Msemaji wa One Game Promotion, Khadija Kalili, akionyesha moja ya tuzo zitakazokadhiwa kwa washindi wa 'Tuzo za Vinara wa Filamu' nchini, zinazotarajiwa kufanyika Mei 30 mwaka huu kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Kulia ni moja wa majaji wa tuzo hizo, Beda Msimbe.
Na Anastazia Anyimike


WASANII nyota kwenye fani ya filamu wameshindwa kuchaguliwa kwenye kinyang'aniro cha tuzo za Vinara huku msanii Single Mtambalike akionekana kutajwa katika vipengele vitatu.

Mtambalike ambaye anajulikana kama Richie amependekezwa kuwania tuzo za mwigizaji bora wa kiume kutokana na filamu ya Agano la Urithi, mtunzi bora msaidizi na mwigizaji bora msaidizi kutokana na filamu ya The Stranger.

Akitangaza majina na filamu hizo, Makamu Mwenyekiti wa jopo la majaji, Cuthbert Kabunga alisema kuwa filamu 20 kati za 70 zilizoshiriki kwenye tuzo hizo zimechagukuliwa kuwa bora.

Alizitaja filamu hizo kuwa ni Agano la Urithi, Behind the Scene, Copy, Crying silently, Diversion of Love, Fake Pastors, Fungu la Kukosa, Karibu Paradiso, Mzimu wa Kolelo, Macho Mekundu, Malipo ya Usaliti, Miss Bongo2, Misukosuko 2, May Sister, Sengito, Silent Killer na Simu ya kifo.

Wanaowania tuzo ya Mwigizaji bora wa kike na filamu zao walizoigiza zikiwa kwenye mabano ni Lucy Komba (Diversion Of Love), Grace Michael (Malipo ya Usaliti), Halima Yahya (The Stranger), Elizabeth Chijumba (Copy), Riyama Ally 'Serena'(Fungu la Kukosa) wakati kwa wanaume ni Mtambalike (Agano la Urithi), Nurdin Mohamed "Chekibudi' (Utata), Jacob Steven (Copy), Haji Adam 'baba Haji' (Miss Bongo) na Yussuf Mlela (Diversion Of Love).

Muigizaji chipukizi wa kike ni Irene James (Miss Bongo II), Irene Uwoya (Diversion Of Love), Fatuma Makame (Karibu Paradiso), Jennifer Mwaipaja 'Shumileta' (Silent Killer), Grace Michael (Malipo ya Usaliti) wakati kwa upande wa wanaume ni Emmanuel Muyamba (Fake Pastors), Laurent Anthony (Karibu Paradiso), Hassan Nguleni (Body Guard), Yussuf Mlela (Diversion Of Love) na Uswege (Malipo ya Usaliti).

Muigizaji msaidizi wa kike ni Irene Uwoya (Diversion Of Love), Mama Frank (Yolanda), Irene James (Miss Bongo II), Susan Lewis 'Natasha' (Behind the Scene) na Tecla Mjata 'mama bishanga'(Macho Mekundu) wakati kwa wanaume ni Aliko Tshmwala (Segito), Mtambalike (The Stranger), Adam Kuambiana (Fake Pastors), Halfan Ahmed (Copy) na Emmanuel Muyamba (Fake Pastors)

Wanaowania tuzo ya mwongozaji bora ni Gervas Kasiga (Fake Pastors), Jimmy Mponda (Misukosuko II), Kulwa Kikumba 'Dude' (Macho Mekundu), Haji Adam (The Stranger), Halfan Ahmed (Copy) wakati Mtunza Sauti Bora ni Adam Waziri (Fungu la Kukosa), Cleophance Ng'atingwa (Kolelo), David Sagala (Copy), Camillius Kanuli (Fake Pastors), Swalehe Juma (Fungu la Kukosa).


Tuzo zingine zinazowaniwa ni Mpiga picha bora wa Filamu, Adui bora wa Filamu, Mhariri bora wa Filamu, Mwandishi bora wa Filamu, Mapambo na Maleba bora, Mtunzi bora wa Filamu wakati filamu zinazowania tuzo ya Filamu Bora ya Mwaka ni Behind the Scene, The Stranger, Diversion Of Love, Macho Mekundu, Misukosuko II, Simu ya Kifo, Copy, My Sister, Silent Killer, Miss Bongo I, Agano la Urithi, Malipo ya Usaliti, Utata, Kilio Moyoni (Crying Silently) na Fake Pastors.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 22, 2008

    Mbona Denzel Washington wa bongo aka Kanumba simuoni kwenye hao nominee?!

    Minongoyo na makeya eti Danzel wabongo...!

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 22, 2008

    Mbona Steve Kanumba hayumo kweye list? Si huyu alipewa award kwenye Red Carpet huko Holyowwd?

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 22, 2008

    Upumbavu tu! Hizi sinema za kiswahili zenye majina ya kiingereza zinanichefua sana! Wameshindwa nini kuzipatia majina ya kiswahili? Au wangeigiza kiingereza basi ieleweke wanatafuta soko la kimataifa! Upuuzi mtupu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 23, 2008

    Je sinema za Da Chemi na Kibira mbona hazimo?

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 23, 2008

    nakuunga mkono ndugu anonymous wa hapo juu.hizi filamu ni upupu mtupu.hapo kwenye kingereza ndo panaponiboa mimi.watu kama wanataka kuigiza kwa kutumia lugha waigize muvi yote kwa lugha. sio fulani production present sijui nini huko afu kinakuja kiswahili!ina maana hawajui hayo maneno kwa kiswahili au?ifike mahali tukubali tu kuwa kiswahili ni chetu na tukinyanyue,wakitaka waweke tafsiri ya kiinglishi pale chini.vinginevyo hayo mafilamu hayaleti maana kabisa!

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 25, 2008

    Nyie wabongo wasanii sana. Kanumba mbona hayumo kwenye hizi awards?

    Na yule matanzania wa Holly-Wood Jonie Mashaka mbona naye hayumo? Hau ni watu kuhongana ndio wapewe tuzo? Tuzo zenyewe zinanini kwani?

    Hongera kwa filamu zenu upupu !!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...