ORCHESTRA SAMBULUMAA...chini ya uongozi wa Nguza Viking (gitaa begani),ni moja ya bendi zilizotingisha anga la muziki Tanzania miaka ya 90. Hapa wana Sambulumaa wakiwa kwenye mazoezi ya mwisho kabla ya kujimwaga kwenye shoo yao ya kwanza Diamond Jubilee. lister elia ni huyo aliyesimama wa tatu toka kulia. wa mwanzo kulia ni king kikii

Lister Elia(kati) ni miongoni mwa waanzilishi wa bendi ya Sambulumaa,alishiriki katika ukung'utaji wa keyboards nyimbo zote za wana Sambulumaa kama "Kadiri Kasimba" utunzi wa Kianga Songa,"CCM imekua" utunzi wake Skassy Kasambula na "Mama Happy" utunzi wake mwenyewe Lister Elia.


Kwa sasa Lister anaendeleza libeneke katika jiji la Tokyo ambako anaishi na kufanya kazi kama mpiga kinanda wa kulipwa na pia Lister ndiye mtunzia wa vitabu viwili vinavyohusu upigaji wa vyombo vya muziki kama Piano na Gitaa.


Kitabu chake cha tatu ambacho ni cha riwaya(novel) kinachoitwa "The mystery of Tamko's death,ambacho ni cha kiingereza na kimetafsiriwa pia kwa kiswahili kipo mitamboni kuchapwa na kinatarajiwa kutoka baada ya muda si mrefu.


Tembelea tovuti ya kijana huyu ugundue mengi. http://www.listerelia.com/



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 18, 2008

    Kaka Michuzi.
    Nyie wazee wa zamani mliokuwepo enzi hizo hebu tufahamisheni sie wa kizazi kipya- Hivi hao wanaosemekana ni wanandugu walikuwa wanavaa MAWIGI toka enzi hizo au ndo AFRO hilo?
    Kaka Kitime na we saidia hapo kwa kuwa ulipiga nao muziki.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2008

    Braza Michu au mdau yoyote hebu nisaidieni hawa mapacha Kasaloo Kianga na Kianga Songa wako wapi siku hizi?nimepoteza kumbukumbu kidogo!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2008

    Kasaloo Kyanga: Bwana shamba iliyetingisha kwenye muziki Tanzania

    na john maduhu, mwanza

    “Usinione bwege Baba ‘Kalubandika aa eeh’, kwa kukubali wito wako Kalubandika, Haya yote ni matatizo ya dunia, nilitaka kujitumbukiza ndani ya moto, Kumbe bwana yule hana kitanda wala shuka, pa kulala hana, analala kwenye stand ya basi, Kalubandika

    yoyoo, acha vituko wewe Baba’.

    Kwa wale wapenzi wa muziki wa dansi kibao hicho kilichotungwa na mwanamuziki maarufu Kasaloo Kyanga akiwa na bendi ya Marquiz Original ya mjini Dar es Salaam katika miaka ya 1980 mwanzoni.

    ‘Kwa maisha hii tumeishi nawe siwezi kuvumilia Almas , Kwa namna hii umenitesa siwezi siwezi kukusahau hadi kifo, Almasi mzazi mwenzangu, kumbuka watoto tumezala mimi nawe, leo unaniacha peke yangu Almasi, ntafanyaje, ntafanyaje, yeeh Almasi eeh baba, eeh Almasi eeh kakaaa.’

    Hii ilikuwa ni katika bendi ya Tomatoma. Lakini pia unaweza kuwa unaikumbuka Kadiri Kansimba. Wimbo ambao uliibeba kwa kiasi kikubwa bendi ya Sambulumaa.

    “Kadiri Kansimba, naonekana mjinga, Kadira Kansimba hayo si maisha, uaminifu wangu kaka naonekana mjinga, nifanye nini sasa mie mapenzi yangu kwako ni bure, niseme nini sasa cherie sema nijue mama, ooh mama Kadiri Kansimba oooh naonekana bwegeee’

    Katika mazungumzo na Bingwa mjini Mwanza, Kasaloo ambaye hivi sasa amejiunga na bendi ya Mwanza Carnival inayomilikiwa na Emanuel Mbwele anasema kuwa kibao hicho kamwe hatakisahau kwa kuwa ni mojawapo ya vibao ambavyo vilimuweka katika chati ya muziki hapa nchini.

    Kasaloo ambaye enzi hizo alivuma katika bendi mbalimbali za muziki wa dansi akishirikiana na pacha mwenzake marehemu Kyanga Songa, anaeleza kuwa biashara ya muziki kwa wakati huu ni tofauti na miaka ya nyuma kwa kuwa ushindani umetoweka na kubakia bendi chache.

    “Wakati ule kulikuwa na bendi nyingi na zenye majina makubwa,wanamuziki tulikuwa tukishindana kutunga nyimbo nzuri kwa ajili ya kuwaburudisha mashabiki na kuinua kipato,hali hivi sasa ni tofauti na hata nyimbo nyingi hazisisimui kabisa,” anasema.

    Kasaloo baba wa familia yenye watoto sita, wanne wakiwa ni wa kiume na wawili wakiwa ni wa kike mapacha alizaliwa nchini Congo katika eneo la Bukavu mwaka 1957 na kusoma katika shule za huko kabla ya kujitumbukiza katika fani ya muziki kwa kuanzia katika Bend ya Gramic Jazz.

    “Hatukuwa na historia ya muziki katika ukoo wetu, hata marehemu Kyanga hakuwa mwanamuziki hapo mwanzoni kwani yeye alisomea ubwana shamba huko nyumbani, siku moja akiwa Bukavu alisikia wimbo wangu mmoja akiwa likizo ambao likuwa nimeurekodi baada ya kuja Tanzania na kuamua kunifuata na kisha naye kujitumbukiza katika muziki,” anasema.

    Kasaloo anasema ameamua kujiunga na endi ya Mwanza Carnival baada ya kushwawishiwa na wanamuziki wengine maarufu aliowahi kupiga nao muziki katika bendi mbalimbali hapa nchini kabla ya kutimkia Nairobi nchini Kenya .

    Anawataja wanamuziki hao kuwa ni Benno Villa Antony pamoja na mpuliza tarumbeta mashuhuri Ally Yahya ambapo tayari ameishatunga nyimbo kadhaa ambazo ni ‘Umekwama’, ‘Mchezo umekwisha’, ‘Zambe Mokale’ ambao ni wa kilingala ukiwa na maana ya Mungu Muumba pamoja na Pokeeni Salaam.

    Anasema kuwa amefarijika kujiunga na bendi hiyo anayoieleza kuwa ni moto wa kuotea mbali baada ya kuwaona wakiimba wimbo wa kuipongeza timu ya Taifa Stars akiwa nchini Nairobi nchini Kenya .

    “Kwa kweli baada ya kuwaona akina Benno na Ally Yahya wakiimba wimbo huo kupitia luninga ya EAT nilipatwa na mshituko mkubwa, sikuamini macho yangu na kuanza kuwasiliana nao,nikawauliza mkoa Dar es salaam, nimeona wimbo wenu mzuri,lakini walinieleza kuwa wako Mwanza, sikuamini kama Mwanza wanaweza kuwa na bendi bora kiasi kile, ndiyo maana nami nimeamua kuungana nao, tutafanya makubwa siku zijazo,” anasema.

    Akizungumzia muziki na jinsi alivyoingia nchini, Kasaloo anasema kuwa baada ya kuvuma katika bendi ya Gramic ambapo pia alikuwa akipiga muziki na mwanamuziki Dk. Remmy Ongara, mwaka 1979 alifuatwa na Mosengo Fan Fan aliyekuwa mpiga solo wa bendi ya TP OK Jazz na kujiunga na bendi hiyo.

    Anasema kuwa hata hivyo hakukaa sana na bendi hiyo kwani alijiunga na bendi ya Super Matimila na kukutana na Ally Yahya pamoja na Skassy Kasambula ambapo hata hivyo walikuwa wakipiga muziki kwa mkataba katika bendi hiyo.

    Septemba 1981 alifuatwa yeye na wenzake na mfanyabiashara Timi Thomas ambaye kwa wakati huo alikuwa akiishi na kufanya kazi zake nchini Botswana na kuanzisha bendi ya Orchestra Toma Toma na kupakua vibao kama Almasi, katika wimbo huo mmoja wa wanawake alikuwa akimlalamikia mwanamume aitwae Almas ambaye aliamua kubadilika kitabia baada ya kuishi na mwanamke huyo kwa kipindi kirefu.

    Baadhi ya beti za wimbo huo niAnasema kuwa wimbo huo pia ulimpandisha chati katika Bendi hiyo ambapo aliondoka na wanamuziki wengine wanane kwenda kuianzisha toka Matimila,na kuwataja wanamuziki hao kuwa ni Skassy kasambula,Abuu Semhando,Kabaa Balele,Ally Yahya,Kaole Mutimanywa na wengineo ambao hawakumbuki.

    “Siwezi kuelekwa kwa nini niliamua kuondoka Matimila kwa wakati ule,kwani tulikuwa tukilipwa vizuri na maisha yalikuwa mazuri,nadhani kikubwa ni ujana na sio vinginevyo”,anasema.

    Anasema akiwa katika bendi hiyo ya Tomatoma alitunga wimbo wa Mwanaidi ambao ulikuwa ukielezea jinsi mwanamke mmoja ambaye alikuwa ameolewa na kuishi na mume wake, lakini baada ya muda akabebeshwa ujauzito na mwanamume mwingine na kuleta kasheshe kwa mumewe wa ndoa.

    Kasaloo anasema kuwa baada ya kukaa mwaka mmoja katika bendi hiyo aliamua kuondoka na wenzake kadhaa na kwenda Arusha na kujiunga na Kurugenzi ambapo hata hivyo hawakukaa sana na kuamua kutimkia nchini Kenya na wenzake kadhaa kwa ajili ya kurekodi nyimbo zao kadhaa.

    “Safari ya Kenya tulitengeneza fedha nyingi sana, lakini tukio la kutaka kupinduliwa kwa serikali ya Kenya chini ya Rais Daniel Arap Moi lilitufanya tuondoke na kurejea nyumbani Tanzania na wanamuziki wenzangu, tulitengeneza kama shilingi 40,000 ya Kenya baada ya kurekodi, kila mtu alirudi fit hapa nchini,” anasema.

    Anaeleza baada ya kurejea nchini alijiunga na tena na Matimila, ambapo hata hivyo aliamua kuondoka na kujiunga na Maquiz na kuwakuta magwiji wa muziki kama Nguza Viking, Kasongo Mpinda, na wengineo na kufyatua vibao kama Kashala, , Ester pamoja na Kalubandika.

    Kasaloo anasema ugonjwa wa kuhama hama Bendi ulikuwa bado haujatoka kichwani mwake na mwaka 1986 kuamua kujiunga na bendi ya Tancut Almasi iliyokuwa ikimilikiwa na kiwanda cha kukata Almasi kilichokuwa mkoani Iringa ambacho kilikuwa kinamiliki wa bendi hiyo.

    “Hapa ndipo nilipoungana na ndugu yangu Kyanga Songa ambaye aliamua kuucha ubwana shamba aliokuwa ameusomea, tulikuwa tukipiga muziki na kulima, mwenzangu ubwana shamba hakuuacha, aliendeleza utaalamu wake, tulinunua shamba kubwa pale tarafa ya pawaga, hali ya kilimo ilituinua na kufanikiwa kununua magari matatu… mambo yalikuwa mazuri sana pale Iringa,” anatamba.

    “Nadhani marehemu Fred Ndala Kasheba ndiye naweza kusema alimshawishi kwa kiasi fulani kaka yangu Marehemu Kyanga kujiunga na muziki na kucha fani yake, walikuwa kwangu pamoja na Issa Nundu na alinikuta nikiwa nao kwangu wakijaribu kuigiza sauti yangu katika wimbo wa Mwanaidi, akaniuliza Kasaloo kumbe una wanamuziki wazuri nipe nami nikafanya nao kazi, alivutiwa nao sana, huo ndio mwanzo wa Kyanga katika muziki,” anasema.

    Anasema akiwa Tancut alitunga nyimbo kadhaa, lakini zilizovuma na kuendelea kumjengea jina ni nimemkaribisha nyoka, Tutasele, Masafa Marefu pamoja na Mbuguswa.”

    Kasaloo anasema mwaka 1993 waliondoka katika bendi hiyo na kuanzisha Sambulumaa akiwa na wanamuziki Said Gotagota, Nguza Vicking, Skassy Kasambula, Moses Maina na wengineo wengi.

    “Yule mmiliki wa Sambulumaa alikuwa na jeuri kweli kweli, fikiria bendi ile ilikuwa ikimilikiwa na kampuni na mkataba wangu na baadhi ya wenzangu ulikuwa umebaki miezi mitatu umalizike, jamaa alifika bei na kuuvunja na kutuchukua kwenda Sambulumaa,” anasema huku akivuta sigara yake kwa pozi.

    Akiwa Sambulumaa alitunga vibao kama Kadri Ka msimba, Mayombo akiwa na wanamuziki Rahma Shally na Zahir Zorro.

    “Wale jamaa (Tancut) licha ya kuondoka kwetu, hawakukata tama walikuwa wakiwasiliana nasi kwa muda, tulipokuwa tumeweka kambi na bendi ya Sambulumaa mjini Shinyanga tukijiandaa kuingia studio kwa mara ya pili kurekodi walituma gari hadi Shinyanga na kuzungumza nao, wakati huo kulikuwa kunatarajiwa kufanyika mashindano ya Top ten ya bendi za muziki hapa Tanzania,” anakumbuka.

    Anaeleza kuwa baada ya kukubaliana na uongozi walikwenda katika mgodi wa Mwadui na kukaa siku nne na kisha wakapelekewa ndege iliyowachukua kuwarudisha kundini Tancut na kujiunga tena na Bendi hiyo walipokaa hadi 1997.

    “Siku moja nikiwa jijini Dar es salaam nilikutana na rafiki yangu Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa na kunieleza kwa nini ninakaa Iringa kwa nini nisikae Dar es salaam, nilimueleza kuwa kule kuna bendi, akahoji kwani mie siwezi kuanzisha bendi nikamueleza unaweza na kunitaka nimpe orodha ya vifaa vya muziki, pamoja na wanamuziki ninaowaona wanafaa, nilimpatia lakini nilijua ni masihara tuu,” anaeleza.

    Anasema kuwa baada ya muda si mrefu waliwasiliana na Ndassa na kumeleza kuwa amekamilisha kila kitu kuhusu vifaa na hapo ndio ikaanza bendi ya Ngorongoro Heroes.

    “Mambo ya Ngorongoro Band yalikuwa makubwa kwa wakati huo tulikuwa tukipiga kambi pale Bahama Mama, tulikuwa timu kamili nikiwa na akina Shaban Yohana ‘wanted’, Maneno Uvuruge na wengineo, tulichukua wanamuziki wengi mahiri kwa wakati huo, tulikuwa tunatisha. Lakini baada ya miaka miwili kuna hila zilifanyika na baadhi ya watu na bendi ikajikuta inakosa uelekeo licha ya kuwa na kila kitu na kila mmoja akaondoka kivyake na mie kutimkia Botswana,” anasema.

    Anasema kabla ya bendi kusambaratika walikuwa wamerekodi nyimbo kadhaa lakini anazozikumbuka ni Naachia ngazi pamoja na Kambwembwe.

    Kasaloo anaeleza kuwa baada ya kukaa kwa muda Botswana aliamua kwenda Lusaka na ndugu yake Kyanga Songa na kuanza kutunga nyimbo za injili na hatimaye kwenda Nairobi kurekodi.

    “Tukiwa huko mwaka Oktoba 2000 sitaweza kuusahau katika maisha yangu kwani pacha mwenzangu Kyanga alifariki dunia na tukamzika huko, kwa kweli Benno Villa Antony alinisaidia sana katika msiba ule.”

    Anasema wakati huo walikuwa wakipiga kwa muda katika bendi ya Orchestre Mangelepa.

    Anasema Agosti mwaka huu aliwasiliana na Benno Villa na kuamua kuja Mwanza na kujiunga na bendi ya Mwanza Carnival, ambapo ameeleza kuwa mwisho wa kutanga tanga na kuhama umefikia ukingoni na kutaka kufungua ukurasa mpya.

    “Katika Bendi hii kuna Yahya, Benno na vijana wengine kama John Williamu maarufu kama Afande,a nayepiga gitaa la solo, kuna Anald Kalala ’baba paroko’, Abinell Mwitula ’mnyalukolo’, anayepapasa kinanda, Sebastian Lukandikija.

    Waimbaji wapo Dogo Rama maarufu kama Zimamoto, Alley maarufu kama Toto Pact, Said Sokopele, Paul Phillph maarufu kama kaposhoo, pamoja na Benno na Ally Yahya, mseto huu ni mkali sana,tutazitesa bendi nyingi sana.

    Hiyo ndiyo safari ndefu ya milima na mabonde ya mwanamuziki nguli Kasaloo Kyanga, mzaliwa wa Bukabu nchini Zaire katika familia ya watoto tisa, ambaye ametamba kutulia nchini na kuelekeza nguvu zake katika Bendi yake mpya.
    Sikonge.

    Maelezo kutoka:-
    www.newhabari.com/bingwa/habari.php?section=Jungu&id=505

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 19, 2008

    Nampongeza sana Lister Elia kwa mafanikio yake makubwa.Bila shaka na wengine wote waliokuwemo katika Bendi ya Sambulumaa.Leo kupitia Blogu hii ya Michuzi ningependa kuwachokoza wanablogu wenzangu kwamba ifike mahali Binadamu tumrejee Mwenyezi Mungu.Nawaomba nyote kuanzia leo hii tarehe 19/05/2008 tushikamane pamoja katika kumwomba Rais wetu Jakaya Mrisho Kikwete aingiwe na Moyo wa Huruma na hakika Malaika wa Mungu amshukie ili akisikie kilio chetu sisi Watanzania ambao tulithamini sana mchango wa Nwanamuziki NGUZA VIKING toka maika yote alipokuwa na Bendi ya Maquis hadi Balaa lilipomkuta yeye pamoja na Wanawe wote wakajikuta wakihukumiwa Kifungo cha Maisha kwa makosa ya kijinsia.Wanablogu wote tushikamane kumwomba Rais Kikwete amsamehe Nguza pamoja na Wanae wote ili wawe huru na warejee maisha yao ya awali na kumtumikia Mungu.Siyo tu kwamba adhabu ile ilikuwa KALI KUPITA KIASI lakini lazima niseme hapa kwamba Adhabu ya Kifungo cha Maisha ni adhabu inayostahili kwa makosa ambayo Mtuhumiwa hawezi kabisa kurekebishika na hivyo kuwa hatarishi kwa maisha ya binadamu wengine.Kosa la kijinsia ni kosa la kimaumbile ambalo mtu anaweza kabisa akabadilika na kurejea katika maisha ya kumcha Mungu.Akawa mtu tofauti kabisa na vile wengine watakavyofikiria .Makosa ya Uuaji(Murder cases/Serial Killers),Majambazi Sugu wanaotumia silaha,Mbakaji Sugu na Muuaji(Serial Rapist/Serial Killer),nk,haya ni baadhi ya makosa ambayo hata mfungwa akiachiwa huna uhakika naye kwamba hawezi kuyarudia tena.Lakini kwa makosa yaliyomkabili Viking Nguza na Wanae kwa hakika ni makosa ambayo mtu anaweza kurekebishika na kuyaacha kabisa na akarejea maisha yake ya kawaida na kuwa raia mwema kama wengine.Nalisema hili kwa uchungu nikielewa kwamba Nguza na Wanawe walihukumiwa na kufungwa maisha kama vile ni watoto yatima waliokosa mtetezi kabisa wa kuwasaidia.Nguza ana asili ya Congo DRC lakini ameishi kipindi kirefu sana hapa nchini na karibu watoto wake wote aliwazalia hapa hapa nchini kwa mwanamke wa kitanzania.Kwa hiyo kwa kiasi kikubwa nathubutu kumhesabu Nguza na Wanae kama Watanzania kabisa wenye uchungu na nchi hii kama wewe na mimi na watanzania wote.Katika kazi yake ya muziki Nguza alitoa mchango mkubwa sana katika Uhamasishaji wa Jamii katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya Tanzania kuanzia mambo ya siasa na CCM hadi masuala ya kitamaduni.Amesaidia sana kuwainua vijana wengi wa kitanzania katika fani ya muziki.Katika kazi yake ya muziki Nguza alikuwa akipendwa na kila mtu.Wanawake wengi hupenda wanamuziki wenye majina makubwa.Vivyi hivyo Nguza nina hakika alikabiliwa na kipindi kigumu cha kuweza kuwakimbia wanawake wengi waliomzonga wakimtaka urafiki wa mapenzi.Hilo limewakabili wanamuziki wengi waliopata mafanikio makubwa katika fani ya muziki.Kiasi kwamba hata Nguza alipokuja kabiliwa na mashitaka yale yaliyomkuta hata akafungwa maisha kwa kweli sisi wapenzi wake wa muziki tuliekuwa naye karibu sana katika maisha yake yote jijini Dar es salaam tulishikwa na bumbuwazi tukishindwa kuamini yaliyo mtokea Nguza na Wanae.Lakini yaliyo tokea yalisha tokea hatuwezi kurudisha mkono wa saa nyuma.Kilicho baki ni kwa rehema zake Mwenyezi Mungu mimi binafsi namuomba Rais Kikwete atumie uwezo alionao na kutoa Msamaha kwa Nguza Viking pamoja na Wanawe warejee maisha yao ya uraiani.Ikiwa Mwenyezi Mungu anasamehe kila kosa binadamu alitendalo,basi na sisi hapa duniani tuchukue mfano huo wa Muumba wetu.Kile kitendo tu cha kumfunga mtu maisha 'mbele ya Mwenyezi Mungu siyo haki,ni dhambi nyingine'.Mtu atafungwa maisha tu iwapo kosa lake HALIREKEBISHIKI au kuwepo kwa mtu huyo katika Jamii ni HATARI KWA WANAJAMII WENGINE KATIKA MAISHA YAO.Nguza hakuwa na historia ya ushenzi kiasi hicho.Hakuna Binadamu asiyetenda kosa.Adhabu ya Kifungo cha Maisha siyo kwa Nguza tu bali pamoja na Familia yake yote kwa kweli MBELE YA MACHO YA MWENYEZI MUNGU HAKIMPENDEZI HATA KIDOGO.Kupitia Blogu hii nawa asa wanablogu wenzangu tumtupie Rais Kikwete kilio hiki chetu sote,hatuwezi kumwacha Nguza yatima kama vile hakuwa na wapenzi na marafiki hapa Tanzania.Rais Kikwete atoe msamaha kwa Viking Nguza na wanae watoke nje na wawe watu huru,wao siyo tishio la amani hata kidogo.Ewe Mwenyezi Mungu pokea kilio chetu!Tutaendelea kuhesabu masaa,siku na miezi macho yetu yakielekezwa kwa Rais Kikwete kuhusu Msamaha huu!Sote katika nyakati tofauti tumemtendea Mungu Makosa lakini alitusamehe.Nasi tutende vivyo hivyo,kwa utukufu wake Mungu,Amina.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 19, 2008

    Wanablogu wote tumwombe Rais Kikwete atoe msamaha kwa Mwanamuziki Nguza Viking pamoja na Wanawe ili wawe huru warejee maisha ya uraiani wamtumikie Mungu.Sote tumewahi kutenda makosa katika nyakati tofauti lakini Mungu alitusamehe.Nasi tutende hivyo kwa wale waliotukosea.Kosa la Nguza na Wanae linarekebishika.Ni kosa la kibinadamu tu Adhabu waliokwisha itumikia kifungoni imetosha.Nguza alitoa mchango mkubwa sana katika jamii ya watanzania.Tuliuthamini sana mchango wake alipokuwa mwanamuziki toka enzi za Maquis hadi balaa lilipomkuta.Hatuwezi kumwacha Nguza na Wanae kama watoto Yatima waliokosa mtetezi hapa nchini.Namwomba Rais Kikwete kwa kutumia uwezo wake afikirie hili ombi langu,Malaika wa Mungu amshukie ili ajawe na moyo wa huruma na ktumia uwezo alionao amtoe kifungoni Nguza Viking pamoja na Wanae.Nguza siyo Serial Killer au Serial Rapist.Kosa lake linarekebishika.Na hana historia ya ushenzi au ujambazi huo wa kijinsia.Namwomba Rais asikilize kilio changu na mamilioni ya watanzania waliotambua na kuuthamini mchango wa Nguza alipokuwa Mwanamuziki na Mhamasishaji Mkubwa wa Jamii katika masuala mbalimbali ya maendeleo hapa nchini.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 19, 2008

    Wewe hapo juu acha kuongea pumba wewe, umetumwa nini?. Unasema hakufanya makosa makubwa wakati yeye na wanawe wamewabaka watoto, tena wa shule ya msingi. Wewe mwanao akibakwa utafurahi? acha ujinga. Wacha apate funzo la kubaka watoto wa wenzie. Kma una undugunae mpelekee machungwa huko jela.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 19, 2008

    Eee bwana Mdau ee.
    Mie namzimia NGUZA pale yeye na KASHEBA wanapozungumza kwa MAGITAA YA SOLO katika ule wimbo wa

    .."mama maria a twakutakia kila la heri mama..." Pumzika a kwa amani Butiama Kijijini Mama.."

    Mwanagu yale masolo jinsi walivyokuwa wanajibizana!

    We acha!

    Asamehewe jamani. Ameshajuta makosa yake.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 20, 2008

    Michuzi .. kama ni huyo wa Sambulumaa .mimi namfahamu kwa jina la LISTER NKHUWALA..KABILA MGOGO..tena toka enzi zile za Bene Bene na akina marehemu Dick Karashani . pale Rungwe OCEANIC Hotel.. pale Kunduchi ulikuwapo hapo Michu ..? wewe mzee wa YMCA .. Hujui hizo..basi enzi hizo usafiri ni kwenda huko zilikuwa basi mbili tu wenyewe tuliviita VILAKSHALI ilkuwapo POP JUICE NA SCUBA SCUBA SCABA LINE...
    Sasa hilo jina la Elia linatuchanganya au ndio majina ya kujilipulia kupata Makaratasi..

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 20, 2008

    Wenye akili,busara na nasaba zao watakuwa wamenielewa nazungumzia nini.Sina muda wa kujibizana na Punguani kama wewe Anonym wa May 19, 2008 6:04pm.Maana wewe ulikuwa unaishi nyumba moja na kina Nguza,Wewe ni Daktari uliyewapima wakati wa tukio,na Wewe ndiye Hakimu unayeijua sheria vilivyo ukawatia hatiani.Watu kama wewe wasiorejesha mioyo yao nyuma wakakumbuka ubinadamu una thamani gani mbele ya Mungu hawakosekani katika jamii.Tanzania ni nchi ya wastaarabu.Tumeweza kusamehe mengi sana mabaya zaidi kuliko hilo la Nguza na Wanae.Katika Kundi la Mamba,kamwe Kenge hawakosekani.Wewe ni mmoja wa wale Kenge wanaojifanya wana sifa ya Mamba!Pole sana mdogo wangu.Bado hujayaona mengi ya maisha.Bado namtumia salaam Rais wangu/wetu Jakaya Kikwete asikilize Ombi letu wapenzi wa muziki na watanzania wastaarabu wanao thamini utu.

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 20, 2008

    NDUGU SAVIMBI UMENIKUMBUSHA MBARISANA ULIPOTAJA ENZI ZA VILAKSHARI KWA KWERI TUMETOKA MBARI,MAANA BAADA YA HIZO SCABA SCUBA POP JOICE NINGEPENDA KUKUKUMBUSHA KUWA ZILIFUATA MUDY PANK,MY FREND NA CASSANOVA ILIYOKUWA DOUBLE COSTER PIA NIMEMKUMBUKA MDAU MKUBWA SANA WA MUZIKI KIPINDI HICHO POPOTE ALIPO AHIJO HAJI BOKASSA.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 20, 2008

    we anonymous wa huko juu acha blaa blaa hapa.. ngusa viking AFUNGWE MAISHAAA! tena tungekua jamaica,angenyongwa.. nyie fans wake msherehekee tu na mirinda sheria za Tanzania zina huruma..mimi kama mwanamke,na kama mama, kimeniuma kuona watoto wa wenzangu wamefanyiwa yale waliyofanyia,AND FOR THAT MATTER... NGUSA VIKING SHALL PERISH!!!!!!

    miss keys!

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 21, 2008

    nataka kutoka na mpenzii wangu seyyaaa,ujue sayaa nakupendaga saanaaa

    seyaa wa mivalooo,seyaaa niko wakoo
    wa kufa na kuponaaa
    seya tutokee wotee
    waseme niko wakoo

    seyaa wa mivaloo,seyaaa seyaaaaa

    JAMANI WASAMEHEWE,KWELI ISHU HII ILITUNGWA,KWAKWELI KWANIINI MWANAUME MZURI KAMA PAPII KOCHA AENDE KUBAKA MTOTO NA ANGEWEZA KUMTONGOZA MWANAMKE YEYOTE NA KUMPATA..AISEE JUSTICE PLEASE BE PREVAILED

    AMINA YUSUF

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 22, 2008

    AMINA YUSUF ONDOA PUMBA FASTA FASTA PLIZ

    miss keys!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...