zimebakia takriban siku 90 kabla mkataba wa kocha mbrazil marcio maximo wa kukochi taifa stars umalizike. mkataba huo wa miaka miwili ulibarikiwa na serikali ambayo ndio inamgharamia kila kitu. je, mkataba huu ukiisha aongezewe mwingine?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 81 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 25, 2008

    mi nafikiri aongezewe mkataba kwa sababu amefanya vizuri ktk kipindi cha hii miaka miwili iliyopita. hongera maximo

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 25, 2008

    what was the return on that investment? kwani hapo tanzania hamna ma-kochi ambao wako qualified. i am sure hapo TZ kuna mwenye uwezo wa ku-kochi kuliko hata huyo maximo. it costs the government 10 times more than having mtu wa hapo nyumbani. mazimo arudi kwao.

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 25, 2008

    Huo mkataba wa kujadili uko wapi? Tutawezaje kujadili kitu ambacho hatujui maudhui yake? Kama analipwa gharama za chakula na malazi tu - basi pengine ni lazima tuuongeze. Kama analipwa kama Mourinho tutajiuliza hizo pesa zinatoka wapi.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 25, 2008

    I think inabidi tutafute kocha mwingine. Huyu ameshindwa kazi ya kutupeleka kwenye African Cup. Now inabidi tutafute kocha mwingine mwenye kiwango cha juu ambae ataionoa Taifa Stars for World Cup.

    Mdau from Karachi,
    Shambani

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 25, 2008

    no doubt! Ameanza kuelewa soka la kiafrica na ameondoa u-father kwenye timu ya taifa, mtu yoyote anaweza kucheza timu ya taifa na wale mafather wa kuchelewa kambini au mdomo mdomo kama Kaseja hawataigusha timu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 25, 2008

    Kwa mtazamo wangu Maximo aondoke kwani ameonyesha upendeleo wa hali ya juu kwa baadhi ya wachezaji hata kama kiwango chao si kizuri mfano amemfanya kipa Ivo Mapunda kuwa kipa namba wani wakati Juma Kaseja ni bora zaidi kuliko kipa yeyote nchini

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 25, 2008

    minaona bora wamuache kama pesa serikali inalipa poa maana bora wamlipe kocha hivyo vijisenti maana vitaliwa in other way anyway..kwa upande wa makocha wabongo naona mdebwedo mara ngapi tim ilikua chini yamakocha wa nyumbani ikawa kichwa chamwendawazim bora kidogo sasa pia watu wanakua nahop kidogo tim ikicheza,acheni presha za chelsea mkitereza mnatimua kocha

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 25, 2008

    wanaoponda waendelee kuponda lakini mafanikio yameanza kuonekana mi nafikiri apewe muda zaidi

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 25, 2008

    Wewe Michuzi sometimes unachekesha sana, utajadili kitu usijokijua? Je analipwa kiasi kwa mwezi? to me, nadhani Maximo anastahili kuongezewa mkataba, is one of the best Coach, ndiyo sababu wanapenda majungu wengi wanaopenda majungu na majina wa wachachezaji hawampendi kabisa kocha huyu, Michuzi acheni usimba na uyanga...
    Nic
    Belgium

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 26, 2008

    hivi ameshajua kiswahili?

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 26, 2008

    Nsema Nsiseme!!!!

    Huyu Bwana Maximo amejitahidi sana katika mazingira ya kazi anayofanyia ambayo yamejaa ukiritimba, ukwasi na utovu wa nidhamu katika kandanda. Nadhani apewe miaka mingine miliwli ili kuimarisha nidhamu katika kandanda ili tuweze kujivuta zaidi kuelekea ngazi nzuri.

    NB: Bwana Michuzi- Hebu tuondelee huu mkwara wako wa "word verification" unaotuwekea hapa. Hausaidii lolote hasa kwa vile baadaye wewe binafsi unamoderate na kuchuja post za kuweka hapa. Ni kero kwa watumiaji wa globu yako tu.

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 26, 2008

    Why the government is paying his salary? Jee Vyombo ya soccer vina kazi gani? Jee pesa wanazokusanya kutoka kwenye viingilio na Ads wanapeleka wapi?

    I don't care kama ataongezewa mkataba or not, what i care is why the government have to subsidized soccer?

    Mdau wa US tawi#1

    ReplyDelete
  13. AnonymousMay 26, 2008

    maximo ikiwezekana tumpe mkataba wa wa muda mrefu zaidi WHY?amefanya mambo ambayo kwa muda mrefu ayaja wahi kufanywa na kocha yeyote,ametupandasha chati wa bongo na yeyey kwa sasa ni zimwi litujalo,hao makocha wetu kwa sasa hakuna ata mmoja mwenye uwezo wa kufananisaha na jamaa tuache unazi tumpe na fasi anastaili pongezi kwa rekodi yetu na tumuombe nafasi ya ukocha wa makipa akupe wewe michuzi enzi zako ulikua nyanda mkali tunaomba ushauri wako brooo!!!!!!!!au vipi,

    ReplyDelete
  14. AnonymousMay 26, 2008

    MAXIMO ANASTAHILI KUPEEWA MKATABA MPYA KWANI TIMU IMEKUWA NA MAFANIKIO MAZURI TU KWA KIPINDI KIFUPI.AKIPEWA MDA ZAIDI ATAWEZA KUSAIDIA SANA KWANI ATAKUWA AMEWEZA KUJUA ZAIDI SOKA LETU.HAO WANAOPIGA KELELE KUHUSU MAKOCHA WANYUMBANI NADHANI HATA SOKA HAWAFATILII.mie naona hapewa mkataba mpya na mumuache hafanye kazi yake mwenyewe.

    ReplyDelete
  15. AnonymousMay 26, 2008

    5 more years!!!

    ReplyDelete
  16. AnonymousMay 26, 2008

    Si vibaya kama tukiachana nae,nafikiri kama tukipata kocha toka Ulaya itakua bora zaidi kuliko South Amerika,maana hata historia ya makocha wa Kibrazil si nzuri sana wakifanya kazi nje ya Brazil.
    Maximo kajitahidi kubadilisha sura ya timu ya Taifa,vivyo tukipata kocha mwingine mwenye sifa sawa au zaidi yake itakua vyema,kwani ataleta mbinu mpya za kisasa na kiufundi zaidi kama ilivyo asili ya mpira wa Ulaya,na kuendelea pale Maximo alipoishia
    gEoRGe

    ReplyDelete
  17. AnonymousMay 26, 2008

    I think he should be kicked out when the contract runs out.we have been unable to qualify for African nations and world cup.Also he failed to deliver on challege cup.we can't give him more time to build up the senior team cos most of the players are locally based.It is time for the Govt to appoint a high profile manager with 6-7 years trackable record.Cheap managers cost alot.we shouldn't go chalsea way.they lost it to Manu just cos their cheap manager was inshort of tactics.Former England boss was sacked cos he failed to meet FA demands as Qualifying for Euro is a minimum requirement for England manager job.The junior team manager should have a long cotract to sharpen potential talents that would boost our Senior team.Iam sick of this guy,let him go.He has not achieved nothing but women , girls and tax money.

    ReplyDelete
  18. AnonymousMay 26, 2008

    Watanzania hatuna shukrani jamani.. Eti hakutupeleka African Cup..unanichekesha unajua? Nani angeweza.. Kumbuka kulikuwa na senegal..tena bado kiduchu tuwapite. Maximo amebadilisha mfumo wa soka Tanzania na amerudisha chachu ya soka Tanzania! Kumbukeni TZ tulikuwa kichwa cha mwendazimu.. hata Kenya na Uganda walikuwa wanatukandamiza kila siku!! Pia sasa kuna nidhamu kali ndani ya timu.. Kama ni nyumba, basi Tanzania ilikuwa ni ya udongo tena iliyochoka..kwa hiyo hawezi akaibadilisha ikawa Kasri baada ya siku moja... Waingereza wanasema "ROME WASN'T BUILT IN ONE DAY!"(Roma haikujengwa kwa siku moja)..Mie nasema tumpe muda Maximo maana ameonyesha DALILI nzuri kabisa...pia tukimfukuza ina maana tunaanza tena na ALIFU...hii itakua soo, maana hata JK atachoka!!

    MAXIMO OYEE !!!!!!!

    ReplyDelete
  19. AnonymousMay 26, 2008

    Maximo hafai ni mbabaishaji mkubwa asipewe tena. huwezi kumpongeza kwani ni looser.

    Timu nyingi zilishindwa kuchukua kombe la Africa zimewafukuza makocha wao na Ghana wamesema hawatampa mkataba mpya kocha wao Claude Reloy.

    Maximo alisema hawezi kuchukua wachezaji wenye miaka zaidi ya 24 timu ya Taifa.

    lakini wachezaji kama DROGBA ana 30,Lampard 29,Cafu wa Brazil alikuwa na 35 final ya world cup ya 2006 amecheza,

    Robert Carlos 33,Michael Ballack ana 31,Henry Thiery ana 30,Vierra 32,Makelele 34,

    Zambrota 32,Canavaloh 32,Gatuso ana 31,PIRLO 31,Kanu 31, Kanoute 30,Okocha alikuwa timu ya Taifa akiwa na miaka zaidi ya 30.

    Beckham 32,Roger Miller alikuwa na miaka 39 akiwa na timu ya Cameroon.Njitap 29.
    Hossam Hassan wa Misri kacheza hadi 40.

    Madaraka suleiman. David James 37.Lehmans 38.Peter Shilton 40.

    wako wengi lakini Maximo akasema haiwezekani kwa wenye umri zaidi ya 24 kuwa timu ya taifa hapo utajua kuwa ni bomu.

    akamfungia Kaseja bila sababu na adhabu ya daima jana Kaseja kachukua milioni 2 kama kipa bora Taifa Cup.

    Akamchukua kipa wa akiba wa simba Bathez na kuwa kipa wa kwanza timu ya Taifa kwenye kombe la challenge.

    sijawahi kuona mchezaji aliye benchi kwenye timu yake. kuwa namba wani kwenye timu ya Taifa.

    juzi kasema kuwa Boban asahau timu ya Taifa, kwani kama kafanya kosa si kuna muda wa adhabu ndio iwe maisha?

    anasema kuwa nidhamu ni ndani na nje ya Timu ya Taifa, sasa kwanini asimfungie IVO Mapunda ambaye imethibitika kuwa aliuza mechi kwenye timu yake na akatumikia kifungo cha miezi sita kwa kosa hilo.

    kama IVO kauza mechi ya Yanga hashindwi kuiza Taifa stars.

    anasema Haruna Moshi alikuwa akinywa pombe mtaani. huo ni umbea kama kanywa mtaani yeye inamuuma nini?
    angekunywa kambini kweli.na adhabu lazima iwe na kipimo.

    mbona kina Gazza na George Best waliwahi kuingia uwanjani wakiwa na Pombe hawakufungiwa maisha.

    Avram Grant amepoteza mechi mbili tu za Barclays ni mechi ya Manchester 2-0 Old Traford na Arsenal 1-0 kwenye first leg.

    ameipeleka timu fainal ya UEFA kwa mara ya kwanza.ameifikisha Final Carling Cup wakafungwa na Tottenham.akaifikisha nusu Fainal kwenywe FA.

    lakini leo ametimuliwa na wenye timu yao.Fotball is about wining games and trophy at the end of the day anakumbukwa bingwa si mshindi wa pili.

    African Cup tumekuwa watatu baada ya Senegal, Msumbiji, Tanzania.

    Kombo la Challengi limechezwa kwetu hata nusu Fainal hatukufika.

    Kumbukeni Timu ya Taifa ya 1994 ya Mziray iliyochukuwa kombe la challengi.Na timu yetu ya 1980 ilifika fainal Lagos chini ya mheshimiwa naibu waziri Bendera kama kocha.

    Maximo kwa nguvu anayopata toka serikalini,TBL, NMB, ana kila kitu lakini hakuna cha maana.

    Timu ya kakakuona ilifika mbali ikiwa haina resources.

    mshahara anaoupata mkubwa sana kuliko anachotupatia.tukitizama makocha waliofanya vizuri huko nyuma Maximo hajawafikia.

    au kwa wale wanao mSupport Maximo labda wameanza kufuatilia au kuupenda mpira baada ya yeye kuja nchini.
    NI mimi Mdau wa soka.

    Jongo toka Kisiju.

    ReplyDelete
  20. AnonymousMay 26, 2008

    Hi Bro michuzi,
    Huyu jamaa anaonekana ni kocha mzuri hivyo aongezewe mkapa mwingine.Ila kuna mambo inabidi ajirekebishe,ni mtu wakupenda u-mimi,hasikilizi ushauri wa wenzake,anafukuza wachezaji ovyo bila sababu za msingi tena ambao hakika wangeweza kuisaidi timu yetu ya taifa,aache chuki binafsi na wachezaji,mfano ni juzi juzi tu alimfukuza mchezaji tegemeo wa timu yetu ya taifa,Haruna Moshi kwa sababu ya kijinga tu hata baada ya kuambiwa na kushauriwa na maofisa wenzake alikaidi na kumfukuza ,labda angecheza leo tungekuwa kifua mbele zaidi,Mfano mwingine ni pale anapokataa kata kata kumuita golikipa temegezi wa Tanzania,Juma Kaseja bila sababu yoyote ya msingi licha ya ushauri anaoupata kila siku kutoka kwa wadau wa soka,eti kwa vile alishangilia pale Senegal ilipoichapa Taifa stars bao nne bila.who cares...!! kwanini yeye aingilie hisia binafisi za mtu,kwani akishangalia Senegal ndiyo kiwango chake cha mpira kinashuka.Haya ni baadhi ya matatizo ya huyu kocha wetu hakika inabidi ajilekebishe kabisaaa....!!!
    Mdau mkuu wa soka la Bongo,
    USA.

    ReplyDelete
  21. Tunatakiwa kumjadili Maximo kama Kocha na matokeo yake kama Kocha sio mkataba haupo hapa.
    Kabla ya mchezo wa jana Taifa Stars ilikuwa imecheza michezo nane ya kimataifa ya kirafiki chini ya Kocha Mkuu Mbrazili Marcio Maximo tangu aanze kibarua hicho karibu miezi 19 iliyopita.

    Katika michezo hiyo Taifa Stars imeshinda mitatu dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Uganda na Zambia na kutoka sare mara nne dhidi ya Kenya, Angola, Zambia na Uganda na kufungwa na Yemen.
    Hivo matokeo si mabaya sana.akipewa muda ataweza.
    Spoti na Starehe

    ReplyDelete
  22. AnonymousMay 26, 2008

    Huyu aondoke, kiwango cha soka kimepanda kwa ajili ya ushirikiano unaotolewa ktk timu ya taifa hasa kiasi kikubwa cha fedha kinachotolewa na wafadhili, kama hali hii ingemkuta kocha mwenye uwezo mzuri Tanzania ingekuwa juu sana. Binafsi sioni mchango wa Maximo hasa ukilinganishwa na fedha alizotumia.

    ReplyDelete
  23. AnonymousMay 26, 2008

    Mithupu, Maximo alipewa kazi ya ukocha wa taifa kwa lengo moja tu "kukuza soka na kufanikisha ushiriki wa tz CAN". Tofauti na matarajio ya wengi ameweza kuturudisha enzi zile za kutokuwa na first eleven na ameonyesha kiasi gani hawezi kurekebisha tabia za wachezaji na kuwasema kwenye vyombo vya habari na wengine kuwaapia kuwa labda on his dead body ndio wataingia stars...this is crazy though JK naye ndio hobelehobela. Kuna umuhim wa kumtimua hana jipya na hatakuwa na jipya kwa sababu hata kijiko cha samba hakuna ni bora tuwape kina Kondic na Profesa. HANA JIPYA ZAIDI YA KUWAONA MAPUNDA NA FUSO NDIO WENYE STARS,ANGALIA NGASA ALIACHWA MPAKA TUKAPIGA KELELE NDIO AKACHAGULIWA. SOKA NI VIPAJI NA KUVIENDELEZA NA KUREKEBISHA TABIA ZA WACHEZAJI NA SIO KUKOMOANA. MAXIMO IS IDIOT

    ReplyDelete
  24. AnonymousMay 26, 2008

    nafikiri umefika wakati wakubadili kocha sasa maana amekaa miak 2 hakuna jpya lltealicho wez yeye nikutoa ufadha ktk timu tuulakini mpira au maendeleo hakuna wala timu haijabadilik kabisa naona hana jipya atafutwe mtu ambaye atakuwa na mawazo mapya..pili misupu vp na kocha wa timu ya vijana ??naona nae tumjadilia maana analipwa mshaara wa bure karibu miaka 2 sasa na hakuna timu ya vijana tumejotoa ktk mashindano sasa yy anakazi gadi hapa bongo??au ndio ufisadi mwingine huo?? maana kuna ufisidi wa namna nyingi

    dalali

    ReplyDelete
  25. AnonymousMay 26, 2008

    Nafikiri Maximo aongezewe muda kwani
    1. Makocha wetu wazuri ila huwa hawana maamuzi imara. mfano wakikosolewa na mashabiki au viongozi (hawajiamini kiasi cha kutosha)
    2. Wengi wanakuwa biased hasa kuchagua wachezaji
    3. Makocha wa hapa kwetu tunategemea walipwe na TFF. sasa hawa TFF mie huwa nashindwa kuwaelewa vituko vyao. vitu vya msingi vya kocha/wachezaji hutolewa kwa mbinde, kitu kitakachokatisha tamaa wachezaji na makocha wetu.
    Maximo ni mtu muhimu sana sasa hivi kwani ameshawajua viongozi na wachezaji pia apewe muda zaidi

    ReplyDelete
  26. AnonymousMay 26, 2008

    SIMPLY HE MUST GO. UWEZO WAKE WA UFUNDISHAJI NI WA KAWAIDA NA HASA KAMA ANAWEZA KUTOKA SARE NA MALAWI BASI MAXIMO MUST GO AND BE REPLACED BY MINIMO.

    ReplyDelete
  27. AnonymousMay 26, 2008

    1-Mkataba uwekwe wazi,2-Kwa upande wa performance yake naona aendelee u-kocha,3-Atafutwe mwingine wa aina yake kufundisha Vijana.

    Wadau wakumbuke kuwa jamaa anafanya kazi za zaidi ya kocha wa kawaida...ana-deal na viongozi wababe perpendicularly na pia ni mhamasishaji.Kumbuka na-train some people who can not be trained(Yaani baada ya kucheza soka la butuabutua muda mrefu wanakuwa wamelizoea).Kocha mmoja wa Kigoma juzijuzi alikiri kuwa wachezaji wa Mchangani licha ya vipaji walivyonavyo wana ugonjwa wa kucheza dk 20 tu za mwanzo accordning to mafunzo then zilizobaki wanapiga kivyao vyao.The same problem anaipata Mshkaji STAZ

    ReplyDelete
  28. AnonymousMay 26, 2008

    HANA CHA MAANA ALICHOFANYA,ARUDI KWAO,KILA SIKU TUNAFUNGWA

    ReplyDelete
  29. AnonymousMay 26, 2008

    Tatizo letu sio uwezo wa kocha Maximo, au yeyote mzuri toka kokote bali setup nzima ya soka la Bongo. Eneo la Ufundi TFF lina walakini ndio maana hata timu za Vijana chini ya Tinoco hazijaonyesha mwangaza wowote hadi sasa. Tusitegemee mafanikio yoyote kama hatutaki kubadilika. Akina Kipingu (Makongo Sec) wanajitahidi kusaka na kuinua vipaji, shughuli ambayo TFF kwa niaba yetu ingeiratibu vyema, kidogo tungekuwa na mwelekeo. Mwenye macho haambiwi tazama.

    ReplyDelete
  30. AnonymousMay 26, 2008

    Mie nafikiri serikari ingewekeza kwa chipukizi zaidi kuliko hao wanao cheza simba na yanga na maximo sijaona ukari wake anazidiwa hata na siang'a ambaye alifikasha simba kwenye kwabu bingwa africa

    ReplyDelete
  31. AnonymousMay 26, 2008

    Mustakbali wa Maximo ni issue...aliletwa ainue kiwango cha soka, ok tulifanya vema kwenye kinyang'anyiro cha african cup lkn Maximo amebadili kikosi zaidi ya mara 10, huyu jamaa ataondoka na atatuacha mikono mitupu na hatutokuwa na chakujivunia...kwa ufupi hamna kikosi ambacho amekifua baada ya kumaliza mkataba tutabaki nacho kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya cameoon...hii haina ubishi.
    Mimi napendekeza yule kocha wa ghana roy angeweza kutusaidia zaidi, anajua soak la kibongo lipoje na atakuwa si ghali sana.....Maximo anatfuanyia madudu ili baadae tumuongezee mkataba, sasa yatosha....tunataka kicha atengeze timu ya miaka 4 mpaka 5 siyo kocha wa kutengeneza kikosi cha kujiandaa na mechi flani, harafu mechi ikiisha anabadili tena kikosi...nasema yatosha.
    Mdau...Kumas

    ReplyDelete
  32. AnonymousMay 26, 2008

    Maximo aongezewe mkatama kama hauna harufu za kifisadi.sasa anaeleweka na vijana wanafanya kazi.

    ReplyDelete
  33. AnonymousMay 26, 2008

    mimi nadhani huyu bwana kabadilsha jina sasa sio kichwa cha mwenda wazimu tena juzi tumewatoa waganda ,wakenya pia endelee tu kwani walimu wakwetu wengi wababaishiji tu nahilo michuzi wewe mwenyewe unalijua

    ReplyDelete
  34. AnonymousMay 26, 2008

    Tuache kuongopeana. Kwa kweli Maximo kazi hakuiweza. Hebu tuhesabu mechi ambazo Stars walishinda wakiwa chini yake halifu tulinganishe na zile walizopoteza. aibu tupu. Tunahitaji kocha Mjerumani kama akina Rudi Gutendorf waliyoifundisha yanga na Stars za Miaka ya 1980s na kuleta mafanikio katika Mashariki na Kati.

    ReplyDelete
  35. AnonymousMay 26, 2008

    Let me be very frank on this.Ukimalizika mkataba wake wa sasa,Maximo asiongezewe mkataba mwingine.Labda kama hatuko serious.Maximo hawezi na hana uwezo wa kuifikisha Taifa Stars Kombe la Dunia!Just Forget about it.Kwa wale wenye chembe ya Ukocha wa Kandanda,ufundishaji na umakini wa Kocha katika kupanga Timu ya Ushindi utajidhihirisha tu katika uchezaji wa Timu yenyewe.Makocha wa Soka au wale wote waliodhamiria kujitumbukiza katika Ukocha wa Kabumbu,wakae wakijua,Thamani ya Kocha ni 'Pale tu Timu yake Itakapo shinda,na si vinginevyo'.Hata kama huko nyuma aliiwezesha timu yake kutwaa ubingwa mara ngapi,pale tu timu yake itakapo anza kupoteza ushindi basi huchukuliwa kwamba uwezo wa Kocha yule umeanza kupungua.Kwa hiyo lazima abadilishwe.Katika ushindani wa Soka,Timu nyingine hazikusuburi wewe ujipange upya.Its a Cut-Throat Competition in Soccer Tournaments!Hakuna lelemama.Kama Kikwete bado atamuhitaji Maximo basi ampangie kazi nyingine katika Wizara ya Michezo LAKINI SIYO TENA UKOCHA WA TAIFA STARS.Kuna maeneo mengi sana ambayo bado yatahitaji wakufunzi katika Soka hapa nchini.Na Tifa Cup wasiruhusiwe kushiriki wachezaji ambao tayari wanayo nafasi ya kujulikana na kuonyesha uwezo na vipaji vyao katika Ligi zingine na Mashindano mengine ya Kitaifa,ili kutoa uwanja mpana zaidi wa vijana wetu wasiojulikana kuweza kushiriki na kuonyesha uwezo wao wa kulisakata kabumbu.Vinginevyo Tifa Cup tutakuwa tunapoteza fedha na MUDA WETU BURE.we ca not afford such a wastefull extravaganza!Lets be more serious on this.Kwa kufanya hivyo,wilaya zitabanwa zaidi kutafuta vipaji vipya kupitia mashuleni na vyuoni pamoja na mchangani!

    ReplyDelete
  36. AnonymousMay 26, 2008

    Jamani Kaseja sio kama si mchezaji mzuri hata max anamkubali ila tatizo aliloliona Max kwa kaseja ni kuwa na NGUVU na anaweza kuyumbisha wachezaji wenzake,eg, MAx akitoa maelekezo wakati wa mapumziko Kaseja anauwezo wa kuwaambia wenzake hiyo sio safi tufanye hivi na wakakubaliana nae kwahiyo MAx anaona huyo si mchezaji mzuri kama akiwa na nguvu hivyo anaweza hata kuhujumu team. HAYO NI MANENO YA MAX mwenyewe.

    mambo mengine ya makataba ni kwamba kama RAIS ndio mlipaji basi ampunguzie nguvu MAX ili tuweze kumsaidia na asiwe mmbishi hata suala la kubadilisha mchezaji anataka aamue yeye wakati hawezi kuperfom sio hiyo..

    ReplyDelete
  37. AnonymousMay 26, 2008

    Kabla ya kumjadilii Maximo tujiulize hadi sasa tumejipanga vipi katika kuwekeza katika michezo,hususani mpira wa miguu.
    Kwa upande wa serikali imewekeza kiasi gani kuhakikisha kuna hatua za makusudi za kuvumbua na kukuza vipaji vya soka nchini.
    Kuna sera gani ambayo ni hai inayotekeleza kwa vitendo haya ninayohoji kama ujenzi wa shule za michezo n.k.
    TFF kama chama cha soka naweza kusema kinamuelekeo mzuri kiasi,lakini kwa mtazamo wangu kina kasoro kubwa sana kiutendaji,mfano suala la Simba kupokonywa pointi dhidi ya Coastal Union,na Temeke kuondolewa mashindanoni Taifa cup ,ni wazi inaonesha utendaji wake sio makini,hasa ktk ufatiliaji wa rekodi na yaonesha pia mfumo mzima wa uwekaji kumbukumbu sio wa kuridhisha.
    Hii ni dalili ya uongozi wa kibabaishaji usioweza kutekeleza malengo.
    Kama itakumbukwa hivi karibuni TFF ilipokea taarifa kutoka CAF/FIFA inayowaagiza kutomtumia Shadrack Nsajigwa kwenye michuano ya kuwania kucheza CAN/WORlDCUP kutokana na mchezaji kuwa na adhabu,lakini yenyewe ilishindwa kuziarifu Simba na Temeke kutotumia wachezaji wasio ruhusiwa,inaoonyesha kwamba haizifanyii kazi rekodi ikisubiri kukurupuka tu.
    Kasoro hizi inaonyesha ni kwa jinsi gani ninavyopata mashaka na viongozi wa TFF kama kweli wanajua wapo madarakani kwa malengo gani na utendaji wao unafanyika chini ya muongozo gani,kwa maana ya je ni kweli kuna shabaha zozote walizojiwekea?mfano hadi ikifika mwaka 2010,TFF iwe na uwezo wa kuwalipa makocha wa timu za Taifa yenyewe kupitia vyanzo vya fedha vya uhakika,au kuzifanya timu zinazoshiriki ligi kuu kujitegemea zenyewe bila kutumia wafadhili,au kuhakikisha hadi 2012 tunakua na wachezaji wa kitanzania kwenye ligi kubwa Ulaya na timu zetu zinapata ushirika na timu kubwa za Ulaya na America n.k.
    Kuhusu Maximo naweza kusema kwamba kajitahidi kuamsha ari ya WAtanzania kupenda timu yetu ya Taifa,na kwa mtazamo wangu hapa alipofikia hatoweza husogea hatua moja mbele katika mazingira ya soka yetu ilivyo,kama ni bidhaa basi ishafikia "maturity stage" kinachofata sasa ni kuanza kuporomoka,hivyo ugumu wa kazi kwake yeye ndio kwaanza umeanza.Ningekua mshauri wake ningemshauri asisaini mkataba mwingine ili tutafute kocha mwingine mweny sifa zaidi yake,aje na jingine jipya la tofauti kabla ya hamasa iliyokuwapo haijaporomoka tukapoteza hata wadhamini tulio nao sasa.
    Ikumbukwe kwamba mpira ni biashara bila wadhamini(sio wafadhili) hamna soka
    gEoRGe

    ReplyDelete
  38. AnonymousMay 26, 2008

    Massimo aondoke. Timu inajitahidi sio sababu ya Massimo ni sababu ya pesa. Huko nyuma kulikuwa hamna wafadhili ndio maana timu ilikuwa inashindwa. Tungekuwa na kocha mzuri na mazingira mazuri kama haya ya pesa hakika tungefanya vizuri. Mnakumbuka sababu ya simba kufika fainali ya CAF ni ahadi ya Kia kwa kila mchezaji. Pia mnaweza kukumbuka kufanya vizuri kwa timu ya vijana waliokuwa chini ya miak 17 ni michango mbalimbali iliyohamasishwa na ITV. Masimo aondoke haraka na onyo serikali wasipomtoa TUTAMTOA KWA NGUVU. Nimemaliza

    ReplyDelete
  39. AnonymousMay 26, 2008

    Hivi Jamani nyie watu Ahaaa. Kuna watu wengine bana. Mimi sijui namna gani. Maximo amefanya makubwa sana eti jamani. Tusiwe watu wasio na shukrani kama tajiri wa Chelsea kumfukuza Grant sijui anategemea nini. Huyu mtu anatakiwa aendelee kabisa halafu atafutiwe chupkizi mmoja wa kumtrain ili akiondoka awe ameacha walau hiyo return on Investment mnayosema wengine sijui hata kama mnaifahamu maana yake.

    ReplyDelete
  40. AnonymousMay 26, 2008

    Acheni upumbavu wa kufananisha vitu vya ajabu.huwezi kulinganisha wachezaji wenyewe zaidi ya miaka 30 wa ligi za kimataifa na wachezaji wa nchi yetu kama kweli unajua soka.wachezaji wote uliowataja hao hapo juu wenye miaka zaidi 30 ni proffesional players ambao wanafanya mazoezi ya huakika na wanapata mlo wa huakika na matibabu ya huakika.huwezi kulinganisha na wachezaji wa nyumbani ambao hawapati mlo wa huakika na wenye virubutisho vinavyotakiwa kwa siku,huduma ya afya ni mbovu na wako katika hali ngumu ya maisha inayo wa affect kisaikolojia pia.sasa ukianza kusema kwanini drogba anacheza mpaka leo ni kwamba hujui soka la nyumbani kwenu kazi kuangalia kwenye tv chelsea vs man united unataka kuja kulinganisha na yanga na simba.unazungumzia history which history we have in soccer to make our self so proud and remembered in the world of soccer? Hata aletwe nani duniani unayemjua wewe tanzania haitafanikiwa soka kwa miaka miwili tu bali inaitaji mpango kabambe sana na wa mda mrefu hili kutoa wachezaji wazuri na kufanikiwa baadae.system ya sasa inaenda vizuri tu sema itarudishwa nyuma na watu kama nyinyi mnaotaka mabadiriko ya kila siku.huwezi kulinganisha na chelsea kufukuza kocha kwani chelsea wanatumia pesa kununua the best players in the world hili kushinda vikombe,matokeo yake wanakuja kufungwa na timu ambazo hazijatumia hata robo ya hela waliotumia wao.hela haiwezi kununua ushindi hata siku moja ni usakaji wa vipaji kwa makini tu.angalia real madrid wanavyo angaika na hela zao kila siku wanataka kununua mastaa.watalipa hio euro millioni 80 kwa ajili ya ronaldo,kati ya hio mil 80 ferguson anachukua mil 10 anaenda kununua mchezaji baada ya miaka miwili anawauzia tena madrid hao hao kwa million 80 nyingine kwani ni wa vivu wa kusuka vipaji vyao wenyewe au kutafuta wachezaji wanataka mafanikio ya haraka haraka.UBOVU WA SOKA LA TANZANIA UNAANZIA HUKU HUKU VILABUNI KWENYE MAKOCHA WETU WA KITANZANIA TUNAOWASIFIA.KAMA VILABU WATAKUWA WANAENDELEA NA MBINU HIZO HIZO ZA ZAMANI BASI SOKA HALITAFIKA POPOTE.MAXIMO HATAKIWI KUMFUNDISHa MCHEZAJI WA SIMBA KUTOA PASI.KAZI YAKE INATAKIWA KUREKEBISHA MAKOSA MADOGO MADOGO TU KUWAPA MOYO WA KUCHEZA KWA KUJIAMINI NA FURAHA KWA NCHI YAO .MAAKOCHA WA TIMU YA TAIFA HUWA NA MDA MCHACHE SANA WA KUANDAA TIMU KWAHIO UNAVYOMPA JUKUMU LOTE MAXIMO PEKE YAKE NA LAWAMA NI KOSA.MABADILIKO YA SOKA YAANZIE KWENYE CLUB ZETU NA TUWEKEZE ZAIDI KWA VIJANA PIA.NA HOJA YA KWAMBA MAXIMO HANA FIRST 11 Ni UJINGA.TIMU YA TAIFA SIO CLUB,TIMU YA TAIFA INAUNDWA NA THE BEST PERFOMING PLAYERS WA WAKATI ULIOPO SIO WAKATI ULIOPITA NDIO MAANA VIKOSI HUWA VINABADIRIKA MARA KWA MARA DUNIANI KOTE SIO MAXIMO PEKE YAKE.KAMA MCHEZAJI HATOWEZA KUMAINTAIN PERFOMANCE YAKE BASI LAZIMA MCHEZAJI MWINGINE ATAPEWA NAFASI AMBAE ANA UWEZO ZAIDI YAKE KWA WAKATI HUO.tuweni wavumilivu wa mafanikio ndugu zangu,HAKUNA MTOTO ALIYEZALIWA AKAANZA KUTTEMBEA ON DAY ONE.
    Mdau mzawa

    ReplyDelete
  41. AnonymousMay 26, 2008

    Sio mkataba tu na Uraia ... ila asimbanie Kaseja

    ReplyDelete
  42. AnonymousMay 26, 2008

    Maximo aongezewe mkataba mwingine wa miaka miwili, baada ya hapo tunaweza kuangalia kiwango cha soka katika Nchi yetu kimefikia wapi. Tusiwe na jaziba ya kusema aondoke. Tukumbuke Rais Wetu Jakaya Kikwete alivyotuasa kwamba tuwe na subira. Mpira wetu ulikuwa katika kiwango cha kichi, tusitegemee katika muda mfupi huu kuona mabadiliko makubwa ya kucheza na kutwaa kombe la Dunia.

    Napenda kuchukua nafasi hii kuishukuru Serkali kwa kukubali kuweka bajet ya michezo na hasa naomba viongozi wa Serkali waone kwamba michezo ni sehemu ya Ajira. Hilo litawapa moyo wachezaji na wale wanaochipukia michezo. Suala jingine nashauri vipaji vya michezo vitafutwe tokea shule za misingi. Pia kuwe na shule kuanzia Primary hadi chuo kushughulikia vipaji vya michezo. Vijana watakaosoma shule hiyo wawe na vipaji vya michezo. Muda wao mwingi utumike kwenye mazoezi. Wakiwa darasani sehemu kubwa wajifunze michezo. Shule hiyo iwe ya Serkali. Mtaala wake utayarishwe mahsusi kwa kuendeleza vipaji vya michezo. Tukifanya hivyo tutapata chipukizi wazuri wa michezo mingi.

    ReplyDelete
  43. AnonymousMay 26, 2008

    WATU WENGINE NI WAJINGA SANA WAMEJAA USIMBA NA UYANGA TU HATA HAWAFIKIRII,MNATAKA KUMLAUMU MAXIMO BUREE WAKATI TATIZO LIPO KWENYE VILABU VYETU,MAXIMO NI KOCHA MZURII NA AENDELEE KUFUNDISHA TUACHANE NA MAWAZO YA WASIOJUA NINI MAANA YA TIMU YA TAIFA,WIVU TU UMEWAJAA.

    ReplyDelete
  44. AnonymousMay 26, 2008

    KABLA YA KUANZA KUMSAKAMA MAXIMO, TUANGALIE MAFANIKIO YA VILABU VYETU TANZANIA. KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MIWILI ILIYOPITA, JE? KUNA TIMU YOYOTE TOKA TANZANIA ILIYOPATA MAFANIKIO KATIKA AFRIKA MASHARIKI NA KATI AU AFRIKA? KUMBUKA, STARS WANACHUKUWA WACHEZAJI TOKA KWENYE CLUBS, KOSA LINAANZIA HUKO HUKO KWENYE KINA SIMBA YANGA, ETC ETC...MATATIZO YAPO HUKO, MAXIMO ANACHUKUA FINAL PRODUCT TU, YAANI HAO TUNAOWAONA WAKICHEZEA STARS "NDIO THE BEST 25" TAIFA STARS CAN PROVIDE! HATA AJE KOCHA TOKA WAPI BURE TU!

    ReplyDelete
  45. AnonymousMay 26, 2008

    Wewe Anonym wa May 26, 2008, 12:39 pm ndiye KUBWAJINGA WA KUTUPA!Aliyekwambia kwamba wachezaji wa Taifa Stars lazima watoke Simba na Yanga ni nani?Kweli Maximo hawezi kupandikiza Individual Skills kwa wachezaji mmoja mmoja.Lakini Winning Tactics lazima zitoke kwake kama Kocha.All in all Kiwango cha Maximo ku Coach timu ya Taifa bado kidogo jamani,tusijidanganye madhali yeye katoka Brazil.No,Hapana.Tunahitaji Kocha mwingine.In fact tunahitaji TEAM MANAGER mwingine ambaye ndiye Kocha Mkuu.Akisaidiwa na Makocha wa Vitengo Mbalimbali vya Soka.Isiwe macho yote kwa mtu mmoja tu,Kocha Mkuu.Aliye fuatilia uchezaji wa Taifa Stars ilipo pambana na Malawi atajua udhaifu wa Maximo.No excuse.Maximo amepata muda wa kutosha kuifundisha Timu na kushiriki Mechi kadhaa za Kimataifa.Ikiwa Grant wa Chelsea pamoja na jitihada yote aliyoifanya kuifikisha Chelsea fainali za UEFA,ilipopoteza kwa bahati mbaya au uchaguaji mbovu wa wapigaji penati BADO AKATIMULIWA, itakuwa na utendaji wa huyu Maximo?Tunachosema Maximo apewe kazi nyingine iwapo mmempenda sana!Lakini siyo Taifa Stars.Eti Mdau Mzawa,mzawa wa kuhi?Fala wewe!

    ReplyDelete
  46. AnonymousMay 26, 2008

    Michuzi!
    Kwa heshima na taadhima naomba uwaulize wadau...Zanzibar ni siku ya 6 sasa hakuna umeme na haturajii umeme kurudi mpaka majuma 3-4 yajayo....ni haki kwa kisiwa hiki kukaa muda huo bila umeme? no radio no tv no water...its damn bullshit, yani viongozi wetu hawana njia mbadala ya kukabili dharura hii? its shame, kuna watu wanatakiwa wawajibike

    ReplyDelete
  47. AnonymousMay 26, 2008

    Nakubaliana na Pope kwa vigezo alivyovitoa na si kuja na kusema hafai asiongezewe au anafaa aongezewe mkataba.Kwa mazingira haya ni sahihi kama Maximo akipewa muda zaidi.

    Kama ni kweli Kaseja alionekana akiishangilia Senegal baada ya Tanzania kufungwa hastahiki kuwa katika timu ya Taifa kwani si mzalendo ukiwa na mchezaji wa namna hii anaweza ata kuuza mechi kwa kitu kidogo.Tuwe wazalendo ata kama hatujachaguliwa kuchezea Taifa star.

    Mimi naamini kuwa let the managers manage.Maximo hastahili kuingiliwa apewe uhuru wa kufanya kazi ili tuweze kuona ufanisi na tukiwa tunamuingilia sasa yeye ndiye atakuwa ameleta ufanisi au sisi.

    Watanzania wenzangu tubadilike.

    ReplyDelete
  48. AnonymousMay 26, 2008

    Kwakweli mie ningependa uyo cocha aendelee. amejitahidi jamani BG UP MAXIMO

    ReplyDelete
  49. AnonymousMay 26, 2008

    Tafadhali jamani tutumie kiswahili maana viingereza vingi vinavyoandikwa humu vinaumiza kichwa.

    ReplyDelete
  50. AnonymousMay 26, 2008

    wadau wa soka la bongo wanapaswa kuzinyoshea vidole timu za simba na yanga kwanza kabla ya kumshambulia Maximo, mpaka leo hii simba hawana uwanja wa kufanyia mazoezi!! na ni timu yenye miaka zaidi ya sabini..mpaka leo hii timu zetu zinaongozwa na watoto wa mjini amba wanaziendesha kiubabaishaji..mpaka leo hii hatuna hata mchezaji mmoja anayechezea timu za maana za Ulaya..na ni jukumu la vilabu vyetu kutngeneza na kuuza wachezaji nje ya bara hili lakini vilabu vyetu ndio hivyo ambavyo havina hata viwanja vya kufanyia mazoezi..Maximo anaweza asiongezewe mkataba, lakini je kuondoka kwa Maximo kutakuwa na faida gani iwapo timu zetu haziwezi kutuzalishia hata supastaa mmoja!!!...wabongo tunapenda sana kulalamika lakini tunapaswa kwa nguvu zetu zote tuvinyoshee vidole vilabu vyetu..vilabu ambavyo havina tofauti yoyote na meza za wauza kahawa!!..vilabu vyetu vimejaa mizaha na kejeli zisizo na maana wakati vilabu vya wenzetu havina kabisa muda wa kuendekeza upuuzi. Watu wanamzungumzia Kaseja kana kwamba ndio mkombozi wetu..wanasahau kwamba Enyimba walimtungua mabao saba katika mechi mbili tu za mwaka huu!!..sijazungumzia mechi walizomtungua katika miaka iliyopita.
    Tatizo letu liko kwenye uendeshaji mzima wa soka letu..hata akija Jose Mourinho au Avram Grant bado atasakamwa kama anavyosakamwa Marcio Maximo.

    ReplyDelete
  51. AnonymousMay 26, 2008

    Hi,
    Anony 10:51 Umeongea point sana kuhusu suala la Maximo kubagua,chuki kwa wachezaji lakini bado haujani-comvince.Hiyo sio sababu ya kutomuita Kasega kwenye kikosi cha timu ya taifa,nafikiri kama hilo ndilo tatizo la Kaseja yeye kama kocha anaweza kulekebisha na akamsikiliza tu.Je na hao wengine aliowabagua,akawafukuza kwenye timu bila sababu za msingi,kama Haruna Moshi....???!!!!
    Mdau,
    USA.

    ReplyDelete
  52. AnonymousMay 26, 2008

    Mdau, Maximo anastahili kubakia katika kilinge yaani aendelee kuinoa stars ila kama atashindwa kuifikisha mahali panapotakiwa afukuzwe.n

    ReplyDelete
  53. AnonymousMay 26, 2008

    kuna mdau mmoja amenichekesha sana..anazungumzia mafanikio ya Serengeti boys kutokana na hamasa iliyoonyeshwa na ITV!!..Anasahau kuwa zaidi ya nusu ya wale Serengeti boys walikuwa ni vijeba na ndio maana CAF wakatufungia kushiriki mashindano yoyote yale ya vijana ya bara la Africa kwa miaka miwili..wabongo tunapenda sana njia za mkato ndio maana kila siku tunamtukana Maximo kwa sababu yeye anathamini mchango wa wachezaji vijana..tunawanyanyapaa sana wachezaji vijana bila sababu za msingi lakini wakianza kung`ara tu, tunaanza eti kuwashabikia!!mfano hai ni jinsi tulivyomuita Jerry Tegete mtalii wakati ule alipokwenda na timu ya taifa kule Brazil na Ulaya..lakini kwa sasa kila mtu anamthamini Tegete..tunaukosefu mkubwa wa uvumilivu na tumejaa kila aina ya ujuaji..wakati wa kubadilika ndio huu na tusingoje kesho

    ReplyDelete
  54. AnonymousMay 26, 2008

    Nadhani Maximo arudishwe kwao mapema iwezekanavyo.Huyu sio kocha ila ni team caretaker.Hapa nchini ma caretaker wapo wengi hata lunyamila naweza kufanya kazi hiyo.Kwa nini Maximo asipewe mkataba.
    1.Suala la Kaseja ni mfano tu wa timu kukosa mwalimu.Kama Kaseja alifanya makosa,mwalimu alipaswa kumuita na kumuonya.Badala ya kusikiliza majungu.Eti kaseja anaigawa timu,Maximo amejifunza lini kiswahili hadi ajue mtu anayegawa timu?Maximo ameshindwa kuondoa itikadi za USIMBA NA YANGA timu ya Taifa so HATUFAI.

    2.Suala la Haruna MOSHI.Pamoja na uwezo mkubwa aliouonyesha,Maximo hakumuita hadi kelele za mashabiki zilipozidi.Sio tu Moshi bali hata Mrisho Ngassa.Kocha ambaye hawezi kujiongoza hadi mashabiki waseme,aende BIG BROTHER sio Mpira.

    3.Aliwahi kusema kuwa hatachagua mcezaji ambaye hajamuona akicheza.Akakataa kumuita Machupa na Pawasa wakiwa Rwanda kisa hajawaona.Swali je Renatus Njohole alimuona wapi hadi akamuita?

    4.Maximo alisema hatamuita mchezaji ambaye hana namba kwenye imu yake.Hii ndio sababu aliyoitumia kumuacha Athuman Iddi baada ya kufunguwa.Swali ni kwamba ALLY MUSTAPHA BARTEZ wa simba hana namba msimbazi.Huwa anampa nini hadi Maximo apindishe taratibu alizojiwekea?

    5.Maximo bado hajatoa SOCCER development plan zaidi ya kuonekana kwenye TV akisema soccer is a process.Maximo kama anataengeneza timu,hahitaji wazee kama MBUNA,GABRIEL na wengineo.Alipokoa kombe la challege akasema ile haikuwa priority yake.Sasa where is priority ya Maximo?

    6.Marcus Tinoko naye kaja eti kutafuta vipaji.Mwaka wa pili sasa hajapata hata mchezaji mmoja wa kumpa maximo.Hawa si matapeli?

    Chonde chonde watanzania.Tutunze hivi vijisenti hata kama ni vya msaada.Maximo haufai bora hata MZIRAI.

    ReplyDelete
  55. AnonymousMay 26, 2008

    Kuna mdau mmoja amenichekesha sana..eti anazungumzia mafanikio ya Serengeti boys yaliyotokana na hamasa iliyoletwa na ITV..anasahau kuwa karibu timu nzima ilikuwa na wachezaji vijeba!!..watanzania tunapenda sana njia za mkato ndio maana timu zetu hazina maendeleo..tunajidanganya eti hatuna muda wa kuwaanda vijan ili waje kuwa nyota bora..ndio maana wakati Maximo anamchukua Jerry Tegete na kwenda Brazil na Ulaya, hatukusita kumfananisha Tegete na mtalii..lakini leo hii wapenzi wale wale waliokuwa wanambeza kijana huyu ndio wanaomshangilia kiunafiki!!..sisi wabongo hatuna kabisa uvumilivu na tumejaa kila aina ya ujuaji..wakati mwingine huwa ninatamani sana na sisi tuwe walao na wachezaji wanane wanaocheza kwenye ligi bora za ulaya ili huu upuuzi wa kuwafanya wachezaji wa simba na yanga kama vile ni miungu watu utoweke..watu wanamzungumzia kKseja kana kwamba ni bora kuliko makipa wote wa nchi hii..wanasahau kwamba Kaseja hawafikii hata robo magolikipa kama Pondamali,Mwameja na Mambosasa, tukiweza kuwa na wachezaji wengi wa kulipwa ambao watakuwa wanakuja kucheza mechi za kimataifa tu..basi hii habari ya kuendelea kuwatukuza wachezaji wa simba na yanga itakufa kifo cha kawaida kabisa..Jana stars imefungwa na Malawi goli zuri sana..lakini tukumbuke kuwa yule aliyetufunga lile goli ni mchezaji wa kimataifa anayecheza mpira nchini Russia..na katika ile timu ya Malawi kulikuwa na wachezaji wa kulipwa zaidi ya sita..sisi tulimtumia Dan Mrwanda kama mchezaji wetu pekee wa kimataifa na bado tuliweza kuwabana sana haswa kipindi cha pili..anayemdharau Maximo anapaswa kugundua kwamba sisi bado tunategemea wachezaji wetu wa ridhaa wapambane na wachezaji wakubwa wa mataifa mengine..kwa nini na sisi hatuna mastaa?..hilo ni swali tunalopaswa kulijibu kwa sababu Maximo amekuja nchi hii mwaka juzi tu lakini tumekuwa tunacheza soka tangu mwaka 1961..kama Malawi wana wachezaji zaidi ya watano wanaocheza mpira nje ya Malawi..sisi tuna matatizo gani?.wadau wenzangu wa soka inapaswa tubadilike na tuanze kuuangalia mpira wa miguu kwa marefu na mapana la sivyo tutakuwa tunaendelea kutoa hoja zinazoelea tu angani bila kuwa na mashiko ya aina yoyote ile.

    ReplyDelete
  56. Maximo aongezewe Mkataba wa Miaka miwili (2) tena.
    Kazi yake ni nzuri sana.
    Amefikisha Mpira wa Tanzania mahali ambapo ni pazuri.

    ReplyDelete
  57. AnonymousMay 26, 2008

    watu wanalia wee na Kaseje na ndiyo sababu ya kumchukia Maximo. Maximo amemfunza Kaseja alitaka kuleta u-father nationa team. Siku hizo huko simba Kaseja ana nidhamu ya kupindukia amejua haendi popote na kuringaringa kwake na kama kweli ni kipa bora si aende Ulaya akadake? Kuhusu makocha wa kibongo naomba nitajiwe mmoja tu ambaye amefikia mafanikio ya Maximo na pia watu mnajifanya hamjui kwamba Ally Bushir yupo pale pia kama kocha au kwa kuwa na mzenji basi siyo mmbongo?

    ReplyDelete
  58. AnonymousMay 26, 2008

    Mzawa nakujibu. unasema tusijifananishe na DROGBA au Chelsea kwani vigezo vyetu vya mpira si waliotutangulia?

    nimekwambia kuwa Maximo hajielewi kawakataa Machupa na Pawasa kuwa umri ni mkubwa wakati wanafanya vitu.Roger Miller alikuwa na 39 anatoka Cameroon timu ambayo tutakutana nao.

    Drogba tutakutana nae kombe la dunia kama uko serious sasa kukataa kujifananisha na Drogba ambaye tungekutana nae CAN-GHANA 2008 ni ujinga wa mchana Kwani hujui kuwa Drogba anatoka Ivory Coast na wapo Kalou,Kole Toure,Eboue, Yahya Toure n.k.

    au timu yako ya Taifa umejiandaa kwa ajili ya kucheza na Malawi na Djibout au Somalia ambayo tuliishinda kwa tabu goli moja.

    wakati haina kocha wa kulipwa wala facilities na iko vitani kama ulitizama challenji.

    juzi Taifa Cup imekwisha Hassan Mgosi kaongoza magoli na ana uwezo mzuri hajamwita.

    Ivo Mapunda kakaa benchi miezi sita lakini alipotoka tu Maximo kampanga na kutufungisha goli moja na Uganda.

    na kama kocha hawezi kuwarekebisha wachezaji hafai kwani ukocha ni sehemu ya kujua tabia na kuzirekebisha.

    Mike Tyson alikuwa na tabia mbovu kuliko Haruna Moshi au Kaseja alipokuwa mdogo.

    lakini yule Trainer wake aliyemuokota mtaani akajua jinsi ya kumrekebisha tabia zake mbovu na kumfanya bondia bora ni pale tu alipofariki yule Trainer ndio Tyson akakosa Mwelekeo.


    Maximo hana anachojua,wenzetu hushtuka mapema wanapoona muelekeo wa kocha haueleweki.

    West Ham ligi kuu ya 2006/07 walikuwa chupu chupu kushuka wakanunua wachezaji Brazil kama Tevez na Mwenzake kocha wao ALAN PARDEW akawa anawaweka benchi na timu inayumba. wenye timu wakamtimua na timu ikabaki kwenye ligi na mwaka huu kuwa nafasi ya kumi.

    Maximo mwaka jana timu yetu ilipocheza na Burkina Fasso ilishinda goli moja lilifungwa na Erasto Nyoni.kijana huyu alicheza mchezo wa hali ya juu lakini mechi inayofuatia akamuweka benchi Nyoni na kumuweka Mecky Maxime kwa vile tu jina lake la ubini (surname) yanafanana hana kiwango wala nini.

    ni sawa na kumuweka DROGBA nje wakati Final ya UEFA wakati nusu Final ni Drogba ndiye aliyewafunga Livrerpool.

    Mchezaji kaonesha kiwango kikubwa mechi iliyopita halafu mechi inayokuja unamuweka benchi.

    Pia ushindi wa Taifa staz wa 2-1 sept 2006 sio kazi ya Maximo kwani alikuwa na siku 11 tu? ni kutokana na hamasa ya watanzania na JK ndio uliwapa motisha wachezaji.

    wanaosema kuwa Maximo alileta ushindi huo ndani ya siku kumi na moja tu. vipi leo ana miaka miwili ameshindwa kuifunga Somalia au Malawi? kama alileta miujiza ndani siku 11 vipi ashindwe sasa?

    huyu si Mwalimu ni bomu.Huwezi kusema Boban hataingia timu ya Taifa maisha yake yote, jee kosa gani alilifanya kabla ya hili?ni sawa na mwalimu wa shule mtoto akichelewa unafukuza,hakufanya kazi darasani unafukuza tu,akipiga kelele unafukuza tu, adhabu ina vipimo vyake.

    Maximo au una bifu na wachezaji wa Simba?

    wewe kila mara unalilia timu iende Brazil kwa mazoezi kwa vile ikienda huko anapata commision kwenye mahoteli n.k na kuipatia pesa nchi yake.

    Timu inatakiwa iende Ulaya si Brazil ambako anaichezesha na timu za mitaani tu.na hatuwezi kuuza mchezaji yeyote, mawakala wako Ulaya sio Brazil ambao nao wana njaa kali.

    Miaka miwili hajafanya kitu hata akipewa tena miaka mitano hawezi kufanya kitu.

    Hana program kila siku anakuja na jipya.

    Nina wasi wasi kama kweli huyu mheshimiwa ana vyeti vya kweli zaidi nahisi ni tapeli fulani.

    alipofika Denmark alimleta Michael Chuma na kusema kuwa ni mchezaji wa timu daraja la kwanza Denmark wakati hakuna ushahidi wowote wa Mtanzania kukipiga daraja la kwanza DENMARK mbona Chris Katongo anajulikana na anaonekana kwenye website za timu ya BROMBY FC?

    Hatufai anatupotezea muda. Mzawa una haki ya kumpenda Maximo labda umejua mpira august 2006.ujio wa Maximo ukakuingiza kwenye kupenda mpira lazima uone ni kiboko kwako.
    ni Jongo wa Kisiju

    ReplyDelete
  59. AnonymousMay 26, 2008

    Siku zote makocha wa TZ hawa-perform vizuri sababu malipo yao huwa mizengwe, with the money this dude is geting paid, we can hire 3-5 high quality tanzanian coaches who will do a very good job.I'm sure even a lot better than Maximo because they will be very satisfied with the pay and not have to worry about vijimiradi ya hapa na pale to survive. But if wakiajiri mbongo halafu mshiko uwe matata tutarudi kule kule...

    ReplyDelete
  60. AnonymousMay 26, 2008

    nakujibu jongo wa kisiju
    nadhani ujanielewa kuhusu swala la wachezaji wenye umri mkubwa ndio nilipomtumia drogba kutokana na mtu kutoa mfano.nilichokwambia kiwango alichofikia drogba au wachezaji wa kwenye ligi za ulaya ambao mtaka kuwafanananisha na wachezaji wetu nyumbani ni ujinga mtupu.mfumo wetu wa soka ni mbovu sana wacheza wa ivory coast ulio wataja hapo wote wengi wametokea kwenye footaball academies hapo ivory coast kitu ambacho tunahitaji nchini kwetu kuwa na shule nyingi tanzania kwa ajili ya vijana wadogo hili kuweza kutoa vipaji.mchezaji kama kolo toure katokea moja kwa moja kutoka asec mimosas mpaka kwenda arsenal kitu ambacho kitawezekana kwa wachezaji wetu kama tutabadilisha mfumo wetu wa kuendesha vilabu.hivi vilabu vyetu inabidi vibinafsishwe hili makampuni yapate nafasi kuekeza kwenye soccer.makampuni yakimiliki watakua wanaendesha kibiashara kuweza kujenga viwanja vya timu pamoja pia kuanzisha timu ndogo za vijana wa vilabu hivyo na tukaanzisha ligi ya timu za vijana under 18.wachezaji wengi watakuwa wanacheza kwa moyo kwani mishahara itakuwa ya huakika na hio itasaidia kiwango cha soka kukua na kupata wachezaji zaidi.tanzania inavipaji vingi sana sema umaskini wa vilabu vyetu ndio unaua vipaji kwani wanakuwa wanacheza mpira huku wakiwa na mawazo mengi na matatizo ya kifamilia .kwahio acheni kumlaumu maximo yeye anafanya kazi kwa resources alizokuwa nazo am not saying he is the best but even if u introduce ferguson to coach our players still we will not get the results we r dreaming of.mpango hufanyike kubadilisha mfumo wa kuendesha klabu na sio migogoro tu kila siku na kusikia wachezaji wanalilia mishahara yao.utafanyaje kazi kwa kujituma kama una njaa au ujalipwa mshahara wako?
    sema ubishi wa kulinganisha chelsea na club zetu za nyumbani huo ni ujinga wa hali ya juu.na nchi ulizozitaja za africa hapo zote zina shule za kufundisha na kukuza vipaji vya watotot ndio kitu ambacho tunatakiwa kuelimisha serikali sio kwamba maximo afukuzwe.
    huyo jamuhuri kiwhelo mnae muona ndio kocha wa maana si ndio aliyeua kajumulo kwenda kusajili marafiki zake?
    SWALA NI KUWEKEZA KWA WATOTO WADOGO NA KUBINAFSISHA VILABU.
    mdau mzawa

    ReplyDelete
  61. AnonymousMay 26, 2008

    MTAPIGA KELELE MTAMALIZA SOKA NI LAZIMA UANZIE KWA WATOTO WADOGO NA PIA KLABU ZIENDESHWE KIBIASHARA HILI WACHEZAJI WANUFAIKE NA WAO SIO KUKANDAMIZWA KILA SIKU KWANI INAWAKATISHA TAMAA.NCHI NTINGI ZA AFRIKA ZINAKUZA VIPAJI.

    ReplyDelete
  62. MAXIMO NI DHAHABU YETU LAZIMA TUMTETE ILI APEWE MKATABA MWINGI COACH HUYU AMEINGIA KUFUNDISHA TAIFA STARS WAKATA TFF KUNA UBABAISHAJI SANA WACHEZAJI WAKIWA WASWAHILI WAVIVU, WATOVU WA NIDHAMU NA MAMBO MENGI MWALIMU HUYU AMEREKEBISHA HATA NIDHAMU IKO JUU SANA KWANZA MAXIMO AMEKUWA AKIFANYA KAZI YA ZIADA ZAIDI KATIKA TEAM YA TIAFA HATA KUWAFUNDISHA WACHEZAJI VITU KAMA CHENGA, KUKABA NA MBINU NYINGINE YAANI ANAFANYA KAZI KUBWA ZAIDI ME NAAMINI KAZI ANGEIFANYA COCHA WA CLUB KWAHIYO MAXIMO NI LULU YETU ME NAMFAGILIA SANA.

    ReplyDelete
  63. AnonymousMay 26, 2008

    Mdau jongo wa kisiju na mimi nakujibu
    mimi sikubaliani kitendo cha kuwalinganisha wachezaji wa tanzania na wachezaji waliokuwa ulaya wa kiafrika kama wakina drogba.nakupa sababu
    .kama ulivyosema ivory coast tunapambana nao ni kweli lakini swala sio wachezaji wake walikuwa nje swala ni kujiuliza ni kitu gani kinafanya ivory coast kutoa wachezaji wengi wakimataifa? hapo ndio itabidi twende kwenye mzizi wa njia wanazotumia je nchi yetu tunazo au la? mfano mzuri mchezaji uliyemtaja kolo toure,kolo katoka moja kwa moja asec mpaka arsenal na kipaji cha kolo kimeanzia kwenye timu za watoto wa mitaani kapiga soka bila viatu kama wachezaji wetu wengine yule.lakini mafanikio yake yalikuja kupitia shule ya watoto wanaocheza soka hapo ndipo nchi yetu imeshindwa kuwekeza hili kukuza vipaji vyetu tunavyoona mitaani.wenzetu hao wanaanzia chini na pia ni lazima vilabu vyetu vibinafsishwe sio mambo ya viongozi wako pale wenye njaa wanaendekeza maslahi yao bila kujali wachezaji kulipwa.vilabu vikibinafsishwa makampuni yataweza kujenga viwanja zaidi vya michezo na pia timu kubwa zitakuwa na uwezo wa kuendesha timu za vijana na tff ikaweza kuanzisha ligi ya vijana pia.timu za vijana za club zitaweza kushiriki katika ligi ya vijana hili ikuze zaidid vipaji.serikali ina hela nyingi sana na wana uwezo wakufanya yote haya na makocha tunao wengi tu wanaweza kuwafundisha na wawe wanauzulia semina mbali mbali hili tufanikiwe.wachazeji wataweza kuonekana na timu za nje kupitia mashindano ya vilabu vya kimataifa pia.kwahio kumfukuza maximo sio dawa bali serikali walazimishwe kutumia hela zaidi kwenye michezo kwani mafisadi wanazichota tu hazina kazi.
    mdau mzawa

    ReplyDelete
  64. AnonymousMay 27, 2008

    MZAWA nakujibu tena ingawa kila majibu yako kwangu lazima utukane mara useme Pumbavu au ujinga hii ni dalili ya kulazimisha hoja zako.

    Umekuwa ukitawaliwa sana na jazba kuliko kujenga hoja.

    Inaonekana labda uko kwenye kamati ya Staz sasa mawazo yangu yanahatarisha kibarua chako.

    Endelea kutukana tu mimi sitajibu matusi yako na jazba ulizo nazo.nitakupa Facts always.

    nimezaliwa naujua mpira sikuupenda mpira August 2006.au sikuwa mpenzi wa mpira baada ya kuingia TV nchini.au kuwa mpenzi wa Chelsea kwa vile tajiri Abromvich kajiunga nao.

    mimi damu damu na michuzi toka enzi hizo niko kwa STEVEN GERRARD.

    Sasa umekuja na hoja kuwa kwa vile hakuna wachezaji waliopita Academic hata akija FERGUSSON timu yetu hatafika popote.

    umesema kiNa KOLO TOURE wametoka Academic.kwa kauli yako hii unaungana na mimi ninayesema kuwa Maximo hatufai aondoke kwani jibu la matatizo yetu ni ACADEMIC ACCORDING TO YOU SAWA?.

    sasa Maximo si Academic basi tusiendelee kupoteza pesa zetu kulipa mishahara mikubwa Maximo na kumuweka hoteli ya elfu sabini kwa siku.

    ni vyema tuwaambie wadhamini wapeleke pesa zao kwenye Academic na huku tukijiimarisha ndio aletwe Maximo baadae baada ya kuwa na Academic za kutosha.

    vinginevyo kuendelea nae ni kupoteza muda na pesa zetu kwani hafanyi bure(Volunteering).

    kwa kauli yako hii unakubaliana na mimi bila kujijua.

    na kama Academic Haruna Moshi na Kaseja wamepitia Makongo Academic labda IVO MAPUNDA ndio hajapita Academic katoka Prison Mbeya.

    Tujiulize jee Academic ni tatizo? kukosa kwetu Academic kunatufanya sisi tusifanikiwe kwenye soka?

    Mfano UK wana Academic kila kona na playgrounds zimejaa. lakini tutizame mafanikio ya Timu ya Taifa ya UINGEREZA.

    TANGU KOMBE LA DUNIA LIANZISHWE WAMECHUKUA MARA MOJA TU 1966.ZAIDI YA MIAKA 42 ILIYOPITA.

    KOMBE LA ULAYA HAWAJAWAHI KUCHUKUA HATA SIKU MOJA.

    KWA KIGEZO CHAKO CHA ACADEMIC TATIZO NI NINI? ACADEMIC AU KITU KINGINE?

    JEE MHESHIMIWA MZAWA ACADEMIC NI KIKWAZO KWA UK? TUKUBALI TANZANIA NI ACADEMIC.


    SIKU ZOTE KOCHA MZURI MWENYE KIWANGO NA UZOEFU NDIO DIRA YA USHINDI.

    PIA USIWE NA CHUKI KUWA WACHEZAJI WA YANGA NA SIMBA NDIO WANAHARIBU TIMU YA TAIFA. HATUCHUKUWI TIMU YA TAIFA KWA KUBALANCE.

    UJUE KUWA SIMBA NA YANGA NDIO KIASI FULANI ZIMEINVEST KWENYE MPIRA MCHEZAJI MZURI ATAKUJA TU TIMU HIZO.

    KAMA ENGLAND LAZIMA WACHEZAJI WATATOKA CHELSEA JOHN TERRY,LAMPARD,MACHESTER RIO FERNAND,BROWN, ROONEY,SCHOLES, HATUJAONA TIMU KUJAZWA WACHEZAJI WA WIGAN,DERBY,CHALTON.

    MAXIMO AONDOKE BWANA MZAWA UKIONA ANAKUFAA MPELEKE KWENYE CLUB YAKO LAKINI TIMU YA TAIFA INATOSHA.

    AWATIZAME KINA VICTOR AU TAMBWE LEYA WALIKUWA NA MBINU ZA MPIRA HAWAKUWA WANABADILISHA TIMU KILA DAKIKA KAMA NDIO KISINGIZIO KAMA MTU WAKO MAXIMO.

    JEE TIMU YETU YA 1980 ILIKWENDA LAGOS ILITOKA ACADEMIC GANI?

    UNAJUA SUNDAY MANARA ALIKUWA NA UWEZO KAMA ZIDANNE AU ZAIDI JEE ALITOKA ACADEMIC IPI?MAULIDI DILUNGA ALIKUWA KWENYE TIMU YA AFRICA JEE ALITOKA MAXIMO ACADEMIC?

    BOSI MZAWA KWA HIYO UNASEMA TATIZO NI ACADEMIC KWA KAULI HIYO MAXIMO ANAPOTEZA MUDA WETU NA PESA AFUNGASHE.

    TATIZO TUNALIJUA DAWA YAKE YANINI TUNAZUNGUUKA?
    NI mimi Ustadh Jongo toka Kisiju. karibu ule nazi mkuu Mzawa.

    ReplyDelete
  65. AnonymousMay 27, 2008

    KUNA MDAU KANIFURAHISHA SANA HAPO JUU ANAULIZA KESHA JUA KISWAHILI???NI KWELI KABISA MAANA WACHEZAJI WENGI WA BONGO KINGENGE NI MAIMUNA KWAO!!INABIDI AJUE KISWAHILI ILI AFUNDISHE KWA KISWAHILI...HALAFU NCHI YENYEWE KWA RUSHWAA!!HATA KAMA ATAKOSA MUDA WA KUENDELEA KUKAA HAPA SI AKIONGEZA DAU LA RUSHWA SI ATAKUBALIWA???MIE SIPO..BYEEE

    ReplyDelete
  66. AnonymousMay 27, 2008

    Mara ya mwisho Yanga kushiriki ligi ya nane bora ilikuwa ni mwaka 1998 na mara ya mwisho Simba kushiriki ligi ya nane bora ilikuwa ni mwaka 2003..Kolo Toure mchezaji wa Arsenal ya Uingereza alikuwa akiichezea Asec mwaka huo huo wa 1998..tujiulize wako wapi wachezaji wa Yanga ya wakati huo ambao walibahatika kupambana na Kolo Toure uwanjani..Vicent Enyeama golikipa wa Enyimba ya mwaka 2003 sasa hivi anacheza mpira kwenye klabu ya Israel..tujiulize akina Said Sued, Pawasa na Christopher Alex wako wapi kwa sasa..mpira wa bongo kwa sasa sio progressive (hauna maendeleo) hata kidogo..wachezaji wengi kwa sababu ya kujilea wenyewe wanakosa kabisa mtazamo wa maendeleo..nina uhakika Kolo Toure analingana kiumri na wachezaji wengi tu wa Yanga ya wakati ule, lakini wachezaji hao wanaolingana nae kwa sasa wanacheza kwenye mechi za maveteran pale leaders club!!..zamani kidogo alikuwepo mchezaji aitwae Athumani China, alikuwa na pumzi kama mbwa wa polisi na alikuwa na kila kitu, lakini kila alipokuwa yuko free alihakikisha anakwenda oysterbay beach kwa ajili ya kujifua mchangani..wachezaji wa sasa wako hivyo?.tunaweza tukajifanya eti tunasikitikia hela nyingi anazolipwa Maximo lakini je tumeshajiuliza ni kiasi gani cha pesa wanacholipwa makocha wa nchi kama Ghana, Nigeria na Tunisia?..tumeshajaribu kujiuliza ni kwa kiasi gani wachezaji wa nchi zilizopiga hatua katika kandanda wanavyofanya mazoezi ya ziada licha ya wao kuwa na utajiri mkubwa?..Simba na Yanga zinaendelea kutuharibia mpira wa bongo kwa sababu wadau wa vilabu hivi ndio wanaowapa ustaa bandia akina Juma Kaseja..wanawafanya hawa wachezaji wasioweza kucheza hata daraja la tatu ulaya wajione kuwa wao ndio wafalme wa soka letu..Kaseja anamzomea Ivo eti kwa sababu kafungwa magoli manne kule Dakar..yeye alishafungwa magoli 5-0 na Rwanda, akafungwa 5-0 na Kenya pale Arusha, akafungwa 4-0 na Gabon na ameshafungwa na mafowadi wa Enyimba jumla ya magoli 16 na hakuna golikipa yoyote yule aliyejitokeza hadharani na kuuponda uwezo wake..kiburi cha Kaseja kinasababishwa na wadau wa soka la bongo kuwapa wachezaji wetu sifa ambazo bado hawastahili kuzipata..timu zetu zinapiga sana siasa za mdomoni kiasi kwamba kocha yoyote yule akija hapa bongo na yeye atajikuta ni sehemu ya siasa za soka letu..Simba na Yanga zilitakiwa kwa sasa ziwe na mitaji isiyopungua dola milioni kumi kwa klabu moja..zilitakiwa ziwe zinafanana na klabu kama Supersports na Enyimba lakini wapi!!. Wengi wanaomlaumu Maximo wanatakiwa wawe wanahudhuria mazoezi ya Stars ili wajionee jinsi Maximo anavyolazimik kufanya kazi mbili kwa wakati mmoja..analazimika kuwafundisha wachezaji wetu mambo ya msingi kabisa na wakati huo huo anawaanda katika suala zima la tactics ili waweze kupambana na timu zenye wachezaji wa kulipwa..tukubali au tukatae..tunatakiwa tuzifanyie mapinduzi makubwa sana hizi timu zinashiriki ligi kuu ya bongo..kama tukiendelea kujidanganya kwamba eti na sisi tayari tunao wachezaji nyota wanaoweza kupambana katika soko la kimataifa basi tujue kwamba tumeula wa chuya..hata akija mtaalam Vicente del bosque au mtaalam Fabio Capello bado atatuambia kwamba tunahitaji miaka kadhaa ili tuweze kufikia katika viwango vinavyokubalika kimataifa , tulijisahau sana katika miaka ya themanini tukaishia kwenye siasa za akina Muhidin Ndolanga na lazima tutambue kwamba wenzetu waliutumia muda ule kikamilifu..lazima tuondokane na ndoto za kutaka kujenga jengo la ghorofa kumi ndani ya wiki moja!!..Kondic alisema wachezaji wetu hawafundishiki, wadau wakaanza kumshambulia kwenye vyombo vya habari lakini message ilikuwa delivered kwa sababu alikuwa anatufikishia ujumbe kwamba hawa wachezaji wetu wana msingi mbovu toka wakiwa wadogo..Maximo anaweza akaondoka lakini kama vilabu vyetu vinaendelea kufanana na vilabu vya wahuni wa mitaani basi sioni mabadiliko yoyote yale..tunaweza tukampa timu ya taifa mtaalam yoyte yule awe wa nje au wa ndani lakini tuachane na kendekeza matarajio yanafanana na ndoto za mchana..tuendelee kuwa wavumilivu ili Dokta Maximo aendelee kuangalia ni dawa ipi inayotufaa kwa sabu tumeshatoka ICU na sasa tunaweza hata kuzungumza.

    ReplyDelete
  67. AnonymousMay 27, 2008

    Mheshimiwa Bosi Mzawa naona umekimbia hoja ya Academic na sasa unasema Kaseja kafungwa magoli 16.
    usimshangae Kipa wa Enyimba sisi kina sunday Manara wamecheza nje hadi marekani. wako wengi Adolph Rishard,Tostao n.k
    nitakujibu baadae kwa kina
    nawahi kuangua nazi zangu.wewe ulaji wako uko mikononi mwa Maximo ambaye umebatiza kuwa ni Dokta mtu ambaye elimu yake ni kidato cha nne kama FERGUSSON.AU ALAN PARDEW wA chalton aliyefukuzwa west ham.

    ReplyDelete
  68. AnonymousMay 27, 2008

    Mimi naona issue ya Maximo kuongezewa mkataba si jambo la msingi. Taifa stars ya sasa hata Mourinho akifundisha hakutakua na mafanikio. We have to invest on the youth and build football academies. That's most important thing.
    At the end of the day, Maximo lazima achague wachezaji waliopo nchini, na kama wachezaji hawana misingi mizuri ya soccer, haitawezekana. Ni kweli Stars wameendelea kidogo under Maximo. lakini sidhani kama kocha mwingine yeyote anaweza kufanya vizuri kuliko Maximo sababu mwisho wa siku, ni wachezaji wa Tanzania ndio wanaenda kucheza. Na kama players waliopo are not good enough, its simply cant work. Huwezi kumfundisha mchezaji wa miaka 26 tecnic ya kukick the ball. Ameshakomaa, hayo ni mambo ya miaka 13. Kwa hiyo mimi naona sasa hivi serikali/TFF ikazanie kwenye youth programs. Wenzetu wa nchi nyingine wanaendelea sababu ya kuwa na better setup ya youth.
    So, kumalizia, naona aongezewe mkataba, sababu at least yeye tunaona maendeleo kidogo.

    ReplyDelete
  69. AnonymousMay 27, 2008

    Mheshimiwa, mimi namshukuru Mungu nina kazi yangu inayonipatia riziki..sihitaji chochote kutoka kwa Maximo..ile sipendi kuona Maximo anabebeshwa mzigo usiokuwa wa kwake!!..unazungumzia akina Sunday na Tostao ambao walicheza mpira miaka ya sabini na themanini..leo hii ni karne nyingine kabisa yenye ushindani tofauti na ule wa miaka ya zamani..Maximo ni mwajiriwa ambae ajira yake inaisha kama ziishavyo ajira nyingine zozote zile..lakini binafsi sipendi kabisa mentality za usimba na uyanga kwa sababu ndio zimetufikisha hapa tulipo..waganda wanapeleka timu yao ya taifa ya vijana barani ulaya na timu hiyo ikienda kushiriki mashindano ya vijana ya afrika mashariki, inagawa dozi nene..majirani zetu wanaangalia mbali lakini sisi tunaishia kwenye ushabiki wa simba na yanga, ushabiki wa kutaniana kwenye bar za bongo..we are not serious..kama tulikuwa na akina Jella Mtagwa na Sunday Manara..leo mbona mastaa wetu akina Mrwanda wanaishia Kuwait?..kitu kinachomfanya nimheshimu Maximo ni ile hali ya nidhamu na msimamo alionao, hakubali kuyumbishwa na mswahili yoyote yule, anasimama katika kile anachokiamini..yuko tofauti na makocha wa kibongo..makocha waliojaa nidhami za uwoga..makocha wanaokubali kufanya kazi wakiwa na dukuduku mioyoni mwao..makocha wanaowababaikia mastaa uchwara wa yanga na simba..kama asingekuwa Maximo basi leo hii tusingemthamini Jerry Tegete pamoja Godfrey Boni..kwa sababu ya msimamo alionao amewachukua timu ya taifa na wanacheza vizuri..huwezi kabisa ukakwepa uwepo wa academies katika maendeleo ya kweli ya soka..nenda karume kaangalie jinsi mastaa wetu wa bandia wanavyoshindwa kufanya mambo ambayo ni basic kabisa..kwa sababu mpira wamejifunzia kwenye timu za kinunda za uswahilini..faida ya academies sio tu kuandaa wachezaji tangu utotoni bali pia zinaweza zikatumiwa katika kuanzisha uhusiano wa kimpira kati ya academies zetu na zile zilizoko katika nchi zilizoendelea na ni rahisi kwa wadau wa soka kutoka katika nchi zilizoendelea kuweza kufuatilia kipaji cha mchezaji wa afrika kutokana tu na ule uhusiano wa academies mbili tofauti..mfano halisi ni jinsi Bolton Wanderers walivyoanzisha uhusiano na Academy ya kipingu..haya ninayoyaandika hapa ni mageni kwa wabongo wengi kwa sababu vilabu vyetu tunavyoviita vikubwa ni sawasawa na timu za mitaani..zinaongozwa kisanii na kihuni..bila kuondokana na tabia ya kutaka kufanikiwa ghafla bila kutoka jasho basi tutajikuta tunaishia hapa hapa tulipo..we have to appreciate at least a bit..tulikuwa hatujawahi kuifunga timu ya afika magharibi nyumbani na ugenini lakini tumeweza kuifunga Burkina Faso nyumbani na ugenini tena kwa kutumia hawa hawa mastaa wa kwenye magazeti yetu..na kama sio uchanga wa wachezaji wetu ambao walishindwa kuconcentrate kwa asilimia mia moja, tulikuwa tumeshawafunga Senegal pale Mwanza. kama nilivyosema hapo juu..we really have to be serious, there is no shortcuts in football lazima tuendelee kuwekeza na tupunguze kuishi katika ndoto kwamba eti kocha bora akija anaweza kuleta maendeleo ya ghafla..makocha wetu walishapewa timu yetu ya taifa zaidi ya mara moja na tukawa tunapewa vipigo vya mbwa mwizi kila tukitia timu uwanjani..tuachane siasa za kuangalia hapa tulipo tu bila kuangalia mbali kutoka hapa tulipo..tuache kujidanganya kwamba kuna miujiza ya ghafla katika soka..kitu kama hicho hakipo na hakiwezi kuwepo kwa sababu mpira ni taaluma na taaluma yoyote inapitia katika hatua zake muhimu ili iweze kukamilika.

    ReplyDelete
  70. AnonymousMay 27, 2008

    JOHN WA KISIJU kwanza asante kwa nazi kwani nimesahau kukwambia mimi ni wakisiju damu kama wewe.pili huyo mdau juu sio mimi huyo ni mwingine aliyezungumzia hoja kaseja.hoja ya academic sijaikimbia sinimeinga mkono katika hoja zangu za mwanzo? ninachopinga mimi kufukuzwa kwa MAXIMO kwani katoa mchango mkubwa tu na tumuache aendelee kufanya kazi yake.
    kuhusu wakina sunday manara na akina adolph richard wote na wajua kwa kina na hao wote walikuwa wanacheza mpira kwa mapenzi ya mchezo wenye ,walikuwa na furaha wanapokuwa uwanjani koenesha vipaji vyao.sasa vijana wetu wa siku hizi wakinyimwa mshahara wanaijumu timu zao wanakuwa wanacheza chini ya kiwanga lakini lazima wakumbuke wanajikomoa wao wenyewe.wao wanatakiwa wapige mpira kwa mapenzi na wajitu kwa moyo wote kwani ndio wataweza kuonekana na timu za nje na kupata mikata bora.
    haya mkuu sina mengi angalia minazi yangu sijaja siku nyingi huko kukwea sasa tafadhali kaa mbali na mashamba ya minazi ambayo sio ya ukoo wako.ha ha ha.
    na tufanye mpango tukuze vipaji kisiju basi sio longolongo la dar tu kwani imejaa matapeli.lazima tushuke na KISIJU BOYS.
    MDAU mzawa

    ReplyDelete
  71. AnonymousMay 27, 2008

    kwako john wa kisiju
    swala lako la uingereza kuwa na academics na bado timu yataifa haipafomu ni kwamba tataizo la uingereza kwanza wachezaji wao hawako techinical na ndio maana wamemleta mtu kama capello atawasaidia sana.lile swala la kuwa na kocha wa nyumbani kwao ndio ilikuwa inawaua kwani walikuwa wanawachukua ma faza ambao wako chini ya kiwango saa nyingine.si umeona capello anavyo wapa nafasi vijana? sasa utaona watakacho vuna.na pia wachezaji wao wa academy wengi huwa hawapati nafasi timu za juu kwa vile wageni wako wengi mno kwenye ligi yao.
    tanzania tunavuna tulicho kipa miaka iliyopita .
    mdau mzawa

    ReplyDelete
  72. AnonymousMay 28, 2008

    Mdau Mzawa.upo?au uko safarini? KWENDA kuongeza kiwango cha Timu yetu?

    Unasema Sunday Manara kacheza karne iliyopita una maana karne ya kina Sunday mpira ulikuwa chini kuliko sasa hivi?

    Lakini ningependa kukuREMIND KUWA TIMU BORA YA KARNE YA FIFA NI YA MWAKA 1970 AMBAYO IMECHAGULIWA NA FIFA NI TIMU YA BRAZIL AMBAYO ILIKUWA NA WATU KAMA KINA PELE,JAZINOH,TOSTAO, CARLOS ALBERTO PERERA N.K

    AMBAYO KWA MUJIBU WA FIFA WANASEMA NI TIMU BORA AMBAYO HAIJAPATA KUTOKEA HADI SASA HIVI.

    SASA KINA SUNDAY MANARA WALIKUWA WANACHEZA KWENYE LEVEL HIZO.

    KWA MTAZAMO WAKO UNATAKA KUSEMA KUWA WAKATI WANACHEZA KINA SUNDAY KUWA KIWANGO KILIKUWA CHINI AMBAPO SI KWELI UNAPINGANA NA FIFA. AU UNATUMIA KIGEZO CHA MAXIMO?

    MZAWA HATA WAZEE WETU KAMA MZEE MANGARA TABU UONI WAO ULIKUWA MKUBWA ZAIDI KULIKO WALIPOKUJA KINA PETER MUSHI NA KUTUSHIA CLUB KAMA PAN AFRICAN.

    KINA MZEE TABU MANGARA WALIZIPELEKA TIMU BRAZIL KWENDA MAZOEZINI TU.WALIWEZA KUIALIKA TIMU KAMA SANTOS TIMU YA PELE KUJA WAKIWA HAWANA MITANDAO,BLOG,MOBILE PHONE, EMAIL WALA WEBSITE.

    KIFUKWE NI MTAALAM WA MAJENGO BY PROFESSIONAL KASHINDWA KUJENGA UKUTA WA YANGA NA UMEBOMOKA.

    WAKATI WAZEE WALE WALIJENGA GHOROFA ZIMA SIO UKUTA TU ULIMSHINDA INJINIA KIFUKWE NA MALINZI.

    KWA MTAZAMO WAKO JERRY TEGETI NI MKALI KULIKO NGURUNGU HUSSEIN,AU NIZAR KHALFAN NI MKALI KULIKO SUNDAY MANARA,HAMIS GAGA, KHALFAN NGASSA ,DOTTO MOKILI,AU ATHUMAN CHINA KWA VILE WALICHEZA KARNE ILE.

    PIA MRWANDA DANNY NI MKALI KULIKO PETER TINO,MAULID DILUNGA,KITWANA MANARA,KASSIM MANARA,TOSTAO N.K

    KIPA WAKO WEWE NA MAXIMO IVO MAPUNDA NI MKALI KULIKO MAMBOSASA,PONDAMALI,MAHADHI BIN JABIR N.K KWANGU MIMI MAPUNDA WAKO HAMFIKII HATA MOSES MKANDAWILE AU JOSEPH FUNGO AU HATA KESSY TARZAN SEMBUSE IDDI PAZI.

    KWA MTAZAMO WAKO HUO HUO TEVEZ NI MKALI KULIKO MARADONA,ROONEY MKALI KULIKO GEORGE BEST KWA VILE WALE WALICHEZA KARNE ILE.

    HIVI UNAJUA KUWA CLUB YA PAN AFRICA ILIKUWA ZAIDI YA TIMU YA TAIFA YA SENEGAL ILIYOKWENDA FAINALI KOMBE LA DUNIA 2002?

    UNAJUA KUWA PAN AFRICA HAWAKUWAHI KUFUNGWA ZAIDI YA GOLI MOJA NA TIMU ZA NIGERIA ZAIDI YA MARA SITA WALIZOCHEZA NIGERIA?

    NDUGU YANGU KIBOSILE MZAWA MPIRA UMEHARIBIKA BAADA YA WATU KAMA WEWE MSIOJUA MPIRA KUVAMIA FAT AU TFF NA VILABU VYA MPIRA, MMETULIA MASHIRIKA YA UMMA NA SASA MMEVAMIA CLUB ZETU ZA MIPIRA HUKU HAMUUJUI MPIRA.

    BWANA MZAWA UMEWAHI KUKAA NA MAREHEMU AMIR BWANAMCHAWI NA UKANYWA NAE KAHAWA? HUKU MKIJADILI MPIRA? UNAMJUA MZEE MWILIMA AU MIKIDADI KASANDA?SHIRAZ SHARIF?

    NAJUA NIKUULIZA WACHEZAJI WA TIMU YA TAIFA YA ZAMANI AU CLUB ZETU HUWAJUI WATU KAMA ELISHA JOHN,ATHUMAN CHUMA, KILAMBO UMEWAHI KUWAONA KWA MACHO? NAJUA WACHEZAJI UNAOWAJUA WEWE NI MACKY MAXIME,IVO MAPUNDA,MAFTAH,KIGGI MAKASI,N.K YAANI KIKOSI CHA MTAALAM ASIYE NA MAFANIKIO MAXIMO.

    MANENO MENGIII KAMA CHIRIKU KWENYE VITENDO VISINGIZIO KILA KUKICHA.

    CHELSEA WALIKUWA NA ACADEMY NA KILA KITU MBONA HAWAKUCHUKUA UBINGWA KWA MIAKA ZAIDI YA 50 HADI KAJA KOCHA MWENYE UWEZO MOURINHO?

    TOTENHAM WALIMBADILISHA KOCHA WAO (MARTIN JOL) NA KUMLETA RAMOS NADHANI UMEONA KIWANGO KILIVYOBADILIKA.

    MISRI WAMECHUKUA KOMBE LA CAN JUZI JUZI WALIKUWA NA KOCHA MZALENDO MWENYE UWEZO.

    ANGOLA WANA KOCHA MWENYE UWEZO MZALENDO NA WANAFANYA VITU.

    HAO CAMEROON NA SENEGAL WALIKUWA NA MAKOCHA BORA NDIO WAKAPIGA HATUA.

    SIJAKATAA KUWA ACADEMY ZISIWEPO NA TAYARI TUNAZO KAMA ZA KIPINGU KULE BAGAMOYO LAKINI LAZIMA TUWE NA MWALIMU WENYE UWEZO SIO BLAH BLAH KILA KUKICHA..

    WEST HAM WANAONGOZA KUWA NA ACADEMY NZURI ILIYOWATOA KINA JOE COLE,LAMPARD,DEFOE,RIO FREDINAND,MICHAEL CARRICK,N.K

    MBONA HAWAJACHUKUA KOMBE?

    LIVERPOOL INA MIAKA 20 HAIJACHUKUA KOMBE LA UBINGWA -UK JEE HAWANA ACADEMY?

    JOS MOURINHO ALIKUJA NA ACADEMY MPYA CHELSEA?

    MDAU MZAWA KAMA INGEKUWA NI MAXIMO NDIE MENEJA WA CHELSEA KWENYE FINAL YA UEFA NA MAN UNITED UNGESEMA KUWA ASAMEHEWE KWANI PENALTY YENYEWE ILIKUWA YA SABA NDIO TUMETOLEWA LAKIN GRANT KANGOKA WATU HAWABAHATISHI.

    MZAWA MIMI SIAMINI WEWE NI MTU WA KISIJU WATU WA KISIJU TUNAUJUA MPIRA UNAMKUMBUKA MANITU BUS SERVICE? UNAJUA KULA DAFU? SIO NDAFU MKUU.
    Wako Jongo toka Kisiju.

    ukijibu uwe unaweka space mwl wangu Mzawa iwe rahisi kukusoma.

    ReplyDelete
  73. AnonymousMay 28, 2008

    Mdau john wa kisiju mimi naona nikupe ushindi manake unabishana kwa nia ya kubishana sio kuelimishana .kila maneno yangu una yabadirisha unayaweka jinsi unavyotaka kwahio muheshimiwa hongera sema unaweza kurudia kusoma hoja zangu kwa ufasaha zaidi.na kuna mdau mwingine pia katoa point za maana nae unawezza kukusanya ukazifanyia kazi. Wasalam.
    Mdau mzawa

    ReplyDelete
  74. AnonymousMay 28, 2008

    Wewe comment zangu zote unazibadirisha unaziweka jinsi unavyotaka.
    Mdau mzawa

    ReplyDelete
  75. AnonymousMay 28, 2008

    Ndugu yangu wa kisiju unapaswa kuelewa kwamba kunywa chai na akina Bamchawi na Mangara sio kuujua mpira,
    kuishi nyumba mmoja na shekhe sio kumjua Mungu,
    kuishi nyumba moja na mchungaji sio kumjua Mungu,
    tatizo letu wabongo tumejaa kila aina ya ujuaji na majivuno yasiyokuwa na msingi.
    Timu tunazozipenda kwa sasa haziwezi kukaa na kocha mtaalam kwa zaidi ya miaka miwili..lazima watamwanzishia majungu na maneno maneno mengi ya kipuuzi ili mradi wamkwaze aondoke.
    Siwezi kuwadharau wachezaji wa zamani kwa sababu ninaheshimu mchango wao katika soka letu.
    Maximo amekuja amekuta Simba na Yanga na vilabu vingine vya kibongo havina programu zozote za maana, akaanza kuwafundisha wachezaji wetu mambo ambayo walitakiwa wawe wameshafundishwa katika timu za vijana za vilabu vyao.
    Rafiki yangu soka la kisasa linahitaji sana mchango wa Academies..lazima tuanze na umri mdogo kama tunataka kuwasaidia wachezaji wetu..na kuanza na umri mdogo pia kunajumuisha suala zima la lishe..hao akina Sunday Manara na Adam Sabu na wengineo walikuwa na nguvu kulinganisha na hawa akina Nizar Khalfan.
    Halafu unaonekana huna kumbukumbu nzuri hata kama uliwahi kunywa chai na akina Bamchawi..timu iliyokwenda Lagos mwaka 1980 ilikuwa ina wachezaji waliofundishwa na Profesa kutoka Romania pale Kaunda Stadium,
    timu ambayo mpaka leo hii inampa kiburi Mziray ni timu iliyotwa kombe la Challenge mwaka 1994..timu ile ilikuwa na wachezaji wengi wa simba ambao walikuwa wameandaliwa kitaalam na kocha Dragan Popadic..bahati mbaya hata mziray nae ameshasahau.
    Wabongo hatuna jadi ya kuheshimu makocha..na tabia hii tumekuwa nayo kwa muda mrefu sana..wadau wanawapuuza makocha halafu wadau wenyewe sio creative..kazi yao ni maneno meengi kwenye vijiwe vya kahawa lakini utendaji ni sifuri
    tujitahidi kwa wakati huu ili hili tabaka la vijana wasomi wanaofanya miujiza yao kwenye makampuni makubwa kama vile Celtel, Tigo na Vodacom waweze kuingia kwenye hizi timu zetu na kuleta mabadiliko makubwa ya uongozi..aina ya uongozi wa Mzee Matunda na Dalali umepitwa na wakati kwa sababu wao wanafahamu mambo ya ushirikina..ambao umeshindwa kutusaidia ili tutoke hapa tulipo.
    Tulitumie kombe la taifa vizuri..makocha wa timu za mikoani wasiwe wavivu katika kusaka vipaji vingi zaidi..hao wakongwe uliowataja walitoka kwenye kombe la taifa..lazima kuwe na mashindano ya kila mkoa ili yaweze kutoa timu moja imara ya mkoa fulani..ile tabia ya akina Julio ya kuchukua wachezaji wa timu mmoja na kusema eti ndio timu ya Ilala haitusaidi kwa sasa.
    huwezi ukailinganisha Chelsea na soka letu la kibongo..Abrahamovich ametumia zaidi ya paundi milioni 500 kwa ajili ya kununulia wachezaji tu..tena wachezaji wanaopatiwa kila kitu kuanzia mafunzo ya uwanjani hadi mshahara.
    Misri inayofundishwa na mzawa Shehata ina makocha kibao wa kigeni katika ngazi ya vilabu na kwa miaka mingi wamefundisha timu za pale kwa mafanikio.
    Kama timu saba za hapa bongo zinakuwa na makocha saba wa kiwango cha Cirkovic wa Simba basi kutakuwa hakuna haja hata ya kuwa na Maximo..Mshindo Msolla na Abdallah Kibaden watakuwa wanatutosha.
    huyu Kondic wa Yanga ndie aliyejenga msingi wa timu ya taifa ya Angola, kabla huyu mzalendo wa sasa hajaanza kuifundisha timu ya taifa ya Angola.
    tabia chafu ya kupenda kudharau taaluma za makocha ndio inayozifanya timu zetu zionekane hazichezi kitimu..kwa sababu kabla hata kocha hajaweza kuifanya timu icheze kwa mtindo na falsafa anayoitaka, tayari unakuta wajuaji wanasema eti kocha hafai..ukiwauliza huyo kocha asiyefaa anatumia formation gani, hawawezi kukwambia..ujuaji wetu ndio umeufanya mpira wetu haswa ngazi ya vilabu kubakia hapa ulipo.
    wachezaji wetu na wao wamezidi kujiona bora kuliko walivyo..mfano ni Juma Kaseja na yule mvuta bangi Haruna Moshi..waliowavimbisha vichwa ni sisi wajuaji tunaojiita wadau wa soka.
    Maximo ameshindwa kutupeleka Ghana na tumeshindwa pia kutwaa kombe la Challenge lakini tangu mwaka 1980 hatujashiriki tena kombe la mataifa huru ya Afrika..ina maana kati ya mwaka 1980 na mwaka 2006 Maximo pia alikuwepo?.
    Kama uliweza kunywa chai na akina marehemu Bamchawi basi ina maana ni mtu nwenye influence kwenye soka la kibongo ..sasa itumie influence hiyo hiyo kwa kuwaambia hao wadau wa soka letu kwamba wakati wa mabadiliko ya kweli ndio huu..na Marcio Maximo ni sehemu tu ya mabadiliko hayo ambayo yanatakiwa yaanzia chini kabisa.

    ReplyDelete
  76. AnonymousMay 28, 2008

    ndau wa kisiju sidhani kama unasoma maoni yangu kwa sababu hayo mambo unayounga mkono ndio mimi pia nimeongelea.sijawazarau wakina sunday manra soma vizuri au unatuma maoni yako kupitia gmail ya michuzi?
    mdau mzawa.

    ReplyDelete
  77. AnonymousMay 28, 2008

    Bosi Mzawa.

    HATUSHINDANI BALI KUELIMISHANA, NDIO MAANA KUNA SEHEMU NIMEKWITA MWALIMU INGAWA LABDA INAWEZEKANA ULIKUWA MWALIMU KWELI HUKO NYUMA.

    SIO KAMA TUNADHARAU MAKOCHA HAJAWAHI KUTUKANWA PROFESSOR VICTOR AU TAMBWE LEYA AU GEFF GUTENDEFF ALIYEFUNSHA STAZ 1982.

    ANAYETUKANWA NI MAXIMO NA ATAZOMEWA SANA KWA VILE SI KOCHA.

    NI MSAANI FULANI ANAYEBANGAIZA KWA KODI ZETU.

    NA KAMA USHINDI UMESHINDA WEWE KWA KUSEMA DANNY MRWANDA NI BORA KULIKO MALOTA SOMA,NTEZE JOHN,ABDALLAH MWINYIMKUU AU ALI KATOLILLAH.

    NA USHINDI WA DHAHIRI KUSEMA KUWA NIZAR NI BORA KULIKO ABDUL(NICO) NJOHOLE,RAMADHAN LENNY(ABEGA)HUSSEIN MASHA N.K

    KIPA WENU WEWE NA MAXIMO, IVO NI BORA KULIKO MAMBOSASA NA IDDI MSAKAA AU JAMES KISAKA.

    BEKI WENU MAFTAH NI MKALI KULIKO KAJOLE,KENNY MKAPA,AHMED AMASHA,TWAHA HAMIDU NORIEGA NA JOHN FAYA.

    KAMA TIMU YA ILALA IMECHUKUA UBINGWA UNAUMIA KWA VILE NI VIJANA WA MSIMBAZI? TIMU YA TAIFA IMEIBINAFSISHA KWA KANDAMBILI SASA HATA TAIFA CUP MNATAKA WACHUKUE KANDAMBILI?

    BOBAN AKIFUTA BANGI INAKUUMA NINI? ANANUNUA KWA PESA YAKE NA AKIWA HANA TUTAMNUNULIA SO LONG ANATUFANYIA KAZI YETU NA TUNAIONA,

    MARADONA ALIKUWA ANABWIA UNGA,FOLLER WA CARDIFF NI MTEJA. SIO BOBAN WA KWANZA.

    NAIJUA VYEMA TIMU YETU YA 1980 YA LAGOS SIKUTAKA KWENDA KWA UNDANI KWA VILE NAJUA MHESHIMIWA MZAWA MPIRA UMEUJUA AUGUST 2006 AU ALIPOANZA DR.RICKY ABDALLAH KUONEKANA KWENYE TV.

    WAZEE NILUOKUNYWA NAO KAHWA WANAUJUA MPIRA NA WALIKUWA NA MAPENZI NAO.NDIO MAANA UKAWA JUU MPIRA, HAWAKUWA NA ELIMU YA HAO VIJANA WA TIGO NA VODACOM,ELIMU NI TOFAUTI NA MPIRA, FERGUSSON NI KIDATO CHA NNE NA AMEFELI.

    WALIOVURUGA MPIRA WETU NI MTU KAMA WEWE,DAVID NGONYA,PETER MUSHI,MPONDELLAH CHARLES,MALINZI,KIFUKWE,UKEREGE, YULE JAMAA ALIKUJA MSIMBAZI ALIKUWA NA KAMPUNI YAKE YA UVUVI NI MAREHEMU SASA(MTEMA),

    WATU AMBAO HAWAKUZALIWA NA KUKULIA KWENYE MPIRA WAMEUTUMIA KAMA NJIA YA AJIRA ZAO.

    TENGA ALIOKOTWA NA HAWA WAZEE WANYWA KAHAWA NA KUMPA USTAARABU MUULIZE?

    MWAKALEBELA ANAUJUA WAPI MPIRA? AU WAMBURA MTU ALIYEKUWA AKIPENDA GOLF LAKINI ALIPOONA MPIRA UNA MASLAHI AKAJIPELEKA HUKO KUTUMIA KAMA NJIA YAKE YA KISIASA.

    MAGORI ANAUJUA WAPI MPIRA? NAMIINI WEWE NDIO KUNDI HILO HILO LA KINA WAMBURA NA MAGORI.

    WAZEE HAO WALIWEZA KUZIALIKA TIMU KAMA ASTON VILLA KIPINDI HICHO. WEWE NA MAXIMO WAKO TUNAOMBA MTULEE FULHAM AU FULMENSE.

    UNARUDIA KUSEMA TUSIJEFANANISHE NA CHELSEA JEE TUKIJIFANANISHE NA NANI?MALAWI,DJIBOUT NA SOMALIA?

    KOCHA WAKO MAXIMO ANA FALSAFA GANI ZAIDI YA KUONA IVO NI KIPA BORA MTU ANATETEMEKA GOLINI KILA DAKIKA.


    MZAWA UMERITHI CHUKI ZA MAXIMO KWA MSIMBAZI? BASI IFANYE DAMU YAKO IWE NJANO AU KIJANI KWANI MWENZIO MAXIMO ANAIPENDA YANGA KWA VILE INAFANANA NA JEZI ZA TIMU YAO YA TAIFA.

    NA PIA ANAJUA KUWA RAIS WETU NI YANGA HIVYO ANALETA NIDHAMU YA UOGA NA KINAFIKI.

    NAOMBA MWALIMU MZAWA UKIANDIKA WEKA NAFASI BAINA YA SENTENSI ILI NIKUJIBU VIZURI.

    PIA NAOMBA UNITAJIE WACHEZAJI WA SIMBA, YANGA, PAN AFRICA 1979-1984.
    USIENDE KWENYE ARCHIVES YA MICHUZI AU DAILY DAILY NEWS.

    JEE HARUOB NADIR CANAVALLOH NI SAWA NA MOHAMED BAKAR TALL AU JELLAH MTANGWA.?

    NI WAKO KIJANA WAKO MAALIM JONGO WA KISIJU MIE SIO JOHN PLS.

    ReplyDelete
  78. AnonymousMay 28, 2008

    mie sio JOHN NI JONGO.
    NAKUBALIE UMESHINDA NA NAKUBALI KUWA NADIR HAROUB CANAVALOH NI MKALI KULIKO JELLAH MTANGWA NA MOHAMED TALL.

    NIZAR KHALFAN MKALI KULIKO RAMADHAN LENNY,ABDUL(NICO) NJOHOLE AU HUSSEIN MASHA.

    MRWANDA NI MKALI KULIKO ALI KATOLILA,ABDALLAH BURHAN,JUSTINE SIMFUKWE,VICTOR MKANWA,JUMA MGUNDA,FUMO FELICIAN

    NAENDELEA KUANGUA NAZI NITARUDI KUKUJIBU.BOSI MZAWA ULIYEJUA MPIRA 2006-AUGUST AU ALIPOANZA KUONEKANA DR.RICKY ABDALLAH KWENYE TV.

    ReplyDelete
  79. AnonymousMay 29, 2008

    Kaka za asubuhi..ndugu yangu najua tunaelimishana na nafurahi sana kuwepo kwa huu mjadala..nakufahamisha tu kwamba mimi ni Simba damu ila usimba wangu haunifanyi nikaichukia timu ya taifa eti kwa sababu timu ya Yanga ina wachezaji wengi katika timu ya taifa!!..kama umekuwa ukinisoma vizuri..nimeandika kwamba tunahitaji wachezaji wengi wa kulipwa ili huu ujinga wa usimba na uyanga uweze kupotea kabisa..sasa hivi wapenzi wa simba wanaona kama vile stars ni yanga..kuna wakati utafika na wapenzi wa yanga nao wataona kama vile stars ni mali ya simba..tukiweza kuwa na professionals wetu kumi na moja wanaocheza soka nje ya afrika basi kocha wetu wa stars awe Maximo, Msola au hata Julio atakuwa na kazi ndogo kuliko ilivyo hivi sasa,
    Haruna Moshi anavuta bangi kwa hela zake mwenyewe lakini madhara ya bangi zake ni makubwa kuliko anavyofikiria..kwa sababu zinamfanya apoteze hata ule uwezo mdogo wa kufikiri alionao kwa sasa
    Mawazo ya kuwaheshimu kina Katolila na Mgunda hata mimi ninayo lakini hali halisi kwa sasa ni kwamba hatuna wachezaji wa aina hiyo..washambuliaji tulionao ni aina ya Abdallah Juma, Mokili Lambos na Mgosi..hatuna kwa sasa striker wa aina ya marehemu Victor Mkanwa au marehemu Mchunga Bakari..kama tungekuwa nao basi Mwaikimba au hata Kaniki asingecheza mechi muhimu kama ile tuliocheza kule Senegal na tukapigwa 4-0.. na wala si kweli kama baadhi ya wapenzi wanavyosema eti machupa na kaseja wanaweza kutusaidia ..stars ya msola ilikuwa inafungwa kila ikitia mguu uwanjani na hao wote wawili wakiwemo uwanjani,
    usimba na uyanga hauna mpango wowote kwa sasa zaidi ya kuturudisha nyuma..hao watu waliokulia kwenye mpira mbona hawajitokezi kuziokoa timu zetu..timu zenye mamilioni ya mashabiki kila kona ya nchi hii lakini benki hawana hata Tshs bilioni moja..timu changa kama Enyimba iliyoanzishwa 1976 ina maendeleo kuliko Simba iliyoanzishwa 1936!!..hao watu wa mpira wanafaida gani zaidi ya kuendekeza majungu pale msimbazi na kaunda?..hao watu wa mpira wanafaida gani ikiwa mpaka leo hii simba wanashindwa kukaa na makocha kwa zaidi ya miaka mitatu?..kila kocha anaikimbia timu tena baada ya muda mfupi tu..hao watu wa mpira wana faida gani ikiwa mpaka leo hii simba inafanya mazoezi kwa kuhamahama ..mara leo wako kawe kesho wako tandika keshokutwa wako chuo kikuu..ni bora tusiendelee kuwa na watu wa mpira kama hawana faida yoyote kwenye mpira wa Tanzania..kuujua mpira zamani sio tija , kama kuujua mpira tangu miaka ya sabini ingekuwa tija basi naamini wajuaji wa mpira wangeshausaidia mpira wetu kutoka hapa tulipokwamia , kwanini nyinyi mnaoujua mpira msubiri mpaka aje Kikwete auinue mpira wetu ndipo mnapoanza kuonyesha ujuaji wenu?..kocha yoyote atakayekuja kufundisha mpira hapa bongo ataitwa msanii kwa sababu sisi ndio wasanii halisi na tunashindwa kutofautisha kati msanii na asiyekuwa msanii..kwa taarifa yako mpira wa kisasa una gharama kubwa sana kuliko unavyofikiri..wabongo kama wewe wanalalamika eti Maximo analipwa pesa nyingi..nani katika dunia ya sasa utamwajiri aje kufundisha wachezaji wako halafu umlipe pesa mbuzi!, wachezaji wenyewe ndio hawa kama akina Haruna Moshi..hata akija kocha wa bei kubwa sio kwamba stars watafikia kiwango cha kuifunga Argentina ndani ya muda mfupi..huyo kocha wa bei mbaya atatuambia maneno tusiyopenda kuyasikia..atasema tunahitaji zaidi ya miaka minne ili tuweze kucheza mpira unaoeleweka..na hapo ndipo tutakapoanza kumuita msanii..hatupendi kuambiwa ukweli.. na kocha msema kweli anaanza kuitwa msanii kwa sababu sisi tunaishi maisha yaliyozungukwa na usanii mwingi!!.
    Ni vizuri ukiwatafuta watu wengi ambao wamezaliwa kwenye mpira ili waje wazisaidie timu zetu zisiendelee kututia aibu ya kuwa na majengo mabovu kama lile la kwetu pale msimbazi na lile la kaunda..lakini wawe wasomi maana mpira unaendeshwa kisomi..huwezi ukamchukua mzee mpiga kelele kila asubuhi pale kwenye meza ya kahawa ya klabu ya simba halafu ukampeleka kwenye kikao cha wadhamini wa klabu..ataongea nini!?.
    Narudia tena na tena kukuelimisha kwamba kocha yoyote anaweza kupewa stars awe ni msola, kibaden, julio na maximo..lakini lazima tuufanyie mapinduzi makubwa mpira wetu kuanzai chini kabisa..huu ndio wakati muafaka kwa watu wa mpira kwa maana halisi kujitokeza na kuyaongoza mapinduzi hayo

    ReplyDelete
  80. AnonymousJune 01, 2008

    Mzawa
    vipi hata Mauritius nao 1-1? maximo kocha au gogoro?
    angekuwa Boban ushindi ungepatikana. anamaliza kodi yetu tu. arudishwe kwao.

    ReplyDelete
  81. AnonymousJune 02, 2008

    Za weekend bro..huyo Haruna Moshi alikuwepo siku tulipofungwa na Msumbiji pale pale uwanja mpya..na kama unaikumbuka vizuri ile mechi ni kwamba alikosa goli la wazi!!..Gabriel alikosa penati..sasa unataka Maximo aingie amfundishe kupiga penati wakati mechi ikiwa inaendelea!!..Simba ilifungwa na Stella Abidgan 2-0 mbele ya mzee Ali Hassan Mwinyi tena kwenye mechi ya fainali ya kombe kubwa barani Afrika..ina maana Kibaden nae hafai kufundisha , ikiwa sisi tume droo na Mauritius tayari imekuwa nongwa!!..acha kuendekeza ushabiki wa kwenye kahawa..washauri wadau wa soka letu juu ya umuhimu wa kuandaa wachezaji wetu tangu wakiwa na umri mdogo..kwa kiwango cha wachezaji wetu na kwa uelewa wao jinsi ulivyo , hata akija Jose Mourinho bado ataonekana hajui kufundisha!!..Gabriel kakosa goli la wazi mara mbili..kina Nizar nao wanakosa magoli mengi tu ya wazi..unataka kocha aingie uwanjani wakati mechi ikiwa inaendelea aanze tena kuwafundisha jinsi ya kufunga!!..Kazi njema.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...