Balozi wetu Uingereza Mh. Mwanaidi Maajar leo amezindua Kitabu cha Kiswahili cha "Mbinu za Ujasiliamali"
Kitabu hiki kinaeleza maana na umuhimu wa kupata mafunzo ya ‘Ujasiriamali’.
Kinaeleza kuwa ili uwe mjasiriamali mwenye mafanikio huna budi kufahamu mambo mbalimbali kama vile:
· Mbinu za kukabili ongezeko la ushindani wa kibiashara;
· Jinsi ya kuunganisha mtaji na uzoefu wako ili kupata mafanikio zaidi;
· Nafasi na umuhimu wa matumizi ya teknolojia na utunzaji kumbukumbu na taarifa sahihi za kibiashara;
· Nafasi na umuhimu wa utafiti wa kibiashara kabla na wakati wa kuendesha biashara ili kuongeza ubunifu mpya katika biashara yako.
Kwa hiyo, hiki ni kitabu kidogo kinachotoa mwongozo juu ya mbinu za kuwa mjasiriamali makini na mwenye mtazamo wa kimaendeleo. Kimeandikwa kwa lugha nyepesi na ambayo inaeleweka kwa urahisi.

Dkt Imani Silver Kyaruzi, ni mwalimu na mtafiti wa ujasiriamali na uchumi. Ana Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD) ya Uchumi na Ujasiriamali (Chuo Kikuu cha Birmingham); Shahada ya Pili (MBA) katika Ujasiriamali na Biashara (Chuo Kikuu cha Central England) na Shahada ya Kwanza (BA Hons) katika Biashara na Utawala kutoka Chuo Kikuu cha Woverhampton.
Wachapaji: Mkuki na Nyota Publishers

Kwa nakala wasiliana na
Ndugu Deo Simba:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 29, 2008

    Heko kwako Dr. Kyaruzi kwa kuzindua kitabu!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 30, 2008

    Naomba nitoe changamoto kama ilivyo kawaida ya wasomi kutiana changamoto.

    Je huyo mwandishi ni mjasiriamali? au ni mwandishi tu wa nadharia za ujasiriamali?

    Maana Tanzania tuna Tatizo nalo ni kuwa unakuta mtu ni Profesa wa kilimo au biashara lakini hana hata kuku mmoja anayefuga au kufanya biashara.

    Wasomi WETU WENGI wa Tanzania hawajambo kwa nadharia (theories & lectures) lakini kwa utendaji kwenye mazingira halisi(PRACTICALS IN THE REAL WORLD) ni sifuri. Ndiyo maana pamoja na kuwa na kitengo na maprofesa waliobobea kwenye uhandisi hadi leo Tanzania haijamudu kuwa na injinia anayeweza kuanzisha kiwanda cha kutengeneza hata vijiti vile vya kuchokonolea meno hotelini hadi inabidi tuagize china wakati miti tunayo kibao na nyembe ziko za kuchonga hivyo vijiti! ila injinia mwenye uwezo huo hayupo!!!!!!!!!!!

    Ukiwauliza wasomi wengi mafanikio yao makubwa katika usomi wao ni nini? wataanza kukuonyesha makala na vitabu walivyoandika kama ushahidi wa mafanikio yao ya kisomi.

    Nadhani Tanzania tufike mahali wasomi wetu WAONYESHE KAZI ZAO BADALA YA MAWAZO YAO,WAONYESHE BIDHAA WALIZOZALISHA BADALA YA VITABU NA MAJARIDA WALIYOANDIKA. .Kama mtu ni Profesa wa Biashara au kilimo ni vizuri atuonyeshe mradi wake wa biashara au kilimo uliofanikiwa badala ya kutuonyesha makala za biashara na kilimo alizozalisha.

    Hata hivyo ni hatua nzuri Dr.Kyaruzi.Hongera kwa kuandika kitabu nadhani utakuwa wa kwanza kufanyia kazi hayo uliyoandika ili yasiishie kwenye nadharia vitabuni kama hujayafanyia kazi.

    Koloboi@yahoo.com

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 30, 2008

    Kama kweli hicho kitabu kipo....basi please...tuambiwe bei na duka kitakapopatikana hicho kitabu.......mambo ya kuanza kuandika maombi ya kitabu yameshapitwa na wakati ndugu yangu....mbinu yako ya upatikanaji wa hicho kitabu ni utata mtupu unless una agenda nyingine.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 30, 2008

    Congratulation Brother!

    Aziz Rwenza.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 30, 2008

    Niliambiwa kuwa Waziri wa zamani Mzee Abel Mwanga ni Mkurugenzi wa Mkuki na Nyota,je siku hizi yuko wapi?. Alikuwa anaishi pale Sinza Palestina.

    ReplyDelete
  6. Nipo kenya. Kitabu chenyewe nipate wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...