Maandalizi ya fainali ya mashindano ya Miss Universe Tanzania 2008 yaanza rasmi ikiwa ni harakati za kutafuta mrithi wa mrembo wa kimataifa – Flaviana Matata (Miss Universe Tanzania 2007), ambaye mwaka jana aliipeperusha bendera ya taifa na kufanikiwa kuingia katika kumi bora ulimwenguni.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania yanaandaliwa na Compass Communications chini ya mkurugenzi wao Maria Sarungi Tsehai.
Warembo wamechaguliwa kupitia mahojiano na msako wa kitaifa na warembo 20 wamepata nafasi ya kushiriki katika fainali itakayofanyika tarehe 29 Mei 2008, katika hoteli ya Moevenpick Royal Palm.
Mashindano ya Miss Universe Tanzania yatawapa nafasi warembo hawa kunolewa na wataalam mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupewa mafunzo ya urembo, mazoezi ya viungo, ngoma za asili na kadhalika.
“Tunaweza kuona ya kuwa viwango vya warembo wetu mwaka huu vimezidi kuwa juu na tunategemea kuona mchuano mkali kwa ajili ya taji hili kubwa,” alieleza Maria Sarungi Tsehai. “Warembo wetu wanawakilisha tamaduni na asili mbalimbali za nchi yetu pana. Fainali itakuwa ni ya kusisimua.”
Warembo wa Miss Universe Tanzania 2008 ni: Catherine Mungure, Joanfaith John, Jamillah Nyangasa, Lucy Tilaha, Lilian Michael, Alicia George, Namrata Mandania, Grace Mumburi, Happy Kimbe, Eline Maronga, Happiness Kisanga, Clara Wekwe, Adeline Kapinga, Fransisca Mushi, Asia Said, MaryStella Swai, Fatma Banka, Zakhia Sheamdoe, Eva Evance na Zubeda Sakuru.
Warembo watakaa kambini katika hoteli ya Belinda Ocean Resort na wamesindikizwa na matron wao Jamilla Munisi na Sarah Martin wa Compass Communications.
Mashindano ya Miss Universe yamedhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Coke Light, SeaCliff Casino, Clouds FM, TBC, Prime Times Promotions, Smoove, Chuo cha uandishi cha TIME, Shear Illusions na Golden Touch Saloon.
Kwa maelezo zaidi wasiliana na Compass Communications:
Tel: 2182405/2182596
au 0784 305122
ka flaviana matata na ka nancy sumari vilibahatisha,tanzaniaa?sijuui!
ReplyDeleteFlavian pekee ndo alitokewa kupendwa na watu wa dunia nzima. Nancy alipendwa bt nah sio kma alivyo pendwa Flavian UK. Walimpenda sababu alikua natural in everything she wasnt ashamed of her para. Ila naomba kusema hivi jamani anae wavalisha sasa hivi ni LETS DO BETTER. Good luck
ReplyDelete