumbumbu wengi sana yaani mtu anajibu kwa madaha huku hajui anachokiongelea. Eti mtu anafikia kusema mtoto anaadhirika mama akifanya mapenzi na mwanaume ambaye si baba wa mtoto. HUU NI UJINGA KABISA KAMA HAUJUI JIBU LA SWALI, just shut the hell up na uache wanaojua wajibu hilo swali. Tatizo wengi hapa ni VIMBELEMBELE wa kujibu mambo ya kitabibu au kisayansi wakati watu wenyewe mmesoma KLF na HKL high schools. Aliepatia ni DR MMIMBAJI na anon mmoja. WENGINE wote mmeandika PUMBA TUPU.

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 24, 2008

    Bro Michu sio kinamama tu wanaoweza kubemenda watoto wao. Hata baba anapotoka kukandamiza mwanamke mwingine na akaja kumbeba mwanaye mchanga atambemenda.

    Ni vizuri kujitunza wote wamama na wababa mnapokuwa na mtoto mdogo ili awe na afya.

    ReplyDelete
  32. taratibu basi muuliza swali!
    we yaani hujui tu, sema ukweli,
    si unawajua mabinti wa kisasa,
    kwa jinsi wanavyopenda anasa,
    basi anakuwa ananyonyesha,
    huku na wanaume akijistaheresha,
    ujuwe hapo anamharibu mtoto,
    ndo hapo kesho yakuwa majuto.
    nimemaliza.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 24, 2008

    Soomoo Esta, kweli hujui au juha?
    Ngoja nikupe nyepesi nyepesi. Hii watoto wa mjini wanaita kwa 'code name' FUNDI VIATU. ili mzazi asijue kama anasemwa yeye.
    Ni hivi, Akina mama wana Hormones kuu mbili, Oestrogen na progestorene, na huwa zinatolewa na Ovaries.
    sasa basi ukiwa na mimba two things happens, 1. level ya hizo hormones mbili zinakuwa juu. 2. Placenta inaanza kazi ya kutoa hizo hormones badala ya ovaries.
    Hizo hormones zinasababisha 'womb' kuwa tayari na MAZIWA kujaa. Kumbuka kama bado unanyonyesha ile balaa ya mtoto Kunyonya hayo maziwa yasiyofaa ndio yanaleta hicho kizaazaa.
    Kwa hiyo awe ni baba wa mtoto au wasaidizi wengine hakikisha unajitahidi usipate mimba.
    a. hesabu circle yako vizuri ambayo mara nyingi inakuwa disturbed baada ya kuzaa.
    b.wavalishe mipira au vaa mpira mwenyewe.
    c.uliza auntie, bibi au kungwi watakueleza nini cha kufanya.
    d.ukipata mimba acha kunyonyesha.
    BADO naendelea na UTAFITI.

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 24, 2008

    JAMANI. NATOA MAONI. WATU WA KABILA MBALIMBALI WAENDELEZE UNYAGO KUELIMISHA VIJANA. KITCHENI PARTY HAZITEKELEZI ELIMU YA VIJANA KATIKA KUJILINDA NA MAISHA YA KILA SIKU NA JAMII KWA UJUMLA. MASWALI KAMA HAYA HAYATAJITOKEZA HUKU KWANI HATOPATA JIBU SAHIHI ATACHANGANYIKIWA BUREE!

    ReplyDelete
  35. Nakubaliana na baadhi ya wadau walotangualia hapo juu, ambao wanasema kuwa hakuna uhusiano kati ya mtoto kudhoofika na kutokua kutokana na jasho la mama iwapo atafanya ngono na mtu mwingine asokuwa mumewe wakati anamnyonyesha mtoto huyo. Ni kweli neno "kubemenda" huko home linahusishwa sana na mama kumuathiri mtoto kutokana na kufanya ngono na asokuwa baba ya mtoto au kubeba mimba, lakini kiutaalam hakuna uhusiano wowote ulothibitishwa kama huo. WHO katika ripoti zake inashajiisha mama kumnyonyesha mtoto wake hata ikiwa amepata mimba. Kuna reserch kibao zinazoonyesha kuwa kupata mimba si sababu ya kumwachisha mtoto kunyonya, ikimaanisha hata maziwa ya baada ya mama kuwa mjamzito yanaweza kumsaidia mtoto na hormone za wakati wa mimba hazina athari mbaya kwa maziwa ya mama.Sikatai kuwa kubemenda kunaweza kutokea, lakini sababu zake si labda hizo tulizozowea kuzisikia kutoka kwa bibi na babu zetu. Lakini pengine mtoto kudhoofika na kutokukua hata kuchelewa kutembea kunaweza kusababishwa na masuala kibao, mojawapo ambalo ni la wazi ni hilo kuwa, mama ambaye atamuacha mwanae bila kumshughulikia vizuri huku akikimbiza wanaume huku na huko, ni wazi kuwa mtoto atapata utapiamlo mbao una madhara kemkem kwa mtoto. Aidha mama ambaye atakuwa hamshughuliki vizuri mwanae, na anashughulikia mijibaba sehemu sehemu, hata mtoto kukosa mapenzi ya kuwa na mamake, sembuse mlo wake muhimu ambao ni maziwa mpaka miaka miwili, ni kweli hatokuwa, atadumaa na kudhoofika. Kwani hakuna ushahidi wowote wa kitaalamu unaoonyesha iwapo, mama atamnyonyesha mtoto wake vizuri, na kumpa mapenzi yote kama mzazi, kumshughulikia kwa mambo mengine kama chanjo, virutubisho na mlo kamili basi mtoto huyo adhoofike na asikue vizuri, hata kama mama huyo anafanya ngono na mwanamme asokuwa baba wa yule mtoto. Kwa hivyo wadau kuhusu maana ya neno kubemenda mimi sikubaliani nalo kama lilivyozoeleka kutumika.

    Obstetrician, Uajemi

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 24, 2008

    jamani lazima tufahamu ya kwamba kila anachokula mama kuna kinachopiiliza na kwenda kwenye maziwa anayonyonya mtoto,ndo maana hata ukila pilipili itamuwasha tuu mtoto kwa kupitia kwenye maziwa na hata ukinywa pombe ni hivyo hivyo, sasa mama anapofanya mapenzi iwe na baba mtoto au mtu tofauti zile sperms zinakwenda zinatengenezwa huko mwilini na kuingia kwenye maziwa na mtoto ananyonya maana pia kuna wengine wakati wa tendo hilo pia zipo zipitazo mdomoni, sasa zikienda kwenye maziwa basi mtoto ananyonya na kwa sababu hazipashwi kuliwa na mtoto hapo ndipo tatizo linapoanza na mtoto anaanza kudumaa, na mama badala ya kukazania kumpa lishe bora akaendekeza ngono basi inakuwa balaa maana mtoto huyo hata akikua atajulikana kwamba alibemendwa ukimuangalia miguu tuu....hivyo wazazi haswa akima mama kuweni makini sana

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 24, 2008

    Kweli washika dau mnapenda kuongea kama huna cha kuongea ni vema uache wenye nacho waelimishe jamii.Nakubaliana na wadau waliosema unyago urejeshwe kwa nguvu zote kitchen party ni kupata vyombo tu na sikingine.
    Mdau.Nyamkwaikure!!!!!!!!

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 24, 2008

    Kumbemenda mtoto ni kuanza kumvutisha Bangi mtoto wakati akiwa ana umri mdogo,wa kuanzia mwaka mpaka miaka 9. kisheria mtoto anatakiwa aanze kuvutishwa bangi akiwa na umri wa miaka 10. kabla ya hapo anaweza kuvuta sigara ya kawaida tu. mdau Dk Komba .

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 24, 2008

    Dr wa Uajemi, hicho ulichokisema ndicho haswa kilichokusudiwa na wazee wetu tangu asili. Ni kuwa mama ashughulike na malezi ya mtoto na si kuhangaika na wanaume huko na kule, na vile vile makabila mengine wanasema hata baba pia anaweza kumbemenda mtoto na wengine huangalia utosi wa mtoto kujua kama baba hutoka nje ya ndoa au hapana. Hii yote ni katika kulinda maadili ya ndoa na afya ya mtoto, ndio maana ikawa mwiko mama kutembea nje ya ndoa na kutembea na mumewe pia mpaka taratibu fulani fulani zinapofanywa. Kumbukeni miiko mingi ilikuwa na malengo mazuri ingawa iliwekwa kwa vitisho. Imagine kijiji kizima wamuone mtoto wako amedhoofika pengine kwa ajili ya uvivu na uzembe wa mama mtoto, unafikiri huyo mama mtoto hatajirekebisha? Itabidi ajirekebisha na akazane kutunza mtoto ili hata mume na ndugu wengine waisone kuwa kumbe ana kabustani pembeni.

    Lingine hilo la kulinda maadili ambalo ni la hatari kwa kweli hufanywa na kabila fulani ambapo wakunga humwambia mama aliyeshikwa na uchungu amtaje baba wa mtoto kabla hawajamsaidia kujifungua. Kwa kina mama waliokwisha zaa nafikiri wanafahamu unakuwa katika hali gani unapokuwa na uchungu wa uzazi, kwa kweli kama ni kweli hii nayo si nzuri kwa sababu inaweza kuwa hapo mzazi anahitaji msaada na huduma wao wamekalia kunga'ngania taja ulitembea na nani zaidi ya mumeo, tena ni wanawake hao perpertuator wa kukandamiza wanawake wenzao.

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 25, 2008

    Kubemenda kwa kiingereza ni kuwa-"domant" just like the way is applicable to volcano mountains.. utandelea kukua lakini taartiiiibu..

    Chanzo: kitu chochote ambacho kita-affect up bringing either be psychological or environmental effects..

    Hayo mambo ya jasho la ngono (even same parents can produce in such), maziwa kuchachuka (how many women get pregnant within three months after delivery?)..

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 26, 2008

    mi sijajua km wachangiaji wengi km muuliza swali alivyotaka unajua mimi nimesoma lindi kunanzia msingi mpaka sekondari ndio nikatoka sasa kwa maana halisi ya lindi NENO KUBEMENDA ni km kumpiga mtoto hii ni tafsiri ya kilindi ya wakazi wa huko na hizi za kisayansi wao awazijui na km wanajua ni wachache sana na hii lugha kwa lindi ni lugha nyepesi sana kwa maana hata km mama yako na baba yupo unaweza ukaongea kwa kumueleza mama yako lkn si kwa tafrisi ya kisayansikuna maneno mengi tu yanaongelewa huko lindi kwa mfano
    mtu akiwa mbaya kwa sura wao wanasema AMENYATA
    2.BAAA WEWE yaani mtu anashangaa kitu
    KUPENDA VYA BWELELE --BURE
    na mengine mengi ambayo nikiyasema michu atanibania maana kwa kikwao ni matusi hila sie kwetu ni maneno ya kawaida tu
    mzee wa lindi
    3.

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 26, 2008

    mi naungana na mdau aliosema kubemenda ni kitendo cha kumvutisha mtoto bangi akiwa chin ya miaka 9,mtoto chin ya miaka 9 anatakiwa avute sigara tu siyo bang.

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 26, 2008

    Ni kumpa mtoto bangi mapema kabla ya miaka kumi ... mtoto kabla ya miaka kumi anatakiwa apewe sigara na gongo tu

    Mdau wa hapo juu hongera sana kwa ufafanuzi mzuri

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 27, 2008

    jamani msichanganye hilo neno kubemenda la kilugha na neno la kiswahili kubumunda. Kubumunda inamaana kumpiga mtu iwe mtoto au au mtu mkubwa alozidiwa nguvu kwa kupigwa na mtu si wa rika lake au mtu alomzidi umri, akimpiga mtu ngumi kisawasawa ile ndio tafsiri ya kubumunda hiyo ya kubemeda mimi ni leo nasikia ndio maana naliita hilo neno kilugha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...