Watanzania,

Kama ambavyo pengine mmesha sikia, Mtanzania mwenzetu Ulimboka Mwaifuna amefariki dunia hapa Wichita.


Marehemu amefariki kwa ajali ya moto nyumbani kwake Jumapili alfajiri May 11, 2008. Kwa bahati, mke na watoto hawakuwepo nyumbani moto ulipotokea.


Marehemu alizaliwa 1978, na ameacha mke na watoto wawili, miaka 4 na miaka 2.


Zoezi linalofanyika sasa ni kuchanga na kukusanya pesa za kutoha ili tuweze kumsafirisha marehemu kurudi nyumbani Tanzania. Tunataka pia kumsafirisha mke na watoto ili waweze kuhudhuria mazishi.


Kwa kuwa nyumba ya marehemu imeungua, nguo za familia na vifaa ndani ya nyumba vimeteketea. Tunaomba watanzania ambao tunaishi hapa Wichita tuweze kukusanya na kuwasaiadia watoto kwa nguo na vifaa mbalimbali ili angalau tuwapunguzie mzigo huo katika kipindi hiki kigumu.

Account maalum imefunguliwa Bank Of America:
Account Number 518002076799.
Name of Acct ni Lunda Asmani.

Kutokana muda mfupi, hatujaweza bado kusajili Memorial Fund ya marehemu. Kwa wale tuliopo Wichita msiba upo nyumbani kwa

Abel Chamriho, 801 S. Christine.


Tunaomba kila Mtanzania atoe $100.00 (minimum), kabla ya Jumatano May 14, 9pm. Kule Tanzania wameshaanza msiba na macho yote yako kwetu sisi marafiki na ndugu tuliopo Marekani ili tuweza kumfikisha mwenzetu nyumbani Tanzania.


Kila siku kutakuwa na kikao saa tatu usiku ( 9pm) hapo msibani.


Tafadhali tunaomba kila Mtanzania ajiandikishe kwenye daftari la michango.


Nashukuru kwa ushirikiano wako.


Map and Directions


801 S Christine St

Wichita,

KS 67218-2635

Kwa taarifa zaidi fungua

www.tawichita.net

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 14, 2008

    Mungu amlaze mahali pema peponi, miaka 30 tu, kweli Mungu ndie anayepanga. pole kwa mama watoto na watoto kwa kipindi hiki kigumu. inna lillahi rajiuuna

    ReplyDelete
  2. RIP Ulimboka Ambelile (St. Anthony's 1994-1997)

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 14, 2008

    Tumshukuru mungu kwa kila jambo.Mungu mlaze mahali pema pepono .Mungu awajalie uvumilivu hasa mke na watoto wa marehemu.Amina

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 14, 2008

    poleni sana wafiwa,na M'Mungu amlaze marehemu peponi.Na M'Mungu ampe mkewe na watoto nguvu.Msiba mzito sana.

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 14, 2008

    RIP WU - Soljah! Big up to another Soljah 'Mbu' up there.

    Peace.

    WU Rep - NY

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 15, 2008

    Poleni wa Wichita , Ndg jamaa na Marafiki.Msiba wetu wote. Tuungane ,kama kawaida yetu tumsafirishe ndg yetu nyumbani.
    Upumzike kwa Amani kaka yetu.

    TX.

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 15, 2008

    Ulimboka, may God Rest Your Soul in Eternal Peace. We Wichitans tutakukumbuka daima. Tunakuombea baraka na fanaka huko uliko. May God give courage and strength to the family, ulimboka's wife and his two kids who are left behind. May God be there to comfort them in these very tough moments that they (family) are facing. God Bless Everyone that has been touched by this shocking news.

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 15, 2008

    Ndagha mlilile mwe gwa kwa America, i am deeply sorry for young man like him to die so soon like that, i hope its high time to rethink about 'WHY ARE WE IN THIS WORLD, OUR LIFE IS SO SHORT COMPARE TO THE ETERNAL GLORY OF HEAVEN, FOR THOSE WHOM THEY WILL DO WHAT GOD SAYS.

    pole nyingi kwa shemeji na watoto.

    mdau
    Canada

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 15, 2008

    too young to die, kweli ajali haina kinga RIP ulimboka
    Ms Bennett

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 15, 2008

    Jamani sikuhizi vijana wanakufa wadogo sana jamani..Salini sana ndugu zangu, kwani hamjui lini nani anafuatia..
    Kwa niaba ya familia ya Lt Colonel Masha, ninapenda kuwapeni pole sana wafiwa, mke wa Ulimboka na watoto.. tupo pamoja na tunamuomba mungu awasimamie ktk kipindi hiki kigum.. Lunda, poleni sana jamani..

    Mg, Brandon, Caitlin and Br..

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 19, 2008

    Hii taarifa haiko sahihi. Wichita Fire Department ilitoa report official ya tukio. Marehemu hukufa kwa kuungua, bali ni moshi aliovuta ndio uliomuua. Halafu moto ulikuwa jikono tu, wala haukusambaa kama ilivyoelezwa. Kwa hiyo mke na watoto hawakupoteza nguo na vitu vingine. Pia kwa ushauri tu, tuanze tabia ya kuwa na life insurance ili tikifa tusianze kusumbua watu na michango, kwa sababu life insurance italipia mazishi na kusafirisha maiti, pamoja na madeni aliyoacha marehemu. Again, LET'S HAVE LIFE INSURANCE PEOPLE. Kama tunaweza kuwa na magari ya kifahari, kwa nini tusiwe na LIFE INSURANCE ambayo kwa mwezi haizidi dollar 10?

    ReplyDelete
  12. watanzania wenzanu naomba tuwe na utu na kujifikiria mara mbili kabla ya kusema mambo. Hata kama mtu unaweza kuwa na ushauri wa maana kwa watu, muda na mahala pa kutoa ushauri huo inaweza isiwe muafaka.
    Kwa anony wa May 19, 2008 3:57 AM, ushauri wako juu ya life insurance ni mzuri. Lakini kwa jinsi uivyotoa (mfano kutumia maneno kama tusianze kusumbua watu na michango sidhani kama ilikuwa ni sahihi wakati huu wa maombolezo. Pengine ungeweza kutuma kwa kaka Michu kama hoja binafsi baada ya kuwa tushamalizana na matatizo haya. Mtu kama umekulia katika tamaduni ya kiafrika, na ni mtu mzima ambaye ushafikwa na matatizo ya msiba, etc. huwezi kutoa maneno kama haya kwa watu wanaoomboleza.
    Hata kuanza kuikosoa taarifa iliyotolewa na michuzi ju ya Msiba. Ni kweli kuwa baadhi ya info hazipo sahihi, lakini ilipokuwa posted habari hii, hiyo ndio taarifa iliyokuwa imesambaa katika mtandao na nadhani ndio taarifa aliyotumiwa Michuzi. Tone aliyotumia ndugu hapo juu inaonesha kukosoa na sio kusahihisha au kurekebisha, jambo ambalo kwa maoni yangu naona sio ustaarabu pia. Mdau anakuwa kama vile ana-imply kuwa waliotoa taarifa hizo walikuwa na nia ya kupotosha makusudi

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 19, 2008

    Rest In Peace Ulimboka............St.Anthony's Sec.School 1994-97 by Winston G.

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 20, 2008

    Ndugu Nalitolela: Ukweli ni kuwa sisi waafrika, aidha unakubali au la, tuna tabia ya majigambo(show off). Tunapenda kuwa na vitu vya gharama sana,hata kama hatuwezi kuvimudu. Kwa mfano: Tunakuwa na magari ya kifahari wakati tunajua kabisa kule nyumbani tulikotoka hali ni mbaya. Badala ya kusaidia familia zetu tulikotoka, tunabaki kufinance Escalade, au Surburban. Tunaacha kuwa na health insurance wakati hatujui lini tutaumwa. Kibaya zaidi, hatuna Life Insurance ambayo tukifa itatuzika, na kulipia gharama nyingine ikiwa ni pamoja na madeni tutakayoyaacha. Kwa nini creditors waanze kuja kumsumbua spouse wako, au watoto washindwe kwenda shule, au wafukuzwe kwenye nyumba kwa sababu spouse wako uliyemwacha hawezi kulipa mortgage? Ndio maana nasema tuanze kujenga tabia ya kununua LIFE INSURANCE. Tatizo lengine wengi wetu tunataka kuishi U.S. kama tunaishi Tanzania. Huwezi kuaply ideas za Tanzania zika work out U.S. Ukiwa U.S. just go with the flow...Walioanzisha Life Insurance hawakuwa wapumbavu.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 23, 2008

    rest in pease...he was soo cute

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...