1993: rais ali hassan mwinyi akiwa katika picha na wachezaji na viongosi wa simba sc na kombe la ubingwa la klabu bingwa soka bongo na ist afrika mashariki. picha kama hii na nyingine kibao utazikuta banda la sabasaba la daily news karibu na banda la kenya ukumbi wa pta

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 28, 2008

    mi nlifikiri mzee mwinyi kachuchumaa wa pili kushoto kumbe ni yule kashika kombe!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 28, 2008

    yaani anon wa kwanza umeuliza swali halafu umejijibu mwenyewe?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 28, 2008

    mbona hapo waliojaa ni vizee na wahindi,sioni wachezaji na makocha walioteseka uwanjani.Nchi nyingine zikienda kumtembelea Rais huwa ni Wachezaji na jopo la makocha ndiyo wanaochukuwa snepu na Rais siyo vijizee vilivyokuwa vinagombania viingilio.Dont get me wrong Azim alistahili kuwemo hapo.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 28, 2008

    Kipindi hicho Brgd. Makame Rashid alikuwa nani? Ninamwona hapo nae kapozi hapo

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 28, 2008

    Mzee Mputa yaani Abdallah Kibaden naye yupo na anapendeza na hilo balagashia na kanzu...great player!!!

    ReplyDelete
  6. dah, kama sikosei huu si ndio Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki ilikuwa Z'bar? Fainali Yanga na simba ikaenda mpaka Penalty. Zilipigwa penalt sijui 10, 10 zile before Mwkalebela hajapaisha.
    Yanga tulikuwa tunajiamini tulitengeneza khanga za ubingwa tayari. Kesho yake tuakishiwa kuchekwa katika katuni ya gazeti la Mfanyakazi

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 28, 2008

    we anon wa pili..mbona sioni alama ya kuuliza kwa anon wa kwanza? hilo swali uliloona liko wapi?

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 28, 2008

    bwana michuzi napenda kukusahihisha,hiyo ilikuwa mwaka 1991 mwanzoni,na ni kombe la Afrika Mashariki na kati baada ya Simba kuwafunga Sc Villa ya Uganda ilioundwa na akina Magid Musisi,Godfrey Higenyi,Sulle Katto.n.k na Simba ilikuwa na 1Iddi Pazi(Father),2 Rafael Paul(marehemu),3 jamhuri kiwelo(mrema),Method Mogella(fundi)(marehemu)5Deogratius Njohole(OCD),6Hamis Thobias GagaRhino,7Issa Kihange,8Khalfan Ngassa,9Edward Chumila,10 Zamoyoni Mogella(Golden Boy)11Itutu Kigi(roadmaster)Benchi Ayubu Mzee,Hassan Afif,Meckenzie Ramadhani,Idd suleiman Meya.kocha Abdalla king Kibadeni.matokeo Simba3 Villa 0.Afif na Mogella 2.mwaka uliofuatia 1992 yalifanyika Zanzibar Mogella Aliomba Simba Wamsajili kwa kuwa anataka ajiuzulu wakamkatalia akaenda Yanga ila walitunguliwa kwenye fainali kwa penalti ni mwaka waliotokea nyota wa Simba akina Mohammed Mwameja,Damien Mrisho Kimti,George Lucas.Abubakar Salum wa Yanga alikosa penalti ya mwisho na za nyongeza Simba wakashinda.Mwaka uliofuata yalifanyika Kampala Uganda huko nako kuliibuka nyota wengine ila safari hii ni kutoka Yanga,Edibily Lunyamila,mohammed Hussein Mmachinga,Zamoyoni Mogella ndoto yake ilitimia Yanga ilitwaa ubingwa baada ya kuwaadhibu Express ya uganda ikiwa na Issa Sekatawa ambae alidhibitiwa na Issa Athumani alichukuwa nafasi ya Salum Kabunda Msudani ambae alidengua kwenda Uganda.

    ocd

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 29, 2008

    azim dewji yupo hapo.
    mzee Mwinyi alikuwa rais wa watu.mnaochukia na chukieni. ni huyu huyu ndio alikiibua kipaji cHA JK.

    RUKSA UMEFANYA MENGI INSHa Allah Mwenyezi Mungu atakulipia kwa kazi uliyoifanya na kuambulia matusi ya wajinga.sasa wanakukumbuka. bila wewe hata hizi blog tusingekuwa nazo.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 29, 2008

    Asante sana ocd, asante ndugu yangu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...