SERIKALI IMETANGAZA TENDA KWA AJILI YA UTENGENEZAJI WA VITAMBULISHO VYA TAIFA NA DOLA 152 AMA SHILINGI BILIONI 180 ZA MADAFU ZIMETENGWA KWA SHUGHULI HIYO. HABARI KAMILI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2008

    Nchi masikini kama Tanzania haihitaji kutumia mapesa katika swala la vitambulisho kwa sasa. Channel that money into University research, pump the money into Education. Suala la vitambulisho ni swala la 'precaution' ktk masuala ya security, TZ inajihami kwa nani? Kwanini tusijihami ktk swala la elimu kwa ujumla. Tuache ulimbukeni wa kutumia mabilioni ktk mambo yasiyo na manufaa mbele kama, rada, ndege ya rais, na sasa vitambulisho. Botswana, UK etc are in a different dimension, tusiige. Shame.
    M Rutachunzibwa
    Zurich, Uswisi

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2008

    yani project mpya ikitokea ujue ni namna ya ku-create ufisadi mwingine, hapo tutafisadiwa tu.hafu mihela ikiisha fisadi anatajwa anahama nchini na vijisenti vyetu punde c punde anafariki na anazikwa huko huko.
    Mungu awasaidie tu na hili dili jipya.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2008

    Ingawa inatumika pesa nyingi ktk kutengeneza vitambulisho vya taifa, mimi naona vina umuhimu hasa kwa sasa ukizingatia kuna wimbi kubwa sana la uhalifu. kitu cha muhimu hapa ni kuangalia kama ubora wa kazi utalingana na ubora wa vitambulisho vyenyewe kwani watu wengi wameandika kwamba hili ni dili la watu. Kwa uzoefu wangu wa tanzania, inawezekana kweli kuna maafisa ambao wanafanya hii kama dili la kujitajirisha hivyo basi tuanze uchunguzi kuanzia sasa ili kama kuna ubadhirifu tuuzuie badala ya kusubiri mpaka kazi ianze. KINGA NI BORA KULIKO TIBA. Nadhani sasa wtz tuingie mitaani ili tutafiti aina ya vitambulisho, taarifa zitakazowekwa n.k na tupeane habari ili tujadili mapema na siyo kusubiri mpaka ziundwe kamati kwani hazinafaida yeyote. NCHI ni yetu wote na si ya mafisadi wachache hivyo kila mtu anawajibika kuzuia ufisadi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2008

    Mi sioni haja ya kuwa na hivyo vitambulisho kwa nini watu wasihamasishwe kuchukua Passport ambayo inaweza kutumika kujua hata family tree. Passport ingetumika hata kuombea kazi,isitoshe pass zina biometric sasa hivyo vi kadi havizuii wasomali, warundi, wanigeria na wengine kuvipata.
    Naungana na mdau hapo juu tunaiga sana hata mambo ambayo si kwa wakati huu sasa hivi nchi ingezingatia hata jinsi ya kupunguza ukali wa maisha bei za Petrol na Vyakula kila siku zinapanda.Miundo mbinu ndio hiyo hadi tumekosa na mechi ambayo tuliisubiri kwa muda mrefu zaidi ya hapo Unguja siku 3 wako gizani.
    Mchangiaji

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 25, 2008

    Vitambulisho vya nini wakati nchi yenyewe haina hata post/zip code? watu bado wanatumia p.o.box halafu serikali inaanzisha vitambulisho. mtu ukiwa unatumia p.o.box ya jirani au ya kazini ukifanya uhalifu watakupata wapi?? jamani vitu vingine bora vingeachwa vifanyike kwenye mataifa yaliyoendelea. hizo hela zielekezwe kwenye sekta nyingine kama vile elimu na afya. Passport zinatosha kuwa kama kitambulisho cha mtanzania.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 26, 2008

    "SIRIKALI" ITUMIE HAYO MABILIONI KUNUNUA MASHUKA YA WAGONJWA MUHIMBILI,VIJIJINI WANANCHI WANAKUFA KWA KUKOSA PANADOL,LEO HII MNATAKA KUTUMIA BILIONS 4 VITAMBULISHO?
    HILO NI DILI LA MAFISADI FLANI FLANI(MM,BM),MAANA WAMEPIGIA DEMBE ISHU YA VITAMBULISHO 4 SUMTYM NOW

    TANZANIA UOZO KWELI,INACHEFUA!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 26, 2008

    RUTACHUNZIBWA UMEONGE UKWELI!!!
    HII SASA NI BENDERA FWATA UPEPO

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 26, 2008

    Zile social ziliishia wapi si zilishaletwa na machine kabisa na watu wakajenga sasa hivi fisadi mwingine anaenda kujenga na hizi vitambulisho

    Na omba omba Matonya ataweka wapi kitambulisho chake...si watakiiba basi wasomali wote? Tutakuwa wabongo kibao sijui kitambulisho cha bibi yangu atakiweka wapi akumbuke kilipo...Na hicho kitambulisho kitasaidiaje watu

    The Govt should allocate the money somewhere else this is so nonsense

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 26, 2008

    VILE VITAMBULISHO VILIVYOWAHI KUTENGENEZWA MIAKA ILIYOPITA NA TUKAAHIDIWA KUPEWA VIMEKWENDA WAPI? HATA HIVYO TENDA HII NI KUTIMIZA WAJIBU TU MBONA TENDA YA KUENDESHA KITUO KIKUU CHA MABASI YAENDAYO MIKOANI UBUNGO HATUONI TENDA YAKE?

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 26, 2008

    MRADI mkubwa wa Vitambulisho vya Taifa bado umegubikwa na utata, huku kukiwa na sura dhahiri ya ukosefu wa uwazi na hata kuonekana ni kinyang’anyiro cha ulaji.

    Wakati Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, akitangaza kuwa zabuni ya mradi huo itatangazwa kabla ya mwisho wa wiki hii, tayari ofisi ya mradi huo ipo na inafanya kazi na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) ameteuliwa.

    Masha anasema: “Ninachofahamu mimi ni kwamba tutatangaza tenda kabla ya mwisho wa wiki. Tutatangaza kwa uwazi kabisa.”

    Raia Mwema ilipowasiliana na maofisa wa Idara ya Uhamiaji, iliambiwa tayari ofisi ya mradi huo ipo Kinondoni, Dar es Salaam, na CEO wake anaitwa Dicksom Maimu.

    Taarifa zilizopatikana zinahoji kuwapo kwa ofisi hiyo, inayofanya kazi, huku zabuni ikiwa haijatangazwa, ikiwa ni kukinzana na Sheria ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPAA).

    Kwa kawaida sheria inataka taasisi ya umma, katika serikali kuu, iwe na bodi ya zabuni pamoja na vitengo vya manunuzi. Kama kuna ofisi au taasisi ya Serikali inakwenda kinyume na utaratibu huo, basi ni uvunjaji wa sheria,” alisema ofisa mmoja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA).

    Kwa mujibu wa ofisa huyo, Sheria ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma inaitaka taasisi ya umma kuwa na bodi ya zabuni yenye wajumbe wanane, ingawa inalegeza masharti kuwa idadi hiyo yaweza kupungua kulingana na udogo wa taasisi.

    Raia Mwema iliwasiliana na maofisa wa Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kuhusu uadilifu kwa maofisa wa serikali kushiriki kwenye utafiti wa mradi kisha hao hao ama wakawa washauri wa kampuni zinazoshiriki kwenye zabuni, au wakakabidhiwa madaraka kwenye taasisi inayozaliwa kutokana na utafiti huo.

    Kwa mujibu wa ofisa mmoja wa Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kama kuna uvunjivu wa maadili kama huo, maofisa wa PPRA wanapaswa kufanya uchunguzi kuhusu malalamiko yanayohusu zabuni au manunuzi.

    “Kwa msingi huo, mimi ninadhani kama kuna watu walishiriki katika kufanya utafiti na halafu wakakabidhiwa mikoba ya kuendesha taasisi waliyoifanyia upembuzi yakinifu, hiyo itakuwa ni kashfa. PPRA wanapaswa kufanya uchunguzi,” anasema ofisa huyo.

    Mradi huo unaonekana kuwa ‘lulu’ ya thamani kubwa.Tangu mwanzo ulikuwa unasimamiwa na maofisa wa serikali kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ofisi ya Rais (Utumishi), kama washauri, ambao sasa tayari wamelipwa kutokana na kazi yao.

    Gharama za sasa za mradi huo zinakadiriwa kufikia Sh. Bilioni 250, zikiwa zimekua kutoka Sh. bilioni 152 za makisio ya awali, ambazo zinakifanya kitambulisho hicho kuwa ghali kuliko hata kile cha nchi zilizoendelea kama Sweden.

    Lakini pia mradi unaonekana kama kinyang’anyiro cha ulaji fedha kwa kuwa baadhi ya watendaji walishiriki katika kufanya upembuzi yakinifu wa mradi, na ndio hao hao sasa wameshika hatamu katika mradi huo.

    Raia Mwema imedokezwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Mradi, Dickson Maimu, alishiriki hatua za awali za maandalizi ya mradi, kisha akateuliwa kuingia katika nafasi hiyo ya juu ya mradi, jambo ambalo linatia shaka.

    Mradi wa Vitambulisho vya taifa umekuwa ukipita katika hatua za kuiva na kufifia, kwa kuwa zabuni ziliwahi kushindaniwa, washindi wakapatikana, lakini hazikutangazwa hadharani, ikiwamo kampuni mmoja kutoka Malaysia.

    Miaka takribani 10 iliyopita, kampuni kutoka Malaysia ilishinda zabuni ya utengenezaji wa vitambulisho vya Taifa, lakini zoezi zima halikutangazwa kwa umma.

    Raia Mwema ilipowasiliana na Masha kuhusu uwezekano wa kampuni hiyo ya Malaysia kwenda mahakamani endapo mshindi mwingine wa zabuni atatangazwa, alisema tayari Serikali ilishitakiwa baada ya kuvunja mkataba na kampuni hiyo.

    “Serikali ilivunja mkataba, kampuni ikaishitaki serikali mahakamani. Law firm yangu ikaitetea ile kampuni na tukashinda kesi,” anasema Masha ambaye sasa wizara yake ndiyo msimamizi mkuu wa mradi huo.

    Lakini pia mradi huo umekuwa na hitilafu nyingine, kwa maana vitambulisho ambavyo vitapatikana vitakuwa na gharama kubwa wakati vikiwa na taarifa chache ndani yake.

    Taarifa zinasema kwamba mradi huo wa fedha nyingi umekuwa ukigombewa na wakubwa: Mambo ya Ndani; Mambo ya Nje; Ofisi ya Waziri Mkuu na ulibuniwa na wajiriwa serikalini na kisha kampuni yao ya Gotham International ikapewa kazi ya upembuzi na hatimaye ikaandaa mchanganuo.

    Kati ya waajiriwa hao wa serikali walikuwamo Jack Gotham mwenye uhusiano wa karibu na viongozi wengi serikalini na John Kyaruzi mwajiriwa wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) ambaye ameelezwa kuwa ndiye aliyevuta kampuni moja ya Afrika Kusini, Business Connection (Bcx) kuunda timu ya Gotham International.

    Vitambulisho hivyo vilikuwa vianze kutoka kabla ya mwaka ujao, lakini sasa baada ya utata huo baadhi ya wataalamu wa masuala hayo wanaona kuwa hakuna haja tena ya kuwa navyo kama havihusishi pamoja na mambo mengine, kama takwimu muhimu za wapiga kura.

    “Hicho kitambulisho kinachotafutwa kwanza ni ghali sana mpaka hata Benki ya Dunia ilihoji kama Tanzania inahitaji kitu ghali kama hicho.

    “Lakini pia sasa Tume ya Uchaguzi inapitia Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, ungetarajia kitambulisho hicho kiwe na taarifa zote hizo, lakini sasa Serikali inataka kuwa na utambulisho wake na Tume ya Uchaguzi nayo utambulisho wake, hii haileti maana,” anasema mtaalamu mmoja wa takwimu.

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 26, 2008

    Sasa MIMI MINECHOKA KUFISADIWA NIACHIENI TENDER HIYO NIFANYIE KAZI. NINA EXPERIENCE NZURI TU YA KUFOJI VYETI. THIS TIME NTATENGENEZA ORIGINAL VYETIZ! NIPATIENI KURA ZENYU.
    MULOX.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 26, 2008

    Mi naona serikali yetu imeshindwa kutambua jambo gani lifanyike sasa na jambo gani lifanyike baada ya miaka 10.
    mi kwa kweli sioni haja ya serikali kutengeneza hivyo vitambulisho kwa muda huu. kama ni swala la ulinzi watafute njia nyingine ya kuilinda nchi yetu. maana sioni hicho kitambulisho kinamsaidiaje mtanzania anaeishi karatu vijijini ambae hata dar hajawahi kufika.
    kama hivyo vitambulisho ni muhimu sana kwa baadhi ya watanzania, basi kingeundwa kitengo maalum ambacho kingetenzeneza hivyo vitambulisho kwa wanaovihitaji halafu hao wa2 wavinunue kwa pesa zao. lakini sio kupoteza mamilioni ya shilingi kutengeneza vitambulisho kwa zaidi ya wa2 millioni 30 nchi nzima.
    kama serikali haiwezi kuwekeza hizo pesa aidha katika elimu au afya, basi watutumie sie wanafunzi tunaosoma nje ya nchi tupate kuneemeka, kuliko kupeteza mamilioni ya pesa kwa kitu kisicho na ulazima wowote kwa sasa.

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 26, 2008

    Nchi hii imejaa viongozi wabinafsi mpaka inatia kichefuchefu, haya Changa jingine la macho hilo !!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 26, 2008

    RADA tulipiga kelele, NDEGE YA RAIS tulipiga kelele, lakini viongozi wakaendelea na deal hawasikilizi wanachi waliowachagua, na sasa VITAMBULISHO tunapiga kelele lakini pia hatutasikilizwa. CCM hoyeee !!!!!

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 26, 2008

    TANZANIA a.k.a BONGOLAND a.k.a FISADILAND

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 26, 2008

    Acheni longolongo kama hamjui direction ya vitu nchini TZ. Kwanza ni kweli kuwa technology ya "smart card" ni very expensive and quite advanced, lakini nchi imeamua kwenda na technology hiyo japo WB and IMF na western wamequestion - ukweli ni kwamba it is going to be extremely difficult to maintain because infrastructure-wise hatujafika huko bado(do you realize that with this technology there has to be a smart card reader everywhere where children are born and people die?)Maybe thats where Dickson Maimu comes in bringing his expertise while at RITA Vizazi na Vifo department, incidently a good and abled man, this Maimu. True, a simple bar-code technology ingeweza kufaa but serikali imeamua itakwenda na "smart card technology"

    Swala la zip code linashughulikiwa as we speak pale TCRA kuendana sambamba na mabadiliko katika idara ya posta - I understand the P. O. Box era is on its way out.

    Hii "smart card" technology inawezekana kabisa "kuikuza" au "build upon on". Suala la itumike kama kitambulisho cha kupiga kura au hata driver's license etc is also possible simply because that smart technology has its own chip that can be added lots of information on it.

    May the best company win the tender! Briefcase businesses hapa itakuwa ngumu kidogo na zile bogus companies kama zile za south africa nazo bomu tupu!

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 26, 2008

    hivi hii serikali sijui niifananishe na kitu gani sijui?kuna vitu muhimu vya kufanya ukiachilia mbali huo upuuzi wa serikali,je huduma za jamii mmeshaziboresha?au mnakurupukia vitu ambavyo ni vya kuiga na hamna uwezo navyo.kamilisheni huduma za jamii kwanza halafu mlete huo upuuzi wenu usiokua na msingi.vitu ambavyo havina msingi ndio mnavikomalia sana lakini vitu vya muhimu mnavisahau.; asante mm mdau

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 26, 2008

    ANOTHER LOOPHOLE FOR THE CORRUPT TO EXCEL!!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 27, 2008

    suala la vitambulisho naona ni zuri na limekuja wakati muafaka na sioni kwa nini tulipige vita>ukiangalia tanzania huwezi kujua nani raia nani mgeni hivyo naliunga mkono.pasipoti zinatolewa kwa usumbufu lakini tukiwa na vitambulisho kutarahisisha mambo mengi

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 27, 2008

    WALE WALIOLAANI KABURI LA BANDA WAKOWAPI WATUELEZE MANUFAA YA MATUMIZI YA HIVI VIJISENTI VYA VITAMBULISHO.JE,NYERERE AKIFUFUKA ATAPONGEZA MATUMIZI HAYA?

    ReplyDelete
  21. AnonymousMay 28, 2008

    Its about time, but hopefull it will go well......maana bongo kwa dili tu. dammmmmm

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...